Tuesday, 02 November 2021 07:50

Kiswahili Activities Questions And Answers - CBC Grade 4 End of Term 2 Exam SET 2 2021

Share via Whatsapp

KISWAHILI
GREDI LA 4
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA 2

SEHEMU YA KWANZA
KUSIKILIZA NA KUONGEA (Alama 15)

  1.    
    1. Andika maneno ambayo mwalimu atakusomea.
      Sikiliza kwa makini, kisha uandike(Alama 5)
      1.      
      2.     
      3.     
      4.      
      5.     
      6.     
    2. Tegua vitendawili hivi (Alama 2)
      1. Teketeke huzaa gumugumu na gumugumu huzaa teketeke
        _______________________________________________
        (yai, macho, nyayo)
      2. Huwa safi kikiwa cheusi na kichafu kikiwa cheupe
        _______________________________________________
        (kalamu na kitabu, ubao)
    3. Taja wakati wa maamkuzi na maagano haya. (Alama 3)
      (asubuhi, jioni, adhuhuri, wakati wowote, usiku)
      1. Hujambo
      2. Lala unono
      3. Sabalkheri
    4. Kamilisha methali hizi.(Alama 2)
      1. Pole pole ndio
      2. Mtoto wa nyoka
    5. Ambatanisha maneno haya ya upole ipasaavyo. Fuata mfano. 
      KISG4et221qE

SEHEMU YA PILI SARUFI (Alama 20)

  1.    
    1. Soma kifungu hiki kisha uchagua nomino kutoka kifungu (Alama 5)
      Mwalimu wangu anapenda kufunza lugha ya Kiswahili. James husoma vizuri katika kipindi cha lugha. Jumatatu masomo ya asubuhi, Naomi pia husoma ufahamu kwa ufasaha, kweli watu wa Mombasa hupedna kiswahili kuliko wengine.
      1.     
      2.     
      3.     
      4.    
      5.  
    2. Tafuta vitendo kumi katika mraba huu. (Alama 10)
      Mfano pika 
      KISG4et221q2b
      Vitendo
      1.    
      2.     
      3.     
      4.     
      5.     
      6.     
      7.      
      8.     
      9.     
      10.      
    3. Andika sentensi hizi upya. Tumia viwakilishi.
      (sisi, wewe, yeye, w 10) badala ya maneno yaliyopigiwa mstari.(Alama 2)
      1. Damiana analima shamba
        ______________________
      2. Wanafunzi tutafunga lini?
        ______________________
    4. Pigia mstari viunganishi katika sentensi hizi.(Alama 2)
      1. Maembe,machungwa na mananasi ni matunda.
      2. Nilimshauri ila hakusikia.
    5. Maneno polepole, vizuri, haraka haraka, upesi na darasani ni (Alama 1)
      ____________________________________________
      (nomino, vielezi, viwakilishi, viunganishi)

SEHEMU YA TATU KUSOMA (Alama 10)
Soma kifungu kisha ujibu maswali.

Asubuhi moja, mama alikuwa tayari kuondoka akielekea kazi pale, Tembea Tuonane. Aliwaita watoto wake na kuwaambia wamsikilize kwa makini.

“Ninaenda kazini. Nimeacha kila kitu kikiwa sawa hapa nyumbani. Ninajua mnapenda mchezo. Nikirudi nipate nyumba na vyombo vyote vichafu. Nipate pia mmekula chakula chote hata cha mtoto, sawa?" mama aliwambia,kwa kujua mazoea ya watoto wake. “Sawa, mama!" wote walijibu. Mama aliondoka akaenda kazini.

Maswali.

  1. Nani alikuwa anaenda kazi asubuhi ile?______________________
  2. Mama aliwataka watoto wasikilize kwa______________________
  3. Mama anaposema, nikirudi nipate nyumba na vyombo vyote ni vichafu ana maanisha nini?______________________
  4. Watoto wale walikuwa na mazoea yapi?______________________
  5. Je, unafikiri mama aliporudi jioni alipata watoto wamefanya nini?______________________

INSHA

Andika insha kuhusu: Sherehe Nyumbani Kwetu

MAAKIZO

sehemu ya kwanza

  1.      
    1. Mwanafunzi anapaswa kuandika maneno ambayo mwalimu atamsomea.
    2.     
      1. yai
      2. ubao
    3.               
      1. wakati wowote
      2. usiku
      3. asubuhi
    4.            
      1. mwendo 
      2.  ni nyoka
    5.          
      KISG4et221qE Copy 

sehemu ya pili

  1.     
    1.    
      1. Mwalimu
      2. James
      3. Jumatatu
      4. Naomi
      5. Mombasa
    2.      
      1. pakua
      2. amsha
      3. andika
      4. tandika
      5. kaa
      6. fagia
      7. anika
      8. sugua
      9. shona
      10. panga
    3.      
      1. Yeye
      2. Sisi
    4.        
      1.  na
      2. ila
    5. vielezi

sehemu ya tatu

  1. mama
  2. makini
  3. anamaanisha kinyume/ anamaanisha wasifanye jinsi alivyosema/ anamaanisha kuwaonya wasifanye hivo alivyosema
  4. ya kucheza
  5. alipata vyombo safi/nyumba safi/ chakula hakijaliwa chote/ chakula cha mtoto hakijaliwa
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Activities Questions And Answers - CBC Grade 4 End of Term 2 Exam SET 2 2021.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.