Wednesday, 25 January 2023 08:37

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Term 1 Opener 2023 Set 2

Share via Whatsapp

 MASWALI    

Soma vifungu vifuatavyo. Fina nafasi mpaka 15. kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya uliyopewa.

Katika baadhi ya ___1___ humu nchini, tatizo la uhaba wa maji ___2___ kuwaka kama ___3___. Wakazi wa maeneo hayo ___4___  changamoto kwani bei ya maji nayo imepanda maradufu. Wanaochuuza maji mitaani kwa ___5___ nao hawana ___6___  kwani ___7___ wakazi wa maeneo hayo na ___8___, wamepandisha bei ya bidhaa hiyo muhimu bila chembe ya hisia.

   A   B   C   D 
 1.   magatuzi   gatuzi   mataifa   mabara 
 2.  yanaendelea   inaanza   linaendelea   unazidi 
 3.  jua la mtikati  moto wa kifuu   hasira za mkizi   upepo wa tufani 
 4.  wamekumbwa   wamekumbana   wamekumba   wamekumbwa na  
 5.  mkokoteni  manowari   rukwama   helikopta 
 6.  amani  mioyo   shukrani   imani 
 7.  hawahurumii  hawawahurumii   hawawahurumi   hawahurumi 
 8.  badala yake  baada yake  kabla yake  mahali pake

 

Elimu ina ladha yake. Ingawa haihisiki kwa ulimi, utamu upo ___9___. Nasema hivi kwa sababu nimeyaona manufaa ya elimu. Nina uwezo wa kutambua maradhi kama ___10___ ambayo huambukizwa na ___11___ na mashairi ya aina nyingi kama vile ___12___ ambapo mshororo wa tano hukamilisha kila ___13___. Licha ya hayo, nimewafahamu wafanyakazi mbalimbali. ___14___ kuwa mfanyakazi anayeshughulikia mitambo ndiye
___15___

   A   B   C   D 
 9.   Ukiujua huu na huu huujui    Elimu ni taa, gizani huzagaa    Aisifuye mvua imemnyea   Msema pweke hakosi 
 10.   malaria  malale   Ukimwi   Korona 
 11.  chawa  kukohoa   ngono   mbung'o 
 12.  takhmisa  tarbia  tathlitha   tathmina 
 13.  mizani  ubeti   kina   ukwapi 
 14.  Ninamjua  Namjua   Ninafahamu   Ninamfahamu 
 15.  mwandishi  mhandisi   injini   sogora 

 

Kutoka swali la 16 hadi 30. jibu swali kulingana na maagizo.   

  1. Chagua sentensi yenye tanakali ya sauti.
    1. Lo! Kumbe alikuwa shangazi yake!
    2. Wanafunzi walisoma kutwa kucha.
    3. Sarafu ilianguka mchangani tifu! 
    4. Baba wa Juma ni mkali kama simba.
  2. Chagua kiwakilishi katika sentensi hii.
    Kijana huyu ni mzuri kushinda yule.
    1. yule
    2. mzuri
    3. huyu
    4. kushinda
  3. Tumia kirejeshi amba badala ya o-rejeshi.
    Wanafunzi waliofuzu vizuri walizawidiwa.
    1. Wanafunzi ambao waliofuzu vizuri walizawidiwa.
    2. Wanafunzi ambao walifuzu vizuri walizawidiwa.
    3. Wanafunzi ambaye walifuzu vizuri walizawidiwa.
    4. Wanafunzi ambayo walifuzu vizuri walizawidiwa.
  4. Kamilisha methali:
    Mwana wa kuku hafunzwi
    1. kuriaria
    2. kutembea
    3. kuchakura
    4. kupuruka
  5. Chagua majina yaliyo katika ngeli ya YA-YA pekee.
    1. Maumbo, maktaba, mate.
    2. Makawa, matatu, maji.
    3. Maradhi, maskanini, makavazi.
    4. Mafuta, mazingira, mauti.
  6. Ni neno gani halijaambatanishwa ipasavyo na jibu lake?
    1. Buriani  -  inshallah
    2. Makiwa  -   tunayo
    3. Alamsiki  -  binuru
    4. Sabalkheri  -  aheri
  7. Chagua sentensi iliyotumia o-rejeshi tamati kwa usahihi.
    1. Wageni wanaokuja ni wetu.
    2. Wanafunzi watakaotutumbuiza waje hapa mbele.
    3. Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
    4. Waliotuzwa wawape nafasi wengine watuzwe.
  8. Chagua sentensi sahihi kutokana na maneno haya:
    Kitabu, cha, nipe, vitate, hiki
    1. Nipe vitate cha hiki kitabu. 
    2. Kitabu hiki cha vitate nipe
    3. Nipe hiki kitabu cha vitate.
    4. Nipe kitabu hiki cha vitate.
  9. Makia ya mabuzi haya ni mafupi katika wastani ni
    1. mkia wa mbuzi huyu ni mfupi.
    2. mikia ya mbuzi hawa ni mifupi.
    3. mikia ya mbuzi hao ni wafupi.
    4. mkia wa mbuzi huyo ni mfupi.
  10. Ni ipi ala ya muziki kati ya maneno yafuatayo?
    1. Parapanda
    2. Manati
    3. Manowari
    4. Nyambizi
  11. Kanusha:
    Ningeenda ningempata akipepeta pojo kwenye ungo.
    1. Singeenda singempata akipepeta pojo kwenye ungo.
    2. Nisingeenda singempata akipepeta pojo kwenye ungo.
    3. Nisingeenda nisingempata akipepeta pojo kwenye ungo.
    4. Nisingeenda nisingepata akipepeta pojo kwenye ungo.
  12. Tegua kitendawili.
    Wanashindana wakifuatana.
    1. Kufuli
    2. Samaki
    3. Mtu na kivuli
    4. Magurudumu
  13. Chagua jibu linaloonyesha sifa iliyoundwa kutokana na nomino.
    1. Saka  -  msasi
    2. Ushujaa  -  shujaa
    3. Cheza  -  mchezo
    4. Lipa  -   malipo
  14. Chagua neno lenye sauti changamano.
    1. Mtoto
    2. Watoto
    3. Mwavuli 
    4. Wayo
  15. Upi ni usemi halisi wa sentensi ifuatayo?
    Maono alisema kuwa alikuwa akiwachukia waliowaajiri watoto.
    1. Maono alisema, "ninawachukia wanaowaajiri watoto.
    2. Maono alisema, "Ninawachukia wanaowaajiri watoto."
    3. Maono alisema, mimi siwapendi wanaowaajiri watoto.
    4. Maono alisema anawachukia wanaowaajiri watoto.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 hadi 40.   

Ajali za barabarani nchini zimeongezeka maradufu. Swali ni je, nani aelekezewe kidole cha lawama? Ni serikali, ni madereva au ni sisi wasafiri? Hiki kimebaki kitendawili kisichoweza kuteguliwa. Kila siku utasikia kutoka kwenye vyombo vya habari watu walioaga dunia kutokana na ajali. Hili ni jambo la kuatua moyo hasa kwa wale wanaofiwa na wapenzi wao katika ajali.

Mojawapo ya kiini cha ajali barabarani kwetu ni barabara mbovu. Barabara zilizoharibika huchangia pakubwa katika kusababisha ajali. Mashimo yaliyojaa barabarani hufanya magari kuyumbayumba na kisha kupoteza mwelekeo. Mwishowe magari hugongana dafrau na hivyo kusababisha vifo vya watu wasiokuwa na hatia. Serikali yetu ina jukumu kubwa katika kukarabati barabara. Wawape kandarasi watu walio na ujuzi
katika ujenzi wa barabara.

Vilevile, magari yanayobeba abiria kupita kiasi husababisha ajali. Dereva na kondakta wake huwasomba abiria ukadhani ni mashehena ya mizigo. Lengo la haya yote ni ulafi wa pesa. Lawama hapa zinafaa kuelekezwa kwa madereva, makondakta na abiria. Ni sharti wenye magari wajali masilahi ya wasafiri, nao wasafiri ningewashauri kutoabiri magari yaliyojaa abiria.

Isitoshe, magari mabovu katika barabara zetu pia ni chanzo cha ajali. Si ajabu kuwaona madereva wakiyaendesha makatara barabarani. Magari hayo huharibikia mahali popote na wakati wowote. Waendeshaji hawa hujipa moyo na kujitetea kwa methali isemayo ukuukuu wa kamba si upya wa ukambaa. Hatua thabiti za kisheria zinafaa kuchukuliwa na serikali ili kuyaondoa magari ya aina hii. Tukumbuke kuwa kinga ni bora kuliko tiba. Aidha, tutahadhari kabla ya hatari.

Fauka ya hayo, madereva wasiohitimu huchangia katika kusababisha ajali. Wao huendesha magari bila kuhitimu. Labda waliwahonga wanaohusika na utoaji wa leseni. Hawajui ishara za barabarani. Kwa mfano, kivuko cha watoto na hata wanyama, barabara zenye matuta na pengine ishara ya kuonyesha kuruba. Wanaotoa leseni wanapaswa kuwajibika na kutoshiriki ufisadi.

Madereva waliotumia dawa za kulevya pia husababisha ajali. Uwezo wao wa kuona vyema huathirika kwa sababu ya vileo. Wao hawamakiniki wanapoendesha magari. Mihadarati pia huwafanya wengine kuendesha magari kwa kasi mithili ya duma. Wao husahau kuwa haraka haraka haina baraka.

Ni sharti sote tuungane mikono ili kukomesha ajali katika barabara zetu. Tukumbuke kuwa nia zikiwa moja, kilicho mbali huja. Sisi ndisi wenye nchi na kumaliza ajali kunatutegemea sisi.

  1. Katika aya ya kwanza, ni nani anastahili kulaumiwa kutokana na ajali?
    1. Madereva
    2. Abiria
    3. Hafahamiki
    4. Serikali
  2. Ni orodha ipi iliyo na vyombo vya habari pekee?
    1. Redio, televisheni, tishali. 
    2. Gazeti, redio, televisheni.
    3. Majarida, kiyoyozi, redio.
    4. Runinga, uyoka, magazeti.
  3. Barabara zilizoharibika husababishaje ajali?
    1. Magari huendeshwa kwa kasi na baadaye kuyumba.
    2. Magari huharibika, kuyumbayumba na kugongana.
    3. Magari hupoteza njia na kugongana. 
    4. Magari huyumbayumba na kuwagonga wapitanjia.
  4. Kwa nini madereva huwabeba abiria kupita kiasi?
    1. Mara nyingi wao huwa na haraka. 
    2. Abiria hupenda kubanana kama ndizi.
    3. Wao huwa na tamaa ya pesa.
    4. Viti huwa vichache mno magarini.
  5. Ni nini maana ya methali ukuukuu wa kamba si upya wa ukambaa?
    1. Tusidharau vitu vya zamani kwa kutamani vipya.
    2. Vitu vya zamani huwa tofauti na vipya.
    3. Tusividunishe vitu vipya kwani vina faida nyingi.
    4. Vitu vya zamani huwa si vizuri kama vipya.
  6. Madereva wasiohitimu huwezaje kupata leseni?
    1. Huzinunua kutoka madukani.
    2. Hupewa na maafisa wa trafiki barabarani.
    3. Hutoa hongo.
    4. Hupewa na serikali.
  7. Kulingana na ufahamu, mihadarati husababisha haya yote ila
    1. shida za kutazama barabarani.
    2. madereva kuugua magonjwa yatokanayo na dawa za kulevya.
    3. madereva kukosa uangalifu wanapoendesha magari.
    4. magari kuendeshwa kwa kasi.
  8. Unafikiri ni njia ipi mwafaka ya serikali kuhakikisha kuwa magari yameendeshwa kwa mwendo wa kadiri?
    1. Kuwa na maafisa wa trafiki katika kila mji nchini.
    2. Kuandaa semina kuwahamasisha abiria.
    3. Magari kutiwa vidhibitimwendo.
    4. Kutoa adhabu kali kwa abiria wanaoabiri magari yaliyojaa abiria.
  9. Ni ushauri upi uliotolewa kwa wale wote wasababishao ajali?
    1. Kuwafahamisha askari wa trafiki kasoro yoyote ya madereva.
    2. Kutowahonga wanaotoa leseni.
    3. Kutoabiri magari yaliyojaa wanaposafiri.
    4. Kuchukua tahadhari wanaposafiri.
  10. Kichwa kinachofaa zaidi ufahamu huu ni kipi?
    1. Athari za ajali barabarani.
    2. Chanzo cha ajali barabarani.
    3. Njia za kuzuia ajali barabarani.
    4. Ufisadi katika sekta ya uchukuzi.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 hadi 50.   

Vumilia alikuwa mtoto wa kike. Alikuwa kifunguamimba katika familia ya mzee Juhudi. Baba wa Vumilia alikuwa maskini wa mali lakini tajiri wa moyo. Alifanya kazi za kijungujiko kuwakimu wanawe na mkewe ambaye walichukuana kama sahani na kawa. Wazee wa vumilia walikula yamini kufanya kila waliloweza ili kumrithisha mwana wao ufunguo wa maisha.

Vumilia alipohitimu darasa la nane, wazazi wake walichochea ari yake ya kufuzu maishani kwa kutumia mifano halisi ambayo Vumilia aliielewa. Wazee hao walimkumbusha binti yao kuwa bidii, utiifu, uvumilivu pamoja na heshima na uadilifu vilikuwa siri kubwa ya fanaka. Naam! Ilibainika kuwa samaki hukunjwa angali mbichi.

Binti wa watu alipopasuliwa mbarika, alikuwa kama mbwa aliyeonyeshwa ufuko, akakataa abadan katan kufa maji. Aliongeza bidii maradufu katika masomo yake na kuwa kama anayetegemea kisomo kuishi. Waliosema kuwa bidii hulipa hawakukosea. Mtihani ulipofanywa na matokeo kutolewa, Vumilia aliwaacha wengi vinywa wazi kwa kuwa alikuwa amewashinda watahiniwa wote nchini.

Halikuwa la mjadala tena. Anayechovya asali hachovyi mara moja. Vumilia hakulegeza kamba wala kuangalia nyuma. Makini yake yalikwama masomoni. Licha ya kuwa kijana, alikataa kuwa bendera ya kufuata upepo. Alimakinikia ndoto yake ya kuwa mhasibu ili kuwaauni wazee wake kama njia ya kushukuru kwa yote waliyoyatenda. Wafadhili wake waliridhishwa na hatua yao ya kumfadhili Vumilia tangu shule ya msingi hadi chuo kikuu.

Hewaa! Hayawi hayawi huwa. Tunapozungumza sasa, Vumilia ni mhasibu mkuu katika benki kuu ya Tulizeni. Amewajengea wazee wake kasri na kuhakikisha kuwa wanapata kila wanalohitaji. Daima huwasomesha wadogo wake na kuwahimiza kufanya bidii za duduvule wakifahamu mno kuwa jasho la leo ndilo faraja ya kesho.

  1. Ni kweli kusema kuwa katika familia ya mzee Juhudi
    1. Vumilia alikuwa mtoto wa pekee.
    2. Vumilia alikuwa yatima aliyefadhiliwa.
    3. kulikuwa na watoto kadhaa.
    4. Vumilia hakuwa na wanuna wowote.
  2. Kifunguamimba ni sawa na
    1. mwanambee.
    2. ndugu mdogo.
    3. mtoto wa pekee
    4. mtoto wa mwisho.
  3. Wazazi wa Vumilia waliichochea ari yake
    1. alipokuwa katika shule ya msingi.
    2. baada ya kumaliza masomo ya sekondari.
    3. alipokuwa katika chuo kikuu.
    4. alipomaliza masomo ya msingi.
  4. Ni sifa gani ambayo wazazi wa Vumilia hawakumfunza kama siri ya fanaka?
    1. Bidii.
    2. Utiifu.
    3. Ujanja.
    4. Uadilifu.
  5. Katika kidokezi samaki hukunjwa angali mbichi, anayelinganishwa na samaki hapa ni
    A. vumilia.
    B. wazazi.
    C. walimu.
    D. wanuna wa Vumilia.
  6. Kilichomwezesha Vumilia kupita vizuri katika mtihani wa darasa la nane ni
    1. utajiri wa wazazi wake. 
    2. hali ya umaskini wao.
    3. ushauri wa wazazi wake.
    4. mtihani kuwa rahisi.
  7. Vumilia alikuwa tofauti na vijana wenzake kwa kuwa
    1. hakushawishika kufuata mkondo mbovu.
    2. aliamua kuwa mhasibu.
    3. alisoma hadi chuo kikuu. 
    4. aliwafaa wazaziwe baadaye.
  8. Amewajengea wazee wake kasri ni 
    1. nahau.
    2. tanakali ya sauti.
    3. istiara.
    4. tashbihi.
  9. Wafadhili wa Vumilia
    1. walijutia uamuzi wao.
    2. walimwonea fahari Vumilia. 
    3. walimwonea wivu Vumilia.
    4. walisikitikia mafanikio ya Vumilia.
  10. Methali gani inayoweza kutumiwa kufupishia ujumbe wa ufahamu huu? 
    1. Heri nusu shari kuliko shari kamili.
    2. Mali bila daftari hupotea bila habari.
    3. Hasara humpata mwenye mabezo. 
    4. Mvumilivu hula mbivu.

MARKING SCHEME

  1. A
  2. C
  3. B
  4. D
  5. C
  6. D
  7. B
  8. A
  9. C
  10. B
  11. D
  12. A
  13. B
  14. C
  15. B
  16. C
  17. A
  18. B
  19. C
  20. D
  21. A
  22. C
  23. D
  24. B
  25. A
  26. C
  27. D
  28. B
  29. C
  30. B
  31. C
  32. B
  33. C
  34. C
  35. A
  36. C
  37. B
  38. C
  39. D
  40. B
  41. C
  42. A
  43. D
  44. C
  45. A
  46. C
  47. A
  48. C
  49. B
  50. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Term 1 Opener 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students