Tuesday, 13 June 2023 08:29

Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 2 Exam 2023 Set 1

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswall 1-5.
(Mwanasiasa na wananchi wamekutana katika ukumbi wa Ulimisukari ili kutathmini maendeleo yaliyofanywa na ahadi zilizotimizwa tangu mwanasiasa alipotwaa uongozi.)

Mwanasiasa: Ni matumaini yangu kuwa hamjambo. Nina furaha mpwitompwito kwa kuitikia wito huu wa kujumuika nanyi hapa. Kwanza, asanteni sana kwa kura zenu.

Mkulima: Mheshimiwa, ulituahidi mbolea ya bei nafuu. Hadi leo hatujaiona. Je, kulikoni?

Mwanasiasa: (Kwa kiburi) Wizara husika imegundua kuwa serikali iliyotangulia ilitumia vibaya pesa, hivyo, bado hatuna pesa. Tumieni samadi. Kunjeni mashati jamani. Endeleeni kukaza misuli!

Mzazi: Bwana Tumbo, hali ya masomo je? Uliahidi kuwa wanafunzi wetu watafanyia majaribio mwezini.

Mwanasiasa: Kuhusu hilo, naomba mnipe muda kidogo niwasafirishe wanangu warudi shuleni ng'ambo kwanza. Kuhusu majaribio mwezini, tumegundua kuwa hali ya anga huko si shwari. Watasalia chini ya miti kwa muda.

Mwalimu: Hatujaona mabadiliko katika sekta ya wafanyakazi wa umma. Ulituahidi magari kwa mkopo, sasa...."

Mwanasiasa: Baiskeli hujui kuendesha, utaendeshaje gari? Mimi naona bora tufungue vyuo vya mafunzo ya udereva kwanza, ama vipi wenzangu? (akiangazaangaza)

Mjenzi: Mheshimiwa, ulituahidi vyakula bila malipo kila mwezi, kugawana mali yako na mifereji ya maziwa. Umeyafumbia macho. Mheshimiwa huoni haya?

Mwanasiasa: Jamani, naomba tuulize maswali ya kiutuuzima! Wewe uliona wapi mifereji ya aina hiyo? Hakuna cha bure! Imeandikwa kila mbuzi atakula kulingana na urefu wa kamba yake. Kuhusu kugawana mali yangu, nadhani hamkunisikia vizuri. Hali ni ngumu jamani. Tugawanaje mali yangu? (kimya) Mimi nadhani hamna mliloniitia. Tuonaneni baada ya miaka mitano. (wanafumukana kwa huzuni)

 1. Kuhusu mbolea ya bei nafuu, mwanasiasa alitoa kisingizio gani?
  1. Hakuwa na pesa za kuigharimia.
  2. Bado serikali yake haikuwa na pesa. 
  3. Mbolea ilikuwa ya bei ghali katika masoko ya kimataifa.
  4. Alitaka wakulima watumie samadi.
 2. Kuhusu hali ya masomo, mwanasiasa alitaka apewe muda ili
  1. ahakikishe usalama mwezini.
  2. akakamilishe masomo yake ng'ambo. 
  3. awasafirishe wanawe ng'ambo wakasome.
  4. wanafunzi waendelee kusomea chini ya miti.
 3. Dhana ya dharau inajitokeza pale ambapo mwanasiasa
  1. anadai kuwa wafanyakazi wa umma hawajui hata kuendesha baiskeli.
  2. anapinga ahadi zote alizoahidi.
  3. anawaahidi wananchi chakula cha bure.
  4. watu wanafumukana kwa hasira na huzuni
 4. Mwanasiasa alimaanisha nini aliposema kuwa kila mbuzi atakula kulingana na urefu wa kamba yake?
  1. Kila familia itapata chakula kulingana na hali yake.
  2. Watu wote huwa na uwezo sawa wa kujipatia riziki.
  3. Mbuzi mwenye kamba fupi hula katika eneo dogo.
  4. Kila mmoja atajipatia riziki kulingana na bidii yake.
 5. Kulingana na mazungumzo haya, ni wazi kuwa
  1. wananchi waliridhishwa na mwanasiasa huyu.
  2. mwanasiasa aliwahadaa wananchi kumpigia kura.
  3. Bwana Tumbo alikuwa kiongozi mwadilifu.
  4. Bwana Tumbo alitimiza baadhi ya ahadi alizotoa.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 8.
Serikali inapaswa kuwaelimisha wakulima nchini. Hivi ni kwa sababu ya upungufu wa mazao ya kilimo. Wakulima wengi wamepungukiwa na ujuzi wa shughuli za ukulima. Hivyo basi, kuna haja ya kuwafunza njia za kunyunyizia mazao yao dawa. Pia inafaa wafunzwe njia bora za upanzi. Kwa wengine, kutumia mbolea huwa ni jambo wasilolijua wala kulithamini.

Kwa wanaofuga wanyama na ndege kama vile kuku, wanapaswa kufundishwa mbinu za kukabiliana na magonjwa kama vile sotoka kwa ng'ombe na kideri kwa kuku. Maafisa wa kilimo hawana budi kuwa katika mstari wa mbele katika kuwapa wakulima misaada ya kila aina maana kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu.

 1. Kulingana na taarifa, ni kwa nini mazao ya kilimo yamepungua?
  1. Wakulima hawafanyi bidii.
  2. Wakulima hawana ujuzi unaohitajika. 
  3. Kuna upungufu mkubwa wa mvua. 
  4. Kwa sababu kuna ukame uliokithiri nchini.
 2. Taarifa hii inasema kuwa kwa wakulima wengine, matumizi ya mbolea
  1. ni kitu muhimu mno.
  2. ni jambo geni wasilolielewa.
  3. hustahili kufunzwa na maafisa wa kilimo.
  4. ni jambo walilo na mazoea makuu nalo.
 3. Kulingana na ufahamu, si kweli kusema kuwa
  1. serikali haina budi kuwapa wakulima mafunzo kemkem.
  2. mashamba yasiyo na rutuba huhitaji mbolea.
  3. sotoka huwaathiri sana kuku huku ng'ombe wakiugua kideri.
  4. si wakulima wote wanatambua mbinu bora za kilimo.
 4. Sehemu iliyopigiwa mstari mwishoni mwa taarifa hii ina maana gani?
  1. Taifa letu linategemea sana kilimo.
  2. Wananchi wengi wa nchi hii ni wakulima.
  3. Wananchi wote wa nchi hii ni wakulima. 
  4. Wakulima wa humu nchini hawana budi kuongeza bidii kazini.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
Ajira za watoto ni kazi ambazo zinawatumia na kuwaathiri vibaya watoto wa kati ya miaka mitano hadi kumi na saba. Kwa namna fulani, watoto huathirika kiakili, kimwili, kimakazi na kimaadili. Pia, ajira hizi ni kizuizi cha watoto kupata elimu. Mateso yanayowapata watoto katika ulimwengu wa ajira duniani ni mengi. Ajira hizi huweza kuwa za nyumbani kwa watu wengine, mashambani au viwandani. Kazi wanazozifanya watoto hawa ni kulisha mifugo, kuchimba mawe, kufyatua matofali, kuchonga mawe, ujenzi wa barabara, kuvuta au kusukuma mikokoteni na za ndani ya nyumba. Zote hizi ni kinyume na haki za binadamu kwa jumla

 1. Tumearifiwa kuwa ajira ya watoto huweza kuwaathiri watoto
  1. kimaadili, kimakazi na kidini. 
  2. kiakili, kimavazi na kimwili. 
  3. kimakazi, kiakili na kimaadili. 
  4. kiakili, kimwili na kiukoo.
 2. Kulingana na kifungu, ajira ya watoto haiwezi kuwa
  1. nyumbani kwa wengine. 
  2. katika viwanda.
  3. mashambani.
  4. shuleni.
 3. Haki za binadamu hazimkubali mtoto 
  1. kuosha vyombo nyumbani kwao. 
  2. kuvuta mikokoteni kwa malipo. 
  3. kulifagia darasa lao.
  4. kufua sare zake.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Juzi tulipokuwa sebuleni tukitazama runinga, mjomba alianza kutusimulia kuhusu umuhimu wa miti. Alianza kwa kusema kuwa mwalimu wao alisema kuwa miti huwa ni maskani ya wanyama mbalimbali, sanasana nyuni ambao hutengeneza viota vyao na kutagia mayai yao humo. Aliendelea kutuambia kuwa wanyama wengine wanaotegemea miti kama makazi ni wanyamapori kama vile simba, chui, pundamilia na wengine. Si hayo tu, aidha, alisema kuwa miti huweza kutumiwa kujengea, kuundia samani na pia kutumika kama dawa ambapo sehemu mbalimbali za miti hutumika kutibia magonjwa mbalimbali. Tulipokuwa tumechoka kumsikiliza, alituaga na kila mmoja wetu akaelekea kulala ili turauke siku iliyofuata.

 1. Msimulizi na wenzake walikuwa wakisimuliwa kuhusu nini? 
  1. Madhara ya wanyama. 
  2. Matumizi ya maji. 
  3. Umuhimu wa miti.
  4. Wanyama wa porini.
 2. Yawezekana kuwa masimulizi haya yalifanyika 
  1. adhuhuri.
  2. asubuhi.
  3. alasiri.
  4. usiku.
 3. Kulingana na habari hii, miti hutusaidia katika haya yote ila kutupatia
  1. dawa. 
  2. kuni.
  3. vifaa vya ujenzi
  4. vifaa vya kutengenezea samani

Soma kifungu kifuatacho. Chagua Jibu faalo zaidi kati ya vale uliyopewa
Visa vya watu kuwaua wake, waume au watoto wao vimekuwa......................16................. sana siku hizi. Si jambo ......................17................. mtu kufikia hatua kama ......................18................. Hakika, ni......................19................. mkubwa. Si hayo tu, wengine hufikia hatua ya kujiangamiza wao wenyewe kwa kujitoa uhai. Binadamu wanafaa kujua njia......................20................. za kusuluhisha matatizo yao kuliko kuchinjana na kuuana.

 1.                  
  1. mingi
  2. wengi
  3. nyingi
  4. vingi
 2.                      
  1. jema
  2. nzuri
  3. baya
  4. mbaya
 3.                
  1. hili
  2. hiyo
  3. hizi
  4. huo
 4.              
  1. mnyama
  2. wanyama
  3. unyama
  4. kinyama
 5.                    
  1. mzuri
  2. fupi
  3. ndefu
  4. bora

Kutoka swali la 21-30. jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.

 1. Chagua sentensi iliyotumia amba kwa usahihi.
  1. Ugonjwa ambayo ulitibiwa ulikuwa hatari.
  2. Wanafunzi ambao waliojiunga nasi walikuwa werevu.
  3. Cherchani ambacho kilinunuliwa ni hiki.
  4. Masomo ambao tulisomeshwa yametufaa.
 2. Je, ni sentensi gani hapa imetumia kivumishi kiulizi ipasavyo?
  1. Kondoo wapi aligongwa na gari? 
  2. Wageni gani watakaolakiwa jioni? 
  3. Unataka nyumba yako ijengwe vipi?
  4. Ufisadi katika nchi hii utakoma lini?
 3. Mikoba hii ni mipya bali ile pale ni mikuukuu. Sehemu iliyopigiwa mstari ni 
  1. kiwakilishi kiashiria.
  2. kivumishi kiashiria.
  3. kielezi cha mahali.
  4. kiwakilishi cha mahali.
 4. Chagua sentensi iliyoakifishwa kwa usahihi.
  1. Wanyama wafugwao ni pamoja na: ng'ombe, mbuzi na kondoo.
  2. Ukienda ng'ambo uniletee haya: vikoi, saa na mkufu.
  3. Ala, kumbe unajua kuendesha baiskeli.
  4. Mwalimu alipoingia darasani! alikuwa na furaha.
 5. Ni sentensi gani haijatumia kivumishi kimilikishi kwa usahihi?
  1. Jirani yangu anaitwa Kenge.
  2. Madarasa yao yalikuwa na vumbi.
  3. Kina mama yao walituzwa kwa usafi wao.
  4. Mwalimu wetu anapenda kutabasamu.
 6. Chagua majina yaliyo katika ngeli ya KI-VI pekee.
  1. Kinu, kisu, choo.
  2. Uzi, utepe, kiazi.
  3. Chanzo, chenza, chupa.
  4. Kijana, kiongozi, kipofu.
 7. Ukuta umepakwa rangi katika wingi ni
  1. nyuta zimepakwa rangi.
  2. makuta yamepakwa marangi. 
  3. ukuta zimepakwa rangi. 
  4. kuta zimepakwa rangi.
 8. Nomino ndizi, nyumba na habari hupatikana katika ngeli ya
  1. LI-YA
  2. U-I
  3. I-ZI
  4. U-ZI
 9. Kamilisha methali
  Mgeni njoo
  1. mwenyeji apite. 
  2. mwenyeji apone. 
  3. kibaya chajitembeza. 
  4. usimwangalie usoni.
 10. Kupiga miguu ni sawa na 
  1. kukimbia kwa kasi. 
  2. kutuliza miguu.
  3. kuteleza matopeni. 
  4. kutembea.

MWONGOZO

kiswahili sdsd

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 2 Exam 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students