Wednesday, 18 May 2022 06:26

Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 6 End of Term 1 Exams 2022 Set 2

Maswali

Maagizo ya mwanafunzi

 • Karatasi hii ina sehemu sita kuu
 • Jibu Maswali yote kulingana na maagizo

Sehemu 1: Mazungumzo ya ana kwa ana (alama 5)
Ugonjwa husorotesha afya ya mwanadamu na kusababisha utumizi wa hela ni lengo lisilofaa.

 1. Ni ugonjwa upi ambao umewapa Wakenya tumbo joto?
 2. Ugonjwa huo ulioutaja katika swali Ia (a) waweza epukika vipi?
 3. Ni ugumu upi uliopata baada ya kutokea kwa ugonjwa huo?
 4. Taja magonjwa mengine yanayowasumbua Wakenya?
 5. Ungekuwa dakatari ungewasaidiaje wagonjwa wanaopata homa ya tumbo kilo mare?

Sehemu 2: Ufahamu wa Kusikiliza (alama 5)
Msikilize mwalimu akisoma kifungu kifuatacho kisha ujibu Maswali yafuatayo

Mimi naitwa Riziki. Nina miaka kumi. Mimi husomea katika shule ya msingi ya Pande. Shule yetu iko katikati ya jimbo Ia Kiambu na Kitui. Nilijiunga na shule hii miaka miwili iliyopita. Sasa niko katika gredi ya site. Mwalimu wetu wa darasa ni Bi. Malimo. Somo ninalolipenda ni la Kilimo. Somo hill hupendwa pia na wanafunzi wenzangu. Mwalimu wetu wa Kilimo ni Bwana Mtume.

 1.  Msemaji ana miaka mingapi?
 2. Je ikiwa msemaji yuko gredi ya site mwaka huu, miaka miwili iliyopita alikuwa darasa lipi?
 3. Eleza pale shule ya msemaji inapatikana?
 4. Kwa nini somo la Kilimo line wanafunzi wengi?
 5. Tajo masomo mengine yaliyo katika gredi ya site?

Sehemu 3: Kusoma kwa sauti (alama 15)

Wanyama hawa wawili walianza safari ya kuelekea kwa 5imba. Walipofika karibu na lango kuu Ia mfalme 5imba, walikuta mkusanyiko wa Wanyama wengine. Wote wakatarajia mfalme wao awape suluhu ya tatizo lao. Walijikokota na kukaribia mzee Tembo. Sungura alimsihi kwa upole amueleze pale wangepata maji. Mzee Tembo alimuonea huruma na kumtilia maji kidogo aliyokuwa ameyaweka kwenye mdomo wake. Mfalme 5imba alionekana akijikokota kwa umbali akija. Alipowafikia akazirai. Wanyama wote walitawanyika na kumwacha Mzee Chui akimuhudumia mfalme wao. Walielekea kwenye mto uliokuwa karibu. Kwa mshangao walipata Mzee Kobe akiyatega maji yaliyokuwa yameanza kutiririka.

Sehemu 4: Ufahamu wa kusoma (alama 6)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali Ia 1 hadi 6

Hapo zamani za kale walikuwepo watu ambao walikuwa wanaishi karibu na pwani. Kazi yao ilikuwa kuvua, na siku zote walikuwa wanavua samaki wadogo wadogo. Siku moja alitokezea bwana mmoja akaenda baharini akabahatika kuvua samaki mkubwa sana. Yeye mwenyewe akaanza kushangaa kumuona yule samaki mkubwa, na akaanza kusema ningempata samaki kama huyu ningetajirika. Kilo siku tunakuja pwani tunapata samaki wadogo wadogo, hapo akajiuliza samaki huyu nimfanye nini?

Akaenda kumwita baba yake. Baba mtu alipofika akaanza kushangaa na kusema samaki huyu mkubwa si jawahi kumuona, sasa wakaanza kushauriana. Baba yake akasema bora tukawaite jamaa waje kumtazama. Wale jamaa walipofika na wao wakaanza kushangaa na kusema; "samaki mkubwa, samaki kama huyu hatujawahi kumvua maisha yetu." Na wao wakasema; "twendeni tukamwite sheha." 5heha alipokuja alishangaa na akasema; "Bora tukawamwite Mfalme aje kumuona." Alipokuja Mfalme no yeye alishangaa na kusema; "Bora tukamwite mzungu aje kumpiga picha."

Hapo waliondoka wakaenda kumchukua mzungu, na mzungu alipofika akasema;"Mngelimuweka kiile nikampiga picha lakini hapa anazunguuka nitampiga vipi?" Wale watu wakajibu mpige hivyo hivyo, na huku maji yanajaa na yule samaki akachukuliwa na maji, na kuenda nke baharini wakakosa utajiri pamoja na samaki.

Maswali

 1. Watu wa Kijiji hiki walikuwa wanafanya kazi gani?
 2. Kamilisha sentensi. Mvuvi alipovua Samaki mkubwa
 3. Jamaa walipoitwa walisihi nani aweze kuitwa?
 4. Mfalme alipoitwa alisisitiza nani ajulishwe kuhusu Samaici huyo mkubwa?
 5. Je, wanaki jiji hawa walipata utajiri waliokuwa wakiomba?
 6. Ipe hadithi hii mada ya kufana?

Sehemu 5: Saruf (alama 24)

 1. Andika maneno haya katika ukubwa     
  1. Mgongo
  2. Ngoma
  3. Mkono
 2. Kamilisha methali         
  1. Mtaka cha mvunguni _______________________________________
  2. _______________________________________ marejeo ni ngamani
  3. Msiba wa kujitakia ________________________________________
 3. Andika sentensi hizi kwa wakati uliopita
  1. Mtoto ataenda shuleni
  2. Mwanafunzi anaandaa sima
  3. Mtego umemnasa paka
 4. Kanusha sentensi hizi
  1. Tulienda kanisani
  2. Vita vilileta njaa
  3. Mjumbe wetu alifanya kazi nzuri
 5. Kamilisha tashbihi hizi
  1. Kigeugeu kama
  2. Mwaminifu kama
  3. Msumbufu kama
 6. Andika vinyume yya vitenzi hivi
  1. Rudi
  2. Vua
  3. Tua
  4. Lia
   01kisG6et122set2q6
 7. Andika kwa maneno
  1. Shilingi 2,345
  2. Vijiko 199
  3. Mkate 1/2
  4. Saa 4.15

Sehemu 6: Kuandika (alma 10)
Kamilisha mtungo ufuatao. Ufanye uwe wa kuvutia mno

Jua lilionekana likichomoza kwa umbalL Nami nilifungua jicho langu kulia, kisha kushoto nakuelekea. 

Mwongozo wa Kusahihisha

Sehemu 1

 • Mwanafunzi anapaswa kuongea na kujibu maswali ipasavyo

Sehemu 2

 • Mwanafunzi anapaswa kuongea na kujibu maswali ipasavyo

Sehemu 3

 1.          
  1. Kuvua samaki
  2. Alishangaa/ alistaajabu
  3. Sheha
  4. Mzungu
  5. La, samaki alitowekea kwa maji yaliyokuwa yamejaa
  6. Sahihisha mada kulingana na muktadha

 Sarufi  

 1.               
  1. Gongo
  2. Goma
  3. Kono
 2.        
  1. Sharti ainame
  2. Mwenda tezi na omo
  3. Hauna kilio      
 3.   
  1. Mtoto alienda shuleni
  2. Mwanafunzi aliandaa stima
  3. Mtego ulimnasa paka
 4.        
  1. Hatukuenda shuleni
  2. Vuta havikuleta njaa
  3. Mtego ulimnasa paka  
 5.         
  1. Kinyonga
  2. Njiwa
  3. Mwanambuzi
 6.          
  1. Enda
  2. Vaa
  3. Tia
  4. Cheka   
 7.                 
  1. shilingi elfu mbili mia tatu arobaini na tano
  2. Vijiko mia moja tisini na tisa 
  3. mkate nusu
  4. saa kumi na robo

Please download the document as PDF to read all it's contents.

Why PDF Download?

 • You will have the content in your phone/computer to read anytime.
 • Study when offline.(No internet/data bundles needed.)
 • Easily print the content to hard copy.

Read 2561 times Last modified on Monday, 23 May 2022 13:05