Friday, 04 February 2022 07:34

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 3 Exams 2022 Set 1

Share via Whatsapp

KISWAHILI
GREDI YA 5
MWISHO WA MUHULA WA 3

MAAGIZO.

 • Hii karatasi ina sehemu sita kuu.
 • Jibu maswali yote ku lingana na maagizo.


Maswali

SEHEMU 1: Mazungumzo ya ana kwa ana (Alama 5)

Ni asubuhi na mapema unaelekea shuleni, kisha unamkuta mzee mgongwe barabarani akid edema.

 1. Ni kitu kipi utakachokifanya unapokutana na mzee huyu?
 2. Eleza salamu utakazomuamkua mzee?
 3. Mzee atajibu vipi?
 4. Utamsaidiaje mzee ili afike alipokuwa akienda?
 5. Taja watu katika jamii wanaohitaji msaada wetu

SEHEMU 2: Ufahamu wa kusikiliza( Alama 4)
Msikilize walimu akisoma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

Siku moja Mwanasiti alipokuwa akichanja kuni alijikata kisigino chake na shoka. Damu ilianza kububujika kwa kasi. Mamake alichukua gari lao na kumpeleka hospitalini.Alipofika hospitalini alibebwa na kupelekwa kwa daktari. Daktari alimdunga sindano ya kuzima kutoka kwa damu, kisha akashona kile kidonda na kutia bendeji. Mwanasiti alipomaliziwa alionywa na daktari kuwa awe makini anapotumia shoka au vitu vyenye makali. 

 1. Unadhani mwanasiti alipofika hospitalini alibebwa kwa
 2. Jina jingine la daktari ni
 3. Taja vifaa vingine viwili ambavyo daktari alitumia kumtibu Mwanasiti?
 4. Ni onyo lipi alilopewa Mwanasiti?

SEHEMU 3: Kusoma kwa sauti (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kwa sauti.

Sikukuu ya Madaraka nchini Kenya huwa tarehe moja, Juni. Siku hii ni ya muhimu sana katika nchi yetu. Wananchi hujumuika katika maeneo mbalimbali kusherehekea ukombozi wetu kutoka kwa wakoloni. Nchi yetu ilikuwa imetawaliwa na wakoloni na mabeberu miaka hamsini na minane iliyopita.

Wengi wa wale waliopigania uhuru katika nchi yetu hukumbukwa siku hii. Wengine hutajwa na kupewa zawadi na raisi wa jamhuri ya Kenya. Wengine hupewa makao. Wale waliopoteza maisha wakati wa ukombozi mabango hujengwa ili kuwakumbuka.

Sisi kama wananchi wazalendo ni lazima tutimize amani. Tuhakikishe kila mmoja wetu ana uhuru wake. Kila jimbo limepewa siku yake ya kuadhimisha sherehe hizi eneo lao. Lengo kuu ni kuwaleta Wakenya pamoja.

SEHEMU 4: Ufahamu wa kusoma
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Chausiku ni msichana mrembo na mwenye umbo la kuvutia. Ni kitinda mimba katika familia ya Mzee Sonu na Bibi Washuka. Msichana huyu ana tabia ya kupendeza. Huwaheshimu wakubwa na wadogo. Akitumwa na mamake yeye huenda bila kupinga. Katika familia yake yeye ndiye mtoto ndiye amesoma hadi darasa la tano. Wengine wote walikwamilia madarasa ya chini na wengine ya chekechea.

Wazazi wake wanampenda sana. Kila mara wanamhimiza awe mwenye hekima na kufanya bidii masomoni. Shuleni, Chausiku anabobea katika masomo na michezo mbalimbali. Mwalimu wake wa darasa anajivunia kuwa na mwanafunzi ambaye hulka yake inatamaniwa na wengine shuleni. Chausiku alichaguliwa kuwa kiranja wa darasa la tano. Kila Ijumaa hukutana na wenzake na kupanga mikakati ya kufaulu masomoni. Kwa kweli mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Chausiku anapendwa na wanafunzi si wa darasa lake tu bali shule nzima na hata walimu wanampenda.

Maswali

 1. Taja sifa mbili za Chausiku?
 2. Ndugu zake Chausiku walifika madarasa gani?
 3. Ni kitu gani wazazi wake Chausiku walikuwa wakimhimiza kila mara?
 4. Chausiku alichaguliwa kama?
 5. Andika methali ingine yenye maana sawa na mtoto umleavyo ndivyo akuavyo?
 6. Ipe hadithi mada inayoifaa?

SEHEMU 5: Sarufi (Alama 20)

Andika wingi wa nomino hizi.

 1. upishi
 2. uwele
 3. uzi

  Kamilisha methali hizi.
 4. Mchumia juani
 5. Mvumilivu hula
 6. Subira huvuta

  Tunga sentensi ukitumia maneno haya. 
 7. Barabara
 8. sketi
 9. kofia

  Andika katika umoja.
 10. Vyandarua vimereruka
 11. Vyakula vimeiva
 12. Vyungu vimepasuka

  Akifisha sentensi zifuatazo.
 13. mama alijipamba kwa herini mkufu na bangili
 14. je mtafungua shule siku gani
 15. nampenda paka wangu niliyemnunua nchini burundi

  Pigilia msitari nomino za dhania.
 16. mwalimu, bidii, kimbia, safi, mlango, uhodari

  Tazama picha kisha utaje nomino ya kundi hilo.

 17.       
  Kis1g5et322q17
 18.        
  Kis1g5et322q18

 19.       
  Kis1g5et322q19

SEHEMU 6: Kuandika(Alama 10)
Tazama picha hii kisha uandike insha fupi kuihusu.
Kis1g5et322q20Mwongozo wa kusahihisha 

SEHEMU A
Sehemu 1: Tathmini
Sehemu 2: Ufahamu wa kusikiliza tathmini
Sehemu 3: Tathmini
Sehemu 4: Ufahamu wa kusoma

 1. Mrembo na mwenye umbo la kupendeza mwenye heshima
 2. Ya chini na chekechea
 3. Awe mwenye hekima na kutia bidii
 4. Kiranja wa darasa la tano
 5. Mti ukunje ungali mbichi
 6. Chausiku

SEHEMU 5: Sarufi

 1. mapishi
 2. mawele
 3. nyuzi
 4. hulia kivulini
 5. mbivu
 6. heri
 7. sentesi iwe kamilifu
 8. sentesi iwe kamilifu
 9. sentesi iwe kamilifu
 10. Chandarua kimeraruka
 11. Chakula kimeiva
 12. Chungu kimepasuka
 13. Mama alijipamba kwa herini, mkufu na bangili
 14. Je, ni siku gani mtafungua shule?
 15. Nampenda paka wangu niliyemnunua nchini Burundi
 16. Bidii, safi, uhodari
 17. Kundi la magari
 18. Tita la kuni
 19. Kundi la magari

SEHEMU 6: Kuandika

Mtungo ni alama kumi. angazia kanuni za usahihishaji wa mtungo kama hati, mtiririko, uasilia na ubunifu.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 3 Exams 2022 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students