Friday, 28 October 2022 12:03

Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 6 KPSEA End Term 3 2022 Set 2

Share via Whatsapp

Maswali

Soma mzungumzo yafuatayo kishu ujibu maswali 1-4

Jona: Shikamoo dada? Umetulia sana hapa jikoni. Unafanya nini?
Hadija: Marahaba ndugu yangu. Nataka nimalize kuosha vyombo. Ningependa kumrahisishia mama kazi atakapokuja kuandaa chajio.
Jona: Huo ni uamuzi wa busara. Hebu nikusaidie ili tumalize kazi hiyo nawe ukafanye kazi ulizopewa shuleni.
Hadija: (Akitabasamu) Asante. Naona unaelewa kuwa kinga na kinga ndipo moto liwakapo.
Jona: (Huku ukizichukia suhuni azioshe kwenye kuro) Wajua ni jukumu letu kuwasaidia wazazi hapa nyumbani. Huu ndio mchango wetu katika kupunguza matumizi. Au wasemaje dada?
Hadija: Kweli kabisa. Hapo umegonga ndipo. Hakuna haja ya wazazi kuwaajiri vijakazi na vitwana wafanye kazi za nyumbani ilhali mzazi ana watoto wakubwa kama sisi.
Jona: Maadamu tumeimaliza shughuli ya usafi naomba uje unielekeze kufanya hesabu mbili zinazonitatiza.
Hadija: Hlewala, nitakusaidia.
Jona: Asante dada. Tahika ndugu ni kufaana, si kufanana.

 1. Mazungumzo haya yanaonyesha kuwa
  1. Jona ni mkubwa kuliko Hladija.
  2. Tadija ni mkubwa kuliko Jona.
  3. Hadija ni mkubwa kuliko Jona.
  4. Jona ni mwerevu kuliko Hadija.
 2. Watoto hawa ni wenye busara kwa sababu,
  1. wanajua umuhimu wa kuwasaidia wazazi.
  2. wanafanya kazi za nyumbani badala ya kusoma.
  3. wanafahamu ubaya wa vijakazi na . vitwana.
  4. wanaogopa kugombezwa na wazazi wao.
 3. Usemi hapo umegonga ndipo' una maana. kwamba
  1. aliyosema Jona si kweli.
  2. aliyosema Jona hayawezekani.
  3. aliyosema Jona yanashangaza.
  4. aliyosema Jona ni ukweli.
  5. Umuhimu wa ndugu kulingana na mazungumzo ni
  6. kuishi pamoja.
  7. kupeana msaada.
  8. kufanana sana.
  9. kufanya hesabu.

Soma kifungu kifuatacho kishú ujibu muswali 5 - 8
             Kobe alikuwa akitoka cheteni kuuza mboga zake. Siku hiyo, mboga zilinunuliwa zote hata akahitajika kupeleka zaidi. Wateja wake walifurahishwa na mboga zake maadamu hakutumia kemikali zenya madhara. Hakutaka wale waliotumia mboga hizo wadhurike.
             Njiani, alikutana na Pundamilia na Ngiri. Aliwasaili kuhusu walikokuwa wakitoka wakati ule. Pundamilia alimjibu, "Tumetoka kupanda miti upande wa mashariki wa msitu huu. Tumegundua kuwa binadamu ameikata miti mingi sana. Hali hii akiendelea kutatokea kiangazi.” Kobe aliwashukuru na kuwapongeza wenzake kwa uamuzi wao wa busara. Kisha akasema, “Hakika mtego wa panya huingia waliokuwemo na wasiokuwemo. Ni muhimu tuzuje hatari ya ukosefu wa mvua kwa kupanda miti. Nitaenda huko kesho nitimize wajibu wangu."
             Baada ya hapo, wanyama wale walipungiana mikono, Kobe akajiendea zake. Akilini aliwaza, "kwa nini binadamu hatumii akili yake razini? Tamaa hii ya kukata miti kwa kutaka utajiri wa haraka, si itamwangamiza? Isitoshe, juzi nilipopita karibu na kijiji chao, niliona wamerundika taka kila mahali. Hakika wasipoubadili mkondo huo watajuta baada ya kuathirika.”

 1. Neno jingine lenye maana sawa na cheteni ni
  1. sokoni 
  2. nyumbani
  3. shambani
  4. mjini
 2. Kwa nini wateja walizipenda mboga za Kobe? Kobe
  1. alikuwa rafiki wa kila mtu.
  2. alikuwa mkulima hodari.
  3. alijali afya ya wateja wake.
  4. aliziuza kwa bei nafuu.
 3. Ahadi aliyotoa Kobe ni kuwa,
  1. A. angezuia uharibifu wa msitu wao.
  2. angeenda kupanda miti siku iliyofuata. 
  3. angemshauri binadamu aache kuharibu mazingira.
  4. angeenda kupeleka mboga upande wa mashariki.
 4. Tabia za binadamu zinazokashifiwa na Kobe ni
  1. uchoyo na uharibifu.
  2. ukatili na uvivu.
  3. mapuuza na kujitenga.
  4. tamaa na uharibifu.

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 9 - 12.
(Sunkuli na Malaika wamekutana njiani)

Sunkuli: Habari rafiki yangu?
Malaika: Nzuri mwenzangu sunkuli. Je, safari ya wapi jioni hii?
Sunkuli: Naenda kwa Mama Fatuma kumpekelekea chakula. Amekuwa akiugua tangu juzi. Mama amenituma nikamjulie hali na kumpa maziwa haya
Malaika: Ooh! Bi Fatuma yuaugua. Kumbe ndiposa sijamwona akipita karibu na kwetu hivi karibuni. Wajua hawezi kupita bila kutoa salamu.
Sunkuli: Kwa hakika Bi Fatuma ni mtu wa watu. Watu wote wangemwiga yeye, taifa lingekuwa na mshikamano mzuri sana. Maovu mengi yangeisha kwani kila mtu angemchukulia mwenzake kama ndugu.
Malaika: Haya ukifika kwa Bi Fatuma umpe salamu zangu. Nitaenda kumjulisha mama kuhusu maradhi yake. Nikipata kibali nitaenda kuzuru kesho mwendo wa adhuhuri.
Sunkuli: Sawa Malaika. Nina uhakika kuwa utapewa idhini hiyo. Wema hauozi. Hakuna mtu anayeweza kumnyima Bi. Fatuma msaada.
Malaika: Haya, hebu nenda usije kuchelewa. Kwaheri.
Sunkuli: Kwaheri na uwe na jioni njema,

 1. Sunkuli alipokutana na Malaika alikuwa,
  1. akitoka kumsaidia Bi Fatuma.: 
  2. ameenda kuona kama Bi Fatuma aliugua.
  3. ameenda kumjulia hali Bi Fatuma. 
  4. ametoka kuchukua maziwa kwa Bi Fatuma.
 2. Neno ooh! ni aina ya
  1. kielekezi
  2. kiingizi 
  3. kihusishi
  4.  kiwakilishi.
 3. Bi Fatuma ni mtu wa watu ndiko kusema,
  1. anajulikana na watu wengi.
  2. anasaidiwa na watu wengi.
  3. amewasaidia watu wote.
  4. anahusiana vyema na watu.
 4. Malaika anaahidi kuenda kumsaidia Bi fatuma. Msaada huu utatolewa ikiwa
  1. atapewa ruhusa.
  2. atapata wakati 
  3. hatakuwa amepona.
  4. hatakuwa na kazi nyingine.

Soma kifungu kifuatacho kisha uyajibu maswali 13 - 15

Shawe alikuwa na mazoea ya kuenda msalani mara kwa mara kwa haja ndogo. Mwalimu wake aligundua jambo hilo. Alimwita mlezi wake ofisini mwake. “Asante kwa kuitikia mwito wangu, Naomba umpeleke mwana wako kwenye hospitali achunguzwe," Mwalimu akasema.
Shawe alipelekwa hospitalini kwanza alipimwa uzani wake. Baada ya kadi yao ya matibabu kukaguliwa, walitumwa maabarani. Damu yake ilifanyiwa vipimo. Daktari alimwuliza maswali kadhaa. “Daktari, kibofu changu hujaa haraka nami hushindwa kustahimili,” Shawe alimwambia tabibu. Shawe alipigwa picha ya eksirei. Picha hiyo ilionyesha kuwa mafigo yake yalikuwa na tatizo. Kwa bahati nzuri tatizo liligunduliwa mapema. Alipendekezwa kulazwa hospitalini ili atibiwe himahima. Ndugu zake, majirani na wanafunzi wenzake walimwombea apate afueni.

 1. Jambo linaloonyesha kuwa Shawe alikuwa na shida ni kwamba
  1. mwalimu alimwita mlezi wake shuleni.
  2. alikuwa akienda msalani mara mojamoja.
  3. alienda kujisaidia mara kwa mara.
  4. mwalimu alimwona amejikunyata darasani.
 2. Shawe alikuwa na bahati kwani,
  1.  shida yake haikuwa hatari.
  2. hakuwa na shida yoyote.
  3. shida yake iligunduliwa mapema.
  4. watu wote walimwombea.
 3. Viungo vya mwili vilivyotajwa hulahta kazi gani?
  1. Kusukuma damu mwilini.
  2. Kusafisha damu.
  3. Kuyeyusha chakula.
  4. Kuhifadhi mkojo.

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 mpaka 20. Kwa kila swali umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Watu     16    wanashiriki, michezo huwa na afya    17   . Jambo hili huwasaidia     18     magonjwa    19    kuhatarisha maisha yao. Hata hivyo, mtu    20   mazoezi, huathirika kiafya.

16. A. ambaye  B. ambapo  C. ambao D. ambayo 
17. A. mzuri  B. njema  C. jema  D. mwema 
18. A. kuepuka  B. kuepusha  C. kuepukana  D. kuepukia 
19. A. zinazoweza  B. inayoweza  C. yanaweza  D. yanayoweza. 
20. A. akishiriki  B. alishiriki  C. anashiriki  D. asiposhiriki. 


Kutoka swali la 21 hadi la 30 chagua jibu lifaalo zaidi kulingana na maagizo uliyopewa.

 1. Tumia kiulizi kifaacho zaidi Kimaru aliwauza sungura
  1. ngapi
  2. mangapi
  3. wagani
  4. wangapi
 2. Lifuatalo ni jedwali la maneno. Kundi lipi lina vielezi pekee?.
  kali  tamu  safi  bora 
  B pole pole  kwa kasi  sana  haraka 
  C sahani  kikombe  maua  uteo 
  D juu ya  kando ya  katikati ya  ndani ya 
 3.  Bakari ni kaka' wa mama yangu. Kwa hivyo nitamwita
  1. mwamu 
  2. mpwa
  3. ami
  4. mjomba
 4. Andika wingi wa:
  Birika hilo lina chai nyingi.
  1. Birika hizo zina chai nyingi.
  2. Mabirika hizo zina chai nyingi
  3. Mabirika hayo yana chai nyingi.
  4. Birika hayo yana chai nyingi.
 5. Tegua kitendawili kifuatacho: .
  Chauma bila meno, chaumiza bila silaha.
  1. Siafu. 
  2. Moto.
  3. Chungu.
  4. Kiraka
 6. Nomino maziwa na mazingira huorodheshwa katika ngeli moja. Itambuc. ngcli hiyo.
  1. YA - YA
  2. I-ZI
  3. U - YA 
  4. U-ZI
 7. Methali zifuatazo zinaonyesha ushirikiano.
  Ni ipi iliyo tofauti?
  1. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
  2. Umoja ni nguvu.
  3. Wawili si mmoja.
  4. Kidole kimoja hakivunji chawa.
 8. . Shairi ambalo huwa na mishororo mitatu katika kila ubcri ni
  1. tarbia 
  2. tathnia
  3. tathlitha
  4. kibwagizo.
 9. Mtu mwenye sifa ya upole hufananishwa na kiumbe yupi?
  1. Fisi
  2. Punda 
  3. Paka
  4. Njiwa.
 10. Kufanya kazi kwa ushirikiano ni :
  1. kujifunga nira
  2. kupinda mgongo
  3. kufanya kikoa 
  4. kupiga deki.

Majibu

 1. C
 2. A
 3. D
 4. B
 5. A
 6. C
 7. B
 8. D
 9. C
 1. D
 2. A
 3. C
 4. B
 5. C
 6. C
 7. B
 8. A
 9. D
 10. D
 1. D
 2. B
 3. D
 4. C
 5. B
 6. A
 7. A
 8. C
 9. D

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 6 KPSEA End Term 3 2022 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students