Monday, 07 February 2022 08:07

Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End Term 3 Exam 2022 Set 2

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma kifungu hiki na ujalize nafasi 1-15
Nilikaa __1__ na __2__ maswali __3__ sana. Pamoja na maswali __4__, nilishangaa ni kwa nini mara __5__ watu __6__ kukitumia Kiswahili shaghalabaghala __7__ ya kutumia Kiswahili aula? Ukweli __8__ jambo __9__ ni __10__ wanadamu wengi hawako tayari kujishughulisha katika kufanya utafiti na __11__ hawana __12__ kwamba utafiti __13__msingi wa kupata ukweli na uhakika wa kitu au jambo __14__. Kiswahili bora hakipatikani __15__ bila kujifunza kwa makini na kwa dhati.

  1.              
    1. Chali
    2. kufudifudi
    3. kingalingali
    4. kitako
  2.                  
    1. Kujiuliza
    2. kuuliza
    3. kumwuliza
    4. kuliuliza
  3.                          
    1. nyingi
    2. mengi
    3. mingi
    4. vingi
  4.                
    1. hayo
    2. hiyo
    3. hizo
    4. hivyo
  5.                    
    1. mingi
    2. nyingi
    3. mengi
    4. vingi
  6.                      
    1. wanaitakia
    2. wanakubali
    3. wanakubalishwa
    4. wanaitishwa
  7.                  
    1. badala
    2. wala
    3. vile
    4. baada
  8.                
    1. ya
    2. wa
    3. la
    4. za
  9.                
    1. hili
    2. huu
    3. hii
    4. hiki
  10.                    
    1. kua
    2. kuua
    3. kwa
    4. kuwa
  11.                      
    1. ila
    2. wala
    3. wale
    4. bila
  12.                          
    1. habari
    2. bahari
    3. bohari
    4. heri
  13.                            
    1. ndiye
    2. ndiko
    3. ndio
    4. ndivyo
  14.                            
    1. yoyote
    2. zozote
    3. lolote
    4. wowote
  15.                    
    1. hivi vivi
    2. vivi hivi
    3. vivyo hivyo
    4. hivyo hivyo

kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi kulingana na maagizo.

  1. Udogo wa neno njia ni ___
    1. Kinjia
    2. jia
    3. kijia
    4. kijijia
  2. Tambua kihusishi katika sentensi ifuatayo
    Nyoka hatari alimuuma mbuzi aliyelala chini ya miti.
    1. chini ya 
    2. mbuzi
    3. hatari
    4. alimuuma
  3. Taja ngeli ya neno ‘uongozi’
    1. U-U 
    2. A-WA
    3. U-YA 
    4. U-ZI
  4. Tumia kauli ya kutendesha kukamilisha sentensi ifuatayo.
    Halima alim___ mgeni wake kabla ya kula.
    1. nawisha 
    2. navya
    3. nawa 
    4. nawiza
  5. konokono no kwa kombe kama vile buibui ni kwa ___
    1. kizimba
    2. utando
    3. sega
    4. kifukofuko
  6. Chagua wingi wa sentensi hii
    Moyo wangu ulidunda nilipokuona
    1. Mioyo yetu ilidunda nilipomwona
    2. Mioyo yetu ilidunda tulipomwona
    3. Nyoyo zetu zilidunda nilipomwona
    4. Nyoyo zetu zilidunda tulipowaona
  7. Neno ‘chuku’ lina sauti ngapi.
    1. 5
    2. 3
  8. Ni tamathali gani yam semi hutumia ulinganisho wa moja kwa moja bila kutumia sifa?
    1. Istiara 
    2. tashbihi
    3. nahau 
    4. methali
  9. Tegua kitendawili kifuatacho.
    Kisima changu hakitindiki maji.
    1. Kinywa 
    2. shimo
    3. moto 
    4. mamba
  10. Asilimia Ishirini na tano ni saw na:
    1. Sudusi 
    2. Robo
    3. humusi 
    4. ushuri
  11. Chagua sentensi yenye kiambishi –po- cha wakati.
    1. Uwele ulipomshika alitibiwa kwa haraka
    2. Painamapo ndipo painukapo
    3. Anapofanyia kazi ni pazuri
    4. Walipohamia pana usalama wa kutosha
  12. Baini sha usemi taarifa.
    “Kesho uje na mzazi,”mwalimu mkuu alimwambia rukia.
    1. Rukia aliambiwa na mwalimu mkuu aende kesho
    2. Mwalimu mkuu alitaka Rukia aende na mzazi siku hiyo
    3. Mwalimu mkuu alimwambia rukia uje na mzazi kesho.
    4. Mwalimu mkuu alimwambia Rukia aende na mzazi siku iliyofuata
  13. Kanusha
    Mtoto ambaye Analia amepigwa
    1. Mtoto ambaye Analia hajapigwa
    2. Mtoto ambaye halii hajapigwa
    3. Mtoto ambaye Analia hakupigwa
    4. Mtoto ambaye halii hakupigwa
  14. Chagua neno baki
    1. Muhibu 
    2. Saibu
    3. Masena
    4. Mwandani
  15. Tambua methali isiyowiana na uliyopewa “Haba nah aba hujaza kibaba”
    1. Tembe na Tembe huwa mkate .
    2. Tone na tone huwa mchirizi
    3. Chovya chovya humaliza buyu la asali
    4. Hayajai hayajai kumbe yanajaa

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 31-40.
Dawa za kulevya ni kitu chochote kinachoathiri hali ya kawaida ya mwili wa binadamu. Dawa hizi pia hutimiwa kwa njia tofauti sawa na madhara yake yalivyo. Dawa hizi ni kama vile: bangi, madraksi, heroini na pombe. Sigara, gundi na chang’aa ni vileo vinavyoouzwa na watu wengi na kupatikana kwa urahizi.
Sababu za kutumia mihadarati ni tofauti kulingana na watu walivyo tofauti. Wengine hutaka kudadisi dawa hizi au kuiga tabia za wengine. Wengine hutumia kwa kuathiriwa na vyombo vya mawasiliano kama runinga na upotovu wa jamii.
Dawa hizi zikitumiwa kwa muda mrefu husababisha uzoefu ambao ni mgumu kuacha. Vilevile zina madhara maridhawa kama vile kukosa makini masomoni, kukosa utaratibu wa kufanya mambo na kuwa kichaa. Uvutaji wa wa sigara na bangi husababisha saratani ya mapafu. Baadhi ya dawa hizi ni ghali mno na husababisha umasikini.
Wengine nao hujipata katika matukio ya kutisha. Kutokana na uzoefu na gharama yake wengi hutumia sirinji moja kujidunga. Katika harakati hizo wengine huambukizwa uwelehatari wa ukimwi. Hatima ya waja hawa ni kuifuata njia ya marahaba. Akina mama wajawazito hujipalia makaa katika vichwa vyao wanapohusika katika uraibu huu. Dawa hizo huathiri watoto ambao hawajazaliwa. Yafaa sote tuupinge ulanguzi kwa vyovyote vile.

  1. Dawa za kulevya ni ________
    1. Vitu vyovyote vya aina mbalimbali
    2. Chochote kinachoathiri binadamu
    3. Chochote kisichopendekezwa na daktari
    4. Chochote kinachotumiwa na kuathiri hali ya mwili wa binadamu.
  2. Madhara ya dawa za kulevya ni ___
    1. Sawa
    2. Tofauti na watu
    3. Tofauti kulingana na dawa
    4. Sawa kwa wote.
  3. Dawa zinazotumiwa sana na wengi ni ___
    1. Madraksi, sigareti na kokeini
    2. Madra, chang’aa na sigareti
    3. Chang’aa, sigara na gundi
    4. Gundi, chang’aa na kokeini.
  4. Taja kisawe cha dawa za kulevya.
    1. Madraksi
    2. Mihadarati
    3. Hadharani
    4. Dawa
  5. Kufuata njia ya marahaba ni ___
    1. Kufaulu katika maisha
    2. Kujibu salamu za ‘shikamoo’
    3. Kuwa maskini
    4. Kuaga dunia
  6. Ni ipi kati ya sababu hizi haiwafanyi watu kutumia mihadarati?
    1. Kuathiriwa na vyombo vya habari
    2. Kufanya udadisi
    3. Upotovu wa jamii
    4. Uchumi wa nchi
  7. Saratani ya mapafu husababishwa na ___
    1. Sigara 
    2. Madraksi
    3. Kokeini
    4. Chang’aa
  8. Kutokana na taarifa hii ni kweli kusema __
    1. Kuna dawa ambazo hudungwa mwilini
    2. Dawa zote huvutwa
    3. Sigara huvutwa na kila mmoja
    4. Dawa za kulevya hupatikana kwa urahisi na kwa bei ya chini.
  9. Dawa za kulevya zikitumiwa na wajawazito____
    1. Huathiri udhaifu mwilini
    2. Huathiri watoto ambao hawajazaliwa
    3. Huwa wenda wazimu
    4. Huwama haraka.
  10. Kichwa kifaacho habari hii ni ___
    1. Faida za dawa za kulevya
    2. Chang’aa, pombe na kokeini
    3. Dawa za kulevya
    4. Tabia mbaya.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50
Baada ya mateso ya muda mrefu kwenye mikono ya mwajiri katili, subira alinyanyuliwa na maafisa wa serikali waliosimamia haki za watoto. Mwajiri wake alijikuta mashakani alipopatikana akimtesa. Siku hiyo kweli ilikuwa ya afua kwa subira Mwajiri wake alitiwa mbaroni.
Subira alipelekwa shuleni aendelee na masomo yake. Kweli liandikwalo na Mungu lazima liwe, naye subira alisoma hadi kilele cha masomo hata ingawa alikuwa maskini hohehahe. Kutokana na misaada ya watu mbalimbali, alihitimu masomo yake ya shule ya upili na kupita vilivyo. Alikwenda chuoni kusomea ukandawala na baada ya kukamilisha kozi hiyo akaajiriwa. Hapo aliweza kupata pesa nzuri hiyo akaajiriwa. Hapo aliweza kupata pesa nzuri kwa mahitaji yake.
Huko nymbani, wavyele wake walizidi kudhoofika kimisha. Waliposikia kuwa mtoto wao wa pekee kupata kazi, wingu la tamaa liliwajia. Ajabu ni kuwa wingu hilo halikuwa mvua ya mafanikio kwao. Subira aliponda mali na kutia kutia masikio nta. Hakukumbuka alikotoka. Maharawa walimzingira kama nzi kidondani. Ama kwa hakika mirija yao ilivukuta uhondo wa kutosha kutoka kwa mwenzao. Waliogelea katika mavuno ambayo hawakuyapalilia wala kunyunyuzia maji.
Kwa bahati mbaya, kutokana na makossa madogo subira alipigwa kalamu. Hapo ndipo lisani , ‘mla naw e hafi nawe ila mzaliwa nawe’ ilisibu.wavyele wake waliposikia hivyo walikwenda kumtafuta wakaisha naye hadi akapata kazi nyingine.

  1. Ni nani aliyekuwa akimtesa Subira?
    1. Mwajiri wake.
    2. Katili wake.
    3. Maafisa wa serikali
    4. Wavyele wake
  2. Methali liandikwalo na Mungu lazima liwe ina maana gani?
    1. Barua kutoka kwa Mungu haisemi uongo.
    2. Subira alipita vizuri alivyoambiwa na Mungu
    3. Jambo lolote alipopenda Mungu litokee lazima litokee.
    4. Subira alisomeshwa kwa sababu Mungu aliamrisha.
  3. Subira alisomea kazi gani?
    1. Kuendesha pikipiki
    2. Kuendesha garimoshi
    3. Kuendesha matwana
    4. Kuendesndege
  4. Chagua jibu ambalo si sahihi kulingana na habari.
    1. Subira alishughulikia wazazi wake vizuri
    2. Wazazi wa subira hawakumbeza alipofutwa kazi
    3. Subira alikuwa na mashoga wengi
    4. Subira alipopata kazi baada ya chuo aliwasahau wazazi wake.
  5. Kauli “Waliongelea kwenye mavuno ambayo hawakuyapalilia wala kuyanyunyuzia maji” inatumika kurejelea nani?
    1. Wavyele
    2. Subira
    3. Marafiki
    4. Waajiri wake.
  6. Kazi ambayo subira alikuwa akiifanya ilikuwa ya aina gani?
    1. Kazi ya sulubu
    2. Kazi ya kijungujiko
    3. Taaluma
    4. Masaragambo
  7. Kwa nini wavyele wa Subira walimtafuta baada ya kufutwa kazi
    1. Walikuwa wamemtafutia kazi nyingine
    2. Marafiki walikuwa wamemtoroka
    3. Subira hakuwa amewatimizia mahitaji yao.
    4. Damu ni nzito kuliko maji .
  8. Tamathali gani ya usumi haiijatumika katika fungu.
    1. Tashbihi
    2. Methali
    3. Nahau
    4. Tanakali za sauti
  9. Kutia masikio nta ina maana gani?
    1. Kupaka nta kuyaziba
    2. Kujifanya husikii lolote
    3. Kusikia kila jambo
    4. Kuwa kiziwi kabisa
  10. Je, jambo gani lilisababisha kufutwa kwa Subira?
    1. Anasa
    2. Chudi kazini
    3. Shirika kufilisika
    4. Alipata kazi kwa njia ya mkato.

MWONGOZO

swa ms

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika Insha yako.
Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa.
Mwandikie rafiki yako barua ukimueleza kuhusu umuhimu wa kutia bidi masomoni.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End Term 3 Exam 2022 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students