Friday, 10 March 2023 11:40

Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 1 Exams 2023 Set 1

Share via Whatsapp

MASWALI

KISWAHILI: INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako
Andika insha ya kusisimua kuhusu mada ifuatayo:

DAKTARI NIMPENDAYE

KISWAHILI: LUGHA
SEHEMU YA KWANZA
Kusikiliza na kuzungumza   (Alama 5)
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
Baraka: Masalkheri Furaha?
Furaha: Akheri Baraka. umeshindaje sahibu?
Baraka: Vyema. (akimtazama kwa makini.) Umetoka wapi?
Furaha: Nimetoka zahanatini.
Baraka: Kwani unaugua?
Furaha: Ndiyo. Juzi nilikaa nje jioni na wenzangu bila sweta na baridi ilikuwa kali. Nilianza kukohoa na nilipozidiwa nikaamua kwenda kutafuta matibabu.
Baraka: Natumai umefanyiwa uchunguzi mzuri ili kujua hasa unakoumia.
Furaha: Ndiyo, nilifanyiwa vipimo na ikabainika kuwa nina kichomi.
Baraka: Kichomi ni nini?
Furaha: Ugonjwa huu pia unaitwa mkamba au nimonia. Unaathiri mapafu na kumfanya mtu awe na shida ya kupumua.
Baraka: Sasa nimeelewa. Je, umepewa dawa?
Furaha: (Akitikisa kichwa) Naam. Ndizo hizi hapa mkobani. Aidha nimepewa maagizo na nitahakikisha nimeyafuata vizuri.
Baraka: Pia uhakikishe umejikinga na baridi.
Furaha: Sasa ninajua kuwa nisipowajibika kujikinga ninaweza kuwa mgonjwa.
Baraka: Ninakutakia afueni ya haraka.
Furaha: Asante sahibu. Ningetaka sasa niende nyumbani ili niweze kunywa dawa na kupumzika. Kwaheri!
Baraka: Kwaheri ya kuonana. (Wote wanaondoka.)

  1. Baraka na Furaha walikutana wakati gani?
    1. Asubuhi
    2. Machweo
    3. Adhuhuri
    4. Usiku wa manane
  2. Ni neno lipi la adabu alilotumia Furaha katika mazungumzo haya?
    1. Nimetoka
    2. Hakika
    3. Asante
    4. Naam
  3. Ni kauli gani si kweli kulingana na mazungumzo haya?
    1. Furaha alikuwa na ugonjwa ulioathiri viungo vya ndani ya mwili
    2. Furaha aliugua kwa sababu ya baridi kali.
    3. Furaha alitibiwa katika hospitali ndogo.
    4. Furaha alitibiwa katika hospitali kuu
  4. Je, ungeyasikiliza mazungumzo ya Baraka na Furaha, ungejifunza nini?
    1. Ni sharti tuwajibikie afya zetu.
    2. Mtu akiugua si lazima atafute matibabu.
    3. Tukijikinga tutapata magonjwa.
    4. Dawa si muhimu katika mili yetu.
  5. Neno lingine ambalo lina maana sawa na daktari ni:
    1. Tabibu
    2. Rafiki
    3. Ndugu
    4. Jirani

Swali la 6 hadi la 8
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
KIJIJI CHA FANAKA
Timu ya kandanda ya Nyota inapatikana katika kaunti ya Nawiri. Nyota ina wachezaji hodari. Nahodha wa timu hiyo anaitwa Sakata. Timu hii huwavutia na
kuwashangaza wengi. Wachezaji wa Nyota ni wenye bidii ya mchwa. Aidha husaidiana katika shughuli zao zote. Huwa wanaamka alfajiri na mapema kufanya mazoezi. Huwa wanakimbia na kupiga kwata uwanjani. Baadaye hucheza mechi ya mazoezi. Wanaamini kuwa mtaka cha mvunguni sharti ainame.
Wakati wa mashindano huwa wanashirikiana ili kupata ushindi. Timu hi haijawahi kushindwa. Hata wakicheza na timu kali namna gani huwa hawashindwi. Ukiwauliza vipi huwa wanapata ushindi, wao hukuambia kuwa jitihada hufaidi. Wachezaji wa nyota hupata mapato makubwa kutokana na mchezo wa kandanda. Wanaweza kujipatia mahitaji yao pamoja na familia zao.

  1. Ni jibu lipi sahihi kulingana na aya ya kwanza?
    1. Timu ya nyota hucheza mchezo wa chesi.
    2. Timu ya nyota haina kiongozi.
    3. Wachezaji wa Nyota ni wazembe.
    4. Timu ya Nyota hucheza mpira wa miguu.
  2. Kifungu kinaonyesha kwamba wachezaji wa Nyota wana bidii kwani:
    1. Huamka mapema kufanya mazoezi na kucheza mechi
    2. Huwa wanashirikiana.
    3. Huamka alfajiri na mapema.
    4. Huwa wanakimbia na kupiga kwata.
  3. Kifungu hiki kimetumia Methali ngapi?
    1. Moja
    2. Tatu
    3. Mbili
    4. Nne

Swali la 9 hadi la 12
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
MALEZI YA MTOTO
Baada ya mtoto kuzaliwa, Mungu humpatia walimu wengi. Mwalimu wa kwanza wa mtoto ni mama. Yeye ndiye anayeanza kuujaza ukurasa mtupu wa ubongo wa mwanawe. Baba pia ana jukumu kubwa katika kumfunza na kumlea mtoto. Sitakosea nikisema kuwa yeye ndiye mwalimu wa pili.
Kazi yake pia ni nyingi. Ni wajibu wake ahakikishe kuwa ameshirikiana na mama malezini kwani mkono mmoja haulei mwana.
Mazingira ya mtoto yanapopanuka yeye huanza kuwa na walimu wengi. Walimu hawa hupatikana shuleni, kanisani, msikitini, nyumbani na mahali kwingine ambako watoto hukutana na watu. Aidha vyombo vya habari na mawasiliano kama vile: Runinga, redio, simu na vinginevyo pia humfundisha mtoto mambo mengi. Hivi vinafaa kutumiwa kwa tahadhari kubwa.
Ikumbukwe kuwa ikiwa mazingira anapokulia mtoto yatamfunza maadili yeye atakuwa na tabia njema. Tuwape watoto mazingira bora ya kujifunza maadili nasi tutafurahia kuwa katika ulimwengu wenye watu waadilifu.

  1. Kwa mujibu wa aya ya kwanza mwalimu wa pili wa mtoto ni nani?
    1. Baba
    2. Mama
    3. Kasisi
    4. Imamu
  2. Ili mtoto apate malezi mema ni lazima baba na mama wawe na:
    1. Utengano
    2. Uzembe
    3. Ushirikiano
    4. Walimu wengi
  3. Kulingana na kifungu, walimu wa mtoto hupatikana katika sehemu hizi zote isipokuwa:
    1. Shuleni
    2. Porini
    3. Kanisani
    4. Msikitini
  4. Watoto wakifunzwa maadili:
    1. ulimwengu utakosa watu wenye tabia mbaya.
    2. tutafurahia kukosa maadili.
    3. tabia njema hazitapatikana.
    4. nidhamu itakosa.

Swali la 13 hadi la 15
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Amina, Maria, Zuhura, Musa na Malaika walimtembelea nyanya yao kijijini. Nyanya hutengeneza mikeka, vikapu na fagio. Yeye hutumia vifaa hivi nyumbani na vingine huvipeleka sokoni kuviuza.
Vijana hawa walimsaidia nyanya yao katika shughuli hiyo. Amina, Maria na Malaika walifuma mikeka. Maria, Musa na Malaika walitengeneza fagio. Wote, isipokuwa Amina na Malaika walifuma vikapu. Wavulana wote walileta vifaa vya kufanyia kazi. Baada ya kumaliza kazi, vijana wote isipokuwa Zuhura walifagia eneo walilofanyia kazi. Vijana wote isipokuwa Maria walimsaidia nyanya kupeleka bidhaa walizotengeneza sokoni.

  1. Nikijana yupi alitengeneza vifaa vitatu?
    1. Zuhura
    2. Musa
    3. Maria
    4. Amina
  2. Ni nani hakumsaidia nyanya kupeleka bidhaa sokoni?
    1. Malaika
    2. Maria
    3. Musa
    4. Amina
  3. Kulingana na kifungu:
    1. Musa, Maria na Zuhura walifuma vikapu.
    2. Malaika, Musa na Amina walifuma mikeka.
    3. Zuhura, Maria na Malaika walifuma mikeka.
    4. Amina, Mariana Musa walifuma vikapu.

Swali la 16 hadi la 20
Soma kifungu kifuatacho. Kwa kila swali umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Johari alisomea shule______16_______Katika ofisi _____17______mwalimu mkuu kulikuwa na _______18______ dirishani. Pia kuna viti vya kukalia. Viti hivi huifanya ofisi _______19______. Kila siku sakafu ya ofisi hiyo_____20_______ili kuondoa vumbi.

  1.                    
    1. nzuri
    2. kuzuri
    3. vizuri
    4. mzuri
  2.                    
    1. kwa
    2. mwa
    3. ya
    4. la
  3.                            
    1. fremu
    2. pazia
    3. kizingiti
    4. Zulia
  4.                  
    1. kupendea
    2. kupendeza
    3. kupendezwa
    4. kupendezana
  5.                    
    1. hupigwa mswaki
    2. hupunga hewa
    3. hupigwa maji
    4. hupigwa deki 

Swali la 21 hadi la 30
Chagua jibu sahihi.

  1. Ni kiungo gani cha mwili hakijaambatanishwa vizuri na kazi yake?
    21 aihdada
  2. Hili ni jedwali la maneno. Chagua jibu linaloonyesha vivumishi vimilikishi pekee?
    22 auygduada
  3. Kati ya maneno haya ni gani litakuja mwisho yakipangwa kialfabeti?
    1. Kabumbu
    2. Gori
    3. Hoki
    4. Jugwe
  4. Kati ya sentensi hizi ni gani imetumia kivumishi kirejeshi 'amba-'kwa usahihi?
    1. Mlango ambayo umefungwa ni huu.
    2. Mgeni ambaye amekuja ni wangu.
    3. Kiatu ambayo kinapendeza ni changu. 
    4. Mti ambaye umekatwa ni mrefu.
  5. Ni sentensi gani iliyoakifishwa vizuri?
    1. Lo! Nyumba imechomeka.
    2. Ngo'mbe ni mnyama mzuri.
    3. Nilinunua kalamu: Winona daftari.
    4. Je, kandanda ni sawa na soka.
  6. Ni sentensi gani yenye kiwakilishi? 
    1. Mpira huu unapendeza.
    2. Watoto wanacheza kibemasa vizuri.
    3. Mimi nitaogelea kesho.
    4. Mabao matano yalifungwa katika mechi hiyo.
  7. Chagua jibu linalounganisha sentensi hizi kwa usahihi.
    1. Imani alimwokea Amara keki.
    2. Amara alimwokea Imani Keki.
      1. Amara aliokewa keki kwa Imani.
      2. Imani aliokea keki kwa Amara.
      3. Amara na Imani waliokewa keki.
      4. Imani na Amara waliokeana Keki.
  8. Chagua sentensi ambayo ni ukanusho wa: Mtoto analilia uji.
    1. Mtoto hatalilia uji.
    2. Mtoto hakulilia uji.
    3. Mtoto halilii uji.
    4. Mtoto hajalilia uji.
  9. Ni sentensi ipi iliyo katika hali ya ukubwa?
    1. Kijia hiki ni kikubwa.
    2. Dege hili limepaa angani.
    3. Kigamia kina njaa kwa sababu ya ukame.
    4. Nyumba yetu ina sebule kubwa.
  10. Chagua jibu lenye nahau iliyoambatanishwa sawasawa na maana yake.
    Piga deki  Pangusa na kusafisha sakafu 
    B Piga mswaki Toka nje ili kujipumzisha
    C Tia mbia Safisha meno kwa mswaki
    D Punga hewa Toa miche ilipomea na kuipanda kwingineko

MAJIBU

kiswahili

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 1 Exams 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students