Displaying items by tag: kiswahili

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 hadi 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua lifaalo zaidi.

Mawasiliano ni sekta mojawapo __1__hatua sana __2__ kuvumbuliwa kwa teknolojia mpya. Siku hizi hata __3__ wanaohifadhi faili na kupokea simu ofisini wamepunguzwa. Ulimwengu umekuwa duara __4__ tu __5__ habari huweza kuenea __6__ katika muda mfupi sana. __7__, hakuna kizuri kisicho na dosari. Watu wenye __8__ mbaya wanatumia fursa hiyo kusambaza uvumi. Wengine husambaza picha zisizofaa __9__. Tusipochukua tahadhari tutaishia kujiuma kidole kwani
__10__.

   A   B   C   D 
 1.   zilizopiga   yaliyopiga   tulizopiga   iliyopiga 
 2.  hadi  tangu   kuliko   kama
 3.  matarishi  masogora   wahazili  mabawabu 
 4.  ndogo  dogo0     kidogo   mdogo
 5.  ingawa  mathalani   lau   madhali 
 6.  zote  kote   yote  lote 
 7.  Labda  Vilevile   Hata hivyo   Isitoshe 
 8.  nia  lengo  madhumuni   kusudi
 9.  redioni  magazetini   dunaini  mitandaoni
 10.   baada ya dhiki ni faraja    majuto ni mjukuu   mstahimilivu hula mbivu    dalili ya mvua ni mawingu 


Tangu siku zake za ujanani, Kiburi hakujua maana ya jirani __11__ siku moja __12__ na ya kumfika. Alikuwa __13__ watu ambao waliamini kuwa wakipatwa na __14__ ndugu atawasaidia. Alisahau kuwa __15__.

   A   B   C   D 
 11.   mpaka   baada ya   kisha   hadi 
 12.  alipofikia   alipofikwa   alifikiwa   alifikwa 
 13.  miongoni ya   katikati ya   kati ya   baina ya  
 14.  siha  adhabu   maarubu   adha 
 15.    fimbo ya mbali haiui nyoka   mtegemea cha nduguye hufa maskini   heri nusu shari kuliko shari kamili   akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki

 

Kutoka swali la 16 hadi 30 jibu kulingana na maagizo.

  1. Neno mwanahewa lina silabi ngapi?
    1. Tisa
    2. Tano
    3. Nne
    4. Nane
  2. Genge ni kundi la watu linalofanya kazi pamoja ilhali kenge ni;
    1. ndege mwenye sura kama ya paka
    2. mnyama wa porini afananaye na mbuzi
    3. samaki afananaye na nyoka
    4. mnyama kama mamba mdogo
  3. Ikiwa jana ilikuwa Alhamisi, mtondo ilikuwa;
    1. Jumatatu
    2. Jumapili
    3. Jumatano
    4. Jumanne
  4. Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.
    Mama: Mwanangu, utanyolewa kesho jioni.
    1. Mama alimwambia mwanangu angenyolewa kesho jioni
    2. Mama akamwambia mwanawe atanyolewa siku iliyofuata jioni.
    3. Mama alimwambia mwanawe kuwa angenyolewa siku iliyofuata jioni.
    4. Mama alimwuliza mwanawe kama atanyolewa kesho.
  5. Joka la indimu ni kwa inda ilhali mkono wazi ni kwa;
    1. ukarimu
    2. uchoyo
    3. ujanja
    4. uvivu
  6. Ni maelezo yapi sahihi?
    1. Tathlitha ni shairi lenye mishororo minne kila ubeti.
    2. Ngonjera ni shairi la historia.
    3. Malenga hutunga mashairi na nyimbo.
    4. Tarbia ni shairi lenye mishororo miwili kila ubeti.
  7. Ki imetumiwaje katika sentensi? Mwalimu alipoingia tulikuwa kukiimba.
    1. Kuonyesha udogo.
    2. Kuonyesha kuendelea kwa kitendo. 
    3. Kuonyesha masharti.
    4. Kuonyesha namna.
  8. Miongoni mwa sehemu hizi za mwili, ni ipi iliyo tofauti na nyingine?
    1. Pafu
    2. Paja
    3. Kiganja
    4. Goti.
  9. Ni methali ipi yenye maana sawa na 'usiache mbachao kwa msala upitao'?
    1. Usione kwenda mbele kurudi nyuma kazi.
    2. Usipoziba ufa utajenga ukuta.
    3. Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno.
    4. Bura yangu sibadili na rehani.
  10. Tambua maneno yaliyopigwa kistari. Mwalimu mgeni atajiunga nasi mwakani.
    1. Kielezi, kihusishi
    2. Kivumishi, kiunganishi
    3. Kivumishi, kielezi
    4. Kiwakilishi, kivumishi.
  11. Ni jina lipi la makundi lisilofaa?
    1. Bunda la nyuki.
    2. Shehena ya mzigo.
    3. Chane ya ndizi.
    4. Kilinge cha wachawi.
  12. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo.
    Karani na wifi walifika jana.
    1. Makarani na wifi walifika jana.
    2. Karani na mawifi walifika jana. 
    3. Makarani na mawifi walifika jana. 
    4. Akina Karani na wifi walifika jana.
  13. Ni sentensi gani iliyotumia kwa kuonyesha sababu?
    1. Amekula wali kwa mchuzi.
    2. Alifurahi kwa kufikia utu uzima.
    3. Tatu kwa tano ya wanafunzi ni wavulana.
    4. Maria ataenda kwa shangazi yake kesho.
  14. Ni nomino zipi zilizo katika ngeli ya I-I?
    1. Maji, marashi
    2. Meza, dawati
    3. Mkate, maembe
    4. Mvua, chumvi
  15. Ni nahau ipi yenye maana ya kupata taabu au shida?
    1. Kula mwata
    2. Kata kamba
    3. Piga mbiu
    4. Laza damu.

Soma kifungui kifuatayo kisha ujibu maswali 31 hadi 40.

Subira alikuwa barobaro ambaye hakujimudu kimasomo. Alikuwa kisubutu masomoni. Hata hivyo, alijaliwa kipawa katika riadha. Alionekana kila asubuhi akifanya mazoezi ya kukimbia. Wapo waliomhurumia kuwa huenda hakuwa na akili razini. Weng walisikika wakisema alikuwa akiadhibiwa na Mungu. Akiwa mkembe walidai kuwa alitumwa na nyanya yake gulioni lakini akakataa.

Watu wengi walijisaili mbona akaanza kukimbia miaka mitano baada ya nyanya yake kutembelewa na Izraili wa kaputi. Baada ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu, Subira alianza kushiriki katika mashindano mbalimbali. Aliposhiriki mara ya kwanza, alishika nanga licha ya mazoezi ya bidii nyingi.

Aliendelea kufanya mazoezi pasi na kwenda nguu. Alivyozidi kujitahidi katika mazoezi ndivyo wengi walivyoendelea kumbeza. Hakubwaga silaha kamwe. Aliamini lisani ya wahenga isemayo kuwa atafutaye hachoki na akichoka keshapata. Mwaka uliofuata akiwa na umri wa miaka kumi na sita alishiriki tena katika mbio za masafa marefu. Alipata mwamko mpya alipofahamu kuwa ingawa hakushinda hali yake ilizidi kuimarika.

Alizidi kujiongeza maarifa. Akawa na matumaini kama tai kuwa siku moja angeibuka kifua mbele. Nusu mwaka baadaye, Subira alichaguliwa kuwa miongoni mwa wawakilishi wa nchi yao katika mbio za masafa marefu duniani. Huo ukawa ndio mwanzo mkoko unaalika maua. Nyota yake ikaanza kung'aa na mambo yakaanza kumwendea mserego. Aliamini lisani ya wahenga isemayo kuwa papo kwa papo kamba hukata jiwe.

Ulimwengu mzima ulishuhudia Subira akinyakua nishani ya dhahabu katika michezo hiyo duniani. Subira aliyekuwa akidhalilishwa na kupakwa tope akawa anasifika kote. Jina lake likawa kibwagizo midomono mwa wengi. Miaka michache baadaye akawa tajiri wa kutajika. Waliomcheka wakakosa pa kuziweka nyuso zao. Walipata funzo kuwa dhamira ni dira na nia zikiwa pamoja, kilicho mbali huja karibu.

  1. Kulingana na aya ya kwanza, ni kweli kusema kuwa;
    1. Subira alikuwa wembe shuleni
    2. Subira alifanya mazoezi ya kukimbia machweo
    3. Subira alihurumiwa na wanakijiji wote
    4. Subira hakujiweza sana masomoni
  2. Baadhi ya wakazi walisema kuwa Subira alikuwa akiadhibiwa kwa sababu;
    1. hakuwa na akili timamu
    2. akiwa mdogo alitumwa na bibi yake lakini akakataa
    3. hakuwa mcha Mungu
    4. mienendo yake haikuvutia
  3. Neno gulioni lina maana gani kulingana na kifungu?
    1. Sokoni
    2. Dukani
    3. Mtoni
    4. Shambani
  4. Ni methali ipi mwafaka kuelezea tabia za Subira baada ya kushindwa katika jaribio la kwanza?
    1. Mbio za sakafuni huishia ukingoni
    2. Asiyekujua hakuthamini.
    3. Kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa upishi.
    4. Mtegemea nundu haachi kunona.
  5. Ni nini maana ya alishika nanga kulingana na kifungu?
    1. Alipoteza matumaini
    2. Alikuwa wa mwisho.
    3. Alibadili nia.
    4. Alikuwa wa kwanza.
  6. Kushinda kwa Subira hatimaye kulitokana na;
    1. ujuzi, bidii na tamaa
    2. umri, ujana na utepetevu
    3. laana, maarifa na bidii
    4. bidii, ulegevu na ujuzi.
  7. "Akawa na matumaini kama tai." Hii ni mfano wa fani ipi ya lugha?
    1. Kinaya
    2. Chuku
    3. Istiara
    4. Tashbihi.
  8. Subira alikuwa akishiriki michezo katika dunia nzima. Hii inamaanisha alikuwa;
    1. hadhi yake ya kimichezo ilipanda 
    2. mtalii wa kutembelea mataifa
    3. mweledi wa kusafiri miji mikubwa
    4. mpenda anasa za dunia.
  9. Ni nini maana ya kupakwa tope kulingana na kifungu?
    1. Kutegemewa
    2. Kuharibiwa jina
    3. kuaibishwa
    4. kuchukizwa.
  10. Kichwa kinachofaa kifungu hiki ni kipi?
    1. Juhudi si pato.
    2. Tusiwe wa kutegemea wengine.
    3. Uvumilivu hutamausha maishani.
    4. Tusikate tamaa.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 hadi 50.

Kila mwanadamu ameumbwa akiwa na uwezo wake maalum. Mungu alifanya hivyo makusudi kabisa. Hebu fikira ulimwengu wenye watu ambao kila mmoja anajitosheleza. Yaani kila mtu anaweza kujifanyia kila kitu apendavyo. Ulimwengu usingehitaji watu wanaosomea kazi mbalimbali wala watu wasingetegemeana. Upendo na huruma vingekuwa havipo dunaini.

Mungu aliwaumba watu na vipawa vyao mbalimbali. Hata wanaofikiriwa kuwa hawana vipawa, ukiwachunguza vizuri utaona kuwa wana upekee fulani katika jambo wanalolimudu vizuri. Wakati mwingine, sio lazima jambo hilo liwe kubwa sana kiasi cha watu kulizungumzia. Kuna watu wasiokuwa na uwezo mkubwa wa kiuchumi lakini waliobarikiwa kwa uwezo wa kuzungumza vizuri au uwezo wa kuwashauri wengine wenye mahitaji mbalimbali. Hili linatukumbusha kuwa hata vipawa tunavyofikiri kuwa si vikubwa vina thamani kubwa ajabu.

Ingawa kila mtu ana kipawa chake, kuna watu wengi wasioweza kutambua vipawa vyao. Sababu moja inayowafanya washindwe kutambua vipawa hivyo ni kule kutokuwa na mtu wa kuwaongoza na kuwahimiza kuandama safari ya vipawa vyao. Sababu nyingine ni kwamba watu wengine hawaviamini wala kuvithamini vipawa vyao. Kwa mfano mtu anaweza kuwa na kipawa cha kucheza kandanda lakini akawa anataka kuwa daktari hata kama huo udaktari haumo katika damu yake. Mtu anapopuuza kipawa chake na kukifuata kingine tofauti huwa hana hamy na raha ya kufanya kazi ambayo hatimaye atakuwa amechagua kuifanya.

Wakati mwingine watu hupotishwa kuviacha vipawa vyao. Jamaa na marafiki huweza kumshawishi mtu kukiacha kipawa chake na badala yake kukifuata kile cha wale wanaomshauri. Mara nyingi wanaomshawishi mtu kuacha kipawa chake huwa hata hawajauelewa uwezo wa wanayemshauri. Japo watu wengine hufanikiwa kwa kuelezwa kufuata njia ambayo haikuwahusu, wengine hushindwa kufanikiwa, huwa kuna asilimia kubwa inayojilazimisha kuifanya kazi amambo haihusiani na talanta yao moja kwa moja.

Ni vizuri kutambua kwamba kuwa na kipawa tu hakutoshi. Kipawa cha mtoto ni mche unaohitaji maji, mwanga na mazingira mazuri yasiyo na magugu ili uweze kuimarika na kustawi, la sivyo utanyauka na kukauka. Mwenye kipawa anafaa kukilea kwa kukifanyia mazoezi ili kukiboresha. Anafaa kuwa na nidhamu ya kukiendeleza hadi kitakapokomaa. Anahitaji kufuata ushauri na mwongozo wa watu wengine ambao wamekitumia vizuri kipawa sawa na chake.

Tunafaa kutambua kuwa vipawa ni vingi jinsi walivyo watu. Vilevile hata watu wenye kipawa kile kimoja wana uwezo tofauti. Kama wasemavyo wahenga akili ni nywele kila mtu ana zake. Tukumbuke kuwa hata vidole havilingani

  1. Kulingana na aya ya kwanza ni kweli kuwa;
    1. bila kuwa na elimu wanadamu hawawezi kusaidiana
    2. kila binadamu ana mambo maalum anayopenda
    3. watu wanaojifanyia kila kitu huwashangaza wanajamii 
    4. hali ya kutegemeana husaidia kujenga maadili.
  2. Kwa mujibu wa aya ya pili;
    1. watu wengi hudhani kuwa wengine hawana vipawa
    2. kuna vipawa vya thamani kuliko vingine
    3. wakati mwingine watu wenye vipawa hawagunduliwi
    4. wasiokuwa na uwezo mkubwa wa kiuchumi wamebarikiwa.
  3. Kifungu kinaonyesha kuwa watu wengi hawawezi kutambua vipawa vyao kwa sababu;
    1. hukosa mwongozo unaofaa wa kukuza vipawa vyao
    2. huwa hawafurahishwi na vipawa vyao kama wenzao
    3. huwaza kuwa kutambua vipawa kunachukua muda mrefu
    4. hufikiri kuwa kipawa cha udaktari ndicho bora maishani.
  4. Ni kauli ipi sahihi kulingana na kifungu?
    1. Wasiojua umuhimu wa kazi huwazuia wengine kushughulikia kazi zao
    2. jamaa na marafiki huweza kumnyima mtu fursa ya kukuza kipawa chake
    3. wanaotoa ushauri kuhusu vipawa huwa wanawajua wenye vipawa hivyo
    4. kubadilisha kazi huifanya isiwe ya kuvutia kwa wale wanaifanya
  5. Kifungu kimebainisha kuwa;
    1. watu hufanya vizuri kuwashauri wengine kuacha vipawa vyao
    2. ushawishi wa marafiki huwa mkubwa zaidi kuliko wa wenye kipawa
    3. baadhi ya wanaoshauriwa kufuata vipawa tofauti na vyao hufaulu maishani
    4. ukujazi wa vipawa hutofautiana kulingana na imani ya mtu kwa Mungu
  6. Ni maelezo yapi si sahihi kulingana na mwenye kipawa?
    1. Anahitaji kukifanyia mazoezi ili kukiboresha
    2. Anahitaji kuhakikisha amekiimarisha hadi kitakapokomaa.
    3. Anafaa kufuata mfano wa wengine wenye vipawa sawa na chake.
    4. Anafaa kuwategemea wengine kukijenga kipawa chake
  7. Ni neno lipi ni kisawe cha kipawa?
    1. Nishani
    2. Ilhamu
    3. Kipaji
    4. Dhima
  8. Maneno... kipawa cha mtoto ni mche unaohitaji maji." yametumia fani ipi ya lugha?
    1. Istiara
    2. Tashbihi
    3. Kinaya
    4. Majazi
  9. Katika kifungu maana ya methali "Akili ni nywele kila mtu ana zake' ni;
    1. watu wenye hamu ya kushirikiana hutofautiana
    2. viwango vya uwezo wa watu vinatofautiana
    3. mitazamo ya watu kuhusu vipawa ni tofauti
    4. watu wanaothamini vipawa hutofautiana.
  10. Ni nini maana ya wanalolimudu kama ilivyotumiwa katika kifungu?
    1. Wanaloweza kulifanya
    2. Wanalolipenda
    3. Wanaloliamini
    4. Wanalofurahia kulipenda.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika Insha yako.

Malizia insha yako kwa maneno haya.

................................................................................................................Hakika tukio la siku hiyo haliwezi kusahaulika maishani.

MARKING SCHEME

  1. D
  2. B
  3. C
  4. A
  5. D
  6. B
  7. C
  8. A
  9. D
  10. B
  11. D
  12. B
  13. C
  14. D
  15. A
  16. C
  17. D
  18. A
  19. C
  20. A
  21. C
  22. B
  23. A
  24. D
  25. C
  26. A
  27. C
  28. B
  29. D
  30. A
  31. D
  32. B
  33. A
  34. C
  35. B
  36. A
  37. D
  38. A
  39. C
  40. D
  41. D
  42. C
  43. A
  44. B
  45. C
  46. D
  47. C
  48. A
  49. B
  50. A

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Ufugaji wa kuku ni njia mojawapo ya uwekezaji __1__sana na watu wengi __2__ kujiimarisha kiuchumi. Kuku hawa hufungiwa ̧__3__ na __4__ vyakula vinavyonunuliwa madukani. Kama __5__ wahenga __6__. Mfugaji __7__ ipasavyo hupata hasara kwani kuku huhitaji kutunzwa kwa makini nyakati __8__. Bila shaka shughuli hii ni __9__ njia za kukabiliana na uhaba wa nafasi za ajira nchini.

       A             B          C           D 
 1.   unaotumika   zinazotumika   inayotumika   unapotumika 
 2.  kwa minajili ya   mintaarafu ya   mithili ya   sambamba na 
 3.  mazizini  matunduni   viambazani   vizimbani 
 4.  kukulishwa  kulishwa   kulishiwa   kukula 
 5.  waliposema  waliosema   walivyosema   wangesema 
 6. mtaka cha mvunguni sharti ainame  mwenye pupa hadiriki kula tamu  kila chombo na wimbile  mtegemea nundu haachi kunona
 7.  asipowajibika  asiowajibika   asiyowajibika   akiwajibika 
 8.  yote  yoyote  wote  zote
 9.  baadhi ya  kati ya  fauka ya  dhidi ya

 

Maki alielewa vyema maana ya methali isemayo __10__ Japo alifanya kazi ya __11__, aliweka akiba __12__ hadi __13__ mtaji wa kuanzisha biashara __14__. Kwa njia hiyo, __15__hali yake ya maisha.

                      A                 B                        C   D 
 10.  tone na tone huwa mchirizi  chururu si ndondondo  kwendako hisani hurudi hisani  mgaagaa na upwa hali wali mkavu
 11.  msaragambo  kikoa   kijungujiko   shokoa 
 12.  dogodogo  kidogokidogo   vidogovidogo   mdogomdogo 
 13.  aliyopata  aliopata  alivyopata   alipopata 
 14.  yake yenyewe  lake mwenyewe   lake lenyewe   yake mwenyewe 
 15.  alimudu kuiboresha alijihimu kuyaboresha  alimudu kuyaboresha   alijihimu kuiboresha

 
Kutoka swali la 16 mpaka 30, jibu kila swali kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.

  1. Andika usemi wa taarifa wa sentensi ifuatayo.
    "Mto huu una mamba wengi," Shindo alisema.
    1. Shindo alisema kuwa mto huo huwa na mamba wengi.
    2. Shindo alisema kwamba mto huo ulikuwa na mamba wengi.
    3. Shindo alisema kwamba mto huo ungekuwa na mamba wengi.
    4. Shindo anasema kuwa mto huo una mamba wengi.
  2. Jora ni kwa vitambaa kama vile kande ni kwa
    1. samaki
    2. maua
    3. vibarua
    4. mawele.
  3. Chagua maelezo yaliyo sahihi.
    1. Pimamaji ni kifaa cha kupimia usawa wa ukuta.
    2. Fuawe hutumiwa na maseremala kutobolea mbao.
    3. Mvukuto hutumiwa na wahunzi kupulizia moto.
    4. Timazi hutumiwa kupimia usawa wa sakafu.
  4. Andika sentensi ifuatayo kwa wingi.
    Wimbi ulipepetwa kwa uteo ule.
    1. Mawimbi yalipepetwa kwa teo zile.
    2. Wimbi ulipepetwa kwa teo zile. 
    3. Mawimbi yalipepetwa kwa teo ile.
    4. Wimbi ulipepetwa kwa teo ile.
  5. Tegua kitendawili kifuatacho.
    Mtoto wangu mvivu hapandi mlima
    1. Upepo
    2. Mvua
    3. Mto
    4. Kobe.
  6. Chagua sentensi yenye kiwakilishi cha pekee.
    1. Vijana wote walishiriki michezo lakini wale walicheza vizuri zaidi.
    2. Dawati langu lina vitabu vingi lakini lake lina vichache tu.
    3. Mji huu na umeme lakini ule hauna miundomsingi muhimu.
    4. Shule yetu ina walimu wa kutosha lakini nyingine zina wachache tu.
  7. Salwa ni mtoto wa dada yangu. Jina linalofaa zaidi kwangu kumtajia Salwa ni
    1. mpwa
    2. umbu
    3. mkoi
    4. mkazamwana.
  8. Tambua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo zaidi.
    1. Mwezi uliopita Februari- kulikuwa na joto jingi.
    2. Tulihitaji viungo vifuatavyo: dania, iliki, karafuu na mdalasini.
    3. Mama aliniambia: usiwe mtu anayependa kustarehe.
    4. Maneno yote; yale yaliyoandikwa; yalikuwa sahihi.
  9. Kipande cha pili katika mshororo wa shairi huitwaje?
    1. Ukwapi
    2. Mwandamizi
    3. Utao
    4. Mloto.
  10. Baada ya hukumu kutolewa, mshatakiwa alituma ombi la kutaka hukumu ile ibatilishwe na kesi isikilizwe upya. Kwa hivyo mshtakiwa
    1. alikata rufaa
    2. aliruka kesi
    3. alitoa dhamana
    4. aliahirisha kesi.
  11. Chagua kitenzi kilichoundwa kutokana na kivumishi
    1. Maandishi - andika 
    2. Upishi-mapishi
    3. Mcheshi - kicheko 
    4. Mwangalifu - angalia
  12. Ni jozi ipi iliyo sahihi?
    1. Punda, nirihi 
    2. Bata, kiyoyo
    3. Paka, kilebu
    4. Ndovu, shibli.
  13. Bainisha matumizi ya kiambishi 'ki' katika sentensi ifuatayo.
    Kijana huyo akipewa nafasi atapambana kishujaa.
    1. Wakati, namna
    2. Kuendelea, jinsi
    3. Masharti, jinsi
    4. Udogo, masharti.
  14. Maelezo yapi hayaonyeshi maana ya neno 'changa'?
    1. Kukusanya fedha ili kutimiza haja fulani.
    2. Kupata maumivu ya viungo.
    3. Hali ya kitu kukosa kukomaa.
    4. Namna ya samaki wa baharini.
  15. Chagua methali yenye maana sawa na hii.
    Nazi mbovu ni harabu ya nzima.
    1. Nzi mmoja huoza ngombe.
    2. Samaki huanza kuoza kichwani.
    3. Mkataa pema pabaya panamwita 
    4. Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 31 mpaka 40.

Mengi yamesemwa kuhusu ufisadi. Si wanasiasa, si mapadre, si mashehe, si viongozi wengineo wa jamii, wote wametoa mchango wao juu ya suala hili nyeti. Kila linaloenda mvange, sababuye ufisadi. Nchi haina ustawi, kiini ni ufisadi. Kusambaratika kwa miundomsingi asili yake ni ufisadi.

Je, hapo ulipo unaelewa ufisadi kuwa ni nini? Huenda umewahi kujituliza na kutafakari juu ya ufisadi. Unahusika vipi na ufisadi? Umewahi kuathirika na ufisadi, wewe binafsi au kupitia kwa aila na masahibu? Kila mzalendo halisi anastahili kujisaili nafsi yake kupitia kwa maswali haya.

Wakati unapoendelea kuzingatia maswali hayo hebu tuzame kwenye kina cha ufisadi. Kijelezi cha ufisadi ni ile hali ya kutenda au kushiriki mambo yanayosababisha uharibifu au uborongaji wa kanuni au taratibu zilizokubalika kutekeleza mambo. Katika hali hii, ufujaji na ubanangaji huwa vyombo vya ufisadi. Madhumuni yake ya jumla ni kubatilisha haki, kuvotana na haki na hatimaye kuifanya isifuate mkondo wake sahihi.

Mbegu ya ufisadi ni uchoyo; kimsingi, chimbuko la ufisadi ni ubinafsi uliokithiri. Dhana ya kujiwazia kibinafsi katika shughuli zote ndiyo humpa ubinafsi nishati ya kujiendeleza. Kila mja ana kiwango fulani cha ubinafsi. Hali hii ndiyo hupelekea kujitahidi kwa jino na ukucha ili kujihifadhi na kujiendeleza. Ubinafsi wa aina hii hauna kasoro kwani humpa binadamu msukumo wa kujishughulikia kwa lengo la kijipatia natija inayofaidi aila, jamii na hatimaye taifa kwa jumla.

Uchoyo wa mimi-hiki, mimi-hicho, mimi-kile na hatimaye mimi-kila kitu ni uchuro. Ufisadi nao ni uchuro. Ni dude, jinyama, jipweza lenye minyiri isiyohesabika. Minyiri hiyo imepenyeza katika nyanja zote za maisha ya mtu binafsi na ya taifa kwa jumla. Ufisadi umeshamiri na kuzagaa hadi kufikia kiwango cha kimataifa.

Vuta taswira hali ya waja wazito wawili ambao zao zimewadia. Mmoja anajiweza anawasilishwa hospitalini kwa gari. Wa pili hana mbele wala nyuma amefika kwa miguu au pengine kwa rukwama. Kisia mwenyewe ni nani atakayehudumiwa kwanza. Ukitafiti utagundua kuwa sababu ni ufisadi. Mmoja atatadarukiwa ilhali mwenzake . atakawilishwa. Haya pengine ni kutokana na matumaini ya kupewa bahashishi ambayo kwa kweli ni namna ya hongo. Kumbuka, wahudumu wawa hawa ni waajiriwa wapokeao mishahara mwisho wa mwezi.

Katika amali za biashara, uborongaji wa taratibu unadhihirika hasa katika utoaji wa zabuni za miradi mbalimbali ambapo suala kubwa ni kasma. Kiasi na jinsi ni baada ya kuhakikisha kuwa tenda imeliendea shirika fulani. Kasma lazima ipatikane! Si hoja kuwa pesa za kugharamia miradi hii zimetokana na ruzuku au mikopo kutoka kwa wafadhili. Ghushi za kila aina zitatumiwa ili kasma ipatikane. Katika hali kama hii, si ajabu matokeo ni kuharibika kwa miundomsingi katika sekta mbalimbali zinazohusika na usambazaji wa huduma kwa wananchi.

Ni dhahiri shahiri kuwa kila mmoja anapaswa kujumuika katika kitali hiki dhidi ya ubinafsi, ufisadi na ubanangaji. Sote tukianzia na viongozi, tunapaswa kujifunga nira kupambana na ufisadi. Wananchi wahamasishwe juu ya wajibu wao katika vita hivi vikali. Sote tuzinduke na kufahamu hicho kidogo cha ziada, hiyo fadhili, mapendeleo hayo ambayo msingi wake ni kuvuruga utaratibu yatatuponza. Changamoto kwa kila mmoja wetu ni: Tuko tayari kuziasa nafsi zetu ili zitambue athari za ubinafsi na hivyo kuzikabili vilivyo? Tutakapotambua kuwa waendelezaji wa ubinafsi ni mimi na wewe, hapo ndipo vita hivi vitakapoanza kufanikiwa.

  1. Kulingana na aya ya kwanza
    1. viongozi mbalimbali wa kijamii wamehusishwa na ufisadi
    2. ufisadi ni chanzo cha kuvurugika kwa mambo mengi katika jamii
    3. viongozi wamepuuza mchango wao katika vita dhidi ya ufisadi
    4. kuharibika kwa miundomsingi kumefanya watu wawe mafisadi.
  2. Si kweli kusema kuwa
    1. mwandishi ana hakika kwamba msomaji amewahi kuwazia ufisadi
    2. wakati mwingine ufisadi haumwathiri mtu moja kwa moja
    3. jamaa na marafiki wanapofikwa na madhara sisi huathirika pia
    4. mtu anayeipenda nchi yake anapaswa kuwaza kuhusu misingi ya ufisadi.
  3. Ufisadi hasa unahusu nini?
    1. Utoaji wa pesa kinyume na sheria. 
    2. Kutojua vizuri sheria za jamii yake.
    3. Njama za kubadilisha mkondo wa haki.
    4. Kujuana na walio katika nafasi za uongozi.
  4. Maana ya 'kujitahidi kwa jino na ukucha' ni 
    1. kuvumilia shida ili uweze kufanikiwa
    2. kushiriki njama ziletazo maangamizi 
    3. kupigana na wale wanaokiuka sheria
    4. kufanya bidii kwa vyovyote vile.
  5. Mwandishi anasema kuwa ubinafsi hauna shida ikiwa
    1. utamletea mtu manufaa anayotarajia
    2. haujagunduliwa na vyombo vya dola
    3. wanaoathirika na hulka hiyo ni wachache 
    4. utazalisha manufaa yatakayowafaidi wote.
  6. Taswira inayotolewa kuhusu hali iliyo hospitalini ni kuwa
    1. wagonjwa hufikishwa kwa njia ainati
    2. huduma zinatolewa kwa mapendeleo 
    3. ukabila unajitokeza katika kuwashughulikia wagonjwa
    4. wanaohudumiwa vizuri hawana shida ya kutoa bahashishi.
  7. Utoaji wa zabuni bila kuzingatia utaratibu ufaao
    1. umeathiri utoaji huduma kwa wananchi
    2. hutokana na juhudi za serikali kukomesha ufisadi
    3. umesababisha kupatikana kwa huduma bora zaidi
    4. haujaliathiri taifa wala watu binafsi.
  8. Ipi si njia ya serikali kupata pesa za kuendesha miradi yake?
    1. Ushuru
    2. Misaada
    3. Mikopo
    4. Rushwa.
  9. Wito wa mwandishi katika aya ya mwisho ni kuwa
    1. tuwatambue mafisadi ili tukabiliane na uovu huu
    2. kila mmoja ajitahidi kugundua madhara ya ufisadi
    3. vita dhidi ya ufisadi vianze kwa sisi wenyewe kujiasa
    4. tuendeleze ubinafsi ili kufanikisha vita dhidi ya ufisadi.
  10. Neno jingine lenye maana sawa na 'kitali' ni
    1. uovu
    2. juhudi
    3. vita
    4. harakati.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 41 mpaka 50.

Mzee Maganga alikuwa tajiri maarufu katika mtaa wa Shwari. Wakazi wengi walimstahi kutokana na idili na maarifa yake ya kuendesha biashara. Aidha mzee huyu asingejumuishwa katika orodha ya adinasi wenye mkono birika. Hakika mzee huyu alikuwa mkwasi wa mali na moyo kwani mbali na kuwakidhia wanawe mahitaji yao yote, aliwasabilia wanakijiji kwa mengi. Wapo waliopewa ruzuku za vyakula, karo za wanao ada ya matibabu na hata vibarua almradi waweze kuzikimu aila zao.

Maganga mwenyewe hakuzaliwa na asali mdomoni. Inasemekana baba yake alikuwa fukara fukefuke. Kwa bahati nzuri alipata msaada wa kanisa akawaelimisha maganga na nduguze hadi vyuo vikuu. Ndugu zake walipata kazi serikalini lakini Maganga ambaye alisomea elimu biashara aliamua kuanzisha kazi yake binafsi. Alikuwa na maduka kadhaa kuanzia yale ya vipuri, ya nafaka, ya vitabu na hata kiwanda cha kukobolea mpunga.

Makali ya umri sasa yalianza kumlemea Maganga. Alikuwa si yule Maganga aliyerauka mapema kuenda kukagua shughuli katika biashara zake. Kila mara alijihisi mnyonge huku mwili wake ukilemewa na maumivu ya viungo. Maganga alijawa na hofu sio kwa sababu ya hali hii mpya kwani alielewa kuwa hii ni ada ya kila mja. Moyo ulimwuma kutokana na hali ya mwanawe wa pekee kuandama anasa kila uchao. Majanga alihofia kuwa angeenda kaburini na biashara zake.

Siku moja, Maganga alimwita mwanawe akamshtakia hali. Alimweleza kinagaubaga kuwa utendakazi wake ulikuwa ukikaribia ukingoni. Kijana alionyesha huruma machoni lakini moyo ulimdunda kwa raha ya kurithi milki ya baba yake. Mzee mwenyewe aliliona hili waziwazi. Hata hivyo alijitia hamnazo. Alimwagiza mwanawe ampelekee shilingi laki moja, pesa taslimu alizozifanyia kazi yeye mwenyewe. Kijana alimweleza mamaye, naye akaahidi kumpa fulusi zile baada ya juma moja.

Baada ya kupokea kitita kile kutoka kwa mama yake, kijana alimwendea mzee Maganga chumbani alimokuwa akiota moto. Bila kuzihesabu pesa zile, mzee alizitupa motoni zikateketea huku kijana amejitazamia tu, akingoja mzee atimize ahadi kwani ahadi ni deni. Hapo mzee alimtazama kijana akasema, "Nenda uniletee shilingi laki moja; jasho lako hasa!”

Kijana alikereka moyoni, akatuhumu kuwa mama alikuwa amemsaliti. Aliwaendea marafiki zake waliozoea kustarahe pamoja. Vijana wale walichanga bia, wakampa kiasi kile akaondoka kwa furaha. "Sasa baba atatambua kuwa mimi pia nina uwezo wa kuchuma”, akajiambia huku akielekea kwa baba yake. Hata hivyo hali ilikuwa kama ile ile ya kwanza. Moyo ulimwuma kijana kwa ujeuri wa babaye akaondoka huku akilaani.

Hamu ya kupata urithi ilimtia kijana ari ya kutimiza matakwa ya baba yake. Alibeba nguo chache akafunga safari kuenda katika mji wa mbali. Alipata kazi ya utwana akaifanya kwa hamu huku akitunduiza kidogo alicholipwa kila mwezi. Kwa miaka miwili, hakuthubutu kununua mavazi mazuri wala kushiriki anasa. Pesa zilipotosha, aliwaaga waajiri kwa heshima akafunga safari ya kurudi nyumbani. Wakati huu, alikuwa na hakika kwamba mambo yake yangetengenea.

Kijana alipofika nyumbani, hali yake ilikuwa ya kuhuzunisha. Alimwendea baba yake akampa pesa kama awali. Baba naye alikirudia kitendo kilekile. Kwa hamaki kuu, kijana aliutia mkono motoni bila kujali majeraha aliyopata akazitoa pesa zile kabla hazijateketea. Alimweleza babaye kimasomaso kwamba hakujali kukosa urithi lakini asingekubali jasho lake litiwe motoni. Aliondoka akajifungia chumbani mwake.

Siku iliyofuata, Maganga aliwaita wasimamizi wa biashara zake. "Sasa naona mwanangu ametambua kuwa uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi. Ninampa usukani wa biashara zangu zote." Hapo ndipo kijana alipolifumbua fumbo la baba yake. Alimwangukia miguuni akamwomba radhi na kumshukuru kwa kumpa elimu isiyopatikana katika chuo chochote. Kijana aliendeleza biashara vizuri huku akijitenga na marafiki waliomshawishi kushiriki anasa. Hakika alifanikiwa hata kuliko baba yake. Akaiyeyusha hofu ya mzee Maganga

  1. Chagua jibu lililo sahihi.
    1. Wanakijiji walimheshimu Maganga kwa utajiri wake.
    2. Maganga alikuwa mja mwenye mkono wazi. 
    3. Wote waliomwendea Maganga walipata msaada wa chakula
    4. Wachache waliyafahamu maarifa ya Maganga katika biashara.
  2. Maisha ya utotoni ya Maganga yalikuwa
    1. ya starehe
    2. yenye dhiki tupu
    3. ya kutia moyo
    4. ya uhitaji.
  3. Maganga alitofautianaje na ndugu zake?
    1. Alikuwa bora zaidi yao masomoni.
    2. Maganga alipenda kusaidiwa kuliko nduguze.
    3. Kinyume na ndugu zake, hakupendelea kazi za ajira.
    4. Maganga alifanikiwa maishani kuliko ndugu zake.
  4. Kulingana na aya ya tatu, ni kweli kuwa
    1. umri ukizidi hudhoofisha utendakazi wa watu 
    2. ugonjwa unaweza kukwamisha ndoto zetu
    3. kufanya kazi kidindia husababisha maumivu ya viungo
    4. unyonge wa nafsi huunyima mwili nguvu zifaazo. 
  5. Hofu ya Maganga hasa ilitokana na
    1. mauti yaliyokuwa yakibisha hodi
    2. uwezekano wa kukosa mrithi afaaye 
    3. tamaa ya mwanawe ya kurihi mali yake 
    4. njama alizofanya mkewe na mwanawe.
  6. Ni kweli kusema kwamba
    1. kijana alimsikitikia baba yake kwa hali iliyomkabili
    2. Maganga hakutaka kumrithisha mwanawe mali
    3. janga la baba lilionekana kama neema na mwanawe
    4. mama hakutaka mwanawe arithishwe mali. 
  7. Haikuwa vigumu kwa mzee kutambua kwamba kijana hakusumbukia pesa mara ya kwanza na ya pili kwa kuwa
    1. zilipatikana kwa urahisi sana
    2. zilipatikana kwa haraka sana
    3. kijana alikasirika zilipoteketezwa
    4. kijana hakuathirika sana zilipoteketezwa.
  8. Mwanawe Maganga aliishi maisha gani katika mji wa mbali?
    1. Ya kujinyima
    2. Ya anasa
    3. Ya kitajiri
    4. Hatujaambiwa.
  9. Maana ya methali "Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi" kulingana na kifungu ni kuwa 
    1. ni mzazi pekee anayezijua dhiki za mwanawe
    2. anayejua thamani ya kitu ni yule aliyesumbuka kukitafuta
    3. mtoto akimkosea mzazi heshima atafikwa na maafa
    4. maovu ya mtoto humwathiri zaidi mzazi wake.
  10. Kijana alifanikiwa kuliko baba yake kwa kuwa
    1. aliwajibika zaidi
    2. alikuwa na maarifa zaidi 
    3. alipata mtaji mkubwa zaidi 
    4. alisaidiwa na watu wengi zaidi.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha isiyopungua kurasa moja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa.
Ufuatao ni mwanzo wa insha. Iendeleze kwa maneno yako mwenyewe huku ukiifanya iwe ya kusisimua zaidi.

Ni kweli kuwa ibilisi wa mtu ni mtu. Ukweli wa methali hii ulibainika siku moja ambapo........................................................

MARKING SCHEME

  1. C
  2. A
  3. D
  4. B
  5. C
  6. A
  7. A
  8. D
  9. B
  10. A
  11. C
  12. B
  13. D
  14. D
  15. A
  16. B
  17. D
  18. C
  19. B
  20. C
  21. D
  22. A
  23. B
  24. C
  25. A
  26. D
  27. B
  28. C
  29. D
  30. A
  31. B
  32. A
  33. C
  34. D
  35. D
  36. B
  37. A
  38. D
  39. C
  40. C
  41. B
  42. D
  43. C
  44. A
  45. B
  46. C
  47. D
  48. A
  49. B
  50. A

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi, chagua jibu sahihi kati ya yale manne uliyopewa.

    Yena__1___kofia aina ya__2___kichwani: Jasho lilikuwa likimtiririka tiriri kwa kuwa kulikuwa na joto__4___mno. Alimwangalia__5___ yake na kushindwa la kufanya. Ajali hiyo ilimwacha mwenzake bila___6__ mmoja. Alipoona watu walimtania na kumbandika jina "kikono." Kutoka siku aliyoipata ajali, rafiki_____ Yona hakuendesha pikipiki tena. Alipowaona vijana wakiendesha pikipiki kwa__8___ aliwaonea__9___ na alipopata nafasi, aliwashauri kuwa haraka haraka haina baraka.

   A B C
 1  alivaa   alifua   alivua   alifaa 
 2  kikuba   kikoi   joho   chepeo 
 3  pake   mwake   yake   kwake 
 4  nyingi   jingi   mingi   kingi 
 5  sahibu   mwendani   hasimu   msena
 6  mwili   mguu   sikio   mkono 
 7     ya       wa    la    cha
 8  mbio   haraka   polepole   kasi
 9  mayo   wivu   huruma   kinyama

 

   Kiongozi___10___alizifuja pesa____11__ za umma na kujenga___12____kubwa ambacho kiliuzwa vinywaji vya aina mbalimbali.__13___ walikasirika na kugoma. Aliliwa___14__ na kupelekwa___15___ ambako alikaa kwa saa kumi. Siku iliyofuata alipelekwa mahakamani.

   A  C  D
 10  shupavu  mihiri   katili   mwadilifu
 11  lote  wote   yote   zote 
 12  baa  mkahawa   klabu   hoteli 
 13  Waliomwajiri  Waliomchagua   Waliochaguliwa   Aliowapenda 
 14  mbaroni  pengu   shime   ufunguo 
 15  kortini  jalani  rumande  korokoroni

 

Kutoka nambari 16 hadi 30, chagua jibu lililo sahihi kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Chagua wingi wa;
    Uwanja wangu una nyasi ndefu.
    1. Nyanja zangu zina nyasi ndefu.
    2. Nyanja zetu zina nyasi ndefu.
    3. Uwanja wetu una nyasi ndefu.
    4. Uwanja wetu una unyasi mrefu.
  2. Chagua jina ambalo ni tofauti na mengine.
    1. Nasaba
    2. Jamaa
    3. Mbari
    4. Nikahi
  3. Uadilifu, wema, ubora ni aina gani ya nomino?
    1. Nomino za wingi
    2. Nomino za dhahania
    3. Nomino za makundi
    4. Nomino za kuhesabika
  4. Chagua kielezi ambacho hakijaambatanishwa vyema na aina yake.
    1. Mwakani - wakati
    2. Haraka - namna
    3. Kidogo - jinsi
    4. Mara mbili - idadi
  5. Je, jina mede huwa katika ngeli gani?
    1. I-ZI
    2. U-YA
    3. A-WA.
    4. I-I
  6. Mimi ni kifaa cha mkulima. Kazi yangu ni kutandaza mchanga au mbolea. Wakati mwingine mimi hukusanya takataka. Mimi ni nani?
    1. Beleshi
    2. Reki
    3. Jembe
    4. Mundu
  7. Kamilisha takanali hii ya sauti. Yeye alifunga mzigo wake
    1. mwaa
    2. nga
    3. ji
    4. ndi
  8. Tambua umbo hiii.
    C8KISWAHILIMT2S52023Q37

    1. Mistari sulub
    2. Mistari sambamba
    3. Mistari mshazari
    4. Mitari butu
  9. Ni sentensi gani inayoonyesha majuto?
    1. Ningalifanya bidii ningalifaulu maishani
    2. Ningekuwa na hela ningenunua kalamu
    3. Nisingefuata ushauri wake nisingefaulu
    4. Nikifuata mawaidha nitafua dafu maishani
  10. Ugonjwa unaofanya mgonjwa kukoja damu huitwaje?
    1. Kaswende
    2. Upele
    3. Safura
    4. Kichocho
  11. Tegua kitendawili hiki:
    Chaenda mbali lakini hakiondoki.
    1. macho
    2. jua
    3. njia
    4. mto
  12. Ni mdudu yupi ambaye hafyonzi damu?
    1. Bunzi
    2. Kiroboto
    3. Chawa
    4. Mbu
  13. Ni sentensi gani inaonyesha ngeli ya KU-KU?
    1. Chumbani inle mlikuwa na kukurukakara
    2. Kule jehanamu kutakuwa na mateso tele
    3. Shuleni petu kuna madaraka mengi sana
    4. Kucheza kwake kuliwafurahisha mashabiki
  14. Ng'ombe hurarama lakini chui
    1. huluza
    2. huvuma
    3. hunguruma
    4. hukorokocha
  15. Neno dunia lina sauti ngapi?
    1. Tano
    2. Tatu
    3. Mbili
    4. Nne

Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali 31 hadi 40.

Vitabu vyote vitakatifu vinatufunza tuwe waaminifu na tusithubutu kamwe kuzungumza uongo kwani mambo ya uongo hayadumu. Nadhani ni kwa sababu hii wahenga wakaeleza kuwa njia ya mwongo ni fupi. Mzee siambiwi alitanabahi kuwa uongo haufai baada ya kuona mambo yamemzonga kama chafu anavyomzonga mbuzi.

Kijiji cha Maganya kiliangukiwa na nyota ya jaha kubwa baada ya wafadhili kujenga chuo cha mafunzo ya watoto yatima na shule. Kila mtu aliyekuwa na watoto yatima alitakiwa kwenda kuwasajili chuoni. Hapo wangesomeshwa mafunzo ya kawaida pamoja na kufunzwa taaluma za ufundi wa kila fani. Kulikuwa na kazi za uashi. Uhadisi, taaluma ya tarakilishi mingoni mwa kazi nyingine. Nafasi zilikuwa wazi kwa mtoto yeyote nchini muradi awe yatima na kufiwa na mzazi mmoja au wote wawili. Vilevile kulikuwa na sehemu ya walemavu wa aina zote katika chuo hicho. Hawa nao walikuwa na rabiba yao ya masomo kulingana na uwezo waliokuwa nao.

Mzee Siambiwi, aliyekuwa mtu bahili na mwenye kupenda kuyakwepa majukumu yake ya malezi alipiga bango vile angefaidika kwa fursa hiyo. Siku moja asubuhi Siambiwi alimwita mkewe na kumketisha kitako. "Sharti nimpeleke kitindamimba wetu nasari ya yatima." Siambiwi alimwambia mkewe huku macho ameyatoa ungedhani ni ya bundi.

Mkewe alikiona hicho kama kioja kikubwa kwani wote walikuwa hawajakata kamba, isitoshe mumewe alijiweza kifedha. Ubishi mkubwa ulizuka. Mzee Siambiwi alisisitiza kuwa kutompeleka mwanawe . asome hapo bure ni sawa na mtu mpumbavu ambaye huacha jua lichomoze ashindwe kuliota kisha alitafute waka wa jioni.

Majadiliano yakakomea hapo kama sentensi iliyowekwa kikomo. Majonzi hayo yalimchoma sana mama inoyoni hadi akapata maradhi ya shinikizo la damu yaliyompeleka jongomeo, bila nauli wala matwana. Asubuhi ya majogoo Mzee Siambiwi na mkembe wake mikononi alikuwa kwenye lango la nasuri ya yatima. Alipokelewa kwa heshima kubwa na bawabu na kuelekezwa alikostahili kwenda huko alimwandikisha mtoto kwa mwalimu mkuu kuwa yeye alimwokota njiani na hivyo ni msamaria mwema. Mtoto alipokelewa na kupewa yaya wa watoto wadogo.
Miaka ilipeperuka ungedhani imepachikwa mbawa. Kitimtim alikua na kuwa mkubwa. Inasomekana alikuwa na bongo la sumaku. Aliongoza kwenye mitihani yake yote hadi akaingia chuo kikuu. Huko alifuzu na kupata kazi ya uhandisi. Alikuwa mhandisi mkuu nchini. Siambiwi wakati huo pesa zilikuwa zimemwishia na kubaki maskini hohehahe.

Siku moja alifunga safari kwenda jijini kumtafuta mwanawe ili akamwombe usaidizi na pia amweleze kuwa yeye ni mzazi wake. Kitimtim alishangaa kukiona kizee kilichodai kuwa mzazi wake kikimlilia machozi kupukupu. Alifahamu tangu utotoni mwake kuwa yatima. Siambiwi alidinda kutoka ofisini na ikabidi polisi waitwe kumtoa nje. Alimshika koti mwanawe na kukatalia kumwachia. Palizuka kizaazaa patashika. Uchunguzi wa kitaalamu wa hospitali na ushahidi ulitolewa. Mzee Siambiwi akawa na bahati kama mtende.

  1. Kulingana na aya ya kwanza ni bayana kuwa
    1. njia ya mwongo huwa ndefu
    2. uongo humletea mtu mambo
    3. mbuzi huzongwa kwa uongo wake
    4. kuna vitabu ambavyo huenzi uongo
  2. Bahati iliyowapata wanakijiji ni gani?
    1. Waliangukiwa na nyota za angani
    2. Walifundishiwa watoto bure bilashi
    3. Walijengewa vyuo vya ufundi
    4. Walipata watu wakusaidia viokote
  3. Waliofaa kujiandikisha chuoni
    1. walikuwa wamepewa barua za mwaliko
    2. walikuwa na watoto wengi
    3. walihitaji msaada wa wafadhili
    4. walitaka kupewa elimu nzuri
  4. Neno jingine lenye maana sawa na uhandisi ni
    1. uinjinia
    2. uhesi
    3. uhasibu
    4. usanii
  5. Chuo hiki cha ufadhili hakikubagua kwa kuwa
    1. kiliwaalika watoto wote wa kijiji
    2. kiliwapa wazazi wote nafasi sawa
    3. kiliwasaidia mayatima na walemavu
    4. kiliwapa mafunzo ya aina mbalimbali
  6. Unafikiri ni kwa nini ratiba nyingine huwa na tofauti?
    1. Vyuo hufunza kozi tofauti
    2. Uwezo wa wanafunzi hutofautiana
    3. Huwa mayatima na wengine wamelemaa
    4. Ulezi wa watoto wote si sawa
  7. Mkewe Siambiwi alienda jongomeo kwa kuwa
    1. mumewe alitaka aoge
    2. mwanawe alienda shule ya yatima
    3. aliugua ugonjwa uliomweza
    4. alilipa nauli ya kwenda jongomeo
  8. Siambiwi ni jina linalolingana na tabia ya mzee huyu. Mbinu hii huitwaje?
    1. Majuzi
    2. Lakabu
    3. Kupanga
    4. Somo
  9. Kitimtim alikuwa mtoto mwerevu kwa kuwa
    1. alimkana babaye ambaye alimtekeleza
    2. alipewa kazi pamoja na ofisi kubwa
    3. alielewa mambo haraka na akawa fundi
    4. alimsaidia babaye na wanakijiji pia
  10. Kulingana na kifungu hiki ni kweli kusema kuwa
    1. Kitimtim alihitaji kusaidiwa ili asome
    2. mamaye Kitimtim alikuwa na pesa nyingi
    3. chuo hicho kilijua Kitimtim ana wazazi
    4. Babaye Kitimtim alikuwa mtu mchoyo sana

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 41 hadi 50

Je, umewahi kutafakari kuhusu namna wanafunzi wengi, ukiwemo miongoni mwao, wanavyosafiri kwenda shuleni? Yumkini jibu lako kwa swali hili litadhihirisha kwamba asilimia kubwa hutembea kwenda shuleni, wengine hutumia baiskeli, magari ya umma na ya kibinafsi, pikipiki na gari mosi. Bila shaka aina ya usafiri hutofautiana kulingana na uwezo wa kiuchumi na umbali baina ya mwanafunzi na shule yake.

Kila aina ya usafiri ina changamoto maalum. Mathalani ikiwa umezungumza na wenzako ambao hutembea kwenda shuleni, haikosi wamekueleza dhiki wanazokumbana nazo. Licha ya safari za aina hii kuwachosha wanafunzi, ni wazi kuwa wanafunzi wengine hata hukosa masomo kwa sababu ya kutopitika kwa njia wakati wa mvua nyingi.

Pengine hata wewe umewahi kujipata katika njia panda baada ya daraja unalovukia kusombwa na maji ya mto uliofurika. Isitoshe, watembeao huweza kuathirika kiafya wakati wa kipupwe. Baridi huweza kuwasababishia pumu au hata kichomi. Wengine huwa katika hatari ya kuteleza kwenye njia zenye matope na kuvunjika viungo vya mwili. Hawa pia wamo katika hatari zaidi ya kutekwa nyara na hata kunyanyaswa kimapenzi.

Wanafunzi wengine huwahusudu wale ambao husafiri shuleni, ama kweli gari la sule, au la kibinafsi. Wakiulizwa kuhusu kiini cha husuda hii, wanasema kwamba wenzao hawa hawachoki kwani magari haya yanawachukua kutoka mlangoni mwa nyumba zao. Hata hivyo ukichunguza vyema utapata kwamba hata hawa wana matatizo sugu. Kwa vile magari ya shule huwabeba wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali, magari haya hayana budi kuanza safari mapema. Hii huwalazimu wanafunzi nao kuamka alfajiri na mapema ili kuyawahi magari haya. Matokeo ni kwamba wanafunzi wengi hawadiriki kulala usingizi wa kutosha. Kuna wale ambao hulala saa nne usiku baada ya kukamilisha kazi za darasani, kisha wanaraushwa saa kumi ili kijitayarisha basi la sa kumi na moja. Wanafunzi wa aina hii hukumbwa na uchovu, na bila shaka husinzia darasani.
Isitoshe, wanafunzi wanaotumia usafiri wa umma hulalamikia msongamano wa magari ambao unawafanya kukawia njiani, na hata kupewa adhabu kwa kuchelewa kufika shuleni. Wengine hata hukataliwa na magari ya abiria, eti wanalipa fedha kidogo na kuwasababishia wenye magari hasara. Wanafunzi hawa huaibika na kulazimika kutembea hadi shuleni. Hali kadhalika magari ya umma humpa mwanafunzii mazingira ya kujifunzia tabia mzuri na mbaya. Pamoja na wanafunzi hawa hupata fursa ya kutengamana na wenzao kutoka shule nyingine, wao pia huweza kuathiriwa vibaya na hulka za wasafiri wengine. Kuna wale ambao huiga lugha, mitindo ya mavazi, namna ya kutembea na hata mienendo mingine ya madereva na utingo. Wengine huishia kuwa waraibu sugu wa vileo kutokana na vielezo wanavyopata kwenye magari haya. Muziki, picha na video na mazungumzo kupitia vyombo vya habari vilivyo kwenye magari haya huchangia kuzorotesha tabia ya wanafunzi. Hii ni kwa sababu baadhi ya maswala yanayozungumziwa ni ya aibu na hayapaswi kusikilizwa na watu wa umri mbichi.

Nihahiri kwamba kila aina ya usafiri ina athari zake. Hata hivyo, baniani mbaya kiatu chake dawa. Usafiri unaitajika katika kufanikisha masomo ya wanafunzi na katika uchukuzi wa bidhaa na vifaa mbalimbali ambavyo wanahitaji shuleni. Ni jukumu la kila mwanajamii kuhakikisha kwamba mikakati ifaayo imewekwa ili kukinga dhidi ya madhara yanayoandahana na kila aina ya usafiri. Wanafunzi nao wakae ange kutambua watu ambao huenda wakatosa katika maovu. Wachujo ya kuiga na ya kukataa.

  1. Ni bayana kuwa usafiri wa wanafunzi
    1. hauna changamoto nyingi
    2. huwa sawa kulingana na mwandishi
    3. huwa rahisi kwa wanaotembea
    4. hutegemea uchumi na umbali
  2. Kulingana na mwandishi ni wazi kuwa kila aina ya usafiri
    1. huwa na changamoto ambazo ni nzuri
    2. humtatiza mwanafunzi kwa njia fulani
    3. humtunza mwanafunzi na kumfanya bora
    4. huweza kumnoa mwanafunzi kimaadili
  3. Wanafunzi hasa wanaotembea huathirika vipi kulingana na kifungu hiki?
    1. Kutekwa nyara na kusikiliza nyimbo mbaya
    2. Kunyanyaswa kimapenzi na wanafunzi wenzao
    3. Kupatwa na magonjwa yanayolewa na baridi
    4. Kutazama runinga na kuvunjika viungo
  4. Ni nini maana ya huwahusudu kulingana na kifungu hiki?
    1. Huponda kwa sababu fulani
    2. Huhimizwa kwa sababu fulani
    3. Huchukia kwa hali fulani
    4. Huvuliwa na starehe fulani
  5. Kulingana na aya ya pili, mwanafunzi huchanganyikiwa iwapo
    1. njia ni mbili na hajui ya kupitia
    2. wachoka na kusombwa na maji
    3. njia anayotumia haipitiki hata kidogo
    4. kuna baridi kali na watekanyara
  6. Ni kauli gani sahihi kulinana na kifungu hiki?
    1. Wanafunzi huraushwa mapema ili wasichelewe .
    2. Wanafunzi wote wanazo changamoto zinzaofanana
    3. Wanafunzi wengi huchoka na hufeli mtihani
    4. Wanaosafiri kwa magari wana starehe sana
  7. Tabia za mwanafunzi zinaweza kuathiriwa na nini?
    1. Madereva wa magari ambao huwa wema
    2. Aina ya usafiri na wanaosoma nao
    3. Wasafiri na mitandao anayoitumia mwanafunzi
    4. Mazingira na watu anaotangamana nao
  8. Kuchelewa kwa mwanafunzi anayesafiri kwa magari ya umma husababishwa na nini?
    1. Madereva na utingo husukisha watu kila stani
    2. Kukaa sana njiani kwa sababu ya msongamano
    3. Kupewa adhabu ya kuchelewa na walimu shuleni
    4. Kukataa kuwabeba wanafunzi na kuwabeba abiria wengine
  9. Hata hivyo, baniani mbaya kiatu chake dawa. Kauli hii inamaanisha
    1. mtu ambaye huwa mbaya huwa mwema siku moja
    2. Usafiri ni mbaya lakini hutufanya watu wema
    3. Tunafaa kuenzi usafiri wa miguu tusipatwe na maafa
    4. Hata kitu kikiwa na madhara, kina umuhimu wake
  10. Kulingana na aya ya mwisho, mwandishi ana mtazamo upi?
    1. Jamii yote yafaa kuona madhara ya usafiri
    2. Tunafaa kuweka mikakati itakayotufaidi safarini
    3. Kusoma kutaimarika tukiimarisha usafiri wetu
    4. Wanafunzi wanafaa kujichagulia namna ya usafiri

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha yakusisimua isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa.

Wewe ni kiranja mkuu shuleni. Andika hotuba utakayotoa katika siku ya michezo shuleni........................

MARKING SCHEME

  1. C
  2. B
  3. A
  4. B
  5. A
  6. D
  7. A
  8. D
  9. C
  10. C
  11. D
  12. C
  13. A
  14. A
  15. C
  16. B
  17. D
  18. B
  19. C
  20. C
  21. B
  22. D
  23. B
  24. A
  25. D
  26. A
  27. A
  28. D
  29. A
  30. B
  31. B
  32. C
  33. A
  34. A
  35. C
  36. B
  37. C
  38. B
  39. C
  40. B
  41. D
  42. B
  43. C
  44. C
  45. C
  46. A
  47. D
  48. B
  49. D
  50. C

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila pengo umepewa majibu manne, Chagua jibu lifaalo zaidi.

__1__ wa mali haujawahi kuwa katika kiwango __2__ hapa nchini Kenya. __3__ mitatu hivi iliyopita, yaani takriban miaka thelathini hivi iliyopita wezi walikuwa wakivunja mabenki na kwa wakati __4__, __5__ ambao ulikuwa ni kuwaibia watu kwa lazima na kuwaumiza kwa silaha. Wazembe hawa __6__ viongozi wa dini ndio waliochukua nafasi za majambazi hawa sugu.
"Viongozi hawa wanaowaghilibu __7__ wauze mali yao na kuwapelekea hela zote kwa kuwa dunia imefika ukingoni ndio wanaopigiwa mfano wa methali, __8__ kwa kuwa hawana stadi inayohitajika.

   A   B   C   D 
1.   Uchoyo   Uchu   Tamaa   Shauku 
2.  kilichofika   uliofikia   kitakachotimia   kisichotimia 
3.  Misimu  Miaka   Miongo   Darzeni 
4.  ingine  wengine   kwengine   mwingine 
5.  wezi wa mabavu   wizi wa kimabavu   ulaghai wa hiari   uchopozi wa siri  
6.  wanaojiita  waliohitimu kuwa   kusomea   kufanywa kama 
7.  waamini  wafugaji   waumini   wanachama 
8.  ndugu ni kufaana si kufanana   akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki  mwana wa ndugu kirugu, mjukuu mtu wa mbali kichwa cha kuku hakistahili kilemba

 

Mwalimu Kijuba __9__mwalimu wangu wa kwanza wa lugha ya Kiswahili.Alinitoa matongo machoni na __10__ masikioni kuhusu lugha hii akhiyari. Mwanzo alinifahamisha kuwa ina sauti 11___. Aidha, alinifunza kuwa sauti hizi zimegawanywa katika sehemu mbili; yaani __12__ na sighuna. __13__ ,nilijuzwa kuwa kuna __14__ kadhaa za lugha kama vile __15__ methali, istiara, tashbihi, misemo, tanakali za sauti na nyingine nyingi.

   A   B   C   D 
 9.   ndiye aliyekuwa   ndio aliyekuwa   ndiye ambao alikuwa   siye aliyekuwa 
 10.   masuo  ukongo   uchafu   nta 
 11.  salasini  thalathini  thelathini   ishirini na tano 
 12.  ghuna  alfabeti  vokali   konsonati 
 13.  Mintarafu  Isitoshe   Maadamu   Seuze 
 14.   tamadhali  mapambo   maneno   tamthali 
 15.  ;  :   ,   . 

 

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi

  1. Andika wingi wa sentensi ifuatayo
    Uta ule aliokujengea umekatika
    1. Ukuta ile alizokujengea imekatika
    2. Nyuta zile mlizowajengea zimekatika
    3. Kuta zile mlizowajengea zimekatika
    4. Nyuta zile waliowajengea zimekatika
  2. Neno 'mhadhara' lina silabi ngapi?
    1. Nne
    2. Sita
    3. Nane
    4. Tatu
  3. Ni sentensi gani iliyotumia kwa' kuonyesha sababu?
    1. Wafanyakazi walinufaika kwa bidii zao
    2. Kutafuta kwa mapana na marefu kutakupeleka mbali
    3. Kuimba kwa furaha kulituchangamsha
    4. Wageni walikula wali kwa mchuzi wa kuku
  4. Bainisha aina za maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo.
    Wanafunzi wako ni bora kuliko wetu,
    1. Kivumishi, kitenzi, kiwakilishi
    2. Kiwakilishi, kivumishi, kielezi
    3. Kivumishi, kiunganishi, kiwakilishi
    4. Kiwakilishi, kitenzi, kivumishi
  5. Akisami 4/7 kwa maneno ni
    1. tusui nne
    2. tusui saba
    3. thuluthi saba
    4. subui nne
  6. Maneno yafuatayo yanafuatana vipi katika kamusi?
    1. nungu
    2. nungunungu
    3. nung'unika
    4. nung'uniko
      1. (ii), (iii), (iv), (i)
      2. (iii), (ii), (i), (iv)
      3. (i), (ii), (iii), (iv)
      4. (iv), (iii), (ii), (i)
  7. Tambua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo
    1. Wanafunzi wote- wale waliohusika - walitumwa nyumbani.
    2. Kanisa hilo lilifungwa! tutajiunga na jingine.
    3. Mtoto (aliyeugua) alipelekwa (hospitalini).
    4. Ewaa! ameumwa na joka kubwa.
  8. Chagua sentensi ambayo haikuendelezwa sahihi kimantiki
    1. Amejipaka mafuta usoni mwake
    2. Wanafunzi wengi waliwahi shambani
    3. Mabata wanapenda kuchezea vidimbwini
    4. Ajali nyingi zinaweza kukingika
  9. Kamilisha methali ifuatayo
    Mla nawe hafi nawe _________________________
    1. usizaliwa naye
    2. ila mzaliwa nawe
    3. kuliko mzaliwa nawe
    4. kama mzaliwa naye
  10. Ndege ni kwa kiota kama vile konokono ni kwa
    1. kizimba
    2. zizi
    3. shimo
    4. kombe
  11. Ni nini maana ya 'kula njama'?
    1. Kufanya mkutano wa siri wenye nia mbaya
    2. Kula nyama nyingi na kushiba sana
    3. Kushiriki katika mkutano wa hadhara
    4. Kuzeeka au kuishi miaka mingi
  12. Tunapata jina gani kutokana na kitenzi 'andika'?
    1. Andikwa
    2. Andikisha
    3. Mwandishi
    4. Andikiana
  13. Tambua mchezo ufuatao
    'Wachezaji huruhusiwa kuukamata mpira kwa mikono na kukimbia nao, na mpira wenyewe ni wa umbo la duaradufu'
    1. Raga
    2. Gozi
    3. Soka
    4. Gori
  14. Ni sentensi ipi inayoonyesha matumizi sahihi ya kiambishi -po- cha wakati?
    1. Alipotoka sipajui
    2. Tunapoishi ni pema
    3. Nilipomwona nilifurahi
    4. Wapo wanaosoma vizuri
  15. Chagua maelezo sahihi
    1. Kishaufu huvaliwa shingoni
    2. Hazama huvaliwa puani
    3. Kikero huvaliwa sikioni
    4. Shemere huvaliwa mguuni

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40

Ujio wa teknolojia umeiwezesha dunia kufanya mambo kwa haraka na wepesi mno. Dunia imedogoshwa na kuwa kama kijiji kidogo kwa kuwa; mazungumzo, midahalo, mawasiliano, sayansi na teknolojia, mikutano na mihadhara vinaweza kufanywa bila kuzingatia kitalifa chochote. Hata hivyo, uvumbuzi huu wa kisayansi unaonekana kuwapunja watoto na vijana wadogo ambao hawaelewi mitambo ya teknolojia ililetwa kwa mintarafu gani. Utawaona watoto wadogo hawana muda wa kucheza ila utawapata wamegandana na rununu au tarakilishi wakicheza michezo ya wazungu isiyoisaidia miili yao katika ukuaji.

Ukuaji wa mwili hususan wa mtoto anayekua unahitaji michezo ya aina ainati. Kwa ukweli, michezo ina faida anuwai. Hii ndiyo sababu watoto wengi huhimizwa washiriki katika michezo . Hali ya wanafunzi kujikalia ubwana madarasani huwa na athari zisizokadirika. Usisahau athari zinaweza kuwa hasi au chanya iwapo ni hasi gharama ya kuzidhibiti huwa ya juu sana ukizingatia ukweli kuwa, tuko na mfumko mkubwa wa bei. Shida nyingi ambazo zinamkumba mtu uzeeni husababishwa na kutozingatia hali ya afya njema mtu anapokua. Hii ndiyo maana utawaona watu wakizeeka na kufa mapema kuliko inavyotarajiwa. Watu wa zamani waliishi miaka mingi kwelikweli.

Vijana wa zamani walienzi na kuithamini michezo kama johari. Wavyele wengi walikuwa na kibarua kigumu kuwarudisha wanao nyumbani. Vijana wa zamani walicheza michezo mingi kama vile gungwi, kibe kibatufe, njugwe, kuzungusha tairi kwenye kiuno na hata kuruka kwa kamba. Enzi hizo hungewapata vijana wengi wamejinenepea kama nguruwe.

Ningetaka uwatazame vijana wa kisasa. Utaona idadi kubwa haiendi uwanjani kucheza ila kustarehe tu na kuzizungumzia timu za Uingereza. Utawaona wakijiita wanaManchester, wanaAsenali, wanaChelsie ilhali hawanufaiki na chochote kutokana na timu hizo. Kwao hawatambui kuwa michezo ina manufaa ya kuhusudiwa. Kwanza inajenga misuli na kuimarisha viungo vya mwili. Ni wazi kuwa unaposhiriki michezo unajihisi mwepesi zaidi na unaweza kutekeleza mengi bila kuhisi kuchoka haraka. Pia kwa wale wanaoshiriki michezo katika ngazi za kimataifa hunufaika na mengi. Wao huambulia fedha nyingi zinazowatajirisha haraka. Wengine huajiriwa kama makocha na marefa wa timu za kimaeneo, kitaifa au kimataifa.

Kulaza damu ni wazo la hasara isiyomithilika. Ni dhahiri shahiri kuwa, akili vivu ni karakana ya maovu. Wale wanaojikalia bure bila kufanya kazi yoyote hujipata wakiwazia mabaya. Usisahau, baadhi yao watazama katika matumizi ya dawa za kulevya au wanaswe na mtego wa kimapenzi kabla ya ndoa. Hata hivyo, yule anayeshiriki katika michezo huwa hana nafasi ya kuyawazia mawi. Kila anapotoka uwanjani huwa amechoka tiki na kukosa zihi za kufanya mawi.

Watoto wanaoshiriki michezo mara nyingi huwa na wepesi wa kushika hata wayasomayo. Hii ni kulingana na utafiti wa kisayansi uliofanywa nchini Marekani. Michezo hukuza kumbukumbu za aliyosoma darasani. Usisahau kuwa uwanjani lazima mchezaji awe mmakinifu na anayechemsha bongo na kukuza ubunifu. Mwanafunzi kama huyo huelewa mambo haraka na kwa wepesi. Isitoshe, michezo huchangia kukuza kumbukumbu za aliyesoma darasani. Usisahau kuwa uwanjani lazima mchezaji awe mmakinifu na anayechemsha bongo na kukuza ubunifu. Mwanafunzi kama huyo huelewa mambo haraka na kwa wepesi. Isitoshe, michezo huchangia kukuza nidhamu na umoja. Michezoni pia kuna sheria kali ambazo zinamsaidia mchezaji kujiheshimu na kuwaheshimu wenzake.

  1. Aya ya kwanza haijaeleza kuwa
    1. teknolojia imekuza michezo chanya ya watoto
    2. teknolojia inawezesha watu kuwasiliana vyema hata wakiwa mbali
    3. wanafunzi wanaweza kupokea mafunzo hata wakiwa mbali
    4. teknolojia imeifanya ulimwengu kuwa kama kata ndogo tu
  2. Ni nani aliyepata hasara kubwa kutokana na teknolojia mpya?
    1. Wanasayansi na wavumbuzi wenyewe
    2. Watu wote wanaotumia vyombo vya teknolojia
    3. Watu wa umri mdogo wasiojua matumizi kamili ya teknolojia
    4. Watu wote wanaohusika na michezo mbalimbali
  3. Michezo aina ainati yaani
    1. michezo inayokuza miili 
    2. michezo ambayo hainufaishi
    3. michezo ambayo haipatikani
    4. michezo ya aina nyingi
  4. Wazee wa kale
    1. hawakuishi miaka mingi ikilinganishwa na sasa
    2. waliishi miaka mingi wakilinganishwa na wale wa kisasa
    3. walitumia mitambo ya teknolojia vyema kuliko wa kisasa
    4. hawakucheza michezo mingi kama ile inayochezwa na vijana wa kisasa
  5. Mtu anaweza kupata athari gani akikaa tu bila kufanya kitu kulingana na aya ya pili?
    1. Kuathiri hali ya kiuchumi ya mtu binafsi
    2. Kuathiri hali ya mapato ya mtu binafsi
    3. Kuhatarisha maisha ya wahasiriwa wote
    4. Kunaathiri hali ya ukuaji wa mwili wake.
  6. Kulingana na kifungu, tunaweza kusema kuwa vijana wa kisasa na wale wa kale ni kama usiku na mchana kwani
    1. vijana wa leo hawathamini michezo
    2. vijana wa leo wanathamini michezo sana
    3. hakuna tofauti hata kidogo kwa kuwa mitazamo yao ni sawa
    4. vijana wa zamani hawakuthamini michezo hata kidogo
  7. Vijana wanaostarehe tu na kushabikia timu za kizungu wanakosa manufaa yafuatayo isipokuwa
    1. kusaidia timu anayeisifia kushinda 
    2. kujenga misuli na kuimarisha viungo vya mwili
    3. kuhisi mwepesi zaidi na bila kuchoka kwa haraka
    4. kupata hela haraka na kutajirika kwa haraka
  8. Michezo katika vijana inafanya nini kulingana na aya ya tano?
    1. Inawafanya kutelekeza afya za miili yao 
    2. Huwasaidia kushabikia timu kubwa za kizungu
    3. Huwasaidia kuepukana na mawi yatakayowahatarisha
    4. Huwafanya kuingilia mihadarati na mapenzi ya haramu
  9. Kulingana na utafiti wa kisayansi uliofanywa Marekani
    1. wachezaji wote huwa werevu
    2. michezo huchangia katika kunoa akili
    3. bora kijana ashiriki michezo atakuwa mwerevu
    4. michezo ndiyo njia ya pekee ya uerevu darasani
  10. Anwani mwafaka katika kifungu hiki inaweza kuwa
    1. Faida za teknolojia ya kisasa 
    2. Madhara ya teknolojia ya kisasa 
    3. Madhara ya michezo mingi
    4. Faida za michezo kwenye afya

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41- 50

Katika msitu mkuu ulio upande wa mashariki mwa Afrika palikuwa na wanyama ambao waliongozwa naye bwana Kifaru. Mfalme huyu aliongoza msitu huo kwa kipindi cha miongo isiyopungua miwili. Kifaru alipounyakuwa uongozi huu kutoka kwa utawala wa Simba I, wanyama wote walishangilia kwa hoihoi, vigelegele na nderemo. Hii ni kwa sababu cheo hicho daima kilikuwa cha familia ya simba. Hata hivyo, muda wa mfalme Kifaru ulikuwa umekamilika. Wanyama walikuwa wananoa makali yao ili kwenda debeni tena.

Kabla ya uchaguzi ambao ulipania kufanywa mwakani, wanyama wazalendo walianza kutathmini kazi ya kiongozi Kifaru. Baada ya mijadala kwenye vyombo vya habari, ilibainika wazi kuwa kiongozi huyo anayeng'atuka alikuwa ameleta maendeleo si haba. Mwanzo, barabara zilikuwa zimenyoka twa! Pili, alikuwa amefungua vyuo vikuu na vyuo anuwai ambavyo vilifadhiliwa kwa asilimia sabini na tano. Waliojiunga na vyuo hivyo walipata ufadhili vile vile wa karo. Wanyama wengi walikuwa wameelimika kuliko misitu mingine majirani. Wengi walisikika wakisema kuwa pasingekuwa na kifungu kwenye katiba kumzuia, wangemruhusu Kifaru kutawala milele. Hata hivyo, uchumi wao ulikuwa umezorota kwa kuwa alikuwa na madeni mengi yaliyozichukua pesa nyingi za walipa ushuru.

Siku ya uchaguzi ilipowadia, wanyama walimchagua mwana wa simba I ambaye alikuwa ameongoza hapo awali. Wengi walimchagua kwa kusingizia kuwa alikuwa na damu ya uongozi kutoka kwa baba yake. Wengine walimpendelea kwa kuwa alikuwa amesoma hadi kiwango cha uzamifu pale katika chuo kikuu cha Uingereza. "Simba II atatuletea maendeleo ya Uingereza," Nyani walisikika wakimmiminia sifa sufufu. Isitoshe, Simba II alikuwa mkakamavu ajabu. Hata hivyo kuna wale waliopinga wakisema kuwa si vyema wanyama kutoka jamii moja kuongoza milele kwa kuwa wengi wapo, Simba II alitawazwa kuwa mfalme wa tatu wa msitu wa Rosana.

Simba II alishika hatamu za uongozi. Alilitawala pori hilo hivi kwamba wanyama wote walimpenda na kumtii. Hata hivyo, kwa kutamani maendeleo ya pupa, aliwatoza wanyama ushuru mkubwa ajabu. Kila mwanzo wa mwezi, wanyama wote walijumuika kwake ili kulipa ushuru. Wengine walitoka mapangoni, chini ya mawe, miti, viota na kwenye milima na mabonde. Walisimama gwarideni na mfalme angeamua kodi ambayo kila mmoja angelipa. Mfalme huyu aliapa na kutangaza kuwa hakuna hata mmoja ambaye angejaribu kukwepa kulipa ushuru.

Wanyama wengi walilalamikia ushuru wa juu lakini wakalipa ila Mamba. Mwezi ulipokamilika, wanyama wote waliwasili nyumbani kwa simba kulipa ushuru. Kama ilivyokuwa kawaida, Mamba hakuwa miongoni mwao. Wakati huu tabia ya Mamba ilikuwa imemfika mfalme kooni. Hakuwa tayari kupokea vijisababu vyake na alisisitiza kuwa lazima Mamba alipe shilingi milioni kumi kwa kuishi majini. Mfalme Simba II aliamua kumtuma Kiboko akamwite Mamba kwenye kasri. Alilalamika kuwa tabia hiyo ya Mamba ilikuwa sasa kia cha mwili.

Mamba alipofikishiwa ujumbe alisema kuwa alikuwa na mfalme wake majini aliyemlipa ushuru. Mfalme aliposikia hayo, alichemka nyongo. Aliondoka shoti hadi majini. Wakati huo, maji yalikuwa safi na yametulia tuli. Simba alinguruma na kutazama ndani. Mle ndani, alimwona Simba mwingine. Papo hapo, aliruka na kutumbukia majini chupwi! Akazama zi! na kutokomea kabisa.

  1. Kulingana na aya ya kwanza;
    1. wanyama walikuwa hawaamini mwanzoni iwapo kuna mnyama mwingine atakayeongoza isipokuwa Simba
    2. aliyeongoza zaidi ya miongo miwili alikuwa ni mfalme Simba
    3. baada ya uongozi wa Kifaru, Simba II alichukua ushukani
    4. kipindi cha mfalme Kifaru hakikuwa kimekamilika
  2. ...wananoa makali ili kwenda debeni..." Kwenda debeni ni nini kulingana na kifungu?
    1. Kuingia kwenye debe
    2. Kumpokea kiongozi mpya
    3. Kwenda kupiga kura
    4. Kuagana na kiongozi wao
  3. Kura zilitarajiwa kupigwa;
    1. mwaka huo
    2. baada ya mwongo mmoja
    3. mwaka uliotangulia
    4. mwaka ambao ungefuata
  4. Kifaru alikuwa amefanya mema yafuatayo ila:
    1. kutengeneza miundombinu kama vile baraste nzuri
    2. kujenga vyuo vikuu na vyuo anuwai ili wanyama wasome
    3. kufadhili ujenzi wa vyuo kwa asilimia mia moja
    4. aliwatawala wanyama vyema hadi wakatamani aendelee
  5. Ni kwa nini haingewezekana Kifaru kuendelea kutawala kwa mintarafu ya wanyama?
    1. Katiba yao haikuruhusu viongozi kutawala milele
    2. Kifaru alitoka familia ambayo haikutarajiwa kuongoza
    3. Uchumi ulikuwa umedorora katika uongozi wa Kifaru
    4. Uongozi wa Kifaru ulikuwa umekopa madeni kupita kiasi
  6. Simba II alikuwa na kiwango gani cha elimu?
    1. Shahada iliyo chini ya shahada ya uzamili
    2. Shahada aipatayo mtu baada ya shahada ya uzamili
    3. Ni shahada mtu apatayo baada ya ile ya astashahada
    4. Ni cheti cha juu zaidi katika kisomo cha duniani
  7. Unafikiri ni kwa nini Simba II alitawazwa kuwa mfalme ilhali wengine walimpinga?
    1. Kiongozi aliyetangulia alikuwa amedororesha uchumi
    2. Kuna wachache walioupenda ukakamavu wake
    3. Simba II alikuwa na kiwango cha juu cha elimu
    4. Simba II alipata ushindi kwa wingi wa kura
  8. "...tabia hiyo ya Mamba ilikuwa sasa kia cha mwili" ina maana kuwa;
    1. yalikuwa mazoea ya Mamba kutolipa ushuru
    2. Mamba alimdharau mfalme
    3. ilikuwa tabia ya Mamba kulalamika
    4. Mamba alikuwa na hasira
  9. Si kweli kusema kuwa
    1. Mamba alilipa ushuru tu baada ya mwaka mmoja
    2. wanyama wote hawakufurahia ushuru waliotozwa
    3. wanyama wote ila Mamba walilipa ushuru
    4. Mamba alitozwa faini ya kutolipa ushuru
  10. Unafikiri alichokiona mfalme majini ni nini?
    1. Mamba aliyedinda kulipa ushuru
    2. Mfalme mgeni wa majini
    3. Mnyama wa majini aliyefanana na Simba
    4. Kivuli cha mfalme Simba II

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukianza kwa kifungu ulichopewa.

Tulianza safari yetu alfajiri na mapema. kwa kuwa siku njema huonekana asubuhi, safari hiyo ilitarajiwa kuwa .....................................

MARKING SCHEME

  1. B
  2. A
  3. C
  4. D
  5. B
  6. A
  7. C
  8. D
  9. A
  10. D
  11. C
  12. A
  13. B
  14. D
  15. B
  16. D
  17. A
  18. A
  19. B
  20. D
  21. C
  22. A
  23. A
  24. B
  25. D
  26. A
  27. C
  28. A
  29. C
  30. B
  31. A
  32. C
  33. D
  34. B
  35. D
  36. A
  37. A
  38. C
  39. B
  40. D
  41. A
  42. C
  43. D
  44. C
  45. A
  46. B
  47. D
  48. A
  49. B
  50. D

 

 

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila pengo umepewa majibu manne. Chagua jawabu lifaalo zaidi.

Mazoezi ya viungo vya mwili.__1___uzingatiaji wa lishe bora___2__ ni njia muhimu ya kuimarisha___3__ zetu. Mtu___4__ viungo vyake mazoezi yafaayo___5___ vibaya kiafya.___6__, watu wengi____7__  kuwa kutofanya kazi zozote, hata zile nyepesi ni___8___cha ustaarabu wao. Si ibra, yaani si___9___ kwa waja kama hawa kudhoofika kiafya.

  A B C D
 1   dhidhi ya  mithli ya   mbali na  kinyume na
 2       ,       :      ___      ;
 3  sifa  miili  ari  siha
 4  asipozifanyia  asipovifanyisha  akifanya  akifanyisha
 5  huathirika   huathirikia  huathiri  huathirishwa
 6  IIhali  Japo  Hata hivyo  Ingawa
 7  hujua   husadiki  huelewa  hung'amua 
 8  kizingiti  kizuizi   kikwazo  kitambulisho 
 9  hoja  nadra  vigumu  ajabu

 

Maimuna___10___kuenda shuleni kama____11___ ada yake. Safari yake ya masomo___12____ na changamoto za kila aina. Hata hivyo, alizidi kujikaza huku akielewa kuwa____13___. Aliiona elimu kama njia ya pekee ya____14___ jamii yake kutokana na umaskini___15___hali zao.

 
10   alishika tariki  alitia nanga  alichana mbuga  aliweka nadhiri
11  iliyokuwa  iliokuwa  ilivyokuwa  ilipokuwa 
12  ilikabidhiwa  ilikabiliwa   alikabiliwa   alizongwa 
13   msasi haogopi miiba  msafiri hana miiko   hamadi kibindoni silaha mkononi   heshima haiji bali huletwa 
14  kuliokoa  kuwaokoa   kumwoka   kuiokoa 
15  uliowazorotesha  uliozizorotesha   uliyoizorotesha  uliyowazorotesha


Kutoka swali 16 - 30, chagua jibu sahihi kulingana na maagizo.

  1. Andika wingi wa sentensi ifuatayo.
    1. Sogora waliwatumbuiza sana kwa kigoma hivyo.
    2. Masogora walikutumbuiza sana kwa vigoma hivyo.
    3. Sogora walikutumbuiza sana kwa vigoma hivyo.
    4. Masogora waliwatumbuiza sana kwa vigoma hivyo.
  2. Chagua jozi iliyo tofauti na nyingine.
    1. Sabalkheri -Akheri.
    2. Alamsiki -Binuru.
    3. Buruani - Buriani dawa.
    4. Usiku mwaka - Majaliwa.
  3. Ni sentensi ipi iliyotumia kiambishi 'ka` kuonyesha kusudi?
    1. Komu alijikwaa akaumia kidole gumba.
    2. Deya aliamka akaandaa kiamshakinywa akala akaondoka.
    3. Salma ameenda nyumbani akawaone wazazi wake.
    4. "Tutaanza safari kesho asubuhi," akasema.
  4. Konokono ni kwa kombe ilivyo kuku kwa
    1. zeriba
    2. kizimba
    3. kifukofuko
    4. kitala.
  5. Bainisha orodha yenye vihusishi pekee.
    1. Kando ya, licha ya, mbali na, katika
    2. Polepole, vibaya, jioni, kwa sauti
    3. Mithili ya, karibu na, dhidi ya, kwenye
    4. Maridadi, gumu, nyepesi, vyenyewe.
  6. Tegua kitendawili kifuatacho.
    Nyumba yangu ina milango mingi.
    1. Kichunguu
    2. Kiota
    3. Uyoga
    4. Kibuyu.
  7. Chagua sentensi yenye maana sawa na hii.
    Hakuenda mjini wala hakununua mboga.
    1. Asingalienda mjini asingalinunua mboga.
    2. Akienda mjini hatanunua mboga.
    3. Angeenda mjini asingenunua mboga.
    4. Angalienda mjini angalinunua mboga.
  8. Kipi ni kivumishi kilichoundwa kutokana na kitenzi?
    1. Andika - Maandishi.
    2. Legevu - Ulegezaji.
    3. Uhodari - Hodari.
    4. Angalia - Mwangalifu.
  9. Bela ni dadaye Patu. Maria ameolewa na Patu. Bela atamwitaje Maria?
    1. Mwamu
    2. Mpwa
    3. Wifi
    4. Mwanyumba.
  10. Andika katika usemi wa taarifa;
    Kaka! Ukinipa nafasi nitakufunza kuuimba wimbo huu.
    1. Kaka alimwomba ampe nafasi ya kufunzwa wimbo huu.
    2. Kaka alimwambia kuwa iwapo angempa nafasi angemfunza wimbo huo
    3. Kaka alimwambia kuwa kama atampa nafasi atamfunza wimbo huu.
    4. Kaka alimwambia kwamba iwapo angempa nafasi angemfunza wimbo huu.
  11. Meza, dawati na kochi, kwa jina moja ni
    1. samani
    2. viti
    3. ala
    4. pembejeo
  12. Kanusha sentensi ifuatayo.
    Mkono uliotibiwa umepona kabisa
    1. Mkono usiotibiwa haukupona kabisa.
    2. Mkono uliotibiwa haukupona kabisa.
    3. Mkono usiotibiwa haujapona kabisa.
    4. Mkono uliotibiwa haujapona kabisa.
  13. "Gae huwa chombo wakatiwe" ni kwa watu wanaowadharau wale waliowahi kuwasaidia. "Mzigo wa chungu ni chembe moja ya mchele" ni kwa watu
    1. wanaopuuza thamani ya vitu vikubwa
    2. wanaotishwa na matatizo ya wenzao
    3. wanaoviona vitu vidogo kuwa na thamani kubwa
    4. wanaovidharau vyao kwa kutamani vya wenzao.
  14. Zipi ni nomino za wingi?
    1. Magari, nyuzi
    2. Ufuta, marashi
    3. Njaa, hamaki
    4. Kombamwiko, askarikanzu.
  15. Sentensi ifuatayo imetumia tamathali gani za usemi?
    Rajab ni kinyago, alituvunja mbavu kwa masimulizi yake
    1. Tashhisi, chuku
    2. Kinaya, tashbihi
    3. Sitiari, kinaya
    4. Sitiari, nahau.

Soma ufahamu ufuatao kwa makini kisha ujibu maswali 31-40.

Nilikuwa chumbani mwangu nikijisomea novela ili kukinaisha uraibu wangu. Mama aliniita ghafla, nikaukunja ukurasa niliokuwa nikisoma kabla ya kutoka. Alikuwa ameshika noti ya shilingi mia tano. "Nenda kwa Bwana Mauzo uninunulie kilo ya sukari, maziwa na paketi ya unga," aliniambia huku akinikabidhi fulusi zile. "Hewala mama," niliitikia huku niking'oa nanga kuelekea kwenye duka hilo lililokuwa takriban kilomita mbili kutoka pale nyumbani.

Njiani nilimkuta rafiki yangu, Aviza akiendesha baiskeli yake. Nilimwamkua naye akaniitikia kwa ucheshi kama ilivyokuwa ada yake. Nilimweleza kuwa mama alikuwa amenituma dukani na kwamba nisingethubutu kuwa kihongwe kwa kuwa sisi watoto tunao wajibu wa kuwaauni wavyele wetu. Huku akikubaliana nami, alijitolea kunisaidia. "Kwa kuwa sina ujuzi zaidi yako katika kucharaza baiskeli, utaendesha wewe nami niketi kwenye karia," alisema kisha akanikabidhi baiskeli ile.

Tuliichupia baiskeli tukaiendesha kwa uangalifu katika barabara ile yenye kuruba nyingi. Siku zote nilizingatia kauli ya wahenga kuwa kinga ni bora kuliko tiba. Muda si muda tulifika
dukani.

Umayamaya wa washitiri ulikazania kununua bidhaa. Wanyonge walikaa kando kusubiri muujiza angaa wanunue. Wenye misuli kama mimi nao waliwasukuma wenzao almradi wapate fursa ya kununua bidhaa walizohitaji. Jambo moja lililowavuta wateja kwa Bwana Mauzo ni kwamba hakudiriki kuwapunja wateja wake licha ya kuwa na duka la kipekee pale kijijini. Wema nao hauozi. Hali ilikuwa hivyo siku zote katika duka lake.
Baada ya kujipenyezapenyeza, nilijipata nimekabiliana ana kwa ana na mwenye duka. Usoni, alionyesha tabasamu yake ya kawaida. Pindi tu tulipotazamana, niliuona uso wake ukibadilika ghafla, akawa kama aliyeona mzimu mbele yake. Hali hiyo ilinitia wahaka kidogo. Nilishuku kuwa labda alifikiri nimeenda kumkopa. Falsfa ya Bwana Mauzo ilikuwa wazi kwa wote "Lipa leo nitakukopesha kesho." Ili kumwondolea hofu yake, nilitabasamu, nikaunyosha mkono huku nikimwonyesha noti aliyonipa mama. Ajabu ni kuwa hakuipokea.

Mara noti ile ilinyakuliwa na mkono mzito kama nanga. Kwa udhia mwingi, niligeuka kumwona hasidi huyo aliyenuia kuchuma riziki kutoka mkononi mwangu pasipo kutoka jasho. Lo! Maneno yalinikauka kinywani, macho yakanitoka pima nisiweze kutamka 'be' wala 'te'. Uso wangu ulikumbana na mtutu wa bunduki. Tuliagizwa kulala sakafuni huku majambazi wale wakijiandaa kutupora. Acha mtafaruku uingie! Hakika angurumapo simba mcheza ni nani?

Wahalifu wawili walijitoma dukani wakaanza kupakia pesa za Bwana Mauzo katika mkoba. Mwanaume mmoja aliyekuwa nyuma yangu alimtazama mmoja wao aliyebaki nje akitutishia kwa bunduki. Sijui alikuwa akiwazia nini. Alitazamana na mwanamume mwenye bunduki akasimama na kupiga hatua akienda kwake.

"Nitakufyatulia risasi kichwani mpumbavu wewe!" Jambazi yule alifoka kwa ukali. “Nina hakika kuwa huna uwezo huo," alijibu mwenzetu huku akitabasamu. Jambazi alibabaika. Kumbe mteja mwenzetu alikuwa askari polisi, kwa hivyo alitambua kuwa bunduki ile ilikuwa bandia. Sote tulipandwa na mori, wengine wetu wakiwashambulia kitutu wahalifu hao. Hofu ilituondokea tuliposikia kuwa bunduki ile ilikuwa bandia.
Kamba zilitolewa pale dukani, wakafungwa kitita na kupelekwa marshimarshi hadi kituoni mwa polisi. Noti yangu ilitolewa mfukoni mwa jambazi aliyeniibia. Nilinunua bidhaa alizonituma mama, Bwana Mauzo akawahudumia wachache kisha akafunga duka ili akaandikishe taarifa kituoni. Japo nilichelewa kurudi nyumbani, nilikuwa na uhondo wa kusimulia aila yangu
kuhusu tukio lile.

  1. Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza.
    1. Mama hakufurahishwa na mazoea ya msimulizi
    2. Msimulizi alikuwa na mazoeza ya kusoma vitabu vya hadithi
    3. Bwana Mauzo alimiliki duka la pekee kijijini.
    4. Aviza alizoea kucheka kila alipomwona msimulizi.
  2. Dukani alikotumwa mwandishi
    1. kulikuwa zaidi ya kilomita mbili kutoka kwao
    2. kulikuwa kilomita mbili kamili kutoka kwao
    3. kulikuwa karibu kilomita mbili kutoka kwao
    4. kulikuwa pua na mdomo kutoka kwao.
  3. Kwa nini Aviza alimpa msimulizi baiskeli yake?
    1. Msimulizi alikuwa hodari zaidi katika kuendesha baiskeli.
    2. Msimulizi alionyesha hamu kubwa zaidi ya kuendesha baiskeli.
    3. Aviza hakujua kuiendesha baiskeli vizuri.
    4. Dukani walikonuia kuenda kulikuwa mbali sana.
  4. Maneno 'Kuwa kihongwe' yametumia tamathali gani ya usemi?
    1. Tashbihi
    2. Chuku
    3. Tashhisi
    4. Sitiari.
  5. Sifa gani zinamwafiki zaidi msimulizi wa kifungu?
    1. Mwenye nguvu, afanyaye mambo kwa uangalifu.
    2. Mwerevu, asiyewadhulumu wanyonge.
    3. Mtiifu, hodari katika mambo mbalimbali.
    4. Mwenye udaku, anayejulikana kijijini.
  6. Wateja walifurika dukani kwa Bwana Mauzo kwa kuwa
    1. hapakuwa na maduka mengine
    2. aliendesha shughuli zake kwa uadilifu
    3. aliuza bidhaa za aina mbalimbali
    4. aghalabu waliendea bidhaa kwa mkopo.
  7. Kulingana na aya ya tano
    1. Bwana Mauzo aliwataka wateja walipie bidhaa papo hapo
    2. mtu alihitajika kununua angaa mara moja ndipo akopeshwe
    3. shaka ya mwenye duka iliondoka alipoonyeshwa pesa
    4. uso wa mwenye duka ulibadilika pindi tu alipomwona msimulizi.
  8. Mwanaume aliyetajwa hakujali alipotolewa vitisho kwa sababu
    1. alikuwa afisa wa usalama
    2. jambazi alikuwa mwoga
    3. alikuwa na uwezo wa kujihami
    4. alitambua kuwa bunduki ile isingemdhuru.
  9. Ni methali gani inayofaa zaidi kupigia mfano kifungu hiki?
    1.  Mwenye nguvu mpishe.
    2. Pwagu hupata pwaguzi.
    3. Akili nyingi huondoa maarifa.
    4. Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.
  10. Neno 'hewalla' kama lilivyotumika A. ni kiingizi cha kusisitiza jambo B. ni kihusishi cha wakati C. ni kihisishi cha kukubaliana na jambo D. ni kielezi cha kufafanua jambo.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia 41 hadi 50.
Hakuna jambo litakalohatarisha maisha yetu humu duniani kuliko ukataji wa misitu. Hakika, ukataji huu si jambo jipya kwetu. Hata mababu na nyanya zetu walikata miti. Walifanya hivyo kwa matumizi mbalimbali kama vile ujenzi, dawa, mavazi na kadhalika. Ukataji miti siku hizo, hata hivyo, ulifanywa kwa uangalifu. Baadhi ya miti ilikatwa kwa ajili ya kafara na kwa matumizi mahsusi lakini leo, miti hukatwa bila kusudi maalum.
Si ajabu kupata miti ikikatwa milimani kwa kusudi la kupanda dawa za kulevya kisiri ili isijulikane na serikali. Aidha, miti imekatwa ili kujenga majumba yetu katika mazingira yaliyo na hewa mwanana bila kujali madhara tunayosababishia mandhari yetu. Tumekata miti kando ya mito ili kulima vishamba vya mboga karibu na chemichemi ya maji. Kile ambacho binadamu hafahamu ni kuwa miti hii ndiyo inayoshikilia udongo usimomonyoke.

Inafahamika kuwa misitu ni asili ya chakula na maskani ya wanyama. Misitu inapokatwa, ama wanyama watakufa au watahamia kwingine. Huko kwingine kunaweza kuwa kwenye makao yetu binadamu. Watavamia mashamba yetu na kuhatarisha maisha yetu na ya wanetu.
Tusisahau kuwa misitu huvuta mvua. Tunapokata miti tunapunguza mvua na tunaharakisha ukame. Bila mvua, mito na maziwa yatakauka. Bila maji sisi hatutakuwa na uhai. Mifugo wetu nao watafuata mkondo uo huo.

Hebu fikiria utafanyaje uamkapo asubuhi na kuambiwa kuwa mfadhili wako ameachishwa kazi katika kiwanda cha karatasi kilichopo hapo karibu. Kuna uwezekano wa hayo kutokea iwapo ukataji wa misitu utaendelea. Viwanda vitakosa malighafi, hivyo vitafungwa na watu kumwaga unga. Basi vitu kama karatasi, mbao, gundi na viberiti vitakosekana au kupanda bei.

Vilevile, misitu inapokatwa, dawa za kienyeji na za kisasa zitapotea kwa maana nyingi kati yazo hutokana na miti. Wagonjwa wengi watatangulia mbele ya haki kwa kukosa dawa. Je, wakataji miti wenyewe wajua wao pia wataangamia?

Misitu mingi yenye manufaa makubwa huchukua muda mrefu kukomaa. Kwa hivyo, tunapoikata bila mpango tunavinyima vizazi vya kesho urithi huu wa kimaumbile. Vijana wengi watakuwa wakizisoma habari za misitu vitabuni bila kuiona misitu yenyewe. Utafiti wa miti pia utakwama na elimu itakoseshwa mahali pa uvumbuzi nyanjani. Sasa iko wapi faida ya kufunza taaluma ya misitu katika shule na vyuo kinadharia tu kama misitu yenyewe haipo?

Miti isipokuwepo hakuna kitu kitakachozuia mmomonyoko wa udongo wetu wenye rutuba. Mimea itadhoofika ajabu. Mchanga nao utajaa kwenye mito na maziwa. Hali hii ikiendelea maziwa yatapotea.

Hakuna mandhari yavutiayo kama yale yenye rangi ya kijani. Mtu atembeapo karibu na miti jioni, hufurahia harufu tofauti; harufu ya maua na mzizimo wa upepo mwanana. Miti ikipotea ghafla hubaki visiki butu vyenye rangi ya hudhurungi au kijivu isiyovutia. Badala ya mzizimo huwa upepo mkali uliobeba vumbi jingi. Matokeo yake ni mawili. Kwanza, upepo huu waweza kusababisha uharibifu kama vile kuangusha miti na hata kung'oa mapaa ya nyumba.

Hasara nyingine ni kuwa upepo husafirisha viini vinavyoeneza magonjwa chungu'nzima ya macho, koo na mapafu. Hewa itachafuka maana hakuna miti ya kuisafisha. Mnaona! sisi wenyewe tunajiua. Tamaa mbele mauti nyuma.

  1. Ni kweli kusema kuwa
    1. ukataji wa misitu ni hatari pekee inayoweza kuwaangamiza watu duniani
    2. hapo awali, ukataji wa miti haukuwa ukifanyika kiholela
    3. wazee wa zamani hawakuthubutu kuikata misitu asilani
    4. awali, miti ilikuwa na matumizi mbalimbali, kinyume na ilivyo sasa.
  2. Wanaokata miti milimani hufanya hivyo ili
    1. wapate miti iliyo bora zaidi
    2. waharibu misitu makusudi
    3. wakuze mboga karibu na chemichemi
    4. washiriki kilimo cha mimea haramu.
  3. Kulima kwenye kingo za mito kuna athari gani kulingana na kifungu?
    1. Kusababisha memonyoko wa udongo.
    2. Kusababisha kukauka kwa vyanzo vya maji.
    3. Kufariki kwa viumbe wa majini.
    4. Kuchafua maji yanayofanikisha kilimo.
  4. Kulingana na aya ya tatu
    1. kukata miti ovyoovyo husababisha mgogoro wa binadamu na wanyama
    2. kukata miti ovyoovyo ni kichocheo kikuu cha ukame
    3. maeneo yasiyo na misitu hayana  binadamu wala wanyama
    4. watu wengine huharibu mazingira kwa nia ya kuanzisha makao yao.
  5. Kufungwa kwa viwanda katika kifungu husababishwa na
    1. ukosefu wa wafanyakazi
    2. hali ngumu ya kiuchumi
    3. kukosekana kwa malighafi
    4. kupungua kwa mvua.
  6. Chagua msemo mwingine wenye maana sawa na 'watatangulia mbele ya haki'.
    1. Watakula mwata.
    2. Wataenda na ulele ngoma.
    3. Watakufa moyo.
    4. Wataenda nguu.
  7. Manufaa ya misitu kulingana na makala haya ni
    1. kufanikisha elimu na dawa za kulevya
    2. kuhifadhi maji na kuzuia mmomonyoko wa udongo
    3. urithi wa vizazi na kubuniwa kwa mitambo
    4. kuongeza nafasi za kazi na kusafisha hewa.
  8. Matokeo ya upepo mkali yanaweza kuwa
    1. magonjwa ya mapafu na ardhi kukosa mvuto
    2. kuvunja miti na kutatiza starehe za watu
    3. kuporomoka kwa majengo na kueneza maradhi
    4. mmomonyoko wa udongo na kupotea kwa maziwa.
  9. Kauli 'sisi wenyewe tunajiua' inaonyesha kuwa
    1. binadamu wanauana wenyewe kwa wenyewe
    2. tunajiangamiza kwa matendo yetu
    3. bila misitu vizazi vijazo havitakuwepo
    4. binadamu amevamiwa na maradhi chungu nzima.
  10. Kichwa kifaacho zaidi kwa makala haya ni
    1. Faida za misitu.
    2. Mmomonyoko wa udongo.
    3. Tamaa mbele mauti nyuma.
    4. Madhara ya uharibifu wa misitu.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa. Ufuatao ni mwanzo wa insha. Iendeleze kwa maneno yako mwenyewe huku ukiifanya iwe ya kusisimua zaidi.

Mchana kutwa sikuweza kupata utulivu. Nilitamani kurudi nyumbani haraka ili............................

MARKING SCHEME

  1. C
  2. A
  3. D
  4. B
  5. A
  6. C
  7. B
  8. D
  9. D
  10. A
  11. C
  12. B
  13. A
  14. D
  15. B
  16. D
  17. A
  18. C
  19. B
  20. C
  21. A
  22. D
  23. D
  24. C
  25. D
  26. A
  27. D
  28. C
  29. B
  30. D
  31. B
  32. C
  33. A
  34. D
  35. A
  36. B
  37. A
  38. D
  39. B
  40. C
  41. B
  42. D
  43. A
  44. A
  45. C
  46. B
  47. D
  48. C
  49. B
  50. D

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifealo zaidi kati ya yale aliyopewa.

Lugha ya Kiswahili hutumika __1__ waafrika __2__ wakoloni. Jukumu la lugha __3__ ile kama wenzo wa mawasiliano__4__kupuuzwa. __5__kila kabila huwa na lugha yake ambayo __6__ kitamaduni na kimila.

   A   B   C   D 
 1.    kuwatambulisha na kuwaunganisha   kuwahamasisha na kuwalinganisha   kuwadumisha na kuwajenga   kuwastawisha na kulenga 
 2.  juu ya  dhidi ya  kando na   kando ya 
 3.  zozote  lolote   yoyote   chochote 
 4.  haiwezi  hauwezi   hayawezi   haliwezi 
 5.  Aghalabu  Lau  Angalau  Ingawa 
 6.  hulitambulisha  huitambulisha  huwatambulisha  hututambulisha 

 

Ni muhimu kufahamu kuwa kiini cha lugha ya Kiswahili ni sauti. __7__ sauti hizi ni zile zinazotetemesha nyuzi za koromea yaani __8__ Mfano wa sauti hizi ni __9__.  __10__. kuna lugha nyingi __11__ulimwenguni, lengo kuu hasa huwa ni __12__ mawasiliano kwa namna __13__. Kila jamii inafaa __14__ lugha yake bila kuiona fedheha maadamu __15__.

   A   B   C   D 
 7.   Katikati ya   Miongoni mwa   Baina ya   Mojawapo ya 
 8.  sighuna  mwambatano   ghuna   changamano 
 9.  b,d,g,z  ch,h,s,tu   f,p,sh,e   w,y,sh,f,h 
 10.   Aidha  Minghairi ya hayo   Ijapokuwa   Waama
 11.  mote  pote   kote   kwote 
 12.  kuyafaulisha   kutufaulisha  kuyatosheleza   kututoshelezea 
 13.  yafaayo  ifaavyo   ifaayo   yafaavyo 
 14.  kuzithamini  kuzidhamini  kuithamini  kuidhamini
 15. mzigo u kichwani, kwapa lakutokeani jasho  mwacha kiwi hanacho na chema kimpotelee  mwacha mila ni mtumwa  bura yangu sibadili na rehani

 

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi.

  1. Chagua sentensi iliyo sahihi kimantiki.
    1. Pale mlipoketi pana unyevu.
    2. Kule mlikoketi mna unyevu.
    3. Mle mlipoketi mna unyevu.
    4. Kule mlimoketi kuna unyevu.
  2. Tambua viambishi vya neno 'walipelekana'
    1. wa-li-pe-le-ka-na
    2. wa-li-a-na
    3. pe-le-ka-na
    4. wa-li-pe-le-k
  3. Chagua sentensi yenye -ni- ya wingi.
    1. Wao ni wanafunzi watiifu.
    2. Majoka yale yalijificha.
    3. Yatunzeni mazingira yenu ipasavyo
    4. Mliponielekeza njia nilifurahi sana.
  4. Kanusha sentensi ifuatayo:
    Utafiti uliofanywa uliridhisha wachache
    1. Utafiti usiofanywa haukuridhisha wachache.
    2. Utafiti uliofanywa uliridhisha wengi.
    3. Utafiti uliofanywa haukuridhisha wachache.
    4. Utafiti usiofanywa hauridhishi wengi.
  5. Chagua methali yenye maana sawa na hii:
    Mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi.
    1. Usitukane wakunga na uzazi ungalipo.
    2. Bura yangu siibadili na rehani.
    3. Zigo la kuliwa halilemei.
    4. Maji ya kifuu ni bahari ya chungu.
  6. Ni sentensi ipi inayoonyesha kusudi la tendo.
    1. Suna aliingia zizini akawafungulia ng'ombe akaelekea malishoni.
    2. Malikia alituambia twende tukavue samaki.
    3. Wafanyakazi walifanya bidii wakamaliza kazi hiyo.
    4. Wageni watakuja watakapokamilisha shughuli.
  7. Chagua jibu lenye maelezo sahihi.
    1. Surua ni ugonjwa wa watoto unaosababishwa na majipu mwilini.
    2. Ukoma ni ugonjwa wa kukatika kwa viungo vya mwili.
    3. Pumu ni ugonjwa wa mapafu unaosababisha kukohoa damu.
    4. Machapwi ni ugonjwa wa kutoa damu na kuvimba fizi.
  8. Chagua usemi halisi wa sentensi hii:
    Kamaliza alisema kwamba wangeenda kuogelea siku ambayo ingefuata.
    1. "Tutaenda kuogelea kesho,” Kamaliza alisema.
    2. "Mtaenda kuogelea siku inayofuata," Kamaliza alisema.
    3. " Nimeenda kuogelea kesho,” Kamaliza alisema.
    4. ' utaenda kuogelea siku inayofuata,” Kamaliza alisema
  9. Komba ni mnyama mdogo jamii ya kima anayelialia wakati wa usiku. Komba aidha ni 
    1. chakula maalum anachokula bwana harusi.
    2. kukusanya vitu na kuviweka mahali pamoja.
    3. kitu kilicho na kina kidogo kama vile
    4. chombo cha miyua, ngozi au kamba kinachotumiwa kurushia mawe.
  10. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo:
    Mtume alisimama karibu na ua wa nyumba hiyo.
    1. Mitume walisimama karibu na nyua za nyumba hizo.
    2. Watume walisimama karibu na maua ya nyumba hizo.
    3. Mitume ilisimama karibu na maua ya nyumba hizo.
    4. Watume walisimama karibu na nyua za nyumba hizo.
  11.  Chagua sentensi iliyounganisha sentensi zifuatazo ifaavyo:
    1. Timu yetu ilicheza vizuri.
    2. Hatukushinda mechi hiyo.
      1. Hatukushinda mechi hiyo kwani timu yetu ilikuwa imejiandaa vizuri.
      2. Ingawa timu yetu ilikuwa imejiandaa vizuri hatukushinda mechi hiyo.
      3. Aidha timu yetu ilikuwa imejiandaa vizuri hatukushinda mechi hiyo.
      4. Hatukushinda mechi hiyo maadamu timu yetu ilikuwa imejiandaa vizuri.
  12. Yapi si matumizi ya alama ya mshazari
    1. Kuonyesha neno lenye maana sawa au kuonyesha 'ama'
    2. Kuandika tarehe.
    3. Kutenganisha shilingi na senti
    4. Kuonyesha maneno au maelezo yasiyokuwa ya lazima. 
  13. Ainisha maneno yaliyoangaziwa katika sentensi hii.
    Mwanafunzi hodari ametuzwa tena.
    1. Kielezi, kiwakilishi
    2. Kivumishi, kielezi
    3. Kitenzi, kiwakilishi
    4. Kiunganishi, kielezi
  14. Tegua kitendawili kifuatacho:
    Nimemwona bikizee amejitwika machicha.
    1. Upango wa jogoo
    2. Nyota angani
    3. Mvi
    4. Chawa
  15. Sentensi ifuatayo itaandikwaje katika kauli ya kutendewa? Farida aliandika barua akamtumia Rukia.
    1. Farida alimtumia Rukia barua aiyoandika
    2. Rukia alitumiwa barua aliyoandikiwa na Farida
    3. Farida aliandikiwa barua na Rukia akatumiwa.
    4. Barua iliandikwa na Farida na kutumwa kwa Rukia.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.

Naikumbuka siku hiyo vizuri. Niliamka alambichtayari kuanza safari kutoka kijijini mwetu hadi mji mkuu. Hii ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kuzuru mji huu. Moyoni nilikuwa na furaha isiyokuwa na kifani maadam siku hiyo ningeuona mji ambao sifa zake nilikuwa nikizisikia tu kutoka kwa wenzangu waliobahatika kuutembelea. Hamu ya kuona majengo marefu, barabara zilizosakifiwa, magari mengi, watu wa asili mbalimbali na bustani za starehe ilinigubika, nikawa sijifai kwa matumaini.

Mjini aliishi rafiki yangu kwa jina pendo. Basi baada ya kuamka niliweza kumkumbusha mama kuhusu ziara ya kumtembelea rafiki yangu aliyekuwa ameandaa sherehe ya kuzaliwa kwake. Mwenyewe nilikuwa nimepata mwaliko wa kushiriki katika karamu ya kuadhimisha mwaliko wa kushiriki katika karamu ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa. Kawaida yangu niliamini kuwa safari ya kesho hupangwa leo. Hivyo basi niliweza kumwarifu mama mapema japo matumaini yangu hayakuwa makubwa kwa sababu mama hakumpenda Pendo asilani. Haya yote yalisababishwa na ukweli kwamba Pendo alitoka katika familia tajiri. Kulingana na mama, watoto matajiri kutokana na kudekezwa, waliishia kuwa watovu wa nidhamu.

Msimamo wa mama asubuhi hiyo ulikuwa ule ule usiotetereka. Hakutaka kamwe nijihusishe na Pendo. Hapo aliweza kunitaka kuvuta taswira niuone usuli wangu wa umaskini ulionifanya kama muwele wa ukoma. Ukosefu wa karo ulikuwa ukinitishia kuniambia kuwa muda wangu wa masomo ulikuwa umekwisha. Mama aliendelea kunisimanga akinikumbusha jinsi alivyochumia juani kunilisha mimi. Alinitapikia yote yaliyokuwa moyoni mwake na kulitua zigo lake la siku nyingi. Mawazo yaliendelea kunijia nikajipata nikilia kwa kite na shake. Kwikwikwi zangu za kilio zikahanikiza chumbani mote. Ghafla nikajipata na ujasiri wa Simba. Nilimkabili mama na kumwambia kuwa ningehudhuria haramu ya Pendo na liwe liwalo. Hapo ndipo mama alinikumbusha kuwa asiyesikia la mkuu huabiri mtumbwi wa mfinyanzi. Hata hivyo maaso haya yote yaliangukia masikio yaliyotiwa tomo.
yangu

Kwa kufuata kauli yangu nilianza kujitayarisha kuhudhuria karamu ya Pendo. Kutokana na ukaidi wangu mama alinikodolea macho kana kwamba hakuwahi kuniona nami nikazidi kujipodoa. Akajaribu kunikataza lakini alikuwa akimpigia mbuzi gitaa. Kuna wale husema siku njema huonekana asubuhi nayo hiyo iliharibiwa na mama. Aidha mkesha wa siku hiyo ulishuhudia milio mingi ya bundi hivyo basi kunitia shaka na shauku. Nikaanza kujisemea kimoyomoyo huku nikinyambua nyayo zangu kuelekea kwenye kituo cha basi. “Hivi ni lazima nihudhurie hii? Huu mlio wa bundi una maana gani? Lakini potelea mbali, na liwe liwalo. Lazima nihudhurie.

Baada ya kujisuta moyoni, niliondoka na kuelekea kwenye kituo cha magari. Likaja basi moja ambalo lilisheheni abiria kupindukia. Nilijisukuma ndani na basi likaanza mwendo. Nikajipata nimening'inia kibavuni pa basi huku nikibinywa na abiria wenzangu. Gari nalo likazidisha mwendo nikaanza kujisuta na kujiuliza ni kwa nini niliingia katika basi hilo. Hapo wazo la kushuka likanijia ili niabiri jingine lakini ujasiri wangu ukanipa kufikiri kuwa kwa shujaa huenda kilio na kwa mwoga huenda kicheko. Lakini kushuka kwangu kungenifanya nionekane limbukeni. Nikiwa katika wazo hilo basi hiliingia katika mtaa wa akina Pendo. Hapo nilitia mkono kibindoni na kumkabidhi utingo nauli yangu Hatimaye basi lilitia nanga na hapo nikashusha pumzi na kushuka. Mimi sikutaka kudekeza hisia za wengi kuwa bundi ni ishara ya mkosi.

Nilipiga masia hadi nyumban pa akina Pendo. Huko sherehe za kila nui ndizo ziliwaongoza wote hata waliokuwa na akili razini. Nani nikajiona nikiumezea mate uhondo niliouona. Walikuja wasena wengi, maghulamu kwa mabanati wengi nisiowajua. Tukaanza kujiburudisha kwa kila aina ya muziki, ya kufokafoka na mengineyo. Vinywaji navyo vikaletwa vile vikali na visivyo vikali. Walio wazoefu wa kunywa vile vikali wakajituma karamuni bila kujali. Nami kwa kuhofia kuonekana limbukeni nikajiingiza katika kumbo hilo. Nikaanza kushiriki ugimbi huo ili kusahau kero za mama. Nikamimina chupa ya kwanza, ya pili na hata ya tatu. Hapo nikajiona nikielea hewani. Nilihisi vyema sana.

Baada ya muda fulani, usiku ukaufumbata ulimwengu nazo sherehe zikaanza kunoga zaidi. Tukawa tunakula na kusakata ngoma bila kujali mpito wa wakati. Kutahamaki nikajipata nikikabiliana na kiza cha usiku wa manane. Magari ya abiria hayakuwa hivyo basi hatukuwa na jingine ila kuabiri gari la akina Pendo. Pendo akawa ndiye dereva wa gari hilo licha ya kuwa alikuwa akitawaliwa na kinywaji. Hata hivyo hatukuwa na jingine la kufanya ila kuridhika na usafiri uliopatikana. Hapo tulijitoma garini tukiwa wanane. Katika hali yetu hakuna aliyefikiria kufunga mikanda ya usalama. Gari likaanza kuserereka kwa kasi. Mara, Lo! Gari letu likakosa kujipinda kwenye kuruba. Hapo ndipo niliona dari la gari letu, miguu ya wenzangu juu ya dari hilo huku wingu kubwa la moshi likipaa juu. Hatimaye kiza cha kaniki kikatanda.

  1. Kulingana na aya ya kwanza
    1. wenzake msimulizi waliwahi kupata fursa ya kuishi katika mji mkuu.
    2. barabara za mji mkuu hazikuwa na mashimo.
    3. mji mkuu una majumba mengi na marefu.
    4. msimulizi ana mwao na hali ilivyo katika mji mkuu.
  2. Kulingana na aya ya pili
    1. mwanzoni mama alikuwa amempa msimulizi ruhusa.
    2. mama wa msimulizi hakumruhusu kutangamana na vijana wenzake.
    3. mama yake msimulizi alikuwa mwenye ubaguzi wa kitabaka.
    4. msimulizi hakumtarajia mama yake kumkatalia katika ombi lake
  3. Ni wazi kuwa
    1. msimulizi alisomeshwa kwa taabu kutokana na umaskini wa familia yao. 
    2. msimulizi hakumaliza masomo yake kutokana na umaskini wa hali ya juu.
    3. msimulizi alisomea katika shule za kifahari alikosomea Pendo.
    4. urafiki wa Pendo na msimulizi ulichipuka walipokuwa katika shule ya upili.
  4. Kibindoni ni
    1. mfuko mdogo ndani ya suruali.
    2. mfuko mdogo mbele ya suruali
    3. mkunjo wa nguo uliyoshonwa kiunoni.
    4. mkunjo wa nguo uliofungy
  5. Taja tamathali mbili za lugha zinazojitok katika kauli hii.
    Huko sherehe za kila nui ndizo zilizowaongoza wote hata waliokuwa na akili razini.
    1. Kinaya, semi
    2. Tashhisi, nahau
    3. Chuku, nahau
    4. Uhuishi, ishara
  6. Kwa nini msimulizi alitumia vinywaji vikali japo hakuvizoea?
    1. Alitaka kusahau kero alizokuwa amepata asubuhi kutoka kwa mama yake.
    2. Alitaka hiyo iwe siku yake ya kwanza kuonja kinywaji kikali.
    3. Alichelea kuonekana duni na wanarika wenzake.
    4. Alichelea kuondolewa kundini na wenzake.
  7. Kwa nini msimulizi wa wenzake waliamua" kutumia gari la wazazi wa Pendo?
    1. Magari ya uchukuzi hayakupitia katika mitaa ya mabwanyenye.
    2. Kupita kwa wakati kulifanya magari yakosekane mtaani humo.
    3. Ulevi wao uliwafanya washindwe kufika kituoni.
    4. Wenyeji wao waliwaomba watumie gari hilo badala ya usafiri wa umma.
  8. Alipofika karamuni, mwandishi aliwapata
    1. wake kwa waume.
    2. marafiki zake.
    3. vijana wa kike na kiume.
    4. pendo, vijana na wazazi wao.
  9. Ni methali pani mwafaka kuelezea jumla ya mbe kauli hii?
    Hata hivyo hatukuwa na jingine la kufanya la kuridhika na usafiri uliopatikana.
    1. Akosaye la mama hata la mbwa huamwa. 
    2. Msafiri ni aliye pwani.
    3. Ajiingizaye kwa yasiyomhusu hupata yasiyo mridhi.
    4. Cha mlevi huliwa na mgema.
  10. Hatimaye kiza cha kaniki kikatanda. Yaani
    1. kukawa na giza totoro.
    2. kukawa na weusi mkubwa.
    3. msimulizi akapoteza uwezo wa kuona.
    4. msimulizi akapoteza fahamu.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50

Somo la Historia hujikita sana katika uwezo wa mtu kukumbuka. Leo hii kuna wale hutusimulia yaliyotukia wakati wa ukombozi na taifa letu. Si ati hawa hawajui wanachosema. Kile wanachosema ni kutokana na uwezo wao wa kukumbuka. Uwezo huu umeweza kudhibitiwa na mambo anuwai. Uwezo huu si wa binadamu pekee. Hata wanyama hukumbuka mengi yaliyotokea awali.

Nao uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu ni mojawapo ya shughuli changamano za ubongo. Shughuli hii hutekelezwa ubongoni kwa namna tatu. Kwanza ubongo wenyewe hunasa jambo kisha hulihifadhi. Baadaye huanzisha mfumo wa kutoa kilichohifadhiwa ubongoni humo. Ubongo ukiathirika kwa namna yeyote katika njia hizi, basi uwezo wa kuyakumbuka mambo huvurugika vururu vururu.

Ukweli unaoaminika ni kuwa uwezo huu hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Hata hivyo wataalamu wa masuala ya kiakili wanabaini kwamba uwezo huu unaweza kuimarishwa. Uimarishaji huu huhitajika mikakati madhubuti. Hii ni kwa sababu kwa kawaida jambo haliwezi kufanyika au kufanikiwa bila ya kuwepo kwa vitu fulani au taratibu zifaazó kulifanyia.

Njia mojawapo ya kustawisha uwezo wa kukumbuka ni kupitia kwa lishe. Vyakula vilivyosheheni vitamini B vyenye Amino Asidi ni muhimu sana. Mifano ya vyakula hivi ni mboga, nyama, (hasa maini), bidhaa za soya, matunda, maziwa, ngano, samaki na mayai. Vyakula vingine muhimu katika ustawishaji huu ni vile vyenye madini ya chuma. Haya huwezesha usambazaji wa hewa katika ubongo wa wepesi. Vyakula ambavyo vina madini haya ni mboga za kijani, mawele, ndengu, soya, matunda kama maembe, ufuta (simsim), nyama hasa maini na mayai. Ukizingatia haya unakuwa na uwezo wa kukumbuka hata yaliyofanyika kabla ya wewe kuzaliwa

Ubongo wa adinasi aliye hai hufanya kazi wakati wote, awe macho au awe amelala. Utendaji kazi wake huendeshwa na glukozi mwilini. Kwa hivyo, vyakula vyenye aina hii ya sukari ni muhimu kuliwa. Hata hivyo, lazima mtu awe mwangalifu kuhakikisha kuwa mwili una kiwango cha sukari kisichohatarisha maisha. Haya yanawezekana kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile mboga na matunda.

Vileo navyo vyafaa kupigwa marafuku mathalani nikotini na pombe. Hii ni kwa sababu vileo hivi huathiri utaratibu wa kunasa, kuhifadhi na kutoa yaliyo ubongoni. Mtu hujipata amesahau hata yale hakujua.

Iwapo mtu ana matatizo ya kuyakumbuka majina ya watu, ni vyema kufanya mazoezi ya kusikiliza kisha kurudia majina haya wakati wa mazungumzo. Ni bora kulihusisha jina na sura ya mtu. Kwa njia hii ubongo utanasa jina na kile kinacholengwa.

Woga na kuvurugika kiakili ni mambo mengine tunayopaswa kuepuka kila wakati. Ni kawaida mtu kupata woga anapokabili jambo asilokuwa na uhakika na mahojiano. Lakini anapaswa kuwa makini. Woga huo usikiuke mipaka na kumvuruga kiakili. Vurugu hizi huathiri kilichohifadhiwa ubongoni na pia namna ya kukitoa.

Aidha mwili wenye rai njema huhakikisha kuwa ubongo ni timamu. Wataalamu wengi wa afya wanakubali kuwa mazoezi ya kunyosha viungo hustawisha ubongo na hivyo kuhakikisha kuwepo kwa uwezo wa kukumbuka mambo. Ni muhimu kuwa na utaratibu wa kunyoosha viungo kila wakati. Fauka ya hayo, mazoezi ya kiakili kama vile kusoma makala yanayovutia, kujaza mraba na michezo mingine kama mafumbo na vitanzandimi ni muhimu katika kustawisha uwezo huu.

Jamii yenye uwezo wa kuyakumbuka mambo hupiga hatua kubwa kimaendeleo. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuandama sera za kuimarisha uwezo wa kukumbuka kila wakati. Yeyote ambaye atakiuka sera hizi, lawama zote zafaa kumrudia yeye

  1. Kulingana na aya ya kwanza, umeweza kudhibitiwa" ina maana gani?
    1. Umeweza kuondolewa.
    2. Umeweza kuzuiliwa.
    3. Umeweza kutibiwa wote.
    4. Umeweza kupunguzwa wote.
  2. Aya ya pili imeonyesha wazi kuwa 
    1. mtu yeyote ana uwezo wa kuyakumbuka mambo.
    2. uwezo wa kukumbuka unaweza kuwepo hata bila uhai.
    3. si lazima mtu awe na uwezo mzuri wa kukumbuka
    4. kuyakumbuka mambo huhusisha ungo vyote mwilini.
  3. Kwa mujibu wa aya ya tatu
    1. uwezo wa kukumbuka mambo ni jambo la kujifunza.
    2. mtu hawezi kuathiri uwezo wake wa kukumbuka.
    3. watu huzaliwa na uwezo sawa wa kukumbuka ila wengine hujiimarisha.
    4. uwezo wa kukumbuka hutegemea sana maumbile ya mtu. 
  4. Ni kundi lipi la vyakula vinavyoimarisha uwezo wa kukumbuka?
    1. Asidi, nyama na mboga.
    2. Mboga, sukari na mayai.
    3. Maini, ngano na mayai.
    4. Soya, matunda na vileo.
  5. Kulingana na aya ya tano, mtu anapolala
    1. uwezo wake wa kukumbuka huimarika.
    2. ubongo wake huendelea kufanya kazi.
    3. ubongo wake huacha kazi ili kupumzika.
    4. bado unaelewa kila jambo linalotokea.
  6. Yapi ndiyo manufaa ya nyuzinyuzi zinazopatikana katika mboga na matunda? 
    1. Zinatoa sukari ya kuendesha shughuli mwilini.
    2. Hupatia mwili madini muhimu ya chuma. 
    3. Huwezesha usambazaji mzuri wa hewa mwilini.
    4. Huchangia kudhibiti kiwango cha sukari mwilini.
  7. Athari za kutumia vileo kwa wingi ni
    1. kuimarisha uwezo wa mtu wa kukumbuka.
    2. hudhoofisha utendakazi wa ubongo.
    3. hunyima mwili viwango vifaavyo vya Sukarı
    4. humnyima mtu hamu ya kujikumbusha mambo.
  8. Hii ni tamathali gani ya lugha?
    Mtu hujipata amesahau hata yale hakujua.
    1. Chuku
    2. Kinaya
    3. Ishara
    4. Tabaini
  9. Rai kulingana na kifungu ni
    1. kusema na mtu kwa maneno mazuri.
    2. kutia mtu chakula mdomoni.
    3. maoni ya mtu juu ya jambo fulani.
    4. hali ya mwili kuwa na afya nzuri.
  10. Chagua methali inayoweza kujumuisha ujumbe wa kauli hii:
    Uimarishaji huu huhitaji mikakati madhubuti. Hii ni kwa sababu kwa kawaida jambo haliwezi kufanyika au kufanikiwa bila ya kuwepo kwa vitu fulani au taratibu zifaazo kulifanyia.
    1. Mti huchongewa ni tundaze.
    2. Mti upigwao mawe ni wenye matunda.
    3. Mti ukupigwao ndio ukufunzao.
    4. Mti hauendi ila kwa nyenzo.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha itakayoanzia kwa maneno yafuatayo:

Nilipomtazama, niliamini kuwa uzembe hauna manufaa ....................................................\

MARKING SCHEME

  1. A
  2. B
  3. C
  4. D
  5. A
  6. A
  7. D
  8. C
  9. A
  10. A
  11. C
  12. A
  13. C
  14. C
  15. D
  16. A
  17. B
  18. C
  19. B
  20. D
  21. B
  22. B
  23. A
  24. A
  25. A
  26. B
  27. D
  28. B
  29. C
  30. B
  31. D
  32. C
  33. A
  34. D
  35. B
  36. C
  37. B
  38. C
  39. A
  40. D
  41. B
  42. A
  43. C
  44. C
  45. B
  46. D
  47. B
  48. A
  49. D
  50. D

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya uliyopewa.

__1__ husema kuwa __2__. Ulimi huu ulidhihirika __3__ hivi majuzi humu nchini pale ambapo mchungaji mmoja maarufu aliwahadaa wafuasi wake kwa kuwaagiza kususia chakula na maji kwa muda wa siku arubaini ili kumwona Mungu. Hatua hii __4__ mauti ya wengi wa wafuasi hao wake huku miili yao ikipatikana katika shamba la mchungaji huyo la zaidi ekari themanini. Iliaminika kuwa mchungaji huyo alikuwa na nia __5__ ambayo haikubainika kwa wakati ufaao. Wengi walisikika wakidai kuwa kuwaamini baadhi ya wachungaji sasa ni sawa na __6__. Baadhi hawaaminiki. __7__.

   A   B   C   D 
 1.   wasemavyo   waemayo   wasemao   wanaposema 
 2. kosa moja halimwachishi mke  papo kwa papo kamba hukata jiwe  papo kwa papo kamba hukata jiwe   uzuri wa kuyu ndani mabuu 
 3.  tenge tahanani  dhahiri shahiri  daima dawamu  liwalo na liwe 
 4.  ilipelekea  ilielekeza   ilileta   ilisababisha 
 5.  fiche  bora   bayana   njema 
 6. kutarajia manufaa baada ya bidii kuchezea shilingi katika tundu la choo kuwarai waumini kujiunga na madhehebu kumtegemea Mungu katika shughuli zetu
 7. Wamevalia ngozi ya chui Wamezifichua kucha zao Wamevalia ngozi ya kondoo Matendo yao yako wazi


Dunia ya sasa inaenda mbio na maisha ya vijana wetu nayo pia __8__ kwa kiasi mithili ya duma. Ugumu wa maisha na __9__ kwa uchumi vinawasukuma baadhi yao __10__ katika uhuni ili __11__. Ni afadhali __12__ na kidogo walicho nacho kuliko kutamani kingi wasicho nacho kwani __13__. Pia, wanaweza kujianzishia miradi ya __14__ badala ya __15__.

   A   B   C   D 
 8.   yakitimika   yakiimarika   yakizorota   yakidumaa 
 9.  kuporomoka   kujengeka   kubomoka   kuimarika 
 10.   kujitoma  kujiondoa   kujitosa  kujikuta 
 11.  kusaka ukata   kusumbua riziki   kuasi umaskini   kutafuta umaarufu 
 12.  watosheleza  wasiridhike   wakinaishwe   wasikinai 
 13.  haba na haba hujaza kibaba   apelekaye mkono kutamalaki si kazi   bura yangu sibadili na rehani   njia mbili zilimshinda fisi 
 14.  kutusaidia  kuniauni   kujikimu   kukuokoa 
 15.  kujikaza kisabuni  kuuma uzi  kujifunga kibwebwe  kupakata mikono

 

Kutoka swali la 16 hadi 30, jibu swali  kulingana na maagizo.

  1. Chagua sentensi iliyo na tashbihi jozi.
    1. Dada yake ana maringo kama tausi.
    2. Rudisha ana mbio mithili ya duma.
    3. Bahasha yangu ni nyeupe ja theluji.
    4. Wanafanana kama kurwa na doto.
  2. Tumia sifa "geni" kusanifisha sentensi ifuatayo;
    Wazo alilotoa kuhusu nchi yake ni
    1. ngeni.
    2. mgeni.
    3. ligeni.
    4. geni.
  3. Chagua ala ya muziki ambayo huchezwa kwa uta mdogo.
    1. Firimbi
    2. Zeze
    3. Marimba
    4. Zumari
  4. Kiulizi "ngapi" huwa tasa katika ngeli gani?
    1. I - ZI
    2. LI-YA
    3. KI-VI
    4. KU-KU
  5. Tenga silabi katika neno "mafunzo"
    1. m-a-f-u-n-z-o
    2. ma- fu- n - zo
    3. mafunzo
    4. maf - un-zo
  6. Kamilisha methali;
    Kukopa harusi
    1. isiyo na vigelegele.
    2. ingawa kulipa ni kugumu.
    3. kulipa matanga.
    4. lakini hakuna raha,
  7. Chagua sentensi iliyo sahihi kisarufi.
    1. Wewe na Musa ndio viranja wa darasa letu.
    2. Utajua aje hesabu bila kufanya mazoezi?
    3. Upande huu ni mpana kuuliko ule.
    4. Kwamba atakuja au atasusia, kwangu ni mmoja.
  8. Je, ni sentensi ipi iliyotumia kiunganifu-a- kwa usahihi?
    1. Rafiki ya Abdala ni Salim.
    2. Katikati mwa jiji kuna msongamano wa magari.
    3. Uwanjani kwa watoto kuna nyasi ndefu.
    4. Shauri ya Omari, hakumaliza kazi ya mwalimu.
  9. Chagua orodha yenye vivumishi pekee.
    1. Yangu, kivivu, yeye, juu ya
    2. Lini, ovyo, ya, ala!
    3. Pona, ona, safi, ghali.
    4. Wao, hiki, nyembamba, mwa
  10. Chagua maneno yaliyo katika ngeli ya I-ZI.
    1. Dahalia, korti, kawa.
    2. Maabara, kalamu, chupa.
    3. Maeneo, mizani, simu.
    4. Kimbilio, maskani, nyumba.
  11. Nomino kudhoofika lina konsonanti ngapi? 
    1. 4
    2. 5
    3. 3
    4. 6
  12. Eleza matumizi ya “na
    Wana huzuni tangu wafiwe na mkoi wao.
    1. Umiliki
    2. Mtendaji
    3. Hali
    4. Kiunganishi
  13. Ni sayari gani kati ya hizi iliyo angavu zaidi?
    1. Mshtarii
    2. Zuhura
    3. Utaridi
    4. Zohali
  14. Nahau enda magamaga ina maana ya 
    1. enda kwa kutanua miguu.
    2. aga dunia.
    3. enda upesi.
    4. tembea polepole.
  15. Kimelea gani hupatikana katika maskani ya kuku?
    1. Siridado
    2. Funza
    3. Papasi
    4. Utitiri

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 hadi 44.

Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Rafiki yangu, Bwana Kenzi almaarufu "mkereketwa❞ alihitaji tuonane uso kwa macho katika eneo la Shambahola siku mbili tatu zilizopita. Maadamu nilikuwa waya, sikuwa na budi ila kuhesabu hatua kuanzia kwangu hadi alipokuwa Kenzi. Si mtu hujikuna ajipatapo bwana!

Njiani walikuwapo wale ndugu zetu wanaoishi na ulemavu wakiwa katika hamsini zao za kuomba chochote kutoka kwa wapitanjia. Wengi wa wapitanjia waliwavalia miwani na kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa. Nilipowatazama, niliwahurumia na kuwasikitikia. Vitoto vyao je? Maskini, moja... mbili... tatu, mbavu hizo!

Nilifahamu kuwa sikuwa na chochote kwa hivyo, ili kuchelea kuunguzwa ndani kwa ndani, ilinipasa kukaza mwendo ili nisiwaone tena. Mara, nilikuwa nimewapa kisogo na kuyoyomea mbali. Moyoni nilijiambia kuwa iwapo Kenzi angenipa hela kidogo, ningepitia mahali pale ili angalau niwaachie kitu.

Baada ya kukinzana na misongamano ya watu na magari, nilijipenyeza hadi katika lango la Shambahola nikaichomoa rununu yangu kuukuu ili nimwarifu Kenzi kuwa nilikuwa nimetia guu. Naam, sifuri, saba, mbili, mbili.... mara shwa! Yarabi! Wewe.... mwizi... mshikeni! Kaniibia simu, mwi... Ikiwa umewahi kubeba maji kwa gunia, basi unafahamu ninachomaanisha. Kumbe mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi tu! Ama kweli, chambacho Kenzi, mjini ni shuleni.

Nilibaki nimejishika kichwa kwa mikono huku nikitweta si haba. Si lazima niandike kuwa nilikuwa nimenyong'onyea ungedhani konokono aliyenyunyiziwa chumvi. Ingawa ni muhimu sana kuyapokea yajayo, iliniwia vigumu kukabiliana na hali hiyo kwa muda huo. Nilihisi nimenyanyaswa na kuonewa pakubwa.

Haidhuru, nilipoingia Shambahola, sikuwa na jingine ila kuangazaangaza macho huku na kule kama pengine ningeangukiwa na nyota ya jaha kumwona Kenzi. Baada ya kuzurura kwa muda, nilimwona jamaa kwa mbali akinipungia mikono. Nilifurahi sana kumwona, Mbio, nilimwelekea ili nimsimulie yaliyojiri.

Nilipomaliza kumweleza yote, alicheka na kutingishika nusuru ya meno yake yaanguke kama si kule kuyashikilia kwa kiganja. Ala! Kwani nini kilichochekesha badala ya kusikitisha? Alicheka nini hasa? Baadaye alinieleza kuwa hiyo ilikuwa desturi kwa wageni mjini. Aliendelea kunifahamisha kuwa shababi huyo aliyenipokonya simu alikuwa mmoja wa wale "walemavu" .... ah

  1. Uhusiano baina ya Kenzi na msimulizi ni kwamba 
    1. walikuwa ndugu wa toka nitoke.
    2. kulikuwa na urafiki mkuu kati yao. 
    3. walikuwa wafanyakazi huko Shambahola.
    4. kulikuwa na uhasama mkuu baina yao.
  2. "...nilikuwa waya..." ni
    1. nahau inayomaanisha kuwa msimulizi hakuwa na pesa.
    2. istiara inayomaanisha kuwa msimulizi alikuwa mwembamba.
    3. msemo wenye maana kuwa ilibidi msemaji kuchukua hatua aliyoichukua.
    4. sitiara inayomaanisha kuwa msimulizi alikuwa mchovu.
  3. Msemaji alisafiri vipi hadi Shambahola? Kwa
    1. matwana.
    2. bodaboda.
    3. matatu.
    4. miguu.
  4. Kulingana na aya ya pili,
    1. wapitanjia hawakuwajali wale waliokuwa wakiomba.
    2. msemaji aliwahurumia bila kuwasikitikia wale ombaomba. 
    3. baadhi ya wapitanjia walikuwa katika hali ya ulevi.
    4. msimulizi wetu aliwahurumia na kuwasikitikia watoto wale.
  5. Dondoo "moja... mbili... tatu, mbavu hizo! inatoa dhana gani?
    1. Mbavu za watoto wale ziliweza kuhesabika.
    2. Afya ya watoto wale iliyumba.
    3. Familia za ombaomba wale zilikuwa katika afya mbaya.
    4. Watoto wale walidhoofika kupindukia.
  6. Mwishoni mwa aya ya tatu mna dhan kuwa
    1. gae huwa chombo wakatiwe.
    2. ndo ndo ndo hujaza ndoo.
    3. kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.
    4. ukiona vyaelea jua vimeundwa.
  7. Chagua kauli iliyo ya kweli kulingana na ufahamu.
    1. Lengo kuu la msimulizi kutoa simu ilikuwa kumwarifu Kenzi mjo wake.
    2. Rununu ya msimulizi haikuwa ndogo.
    3. Wazalendo walimsaidia msemaji katika kumkamata mkwepuzi yule.
    4. Watu wa Shambahola hujalishwa na matatizo ya wenzao.
  8. Ni hali gani iliyomwia vigumu mwandishi kukubaliana nayo? Hali ya
    1. kuyapokea yajayo.
    2. uchovu, wasiwasi na sintofahamu.
    3. kutafakari dhuluma aliyotendewa.
    4. kumsimulia Kenzi kisa kilichomkabili.
  9. ".... alicheka na kutingishika nusura meno yake yaanguke...."
    1. ni fani tu ya lugha ya kutilia chumvi.
    2. inamaanisha kuwa Kenzi alibahatika kwa kuwa meno yake yangeanguka.
    3. inatoa dhana kuwa kisa cha msemaji kilikuwa cha kuchekesha.
    4. ni mojawapo ya njia za kujieleza ueleweke vyema.
  10. "Walemavu"
    1. walihitaji kuonewa huruma.
    2. walikuwa sawa na chui ndani ya ngozi ya kondoo.
    3. walikuwa sawa na kuku mgeni asiyekosa kamba mguuni.
    4. waliwaibia watu simu, hasa wageni mjini.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 hadi 50.

Wakazi wa mitaa ya mabanda huogelea katika bahari kubwa sana ya changamoto. Baadhi ya changamoto zinazowakabili ni zile ambazo kwa yakini, wana uwezo wa kuzisitisha. Hata hivyo zipo nyingine ambazo kwa kweli juhudi za kuzisitisha zipo nje ya uwezo wao.

Mojawapo kati ya masaibu tumbi akidi yanayowatafuna ni hali duni ya usafi. Mingi ya mitaa hii hujulikana na kutambulika katika udororaji wa viwango vya usafi humo mitaani mwao. Si siri kuwa mitaa mingi ya mabanda haina misala, hivyo, huwalazimu wenyeji kutimizia haja zao kokote, hata vyumbani mwao! Ajabu iliyoje? Haya ni baadhi ya masaibu ya vitongoji duni.

Tatizo jingine ni la ukosefu wa usalama miongoni mwa wakazi wa mitaa husika. Wananchi wengi huamini na kusadiki kuwa baadhi ya wezi na majambazi sugu ambao majina yao hugonga vichwa vya habari kila wakati huishi mumo humo mitaani mwa mabanda. Utovu huu wa usalama umekithiri kiasi cha wakazi kuishi maisha ya roho mikononi. Dua za wakazi hawa daima huwa, "Nakuche tukushukuru, ewe Manani...."

Si suala la mjadala 'uwa asilimia kubwa sana vya watoto humo mitaani haitazamiki kwa mara ya pili. Si lolote, si chochote, vimbaumbau hasa! Ni nani atajali ilhali wazazi wao hupata wajaliwalo tu na wala si watakalo? Msamiati kama sodo kwa vitoto vya kike vilivyovunja ungo humo mitaani huwa ndoto. Si ajabu kurekodi kuwa kuishi huku gizani kwa wasichana hao maskini ndiko chimbuko hasa la ongezeko la visa vya utungwaji mimba mapema.

Ni jambo la kutia simanzi sana kuona kuwa katika mitaa mingi ya mabanda, viwango vya elimu viko chini sana ikilinganishwa na maeneo mengine ya nchi. Hali hii huchangiwa na kuwa wazazi wengi humo hawana ajira za kutajika. Ni zile familia za "bora mate tumboni". Ndiyo, upo mpango wa elimu ya dezo katika shule za umma nchini. Swali ni: ikiwa ni pesa za kujipatia angalau kibaba cha unga ili kuokoa majahazi ya familia yanayozama ni kizungumkuti, seuze hiyo koto?.... Sare je?

  1. Mitaa ya mabanda ni sawa na 
    1. maeneo ya umaskini.
    2. majumba mabovu mabovu. 
    3. vitongoji duni.
    4. vijiji vinavyohangaika.
  2. Ni neno lipi halina maana sawa na kuzisitisha?
    1. Kuzikomesha.
    2. Kuzitamatisha.
    3. Kuzihitimisha.
    4. Kuzikatiza.
  3. Ni kitambulisho gani huweza kutumiwa kuijulia mitaa ya mabanda?
    1. Hali duni ya usafi.
    2. Usafi uliokithiri.
    3. Uchafu wa wakazi.
    4. Usafi wa mazingira.
  4. Chagua kisawe cha neno misala kulingana na habari.
    1. Choo.
    2. Mkeka.
    3. Mikeka.
    4. Vyoo.
  5. Kutokana na uhaba wa usalama miongoni mwa wakazi wa mitaa ya mabanda, wenyeji huishi
    1. katika hali ya sintofahamu.
    2. katika hali ya woga mwingi.
    3. wakiwa na wasiwasi mwingi.
    4. maisha ya ajabu sana.
  6. "...asilimia kubwa sana ya watoto humo mitaani haitazamiki kwa mara ya pili...." kwa sababu
    1. wanakera na kukirihi.
    2. wanatia aibu kwa mtazamaji.
    3. wanahuzunisha pakubwa.
    4. wao hulialia kila mara.
  7. Wakazi wengi wa mitaa ya mabanda ni
    1. walalahai.
    2. walalahoi.
    3. walalaheri.
    4. walanguzi.
  8. Mimba za mapema kwa wasichana humo mitaani huchangiwa na
    1. wasichana husika kutoielewa miili yao vyema.
    2. wasichana hao kutofahamu matumizi ya sodo.
    3. watoto hao wa kike kushiriki ngono kiholela.
    4. watoto hao wa kike kutojua namna ya kutumia sodo.
  9. Suala la viwango vya elimu kuwa duni humo mitaani mwa mabanda
    1. linafurahisha.
    2. linasumbua.
    3. linahamasisha.
    4. linahuzunisha.
  10. Wazazi huenda wasimudu karo na sare kwa kuwa
    1. pesa zao zatosha chakula tu.
    2. pesa zao zatosha sare tu.
    3. hawana pesa za kutosha.
    4. hawana pesa.

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Kamilisha insha ifuatayo kwa maneno yako mwenyewe na uifanye iwe ya kusisimua.

Si rahisi kuyasahau yaliyonikumba katika msitu wa Ngomeni. Awali, wazazi wangu walikuwa wamenikanya dhidi ya kwenda humo msituni, nami nikatia komango masikioni. Asubuhi hiyo,.............................................................................................................

MARKING SCHEME

  1. C
  2. D
  3. B
  4. D
  5. A
  6. B
  7. A
  8. A
  9. A
  10. A
  11. C
  12. C
  13. C
  14. B
  15. D
  16. D
  17. D
  18. B
  19. A
  20. B
  21. C
  22. D
  23. C
  24. D
  25. B
  26. A
  27. C
  28. B
  29. A
  30. D
  31. B
  32. A
  33. D
  34. A
  35. B
  36. C
  37. A
  38. C
  39. A
  40. B
  41. C
  42. C
  43. A
  44. D
  45. C
  46. C
  47. B
  48. A
  49. D
  50. C

Swali la 1 hadi la 5

Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali:

GRADE6KISWAHILISET1ET22023Q1

Kaka Mbweha: (Akicheka kwa kejeli) Bi. Ngiri, mkulima hodari wa mihogo anayeheshimika katika kanda ki, hujambo?

Bi. Ngiri: (Akihema kwa uchovu, mzigo alio nao kichwani unaonekana kumlemea) Sijambo, lakini nina swali. Unacheka nini? Ama ndio njia yako ya kumfariji anayetaka kuchanika kwenye mpini siku nzima?

Kaka Mbweha: (Anacheka zaidi) Ati kuchanika kwenye mpini? Wachapa kazi kama mimi hawana haja ya kujichosha. Wanafanya kazi kwa kutumia akili.

Bi. Ngiri: (Kwa dharau) Mhhh! Heri nyinyi mabingwa wa kutumia akili. Sisi wengine inabidi tujikaze kisabuni ili tupate riziki.

Kaka Mbweha: (Akionyesha kushangaa) Nyinyi wengine! Wewe na kina nani? Je, huna habari kwamba rafikiyo Sungura hapandi wala kuvuna lakini daima ana shibe?

Bi. Ngiri: (Kwa sauti ya chini) Hayo ya Sungura hayanihusu ndewe wala sikio. Isitoshe, unavyoona nimechoka. Shamba langu la mihogo liko umbali wa kilomita kumi na tano kutoka kwangu. Bado nina mlima mmoja wa kukwea ndipo nifike. Kaka Mbweha: Haya basi niazime vipande viwili vya mihogo. Nitarejesha nitakapovuna.

Bi. Ngiri: Kaka Mbweha, umesahau kuwa tayari una deni langu la mihogo? Lipa hilo kwanza.

Kaka Mbweha: (Kwa unyenyekevu) Nitalipa tu.

Bi. Ngiri: Utanilipa mihogo ilhali hukuvuna? Unastahili kufanya kazi kwa bidii. Kumbuka ajizi ni nyumba ya njaa.

  1. Bi. Ngiri anasifika kwa sababu gani?
    A. Bidii
    B. Ukulima
    D. Urafiki
  2. Wachapa kazi kama mimi hawana haja ya kujichosha.' Kauli hii inaonyesha tabia gani ya Kaka Mbweha?
    1. Yeye ni mvivu
    2. Ana jitihada kazini
    3. Ana akili
    4. Ana ukarimu
  3. Maneno, 'Tujikaze kisabuni yametumika katika mazungumzo. Ni tamathali gani ya lugha?
    1. Kitendawili
    2. Methali
    3. Nahu
    4. Tashbihi
  4. Wahusika katika mazungumzo haya ni _____
    1. watu
    2. Mifugo
    3. wanyamapori
    4. ndege
  5. Kisawe cha neno kukwea kwa mujibu wa kifungu hiki ni nini?
    1. Kupanda
    2. Kushuka
    3. Kuteremka
    4. Kupumzika

Swali la 6 hadi la 9

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
                                                                   GRADE6KISWAHILISET1ET22023Q6

Siku moja mimi na sahibu yangu Dan tulikuwa tukipalilia mimea kwenye mradi wetu shuleni, Tulipiga gumzo huku tukiipinda migongo yetu. Ghafla bin vuu, sahibu yangu Dan alipasua ukemi. Alikuwa amejidunga kwenye mguu wake wa kulia! Bila kupoteza muda, nilikimbia hadi kwenye ofisi ya mwalimu wa zamu na kumuarifu kilichokuwa kimetokea. Bi Okero, aliyekuwa mwalimu wa zamu alichukua hatua mara moja. Aliwaita maskauti wapatao watatu tukaandamana nao.

Tulipofika alipokuwa ameketi Dan, Bi Okero aliwaelekeza maskauti jinsi ya kumpatia majeruhi huduma ya kwanza. Walichukua kitambaa safi na kufunga jeraha. Damu ilipokoma kutoka waliosha lile eneo kwa maji safi yaliyotiwa chumvi. Kisha walifunga kidonda bandeji na kumpeleka Dan kwenye zahanati iliyokuwa karibu. Tangu siku hiyo niliamua kujiunga na chama cha maskauti.

  1. Dan alikuwa akifanya nini alipoumia?
    1. Akifyeka
    2. Akinyunyizia mimea maji
    3. Akiondoa magugu shambani kwa jembe
    4. Akikata matawi ya mimea
  2. Je, ni nini kisichoonyesha kwamba Bi Okero anawajibika?
    1. Alikuwa katika zamu.
    2. Alichukua hatua mara moja.
    3. Aliwaelekeza maskauti kumpa majeruhi huduma ya kwanza.
    4. Alijiunga na chama cha maskauti.
  3. Kisawe cha zahanati ni nini?
    1. Hospitali
    2. Kliniki
    3. Dispensari
    4. Wadi
  4. Bi Okero aliwaelekeza maskauti jinsi ya kumpatia majeruhi huduma ya kwanza.' Je, majeruhi ni nani?
    1. Mgonjwa mahututi
    2. Mtu aliyejeruhiwa
    3. Mtu aliyepata nafuu
    4. Kiongozi wa maskauti

Swali la 10 hadi la 12

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
                                           GRADE6KISWAHILISET1ET22023Q10

Baraka alikuwa kiongozi wa kijiji cha Mwanga. Kiongozi huyu alijulikana kwa ushauri wake kwa wanakijiji. Ushauri huu ulilenga zaidi njia bora za kuwekeza. Aliwapenda wanakijiji wake nao wakampenda kwa sababu ya uongozi wake mzuri.

Baraka na wanakijiji walifanya mikutano mara kwa mara. Katika mikutano hii walijadili njia mbalimbali za kuendeleza miradi katika kijiji chao.Umuhimu wa elimu ulisisitizwa. Kwa hivyo, wazazi na walezi waliwapeleka watoto wao shuleni bila kulazimishwa. Walitambua kuwa elimu inaleta heri maishani.

Wakulima walipewa mafunzo kuhusu kilimo bora. Walifundishwa kuhusu kilimo biashara. Walifundishwa kuhusu umuhimu wa kupanda mbegu zinazofaa kwa kila msimu. Waliwekeza katika kilimo wakapata mavuno tele. Wanakijiji walipata chakula cha kutosha. Mavuno ya ziada yaliuzwa. Wanakijiji hawa walipata faida kubwa. Kutokana na pesa walizopata waliendeleza kilimo. Isitoshe, walianzisha miradi ya ufugaji kuku, nyuki na
sungura.

Wafanyabiashara nao walipata maarifa ya kuboresha biashara zao. Walianzisha vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana pesa. Biashara zao zikaimarika.

Sifa za kijiji cha Mwanga zilienea kote. Wageni kutoka vijiji jirani walikuja kujifunza jinsi ya kujiendeleza. Baraka na wanakijiji waliwapokea na kuwapa maarifa ya kuwekeza.

  1. Baraka alijulikana sana kwa sababu gani?
    1. Uwekezaji
    2. Upendo
    3. Mawaidha
    4. Uongozi
  2. Kwa nini wazazi waliwapeleka watoto wao shuleni?
    1. Umuhimu wa elimu ulisisitizwa katika mikutano
    2. Walilazimishwa na Baraka
    3. Walianzisha miradi
    4. Watoto walijipeleka
  3. Wafanyabiashara walianzisha vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana pesa.' Neno akiba lina maana gani?
    1. Pesa za ziada anazopata mtu baada ya kuuza kitu.
    2. Pesa anazochukua mtu kutoka kwa mwingine ili alipe baadaye.
    3. Pesa anazopata mtu baada ya kufanya biashara.
    4. Pesa zinazowekwa kwa sababu ya matumizi ya baadaye.

Swali la 13 hadi la 15

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

                                                  GRADE6KISWAHILISET1ET22023Q13

Ng'ombe ni mnyama ambaye anafugwa na binadamu. Mnyama huyu ana manufaa tele kwetu. Kwanza kabisa, huchinjwa ili tupate nyama. Ngozi yake hutumiwa kutengeneza bidhaa kama vile viatu na kanda zinazofungwa viunoni.

Ng'ombe jike hutupatia maziwa. Tunayatumia maziwa kupikia chai na pia kuyanywa. Jibini, ambacho ni chakula kitamu kwetu, hutengenezwa kutokana na maziwa yayo hayo. Mbali na nyama, ngozi na maziwa, Ng'ombe pia huuzwa. Fedha zinazotokana na mauzo hayo huweza kutumika kutimiza mahitaji mbalimbali. Fahali nao huenda wakatumika kulima mashambani. Isitoshe, tunaipata samadi kutoka kwa Ng'ombe. Samadi huweza kutumiwa kama mbolea.

  1. Ni manufaa mangapi ya ng'ombe yaliyotajwa katika kifungu hiki?
    1. Saba
    2. Sita
    3. Kumi
    4. Matano
  2. Kulingana na kifungu hiki ni ng'ombe yupi hutumiwa kulima?
    1. Wa kike
    2. Wa kiume
    3. Ndama
    4. Wa kike na wa kiume
  3. Kati ya vitu hivi ni gani hatupati kutoka kwa ng'ombe wa kiume?
    1. Samadi
    2. Nyama
    3. Ngozi
    4. Maziwa

Swali la 16 hadi la 20

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 mpaka 20. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Timu ya Bingwa ilishinda mechi ya fainali. Ushindi ___16__ ulitokana na ushirikiano au __17___  waokatika mazoezi. Wachezaji wote walikuwa wenye bidii ___18__ mchwa. Baada ya mechi, wachezaji waliondoka uwanjani wakishangiliwa  na ___19___ Timu pinzani ___20__ wao katika kwamba imepoteza mechi hiyo.

   A
 16  yao  wao   kwao  mwao 
 17  utaratibu  utengano  umoja   uzalendo 
 18  kama kama vile   kwa sababu   kuliko
 19  refa  golikipa   walinzi   mashabiki 
 20  haijaamini haitaamini   haiamini   haikuamini 

 

Swali la 21 hadi la 30

Chagua jibu sahihi.

  1. Chagua sentensi ambayo ina maneno yenye silabi tatanishi.
    1. Uga ule umenyunyiziwa unga wa chokaa.
    2. Sisi tunapenda kwenda pwani likizoni.
    3. Jungu alilopikia nyama juzi limesafishwa.
    4. Wale wamechuma maua na kuyauza mbali.
  2. Zifuatazo ni jozi za maneno. Ni jozi gani iliyo na vimilikishi?
    1. Huyu, yule
    2. Changu, lake
    3. Tatu, tele
    4. Bora, hodari.
  3. Chagua neno ambalo linapatikana katika ngeli ya U - I:
    1. Mkebe
    2. Mtoto
    3. Unywele
    4. Meza
  4. Katika kamusi, maneno hupangwa kulingana na herufi za alfabeti. Kati ya Maneno haya ni gani litakuja mwanzo?
    1. Gonga
    2. Ganda
    3. Gamba
    4.  Godoro
  5. Kati ya sentensi hizi, ni gani haina kiwakilishi?
    1. Mimi huenda shuleni kila siku.
    2. Huyu anasoma kwa bidi.
    3. Watano watapewa zawadi.
    4. Viatu vitatu vimeoshwa.
  6. Andika sentensi ifuatayo katika wingi. Wavu wa mvuvi unastahili kuwa na shimo kubwa.
    1. Nyavu za mvuvi zinastahili kuwa na shimo kubwa.
    2. Wavu wa wavuvi unastahili kuwa na mashimo makubwa.
    3. Nyavu za wavuvi zinastahili kuwa na shimo kubwa.
    4. Nyavu za wavuvi zinastahili kuwa na mashimo makubwa.
  7. Kanusha sentensi ifuatayo: Maseremala watatutengenezea madawati.
    1. Maseremala hawatatutengenezea madawati.
    2. Maseremala hawajatutengenezea madawati.
    3. Maseremala hawakututengenezea madawati.
    4. Maseremala hawatutengenezei madawati.
  8. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa. Mlango ulipakwa rangi ukapendeza.
    1. Malango yalipakwa rangi yakapendeza.
    2. Kilango kilipakwa rangi kikapendeza.
    3. Lango lilipakwa rangi likapendeza.
    4. Milango ilipakwa rangi ikapendeza.
  9. Umesimuliwa hadithi na mlezi wako. Sasa ni wakati wa kulala. Chagua maagano utakayotumia kumuaga mlezi wako.
    1. Kwaheri
    2. Alamsiki
    3. Buriani
    4. Safiri salama
  10. Chagua methali isiyohusu malezi.
    1. Mtaka cha mvunguni sharti ainame
    2. Mtoto akibebwa hutazama kisogo cha nina.
    3. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
    4. Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu

INSHA

Andika insha kuhusu:

Barua rasmi kwa mwalimu anayesimamia chama cha mazingira ukimwomba nafasi ya kujiunga na chama hicho.

MARKING SCHEME

  1. B
  2. A
  3. C
  4. C
  5. A
  6. C
  7. D
  8. C
  9. B
  10. C
  11. A
  12. D
  13. B
  14. B
  15. D
  16. B
  17. C
  18. A
  19. D
  20. A
  21. A
  22. B
  23. A
  24. C
  25. D
  26. D
  27. A
  28. C
  29. B
  30. A

 

 

 

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi, chagua jibu sahihi kati ya yale manne uliyopewa.

    Yena__1___kofia aina ya__2___kichwani: Jasho lilikuwa likimtiririka tiriri kwa kuwa kulikuwa na joto__4___mno. Alimwangalia__5___ yake na kushindwa la kufanya. Ajali hiyo ilimwacha mwenzake bila___6__ mmoja. Alipoona watu walimtania na kumbandika jina "kikono." Kutoka siku aliyoipata ajali, rafiki_____ Yona hakuendesha pikipiki tena. Alipowaona vijana wakiendesha pikipiki kwa__8___ aliwaonea__9___ na alipopata nafasi, aliwashauri kuwa haraka haraka haina baraka.

   A B C
 1  alivaa   alifua   alivua   alifaa 
 2  kikuba   kikoi   joho   chepeo 
 3  pake   mwake   yake   kwake 
 4  nyingi   jingi   mingi   kingi 
 5  sahibu   mwendani   hasimu   msena
 6  mwili   mguu   sikio   mkono 
 7     ya       wa    la    cha
 8  mbio   haraka   polepole   kasi
 9  mayo   wivu   huruma   kinyama

 

   Kiongozi___10___alizifuja pesa____11__ za umma na kujenga___12____kubwa ambacho kiliuzwa vinywaji vya aina mbalimbali.__13___ walikasirika na kugoma. Aliliwa___14__ na kupelekwa___15___ ambako alikaa kwa saa kumi. Siku iliyofuata alipelekwa mahakamani.

   A  C  D
 10  shupavu  mihiri   katili   mwadilifu
 11  lote  wote   yote   zote 
 12  baa  mkahawa   klabu   hoteli 
 13  Waliomwajiri  Waliomchagua   Waliochaguliwa   Aliowapenda 
 14  mbaroni  pengu   shime   ufunguo 
 15  kortini  jalani  rumande  korokoroni

 

Kutoka nambari 16 hadi 30, chagua jibu lililo sahihi kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Chagua wingi wa;
    Uwanja wangu una nyasi ndefu.
    1. Nyanja zangu zina nyasi ndefu.
    2. Nyanja zetu zina nyasi ndefu.
    3. Uwanja wetu una nyasi ndefu.
    4. Uwanja wetu una unyasi mrefu.
  2. Chagua jina ambalo ni tofauti na mengine.
    1. Nasaba
    2. Jamaa
    3. Mbari
    4. Nikahi
  3. Uadilifu, wema, ubora ni aina gani ya nomino?
    1. Nomino za wingi
    2. Nomino za dhahania
    3. Nomino za makundi
    4. Nomino za kuhesabika
  4. Chagua kielezi ambacho hakijaambatanishwa vyema na aina yake.
    1. Mwakani - wakati
    2. Haraka - namna
    3. Kidogo - jinsi
    4. Mara mbili - idadi
  5. Je, jina mede huwa katika ngeli gani?
    1. I-ZI
    2. U-YA
    3. A-WA.
    4. I-I
  6. Mimi ni kifaa cha mkulima. Kazi yangu ni kutandaza mchanga au mbolea. Wakati mwingine mimi hukusanya takataka. Mimi ni nani?
    1. Beleshi
    2. Reki
    3. Jembe
    4. Mundu
  7. Kamilisha takanali hii ya sauti. Yeye alifunga mzigo wake
    1. mwaa
    2. nga
    3. ji
    4. ndi
  8. Tambua umbo hiii.
    C8KISWAHILIMT2S52023Q37

    1. Mistari sulub
    2. Mistari sambamba
    3. Mistari mshazari
    4. Mitari butu
  9. Ni sentensi gani inayoonyesha majuto?
    1. Ningalifanya bidii ningalifaulu maishani
    2. Ningekuwa na hela ningenunua kalamu
    3. Nisingefuata ushauri wake nisingefaulu
    4. Nikifuata mawaidha nitafua dafu maishani
  10. Ugonjwa unaofanya mgonjwa kukoja damu huitwaje?
    1. Kaswende
    2. Upele
    3. Safura
    4. Kichocho
  11. Tegua kitendawili hiki:
    Chaenda mbali lakini hakiondoki.
    1. macho
    2. jua
    3. njia
    4. mto
  12. Ni mdudu yupi ambaye hafyonzi damu?
    1. Bunzi
    2. Kiroboto
    3. Chawa
    4. Mbu
  13. Ni sentensi gani inaonyesha ngeli ya KU-KU?
    1. Chumbani inle mlikuwa na kukurukakara
    2. Kule jehanamu kutakuwa na mateso tele
    3. Shuleni petu kuna madaraka mengi sana
    4. Kucheza kwake kuliwafurahisha mashabiki
  14. Ng'ombe hurarama lakini chui
    1. huluza
    2. huvuma
    3. hunguruma
    4. hukorokocha
  15. Neno dunia lina sauti ngapi?
    1. Tano
    2. Tatu
    3. Mbili
    4. Nne

Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali 31 hadi 40.

Vitabu vyote vitakatifu vinatufunza tuwe waaminifu na tusithubutu kamwe kuzungumza uongo kwani mambo ya uongo hayadumu. Nadhani ni kwa sababu hii wahenga wakaeleza kuwa njia ya mwongo ni fupi. Mzee siambiwi alitanabahi kuwa uongo haufai baada ya kuona mambo yamemzonga kama chafu anavyomzonga mbuzi.

Kijiji cha Maganya kiliangukiwa na nyota ya jaha kubwa baada ya wafadhili kujenga chuo cha mafunzo ya watoto yatima na shule. Kila mtu aliyekuwa na watoto yatima alitakiwa kwenda kuwasajili chuoni. Hapo wangesomeshwa mafunzo ya kawaida pamoja na kufunzwa taaluma za ufundi wa kila fani. Kulikuwa na kazi za uashi. Uhadisi, taaluma ya tarakilishi mingoni mwa kazi nyingine. Nafasi zilikuwa wazi kwa mtoto yeyote nchini muradi awe yatima na kufiwa na mzazi mmoja au wote wawili. Vilevile kulikuwa na sehemu ya walemavu wa aina zote katika chuo hicho. Hawa nao walikuwa na rabiba yao ya masomo kulingana na uwezo waliokuwa nao.

Mzee Siambiwi, aliyekuwa mtu bahili na mwenye kupenda kuyakwepa majukumu yake ya malezi alipiga bango vile angefaidika kwa fursa hiyo. Siku moja asubuhi Siambiwi alimwita mkewe na kumketisha kitako. "Sharti nimpeleke kitindamimba wetu nasari ya yatima." Siambiwi alimwambia mkewe huku macho ameyatoa ungedhani ni ya bundi.

Mkewe alikiona hicho kama kioja kikubwa kwani wote walikuwa hawajakata kamba, isitoshe mumewe alijiweza kifedha. Ubishi mkubwa ulizuka. Mzee Siambiwi alisisitiza kuwa kutompeleka mwanawe . asome hapo bure ni sawa na mtu mpumbavu ambaye huacha jua lichomoze ashindwe kuliota kisha alitafute waka wa jioni.

Majadiliano yakakomea hapo kama sentensi iliyowekwa kikomo. Majonzi hayo yalimchoma sana mama inoyoni hadi akapata maradhi ya shinikizo la damu yaliyompeleka jongomeo, bila nauli wala matwana. Asubuhi ya majogoo Mzee Siambiwi na mkembe wake mikononi alikuwa kwenye lango la nasuri ya yatima. Alipokelewa kwa heshima kubwa na bawabu na kuelekezwa alikostahili kwenda huko alimwandikisha mtoto kwa mwalimu mkuu kuwa yeye alimwokota njiani na hivyo ni msamaria mwema. Mtoto alipokelewa na kupewa yaya wa watoto wadogo.
Miaka ilipeperuka ungedhani imepachikwa mbawa. Kitimtim alikua na kuwa mkubwa. Inasomekana alikuwa na bongo la sumaku. Aliongoza kwenye mitihani yake yote hadi akaingia chuo kikuu. Huko alifuzu na kupata kazi ya uhandisi. Alikuwa mhandisi mkuu nchini. Siambiwi wakati huo pesa zilikuwa zimemwishia na kubaki maskini hohehahe.

Siku moja alifunga safari kwenda jijini kumtafuta mwanawe ili akamwombe usaidizi na pia amweleze kuwa yeye ni mzazi wake. Kitimtim alishangaa kukiona kizee kilichodai kuwa mzazi wake kikimlilia machozi kupukupu. Alifahamu tangu utotoni mwake kuwa yatima. Siambiwi alidinda kutoka ofisini na ikabidi polisi waitwe kumtoa nje. Alimshika koti mwanawe na kukatalia kumwachia. Palizuka kizaazaa patashika. Uchunguzi wa kitaalamu wa hospitali na ushahidi ulitolewa. Mzee Siambiwi akawa na bahati kama mtende.

  1. Kulingana na aya ya kwanza ni bayana kuwa
    1. njia ya mwongo huwa ndefu
    2. uongo humletea mtu mambo
    3. mbuzi huzongwa kwa uongo wake
    4. kuna vitabu ambavyo huenzi uongo
  2. Bahati iliyowapata wanakijiji ni gani?
    1. Waliangukiwa na nyota za angani
    2. Walifundishiwa watoto bure bilashi
    3. Walijengewa vyuo vya ufundi
    4. Walipata watu wakusaidia viokote
  3. Waliofaa kujiandikisha chuoni
    1. walikuwa wamepewa barua za mwaliko
    2. walikuwa na watoto wengi
    3. walihitaji msaada wa wafadhili
    4. walitaka kupewa elimu nzuri
  4. Neno jingine lenye maana sawa na uhandisi ni
    1. uinjinia
    2. uhesi
    3. uhasibu
    4. usanii
  5. Chuo hiki cha ufadhili hakikubagua kwa kuwa
    1. kiliwaalika watoto wote wa kijiji
    2. kiliwapa wazazi wote nafasi sawa
    3. kiliwasaidia mayatima na walemavu
    4. kiliwapa mafunzo ya aina mbalimbali
  6. Unafikiri ni kwa nini ratiba nyingine huwa na tofauti?
    1. Vyuo hufunza kozi tofauti
    2. Uwezo wa wanafunzi hutofautiana
    3. Huwa mayatima na wengine wamelemaa
    4. Ulezi wa watoto wote si sawa
  7. Mkewe Siambiwi alienda jongomeo kwa kuwa
    1. mumewe alitaka aoge
    2. mwanawe alienda shule ya yatima
    3. aliugua ugonjwa uliomweza
    4. alilipa nauli ya kwenda jongomeo
  8. Siambiwi ni jina linalolingana na tabia ya mzee huyu. Mbinu hii huitwaje?
    1. Majuzi
    2. Lakabu
    3. Kupanga
    4. Somo
  9. Kitimtim alikuwa mtoto mwerevu kwa kuwa
    1. alimkana babaye ambaye alimtekeleza
    2. alipewa kazi pamoja na ofisi kubwa
    3. alielewa mambo haraka na akawa fundi
    4. alimsaidia babaye na wanakijiji pia
  10. Kulingana na kifungu hiki ni kweli kusema kuwa
    1. Kitimtim alihitaji kusaidiwa ili asome
    2. mamaye Kitimtim alikuwa na pesa nyingi
    3. chuo hicho kilijua Kitimtim ana wazazi
    4. Babaye Kitimtim alikuwa mtu mchoyo sana

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 41 hadi 50

Je, umewahi kutafakari kuhusu namna wanafunzi wengi, ukiwemo miongoni mwao, wanavyosafiri kwenda shuleni? Yumkini jibu lako kwa swali hili litadhihirisha kwamba asilimia kubwa hutembea kwenda shuleni, wengine hutumia baiskeli, magari ya umma na ya kibinafsi, pikipiki na gari mosi. Bila shaka aina ya usafiri hutofautiana kulingana na uwezo wa kiuchumi na umbali baina ya mwanafunzi na shule yake.

Kila aina ya usafiri ina changamoto maalum. Mathalani ikiwa umezungumza na wenzako ambao hutembea kwenda shuleni, haikosi wamekueleza dhiki wanazokumbana nazo. Licha ya safari za aina hii kuwachosha wanafunzi, ni wazi kuwa wanafunzi wengine hata hukosa masomo kwa sababu ya kutopitika kwa njia wakati wa mvua nyingi.

Pengine hata wewe umewahi kujipata katika njia panda baada ya daraja unalovukia kusombwa na maji ya mto uliofurika. Isitoshe, watembeao huweza kuathirika kiafya wakati wa kipupwe. Baridi huweza kuwasababishia pumu au hata kichomi. Wengine huwa katika hatari ya kuteleza kwenye njia zenye matope na kuvunjika viungo vya mwili. Hawa pia wamo katika hatari zaidi ya kutekwa nyara na hata kunyanyaswa kimapenzi.

Wanafunzi wengine huwahusudu wale ambao husafiri shuleni, ama kweli gari la sule, au la kibinafsi. Wakiulizwa kuhusu kiini cha husuda hii, wanasema kwamba wenzao hawa hawachoki kwani magari haya yanawachukua kutoka mlangoni mwa nyumba zao. Hata hivyo ukichunguza vyema utapata kwamba hata hawa wana matatizo sugu. Kwa vile magari ya shule huwabeba wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali, magari haya hayana budi kuanza safari mapema. Hii huwalazimu wanafunzi nao kuamka alfajiri na mapema ili kuyawahi magari haya. Matokeo ni kwamba wanafunzi wengi hawadiriki kulala usingizi wa kutosha. Kuna wale ambao hulala saa nne usiku baada ya kukamilisha kazi za darasani, kisha wanaraushwa saa kumi ili kijitayarisha basi la sa kumi na moja. Wanafunzi wa aina hii hukumbwa na uchovu, na bila shaka husinzia darasani.
Isitoshe, wanafunzi wanaotumia usafiri wa umma hulalamikia msongamano wa magari ambao unawafanya kukawia njiani, na hata kupewa adhabu kwa kuchelewa kufika shuleni. Wengine hata hukataliwa na magari ya abiria, eti wanalipa fedha kidogo na kuwasababishia wenye magari hasara. Wanafunzi hawa huaibika na kulazimika kutembea hadi shuleni. Hali kadhalika magari ya umma humpa mwanafunzii mazingira ya kujifunzia tabia mzuri na mbaya. Pamoja na wanafunzi hawa hupata fursa ya kutengamana na wenzao kutoka shule nyingine, wao pia huweza kuathiriwa vibaya na hulka za wasafiri wengine. Kuna wale ambao huiga lugha, mitindo ya mavazi, namna ya kutembea na hata mienendo mingine ya madereva na utingo. Wengine huishia kuwa waraibu sugu wa vileo kutokana na vielezo wanavyopata kwenye magari haya. Muziki, picha na video na mazungumzo kupitia vyombo vya habari vilivyo kwenye magari haya huchangia kuzorotesha tabia ya wanafunzi. Hii ni kwa sababu baadhi ya maswala yanayozungumziwa ni ya aibu na hayapaswi kusikilizwa na watu wa umri mbichi.

Nihahiri kwamba kila aina ya usafiri ina athari zake. Hata hivyo, baniani mbaya kiatu chake dawa. Usafiri unaitajika katika kufanikisha masomo ya wanafunzi na katika uchukuzi wa bidhaa na vifaa mbalimbali ambavyo wanahitaji shuleni. Ni jukumu la kila mwanajamii kuhakikisha kwamba mikakati ifaayo imewekwa ili kukinga dhidi ya madhara yanayoandahana na kila aina ya usafiri. Wanafunzi nao wakae ange kutambua watu ambao huenda wakatosa katika maovu. Wachujo ya kuiga na ya kukataa.

  1. Ni bayana kuwa usafiri wa wanafunzi
    1. hauna changamoto nyingi
    2. huwa sawa kulingana na mwandishi
    3. huwa rahisi kwa wanaotembea
    4. hutegemea uchumi na umbali
  2. Kulingana na mwandishi ni wazi kuwa kila aina ya usafiri
    1. huwa na changamoto ambazo ni nzuri
    2. humtatiza mwanafunzi kwa njia fulani
    3. humtunza mwanafunzi na kumfanya bora
    4. huweza kumnoa mwanafunzi kimaadili
  3. Wanafunzi hasa wanaotembea huathirika vipi kulingana na kifungu hiki?
    1. Kutekwa nyara na kusikiliza nyimbo mbaya
    2. Kunyanyaswa kimapenzi na wanafunzi wenzao
    3. Kupatwa na magonjwa yanayolewa na baridi
    4. Kutazama runinga na kuvunjika viungo
  4. Ni nini maana ya huwahusudu kulingana na kifungu hiki?
    1. Huponda kwa sababu fulani
    2. Huhimizwa kwa sababu fulani
    3. Huchukia kwa hali fulani
    4. Huvuliwa na starehe fulani
  5. Kulingana na aya ya pili, mwanafunzi huchanganyikiwa iwapo
    1. njia ni mbili na hajui ya kupitia
    2. wachoka na kusombwa na maji
    3. njia anayotumia haipitiki hata kidogo
    4. kuna baridi kali na watekanyara
  6. Ni kauli gani sahihi kulinana na kifungu hiki?
    1. Wanafunzi huraushwa mapema ili wasichelewe .
    2. Wanafunzi wote wanazo changamoto zinzaofanana
    3. Wanafunzi wengi huchoka na hufeli mtihani
    4. Wanaosafiri kwa magari wana starehe sana
  7. Tabia za mwanafunzi zinaweza kuathiriwa na nini?
    1. Madereva wa magari ambao huwa wema
    2. Aina ya usafiri na wanaosoma nao
    3. Wasafiri na mitandao anayoitumia mwanafunzi
    4. Mazingira na watu anaotangamana nao
  8. Kuchelewa kwa mwanafunzi anayesafiri kwa magari ya umma husababishwa na nini?
    1. Madereva na utingo husukisha watu kila stani
    2. Kukaa sana njiani kwa sababu ya msongamano
    3. Kupewa adhabu ya kuchelewa na walimu shuleni
    4. Kukataa kuwabeba wanafunzi na kuwabeba abiria wengine
  9. Hata hivyo, baniani mbaya kiatu chake dawa. Kauli hii inamaanisha
    1. mtu ambaye huwa mbaya huwa mwema siku moja
    2. Usafiri ni mbaya lakini hutufanya watu wema
    3. Tunafaa kuenzi usafiri wa miguu tusipatwe na maafa
    4. Hata kitu kikiwa na madhara, kina umuhimu wake
  10. Kulingana na aya ya mwisho, mwandishi ana mtazamo upi?
    1. Jamii yote yafaa kuona madhara ya usafiri
    2. Tunafaa kuweka mikakati itakayotufaidi safarini
    3. Kusoma kutaimarika tukiimarisha usafiri wetu
    4. Wanafunzi wanafaa kujichagulia namna ya usafiri

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha yakusisimua isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa.

Wewe ni kiranja mkuu shuleni. Andika hotuba utakayotoa katika siku ya michezo shuleni........................

MARKING SCHEME

  1. C
  2. B
  3. A
  4. B
  5. A
  6. D
  7. A
  8. D
  9. C
  10. C
  11. D
  12. C
  13. A
  14. A
  15. C
  16. B
  17. D
  18. B
  19. C
  20. C
  21. B
  22. D
  23. B
  24. A
  25. D
  26. A
  27. A
  28. D
  29. A
  30. B
  31. B
  32. C
  33. A
  34. A
  35. C
  36. B
  37. C
  38. B
  39. C
  40. B
  41. D
  42. B
  43. C
  44. C
  45. C
  46. A
  47. D
  48. B
  49. D
  50. C

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.

Hali ngumu ya maisha ___1___ waja wengi humu nchini ___2___; yaani kupoteza matumaini. ___3___ ya waja hawa ___4___ hata kukimu mahitaji yao ya kimsingi; ___5___. Mambo ___6___ zaidi na uhaba wa nafasi za ajira___7___ idadi kubwa ya vijana___8___. Ipo haja ya ___9___ vijana wakumbatie kazi za ufundi na zaraa ili mambo yao yasizidi ___10___.

   A   B   C   D 
 1.   yamewanya   imewafanya   zimewafanya   limewafanya 
 2.  kuenda nguu   kula mumbi   kula mwande  kuenda mserego 
 3.  Kati ya  Fauka ya   Miongoni   Baadhi 
 4.  mmeshindwa  tumeshindwa   wameshindwa   wameshindikana 
 5.  kujimudu  kujiweza   kujiendeleza   kujitosheleza 
 6.  imezoroteka  yamezoroteshwa   yamezorota  zimeharibiwa 
 7.  ambao  ambavyo   ambapo   ambako 
 8.   haina kazi wala bazi    hawana mbele wala nyuma   hawana kazi wala bazi   haijijui haijitambui 
 9.  kuwatia shime  kuwatia hima  kuwatilia mrija  kuwatia kapuni
 10.   kughafilika  kutambulika  kuajabia  kudidimia

 

___11___, wavyele wa Mwasi wakamwambia huku ___12___ na machozi ya majonzi  usione umepata kazi ukafikiri kuwa hutahitaji tena msaada wetu. Mwasi alikuwa ___13___. ____14___ alipopata kazi yake yenye mshahara mnono, katika idara moja serikalini, alijiona kafika kwelikweli. Wazazi waliamua lao liwe jicho tu hadi siku___15___ afikiwe na fimbo ya ulimwengu.

   A   B   C   D 
 11.   hasidi aangukapo mnyanyue   kutangulia si kufika   usitukane wakunga na uzazi ungalipo   usiache mbachao kwa msala upita
 12.  wamedondokwa  wakidondokwa   walidondokwa  wakadondokwa
 13.   haliki hatafuniki  hamjui aingiaye wala atokayo    hazidishi hapunguzi  haoni hasikii
 14.  Mpaka  Hadi   Lau   Tangu 
 15.  itakaofika  itakakofika   itakapofika  ifikayo

 

Kuanzia nambari 16 mpaka 30, chagua jibu lifaalo zaidi.

  1. Tambulisha sentensi inayoonyesha hali ya masharti.
    1. Mwadime alijikwaa akaumiza dole lakc.
    2. Lau ungefika mapema ungemkuta mjomba kwake.
    3. Mtoto alikuwa akilia kwa sababu ya njaa.
    4. Msichezee karibu na barabara yenye magari.
  2. Chagua maelezo sahihi kati ya haya.
    1. Manju ni mcheza ngoma stadi. 
    2. Mghani hutunga na kuimba mashairi.
    3. Mshenga ni mtu ambaye hupeleka habari za posa.
    4. Mjumu ni fundi wa kutia nakshi katika vyombo vya madini.
  3. Tumia viambishi mwafaka. 
    Shoka ______________________ lilomkata ndi ________________________ hili.
    1. li, lo
    2. i, yo
    3. u, o
    4. ki vyo
  4. Andika umoja wa sentensi ifuatayo.
    Mbao zilizoletwa zitatumiwa kujengea mabanda.
    1. Mbao iliyoletwa itatumiwa kujengea banda.
    2. Ubao ulioletwa utatumiwa kujengea banda.
    3. Mbao iliyoletwa itatumiwa kujengea kibanda.
    4. Ubao ulioletwa utatumiwa kujengea kibanda.
  5. Nomino ipi ya makundi imekamilishwa ipasavyo.
    1. Mkuo wa sabuni.
    2. Wingu la moto.
    3. Halmashauri ya wanafunzi.
    4. Kaumu ya ng'ombc.
  6. Chagua sentensi iliyotumia kiambishi ku kama kiwakilishi cha nafasi.
    1. Ulipofika hukujua tulikuwa chumbani.
    2. Kuliko na gharika kunahitaji msaad
    3. Kulipopambazuka nyinyi mlianza shughuli papo hapo.
    4. Alipokuona alikukimbilia kwa furaha tele.
  7. Gao ni ukubwa wa ngao. Aidha gao ni
    1. Mahali palipohamwa na hapana watu waishio hapo.
    2. Samaki mwenye rangi nyeupe tumboni na ya kijivu mgongoni.
    3. Kiganja cha mkono kilichokunjwa kwa ajili ya kutia kitu.
    4. Chombo cha seremala cha kushikia mbao.
  8. Andika usemi wa taarifa wa sentensi;
    Mwalimu aliwaambia wanafunzi, "Liwekeni darasa lenu safi kila siku."
    1. Mwalimu aliwaagiza wanafunzi wawe wakiliweka darasa lao safi kila siku.
    2. Mwalimu aliwaambia wanafunzi kuwa yeye hutaka darasa liwe safi kila siku.
    3. Mwalimu aliwaomba wanafunzi wawe wakilisafisha darasa lao kila siku.
    4. Mwalimu alisema kuwa angetaka wanafunzi wawe wakiliweka darasa lao safi siku hizo
  9. Kidani ni kwa shingo kama ilivyo ______________________ kidevuni.
    1. furungu
    2. kikuba
    3. utondoti
  10. Nomino zipi hupatikana katika ngeli wa YA-YA pekee?
    1. Manukato, mazingira
    2. Magari, maegesho
    3. Mate, mapato
    4. Mashaka, maembe
  11. Upi ni muungano sahihi wa sentensi ifuatayo?
    Mvua ilinyesha vizuri. Mavuno hayakuwa mengi.
    1. Mvua ilinyesha vizuri aghalabu mavuno hayakuwa mengi.
    2. Lau mvua ilinyesha vizuri mazao hayakuwa mengi.
    3. Mazao hayakuwa mengi almradi mvua ilinyesha vizuri.
    4. Mazao hayakuwa mengi licha ya mvua kunyesha vizuri.
  12. Ipi ni sifa iliyoundwa kutokana na nomino.
    1. dhoofu- dhaifu
    2. wema - jema
    3. refusha - urefu
    4. kimbia - kimbilio
  13. Ni sentensi ipi iliyo na kivumishi cha idadi.
    1. Wanafunzi wote watapewa vipakatalishi mwakani.
    2. Maswali mengine hayakuweza kujibika.
    3. Watalii huja hapa mara kwanmara.
    4. Tulipanda miti kadhaa msimu.
  14. Tunasema mrefu kama mlingoti na pia mwaminifu mithili ya
    1. jua
    2. malaika
    3. mchana
    4. kondoo
  15. Chagua jozi ya methali zenye maana sawa.
    1. Kuishi kwingi ni kuona mengi. 
    2. Moto wa kumvi hudumu.
    3. Ngoma ya wana haikeshi.
    4. Jungu kuu halikosi ukoko.
    5. Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura.
      1. (ii), (iv)
      2. (i), (iii)
      3. (ii), (v)
      4. (i), (v)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia 31 mpaka 40

Mwendo wa saa mbili na ushei, lange la tarabe lilifunguliwa taratibu. Ni mara chache sana ambapo Mwapuza aliweza kuiona sehemu ya nje ya lango hilo. Awali, aliliona pale tu yeye na wafungwa wenzake walipopelekwa chini ya ulinzi mkali ama kunadhifisha sehemu za umma mjini au kushiriki shughuli nyinginezo kama walivyohitajika. Lango hili lilikuwa limemdhibiti kwa nusu mwongo sasa, japo kwa Mwapuza hii ni miongo mitano! Lakini leo, imesibu kuwa hauchi hauchi unakucha. Wake umekucha che! Na kumwangazia waa! Kwa nuru ya uhuru.

Kumbukumbu za Mwapuza zilimregesha katika siku zake za kisogoni, akakumbuka akiwa danga la mwana katika shule ya msingi ya Hekima. Wavyele wake walalahai walijikaza masombo mwana wao akapata hiki na kile, almradi aweze kujitegemea na kuwa taa ya jamaa na jamii iwapo yatakuwa majaliwa. Siku zote Mwapuza akawa akiahidi kuinamia cha mvunguni na kuibuka na mzo wa maarifa.

Mnamo mwaka wake wa saba katika shule ya msingi, Mwapuza alipatana na wasena watundu akanolewa akapata. Kufumba na kufumbua akajipata ameabiri dau la mihadarati. Kila uchao, wavyele wake walisikika wakilaani kuwa fulusi zao zilitoweka kimiujiza. Ambalo hawakujua ni kuwa njenje zao zilitumika kugharimia starche za mwana wao. Baadhi ya vitu vya thamani chengoni aidha vilianza kuota mbawa ́ kiajabuajabu.`

Baada ya kushauriana, wavycle walikata shauri la kutohifadhi ghawazi nyumbani. Waliafikiana kwa kauli moja kuwa benkini ndiko mikono mirefu isikofika kwa urahisi. Mwapuza alipohojiwa alikula mori na kuanza kuwafokea wazee wake. "Hivi mmenikosea thamani kiasi cha kuanza kuniita pwagu?" Akauliza kwa ukali. Hapo alilia hadi kifua chake kikalowa na kabisa kwa machozi. "Tazameni mlivyonitelekeza," akaendelea. "Hata masrufu hamnipi tena. Mbona mlinizaa kuja kunitesa," alisaili kwa uchungu.

Mama mtu alipojaribu kumtuliza mwanawe, alifunguliwa mfereji wa matusi akapigwa na mughma. Hakuamini masikio yake. "Huyu ni yule mwanangu niliyemzaa, nikamwamisha na kumchuchia alipolia hadi akatulia? Leo hii anathubutu kunivunjia heshima kiasi hiki? Ama kweli, ivushayo ni mbovu." Machozi yalimdondoka njia mbilimbili; machozi ya uchungu wa mwana ambao aujuaye ni mzazi.

Jioni iyo hiyo, Mwapuza aliwasimulia wasena wake masaibu yote yaliyomsibu. Wakamsikitikia sana. Papo hapo, walikula nyama ya kuguria mjini. Walipowasili huko, walitumia fulusi kichele walizokuwa nazo kununulia mihadarati na kushiriki anasa. * Walilosahau ni kuwa chovyachovya humaliza buyu la asali.

Pesa zilipotindika, waliamua kuingilia uhalifu ili kukidhi mahitaji yao. Awali, walivamia gereji moja na kuiba vipuri vya magari. Baadaye waliviuza kwa bei ya kutupa na kuendesha maisha yao. Ujanja wao uliishia jangwani usiku mmoja waliponaswa na polisi walioshika doria. Hawakuweza kueleza vizuri walikotoka usiku huo wala walikopata vipuri vya magari. Basi walinda usalama wakajijazia. Visa vya wizi wa vipuri vilikuwa vimeshamiri mjini humo.

Hatimaye Mwapuza na wenzake walifunguliwa mashtaka na kuhukumiwa. Mwapuza mwenyewe hakuona haja ya kukata rufaa. Ushahidi dhidi yake haukuwa na ati-ati. Wenzake walishindwa kuvumilia mateso gerezani wakasalimu amri. Mmoja wao aliugua na kutangulia mbele ya haki. Mwenzake naye alishiriki mapigano akaangamizwa na mfungwa mwenzake. Kwa Mwapuza, ilikuwa heri nusu ya shari kuliko shari kamili.

Wakati huu, Mwapuza aliona jambo moja tu. Alitaka kuwaona wavyele wake awaangukic miguuni na kulia kama mtoto mdogo. Alitamani afike kama yule mwana mpotevu na kuomba radhi kwao. Tayari machozi ya majonzi yalikuwa yakimdondoka ndo ndo ndo!

  1. Chagua jibu sahihi kwa mujibu wa aya ya kwanza.
    1. Aghalabu lango lilifunguliwa baada ya saa mbili.
    2. Haikuwa kawaida kwa Mwapuza kuwa huru nje ya lango. 
    3. Mwapuza alizoca kuenda kudumisha usafi mjini.
    4. Tofauti na awali, Mwapuza alijifungulia lango mwenyewe.
  2. Kulingana na makala, ni kweli kusema kuwa wazazi wa Mwapuza
    1. walichelea mwana kulia wakalia wao.
    2. walikuwa na uhitaji mkubwa wa kifedha.
    3. walikuwa watu wenye nafasi na hali katika jamii.
    4. walikuwa watu wa kima cha kati.
  3. Jambo linalodhihirisha kuwa wavyele wa Mwapuza ni wenye busara ni kwamba:
    1. wameamua kumwekea mwana wao msingi ufaao.
    2. walijinyima kila kitu wakampa mwanao mahitaji yote.
    3. hawataki kugombana na mwanao licha ya kupotoka.
    4. wanatarajia mwana wao awafae atakapohitimu masomo.
  4. Msemo, 'akanolewa akapata' kama ulivyotumika una maana ya
    1. akashauriwa na kukaidi. 
    2. akacrevushwa na kuerevuka.
    3. akarubuniwa na kupotoka.
    4. akahimizwa na kuzingatia.
  5. Chagua madhara ya mihadarati yaliyojitokeza katika kisa hiki.
    1. Madhara ya kiafya na kuingilia uhalifu.
    2. Kuwa mwizi na kutiwa nguvuni.
    3. Kupotosha maadili na kuingilia uhalifu.
    4. Kujiunga na marafiki na kuwaibia wazazi.
  6. Mwapuza alishiriki haya yote ila
    1. kujibizana na mamaye.
    2. kuyaasi masomo yake.
    3. kutoroka nyumbani.
    4. kumpiga mamaye.
  7. Kilichochangia kutiwa mbaroni kwa Mwapuza na wenzake hasa ni kuwa
    1. wizi wa vipuri ulikuwa umekithiri mjini.
    2. walipatikana na bidhaa zilizokuwa zikitafutwa.
    3. ilikuwa haramu kutembea na vipuri usiku.
    4. walionyesha mienendo ya kutiliwa shaka.
  8. Kwa nini Mwapuza hakukata rufaa?
    1. Hakuona uwezekano wa kushinda kesi.
    2. Alikuwa amekata tamaa kabisa maishani.
    3. Hakuwa na pesa za kuwasilisha rufaa.
    4. Hakuwa na maarifa kuhusu kesi yake.
  9. Kichwa kifaacho zaidi kwa makala haya ni
    1. Mui huwa mwema
    2. Majuto ni mjukuu.
    3. Siku za mwizi ni arubaini.
    4. Ivushayo ni mbovu.
  10. Masrufu kulingana na muktadha ni;
    1. pesa za kufidia masomo shuleni.
    2. fedha za matumizi ya kila siku.
    3. malipo ya kununulia vitu vya masomo.
    4. pesa za kununulia mihadarati.

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali kuanzia nambari 41 mpaka 50

Ugatuzi ni mfumo wa kiutawala ambapo baadhi ya mamlaka huhawilishwa kutoka kwa serikali kuu hadi kwenye maeneo mengine kama magatuzi au majimbo. Nchini. Kenya, mfumo huu ulianza kutekelezwa wakati katiba ya mwaka wa elfu mbili na kumi ilipoanza kutekelezwa. Tangu kuanzishwa kwake, mfumo huu umekuwa na manufaa tele. Hata hivyo, kuna changamoto ambazo zimeukumba. La kutia moyo ni kuwa manufaa yake yamezipiku.

Kwanza, ugatuzi umchakikisha kuwa kuna ugavi sawa wa rasilimali za umma. Ilali. hii imetokana na ukweli kuwa kila jimbo hutengewa kiasi fulani cha fulusi za maendeleo. Hii ni kinyume na ilivyokuwa hapo awali, ambapo baadhi ya maeneo yaliendelea kunawiri kimaendeleo huku wengine yakidorora. Tumeshuhudia miradi ya miundombinu ikiendelezwa katika sehemu mbalimbali za magatuzi zilizokuwa zimetengwa kimaendeleo.

Pia, ugatuzi umeleta ushindani chanya baina ya majimbo; hivyo kuharakisha maendeleo. Jambo hili limetokana na hofu ya baadhi ya magavana kushindwa kimaendeleo. na wenzao. Wengi wao humotishika kutekeleza miradi mbalimbali ili kutimiza ahadi kwa raia waliowachagua ili waweze kuchaguliwa tena. Viwanda mbalimbali kama vile vya maziwa, vya majani chai na hata vya maembe vimeanzishwa katika baadhi ya kaunti. Hii imeimarisha uchumi wa majimbo haya.

Isitoshe, nafasi za kazi zimeweza kubuniwa kutokana na mfumo wa ugatuzi. Si jambo la mjadala kusema kuwa kuna watu wengi walioajiriwa kufanya kazi katika afisi mbalimbali za kaunti na hata viwandani. Wengi wameweza kuyakidhi mahitaji ya kila siku huku maisha yao yakiboreka. Kutokana na hali hii, kiwango cha uhalifu kimepungua Baadhi ya vijana waliokuwa wametamauka hapo awali wamepata matumaini maishani baada ya kupata kazi katika serikali hizi.

Vilevile, huduma za serikali kwa wananchi zimeletwa karibu nao. Ukweli ni kuwa hapo awali, baadhi ya wananchi walihitajika kusafiri mbali kama vile hadi Nairobi kw lengo la kuhudumiwa. Wengi walikuwa wakichelewa, hivyo kuyafanya mambo yao kuenda mvange baada ya kukosa huduma walizohitaji. Hivi leo mambo ni tofauti madhali huduma nyingi wanazohitaji zinapatikana majimboni. Hili linasababisha uokoaji wa muda ambapo huweza kutumia muda wao kutekeleza kazi za kimaendeleo.

Zaidi ya hayo, climu imeboreshwa pale ambapo baadhi ya ujenzi wa shule umefadhiliwa na serikali za kaunti. Watoto wengi wameweza kujiunga na shule na kupat elimu. Nafasi za ajira kwa walimu wanaopata kazi katika shule mpya zinazoanzishwit wamenufaika pakubwa. Hapo awali, watoto katika maeneo yaliyokosa shule waliscleic kwenye mwina wa urumo bila matumaini ya nyota yao kung'aa maishani.

Kwa kuwa hakuna masika yasiyokuwa na mbu, serikali za kaunti zimekumbwa n changamoto mbalimbali. Ukabila ni tatizo mojawapo ambalo limezivamia serikali hizi.. Baadhi ya magavana wamekuwa wakiwaajiri watu kutoka kaunti zao pekee. Wengine wamekuwa wakipendekeza asilimia kubwa ya nafasi za kazi zipewe watu kutoka majimbo yao. Hali hii inahatarisha utangamano nchini. Kutokana na serikali za magatuzi, ufisadi umeshamiri. Pamekuwa na visa vingi vinavyoripotiwa ambapo baadhi ya watumishi wa kaunti wamekuwa wakibadhiri mali ya umma, Hali hii imedumaza maendeleo katika majimbo kama haya.

Licha ya serikali za ugatuzi kukumbwa na changamoto, ni ukweli kuwa zina manufaa tele. Kwa kuwa umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, viongozi wa majimbo pamoja na wananchi wanafaa kushirikiana kupambana na changamoto hizi. Hili likitekelezwa, serikali hizi zitaendelea kuwafaa wananchi. Majimbo husika yatapiga hatua kubwa za kimaendeleo na kuboresha maisha ya wananchi.

  1. Ni nini maana ya ugatuzi kulingana na kifungu?
    1. Kuhawilisha mamlaka kutoka scrikali moja hadi nyingine.
    2. Kuhamisha baadhi ya mamlaka kutoka serikali kuu hadi serikali za majimbo.
    3. Kuhawilisha majukumu ya serikali za ugatuzi hadi kwenye serikali kuu. 
    4. Kuhamisha baadhi ya majukumu ya serikali za magatuzi au majimbo. 
  2. Kenya ilianza kutekeleza mfumo wa ugatuzi lini?
    1. Mwaka wa elfu mbili na mbili.
    2. Kabla ya mwaka wa elfu mbili na mbili.
    3. Wakati katiba mpya ya Kenya ilipokuwa ikipitishwa.
    4. Katika mwaka wa elfu mbili na mbili ilipoanza kutekelezwa.
  3. Si kweli kusema kuwa, mfumo wa ugatuzi una
    1. manufaa pekee.
    2. faida na madhara.
    3. manufaa tele.
    4. changamoto zake.
  4. Kulingana na aya ya pili,
    1. mfumo wa ugatuzi umeimarisha usawa wa kimaeneo.
    2. ugatuzi umesaidia baadhi ya maeneo kuendelea kuliko mengine.
    3. awali, miundombinu ilikuwa imepuuzwa na serikali.
    4. hakuna eneo lililoendelea kuliko jingine chini ya mfumo wa ugatuzi.
  5. Maoni ya mwandishi ni kuwa;
    1. ushindani ni adui wa maendeleo.
    2. bila ushindani maeneo hayawezi kujiendeleza
    3. ushindani ukitumiwa vizuri unaweza kuharakisha ustawi.
    4. ushindani nzuri unaweza kuathiri maendeleo kwa njia hasi.
  6. Uchumi wa majimbo utaimarishwa zaidi na;
    1. kuzinduliwa njia mpya za uzalishaji.
    2. migao inayotolewa mara kwa mara.
    3. mikopo kutoka mataifa ya kigeni. 
    4. juhudi za viongozi za kutaka wachaguliwe tena.
  7. Kifungu kimedokeza kuwa uhalifu huchangiwa na;
    1. kupuuzwa kwa maeneo mengi na serikali.
    2. kukosa namna ya kujikimu kimaisha.
    3. ukosefu wa utawala madhubuti katika taifa.
    4. kutokuwepo kwa viwanda katika . maeneo.
  8. Huduma zikiletwa karibu na wananchi,
    1. watakuwa na muda wa kupumzika kwani hawaendi popote.
    2. watahudumiwa kwa wingi na wahudumu wachache.
    3. watapata huduma zenyewe bila gharama yoyote.
    4. watapata muda zaidi wa kufanya shughuli za ujenzi wa taifa.
  9. Ni kweli kuwa hakuna masika yasiyokuwa na mbu maadamu ugatuzi,
    1. umeimarisha miundomsingi shuleni, umeongeza maendeleo mashinani.
    2. umeleta tatizo la ukabila, umesababisha ubadhirifu wa mali ya umma.
    3. umerahisisha utoaji huduma, unavuruga umoja wa kitaifa. 
    4. umeongeza nafasi za kazi, umesababisha kubaguliwa kwa wenyeji wa magatuzi.
  10. Kulingana na aya ya mwisho;
    1. changamoto za ugatuzi ni manufaa kwa wananchi.
    2. kufanikiwa kwa ugatuzi .kunategemea ushirikiano wa watawala na watawaliwa.
    3. ufisadi umedumaza maendeleo katika baadhi ya maeneo.
    4. si vizuri kutoa nafasi za kazi kwa watu wa maeneo mengine.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Endeleza insha ifuatayo kwa * maneno yako mwenyewe huku ukiifanya iwe ya kusisimua zaidi.

Tulikuwa tumeisubiri ziara hiyo kwa hamu na ghamu. Asubuhi ilipofika.....................

MARKING SCHEME

  1. B
  2. A
  3. C
  4. C
  5. D
  6. B
  7. C
  8. A
  9. A
  10. D
  11. C
  12. B
  13. A
  14. C
  15. C
  16. A
  17. C
  18. A
  19. B
  20. A
  21. D
  22. C
  23. A
  24. D
  25. B
  26. D
  27. B
  28. D
  29. C
  30. A
  31. B
  32. D
  33. A
  34. C
  35. C
  36. D
  37. D
  38. A
  39. B
  40. B
  41. B
  42. D
  43. A
  44. A
  45. C
  46. A
  47. B
  48. D
  49. C
  50. B
Page 2 of 14