Wednesday, 29 March 2023 13:27

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 6

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma vifungu situatavyo. Vina nafasi I mpaka 15. Kva kila pengo umepeva majibu manne. Chagus jibu lifaalo zaidi.

Waba ni ......................1......................Maradhi haya huwaambukia hususan waja ambao......................2.....................usafi wa vyakulana maji katika ulaji wao. Ulaji wa vyakula vilivyopikwa vizuri na unywaji wa maji .......................3.................... ....................4.......................mara kwa mara lakini wengi wanaonekana ....................5....................... dhidi ya wazo hili. Mapuuza haya yamesababisha hasara kubwa. .........................6.................. kutapika na kuendesha sana ni hatari zaidi kwa maisha ya mwanadamu .......................7.................... Watu wasipochukua tahadhari hususan dhidi ya unywaji wa maji machafu ukongo huu.......................8.................... ya adinasi wengi.

  1.                              
    1. ugonjwa wa kuambukiza wa kuhara na kutapika sana
    2. ugonjwa wa kuambukiza kutokana na maji maji yanayomtoka mtu
    3. ugonjwa unaosababishwa na kuumwa na mbu wa kike
    4. ugonjwa wa kuambukiza unaomfanya mtu kukohoa na kutema damu
  2.                              
    1. wanatumia
    2. hawachachawizwi 
    3. wanazingatia
    4. hawazingatii
  3.                      
    1. masafi
    2. machafu
    3. safi
    4. chafu
  4.                          
    1. kumekuwa kukisisitizwa 
    2. umekuwa ukisisitizwa
    3. yamekuwa yakisisitizwa
    4. imekuwa ikisisitizwa
  5.                
    1. kutiatia na kutoatoa
    2. kuvalia njuga
    3. kukata shauri
    4. kutia nta masikioni
  6.                        
    1. Hapa
    2. Hio
    3. Kule
    4. Hiyo
  7.                                    
    1. yeyote
    2. wowote
    3. yoyote
    4. chochote
  8.                  
    1. yanawadhuru
    2. utawadhuru
    3. inawadhuru
    4. yatawadhuru

Mali yaliyokuwa .................9................ na bwana Bwale yalimfanya mwanawe  ...............10.................. na kukataa kuendelea kusoma. Kijana huyu, kwa kulelewa katika ukwasi mkubwa, majivuno  .................11................ Aliwadharau waadhiri na wale wa rika lake. Heshima kwake ilikuwa  ................12................. Tabia hizi zilisababisha wana wa hirimu yake ................13................. kama mwasiriwa wa ukoma. Kwa kuwa hakuwa na manufaa yoyote .................14................Aligeuka na kuwa mkia wa mbuzi. Wazazi wake walijaribu kuficha ................15................. cha mwana wao bila kujua kuwa tunda likioza ni sharti linuke fee!

  1.                          
    1. yamepeana
    2. yametwaliwa
    3. yamekabidhiwa
    4. yamehodhiwa
  2.                            
    1. kuvimba kichwa
    2. kuasi ukapera
    3. kuuma uzi barabara
    4. kujikaza kisabuni
  3.                
    1. yalimvaa kama liliwala
    2. yalimvaa kama kiko na digali
    3. yalimvaa na kinu bila mchi
    4. yalimvaa kama shetani
  4.                  
    1. mwiku
    2. mwiko
    3. desturi
    4. kawaida
  5.                
    1. walimpendelea
    2. walimwambaa
    3. walimpenda
    4. walimkataa
  6.                
    1. kwenu.
    2. kwetu
    3. kwake
    4. kwao
  7.                  
    1. mwendo
    2. kitiba
    3. mwenendo
    4. tabia

Kutoka swali la 16 hadi la 30. chagua jibu sahihi.

  1. Mbwa yule akikuona atabweka kishujaa.
    'ki' katika sentensi imetumiwa kuonyesha ................................. na ............................... mtawalia.
    1. masharti, nomino
    2. wakati, nomino
    3. masharti, namna
    4. wakati, namna
  2. Ni kundi lipi lenye sauti ghuna pekee?
    1. b, m, dh
    2. v, b, r
    3. gh, th, b
    4. sh, l, r
  3. Sentensi zifuatazo zinaweza kuunganishwa vipi kisahihi?
    Masden ni mzungu.
    Masden anazungumza Kiswahili sanifu.
    1. Masden ni mzungu maadamu anazungumza Kiswahili sanifu.
    2. Masden anazungumza Kiswahili sanifu licha ya kuwa yeye ni mzungu
    3. Masden ni mzungu madhali anazungumza Kiswahili sanifu.
    4. Masden anazungumza Kiswahili sanifu mighairi ya yeye ni mzungu.
  4. Chagua sentensi yenye kiwakilishi kimilikishi.
    1. Mtoto wako alichelewa ilhali wangu alifika mapema.
    2. Shamba lao lililimwa vizuri lakini hili halikulimwa kabisa.
    3. Mwanafunzi wa kwanza alituzwa lakini wengine waliahidiwa.
    4. Rais wa kwanza aliupigania uhuru lakini huyu aliinua uchumi.
  5.  Riba ni
    1. faida anayopata mtu aliyekopesha watu fedha ambayo ni ziada ya fedha aliyokopesha
    2. sehemu ya bei ya kitu inayotolewa mwanzoni.
    3. sehemu ya fidia anayolipwa mtu mwanzoni.
    4. sehemu ya malipo ya kukopea kitu mwanzoni.
  6. Chagua sentensi iliyo sahihi kisarufi
    1. Kibaka hicho ndicho kilichowatisha watu.
    2. Mabata wadogo waliyachezea maji.
    3. Kipepeo chochote chenye rangi hufurahisha.
    4. Shingo la Mwakideu linauma.
  7. Sehemu ya chini ya mguu kati ya vyanda na kisigino ni
    1. kisugudi
    2. utosi
    3. shavu
    4. wayo
  8. Tambua tashbihi inayofaa kukamilisha.
    Mwajuma ni msiri kama...
    1. giza
    2. mwizi
    3. kaburi
    4. kinyonga
  9. Akifisha ipasavyo
    Mwalimu aliwauliza kwa nini hamkukamilisha kazi kwa wakati.
    1. Mwalimu aliwauliza, "Kwanini hamkukamilisha kazi kwa wakati?"
    2. Mwalimu aliwauliza, "Kwanini hamkukamilisha kazi kwa wakati."
    3. Mwalimu aliwauliza "Kwanini hamkukamilisha kazi kwa wakati?"
    4. Mwalimu aliwauliza "kwa nini hamkukamilisha kazi kwa wakati."
  10.  Ni nini kinyume cha sentensi ifuatayo? "Jua lilipozama msichana alianua nguo." 
    1. Jua lilipopanda kijana alianika nguo.
    2. Jua lilipochomoza mvulana alianika nguo.
    3. Jua lilipozama kijana alianika nguo.
    4. Jua lilipochomoza msichana alianika nguo.
  11. Kitenzi 'lia' katika kauli ya kutendesha ni
    1. lilisha
    2. liliza
    3. lilishana
    4. liza
  12. Toti alikuwa akielekea upande wa kaskazini magharibi wakati wa asubuhi. Je, kivuli chake kilielekea upande gani?
    1. Kusini mashariki
    2. Magharibi
    3. Mashariki
    4. Kusini magharibi
  13. Ni sentensi gani kati ya zifuatazo imetumia kihisishi kifaacho?
    1. Poleni jamani! nyote mmekuwa washindi
    2. Aha! wewe usinikere hivyo
    3. Alhamdulilahi! Mterehemezi awajalie mema
    4. Acha! Umetuzwa tuzo bora zaidi
  14.  Mtu anayezitoa siri za nchi yake kwa nchi adui ni
    1. mkimbizi
    2. msaliti
    3. mlowezi
    4. mtoro
  15. Jibu maagano yafuatayo.
    "Buriani!"
    1. Buriani dawa
    2. Alamsiki
    3. Nawe pia
    4. Binuru

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40

Katika jiji la Tuleraha palikuwa na asilimia kubwa ya watu ikilinganishwa na maeneo mengine katika nchi ya Wakonga. Hapakuwa na mila wala desturi katika jiji lile. Wakonga walikuwa wametangamana kutoka maeneo yote ambapo palikuwa na zaidi ya makabila arubaini na mawili. Kila mmoja alitengana na mila zake punde tu alipogura mashinani. Watu wa Tuleraha waliiga mila za wazungu na wakawafuata wazungu namna bendera ifuatavyo upepo. Mitandao ya kijamii ndiyo iliyokuwa walimu wa vijana wengi pale. Chochote ambacho mzungu alifanya kilikuwa kinaonekana sawa. Mavazi yao ya Kiafrika waliyatupilia mbali, sisemi vyakula na ustaarabu wao. Wale wazee wachache waliojaribu kukuza utamaduni walionekana kuwa na kubaki nyuma kimaendeleo.

Kwa sababu ya kuiga zaidi mambo ya magharibi, jiji hili lilikuwa maarufu sana kwa anasa. Watu wa pale walijulikana kwa kupenda raha kupindukia. Ingawa walikuwa wachapa kazi, sehemu kubwa ya pato lao liliishia kwenye maeneo ya burudani kama vile katika mabaa na madanguro. Wengi wa watu hawa walikuwa wasomi wa ajabu. Palikuwa na taaluma kibao jijini kama ville: waandisi, madaktari, wanasheria, walimu na wengine. Mtu atadhani kuwa kule kusoma kungewapatia ustaarabu kumbe ndio waliopotoka zaidi kuliko mazuzu waliozitazama tu shule kwa mbali. Shahada, shahada za uzamili, shahada za uzamifu na uprofesa wao ungetumiwa bora zaidi kama maadili yale yangezin gatiwa.

Katika mazingira yale, vileo na dawa nyingine za kulevya ndizo zilikuwa starehe kamili. Palitokea binti mmoja aliyekuwa na aina mpya ya kileo alichouza kisirisiri. Kiliwavutia sana wanaume kwani kila wakati walitaka kumwona pembeni ili wafaidi kileo hicho cha faragha na kipya. Waliokionja waliishia kuwapelekea wake zao ambao walikifurahia bila kujua kilikuwa haramu. Vijana wadogo waliposikia habari za kileo hiki na utamu wake, walifanya juu chini kuona kuwa walipata fursa ya kukionja. Mzee Mkarara alikuwa na barobaro kwa jina Maraha na mjakazi aliyeitwa Sijali. Mkarara alipitia pale na kupewa sehemu yake.

Babake Maraha alipofika akiwa mlevi, hakusita kumwita Sijali kwani mkewe alikuwa safarini kikazi. Alimshawishi Sijali kukionja kileo kile kidogo na alipokataa, alimtishia kumwachisha kazi ndipo maskini binti wa watu akaridhia kuonja kwa madai kuwa iwe mara ya mwisho. Siku iliyofuata Sijali alimwita Maraha na kumshawishi kuonja kileo alichomwachia baba yake. Maraha aliona raha kweli.

Haukupita muda mrefu ikabainika kuwa kileo kile kilikuwa na madhara makubwa kwa mtumizi. Wote waliokitumia walianza kulalamika na walipopimwa, walipatikana na sumu fulani mwilini ambayo ilianza kuwaua polepole. Mke wa Mkarara alipopata habari akaamua kuwaita madaktari kuipima familia yake. Ajabu ni kwamba ni binti yake tu aliyeonekana salama kwani kila mtu alikuwa na sumu ile mwilini.

Alipoulizia Maraha alikiri kuonjeshwa na Sijali baada ya kupewa na babake, mzee Mkarara. Hata mkewe pia aliugua kwa kuambukizwa na mumewe. Jamaa nzima iliangamia kwa sumu ila Makini, binti yao aliyekataa katakata kuwa bendera. Wafu hawa wa familia ya Mkarara walizikwa kwa mazishi ya pamoja. Wale madaktari waliotambua sumu ile walikuwa kwenye maombolezo. Walipata nafasi na kuelezea kilichoangamiza familia ile. Walinadi kuwa walikuwa wamekunywa kinywaji ambacho kilikuwa kimetiwa madini yanayotumiwa kuhifadhi maiti ufuoni. Walisema kuwa sumu hiyo ilipoingia mwilini iligandisha damu na kusababisha saratani ya damu. Watu wengi walianza kubabaika kwani idadi kubwa ilikuwa imekionja kileo kile. Daktari aliwashauri wote waende wakapate vipimo kamili ili kubaini hali yao ya afya.

Yule 'mgema' alipoipata taarifa ile alichana mbuga. Alijua kuwa angeshikwa angekula kalenda kwa kuwagemea watu sumu. Serikali ilipitisha sheria kali dhidi ya vileo vile visivyohalalishwa. Isitoshe, muda wa starehe za mvinyo ulifupishwa wala si wakati wote ilivyokuwa awali. Serikali iliwashauri wakazi wa mji huo mkuu kuwajibika na kurudisha maadili mema lau jamii yote ingekwisha.

  1. Kulingana na aya kwanza
    1. wakazi wa Tuleraha walitoka sehemu ambazo hazikuwa na mila wala desturi 
    2. wazee wachache waliojua tamaduni waliruhusiwa kuwafunza wengine
    3. mambo mengi yaliyofanywa na wana Tuleraha yalichochewa na wazungu na uzungu
    4. tamaduni zilizotalikiwa si pamoja na mavazi, vyakula na ustaarabu
  2. "Mitandao ya kijamii ndiyo iliyokuwa walimu wa vijana wengi pale." Huku ni kumaanisha kuwa
    1. wanafunzi wengi walitumia mtandao kusoma
    2. nchi hiyo ilikuwa imepiga hatua kubwa kidijitali
    3. hapakuwa na walimu wa kufunza vijana katika nchi ile
    4. wakazi walitegemea na kuyafuata yaliyonadiwa mitandaoni
  3. Shahada ya uzamili ni shahada gani? 
    1. Ni shahada ya pili baada ya kupata shahada ya kwanza
    2. Ni shahada ya mwisho zaidi katika masomo
    3. Ni shahada inayotwaliwa na waandisi pekee
    4. Ni shahada ya tatu inayompatia mtu udaktari
  4. Kinywaji kinachozungumziwa katika aya ya tatu kilipendwa zaidi kwa kuwa
    1. kilikuwa kikiuzwa kisirisiri
    2. kilikuwa katika ile hali ya kunoga 
    3. kilitumiwa na wazee pamoja na vijana
    4. kilikuwa kinywaji kipya pale jijini
  5. Kijiji cha Tuleraha kilijulikana kwa sifa gani?
    1. Ulevi chakari
    2. Vileo chakari
    3. Raha chakari
    4. Madanguro chakari
  6. Ni ipi si sahihi kulingana na habari uliyoisoma?
    1. Watu wote waliangamia katika familia ile
    2. Binti wa mzee Mkarara ni Maraha
    3. Sijali alikionja kileo kile kwa kusurutishwa
    4. Maraha alionja kileo cha sumu
  7. Ni nani aliyemwonjesha Maraha kileo cha sumu?
    1. Karamka
    2. Makini
    3. Tuleraha
    4. Sijali
  8.  Ni kipi kilichokuwa kilele cha madhara ya sumu ile inayozungumziwa?
    1. Kuwapofusha watumizi
    2. Kusababisha watu kugandishwa damu
    3. Kusababisha mauko baina ya jamii.
    4. Kusababisha maradhi ya saratani
  9. Kulingana na taarifa uliyoisoma
    1. ni familia nyingi zilizoathiriwa na sumu ile
    2. familia nyingi huenda ziliathiriwa na sumu ile
    3. serikali ilijitia hamnazo kuhusu suala la sumu
    4. ni uajibikaji wa serikali tu utakaoiokoa jamii ile
  10. Ni kichwa kipi kinachofaa ufahamu uliosoma?
    1. Bendera hufuata upepo
    2. Raha nyingi ni karaha
    3. Kila kilevyacho si tembo
    4. Ulevi unamfaidi mlevi

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50

Bila shaka umewahi kusikia watu wakimtaja mwenzao kuwa ni mhalifu. Mimi kwa kweli neno hili uhalifu sielewi maana yake hasa. Labda nisake ushauri wa wataalam kama Bwana Hussaini Khali ambaye amebobea na kutopea kwenye lindi la uswahili. Naam! Imara ya jembe ka ingoje shambani.

Ama kwa kweli, uhalifu ni hali ya uvunjaji sheria za nchi au jamii. Kwa mintarafu hii anayevunja sheria moja kwa moja hujibatiza jina la mhalifu. Mhalifu ni mtu asiyependwa na wengi kwani anaaminika kuwa mtu wa kuvuruga staha za wenzake. Mtu kama huyu aghalabu huelekea kukosa hata mtu wa kumnasihi kwa namna watu wacheleavyo kushirikiana naye.

Pwagu aidha ni mhalifu, yeye huvunja amri isemayo asiibe. Atakuja kukujulia hali ukakaramka kuwa pako kutokea ajinabi kumbe amekuja kuchunguza jinsi hali yako ilivyo. Baadaye akishapata ramani ya maskani yako, hutokomea kuandaa kikosi cha wageni wasioheshimu wenyeji, Kwa kupumbazika na kutekwa bakunja na ubinadamu ghushi aliokuonyesha, utashtukia pamejiri mikasa na wizi wa mabavu na huenda ukapoteza hata uhai. Naam! Mgeni kumpokea kumbe ni kujihasiri.

Watu wanaowaajiri watoto wanavunja sheria hususan wale wanaowaadhibu watoto kijeshi kwa mijeledi, fimbo na makofi. Wafahamu kuwa ni ukiukaji wa haki za watoto. Waelewe kwamba siku watakapotiwa mbaroni wataishia na kilio cha mbwa mdomo juu, ndipo watalazimika kutia akilini msemo, majuto ni mjukuu huja kinyume na mwiba wa kujidunga hauambiwi pole.

Wavyele wanaokataa katakata kuwapeleka wana wao shuleni watambue kuwa wamo katika uhalifu jinsi walivyo wahuni na wachopozi. Hata hivyo, yafaa waelewe kuwa mbio za sakafuni huishia ukingoni na nguvu ya mayonda huishia jangwani. Wanaoshuhudia uongo na kuwasingizia wenzao mambo ambayo hayana msingi madhubuti aidha wamevunja kanuni za nchi. Unaposhiriki porojo bila shaka una mshabaha na wanyang'anyi wa kutumia mabavu.

Abiria wawapo safarini kisha wakarakibu daladala, huhitajika kujisetiri kwa mikanda ya usalama. Watu wanaokosa kujifunga mikanda ya usalama hawatii sheria ambao wao aidha ni wahalifu. Fahamu kwamba asiyetii hutiwa. Ni jambo bora na mwanana endapo lusi razini watakuwa watiifu angalau kuepuka lawama na majuto. Bora kuzuia majuto tukifahamu kuwa kinga yashinda tiba.

  1.  Mtu avunjaye amri za nchi au jamii bila shaka si
    1. mwadilifu
    2. maadili
    3. mwasi
    4. mzalendo
  2. Bwana Hussaini Khali anatajika kifunguni kama
    1. msomi
    2. mswahili mahiri
    3. mhandisi
    4. kandawala
  3. Ni usemi gani utakoingiana barabara na aya ya tatu?
    1. Mgeni aje mwenyeji apone.
    2. Mgeni hachomi chaza mtaani
    3. Mgeni kumpokea kumbe ni kujitongea 
    4. Mgeni ni kama kengewa huruka akenda kwao
  4. Mhalifu si rahisi kutangamana na wenzake kwakuwa
    1. ana sura mbaya
    2. hana afya njema
    3. hana imani mwafaka
    4. ni mfano mbovu
  5.  Ni kauli ipi kutokana na taarifa isiyo ya kweli?
    1. Mshabaha upo baina ya dini na sheria za nchi
    2. Sheria za nchi hazihusiki na dini yoyote 
    3. Wafanyayo makosa yoyote ni wahalifu
    4. Lusu si mwasi
  6.  Neno ajinabi lilivyotumika yamkini linia maana ya
    1. mgeni
    2. kigeni
    3. desturi
    4. sherehe
  7.  Wageni wasioheshimu wenyeji... ni kina nani hawa?
    1. Majangili
    2. Majambazi
    3. Makaidi
    4. Wahalifu
  8. Kwenye aya ya tatu, mwandishi anatoa tahadhari kuhusu
    1. kukirimu wageni
    2. kutunza wageni
    3. kupokea wageni
    4. kushuku wageni
  9. Abiria aliye kwenye matwana aweza kuitwa mhalifu kwa
    1. kutolipa nauli
    2. kujifunga mkanda wa usalama
    3. kutovuta sigara
    4. kutulia garini
  10. Kwenye aya ya mwisho, mwandishi anatoa nasaha inayoandamana na msemo
    1. kuepukana na tatizo kuliko kusubiri balaa ikufike kwanza ni bora
    2. heri ungoje ujionee
    3. kujionea balaa ni vizuri
    4. heri kungoja maana utakuwa shujaa

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako

Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu huku ukianza kwa kifungu ulichopewa.

Ilikuwa siku ya michezo ya riadha shuleni kwetu Bahati. Hivyo basi.......

MAJIBU

swa scheme

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 6.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students