Tuesday, 08 February 2022 12:24

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 2 End of Term 3 Exams SET 1 2022

Share via Whatsapp

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA (ALAMA 5)
Mwalimu akuulize maswali yafuatayo ukijibu.

  1. Unapenda mnyama gani.
  2. Kwa nini unampenda mnyama huyo?
  3. Taja jinsi unavyomlea mnyama wako.
  4. Eleza umuhimu wa mnyama unayempenda.
  5. Mnyama unayempenda ana miguu mingapi?

KUSOMA KWA SAUTI (ALAMA 10)
Darasa Letu huwa safi kila wakati. Wanafunzi wote huhusika katika kulisafisha darasa letu. Mwalimu wetu wa darasa ametupanga kila mtu na siku yake ya kusafisha darasa. Tunapenda mazingira safi.Tuko na pipa darasani. Sisi hutupa taka kwenye pipa hilo kisha mmoja wetu hupeleka uchafu huo kwenye Jaa pindi lijaapo. Sote tunajua mazingira safi ni afya bora. Hatutaki kuugua. Tunapenda mazingira safi.

Ufahamu (Alama5)
Nuru anapenda chakula, Yeye ana afya nzuri. Mamake Nuru hupika vyakula vya kila aina. Hivi huhakikisha Nuru anapata lishe bora ili aepuke magonjwa mbalimbali. Mama yake Nuru hupika vyakula kama vile wali, ugali, mchicha, kabeji, samaki, nyama na maboga. Yeye pia huhakikisha ameandaa sahani ya Matunda ya kila aina. Matunda hutusaidia kukinga mili yetu dhidi ya magonjwa.

  1. Nuru anapenda nini
  2. Kwa nini mama humpikia Nuru chakula chenye lishe bora.
  3. Andika vyakula vitatu anavyopika mamake.
  4. Taja mboga tatu zilizotajwa kwenye kifungu.
  5. Matunda hutusaidia vipi mwilini?

Sarufi (Alama20) Andika wingi wa sentensi zifuatazo.

  1. Mgeni alichelewa kufika.
  2. Ng'ombe alitibiwa mguu.
  3. Mbona unapenda kusoma? 

Chagua neno mwafaka la kujaza mapengo.

  1. Mgeni anapoondoka akisafiri yeye hutuaga (kwaheri, masala)
  2. Mwalimu hutuamkua (asante, shikamoo) anapofika asubuhi.
  3. Unaporudishiwa kitu ulichopoteza utamwambie aliyekurudishia (Marahaba, Asante)
  4. Sabalkheri ni salamu ya wakati upi?(Jioni, Asubuhi)

Taja majina ya picha zifuatazo.
1


Kamilisha Maneno yafuatayo. 

  1. k             m        
  2. gh        l        
  3.        r        sh        
  4. mw        l        m

Andika kwa herufi ndogo.

  1. MAUA
  2. ZAWADI

Kamilisha sentensi zifuatazo.

  1.         vya         vimenunuliwa. (vyoo, vioo)
  2. Alipoteza        vyake jana. (vyatu, viatu)
  3. Kitabu chenyewe ni bei        (ghali, kali)

Kuandika (Alama 10)
Andika sentensi tano sahihi kuhusu KUKU
2



MARKING SCHEME

Ufahamu.

  1. chakula
  2. ili asipatwe na magonjwa
  3. ugali ,wali na samaki, kabeji, mchicha
  4. mchicha, kabeji,
  5. hutukinga na maradhi

Sarufi

  1. wageni walichelewa kufika.
  2. ng'ombe walitibiwa miguu.
  3. Mbona mnapenda kusoma
  4. Kwaheri
  5. shikamoo
  6. asante
  7. asubuhi
  8. saa
  9. kiti
  10. turfaha
  11. embe
  12. kalamu
  13. ghala
  14. dirisha
  15. mwalimu.
  16. maua
  17. zawadi
  18. vioo vyoo
  19. viatu
  20. ghali

Kuandika. 
Kila sentensi atamna mbili. Sahihisha sentensi fupifupi zilizo sahihi.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 2 End of Term 3 Exams SET 1 2022.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.