Tuesday, 19 April 2022 13:20

Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End of Term 1 Exams 2022 Set 2

Share via Whatsapp

QUESTIONS

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaku 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Usiku _1_Bw. Mateso hakupata hata _2_. Ujumbe wa _3_  ule ulimwangaisha _4_. Aliwaza na kuwazua namna _5_ naye. Usiku wa manane _6_, usingizi ukamchukua na punde si punde akalala _7_. La ajabu ni kuwa _8_ msituni asubuhi huku amezingirwa na majitu _9_ silaha hatari.

 1.                    
  1. hiyo
  2. huo
  3. hii
  4. huu
 2.                            
  1. sauti kidogo
  2. kiamsha kinywa
  3. furaha riboribo
  4. lepe la usingizi
 3.                    
  1. barua
  2. arafa
  3. waraka
  4. tangazo
 4.                  
  1. usiku kucha
  2. mchana kutwa
  3. usiku kutwa
  4. mchana kutwa
 5.                    
  1. watakayekutana
  2. atakutana
  3. atakavyokutana
  4. waliokutana
 6.                                      
  1. ilipoingia
  2. uliingia
  3. yalipoingia
  4. ulipoingia
 7.                        
  1. ndindindi
  2. fofofo
  3. goigoi
  4. rovurovu
 8.                            
  1. alijipata
  2. walijipata
  3. ilijipata
  4. yaliwapata
 9.                    
  1. zenye
  2. wenye
  3. yenye
  4. mwenye

Nilikaa _ 10_ huku nikijikuna kichwa kuhusu _11_ kutatua shida _12_. Mkururo wa matatizo mengi _13_. Hakika _14_. Kupata chakula kwangu kulikuwa kumeadimika kama _15_. Hata hivyo, hatimaye nilifua dafu na ninamshukuru Mungu.

 1.                          
  1. nyuma
  2. kitako
  3. chini
  4. chali
 2.                      
  1. jinsi ya
  2. hali ya
  3. mambo ya
  4. vile ya
 3.                      
  1. hayo
  2. hilo
  3. hiyo
  4. hayo
 4.                
  1. ulinifuata
  2. yamenifuata
  3. iliyonifuata
  4. zilizonifuata
 5.                    
  1. vyote ving'aavyo si dhahabu
  2. hakuna kubwa lisiloshindwa
  3. muumbiko ubichi hula mbivu
  4. la kuvunda halina ubani
 6.                  
  1. wali wa daku
  2. kinu na mchi
  3. sahani na kawa
  4. uta na upote

Kuanzia swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi kulingana na maagizo.

 1. Chagua neno ambalo ni nomino maalum katika sentensi hii:
  Hadija alienda kwale jumapili asubuhi.
  1. Hadija. 
  2. Kwale. 
  3. Jumapili. 
  4. Asubuhi.
 2. Ni sentensi ipi iliyo na kivumishi cha pekee? 
  1. Wakulima wetu hupanda mikorosho mingi. 
  2. Wanafunzi wengine wamejiunga na shule yetu.
  3. Mabasi mengi ya shule yetu ni mazuri.
  4. Wanariadha kadhaa hufanya mazoezi.
 3. Watu walio na uhusiano wa damu wasiopaswa kuoana huitwa,
  1. binamu 
  2. mwanyumba.
  3. wakwe. 
  4. maharimu
 4.  Ni methali gani kati ya hizi inaonyesha bidii? 
  1. Laraka haraka haina baraka. 
  2. Kidole kimoja hakivunji chawa. 
  3. Mchumia juani hulia kivulini. 
  4. Asiyefunza na mama hufunzwa na ulimwengu
 5.  Kikembe cha ng'ombe ni ndama kama vile kikembe cha sungura ni,
  1. kisuse. 
  2. kiwavi. 
  3. kinegwe.
  4. kitungule.
 6. Kazi aliyomaliza ni moja kwa tatu kwa imetumika konyesha. 
  1. Baba amcenda kwake. 
  2. Sofia amerudi kwa jirani. 
  3. Tulimshangilia kwa sauti kuu. 
  4. Schemu ya kazi aliyomaliza.
 7. Ni orodha ipi inayoonyesha mpangilio wa siku sawasawa?
  1. Asubuhi, alfajiri alasiri, adhuhuri.
  2. Alasiri, adhuhuri, asubuhi, alfajiri.
  3. Alfajiri, asubuhi, adhuhuri, alasiri.
  4. Alasiri, asubuhi, adhuhuri, alfajiri.
 8. Chagua ukubwa wingi wa Simu yangu ni mpya. 
  1. Simu zetu ni mpya. 
  2. Jisimu langu ni jipya. 
  3. Majisimu yetu ni mapya. 
  4. Vijisimu vyetu ni vipya.
 9. Ni sentensi ipi ina "ji' nafsi au kirejeshi?
  1. Majiji ya taifa letu yamepanuka sana. 
  2. Wananchi walijichagulia kiongozi wao. 
  3. Mtangazaji hodari alituzwa
  4. Uogeleaji wake ulifurahisha mashabiki. 
 10. Chagua sentensi iliyotumia kiunganishi almuradi sawasawa. 
  1. Nilikuwa almuradi sikushiba.
  2. Sikumwona almuradi atafika. 
  3. Alishindwa kununua simualmuradi gani? 
  4. Unaweza kuenda kucheza almuradi urudi mapema.
 11. Kinyume cha panga ni,
  1. kutopanga.
  2. pangia.
  3. pangua
  4. punguza.
 12. Chagua sentensi iliyo sahihi.
  1. Sisi ndizi wanafunzi bora. 
  2. Nyinyi ndinyi mashabiki wa timu ile. 
  3. Wao ndiyo waliozawadiwa jana.
  4. Mimi siye niliyeandibiwa. 
 13. Majumba ya kumbukumbu za mambo ya kale huitwa, 
  1. makazi. 
  2. maktaba .
  3. maabae.
  4. makavazi
 14. Bainisha aina gani ya neno lililopigiwa mstari
  Mgeni wake alifika jana jioni.
  1. kiashiria. 
  2. kiele
  3. kimilikishi.
  4. kivumishi. 
 15. Neno nyadhifa'lina sauti ngapi?
  1. sita 
  2. talu.
  3. nane.
  4. tano

Soma taarifa ifuatayo kwa makini kisha ujibu maswali 31 - 40
Baada ya mateso ya muda mrefu kwenye mikono ya mwajiri katili. Vumilia alinyanyuliwa na maafisa wa serikali waliosimamia haki za watoto Mwajiri wake alijikuta mashakani alipopatikana akimtesa. Siku hiyo kweli ilikuwa siku ya afua kwake Vumilia. Mwajiri alishikwa na askari na kupelekwa ndani
Vumilia alipelekwa shuleni aendelee na masomo yake. Kweli liandikwalo na Mungu lazima liwe, naye vumilia alisoma hadi kilele cha masomo hata ingawa alikuwa maskini hohehahe. Kutokana na misaada ya watu mbalimbali, alikamilisha masomo yake ya shule ya upili na kupita vilivyo. Alikwenda chuoni kusomea Urubani. Baadaye aliajiriwa kazi na shirika la ndege la Kenya. Hapo, aliweza kupata pesa za kutosheleza mahitaji yake.
Huko nyumbani, wazazi wake walizidi kudhoofika kimaisha kwajumla. Waliposikia kuwa mtoto wao wa kipekee kapata kazi, wingu la tamaa liliwajia. Lakini ajabu ni kuwa wingu hilo halikuwa mvua ya mafanikio kwao. Vumilia aliponda mali na kutia masikio nta. Hakufikiria nyuma bali alisonga mbali na kuponda mali. Vinika njia walimzingira kama nzi kidondani. Ama kwa kweli mirija yao ilinyonya uhondo wa kutosha kutoka kwa mwenzao. Waliogelea kwenye mavuno ambayo hawukuyapalilia wala kuyanyunyizia maji. Kwa bahati mbayu, kutokana na makosa madogo madogo. Vumilia alifutwa kazi. Hapo ndipo marafikize wote walimtoroka. Wazazi wake waliposikia hivyo walienda kumtafuta wakaishi naye hadi akapata ajira nyingine.

 1. Ni nani aliyekuwa akimtesa Vumilia?
  1. Mwajiri wake
  2. Wazazi wake,
  3. Askari wa kusimamia haki za watoto.
  4. Walimu wake
 2. ...... alishilowa na askari na kupelekwa ndani" maana yake ni alishikwa,
  1. na kupelekwa kwake
  2. na kutiwa nyumbani 
  3. na kuwekwa korokorini
  4. na kuachiliwa
 3. Methaliliandikwalo na Mungu lazima liwe ina maana gani? 
  1. Barua ya kutoka kwa Mungu haisemi uongo 
  2. Jambo lolote alilopenda Mungu litendeke, ni lazima litendeke.
  3. Vumilia alisomeshwa kwa sababu Mungu aliamrisha, 
  4. Vumilia alipita vizuri kama alivyoambiwa na Mungu.
 4. Vumilia alisomea kazi gani?
  1. Urubani wameli
  2. Unahodha
  3. Urubani wa ndege.
  4. Uhandisi.
 5. Vumilia aliajiriwa na shirika lipi kati ya haya? Shirika la.
  1. meli la Kenya 
  2. ndege la Kenya. 
  3. la Kenya 
  4. urubani la Kenya.
 6. Moja ya yafutayo si ukweli, ni lipi? Vumilia.
  1. aliwashughulikia wazazi wake vyema. 
  2. hakuwashughulikia wazazi wake. 
  3. alipatana na wazaziwe alipofutwa kazi. 
  4. alikuwa na marafiki wa dhati.
 7. Nini maana ya kutia masikio nta?
  1. Kupata nta na kuyazibu kabisa 
  2. Kusikia kila jambo. 
  3. Kujifanya husikii lolote. 
  4. Kuwa kiziwi kabisa.
 8. "Waliogelea kwenye mavuno ambayo hawakuyapalilia wala kuyanyunyizia maji" Maana yake ni
  1. Kulima na kuvuna bila kupalilia wala kunyunyizia maji. 
  2. Kuogelea katika maji ya kunyunyizia mimea 
  3. Kutumia mali ambayo hukuyatafuta hata kidogo 
  4. Kutumia mali ambayo yalitokana na ukulima mbaya
 9. Kwa nini marafiki walimtoroka Vumilia? Vumilia
  1. aliwafukuza 
  2. alihara alikoishi.
  3. alifutwa kazi 
  4. aliwapatia kazi
 10. Je, Vumilia alipata kazi tena?
  1. La hakupata 
  2. Ndio alipata.
  3. Alikuwa na tamaa ya kupata. 
  4. Akutafuta sana, hakupata.

Soma kifungu kifuatacho bva makini kisha ujibu wa wall 41 - 50
Teknolojia mpya ni tawi la maarifa linalohusiana na sayansi kwa upande mmoja waruhandisi (uijimia) kwa upande mwingine. Sayansi ni elimu inayotokana na uchunguzi na majaribio katika mabara. Nao uhandisi ni ujuzi wa kuunda mitambo. Maarifa ya sayansi yanapotumiwa kutengeneza vitu viwandani, hali hii inakuwa teknolojia.
Vao mojawapo la teknolojia mpya ni ruhunu. Watu vijijini sasa wanawasiliana na jamaa zao walio mbali. Akipa nyanya wanapopanda jugu, kupalilia migomba, kukama ng'ombe na kukuna nazi, wanaweza kuzungumza na wajukuu wao walio uingereza, uchina na kwingine kule, hakuna mahali ambapo hapajafikiwa na teknolojia mpya. Tukitembelea baadhi ya nyumba tutaona vifaa kama vitu tanuri ya miale. Vile vile kuna jiko la mvuke ambalo linapika maharagwe yakaivat kwa dakika chuche tu. Majokofu nayo yanatuwezesha kuhifadhi vyakula bila kuharibika. Hata maiti nu mizoga inaweza kuhifadhiwa kwa miaka mingi kwa ajili ya utafiti bila kuaza katika ufuo wa mochari
Kwa upande wa kilimo, teknolojia imefanya makubwa. La kustaajabisha ni intu mmoja kulima eneo kubwa la shamba kwa trekta. Halafu akapanda kwa tandazi, akanyunyizia dawa kukausha magugu, akavuna na kukoboa mahindi akiwa peke yake. Siku hizi inawezekana kukuza mimea na kufuga wanyama wanaokomaa kwa muda mfupi na kutoa mazao maradufu kwa sababu ya teknolojia mpya. Teknolojia imewezesha watu kuvumbua aina nyingi za nishati. Badala ya kutegemea umeme unaotokana na maji tu, sasa watu wanatumia mvuke, nguvu za upepo na nishati ya jua kupata umeme. Kwa sababu hii hata mababu zetu vijini wanatazama televisheni bila shida au wahaka
Kwa upande mwingine, teknolojia ina madhara yake kwa mfano, uundaji wa silaha kali unaendelea kuwaangamiza watu wengi. Mabomu ya kitonoradi yaliyoangushwa Hiroshima na nagasaki Japani mwaka wa 1945 ni zao la kisayansi. Haya yaliwaua watu wengi na madhara yake bado yanadhihirika hata le katika maumbile ya watoto wanaozaliwa na upungufu Tena magaidi na wahalifu wa kimataifa wanatumia Icknolojia mpya kuimarisha mbinu zao za kutenda maovu. Isitoshe, inawezekana kutumia teknolojia kuagiza benki kutumia pesa nje ya nchi bila mwenye hazina kajua.
Wahalifu wanaweza kusikiza mawasiliano ya watu kwa simu hata ikiwa ni baina ya polisi. Kisha matatizo mengi ya kiafya yasemekana yanatokana na vyakula vilivyokuzwa kwa kutumia teknolojia mpya. Ingawa mwendo wake ni wa kasi kasi na stima huweza kusababisha ajali mbaya mno.

 1. Teknolojia mpya ni tawi linalohusiana na
  1. uchunguzi wa maabarani.
  2. sayansi na uhandisi 
  3. ujuzi wa kuunda mitambo. 
  4. utengenezaji wa vitu viwandani.
 2.  Baadhi ya mazao ya teknolojia ni.
  1. chungu, seredani, stovu na kuwa
  2. stuli, meza, kiti na kabati
  3. rununu, trekta, mikrowevu na tandazi.
  4. palasi, tupa, bisibisi na sepetu.
 3. Ni sentensi ipi si sahihi kulingana na kifungu? 
  1. Maarifa ya sayansi hayatumiwi kutengeneza vitu viwandani.
  2. Teknolojia limewezesha watu kuvumbua aina nyingi za nishati, 
  3. Gari moshi kutumia stima badala ya makaa. 
  4. Wanavijiji wanawasiliana na jamaa zao walio mbali.
 4. Neno kuhifadhiwalimepigwa mstari maana yake ni.
  1. kulaza
  2. kufichua
  3. kuharibu
  4. kulinda
 5. Taja baadhi ya vifaa vya mekoni ambavyo ni vya teknolojia
  1. Tanuri, stovu na jokofu.
  2. mikroevu, seredani, stovu. 
  3. jokofu, tanuri najiko la maliga 
  4. jokofu, tanuri na jiko la mvuke.
 6. Kisawe cha neno nishati ni.
  1. kawi 
  2. mwangaza.
  3. mvuke.
  4. joto.
 7. Maumbile ya watoto wanaozaliwa ya upungufu kwa sababu ya 
  1. risasi.
  2. mabomu. 
  3. mizinga 
  4. manowari.
 8. Kulingana na makala haya sentensi ipi ni sahihi? 
  1. Mtu hawezi kutuma pesa nje ya nchi. 
  2. Mabomu ya kitontoradi yaliyorushwa hayakulcta madhara. 
  3. Mtu anaweza kuagiza benki kutuma pesa nje ya nchi. 
  4. Magaidi hawawezi kutumia teknolojia mpya kuimarisha mbinu zao.
 9. Kwa mujibu wa aya ya mwisho, madhara ya fuatayo yamezungumziwa ila ya 
  1. afya. 
  2. mawasiliano 
  3. usafiri 
  4. elimu
 10. Kichwa mwafaka cha kifungut ikini.
  1. Teknolojia. 
  2. Elimu
  3. Afya 
  4. Madhara.

MARKING SCHEME

swa ms

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako

Wewe ni Kiranja wa shule yako. Toa hotuba kwa wenzako ukiwaeleza jinsi ya kujiandaa katika masomo shuleni.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End of Term 1 Exams 2022 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students