Monday, 07 February 2022 12:43

Shughuli za Kiswahili Maswali na Majibu - CBC Grade 4 End of Term 3 Exam SET 1 2022

Share via Whatsapp

Maswali

SEHEMU 1: Mazungumzo ya ana kwa ana (Alama 5)
Kila nchi ina bendera yake maalum. Bendera husimamia mambo mengi kuhusu nchi husika. Nchi yetu ya Kenya pia twajivunia bendera yetu. Je? 

 1. Taja rangi zote za bendera ya taifa. 
 2. Bendera inapopandishwa au kushukishwa mtu hufaa kufanya nini? 
 3. Kifaa kipi kinachopulizwa wakati wa kupandisha au kushikisha kwa bendera? 
 4. Rangi nyekundu katika bendera huonyesha nini? 
 5. Taja maeneo mawili utapata bendera ya taifa?

SEHEMU 2: Ufahamu wa kusikiliza (Alama 4)
Msikilize mwalimu akisoma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo.
Sare zangu za shule zilikuwa zimechakaa. Mwalimu wa darasa aliniita na kunisihi nikamweleze mzazi wangu anitafutie sare zingine. Kwa kweli sare za shule zina manufaa mengi mno. Huwezesha kujua na kutofautisha wanafunzi wa shule tofauti. Sare pia huwafanya wanafunzi wawe na usawa. Kuna sare tofauti za kike na za kiume. Wanafunzi wa kike huvaa blauzi na sketi, marinda au suruali. Wanafunzi wa kiume huvaa shati na kaptura au na suruali.

 1. Sare za msimulizi zilikuwa zime 
 2. Taja manufaa ya kuvaa sare za shule? 
 3. Wavulana huvaa sare gani? 
 4. Je, hapa shuleni wanafunzi wanavaa sare za rangi gani?

Sehemu 3: Kusoma kwa sauti
Soma kifungu kifuatacho kwa sauti.
Jana jioni baba alienda dukani. Alinunua sukari kwa shilingi mia moja hamsini na unga wa ngano kwa shilingi mia mbili. Aliporejea nyumbani alikuwa anatokwa na kichasho chembamba. Alipoulizwa na mama kwa nini anahema. Alisema vitu vimekuwa ghali mno. Mama alimsihi atulie ampe maji. Ilibidi nimweleze baba kuwa mambo yamebadilika. Vitu vimekuwa ghali kwa sababu viongozi hawajali wananchi.
Baba alitusihi tusome kwa bidii ili usoni tuchague viongozi wazuri. Maisha yanaweza kuwa mepesi tu kwa kuwa na elimu bora na viongozi wema. Alitupa mifano ya viongozi waliosoma kwa bidii na wema. Alituonyesha sinema zinazoonyesha kutii walimu na kuwa na bidii. Nakumbuka siku moja babu alipotutembelea alitueleza kuwa teknolojia itazidi kubadilika na kunawiri. Maisha nayo yatabadilika ikimlazimu mwanadamu naye awe mwenye kujielimisha kila siku.

Sehemu 4: Ufahamu wa kusoma
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Shule zinapofungwa wazazi wangu hunipeleka kuwatembelea babu na nyanya. Babu hunifunza jinzi ya kulima shambani. Yeye hunielekeza jinsi ya kuinua jembe na kupalilia mimea. Mara nyingi huwa napalilia mboga na mihindi. Mboga anazozipenda ni kama mchicha, Sukuma na mkunde.
Mkunde hutupa kunde na mbegu zake hutumika kama nafaka. Nafaka hizi zaweza sagwa na kuwa unga wa uji au kupilewa kama kitoweo. Waweza uza kunde na nafaka hizi sokoni ili upate hela za matumizi mengi.
Mchicha ndio mboga tamu ya bibi. Yeye huchanganya mchicha kwa kila chakula. Si wali, si pure si sima kwa nyama. Bibi husema kuwa mboga hizi zina madini ambayo huwezesha afya kuwa bora. Baada ya likizo babu hunipa zawadi murwa. Zawadi hizi ni kama kuku, sungura na njiwa.
Tangu nianze kuwatembelea babu na nyanya nimeweza kuzawadiwa sungura wanne. Sungura wawili ni weupe na wengine ni wa kijivu. Sungura wangu wakiwa wakubwa nitachinja mmoja mweupe awe kitoweo na wa kijivu nimpe mwalimu wangu wa Kiswahili kama zawadi.
Maswali

 1. Msimulizi huwatembelea nani shule zikifungwa? 
 2. Msimulizi alifundishwa nini na babu! 
 3. Ni manufaa gani anayopata mtu kwa kula mchicha na mboga zingine?
 4. Msimulizi ana uhusianio upi na bibi?
 5. Bibi hupenda mboga gani?
 6. Andika maana ya maneno yafuatayo. 
  1. babu 
  2. bibi

SEHEMU 5: Sarufi (Alama 20)
Nyambua vitenzi hivi katika kauli ya kutendwa?

 1. pika ...............................................................
 2. jenga ...............................................................
 3. penda ...............................................................
  Taja kisawe cha neno. 
 4. tembo  ...............................................................
 5. bibi ...............................................................
 6. runinga ...............................................................
 7. abu ...............................................................
  Tunga sentensi ukitumia maneno haya. 
 8. jua ...............................................................
 9. giza ...............................................................
 10. jengo ...............................................................
 11. kia ...............................................................
  Andika katika umoja. 
 12. Vyandarua vimeraruka. ...............................................................
 13. Vyakula vimeiva. ...............................................................
 14. Vyungu vimepasuka. ...............................................................
 15. Wakulima watavuna miwa. ...............................................................
  Piga mistari maneno yanayopatikana katika ngeli ya LI-YA. 
 16. Jembe, mlango, jani, sufuria, kochi, kalamu Eleza maana ya neno lifuatalo, 
 17. Mpwa
  Eleza maana ya maneno yafuatayo. 
 18. Mstari mmoja wa shairi huitwa? 
 19. Mishororo ikiwekwa Pamoja huitwa
  Chora kitu chochote kinachopatikana katika ngeli ya A-WA 
 20. 8n huhsfiuh

SEHEMU 6: KUANDIKA (ALAMA 15)
Andika insha ya wasifu kuhusu
NYUMBANI KWETU

Majibu

Sehemu 1: Mazungumzo ya ana kwa ana
Maagizo

 1. Andaa mazingira mazuri ya tathmini. Mkaribishe mwanafunzi.
 2. Mwamue na kumwomba akae.
 3. Jitambulishe kwake kwa kusema, 'Mimi ni mwalimu ..............................'
 4. Muulize jina lake.
 5. Anza tathmini.

Sehemu 2: Ufahamu wa Kusikiliza
Maagizo maalum

 1. Msomee mwanafunzi kifungu mara mbili.
 2. Mjulishe kuwa atajibu maswali baada ya kusomewa' kifungu mara ya pili. 
 3. Mpe alama moja kwa kila : swali analojibu vikamilifu..

Sehemu 3: Kusoma kwa sauti
Maagizo maalum

 1. Mfahamishe mwanafunzi matarajio ya Zoezi la Kusoma. 
 2. Mpe mwanafunzi nakala atakayoisoma kwa sauti. 
 3. Mwanafunzi anaposoma, sikiliza na kurekodi idadi ya maneno anayosoma kwa muda wa dakika moja.
 4. Onyesha kwa mshazari (√) mahali mwanafunzi alipofikia kusoma dakika moja ikikamilika.
 5. Mruhusu mwanafunzi kusoma mpaka mwisho wa kifungu
 6. Pigia mstari maneno yote ambayo mwanafunzi atashindwa kuyasoma au kuyatamka vizuri. 
 7. Rekodi viwango vya umlisi wa mwanafunzi.
 8. Hakikisha una nakala ya kurekodia tathraini hii. (!we na majina ya wanafunzi wote.)

Sehemu 4: Ufahamu wa kusoma

 1. Babu na nyanya 
 2. Kupalilia mimea 
 3. Kuwa na afya njema 
 4. Mjukuu 
 5. Mchicha
 6.                      
  1. babu-baba yo mama
  2. bibi-nyanya, mama ya mama au baba

Sehemu 5: Sarufi

 1. Pikwa 
 2. Jengwa 
 3. Pendwa 
 4. Ndovu 
 5. nyanya
 6. televisheni
 7. baba
 8.                        
 9.                         
 10.                      
 11.  Sahihisha sentensi zilizokamilifu
 12. Chandarua kimeraruka.
 13. Chakula kimeiva.
 14. Chungu limepasuka. 
 15. Mkulima atavuna muwa.
 16. Jembe,jani, kochi 
 17. Mtoto wa dada au kaka yangu
 18. Mshororo 
 19. Ubeti 
 20. Mchoro wa mnyama, nyani, binadamu, mdudu

Sehemu 6: Kuandika
Mtungo ni alama kumi.
Angazia kanuni za usahihishaji wa mtungo kama; hati, mtiririko, uasilia na ubunifu.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Maswali na Majibu - CBC Grade 4 End of Term 3 Exam SET 1 2022.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


.