Thursday, 01 September 2022 08:58

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End term 2 2022 Set 2

Share via Whatsapp

Maswali 

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.

Amani ni uwepo wa hali     1    utulivu katika eneo fulani. Nchi     2     na amani     3     kichumi      4     raia wake huishi    5    . Ni jukumu la kila kutetea hali ya amani kwa vyovyote vile.     7     hatuwezi kuwaachia viongozi wa kidini na vyombo vya usalama pekee    8     wajibu huu muhimu.

  A B C D
1  na   wa   ya  kwa 
2  isiokuwa  kuskokuwa  lisilokuwa  isipokuwa
3  haiathiriki tu  huathirika tu   ikiathirika tu  itaathirika tu
4  mbali na  bali pia   ilhali  angaa
5  roho mkononi  shingo upande    mkono kinywani  moyo kifuani
6  mlowezi  mhaini   mdhamini  mzalendo
7  Papo kwa papo kamba hukata jiwe  chelewa chelewa utapata mwana  si wako   Kingana kinga ndipo moto  Hiari yashinda utumwa
8  kuutekeleza kuutelekeza  kuuteketeza  kuuelekeza


Sherehe zilihudhuriwa na     9    watu. Nyimbo za kitamaduni zilitamalaki kote    10           11     ngoma kwa ustadi mkubwa. Vijana wa shule      12       mashairi yenye mishororo mitatu, yaani     13      . Sherehe zilifana sana. Hata baada ya    14     niliondoka nikijivunia utamaduni wa jamii zetu. Ilikuwa sherehe ya    15   

  A B C D
9  kigaro kikubwa cha   umayamaya mkubwa wa   genge kubwa la  msoa mkubwa wa
10  Masogora  Malenga   Wajumu  Wazegazegà
11   wakicheza  wamecheza   walicheza  wangecheza
12   walilonga  walitamba   walisimulia  walighani
13   tathnia   thuluthi   tathlitha  tarbia
14   kujumuika   kufumukana   kutangamana  kufungamana
15   ndovu kumla mwanawe  nyani kuvaa miwani   mbwa apige mswaki  lila na fila kutangamana


Kuanzia swali la 16 puku 30, jibu kila swali kulingana na maagizo uliyopewa

 1. Chagua sentensi isiyoonyesha hali ya masharti
  1. Ungefika mjini ungejionea mambo mengi
  2. Mtoto akielekezwa vyema atakuwa mwadilifu
  3. Kikulacho ki nguoni mwako.
  4. Mimea ingalinyunyiziwa maji ingalinawiri
 2. Ainisha maneno yaliyoanagziwakatika sentensi ifuatayo:
  Wengi wamekuwa wakiharibu misitu kiholela.
  1. kiwakilishi, kivumishi
  2. kivumishi,kielezi
  3. kivumishi, kiwakilishi
  4. kiwakilishi, kielezi
 3. Andika wingi wa sentensi ifuatayo:
  Uwele uliovunwa utahifadhiwa katika ghala.
  1. Ndwele zilizovunwa zitahifadhiwa katika maghala.
  2. Uwele uliovunwa utahifadhiwa katika ghala.
  3. Mawele yaliyovunwa yatahifadhiwa katika ghala.
  4. Mawele yaliyovunwa yatahifadhiwa katika maghala.
 4. Chagua maelezo yaliyo sahihi.
  1. Bambo ni fimbo ya kutembelea lakini pambo ni kitu kinachoongeza uzuri.
  2. Tanga ni mkutano wa kupanga mazishi lakini danga ni maziwa ya kwanza ya myama aliyezaa.
  3. Kombo ni kukosa kunyooka lakini gombo ni sura moja ya kitabu.
  4. Zihi ni nguvu ya kufanya kazi lakini sihi ni hali ya kuwa na afya.
 5. Orodha gani ina msamiati wa aina moja.
  1. buli, uteo, kumbwewe
  2. zuhura, mirihi, almasi
  3. kekee, bisibisi. pimamaji
  4. kiwanja, kuli, plau
 6. Tegua kitendawili kifuatacho:
  Ana mikono lakini hawezi kushika kitu.
  1. Konokono
  2. nyuni
  3. maji
  4. upepo
 7. Buda ni kwa ajuza ilhali beberu ni kwa
  1. kikwara
  2. mbarika
  3. mtelea
  4.  mtamba
 8. Chagua kitenzi chenye kiwakilishi tu cha mtenda
  1. Tutawatembelea
  2. Alitujulisha
  3. Walituona
  4. Ulitutambulisha
 9. Ni sentensi gani iliyo katika wakati uliopita hali ya kuendelea?
  1. Mjomba alikuwa amebeba kikapu chenye matunda.
  2. Mwanahamisi atakuwa akiliwakilisha eneo lake.
  3. Juma alikiona kigari hicho kilipopita.
  4. Shemeji alikuwa akifua nguo zake nilipofika
 10. Ni sentensi ipi iliyoakitishwa ipasavyo?
  1. Shughuli zote, zile ulizotuachia, vimekarnilika.
  2. Mwalimu alituita ofisini mwake: alitaka kutushauri.
  3. "Kesi hii." alisema mlalamishi. "Imechukua muda mrefu."
  4. Wageni - wote wale - walioalikwa wamewasili.
 11. Kanusha: Mtoto akilelewa vyema atakuwa mwadilifu.
  1. Mtoto akilelewa vyema hatakuwa mwadilifu. 
  2. Mtoto asiolelewa vyema hatakuwa mwadilifu.
  3. Mtoto asipolelewa vyema hatakuwa mwadilifu.
  4. Moto asipolelewa vyema atakuwa mwadilifu.
 12. Ni sentensi gani iliyotumia karibu ya nusura?
  1. Maguri yaliegeshwa karibu na maktaba.
  2. Karibu Orenge aibuke mshindi wa mbio hizo. 
  3. Mkutano ulikuwa wa karibu watu hamsini?
  4. Siku ya michezo iko karibu kufika.
 13. Akisami 3/8 kwa maneno ni
  1. thuluthi nane
  2. khumusi tatu
  3. thumni tatu
  4. thuluthi tatu
 14. Nahuu gani imeambatanishwa ipasavyo na maana yake.
  1. Kula debe - aibika kwa kukosa kitu.
  2. Kula kisogo-kujifanya humwoni mlu.
  3. Piga shoti- pata hasara katika jambo.
  4. Piga taswira - eleza mtu ukweli.
 15. Sentensi ifuatayo imetumia tamathali gani za usemi?
  Timu hiyo ni jogoo, hufunga mabao kumi kila dakika.
  1. tashbihi, kinaya
  2. taswira.chuku
  3. sitiari, kinuya
  4. sitiari chuku

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali kuanzia nambari 31 mpaka 40

            Pasi alipojiunga na shule yetu, wengi tulimchukulia kama kijana wa kawaida tu aliyeletwa shuleni na kiu ya masomo. Sikuliona lolote la ajabu kwake kwani kimo, umri na hata sura yake illifanana na zetu kama shilingi kwa ya pili. Uwezo wake masomoni ulikuwa wa wastani kwa hivyo sikumchukulia tishio lolote kwa nafasi yangu ambapo nilikuwa na kifuambele wakati wote. Sio kwamba nilikuwa na kinyongo naye ila uhusiano wetu ulikuwa vuguvugu tu.
           
Kwa baadhi ya wanafunzi, Pasi alikuwa muujiza wa kame hii. Madhali alitoka mjini, wengi waliajabia waledi wake wa lugha ya kimombo na lugha ya vijana ambayo ni mseto wa Kiswahili. KIngereza si lugha ya mama. Hata mimi binafsi nilijiona kama limbukeni mbele yake hususan kwa kuwa nilisitasita wakati wa kunena nilipojaribu kutema msamiati mwafaka wa kutumia. Wengi tulijitahidi kutumia Kingereza kwa ufasaha ilimradi tumridhishe Pasi. Nililobaki kujivunia zaidi ni ugwiji wangu wa Kiswahili ambuo niliuonea fahari siku zote.
            Si hayo tu yaliyowapumbaza wengi kumhusu Pasi. Maarifa yake kuhusu filamu mbalimbali, vifaa vya kidijitali na vipindi vya runingani hayakuwa na mshindani. Wakati wa buraha na hata katika haadhi ya vipindi vya masomo, wanafunzi wengi walimzingira jinsi siafu wamzungukavyo mdudu mfu kwani hawakusema wasemao mtegemea nundu haachi kunona? Jitihada za kiranja wa darasa za kuwatuliza ziliambulia kidole gutu. Hapo ilibidi niingilie kati nikawakumbusha kuwa mwangata mbili moja humponyoka. Wengine wakanitupia jicho upembe lakini walipoona nimesimama kidete wakarudi kwenye madawati yao.
            Haukupita muda mrefu tulipoanya mtihani wetu wa kaatikati ya muhula. Wanafunzi wengi hawakuweza kutimiza malengo yao. Kuna wale waliojiasa wakaanza kuinamia cha mvunguni. Hata hivyo, asilimia kubwa ilijitia hamnazo kucheza ngoma watakazo. Hawa walikuwa chombo cha kuzama ambacho hakina rubani.
Pasi aliwapa siri mpya ya kukabiliana na hali yao. Idadi ya wafuasi wake sasa iliongezeka maradufu. Kila mara alipokuwa nje ya darasa, aliandamwa kama imamu na maamuma wake. Hapo alijiona kama jemedari mwenye jeshi kubwa. Wafuasi hawa walishaanza kuigiza ile lugha ya kiongozi wao. Matokeo yao nayo yaliendelea kudidimia dididi japo hakuna kati yao aliyeonekana kujali togo wala jando.
            Mambo yalipomfikia mwalimu wa darasa kooni, alikata shauri kupeleleza kiini cha hali hii. Uchunguzi wake ulibaini kwamba Pasi na genge lake lilikuwa likibugia dawa haramu. Alimfikishia kinara wa shule taarifa hiyo naye hakusita kuwaita wavyele wa vijana hawa. Kwa kuelewa kuwa mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo, wazazi walirauka na kufika hata kabla ya wakati waliopangiwa. Vijana waliitwa kadamnasi wakasomewa mashtaka ambayo walikiri kwa fedheha. Ungaliwaona walivyoshusha nyuso kwa tua usingalikosa kuwaonea shufaka.
            Kikao kilipomalizika ilipitishwa kwamba idara ya ushauri nasaha iwashughulikie vijana hawa. Hapo ndipo liliponijia wazo la kuanzisha kilabu cha ushauri wa marika shuleni. Amini usiamini! Pasi na wafuasi wake ndio waliokuwa wafuasi wa kwanza wa kilabu kile waliamua kutupa jongoo na mti wake. Hata ninapovuta taswira na kuona hatua zilizopigwa hadi kulikweza jina la shule yetu kileleni, fahari hunivaa hata nikajipata nikishusha pumzi kwa bashasha.

 1. Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza
  1. Uwepo wa Pasi katika shule ya msimulizi uliwashangaza wengi
  2. Sare na umri wa Pasi ulimfanya msimulizi kumpuuza Pasi
  3. Pasi hakuweza kufanya vyema katika masomo yake shuleni.
  4. Kuja kwa Pasi hakukuathiri utendaji wa msimulizi darasani.
 2. Uhusiano wetu ulikuwa vuguvugu tu ndiko kusema.
  1. Msimulizi nu Pasi hawakuweza kupatana.
  2. Uhusiano wa Pasi na msimulizi ulikuwa wa kawaida
  3. Msimulizi alihofia nafsi yake kunyakuliwa na Pasi.
  4. Uhusiano wa Pasi na msimulizi ulikuwa motomoto.
 3. Maelezo yapi ni kweli kuhusu Pasi kwa mujibu wa kifungu hiki?
  1. Alikuwa na welewa mzuri ya Kiingereza, Kiswahili na lugha ya mama.
  2. alikuwa bingwa wa Kiswahili na teknolojia ya kisasa.
  3. Alikuwa na ujuzi wa kidijitali licha ya udhaifu katika lugha ya Kiswahili.
  4. Alikuwa mwenye bidii licha ya kutofanya vyema masomoni.
 4. Si kweli kusema kuwa,
  1. msimulizi alikuwa kielezo darasani kwa mambo yote.
  2. zipo nyakati ambapo msimulizi alijiona duni mbele ya Pasi.
  3. wale waliompuuza Pasi hawakuathirika masomoni.
  4. msimulizi alikuwa mweledi wa lugha ya Kiswahili.
 5. Methali mtegemea nundu haachi kunona ina maana kuwa
  1. waliomfuata Pasi waliishia kufanya vibaya darasani
  2. waliomfuata Pasi walijifunza mengi kuhusiana na teknolojia. 
  3. waliompuuza Pasi walipoteza nafasi ya kuuona ukakamavu wake.
  4. waliompuuza Pasi walijikosesha nafasi ya kujiimarisha kwa vifaa vya kidijitali.
 6. Msimulizi
  1. hana marafiki darasani mwake.
  2. anaogopwa na wanafunzi kwa ukali wake.
  3. alikuwa kiranja wa darasa lake.
  4. ni mwenye kipawa cha uongozi.
 7. Baada ya mtihani wa katikati ya muhula.
  1. Msimulizi na wenzake hawakutimiza malengo yao.
  2. Pasi na baadhi ya wanafunzi walibadili hulka zao.
  3. Wanafunzi waliotambua kosa lao walianza kujibidiisha..
  4. Waliotia masikio nta walianza kujiimarisha
 8. Wazazi wa vijana waliohusika
  1. walijua umuhimu wa kuziba ufa. 
  2. ni wachelea wana kulia.
  3. wanakataa mwito bali si waitiwalo.
  4. wamepuuza malezi bora ya wana.
 9. Jambo linalomtia fahari mwandishi wa kifungu hiki ni
  1. kujiona akiwa kidede katika darasa lake.
  2. mchango wake katika kuinua hadhi ya shule.
  3. idadi ya vijana waliojiunga na kilabu chake.
  4. hatua alizochukua za kuripoti maovu.
 10. Neno kiini jinsi lilivyotumika lina maana ya,
  1. moyo wa kitu.
  2. undani wa jambo.
  3. chembechembe za kitu. 
  4. matokeo ya hali.

Yasome makala hawa wanaofuata kishu wiibu maswali kuanzia namba 41 mpaka 50

            Zaraa ni uti wa mgongo wa mataifa mengi ikiwemo Kenya. Viwanda vingi nchini hutegemea kilimo kupata malighafi yake. Aidha, taifa haliwezi kujilisha ikiwa shughuli za kilimo zitapewa mgong.  Licha ya umuhimu wa sekta hii, mkulima, ambaye ndiye nguzo muhimu, anaendelea kukabiliwa na matatizo atinati yanayokwamisha juhudi zake.
            Mojawapo ya matatizo yanayomzonga mwanazaraa ni ukosefu wa ushauri unaohitajika. Wataalamu wanaotarajiwa kumshauri mkulima kuhusu nija bora za kuzalisha na kuongeza pato lake ni haba akilinganishwa na idadi ya wale wanaohitaji nasaha yake. Walioko nao wanakwamishwa na mambo tofauti. Mathalani, utawapata hawaendi nyanjani ili kukutana na wakulima kwa kuwa hawana usafiri. Iwapo usafiri upo, huenda petroli ikawa ni kizungumkuti.
            Halikadhalika baadhi ya wataalamu huwa ni walaza damu na mafisadi. Kuna wale wanaofika ofisini na kushinda kutwa nzima wakisoma magazeti huku wakijaza mirabu, wakicheza bao au karata. Kuna wale ambao huangika koti au sweta kitini ili waonekane kuwa bado wapo na kisha kutokomea kuenda kushughulika masuala yao ya kibinafsi yanayohusu ndewe wala sikio kazi waliyoajiriwa kufanya.
            Ukosefu wa sera mwafaka kuhusa ardhi nao ni suala jingine linalotatiza kilimo nchini. Serikali haijaweka sera mahsusi kuhusu matomizi ya ardhi.  Waja wengi huongozwa na ta jamaa zao. Taratibu hizi kupendekeza ugawaji wa ardhi kwa minajili ya urithi kulingana na warithi waliopo. Si ajabu kuwa kote nchini ardhi inayofaa kwa kilimo imekatwakatwa vipande vidogovidogo ambavyo haviwezi kuwa na faida kwa zaraa.
            Kushindwa kwa mkulima kuongeza virutubishi ardhini ni changamoto nyingi inayokabili kilimo nchini. Ulimaji wa kile kipande miaka nenda miaka rudi minghairi ya kukipa nafasi ya kupumzika huufanya udongo kupoteza virutubishi muhimu vinavyohitajika na mimea. Ili kutatua tatizo hili, wakulima wengi hukimbilia mbolea za kisasa ambazo badala ya kuwasaidia huwaongezea madhila. Mbolea hizi zinatumbulika kuchangia uchafuzi wa mchanga na ardhi.
            Mabadiliko ya hali ya anga yamemfanya mkulima kushindwa kupanga wakati anaotakiwa kutayarisha shamba, kupanda, kupalilia, kunyunyizia dawa na kadhalika. Mvua imekuwa adimu. Badala yake panakuwa na vipindi virefu vya kiangazi ambavyo huathiri bidii za mkulima. Maji nayo yanaendelea kupungua na mkulima hawezi kukimu mahitaji ya unyunyiziaji wa maji shambani.
            Maradhi pamoja na wadudu waharibifu kama vile viwavi, kupe, na mbung'o ni changamoto nyingine inayotatiza juhudi za mkulima nchini. Haya hupunguza uzalishaji katika kilimo au wakati mwingine kupunguza mimea au mifugo wao.
            Mbali ya haya ukosefu wa chete, matatizo ya uchukuzi, gharama ya juu ya uzalishaji na mashindano tobana na bidhaa za nje ni changamoto kubwa. Mkulima wa Kenya anahitaji msaada wa dharura ili aweze kunyanyua kilimo. Lau haya hayatafanyika, uchumi wetu utaendelea kudidimia

 1. Maneno, zaraa ni uti wa mgongo wa taifa yana maana kuwa
  1. kilimo kimepewa kipaumbele nchini.
  2. umuhimu wa kilimo unajulikana kote nchini.
  3. kilimo kinategemewa sana nchini.
  4. manufaa ya kilimo yanaendelea vyema nchini.
 2. Viwanda vinahusianaje na kilimo nchini?
  1.  Mazao ya shambani huishia kupelekwa viwandani.
  2. Mali ya kuundia bidhaa mbalimbali hukuzwa mashambani.
  3. Viwanda vya kuundia bidhaa aghalabu hujengwa mashambani.
  4. Mbegu zinazokuzwa mashambani huhifadhiwa viwandani.
 3. Chagua kauli sahihi kulingana na hii nakala
  1. Njia mbovu za usafiri zina madhara kwa kilimo.
  2. Kuwepo kwa vipindi vya kiangazi ni balaa kwa mkulima.
  3. Maafisa wote wa nyanjani hawana uwajibikaji.
  4. Ufisadi ukikomeshwa matatizo yote yataisha.
 4. Mwandishi anapendekeza sera ya ugavi wa ardhi iwe;
  1. waja wote wagawiwe viwango sawa vya ardhi.
  2. ardhi igawanywe vipande vidogovidogo ili viendeleze upesi.
  3. watu wakiuke tamaduni zao ili wagawiwe ardhi.
  4. vipande vikubwa vya ardhi vitengwe ka minajili ya kilimo.
 5. Yote haya hupunguza rotuba ardhini isipokuwa
  1. kulima shamba moja kwa bidii mwaka baada ya mwaka.
  2. matumizi ya mbolea vinazotoka viwandani kwa wingi.
  3. kuzingatia njia za utaalamu wa kilimo
  4. kumomonyoka wa udongo katika sehemu husika.
 6. Uhaba wa mvua kwa kawaida huchangia
  1. mafuriko
  2. kiangazi
  3. vuli
  4. ukame.
 7. Upi ni utaratibu mwafaka wa matayarisho shambani?
  1. Kupanda, kulima, kupalilia, kuvuna.
  2. Kuvuna, kulima, kupanda, kupalilia
  3. Kulima, kupanda, kupalilia, kuvuna.
  4. Kapalilia, kupanda, kulima, kuvuna.
 8. Lipi halijatajwa kama tatizo mojawapo la mkulima?
  1. Ukosefu wa soko la mazao.
  2. Kutatizwa na wadudu waharibifu.
  3. Kubadilika kwa utaratibu wa majira.
  4. Uhaba wa bidhaa za masoko ya nje.
 9. Kulingana na aya ya mwisho, mwandishi anasema kuwa,
  1. sharti wakulima waungane kuimarisha kilimo. 
  2. wakulima wakipigwa jeki uchumi utaimarika.
  3. kilimo kimechangia kudorora kwa taifa letu.
  4. wakulima watafute njia mbadala za kusaka riziki.
 10. Neno kukimu lina maaya ya
  1. kutosheleza
  2. kupata
  3. kununua
  4. kuhifadhi

INSHA 

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Malizia insha kwa maneno yafuatayo huku ukiifanya iwe ya kusisimua zaidi. 

..................... Ama kweli sherehe hiyo ilifana sana; kila mmoja aliondoka akisimulia matukio ya siku hiyo.

Majibu

 1. C
 2. D
 3. A
 4. B
 5. A
 6. D
 7. C
 8. A
 9. B
 10. A
 11. C
 12. D
 13. C
 14. B
 15. A
 16. C
 17. D
 18. D
 19. A
 20. C
 21. B
 22. B
 23. A
 24. D
 25. A
 26. B
 27. C
 28. C
 29. A
 30. D
 31. D
 32. B
 33. C
 34. A
 35. B
 36. D
 37. C
 38. A
 39. B
 40. B
 41. C
 42. B
 43. A
 44. D
 45. C
 46. D
 47. C
 48. D
 49. B
 50. A

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End term 2 2022 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students