Wednesday, 09 February 2022 06:42

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 1 End of Term 3 Set 2 2022

Share via Whatsapp
 1. UFAHAMU (Alama 10)
  Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata: Alama 5)
  Usafi ni jambo la muhimu sana kwa maisha ya binadamu. Ni lazima tukate kucha, kunyoa nywele, kusafisha nguo, kusugua meno, kunawa mikono, kuoga na kufuta kamasi kwa kutumia kitambaa safi. Tukizingatia haya yote tutajiepusha na magonjwa mengi.
  1. Andika mambo matano ambayo ni njia za kuzingatia usafi.
   i) 
   ii) 
   iii)
   iv)
   v)
   Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali (alama 5)
   Mwalimu wetu alitufunza kuhusu vyakula vya kiasili. Alitueleza kuwa tukila vyakula kama mihogo, viazi, mahindi, maharagwe, mboga, machungwa na ndizi tutajiepusha na magonjwa yanayosababishwa na kula vyakula ambavyo si vizuri kwa afya zetu.
   1. Mwalimu alifunza kuhusu nini?(alama 1)
   2. Andika vyakula vinne vilivyotajwa katika kifungu.(alama 4)
 2. SARUFÍ (Alama 15)
  1. Unda maneno: (Alama 5)
   Kwa mfano : za + ma = zama
   1. ha + ma =
   2. ti + sa =
   3. go + ti =
   4. ki + ma
   5. me + za
  2. Andika umoja wa maneno haya katika umoja:(Alama 5)
   1. vichwa
   2. mikono
   3. midomo
   4. masikio
   5. macho
  3. Andika maneno haya vizuri:(Alama 5)
   1. kusi
   2. tiki
   3. jima
   4. auma
   5. miku
 3. KUANDIKA.(Alama 10)
  Andika maneno matano utakayosomewa na mwalimu.


MARKING SCHEME

UFAHAMU

 1. tukate kucha
 2. kunyoa nywele
 3. kusafisha nguo
 4. kusugua meno
 5. kunawa mikono

Hadithi

 1. Kuhusu vyakula vya kiasili
 2.      
  • mihogo
  • viazi
  • mahindi
  • maharagwe

SARUFI

 1.      
  1. hama
  2. tisa
  3. goti
  4. kima
  5. meza
 2.      
  1. kichwa
  2. mkono
  3. mdomo
  4. sikio
  5. jicho
 3.      
  1. siku
  2. kiti
  3. maji
  4. maua
  5. kumi

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 1 End of Term 3 Set 2 2022.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


.