Thursday, 16 September 2021 06:44

Insha - Class 7 Kiswahili Revision Notes

Share via Whatsapp


Insha ya Masimulizi

Insha hii huwa na hisi mbili: furaha na huzuni

Vinaweza visa vya kubuni au halisi

Mtahiniwa aweza kutahiniwa mara tatu

Mwanzo wa handithi – dokezo
Huhitajika aendeleze
Kimalizio/tamati

Mtahiniwa lazima aane insha na atamatishe kwa kutumia kimalizio hicho

Huzuni au Tanzia

Visawe vya huzuni ni masikitiko, majonzi, jitimai, buka, chonda na msiba

Hivi ni visa vinanyoleta majonzi, huzuni, simanzi, sikitiko au jitimai

  • Mikondo
  • Ujambazi/unyang’anyi/uporaji/wizi
  • Utekajinyara
  • Ujangili
  • Wizi wa mifugo
  • Ulaghai
  • Magendo
  • Ugomvi wa kijamii
  • Uvamizi na watu katili
  • Migomo

Misamiati na mapambo

  • Mayowe – ukemi, usiahi, mayowe
  • Wasiwasi- jekejeke, jakamoyo, kiherehere
  • Kufa – kata kamba, enda ahera, jongomeo
  • Hasira – pandwa na mori, kuwa na tumbo joto, kama zaibaki kwenye kipimajoto
  • Nilinyapianyapia/nilinyatianyatia nyatunyatu
  • Joho la kiwewe lilinivaa
  • Nilichana mbuga/nilitifua vumbi ili kuyaokoa maish -
  • Moyo ulinidwikadwika/ulinipapa kama ngoma za mahepe
  • Malaika yalinisimama wima
  • Tulisikia sauti zilizotweta kama
  • Sikuyaamini macho nilipoona
  • Nilipiga usiahi ambao ungewafufua wafu
  • Ulimi uliniganda kinywani
  • Nililia kwa kite na imani lakini kilio si dawa
  • Nilitoka shoti kama
  • Ngeu ilimtiririka kama
  • Milio ya risasi ilitamalaki kwenye anga
  • Parafujo za miguu ziliregea
  • Macho yalinitoka pima kama
  • Nilitetemeka kama unyasi nyikanu
  • Kijasho chembamba kikaanza kunitoka

Methali

  • Mbwa hafi maji akiona ukoko
  • Damu ni nzito kuliko maji
  • Tama mbele mauti nyuma
  • Unjanja wa nyani huishia jagwani
  • Siku za mwizi ni arubaini
  • Pwagu hupata pwaguzi

Ragba

  • Juhudi ziligonga mwaba
  • Maisha yalianza kuingia ufa
  • Jaribu kwa udi na uvumba
  • Sijui alipandwa na pepo gani
  • Mambo yalimwendea tege/upogo upogo
  • Alitoka na michirizi ya damu
  • Alipigwa kitutu/kipopo

Dekeza

  • Alifunzwa na ulimwengu usiokuwa na huruma
  • Huruma zake ziligeuka kama umande
  • Alilia kilio cha kite na shake bila kufahamu kilio si dawa
  • Alivamiwa vaa bin vu

Takriri

  • Haambiliki hasemezeki
  • Hana hanani
  • Hazindishi hapunguzi
  • Hapiki hapakui
  • Jando wala togo

Insha ya Mikasa

Mikasa ni matukio yaletayo maafa, masaibu na matatizo kwa watu
Visawe

  • Msiba
  • Balaa
  • Zani
  • Baa
  • Maafa
  • Janga
  • Belua

Mifano ya mikasa

  • Moto
  • Wizi
  • Ajali barabarani
  • Ugaidi
  • Ubakaji
  • Utekaji nyara
  • Zilizala
  • Kuza maji
  • Maporomoko ya ardhi
  • Mlipuko wa bomu
  • Ukame
  • Kabobo

Jinsi yakujadili

  • Eleza mahali pa mkasa
  • Jinsi tukio lilivyotukia
  • Wakati
  • Msaada uliotoa
  • Maafa/hasara
  • Utafiti
  • Changamoto
  • Mkasa wa moto

Mada

  • KIFO KICHUNGU
  • JEHANAMU DUNIANI
  • NDIMI ZA JEHANAMU
  • MOTO WA KUTISHA
  • NDIMI ZA MANAYA/MAUTI
  • NARI YA KUTISHA

Msamiati

  • Ndimi za moto
  • Jiko lililolipuka laweza kuwa gesi, umeme , mbomba la mafuta.tangi la mafuta
  • Mavundo ya moshi yalifuka
  • Mashungi ya moto
  • Cheche za moto
  • Moto ulitatarika an kurindima
  • Upepo ulivuma kwa ghamidha na ghadhabu
  • Matagaa na mapogoo mabichi
  • Kujitoma ndani ya nyumba kama mwehu
  • Nahodha hodari haogopi mawimbi
  • Moto ulifakamia majengo kama nzige wavamiavyo shamaba la mihogo
  • Wengine walichomeka kiwango cha kutotambulikavilio vilinywewa na kuwapwetea
  • Nilifadhaika kwa fadhaa na wahaka
  • Kichwa kilinizunguka kama tiara
  • Vilio vya ving’ora vya makarandinga na ambulensi vilitanda na kuhinikiza hewa
  • Uma uliuputa moto na kuwaokoa manusura
  • Tulitoa huduma za kwanza
  • Wengi walisali/kufanya dua zisizoeleweka

Msamiati mwingine

  • Nilibaki kinywa wazi
  • Machozi ya majonzi yalinilengalenga
  • Machozi yalinienda njia mbilimbili
  • Lia kwikwikwi
  • Nilifikiri macho yangu yalikuwa yakinchezea shere
  • Choka hoi bin tiki
  • Fafanua kinaga ubaga
  • Pigwa na butwaa
  • Nilibung’aa na kuduwaa waa
  • Ponea chupuchupu

Ragba

  • Alipovunja ungo alianza kuwa na mienendo benibeni
  • Mambo yalimwendea upogo/tenge/msobemsobe
  • Alitokwa ma michirizi ya damu ______________ baada ya kupigwa kipopo/kitutu
  • Kijasho chembamba kilianza kumtoka
  • Aliondoka kichwa kifuani kama kondoo /shikwa na zabaiki ya uso, tayarini/haya/soni
  • Uzuri wake ulimteka bakunja akawa haoni hasikii
  • Akasahau penye urembo ndipo penye ulimbo
  • Aliyatemea mawaidha/nasaha mate
  • Alikuwa hayawani kwenye ngozi ya binadamu
  • Ama kweli _____________
  • Dekeza/engaenga kama yai
  • Alifunzwa na ulimwengu usiokuwa na huruma
  • Huruma zake ziligeuka kama umande
  • Alilia kilio cha kite na shaka bila kufahamu kuwa kilio si dawa
  • Alikuwa ndumakuwili kikulacho ki nguono mwako
  • Husuda/wivu zilimzidi hadi akakosa utulivu
  • Alivamiwa ghafla bin vuu

Methali

  • Maji hufuata mkondo
  • Bendera ikipepea sana huraruka
  • Mpiga ngumi ukuta huumia mwenyewe
  • Mpiga mbizi kwenye nchi kavuhuchunue usoni
  • Pwagu hupata pwaguzi
  • Mchimba kisima huingia mwenyewe
  • Vyote ving’aavyo si dhahabu
  • Vyote viowevu si maji
  • Njia ya mhini na mhiniwa ni moja

Takriri

  • Haambiliki hasemezeki
  • Hana hanani
  • Hazidishi hapunguzi
  • Hapiki hapakui
  • Jando wala togo
  • Vihusishi
  • Lahaula!
  • Yarabi!
  • masalaale!
  • Lo!
  • Lakwata!
  • Usaindizi
  • Walitupiga njeki
  • Niliwatupia upondo
  • Niliwapa mkono
  • Tulisaidiana kama kiko na dagali, maiti na jeneza

Tamati

  • Hakika, hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe
  • Daima dawamu sitalisahau tukio hilo
  • Matukio hayo hayatafutika kutoka tafakirini mwangu
  • Ninapokumbuka kisa hicho, machozi hunitiririka njia mbilimbili


Hisia za Furaha

Furaha hutokana na

  • Sherehe – harusi
  • Mwakampya
  • Kuzaliwa kwa motto
  • Sikukuu ya krismasi
  • Sikukuu ya pasaka
  • Mahafali – sherehe za kufuzu
  • Siku ya tuzo/harambee
  • Kutembelewa na wageni
  • Sherehe za kitaifa
  • Sherehe za asili

Msamiati na mapambo

  • Maua ya kila ainati – si asmini, mawaridi
  • Ukumbi ulijaa na kuwatapika adinasi
  • Vipaza sauti vilihinikiza sauti
  • Vyakula vya kila aina/jamii vilitishia kuangusha meza
  • Msichana /kidosho/kipusa alitembea kwa madaha
  • Mkalimani na mfawidhi walishirikiana kama
  • Tulilakiwa kwa kupigwa pambaja
  • Waja walijaa si si si si
  • Waja waliwasili makundimakundi/mmoja mmoja/pacha pacha
  • Nikitembea aste aste hadi jukwaani
  • Kula/kushtaki njaa/fanyia mlo haki
  • Nilikumbuka nilivyojifunga kibwebwe/masombo
  • Kaka angeasi ukapera
  • Waja walisakata ruma/dansi
  • Msafara/mlolongo wa magari
  • Mrembo/spoti/sawa na hurulaini kutoka peponi
  • Wapambe walivalia sare za kupendeza
  • Kusakata rumba/dansi/kunengua viungo
  • Msafara/mlolongo wa magari
  • Mtibwiriko wa kukata na shoka
  • Sheheneza pongezi sufufu
  • Mkono wa tahania
  • Pofushwa na vimulimuli vya wapiga picha
  • Walijaa sisisi/pomoni
  • Hojiwa na sailiwa na wanahabari

Vipokezi vya methali

  • Yakini, ___________
  • Waama, _____________
  • Ama kweli ________________
  • Wahenga hawakukosea walipokili _______________

Methali

  • Chanda chema huvishwa pete
  • Baada ya dhiki faraja
  • Hauchi hauchi unakucha
  • Siku njema huonekana asubuhi
  • Mvumilivu hula mbivu
  • Safari ys kesho hupangwa leo
  • Msafiri ni aliye bandarini

Insha za Ndoto/Njozi/Ruya/Ruiya

Ni maono anayoyapata mtu akiwa usingiziniBarua/Waraka

Huketa hisia za furaha au huzuni

Mtu anaweza kupiga mayowe au kuweweseka kulinga na ndoto

Ndoto za huzuni zinaweza kuhusu

  • Kifo
  • Wizi
  • Moto
  • Mafuriko
  • Kutishwa na viumbe hatari

Wakati mwingine mhusika hutokwa na jasho, kutabawali au kujikuta mvunguni mwa kitanda

Ndoto ya furaha humfanya mhusika kujilaumu kuwa ilikuwa ni ndoto tu. Inaweza kuhusu

  • Mahafali
  • Kuwa tajiri
  • Kapasi mtihani
  • Kuzaliwa mahali kama ikulu

Mwandishi asianze kwa kusema kuwa alianza kuota

Mapambo

  • Baada ya kula chajio _____________
  • Nilikuwa nimechoka hoi bin tiki _______________
  • Niliubwaga mgogole wangu kwenye kitanda ____________
  • Nilijifunika gubigubi na kulala fo fo fo
    Hisia za furaha
  • Nilifurahi ghaya ya kufurahi
  • Furaha upeo wa furaha
  • Nilidamka wanguwangu na kushika hamsini zangu
  • Niliamka alfajiri ya Mungu/ya musa
  • Ukumbi ulijaa shangwe, nderemo na hoi hoi
  • Nilipaa na kuelea angani
  • Vicheko vilishika hatamu jari moja
    Hisia za huzunu – jinamizi
  • Maji yalikuwa yamenifika shingoni
  • Ulimi uliniganda kinywani
  • Moyo ulinipapa kama kwamba ulitaka ufunguliwe utoke
  • Nilishindwa kuongea ni kawa kama mja aluyepokonywa ulimi
  • Malaika alinisimamia tisti/wima/kititi
  • Mambo yaliniendea mpera mpera
  • Nilipiga usiahi/mayowe ambayo yangewafufua wafu
  • Zogo na zahama lilizuga
  • Nililia kwa kite na imani lakini hakuna aliyenihurumia
  • Niliduwaa na kubung’aa kama mzungu wa reli
  • Kilio cha kikweukweu kilihitimu kikawa cha mayowe


Barua/Waraka

Kuna aina mbili

  1. Barua ya kirafiki
  2. Barua rasmi

Barua ya Kirafiki/Kidugu

Huandikwa ili kupeana mwaliko, kujuliana hali, kufahamisha au kuarifu kuhusu jambo

BIDII FAULU,
S.L.P 93,
NAIVASHA.
18-11-2015

Kwa sahibu yangu, fundi msanifu ,
Utangulizi _______________
Mwili

Hatima
Ni mimi wako,
Jina lamwandishi

Sehemu muhimu za barua hii ni anwani ya mwandishi

  • Huandikwa pembeni kabisa wa kulia sehemu ya juu
  • Hujumuisha jina la mwandishi au anakosomea au kufanya kazi
  • Huwa pia na mahali anakoishi na sanduku la posta

Kianzio

  • Hudhihirisha anayeandikiwa
  • Hubainisha uhusiano wake na mwandishi
  • Kwa mpendwa
  • Kwa laazizi
  • Rafiki yangu
  • Kwa mwanangu mpendwa

Utangulizi

Haya ni maamkizi na kujuliana hali
Mfano

  • Pokea salamu sufufu/furifuri
  • Mimi ni buheri w afya/mzima kama

Mwili

  • Hubeba ujumbe au kusudio la barua
  • Lengo/nia/azma ya kukuandikia barua hii ni __________
  • Jina la
  • Ninaomba unitendee hisani/fadhila
  • Kwa kuwa wema hauozi
  • Ninakuhakikishia kuwa nitatia bidii
  • Ningependa kukujuvya kuwa
  • Tumia viunganishi ili kuunganisha mawazo
    • Isitoshe, zaidi ya hayo, aidha

Tamati

  • Ningependa kutia nanga kwa kukueleza
  • Ningependa kukunja jamvi
  • Kwa kuwa muda umenip kisogo
  • Ni mimi wako mpenzi,
  • Ni wako mpendwa,
  • Jina la mwandishi

Barua Rasmi

  • Huandikwa ili kuwasilisha ujumbe maalum
  • Huandikwa ili kuomba msamaha
  • Kuomba nafasi kwa kazi
  • Kuwasilisha malalamishi
  • Kuagizia/kuthibitisha mapokezi ya kampuni, shirika , idara

Sehemu

Anwani ya mwandishi

  • Huandikwa pembeni kabisa upande wa kulia sehemu ya juu ya karatasi
  • Hujumuisha jina la mwandishi, sanduku la posta, mahali anakoishi na tarehe baada ya anwani vuka mstari mmoja

Anwani ya mwandikiwa

  • Hutaja cheo cha anayeandikiwa
  • Taja jina la kampuni/shirika/dara
  • Taja S.L.P

Kianzio

  • Huanzia chini ya anwani ya mwandikiwa
    • Bwana/BW
    • Bibi/BI
    • Mabibi
    • Mabwana

Mtajo

  • Huelezea lengo la barua
  • Hutangulizwa kwa MINT: (mintirafu), KUH: (kuhusu), OMBI: , kumb: (kumbuka)
  • Pigia mstari ujumbe wenyewe

Mwili

Hubeba ujumbe wa barua

Maudhui hutegemea nia au lengo la barua

Lugha iwe rasmi

Msamiati

  • Nina furaha riboribo/kuu/firifuri
  • Nina bashasha belele
  • Ninasikitika ninapokuandika waraka huu ____________________
  • Ningependa kuchukua fursa/wasaa/nafasi
  • Kurejelea habari Fulani
  • Kwa mujibu w habari niliyoisoma/kutokana na taarifa/ kulingana na ______________
  • Shule.kampuni/shirika _____________ imesifika
  • Imetajwa na kutajika
  • Sifa zake zimeenea kote _______________ kamamoto nyikani kama wakati wa hari/kiangazi
  • Katika Nyanja za michezo ____________________ idara/shirika/shule yako
  • Wasifu/tawasifu _____________ mimi ni mwananchi kindakindaki/halisi
  • Nina nidhamu na taadhima ya hali ya ___________________
  • Nina talanta katika fani ya riadha uimbaji
  • Nina sauti ya ninga
  • Nitakuwa kielelzo dhabiti kwa
  • Nitatia bidii za mchwa ajengaye kichunguu
  • Nitavumilia/nitajikaza kisabuni ili kuafikia ndoto yangu
  • Vyeti vyangu vimeambatanishwa pamoja na waraka huu

Tamati

Ni mwisho wa barua
Huandikwa pembeni upande wa kulia sehemu ya chini
Herufi ya kwanza iwe kubwa



Insha ya Methali

Methali ni usemi wa kisanii wa kimapokeo unaofikiliwa na jamii na hutumiwa kufumbia jambo fulani

Methali hutahiniwa kwa namna tatu

Ikiwa kama mada

Mwanafunzi anafaa aeleze maana ya juu na ya ndani yake na matumizi yake iwapo anaifahamu vyema

Methali za Majuto, Maonyo na Tahadhari

  • Hutumiwa kuonyesha athari au madhara yanayotokea baada ya mtu kugaidi maagizo, nasaha au maonyo
  • Methali hutahiniwa kwa njia tatu
    Ikiwa mada
    Mwanzo – mwanafunzi huhitajika kuendeleza bila kufafanua maana ya methali
    Kimalizio – lazima kisa kishahibiane na methali ile.

    Tanbihi
    Ikiwa methali itakuwa mada, mtahiniwa atahitajika kueleza maana ya nje, ya ndani na matumizi endapo anafahamu

  • Hutumiwa kutoa funzo kwa wenginekutokana na dhiki na majuto yaliyomfika mhusika
    • Asiyefunzwa na mamaya hufunzwa na ulimwengu
    • Asiyeskia la mkuu huvunjika guu
    • Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe
    • Mbio za sakafuni huishia ukingoni
    • Mchuma janga hula na wa kwao
    • Ujanja wa nyani huishia jangwani
    • Majuto ni mjukuu huja kinyume
    • Mchimba kisima huingia mwenyewe
    • Msiba wa kujitakia hauna kilio
    • Kilio si dawa
    • Asiyeangalia huishi laiti ningalijua
    • Mkata pema pabaya panamwita
    • Sikio la kufa halisikii dawa
    • Haraka haraka haina baraka
  • Vipokezi vya methali
    Yawe yasiwe ____________
    Aisee! __________
    Labeka! _________________
    Lahaula! Lakwata ____________
    Chambilecho wenye ndimi walihenga ______________
    Hapo ndipo nilipoamini na kusadiki kuwa ______________
    Waledi wa lugha waligonga ndipo walipoganga kuwa _______________
    Wakale hawakupanda upepo wakavuna tufani _____________
  • Visa husika
    • Wizi
    • Utumizi wa dawa za kulevya
    • Kujiingiza katika anasa

Mapambo na msamiati

  • Kutofuata ushauri
    • Alikuwa hakanywi hakanyiki
    • Hasikii la mwadhini wala la mteka maji msikitini
    • Alikuwa haliki hatafunuki
    • Haambiliki hasenezeki
    • Alikuwa hajijui hajitambui
  • Kujuta
    • Aliishia na laiti kinywani
    • Alijiuma kidole/alilia chanda kili kinywani
    • Nilikabiliana ana kwa ana na ulimwengu usiokuwa na huruma
    • Niliyaona ya firauni
    • Nilikiona kilichomtoa kanga manyoya
  • Kupuuza
    • Alivalia miwani mashauri
    • Niliyatemea mate mawaidha
    • Alijitia hamnazo
    • Aliyatia kapuni yota aliyoambiwa
  • Mambo kuharibika
    • Mambo yalimwendea pete/tenge/mrisi/shoto/shambiro
    • Kutowezekana kwa
    • Ilikuwa sawa na kukama tetere
    • Kufunuka jua kwa ungo au chekeche
    • Kuchota maji kwa pakacha
  • Tashbihi
    • Pukutikwa na machozi kama ngamia
    • Tiririkwa na machozi kama maji mlimani
    • Mchafu kama kilihafu/fungo
    • Nuka kama mzoga/beberu/kindonda
  • Unafiki na kujitakia shida
    • Chui aliyevalia ngozi ya kondoo
    • Panya aliyeumia na kuvuvia
    • Kujipali makaa kama chachandu
    • Kuogelea katika bahari ya moto
    • Methali ni usemi wa kisanii wa kimapokeo unaofikiliwa na jamii kuwa wa kweli na unaotumia kufumbia
  • Ragba
    • Aliona cha mtema kuni
    • Kilichompata peku na lungo kilimpata
    • Mambo yalimwendea visivyo
    • Alitamani mauti yaje yamwokoe
    • Maji yalizidi ynga
    • Alitamani dunia ipasuke immeze mzima mzima
    • Kumwashia kipofu taa
    • Alitia masikio pamba
    • Machozi ya majonzi
    • Lia kilio cha kite na shaka
    • Machozi yalimtoka kapakapa
    • Pyorea mdomo
    • Huzunika ghaya ya kuhuzunika
    • Machozi yalinienda mbilimbili
    • Kuwa na kamusi ya matusi
  • Tashbihi
    • Pukutikwa na machozi ka,a ngamia
    • Tiririkwa na machozi kama maji mlimani
    • Bubunjikwa na machozi kama mfereji
    • Nuka kama mzoga
    • Mchafu kama fugo
  • Takriri
    • Hakiri hakubali
    • Hajali jando wala togo
    • Si wa uji si wa maji
    • Kutomjulia heri wala shari
    • Akiulizwa haungani

Methali za Kutohadaika na Uzuri wa Nje wa Kitu na Tamaa

Hutumiwa kuwaonya adinasi dhidi ya kudanganyika au kuhadaika na uzuri wa kitu bila kudadisi matokeo na athari zake.

Methali ikiwa kama kichwa huhitajika kuelezea maana ya nje, ya ndani na matumizi
Mfano wa visa

  • Kumkaribisha mtu nyumbani
  • Kupatiwa lifti
  • Biashara gushi
  • Urembo
  • Fisadi

Methali

  • Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti
  • Hakuna kizuri kisichokuwa na dosari
  • Penye urembo ndipo penye ulimbo
  • Uzuri wa mkakasi, ukipata maji basi
  • Vyote ving’aavyo sio dhahabu
  • Tama ilimwua fisi
  • Uzuri si hoja hoja ni tabia
  • Mpanda farasi wawili hupasuka msamba
  • Mtaka yote hukosa yote
  • Mbio za sakafuni huishia ukingoni
  • Mla kwa wawili hana mwisho mwema
  • Penye uhondo pana uvundo
  • Uzuri wa biyu ndani mabuu
  • Usiache mbachao kwa msala upitao

Vipokezi vya methali

  • Kwa yakini ______________
  • Taib ___________
  • Ama kweli ______________
  • Kuntu _____________
  • Ni jahara kama pengo kuwa _____________
  • Ni wazi kama ju ala mtikati kuwa _____________
  • Chambilecho wahenga au wazee wenye tabasuri tepetepe _______________

Nahau

  • Maji kuzidi unga
  • Kitumbua kiliingia mchanga
  • Valia miwani
  • Meza mrututu
  • Meza mate machungu
  • Tulia huku ukitolea kule
  • Vimba kichwa
  • Kuwa na mkono mrefu
  • Bwaga zani

Takriri

  • Dhahiri shahiri
  • Haambiliki hasemezeki
  • Hakanywi hakanyiki
  • Kuwa kiguu na njia
  • Hana harusi hana matanga

Ragba

  • Walimdekeza mwana wao
  • Alikuwa ndumakuwili aliyeuma ndani yakini kikulacho ki nguoni
  • Alijaribu bahati kwani asiyekuwa na bahati habahatishi
  • Pigwa kipopo
  • Temea mate
  • Kumwonea gere
  • Mambo yalimwendea sambejambe
  • Alilia kilio cha kite

Tashbihi

  • Huzunika kama mfiwa
  • Kuwa na wasiwasi kama mwasi
  • Aminika kama njiwa
  • Jambo wazi kama mchana
  • Kuwa mzembe kama kupe


Insha ya Maelezo

Huitwa wasifu

Hutoa ufafanuzi kuhusu jambo, mtu, mahali au kitu fulani

Maelezo haya huwa ni sifa au hoja maalum

Insha hizi hutahadharisha, huelezea, huarifu na huburudisha

Mtahiniwa atangulize kwa ufafanuzi wa mada yake

Ahitimishe kwa kutoa changamotokwa waliohusika

Mtahiniwa asijadili chini ya hoja sita. Atoe hoja za ukweli

Mfano

  • Athari za ukimwi
  • Athari za dawa za kulevya
  • Faida na Athari za teknolojia
  • Mchezo niupendao
  • Haki za watoto
  • Faida ya elimu, miti na wanyamapori
  • Ukosefu wa usalama
  • Dawa za Kulevya

Haki na Ajira za Watoto

  • Haki ni mstahiki au ni jambo ambalo ni halali ya mtu
  • Mstahiki pia ni mtu mwenye haki ya kupata kitu
  • Ajira ni kazi zinazofanywa katika mashamba, viwanda, nyumbani na migodini
  • Watoto wanapopewa ajira ni kinyume cha sheria
  • Baadhi ya haki hizi ni
    • Lishe bora
      • Watoto wanafaa wapewe mlo ulio na viinilishe muhimu kwa protini, kabohaidrati, madini na maji safi.
      • Wasipolishwa huenda wakaathiriwa na magonjwa kama kwashakoo, utapiamlo.
    • Mavazi
      • Humkinga dhidi ya mabadiliko ya hali ya anga
      • Huzuia maradhi kama mafua, nimonia na pumu
        Methali
        Kinga ni bora kuliko tiba
    • Makao salama
      • Humsitiri dhidi ya wanyama hatari, maadui na mabadiliko katika hali ya anga
    • Kupata elimu
      • Asibaguliwe kwa misingi ya jinsia, kidini, kikabila au rangi ya ngozi
      • Wasichana wasiozwe mapema
      • Wasijiingize katika vitendo vya ukosefu na maadili kama ukahaba
      • Wafundishwe maadili na nidhamu
        Methali
        Elimu haitekeki
        Elimu ni bahari
        Elimu haina mwisho
    • Afya njema
      • Watoto wanafaa kukulia katika mazingira safi
      • Wapewe matibabu wanapougua
      • Wapewe lishe bora
        Methali
        Afya ni bora kuliko mali
        Kinga ni bora kuliko tiba
    • Wakingwe dhidi ya dhuluma
      • Hii ni kama kuchomwa na kukatakatwa mwilini
      • Waadhibiwe kwa kadiri na wastani
      • Wakuzwe vyema kwa maadili na mapenzi
        Methali
        Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
        Masukuzi ya leo ndio msitu wa kesho
    • Wasiajiriwe
      • Hii ni kinyume na sheria katika katiba ya nchi
      • Waajiri huwatesa na kuwanyanyasa watoto
      • Wengine huwarapua kwa mijeledi
      • Wengine huajiri kama vijakazi, watwana

Michezo

Ni jambo lifanywalo kwa ajili ya kujifurahisha kujichangamsha au kupoteza wakati

Baadhi ya michezo

  • Jugwe
  • Gugwi
  • Bembea
  • Kibe
  • Msabaka
  • Kandanda
  • Riadha
  • Sarakasi
  • Netiboli
  • Naga
  • Voliboli
  • Gololi
  • Hoki
  • Langalanga
  • Kriketi
  • Mpira wa wavu

Kandanda

Pia huitwa kambumbu, soka , gozi au mpira wa miguu

Hushirikisha timu mbili pinzani
Wachezaji huvalia

  • jezi
  • Daluga
  • Soksi
  • Bukta

Katikati  ya uwanja huitwa kitovu/senta
Otea – kujificha kwa makusudi ya kushambulia kwa ghafla
Penalty – adhabu kwa mlindalango
Mlindalango, mdakaji, golikipa
Kimia
Refa/refarii
Mshika bendera/kibendera
Mhimili/goli
Ngware – cheza visivyo
Kipindi cha lala salama ni kipindi cha nwishi
Kadi nyekundu huonyesha kutimuliwa kwa mchezaji
Kadi ya jano – onyo

Huwa na wachezaji kumi na mmoja katika kila upande

  • Walinzi au difensi
  • Wachezaji wa kati
  • Safu ya mashambulizi
  • Wachezaji wa akiba
  • Piga mkwanju
  • Kocha/mkufunzi

Mapambo

  • Uwanja ulijaa hadi pomoni
  • Wachezaji walishonona
  • Mdakaji aliudaka mpira ungedhani ni tumbili aliyedadia tawi la mti
  • Pasi fupifupi na za uhakika ungedhani walikuwa na mashine miguuni
  • Mpira haukulenga goli _______ kweli kulenga si kufuma
  • Kuutia mpira vifuani kana kwamba una spaki za kuunasa
  • Walinda ngome walikuwa imara kama chuma cha pua
  • Kwenda kubwaga moyo baada ya kipindi cha kwanza
  • Safu ya ilinzi ulikuwa imara kama ukuta uliotengenezwa kwa zege
  • Enda nyatunyatu na kufyatua zinga la kombora
  • Visha kanzu
  • Nyota ya jaha
  • Bao la kuta machozi
  • Piga kombora kimo cha mbuzi , kuku au ngamia
  • Mashabikiwalijawa na bashasha
  • Kipindi cha pili tukihisi kuwa na nishati mpya
  • Bao la bua liliweza kuzitubua nyoyo za wapinzani wetu
  • Mrisi bin kappa

Dawa za Kulevya

Hatua

Kufafanua maana

Ni kitu chochote kinachoathiri fahamu au mwili wa binadamu
Dawa hizi ni kama vile

  • Bangi
  • Sigara
  • Heroini
  • Miraa/mirungi
  • Pombe haramu

Anayeuza dawa hizi huitwa mlaguzi
Njia ya kutumia dawa hizi ni

  • Hunuswa
  • Hunywewa
  • Hudungwa
  • Hulambwa
  • Hutafunwa

Madhara ya dawa za kulevya

  • Kuvurugika kwa akili
  • Mja hugeuka kuwa zuzu, mkia wa mbuzi
  • Hupata ujasiri bandia
  • Hujiingiza katika visanga
  • Hudhuru afya
  • Hukonda na kukondeana kama ng’onda
  • Sura huambuliwa na kusawijika kama sokwe
  • Utovu wa nidhamu
  • Husheheni cheche za matusi
  • Kutabawali kadamnasi
  • Vaa mavazi vichungi na vioo
  • Kuzorota kwa uchumi
  • Kukosa elimu
  • Jamaa hukosa mavazi, makao na mlo
  • Humtilisha mtumiaja
  • Husababisha uraibu
  • Hushinda kutwa kucha wakitumia dawa hizo
  • Huwa kupe
  • Huwa maajenti wa mawakala
  • Chanzo cha maafa
  • Madereva hukosa kuwa waangalifu
  • Huleta shinikizo la damu mwilini
  • Ajali barasteni
  • Wizi wa mabavu
  • Kufanya mapenzi bila kinga

Tamati

  • Changamoto/nasaha
  • Wasiwe pweza kujipalia makaa
  • Kizazi cha baadaye kitaangamia
  • Kushirikiana kama kiko na digali kuangamiza janga hili
  • Wito kwa serikali – kuwasaka
  • Kufungua mashtaka

Mada

  • KIDIMBWI CHA MANAYA
  • NAULI YA AHERA
  • BARABARA YA KUZIMU
  • TARIKI YA MAUKO

Misemo

  • Kujipalia makaa
  • Bwaga zani
  • Meza mrututu
  • Tumbulia macho
  • Gofu la mtu

Takriri

  • Kufa kupona
  • Kwa hali na mali
  • Liwalo liwe
  • Balaa belua
  • Methali
  • Tahadhari kabla ya hatari
  • Mwiba wa kujidunga hauambiwi pole
  • Ajali haina kinga
  • Mchezea mavi humnukia
  • Nzi kufia juu ya kindonda si haramu
  • Masukuzi ya leo ndiyo msitu wa kesho
  • Wazee hukumbuka vijana hukumbushwa

Tashbihi

  • Konda kama ng’onda
  • Nyong’onyea kama muwele wa malaria
  • Dhaifu kama mkufu
  • Epuka ambao kama mgonjwa wa ukoma/ebola

Umuhimu wa Maji

Mwongozo ambao ni mwanzo wa insha kisha aendeleze
Mfano
“maji yana manufaa anuwai ___________ ”

  • Atoe hoja zisizopungua sita
  • Iwe na mtiririko mmoja
  • Sehemu ya hitimisho;atoe change moto kwa jamii au serikali

Mfano

UMUHIMU WA MAJi

Utangulizi

Maana ya maji
Maji ni kiowevu kisicho na rangi kinapatikana mtoni, ziwani, baharini na hata kutokana
na mvua
Maji ni uhai

Umuhimu wa maji

  • Kukonga roho au kukata kiu
    Adinasi hukonga roho
    Huweza kuishi bila shabuka au shida yoyote
    Husaidia usagaji wa chakula
    Mapishi ya vyakula
    Chakula hulainika na kuwa na ladha
    Huimarisha siha/udole wa binadamu
    Humweupusha mlimwengu na magonjwa
  • Usafi na unadhifu
    Kutakata mili ili kuepukana na magonjwa
    Kupiga deki
    Kusafisha mashine viwandani
    Kuwa mchafu kama fungo
    Kusafiri jongomeo baada ya kugua maradhi
  • Usafiri baharini, maziwani na mitoni
    Kusafirisha shehena za mizigo
    Mizigo mizito kama nanga
    Vyombo hivi vya usafiri ni meli, motaboti, ngalawa, merikebu, mashua, manahodha na maserahangi
  • Kuzungusha mitambo au mashine
    Hupata nguvu za umeme au nishati
    Nishati hizi huweza kutengeneza bidhaa za madini, vyakula na mavazi
  • Makao ya wanyama
    Kama samaki, kiboko, mamba, kamba na kasa
    Samaki ni chakula murua kwa mja na humzuia mja kuoata ndwele
  • Burudani na michezo
    Hamamu na mandibwi ya maji hutumika na wanamichezo kwa mashindano ya kuogelea
  • Huwa sehemu ya ajira
  • Huletea nchi pesa za kigeni
  • Kuondoa uchafu baada ya kazi
  • Maji ni asili ya uhai
  • Kuuzima moto
  • Kivutio cha watalii
  • Kunyunyizia mimea maji

Viunganishi

  • Mbali na _____________
  • Fauka ya ______________
  • Isitoshe _______________
  • Zaidi ya ______________
  • Hali kadhalika _______________

Hitimisho

  • Nikilikunja jamvi ninawashauri ________________
  • Hatuna la msalie mtume wala nabii ili kuyatumia maji ipasavyo __________________
  • Ama kweli maji ni kito cha dhamani ambacho kinafaa kulindwa kwa hali na mali

Methali

  • Maji yakimwagika hayazoleki
  • Maji ya kifuu ni bahari ya uchungu
  • Maji mapwa hayaogwi
  • Maji ni uhai
  • Maji hufuata mkondo
  • Maji ukiyavulie nguo yaoge


Hotuba

Hotuba ni maneno au malezo maalum yanayotokana na mtu mmoja mbele ya hadhira

Anayetoa hotuba huitwa hatibu

Hadhira ni watu wanaohutubiwa

Hotuba inaweza kuwa ya

  • Mwalimu mkuu juu ya wazazi
  • Mwanasiasa nyakati za kampeni
  • Maafisa wa serikali katika sherehe tofauti
  • Rais akihutubia taifa

Mambo ya kuzingatia

  • Kufuata itifaki
  • Kutambua waliohidhuria kufuata cheo/mamlaka na umri
    Mfano “mwalimu mkuu, naibu wa mwalimu mkuu, viranja na wanafunzi wenzangu hamjambo? ______
  • Wakati uliopo hutumika yaani usemi halisi
  • Nafsi ya kwanza na ya pili hutumika
    Mfano
    Nimesimama kadamnasi nikiwa mzima kama kigongo ________
  • Hutumia alama za kunukuuu ikiwa unahutubia kwa niaba ya mtu mwengine
    Mfano
    rais, naibu wa rais ______
  • Kila hoja husimuliwa katika aya yake
  • Hitimisho huhusu kuwashukuru wasikilizaji na pia kuwapa funzo au changa moto au nasaha

Umuhimu wa Elimu

Elimu ni mafunzo yanayopatikana shuleni na maishani
Hupevusha fikira
Mja hujielewa, huelewa wengine na ulimwengu
Huheshimiana
Huweza kutumia raslimali vilivyo
Elimu huondoa ujinga/ujuha
Mwanafunzi humakinika katika maisha ya baadaye
Msamiati

  • Leo si jana, jana si leo
  • Enda na ucheo, siende na uchwao

Elimu ya vitabu humsaidia mtu kuhifadhi siri ujumbe na kumbukumbu za kutumia na kizazi cha baadaye

Msamiati

  • Elimu huboresha maisha
  • Kujenga makao mazuri
  • Kuwasaidia jamaa na jamii
  • Elimu ni daraja la kuvusha mtu kwenye gange/kazi yenyefulusi nono
  • Mtu hupata hela za kujimudu pasi kuwategemea wengine
    Methali
  • Mtegemea cha nduguye hufa maskini
  • Mtegemea nundu haachi kunona
  • Mja hupewa heshima
    Ragba
  • Nimesimama imara kama chuma cha pua
  • Tisti kama ngarange za mvule
  • Kidete kama kitawi cha mkarakala
    Pongezi za dhati
  • Ninawapa mkono wa tahania kwa kufanya bidii za mchwa na duduvule
  • Nawamiminia shukrani sufufu
  • Ninawashukuru kwa kujitolea mhanga na kujifunga kibwebwe/masombo/kujikaza kisabuni

Methali

  • Elimu ni bahari
  • Elimu maisha si vitabu
  • Elimu ni taa gizani hung’aa
  • Elimu ni mali ambayo adui hawezi kuteka
  • Elimu bila mali ni kama nta bila asali

Tashbihi

  • Bidii za mchwa /duduvule
  • Ng’aa kama mbalamwezi
  • Pesa kama njugu
  • Julikana kama pesa

Misemo

  • Kujitolea mhanga
  • Shika usukani
  • Kuna kichwa
  • Ambua kitu
  • Tia pamba/nta


Mjadala

Insha sampuli hii huwa na sehemu mbili: Kuunga na kupinga
Mwanafunzi ana uhuru wa kuunga ama kupinga

Katika sehemu ya hitimisho mtahiniwa anatarajiwa kutoa mawazo yake

Tamati
Ningependa kuwajuza kuwa ______________
Ningeomba sote tupinge kwa jino na ukucha _____________
tusiwe kama chachandu wa kujipalia makaa kwa ______________

Teknolojia

Ni maarifa ya sayansi na matumizi yake katika mitambo, vyombo na zana katika viwanda, kilimo, ufundi na njia za mawasiliano
Mifano

  • Kilimo 
    Trekta   
    Beleshi   
    Pilau   
    Mbolea   
    Toroli   
  • Zana za vita   
    Manowari   
    Bazooka   
    Vifaru
    Darubini   
    Grunedi   
    Bunduki   
    Bastola
    Gomborora
    Nyambizi
    Mzinga
    Kombati
    Dirizi/dereya
  • Mawasiliano
    Simu – tamba/rununu/mkono
    Tarakilishi
    Tovuti
    Kitenzambali
    Barua meme
    Kikotoo
    Kimemeshi
  • Mitambo
    Kiyoyozi/feni/pauka/pangaboi
    Lifti/eleveta
    Kreni/winchi/kambarau
    Meli
    Ndege
    Mashua

Faida za Teknolojia

  • Mawasiliano – kupasha habari
  • Elimisha na kutumbuiza
    Methali
    Kipya kinyemi ngawa kindonda
  • Utafiti
    Kuvumbua dawa za ndwele/mitambo kurahihisha kazi
    Mitambo ya kuchunguza hali ya anga
  • Elimu
    Matumizi ya mitambo
    Kanda za video
    Methali
    Elimu ni bahari
    Elimu haitekeki
    Mali bila daftari hupotea bila habari
    Elimu bila mali ni kama sega bila asali
  • Usalama
    Zana za vita
    Donge nono hupatikana baada yakuuza vifaa
    Methali
    Tahadhari kabla ya hatari
    Kilimo na ufugaji
    Pembenjeo – mbegu, mbolea, dawa
    Ghala la kuhifadhi mazao
    Mashine za kukama ng’ombe
    Methali
    Tembe na tembe huwa mkate
  • Usafiri
    Vyombo vya majini, nchi kavu au barabara
    Kuokoa wakati na maisha
    Methali
    Ngoja ngoja huumiza matumbo
  • Mavazi
    Rahisisha kazi
    Kuimarisha uchumi wa nchi

Madhara

  • Mmomonyoko wa maadili
  • Huleta maradhi kama saratani
  • Huleta maafa
  • Punguza nafasi za kazi
  • Kuiga tabia za kigeni
  • Vita
  • Kuwafanya waja kulaza damu
  • Mambo mengine muhimu

Viunganishi vya insha ya maelezo

  • Licha ya
  • Fauka ya
  • Aidha
  • Zaidi ya
  • Pia isitishe
  • Mbali na
  • Hali kadhalika


Insha ya Mazungumzo

Mazungumzo ni maongezi, mahojiano ama malimbano baina ya mtu na mwengine au kundi moja na jengine
Yanaweza kuwa Porojo/soga/domo
Ni mazungumzo ya kupitisha wakati
Kutafuta ujumbe maalum
Hufanywa kwa njia ya mahojiano
Kudadisi au kumwelekeza mtu
Baina ya mtu na tajriba na Yule anayetakamsaada

  • Mhusika mmoja asichukue nafasi kubwa
  • Tumia alama za uakifishaji kama vile koloni, kitone na kipumuo
  • Sharti pawe na mahali pa kumchachawiza
  • Vitendo viweze kuandikwa katika alama za mabano
  • Fani za lugha zitumike ili kuleta uhondo
  • Pawe na maagano

Hatua

  • Mada/kichwa
    Huandikwa kwa herufi kubwa kupigiwa mstari
  • Maudhui
    Ni lengo au kusudi la mazungumzo
    Msamiati kutegemea lengo la mazungumzo
  • Vitendo na ishara
    Haya yataandikwa katika mabano (akitari, akilia, akicheka)
  • Alama za uakifishaji
    • Koloni( : ) Huandikwa baada ya jina au cheo cha watu
    • Alama za dukuduku ( _ _ _ ) Mazungumzo yanaendelea
    • Parandesi au mabano ( ) Kubana maneno ambayo hayatasemwa
    • Alama ya hisi ( ! ) Hutumiwa pamoja na viigizi kuonyesha hisia


Insha za Hadithi

Hadithi hutambiwa kwa njia ya kusimuliwa
Hurejelea matukio au visa vyenye nasaha kwa jamii
Visa hivi hutumiwa

  • Kuelimisha
  • Kushauri
  • Kuonya
  • Bidii
  • Kuonyesha umoja

Enzi za kale watoto walisimuliwa visa hivi na babu au nyanya wakati wa jiono
Mifano

  • Abunuwasi
  • Shamba la wanyama
  • Sungura mwenye pembe
  • Shujaa fumo liyongo

Ikiwa kisa kilisimuliwa na mwingine mwanafunzi atahitajika kunukuu kazi yake
Mfano
“ babu alizoea kutuambia ngano.alianza hivi ____________”

Baada ya kuhitimisha kisa mtahiniwa anahitajika kufunga
Ahitimishe kwa ushauri au nasaha

Insha hii yaweza kuchukua mikondo tofauti

  • Furaha
  • Majuto
  • Huzuni
  • Bidii

Tanbihi
Sanasana wahusika huwa wanyama ambao huwa na hisia za binadamu

Jinsi ya kuanzisha

  • Paukwa?pakawa!
  • Aliondokea chanjagaa kujenga nyumba kaka mwanangu mwana siti kijino kama chikichi cha kujengea vikuta na vilango vya kupitia
  • Hapo zama za zama _____________
  • Hapo kale ___________
  • Hapo jado aliondokea _____________
  • Enzi za konga mawe ______________
  • Miaka na dahari iliyopita ___________________
  • Katika karne za mababu na bibi zetu _____________________
  • Miaka na mikaka iliyopita _____________
  • Hadithi!hadithi! hapo zama za kale katika kaya/kijiji ______________

Fani za lugha

Takriri

  • Miaka na mikaka
  • Dhahiri shahiri
  • Hana hanani
  • Maskini hohehahe
  • Daima dawamu
  • Afriti kijiti

Misemo

  • Salimu amri
  • Shika sikio
  • Temea nasaha mate
  • Valia miwani
  • Tia kapuni
  • Mambo kuenda shoro
  • Kutojulia heri wala shari
  • Kuwa fremu ya mtu

Tashbihi

  • Roho ngumu kama paka
  • Zurura kama mbwa msokwao/mbwakoko
  • Tabia kunuka kama kindonda/beberu
  • Macho mekundu kama ngeu/damu
  • Kuchukua wekundu wa moto

Methali

  • Bendera hufuata upepo
  • Sikio la kufa halisikii dawa
  • Kutosikia la mwadhini wala la mteka maji msikitini
  • Nzi kufia juu ya kindonda si haramu
  • Maji hufuata mkondo
  • Aambiwaye akakataa hujionea

Ragba

  • Kabla ya mwadhini kuadhana adhna zake
  • Maji kwa pakacha
  • Julikana kwa ufedhuli
  • Kuwa sawa na kutumbutia maji
  • Andamana na makundi yenye mienendo benibeni
  • Heshima likawa neno geni kwake
  • Lala kitandani hoi akiwangoja pumzi yake ya mwisho
  • Lia kilio cha mbwa

Hitimisho

  • Nyanya/babu alitueleza bayana umuhumu wa
  • Hapo ndipo niliposandiki kuwa
  • Ulumbi wa ulidhihirika waziwazi kuwa
Join our whatsapp group for latest updates

Download Insha - Class 7 Kiswahili Revision Notes.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students