Monday, 01 November 2021 13:19

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 4 End Term 2 Exams 2021 SET 1

Share via Whatsapp

Mwalimu ajaze mjalizo baada ya kusahihisha kazi ya mwanafunzi

Jumla ya alama = 50
Viwango vya kutathmini   
Kuzidisha matarajio
(50)
 kufikia matarajio 
(25 - 49) 
kukaribia matarajio 
(16-24)
Mbali na matarajio
(0 - 15) 
       


MASWALI

SEHEMU YA KWANZA  (Alama 20)
Kusikiliza na kuzungumza.

 1. Soma maneno haya.
  Kizingiti                  Tumbuu              Globu            Tendeguu           Kochi
  Kinu                        Mchi                   Dari               Balbu                 Sebuleni
 2. Taja wanyama watano wanaofugwa nyumbani.
  1. .....................................
  2. .....................................
  3. .....................................
  4. .....................................
  5. .....................................
 3. Taja vifaa vitano vya nyumbani.
  1. .....................................
  2. .....................................
  3. .....................................
  4. .....................................
  5. ..................................... 

SEHEMU YA PILI
KUSOMA
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.    (alama 10)
Shangazi yangu anaitwa Chaurembo. Zamani alifanya kazi katika hospitali. Aliacha kazi hiyo na kuanza biashara ya kuuza bidhaa sokoni. Biashara hiyo inamletea faida. Wanunuzi wanampenda sana. Anawauzia bidhaa kwa bei nafuu. Anawauzia pia bidhaa nzuri na halali.
Kibanda chake ni safi. Shangazi Chaurembo ni mwaminifu. Anatumia ratili kupima bidhaa zake. Anarudishia mnunuzi baki sahihi. Chaurembo ni muuzaji kwa mzuri wanunuzi wa bidhaa zake. Ni mfanyibiashara maarufu.

 1. Shangazi yangu anaitwa nani?.....................................
 2. Hapo zamani alifanya kazi wapi?.....................................
 3. Chaurembo anatumia nini kupima bidhaa zake!.....................................
 4. Taja sifa mbili za bidhaa ambazo shangazi Chaurembo anawauzia wanunuzi.
  1. .....................................
  2. .....................................
 5. Sema ndio ama la.
  1. Shangazi yangu anaitwa Chausiku.
  2. Shangazi hakuacha kazi hospitalini.
  3. Chaurembo huuza bidhaa sokoni.
  4. Shangazi yangu ni mwaminifu. 
  5. Kibanda cha shangazi yangu si safi. 

SEHEMU YA TATU      (Alama 20)
SARUFI
Kanusha maneno haya.

 1. Anaimba
 2. Anakula 
 3. Tulienda 
 4. Watacheza
 5. Mlituburudisha 

Tumia viwakilishi 'mimi', 'sisi'. 'wewe', au 'wao' kujaza pengo.

 1. .....................................unapenda somo lipi?
 2. .....................................ninasoma hadithi fupi.
 3. .....................................utaniletea maziwa kesho?
 4. .....................................tunakariri mashairi darasani. 
 5. .....................................walikula chakula kitamu jana. 

Andika wingi wa sentensi hizi.

 1. Kitabu changu kimeraruka. .....................................
 2. Mpira unachezwa. .....................................
 3. Mtoto analia. .....................................
 4. Ukuta umebomoka. .....................................
 5. Kalamu imevunjika......................................

Andika kwa nambari. 

 1. Themanini na saba.  - .....................................
 2. Mia nne hamsini na sita.   - .....................................
 3. Mia saba na tisa.   - .....................................
 4. Tisini na nne.   - .....................................
 5. Elfu moja.   - .....................................


Marking Sheme

 1. Chaurembo
 2. Hospitalini. 
 3. Ratili,
 4.                        
  1. bidhaa nzuri.
  2. bidhaa halali.
 5.                    
  1. la
  2. la
  3. ndio
  4.  ndio
  5. la
 6. haimbi
 7. hali
 8. hatukuenda 
 9. hawatacheza
 10. hamkutuburudisha
 11. wewe 
 12. mimi 
 13. wewe
 14. sisi
 15. wao
 16. vitabu vyetu vimeraruka. 
 17. mipira inachezwa. 
 18. watoto wanalia.
 19. kuta zimebomoka.
 20. kalamu zimevunjika. 
 21. 87 
 22. 709
 23. 1000
 24. 456
 25. 94

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 4 End Term 2 Exams 2021 SET 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


.