Monday, 03 July 2023 07:17

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Opener Exams Term 2 2023 Set 2

Share via Whatsapp

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali

G5SwaT2OS22023Q1
(Nyanya ameketi chini ya mti akifuma sweta. Anaiweka sweta kando anapomwona Wakesho)
Wakesho :  (akimkaribia nyanya) Shikamoo nyanya?
Nyanya :     (kwa tabasamu) Marahaba mjukuu wangu! Habari za shule?
Wakesho :  Njema nyanya! (kimya) Nyanya, nikwambie kitu?
Nyanya :     Naam, niambie mjukuu wangu.
Wakesho :  Wenzangu walinichagua kuwa kiranja wa darasa.
Nyanya :     Hongera! Jambo zuri sana.
Wakesho :  (akijikuna kichwa). Lakini Nyanya, sijui ninastahili kufanya nini ili niwe kiongozi bora.
Nyanya :     Aha! Wakesho, sikiliza. Ili kuwa kiongozi bora unastahili kuwa na maadili.
Wakesho :  Ooh! Maadili
Nyanya :     Naam mjukuu wangu. Unaweza kuonyesha maadili kwa namna mbalimbali. Kwanza usiwe na ubaguzi unapowahudumia wenzako.
Wakesho :  Kweli Nyanya, ninafikiria pia ninastahili kuwa na upendo.
Nyanya :     Ndiyo Wakesho. Unaweza kufanya hivyo kwa kuwajali na kuwasaidia wenzako wanapokuwa na shida.
Wakesho :  Kweli Nyanya! Ninaona kwamba ushirikiano ni jambo muhimu.
Nyanya :     Haswa! Kidole kimoja hakivunji chawa. Je, unaweza kushirikiana na wengine kwa njia gani?
Wakesho :  (Kwa ujasiri) Kwa kuwahusisha katika mambo mbalimbali.
Nyanya :     Vyema! Unastahili pia kuwa na uaminifu. Tunaonyesha uaminifu kwa kusema ukweli na kufanya mambo inavyostahili.
Wakesho:   Asante Nyanya! Hakika umenifunza mengi.

  1. Wakesho alipoulizwa na Nyanya kuhusu habari za shule alimjibu vipi?
    1. Naam
    2. Njema
    3. Shikamoo
    4. Marahaba
  2. Ni neno gani ambalo nyanya alitumia kumpongeza Wakesho kwa kuchaguliwa kuwa kiranja?
    1. Hongera!
    2. Naam
    3. Ndiyo
    4. Haswa!
  3. Kulingana na kifungu, kiongozi mwema hafai kuwa na ____________________________
    1. ushirikiano
    2. heshima
    3. upendo
    4. ubaguzi
  4. Baada ya mazungumzo haya Wakesho anafaa kufanya nini?
    1. Kufurahia kuwa kiongozi shuleni.
    2. Kufuata mawaidha ya nyanya
    3. Kueleza wenzake kuhusu nyanya yake
    4. Kuwashukuru wenzake
  5. Maadili ni nini?
    1. Ushauri
    2. Kuwajali wengine
    3. Uongozi mzuri
    4. Mwenendo mzuri

Swali la 6 hadi la 9

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

G5SwaT2OS22023Q3

Simba mwenye njaa, katika pitapita zake za kuwinda, alimkuta Sungura akiwa amelala fofofo. Alishusha pumzi, akatabasamu na kumshukuru sana Mungu kwa ukarimu wake wa kumpatia chakula bila kukifanyia kazi.

Taratibu alimsogelea Sungura ili asije akamwamsha, akalala yeye... Alipoinua miguu yake kutaka kumkamata, mara akatokea swara mnono ambaye alipita akikimbia karibu naye, akielekea upande wa kaskazini kwenye nyasi fupi.

Simba alimwacha Sungura na kumkimbiza yule Swara.Kelele za Simba akimkimbiza swara zilimgutusha na kumwamsha Sungura ambaye aliamka na kutimua mbio kuelekea upande wa kusini.

Baada ya kumkimbiza swara kwa muda mrefu Simba alishindwa na kuamua kurudi ili akamle yule Sungura.

Alipogundua kuwa Sungura naye alikuwa ameamka na kukimbia, Simba alisema kwa kujilaumu, "Ama kweli nimepata nilichostahili; kwa kuwa nilikiacha chakula nilichokitia mkononi tayari kwa tamaa ya kutaka kupata zaidi."

  1. Ni wanyama wangapi waliotajwa katika kifungu hiki?
    1. Watatu
    2. Wawili
    3. Wanne
    4. Mmoja
  2. Kati ya wanyama walio kwenye kifungu ni yupi hali nyasi?
    1. Swara
    2. Sungura
    3. Simba
    4. Wote
  3. Hadithi hii inatufunza nini?
    1. Tuwe na ukarimu
    2. Tusiwe na tamaa
    3. Tukifanya makosa tujilaumu
    4. Tuwe watu wenye shukrani
  4. Kinyume cha kitenzi tabasamu ni nini?
    1. Cheka
    2. Lia
    3. Nuna
    4. Waza

Swali la 10 hadi la 12

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Wanafunzi wa gredi ya tano katika Shule ya msingi ya Faulu walipewa mradi wa kutafuta aina mbalimbali za mapambo kwenye mtandao.Wanafunzi waligawanywa katika vikundi vinne kama ifuatavyo: Starehe, Amani, Upendo, Nuru. Kila kikundi kilitafuta mapambo yake. Tazama jedwali hili kisha ujibu maswali

 VIKUNDI   Mapambo   Mapambo   mapambo 
 Starehe  Herini   Pete   Mkufu 
 Amani  Mkufu   Bangili   Herini 
 Upendo  Pete   Mkufu   Bangili 
 Nuru  Bangili   Herini  Pete

 

  1. Ni kikundi kipi hakikupata mapambo ya masikioni?
    1. Starehe
    2. Upendo
    3. Amani
    4. Nuru
  2. Ni kikundi kipi hakikupata bangili?
    1. Nuru
    2. Amani
    3. Upendo
    4. Starehe
  3. Ni kikundi kipi hakikupata pambo la shingoni? 
    1. Starehe
    2. Upendo
    3. Nuru
    4. Amani

Swali la 13 hadi la 15

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

G5SwaT2OS22023Q2

Huduma ya kwanza ni muhimu sana katika maisha yetu. Mtu hupewa huduma ya kwanza anapopata ajali au anapokuwa mgonjwa. Huduma ya kwanza humsaidia mwathiriwa aweze kufika kwa daktari ili kupata matibabu. Mtu akikosa kupewa huduma ya kwanza anaweza akaaga dunia.

Shuleni kuna ajali mbalimbali ambazo hutokea. Ajali hizi ni kama vile: Kuzirai, kuteguka mguu, kuvunjika viungo vya mwili, kuchomeka, muhina (kutokwa na damu puani) kukatwa na kifaa chenye makali na kuumwa na mdudu.

Mtu akizirai kagua kama ameumia kwanza. Kisha mbebe hadi mahali penye hewa safi kama vile kivulini, mlaze chali na uinue miguu yake juu kidogo. Legeza mavazi yaliyombana kwa kufungua mshipi wake, ukosi au mavazi mengine yaliyombana ili apate hewa safi.

Mtu akitokwa na damu puani, mketishe wima huku akiinama upande wa mbele, finya taratibu sehemu iliyo laini ya pua na umwagize apumue kupitia mdomoni kisha uendelee kufinya taratibu kwa muda wa dakika kumi hadi kumi na tano. Mpatie hanchifu ashikilie upande wa pua.

Njia hizi na nyingine ni muhimu kuzijua ili kuweza kuokoa maisha.

  1. Umuhimu wa huduma ya kwanza ni gani?
    1. Kumwezesha aliyeumia kufika kwa daktari.
    2. Kumsaidia mwathiriwa apone.
    3. Kuleta pesa kwa anayefanya huduma ya kwanza.
    4. Kumsaidia mwathiriwa kuaga dunia.
  2. Ni nini maana ya msemo kuaga dunia?
    1. Kuhamia nchi nyingine
    2. Kupona
    3. Kufa
    4. Kupata nafuu.
  3. Ni njia ngapi za kufanya huduma ya kwanza zilizoelezewa?
    1. Moja
    2. Tatu
    3. Nne
    4. Mbili

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Katika gredi ya tano tumefunzwa mambo __16__. Katika matamshi bora mtu anafaa kusema__17__anapomaanisha kuosha nguo. Vilevile sasa najua kuwa kwaheri ni aina ya __18__. Isitoshe ninaweza kutega na __19__ vitendawili. Zaidi ya hayo ninafahamu kuwa kikosi cha askari ni nomino ya __20__.

   A   B   C   D 
 16.   mengi   mingi   vingi   wengi 
 17.  fua  mvua   vua   vuka 
 18.  salamu   methali   tashbihi   maangano 
 19.  kutegua   kujibu   kufumbua   kutegewa 
 20.  wingi  makundi   kitenzi-jina   dhahania 


Swali la 21-30
SARUFI
Kutoka swali la 21 hadi 30, chagua jibu sahihi.

  1. Ni picha gani haijaambatanishwa sawasawa na nomino yake ya makundi?
    G5SwaT2OS22023Q21
  2. Watoto wenye nidhamu, huheshimu walimu ____________________A
    1. wao
    2. yao
    3. zao
    4. vyao
  3. Anwanipepe hutumika katika uandishi wa
    1. Barua rasmi
    2. Barua ya kirafiki
    3. Baruapepe
    4. Barua ya kiofisi
  4. Chagua wingi wa: Nyumba yangu inapendeza
    1. Nyumba yetu inapendeza.
    2. Majumba yetu yanapendeza.
    3. Vijumba vyetu vinapendeza.
    4. Nyumba zetu zinapendeza
  5. Zawadi alimsaidia Nuru kuchora picha. Kwa hivyo Zawadi
    1. alimchoresha Nuru picha.
    2. alimchorea Nuru picha.
    3. alichoreshwa picha na Nuru. 
    4. alichoreshea Nuru picha.
  6. Ni sentensi ipi sahihi?
    1. Chakula hizi imeiva.
    2. Mti huu umekatwa.
    3. Giza hili linatisha.
    4. Gazeti hii imesomwa.
  7. Ni sentensi ipi iliyoakifishwa vyema? 
    1. Nimefurahi sana!
    2. Ninajua kutumia dira?
    3. Tulicheza soka, chesi na jugwe. 
    4. Ngombe ni mnyama mzuri.
  8. Chagua ukubwa wa nomino mto:
    1. Kito
    2. Kijito
    3. Jito
    4. Mito
  9. Chagua jibu lisilo sahihi.
    1. Fupi kama nyundo
    2. Miguu mirefu kama korongo
    3. Mrefu kama mlingoti 
    4. Shingo ndefu kama mbilikimo
  10. Kamilisha Methali hii: Mtoto umleavyo ____________________________________
    1. huvunjika guu
    2. hutazama kisogo cha nina
    3. hufunzwa na ulimwengu
    4. ndivyo akuavyo

KISWAHILI: INSHA

Andika insha kuhusu mada ifuatayo:

SIKU NILIYOFURAHIA SANA  

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Opener Exams Term 2 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students