Wednesday, 14 June 2023 08:03

Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Mid Term 2 Exam 2023 Set 1

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
Kaka Mbweha: (Akicheka kwa kejeli) Bi Ngiri, mkulima hodari wa mihogo anayeheshimika katika ukanda huu, hujambo?

Bi Ngiri: (Akihema kwa uchovu) Sijambo, lakini nina swali. Unacheka nini? Ama ndio njia yako ya kumfariji anayetoka kuchanika kwenye mpini siku nzima?

Kaka Mbweha: (Anacheka zaidi) Eti kuchanika kwenye mpini? Wachapakazi kama mimi hawana haja ya kujichosha. Wanafanya kazi kwa kutumia akili.

Bi Ngiri: (Kwa dharau) Mhh! Heri nyinyi mabingwa wa kutumia akili. Sisi wengine inabidi tujikaze kisabuni ili tupate riziki.

Kaka Mbweha: (Kwa mshangao) Nyinyi wengine? Wewe na kina nani? Je, huna habari kwamba rafiki zako sungura na fisi hawapandi wala kuvuna lakini daima wana shibe?

Bi Ngiri: (Kwa sauti ya chini) Hayo ya kina sungura hayanihusu ndewe wala sikio. Isitoshe, unavyoona nimechoka. Shamba langu la mihogo liko mbali na kwangu. Bado nina mlima mmoja wa kukwea ndipo nifike.

Kaka Mbweha: Haya basi niazime vipande viwili vya mihogo. Nitarejesha nitakapovuna.

Bi Ngiri: Kaka Mbweha, umesahau kuwa tayari una deni langu la mihogo? Lípa hilo kwanza.

Kaka Mbweha: (Kwa unyenyekevu) Nitalipa tu.

Bi Ngiri: Utanilipa vipi ilhali wewe mwenyewe hukuvuna? Unastahili kufanya kazi kwa bidii. Kumbuka ajizi ni nyumba ya njaa.

 1. Kulingana na mazungumzo haya, Bi Ngiri anasifika kwa sababu ya nini? 
  1. Kutembea mwendo mrefu kwenda shambani mwake.
  2. Ukulima wa mihogo.
  3. Bidii katika shughuli za shambani. 
  4. Kuwashauri wakulima wenzake.
 2. Chagua sifa inayomfaa zaidi kaka Mbweha kulingana na mazungumzo haya.
  1. Mchapakazi
  2. Mnyenyekevu
  3. Mwerevu
  4. Mvivu
 3. Mazungumzo haya yanaweka wazi kuwa anayejitegemea ili kujilisha kikamilifu ni
  1. fisi.
  2. sungura.
  3. kaka Mbweha.
  4. Bi Ngiri.
 4. Ni kwa nini Bi Ngiri alimwambia kaka Mbweha kuwa bado alikuwa na mlima mmoja wa kukwea? Ili 
  1. kumjulisha kuwa kulikuwa na milima huko.
  2. waandamane kuelekea kwake. 
  3. akatize mazungumzo na amruhusu aende akapumzike.
  4. kumweleza umuhimu wa kuwa na shamba mbali na nyumbani.
 5. Mazungumzo haya yanatufunza kuhusu
  1. ubaya wa uzembe.
  2. umuhimu wa kutumia akili. 
  3. kilimo cha mihogo. 
  4. matumizi ya mashamba. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 9.
Ni wajibu wa kila mkenya, awe kijana au mzee, kushiriki katika uhifadhi na ulinzi wa misitu yetu. Kila mmoja ana nafasi yake ya kutekeleza kulingana na umri na uwezo wake. Upanzi wa miti unafaa kuongozwa na vijana kwa sababu wana nguvu ya kutosha. Msimu mzuri wa kupanda miche ni msimu wa mvua nyingi.
Ili kuipanda miti mingi nchini, serikali imetenga siku moja kwa mwaka iwe ya upanzi wa miche, yaani miti michanga. Wengi hivi karibuni wamekosa kuitilia maanani siku hii muhimu. Hapo awali, shughuli hii ilikuwa ikichangamkiwa na kila mmoja katika jamii.

 1. Kulingana na ufahamu, uhifadhi wa misitu ni wajibu wa
  1. vijana.
  2. watu wazima. 
  3. watu wote.
  4. wanafunzi.
 2. Je, ni kwa nini vijana ndio wanaofaa kuongoza katika upanzi wa miti?
  1. Wana nguvu ya kutosha.
  2. Wanajua kupanda miche zaidi. 
  3. Wao ndio wengi nchini.
  4.  Hiyo ni sheria ya nchi yetu.
 3. Katika mwaka mzima, siku ngapi zimetengewa upanzi wa miti?
  1. 3
  2. 2
  3. 4
  4. 1
 4. Kulingana na ufahamu, 
  1. hata sasa, wanajamii wanachangamkia upanzi wa miche.
  2. miti michanga sana huitwa miche.
  3. hapo awali, watu hawakupenda kupanda miche.
  4. miti ina faida kwa vijana pekee. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
Mayowe aliketi kando ya ghala lake tupu. Tumbo lilimnguruma kwa njaa. Aliishi hivyo kwa siku tatu. Mtama aliokuwa ameuweka katika ghala uliibwa na manyani na tumbili waliotoka katika msitu wa Marura. Mahindi nayo yaliyokuwa tele humo ghalani yaliliwa yote na kuchakulo. Kando yake kulikuwa na kibuyu. Kibuyu hicho kilisoma akili yake haraka na kumwambia kwa sauti, "Fanya chaguo!" Mayowe alisema kwa sauti, "Ninataka chakula!" Ghafla bin vuu, ghala likajaa mihogo na viazi. Mayowe alifurahi kuliko siku zote za maisha yake.

 1. Mwanzoni mwa ufahamu, ghala la Mayowe lilikuwa na nini?
  1. Mihogo na viazi.
  2. Lilikuwa tupu.
  3. Mahindi na mtama.
  4. Mtama na viazi.
 2. Tumeambiwa kuwa Mayowe alihisi njaa kwa muda wa
  1. wiki tatu.
  2. miaka mitatu.
  3. saa tatu
  4. siku tatu.
 3. Manyani na tumbili wezi walitoka wapi?
  1. Katika kijiji jirani.
  2. Mlimani.
  3. Mtoni Marura.
  4. Msituni Marura.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Kuna umuhimu mkuu wa kudumisha afya bora. Binadamu akiwa na afya bora huweza kufanya shughuli zote vizuri na kwa wakati unaofaa. Ili kuwa na afya bora, ni vizuri kuzingatia lishe bora. Chakula tunachokila lazima kiwe na kabohaidreti, protini na vitamini kwa viwango vinavyofaa mwilini. Vilevile, ni vizuri kunywa maji safi na salama kila siku. Je, wajua kuwa matunda hutukinga tusiwe wagonjwa? Wapishi na watu wote wanaoandaa chakula ni lazima wawe safi ili tusipatwe na magonjwa.

 1. Taarifa hii inasema kuwa inatulazimu kudumisha
  1. lishe bora.
  2. chakula bora.
  3. afya bora.
  4. usafi wa hali ya juu.
 2. Tumean.biwa kuwa chakula chetu ni vyema kiwe na
  1. kabohaidreti na protini.
  2. vitamini na kabohaidreti.
  3. kabohaidreti na protini.
  4. vitamini, kabohaidreti na protini.
 3. Kulingana na taarifa hii, matunda
  1. hutuletea magonjwa.
  2. hutukinga dhidi ya magonjwa.
  3. huwa na ladha ya kuvutia.
  4. yanafaa kuwa safi na salama. 

Soma kifungu kifuatacho. Chagua libu lifealo zaidi kati ya yale uliyopewa

Wapo wanyama mbalimbali ...................16................. katika mbuga zetu. Kuna wale ambao huwawinda wenzao kama vile simba, chui na  ...................17.................. Hawa huwa  ...................18................. mchana wote.  ...................19.................kuwaona, lazima ufike mbugani mapema kabla ya  ...................20.................kuchomoza.

 1.                        
  1. zilizo
  2. iliyo
  3. aliye
  4. walio
 2.                
  1. farasi
  2. ngamia
  3. duma
  4. ndovu
 3.            
  1. hawalali
  2. hawaamki
  3. wamelala
  4. wanalala
 4.            
  1. Hili
  2. Ili
  3. Hii
  4. Kwa sababu
 5.              
  1. giza
  2. mwezi
  3. nyota
  4. jua

Katika swall la 21-30, libu swall kulingana na maagizo uliyopewa. 

 1. Chagua kundi la nominoambata pekee. 
  1. Umati, kicha, mlolongo.
  2. Mjombakaka, mjusikafiri, mlariba.
  3. Huzuni, furaha, hasira.
  4. Meza, kalamu, darasa.
 2. Chagua nomino iliyo tofauti na nyingine.
  1. Alhamisi.
  2. Upendo.
  3. Agosti.
  4. Jumanne.
 3. Chagua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo.
  1. Alisema kuwa amemaliza kazi. 
  2. Kwani mzazi wako hajafika. 
  3. Wanafunzi wenzangu ni Timami, Maimuna na Recho.
  4. Naam, nimekuelewa sasa.
 4. Je, ni pambo gani hapa linaloweza kuvaliwa masikioni?
  1. Bangili.
  2. Kipuli.
  3. Ushanga.
  4. Hina.
 5. Chagua nomino zilizo katika ngeli ya I-ZI.
  1. Gari, tunda, tausi
  2. Uzi, ushanga, ukuta.
  3. Kinyonga, kiwavi, kinda.
  4. Pua, shingo, karatasi.
 6. Umepewa maneno manne hapo. Chagua litakalokuwa la kwanza katika kamusi.
  1. Kofia
  2. Konsonanti
  3. Koleo
  4. Kondakta
 7. Mwenzako akikuambia alamsiki utamwambiaje?
  1. Nawe pia 
  2. Binuru
  3. Jaala
  4. Inshallah
 8. Kanusha sentensi ifuatayo: Nilimwona akiingia.
  1. Nilimwona akiondoka. 
  2. Sikumwona akiondoka. 
  3. Sikumwona akiingia. 
  4. Nilimwona akija.
 9. Ukubwa wa nomino mti ni
  1. miti.
  2. jiti.
  3. kijiti.
  4. vijiti.
 10. Kamilisha tashbihi ifuatayo:
  Mzee Mapunda ni mkali kama
  1. wembe.
  2. shubiri.
  3. pilipili.
  4. simba.

MWONGOZO

swa ad

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Mid Term 2 Exam 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students