Tuesday, 08 February 2022 13:56

Shughuli za Kiswahili Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma kwa Sauti - CBC Grade 1 End of Term 3 Exam SET 2 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

1. KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA (Alama 5)
Nitakusomea hadithi kisha nitakuuliza maswali. Kwa hivyo sikiliza kwa makini,
Nilipoamka asubuhi nilimpata baba ameketi sebuleni akinywa chai. Nilimuamkua, “Shikamoo baba,” Naye alinijibu, “Marahaba mwanangu." Baba alifurahi kuona kuwa nilijua kuamkua wakubwa wangu.

  1. Nilipoamka nilimpata nani?
  2. Alikuwa ameketi wapi?
  3. Nilifanya nini? 
  4. Jibu la shikamoo ni nini?
  5. Kwa nini boba alifurahi?

KUSOMA KWA SAUTI
Soma hadithi hii kwa sauti.
Mama alienda shambani kupalilia mimea aliyokuwa amepanda. Mamu alikuwa amepanda mboga na mahindi. Mama alitumia jembe kupalilia. Baadaye mimea ilipokomaa aliivuna na kuipeleka sokoni kuuza. Mama alipata pesa za matumizi mengine.

MAJIBU

  1. baba
  2. sebuleni
  3. nilimuamkua
  4. marahaba
  5. Baba alifurahi kuona kuwa nilijua kuamkua wakubwa wangu
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma kwa Sauti - CBC Grade 1 End of Term 3 Exam SET 2 2022.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.