Monday, 25 April 2022 09:02

Shughuli za Kiswahili Homework Activities - CBC Grade 1

Share via Whatsapp

Fanya shughuli zote

Kusikiliza na kuzungumza

Jibu maswali haya kwa kuzungumza,Mwalimu, mgzazi, akuulize maswali haya

 1. Je, unaitwa nani? ________________
 2. Wewe nu familia yako mnaishi wapi?  ________________
 3. Baba yako anaitwaje?  ________________
 4. Baba yako anafanya kazi gani?  ________________
 5. Mama yako anaitwaje?  ________________
 6. Mama anafanya kazi gani?  ________________
 7. Je, una ndugu wadogo?  ________________
 8. Je una ndugu wakubwa?  ________________
 9. Nyanya na babu wanaishi wapi?  ________________
 10. Nyanya na babu wanafuga wanyama gani?  ________________

Mwambie mzazi au mlezi wako akusomee taarifa hii kish akuulize maswali. Jibu kwa sauti kubwa.

Zainabu alipoanza kufanya kazi yoke ya wakili alinunua shamba. Alitaka kuwa mkulima wa michungwa. Aliwapa watu kazi wakamlimia shamba lake na kupanda michungwa mingi. Michungwa ilianza kuwa mikubwa na shamba lake likapendeza. Baadaye michungwa yalikomaa akaanza kuwauzia watu. Siku hizi shamba hill linajulikana sana.

Maswali

 1. Zainabu alikuwa akifanya kazi gani?
 2. Zainabu alinunua nini?
 3. Zainabu alikuwa mkulima wa
 4. Shamba la Za inabu sasa lira
 5. Michungwa huzaa matunda yanayoitwa

Kusoma maneno
Soma kwa sauti

maziwa  kiatu   shingo  wema
mafuta  kuku  kiuno  safisha
mwa  mkebe  utosi  viazi
uyoga  ndizi  bizari  nyumbani
sufuria  mihogo  asali  taulo

Soma sentensi hizi

 1. Hill ni dawati. 
 2. Mwalimu anaandika ubaoni. 
 3. Wao wanatumia tabieti. 
 4. Huyu ni rafiki yangu. 
 5. Mimi ni mfupi.
 6. Ndege wako angani.
 7. Jumatatu tunaenda shuleni.
 8. Kaka amebeba ua.
 9. Alimtembelea hospitalini.
 10. Ninaokota taka.

Msomee mzazi au mlezi wako hadithi hii kwa sauti. Tamka maneno vizuri

Hadithi ya kwanza

Mimi ninaitwa Mwakasi. Nyumbani ninafuga bata. Bata huyu nilipewa na babu. Nilienda kumtembelea mashambani.
Babu aliserna nikimpa bata chakula atakuwa mkubwa. Akiwa mkubwa atanipa nyama na mayai. Niliendelea kumpa chakula na maji. Akawa mkubwa. Akapata watoto. Wanaitwa Viyoyo.

Hadithi ya Pili

Jina Iangu ni Asha. Ninasomea katika shule ya Tuko Mbele. Ni shule kubwa. Kuna wavulana na wasichana. Wasichana ni wengi kuliko wavulana. Mimi ni mwanafunzi wa gredi ya kwanza. Mwalimu mkuu anaitvva Bi. Chaurembo. Yeye ni mrembo. Anawapenda watoto wote shuleni. Wakati mwingine yeye hutuletea wageni. Wageni hawa hutupatia zawadi. Mara nyingi hutuambia tusome kwa bidii. Mimi ningependa kuwa mwalimu. Kwa hivyo nitafanya bidii shuleni. Je, wewe ungependa kufanya kazi gani?

 1. Jaza mapengo kwa jibu sahihi
  1. __________ kwa kupoteza katamu (Pole, Asante)
  2.  __________niruhusu nipite. (Tafadhali, Asante)
  3. __________ sikusikia swati tako. (Samahani, Habari )
  4. Mwalimu __________ nimechelewa kuingia darasani.
   (niwie radhi, naomba)
  5. __________ tutaonana tena Jumapiti (Sijambo, Kwaheri)
 2. Jibu salamu hizi
  1. Hujambo? __________
  2. Hamjabo? __________
  3. Habari yako?__________
  4. Umeshindaje? __________
  5. Je, umeamkaje? __________
 3. Je, wajua vitu unavyovitumia darasani? Michoro hii inaonyesha vitu hivyo. Hebu vitaje.
  kis01.JPG
 4. Tazama picha hii. Sema watoto wanacheza mchezo gani?
  kis02
  ____________________
 5. Je unaona wanyama gani kwenye picha hizi
  kis03
 6. Tambua sauti zinazounda maneno haya
  K.m Kiti   = K + ti 
  1. boksi
  2. kipepeo =
  3. paka =
 7. Watoto hawa wamepewa maagizo ya kugusa sehemu gani za mwili?
  kis04

KUSOMA

Soma hadithi kisha ujibu maswali

Hadithi ya kwanza
Tunatumia mikono kulia chakula. Mono inaweza kumega ugali na kuchukua mboga kisha kuweka kinywani. .Tunatumia meno kutafuna chakula. Chakula huvunjwavunjwa no kuwa chepesi na rahisi. Mate nayo hukitayarisha chakula na kukipeteka tumboni Kupitia kooni. Mtu akishiba huwa haoni njaa.

Maswali

 1. _________________ hutafuna chakula.
 2. _________________ huzungusha chakula kinywani.
 3. Chakula hupitia _________________ iii kuweza kufika tumboni.
 4. Mtu hula kwa sababu anahisi _________________
 5.  Tunatumia nini kuchukua mboga? _________________

Hadithi ya pili
Mazingira ni kitu chochote kinachotuzunguka. Tunafaa kutunza mazingira yetu. Tunaweza kuyatunza kwa kupanda miti. Miti ni mizuri. Miti ikiwa mikubwa hutupa mahati pazuri pa kukaa tunaposoma au kupumzika kwenye kivuli. Mahali penye miti mingi huitwa msitu. Miti pia huleta mvua. Wakulima hutumia mvua kukuza mimea shambani. Ningewaambia watu wapande miti mingi ili tupate kivuli na mvua.

Maswali

 1. Mid ina umuhimu gani ?
  1. __________________
  2. __________________
 2. Wewe unajua miti gani ambayo hutupatia matunda?
  1. __________________
  2. __________________
 3. __________________ ni chochote kinachotuzunguka
 4. Mahaii penye mid mingi huitwa __________________
 5. Wakulima hutumia __________________ kukuza mimea.

Hadithi ya tatu

Baba yangu ni fundi wa mbao. Pia anaweza kuitwa seremala. Yeye ni fundi wa kutengeneza vitu kwa mbao kama meza na viti. Watu wanapenda kutengenezewa fanicha na baba yangu. H ii ni kwa sababu anapenda kazi yake. Yeye hutengeneza meza, viti na kabati vizuri. Kazi hii ndiyo hutupa pesa za chakula. Pia humpatia pesa na kutuIipia shule na kutununulia nguo. Baba ameifanya kazi hii kwa miaka mingi. Anajulikana sana.

Maswali

 1. Baba hufanya kazi gani? __________________
 2. Fundi wa mbao huitwa _________________
 3. Baba hutengeneza __________________., __________________ na __________________
 4. Watu wanapenda baba awatengenezee __________________
 5. Baba amefanya kazi kwa miaka __________________

KUANDIKA

 1. Jaza mapengo kwa kutumia "a"
  1. K __ l __mu (d)
  2. M __ kosa (e)
  3. Mez___
  4. K_ b__ ti
   P___ zi___
 2. Andika maneno haya kwa herufi kubwa
  1. ndovu:_________________
  2. simba: _________________
  3. kunguru: _________________
  4. jogoo:_________________
  5. ngamia: _________________
 3. Panga herufi ill kuunda neno
  1. nija: _________________
  2. tmake: _________________
  3. mokon: _________________
  4. ynuamb: _________________
  5. usim: _________________
 4. Jaza mapengo kwa silabi zinazofaa
  1.  _____ che  _____   _____   chu 
  2.  _____  _____   _____  fo fu
  3. Ha _____ _____ _____ _____
 5. Tenganisha silabi kutoka maneno haya
  1. Kitabu  __________________
  2. Darasa  __________________
  3. Kalenda  __________________
  4. Chati  __________________
  5. Kabati  __________________
 6. Andika majina ya picha hizi;
  kis05
 7. Watoto hawa wanafanya nini?
  kis06
 8. Andika vifaa vya kusafisha nyumba unavyovijua
  1. ____________________________
  2. ____________________________
  3. ____________________________
  4. ____________________________
 9.  Jaza mapengo
  1. Baba  ____________ kesho kutwa (anakuja, atakuja).
  2. Mimi hupiga pasi   ____________ kuvaa nguo.(kabla ya, baada ya)
  3. Ni  ____________ kuwa na adabu. (vizuri, vibaya)
  4. Mtoto  ____________ huwa na heshima. (mbaya, mzuri)
  5. Mimi ninapenda  ____________ (usafi, uchafu)


SARUFI

 1. Andika wingi wa sentensi
  1. Mimi ninaandika.____________________
  2. Mimi ninasoma . ____________________
  3. Mimi ninaimba. ____________________
  4. Mimi nnakula. ____________________
  5. Mimi ninasikia. ____________________
 2. Andika wingi wa maneno haya:
  1. Jicho __________
  2. Mguu __________
  3. Mkono __________
  4. Kidole __________
  5. Kichwa __________
  6. Goti __________
  7. Sikio __________
  8. Bega __________
  9. Mdomo __________
  10. Unywele __________
 3. Tumia "huyu" au "hawa"
  1. __________ ananawa mikono.
  2. Mvulana __________ anacheza.
  3. Wanafunzi __________ wanasoma.
  4. Mwalimu __________ anafundisha.
  5. Watoto __________ wanacheza nje.
  6. Wazazi __________  wanapika.
 4.  Tumia maneno haya kujaza mapengo
  zangu , letu, vyetu, wangu, kwetu, yangu
  1. Hili ni shamba ___________
  2. Meza hizi ni ___________
  3. Mtoto ___________ analia
  4. Ninaenda nyumbani ___________
  5. Vitabu ___________ vimeraruka
  6. Sahani hii ni ___________
 5. Jaza mapengo
  1. Mfuko ___________ una penseti (yangu, wangu)
  2. ___________ si mbati na kanisa (kwangu, lao)
  3. Shamba ___________ lina matunda (letu, kwetu)
  4. Kitabu ___________ kimejaa uchafu (langu, change)
  5. Nilipoteza rula za shule ___________
 6. Ambatanisha jina na picha
  kis07
 7. Panga maneno hays iii kuunda sentensi
  1. vizuri analima mkulima
  2. kupigana si vizuri
  3. asubuhi kilo ninaomba
  4. ni unga huu
  5. ni zuri letu pazia
 8. Jaza mianya kwa herufi ("i")
  1. Sh ___ kamoo
  2. Tafadhal___
  3. Samahan__
  4. Kar___ bu
  5. N ___nashukuru
 9. Jaza mapengo
  1. Mw__ lim___
  2. Dere __ a
  3. Diw ___ ___ ____
 10. Andika majina ya vitu hivi
  kis08

MSAMIATI

 1. Paka rangi
  kis09
 2. Andika majina ya sehemu za mwili katika nambari. Chagua kati ya yale yaliyo hapo chini.
  kis10
  Shingo, utosi ,goti, mkono, Kiuno, vidale,mdomo kisigino
 3. Jaza mapengo kwa majibu sahihi
  1. Wiki moja ina siku ngapi?
  2. Katika wiki moja tunaenda shuleni mara ngapi?
  3. Sehemu ya mwili inayotumiwa kuona ni
  4. hutupa maziwa (kuku, ng'ombe)
  5. Mbuzi ana miguu mingapi?
  6. Suruali hufungiwa kwenye
  7. Sisi hutembea kwa kutumia
  8. Kisogo hupatikana
  9. Kidole kikubwa cha mkono huitwa
  10. Sisi hunusa kwa kutumia
  11. Ndizi ikiiva ina rangi ya
 4. Chagua jibu sahihi.
  1. Tunanunua bidhaa kama sukari na chumvi_______________(nyumbani, dukani)
  2. Tunaenda ____________ kwa haja ndogo. (msituni, chooni)
  3. Ukila ___________ utang'olewa jino. (pipi, bibi, baba)
  4. Tunaweka __________ kwenye chakuta. (asali, chumvi)
  5. Watu hulala juu ya ______________
 5. Tumia majina yanayofaa.
  1. Dada wa mama anaitwa? __________________ (halati, babu) 
  2. Mama ya baba yangu ni __________________ (nyanya, babu)
  3. Baba ya baba yangu ni __________________ (babu, bibi)
  4. Anayewatibu watu ni __________________ (mwalimu, Daktari)
  5. Samaki, mboga, viazi ni aina ya __________________ (matunda, vyakuta)
 6. Tazama vyakuta hivi. Mimi ninapenda kula
  kis11.JPG


Mwongozo wa Kusahihisha

 1. -10: majibu tofauti
  1. Ya wakili
  2. Shamba
  3. Michungwa
  4. Julikana
  5. Machungwa

Hadithi ya pili

Hadithi ya kwanza

 1.                 
  1. Pole
  2. Tafadhali
  3. Samahani
  4. Niwe radhi
  5. Kwaheri
 2.         
  1. Sijambo
  2. Hatujambo
  3. Nzuri/njema
  4. Vyema/ vizuri 
  5. Vizuri/ vyema
 3.         
  1. Raba
  2. jalala
  3. chaki
  4. begi
  5. Kalamu
  6. Kifutio
  7. Kitabu
  8. Dawati
 4. Kuruka ka:
 5.      
  1. Mbwa
  2. Paka
  3. Farasi
  4. Jogoo - Kuku
 6.    
  1.  bo+k+si
  2. ki+pe+pe+o
  3. pa+ka
 7.        
  1.  Kichwa
  2. Jicho
  3. Tumbo
  4. Miguu

KUSOMA
Hadithi ya Kwanza

 1. Meno
 2. Ulimi
 3. Kooni
 4. Njaa
 5. Mikono

Hadithi ya pili

 1.     
  1. huleta mvua
  2. hutupa kivuli
 2.           
  1. Michungwa
  2. Miembe
  3. Mipera
  4. Mipapai
 3.  
 4. Msitu
 5. Mvua

Hadithi ya tatu

 1. Ya useremala
 2. Seremala
 3. Meza, viti, kabati
 4. Fanicha
 5. Mingi

KUANDIKA

 1.        
  1. Kalamu
  2. Makosa
  3. Meza
  4. Kabati
  5. Pazia
 2.       
  1. NDOVU
  2. SIMBA
  3. KUNGURU
  4. JOGOO
  5. NGAMIA
 3.         
  1. Njia
  2. Mkate
  3. Mikono
  4. Nyumba
  5. Simu
 4.         
  1. Cha, chi, cho , chu
  2. fa, fe, fi
  3. He, hi, ho, hu
 5.        
  1. ki+ta+bu
  2. Da+ra+sa
  3. ka+le+nda
  4. cha+ti
  5. ka+ba+ti
 6.          
  1. Ng'ombe
  2. Ngamia
  3. Saa
  4. Mpira
 7.          
  1. Kula ndizi
  2. Kufua nguo
  3. Kuandika
 8.    
  1. Fagio
  2. Ndoo
  3. Ragi 
 9.     
  1. atakuja
  2. kabla ya
  3. vizuri
  4. mzuri
  5. usafi

SARUFI

 1.         
  1. Sisi tunaondoka
  2. sisi tunasoma
  3. sisi tunaimba
  4. sisi tunakula
  5. sisi tunasikia
 2.      
  1. Macho
  2. Miguu
  3. Mikono
  4. Vidole
  5. Vichwa
  6. Magoti
  7. Masikio
  8. Mabega
  9. Midomo
  10. Nywele
 3.        
  1. Huyu 
  2. huyu
  3. hawa
  4. huyu
  5. hawa
  6. hawa
 4.           
  1. Letu
  2. zangu
  3. wangu
  4. kwetu
  5. vyetu
  6. yangu
 5.        
  1. wangu
  2. Kwangu
  3. letu
  4. changu
  5. yetu
 6.          
  1. Ndege
  2. Kitanda
  3. Simba
  4. Mti
  5. Kikombe
  6. Tembo
 7.              
  1. Mkulima analima vizuri
  2. Si vizuri kupigana
  3. Kila asubuhi ninaomba ninaomba.
  4. Huu niunga
  5. Pazia zuri ni letu /pazia letu ni zuri
 8.       
  1. i
  2. i
  3. i
  4. i
  5. i
 9.       
  1. a, u
  2. v
  3. ani
  4. a, a
  5. u,I,a
 10.      
  1. Kufuli
  2. sweta
  3. yai
  4. Dirisha

MSAMIATI

 1. Kupaka rangi
 2.            
  1. Shingo
  2. Mkono
  3. vidole
  4. Goti
  5. Kisigino
  6. Kiuno
  7. Mdorno
  8. utosi
 3.    
  1. Saba
  2. Tana
  3. Macho
  4. Ng'ombe
  5. Minne
  6. Kiuno
  7. Miguu
  8. Nyuma
  9. Gumba
  10. Pua
  11. manjano
 4.      
  1. dukani
  2. Chooni
  3. pipi
  4. Chumvi
  5. Kitanda
 5.     
  1. Halati
  2.  Nyanya
  3.  Babu
  4. Daktari
  5. vyakula
 6.   
  1. Mahindi
  2.  boga
  3. Mihogo
  4. Maharagwe
  5.  Papai
  6. Nyanya
  7. Chapati
  8. Kabeji
 7.     
  1. Mbili
  2. tano
  3. saba
  4. Nane
 8.     
  1. Jumamosi
  2. Jumatatu
  3. Ijumaa
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Homework Activities - CBC Grade 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


.