Friday, 28 October 2022 12:06

Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 3 November 2022 Exams Set 2

Share via Whatsapp

MASWALI
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Mwamba na Baruti ni wakulima katika kaunti ya Jashotamu. Yafuatayo ni  mazungumzo yao walipokutana kijijini.)
Baruti:Salaam aleikum bwana Mwamba! Sikudhani kuwa tungekutana hapa wakati kama huu. Niliarifiwa kuwa ulisafiri hadi Mchangabaridi kwa maonyesho ya kilimo. (Wanakumbatiana kwa furaha)
Mwamba:Aleikum salaam yakhe. Sikupata uwezo wa kufika huko bwana. Mazao niliyoyapeleka sokoni hayakupata wateja kutokana na kuwa hayakuwa bora kama msimu uliopita. (akionyesha uso wa majonzi)
Baruti:Inawezekana kuwa ulitumia mbinu zisizofaa za ukulima. Mbolea uliyokuwa ukitumia haikuwa salama kwa udongo na hata mazao. Nilikushauri kutumia samadi zaidi badala ya mbolea nyingi za madukani.
Mwamba:Ni kweli ndugu Baruti. Tatizo ni kuwa tayari nilikuwa nimekwishayamimina makopo kadhaa ardhini. Matokeo yake ni kuwa maboga na matikiti niliyoyavuna hayakuwa lolote wala chochote... madogo na yenye rangi isiyopendeza. 
Baruti:(Huku akimliwaza kwa kumpapasa bega) Usihofu bwana mkubwa. Naelekea mkutanoni sasa. Nitakaporudi, nitakupigia simu ili tukutane pale Makutano mkahawani nikupe ushauri zaidi kuhusu mbinu bora za kilimo.
Mwamba:Inshallah bwana! Tupatane wakati huo.

 1. Bwana Baruti hakutarajia kukutana na bwana Mwamba kwa kuwa 
  1. kulikuwa na giza nene. 
  2. bwana Mwamba alipaswa kuhudhuria maonyesho. 
  3. bwana Mwamba hakupenda kutembea kijijini. 
  4. kazi zilikuwa nyingi mashambani.
 2. Bwana Mwamba hakuweza kuhudhuria maonyesho ya kilimo kwa sababu
  1. yaliandaliwa mbali mno na kijiji chao.
  2. hakutaka kuhudhuria maonyesho hayo
  3. hakuwa na pesa za kumfikisha huko.
  4. maonyesho hayo hayakuwa na maana kwake.
 3. Mazao ya bwana Mwamba hayakuweza kununuliwa kwa sababu 
  1. hakujua mbinu bora za kuvuna. 
  2. yalikuwa bora zaidi. 
  3. haukuwa msimu mzuri. 
  4. hayakuvutia.
 4. Mazao yaliyotajwa katika mazungumzo haya ni 
  1. matikiti na maboga. 
  2. mboga na matikiti.
  3. maharagwe na maboga. 
  4. matikiti na mahindi.
 5. Bwana Baruti alikuwa amemshauri bwana Mwamba
  1. kutumia samadi zaidi.
  2. kuhudhuria maonyesho ya kilimo. 
  3. kukutana naye huko Makutano. 
  4. kuhudhuria mkutano.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 9.
Kijiji cha Twangapepeta kilikuwa kimekumbwa na janga la maporomoko ya ardhi. Japo hakuna aliyeaga dunia, nyumba nyingi zilifunikwa na udongo. Kwa kuwa wakazi waliishi kwa upendo, waliamua kuungana pamoja ili kuzisaidia familia zilizoathirika. Waliamua pamoja kuwajengea wenzao makao mapya katika maeneo salama. Ingawa mwanzoni ujenzi huo ulionekana kuwa kazi ngumu na nzito, kufanya kazi pamoja kuliifanya iwe rahisi ajabu.
Vilevile, kila mmoja alifanya kazi kwa zamu ili kuimaliza kazi hiyo haraka. Serikali nayo haikuachwa nyuma. Iliwasaidia wanakijiji walioathirika kwa kuwapa mahitaji muhimu kama vyakula, dawa, mavazi na maji. Kufanya kazi bega kwa bega na serikali kuliwapa moyo waathiriwa.

 1. Ni kwa nini wanakijiji waliamua kuwajengea wenzao makao mapya? 
  1. Walikuwa na upendo. 
  2. Walitaka kujionyesha. 
  3. Walikuwa na pesa nyingi. 
  4. Kujenga kulikuwa rahisi.
 2. Nijanga gani lilikikumba kijiji cha Twangapepeta? 
  1. Mafuriko ya kutisha. 
  2. Ukame wa hali ya juu. 
  3. Maporomoko ya ardhi. 
  4. Magonjwa ya kila aina.
 3. Mahitaji muhimu yaliyotajwa si pamoja na
  1. vyakula.
  2. dawa.
  3. mavazi.
  4. elimu.
 4. Serikali iliposhirikiana na wanakijiji, ilionyesha kuwa 
  1. haraka haraka haina baraka.
  2. kidole kimoja hakivunji chawa.
  3. serikali ina mkono mrefu. 
  4. heshima si utumwa.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
Maisha ya mwanadamu yana changamoto. Pia yana mazuri na mabaya. Mtu akitaka kuishi vizuri hapa duniani, ni muhimu amtegemee Mungu. Wahenga walisema kuwa mwomba Mungu si mtevu. Ni lazima mwanadamu awaheshimu wanadamu wenzake kwa sababu heshima si utumwa. Mwanadamu anafaa kuwa mwadilifu na asiyejiingiza katika mambo mabaya kama vile ulevi, wizi, chuki, vita na uvivu. Awaepuke marafiki wabaya ambapo hawana faida yoyote kwake. Hawa matokeo yao huwa ni hasara tu. Ni vizuri mwanadamu aipende elimu kwa sababu elimu ni ufunguo wa maisha mazuri. Mtu anafaa aitumie elimu kujiendeleza na kuwaendeleza wengine. Ni jambo muhimu mwanadamu kuitunza afya yake na ya wengine. Kila mtu anafaa kujiepusha na mambo ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yake na ya wenzake. Vyema pia ni kuyatunza na kuyalinda mazingira. Tukumbuke kwamba tukiyatunza mazingira, nayo yatatutunza. Tukiyaharibu nayo yatatuharibu.

 1. Mwandishi anasema kuwa maisha ya mwanadamu yana
  1. changamoto.
  2. mazuri.
  3. mabaya.
  4. mabaya, changamoto na mazuri.
 2. Ni gani orodha ya mambo mabaya yaliyotajwa katika kifungu ulichokisoma?
  1. Ulevi, uadilifu na chuki.
  2. Bidii, vita na uvivu.
  3. Wizi, chuki na uvivu. 
  4. Chuki, vita na lawama.
 3. Kwa maoni yako, tunawezaje kuyatunza na kuyalinda mazingira? Kwa 
  1. kutumin kuni zaidi katika upishi. 
  2. kuchoma makaa kwa wingi. 
  3. kupanda miche ili kukuza miti. 
  4. kuoga na kufua mitoni.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswall 13 hadi 15.
Siku iliyofuata, tulirauka tayari kuianza safari yetu ya kurejea jijini Bisenta. Ingawa tulianza safari mapema, tulikwama katika eneo la ukaguzi la Soweto. Magari mengi yaliyotutangulia yalikuwa pale pale, nayo yakatuzuia kupita. Ilibidi nasi tusubiri ukaguzi ukamilike. Kilichofurahisha mno ni mbinu ya usafiri ya wale wasio na magari ya kibinafsi. Kwa kuwa eneo hili halina huduma ya mabasi wala matatu, abiria hulazimika kusafiri juu ya malori. Wakati mwingine, malori mengine huwa yamewabeba wanyama kama ng'ombe mbuzi na kondoo hivyo huwabidi wasafiri kuwa makini ili wasiwaangukie wanyama hawa. Safari kama hii huchukua muda wa hadi siku tatu kufika Bisenta na huwabidi wasafiri kuvumilia miale ya jua, upepo, vumbi na hata mvua. Wanaobahatika kusafiri kingwana hukaa kando ya madereva ingawa huwa ghali mno.
Hatimaye magari yalianza kuondoka moja moja huku yakiacha mawingu ya vumbi yaliyomtatiza dereva wetu, Rungu, kuendesha vizuri.

 1. Ni kwa nini kina mwandishi walikwama walipofika Soweto?
  1. Kulikuwa na vumbi jingi barabarani.
  2. Kulikuwa na shughuli ya ukaguzi. 
  3. Hakukuwa na namna ya usafiri.
  4. Watu walikuwa wengi barabarani.
 2. Kulingana na habari hii, ni nini kilichofurahisha? 
  1. Jinsi wasafiri walivyowaangukia wanyama
  2. Namna Rungu alivyoshindwa kuendesha gari.
  3. Mbinu ya usafiri ya wale wasio na magari yao.
  4. Wasafiri walivyovumilia jua, upepo, vumbi na mvus.
 3. Ni nini kilimzuia Rungu kuendesha vizuri?
  1. Jua.
  2. Mvua.
  3. Upepo.
  4. Vumbi.

Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa

Chakula _16_ ni ugali. Chakula hiki hupikwa kwa kutumia_17_. Chakula hiki huupa mwili wangu nguvu ya _18_ na pia kufanya kazi. Ugali huweza kuliwa pamoja na nyama, samaki, maziwa au mboga. Mimi hufurahia ugali kwa kabeji. Kabeji ni _19_nazo mboga huipa miili yetu vitamini ambayo hutukinga tusipate _20_

 1.    
  1. nikipendacho
  2. ninakula
  3. nitakayo
  4. nipendacho
 2.    
  1. nyanya
  2. unga
  3. vijiko
  4. mikono
 3.    
  1. kusinzia
  2. kulala
  3. kunguruma
  4. kucheza
 4.    
  1. mboga
  2. boga 
  3. mtamu.
  4. zuri
 5.    
  1. shida
  2. kuungua
  3. magonjwa
  4. dawa

Katika swall la 21-30. Jibu swall kulingana na magsize uliyopewa.

 1. Kitenzi piga katika kauli ya kutendana huwa
  1. pigwa.
  2. pigana
  3. pigiwa.
  4. pigika.
 2. Ni neno lipi  halijaambatanishwa na kisawe chake?
  1. Shule--darasa. 
  2. Haraka--upesi. 
  3. Tarakilishi--kompyuta. 
  4. Runinga--televisheni.
 3. Tambua nomino iliyo katika ngeli ya KU-KU
  1. Kuni.
  2. Kuku.
  3. Kuona.
  4. Kumi.
 4. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo: Upishi umekamilika.
  1. Upishi umekamilika. 
  2. Wapishi wamekamilika. 
  3. Pishi zimekamilika. 
  4. Mapishi yamekamilika.
 5. Chagua nahau inayohusiana na usafi.
  1. Piga pasi
  2. Angua kicheko
  3. Piga hatua
  4. Kata kamba
 6. Ni methali gani kati ya hizi inahusu bidii?
  1. Tamaa mbele mauti nyuma.
  2. Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
  3. Kawia ufike.
  4. Haraka haraka haina baraka
 7. Ni ipi orodha ya nomino za makundi pekee? 
  1. Umati, upepo, utajiri. 
  2. Sukariguru, batamzinga,kombamwiko. 
  3. Kusoma, kupika, kucheza.
  4. Kicha, mlolongo, safu.
 8. Ni ukifishi upi ulio sahihi? 
  1. Darasa la kina Roda limepakwa rangi. 
  2. Kwa nini hamjawaletea wageni sharubati. 
  3. Uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa wa amani furaha na upendo. 
  4. Tutaandika insha alhamisi ijayo.
 9. Bangili ni pambo ambalo huvaliwa wapi? 
  1. Shingoni.
  2. Mguuni
  3. Mkononi.
  4. Kiunoni.
 10. Chagua orodha ya wanyamapori pekee. 
  1. Farasi, paa, tembo. 
  2. Punda, twiga, pundamilia. 
  3. Kondoo, ng'ombe, mbuzi. 
  4. Ndovu, kifaru, nyati


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. B
 2. C
 3. D
 4. A
 5. A
 6. A
 7. C
 8. D
 9. B
 10. D
 1. C
 2. C
 3. B
 4. C
 5. D
 6. A
 7. B
 8. D
 9. A
 10. C
 1. B
 2. A
 3. C
 4. D
 5. A
 6. B
 7. D
 8. A
 9. C
 10. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 3 November 2022 Exams Set 2.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students