Displaying items by tag: kiswahili

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1 hadi 5.

Kutoka: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.                                                       11/5/2021                                                                        10:00a.m
Kwa: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

MADA: NAFASI YA KUJIFUNZA

Hujambo rafiki mpendwa? Nataraji ujumbe huu utakupata ukiwa mzima. Habari ya huko kwenu? Nimekuandikia hii barua ili kuomba ruhusa ya kuja kukutembelea wakati wa likizo ya Agosti. Ningependa kujifunza mengi kuhusu intaneti katika duka lenu la "Kituo cha Kompyuta."

Mwalimu wetu ametuhimiza kuzuru mahali panapotoa huduma ya intaneti. Tafadhali nifahamishe tarehe na siku utakapopatikana. Tumia anwani yangu. Mola akubariki.

Wako mpendwa,
Njeri.

  1. Mwandishi wa barua pepe hii ni nani?
    1. Rafiki
    2. Njeri
    3. Mary
    4. Hatujui
  2. Nia kuu ya Njeri kuomba ualishi ni
    1. kwenda shereheni
    2. kuzuru kwao
    3. kujifunza kompyuta
    4. kuwasabahi
  3. Ni nani aliyetoa himizo la kuzuru palipo na huduma ya kompyuta?
    1. Mwalimu
    2. Mzazi
    3. Njeri
    4. Mary
  4. Ni duka la akina nani kuna huduma ya kompyuta na intaneti?
    1. Mary
    2. Mwalimu
    3. Njeri
    4. Mary
  5. Barua hii inahusu nini?
    1. Kujifunza mambo yanayohusu intaneti na kompyuta
    2. Marafiki
    3. Jumba la huduma ya kompyuta
    4. Hatujaelezwa

Soma shairi hili kisha ujibu maswali 6 - 10.  

Kioo!
Kioo!
Kuna mzuri
niambiye
Kuliko miye?

Aha!
Kwani una doa?
Labda una ila!
Au una dosari!
Pengine una walakini!
Kweli umejiangalia?

Hebu songea karibu
Uwe kama pua na madomo
Sasa jitazame!
Sasa jipekue!
Sasa jichunguze!

Umegundua nini?
Umeridhika na uloona?
Nakuasa mwandani;
Uzuri wa mkakasi
Ndani kipande cha mti!

  1. Mwandishi alitaka kujua iwapo
    1. kuna mzuri kuliko yeye
    2. wengi wabaya
    3. wengine
    4. ni mzuri
  2. Walakini na dosari ni maneno yenye maana sawa. Maneno yenye maana sawa huitwa
    1. vitawe
    2. vitate
    3. visawe
    4. nomino
  3. Uwe kama pua na domo ni mfano wa
    1. istiara
    2. tashbihi
    3. msemo
    4. kitenda
  4. Shairi hili linazungumzia nini?
    1. Sura
    2. Raha
    3. Kujitazama
    4. Kioo
  5. Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti ni
    1. kitendawili
    2. msemo
    3. methali
    4. istiara

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali yafuatayo 11 - 15.

Ukulima ni mojawapo ya kazi muhimu katika nchi yetu. Faida za ukulima ni nyingi na hazina hesabu.

Faida ya kwanza ya ukulima ni kwa wananchi. Kila mwananchi anahitaji chakula ili aweze kupata afya ya kumwezesha kufanya kazi. Ili taifa kuendelea linahitaji wananchi wenye afya. Afya hii hutokana na chakula kinachotokana na ukulima.

Faida ya pili ya ukulima ni kwa mkulima. Mkulima anapouza mazao ya shamba hupata pesa. nyingi. Pesa hizi humwezesha kujifanyia shughuli zake kama vile kujijengea nyumba, kulipia watoto wake karo, kulipa bili ya umeme na kadhalika. Kwa jumla ukulima unaweza kumwezesha mkulima kuishi maisha ya raha na jamii yake.

Vilevile faida ya ukulima ni kwa serikali. Kuna mazao ya shambani ambayo huuzwa katika nchi za nje na kuletea nchi yetu pesa nyingi za kigeni. Serikali inapopata pesa za kigeni huzitumia kufanya maendeleo mbalimbali kama vile kujenga barabara, hospitali, shule na kufanya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Viwanda mbalimbali vya kutengeneza bidhaa za kilimo pia hujengwa. Hii inamaanisha kuwa wananchi watapata ujira viwandani. Wananchi hupata mshahara wa kuwawezesha kuendelea na maisha yao nayo serikali itapata kodi kutoka kwa wafanyakazi na wenye viwanda.

  1. Ukulima ni
    1. kati ya kazi nyingine muhimu
    2. ambapo hakuna ya faida
    3. isiyohitajika taifani
    4. taifa litaendelea bila
  2. Ipi si faida ya ukulima?
    1. Kutoa kipato
    2. Kutoa chakula
    3. Kutoa uhasama
    4. Kutoa kazi
  3. Mshahara ni
    1. pesa nyingi
    2. pesa zinazolipwa baada ya kufanya kazi mwishoni mwa mwezi
    3. msamaha kazini
    4. pesa za kulipwa kila siku baada ya kazi
  4. Serikali hupata kodi kutokana na
    1. wafanyabiashara wanaolipa kodi
    2. kuiba
    3. huomba
    4. hupanda
  5. Ukulima humwezesha mkulima kuishi maisha ya
    1. shida
    2. raha
    3. taabu
    4. matatizo

Jaza pengo hizi nambari 16 hadi 20.

Madereva wanaokiuka sheria (16)_____________ barabara (17)____________kutiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka. Hata kama (18)_______________ ajali (19) _____________zinaweza (20)_______________.

   A   B   C   D 
 16.   ya   za   cha   kwa 
 17.  zafaa   yanafaa   wanafaa   inafaa 
 18.  mtu pweke ni uvundo    asiyekuja hakuthamini   asiyekuwepo na lake halipo   ajali haina kinga 
 19.  nyingine  nyingineyo   zingine   zingineyo 
 20.  kuzuia  kuzuilika   kuzuwika  kuzuilisha

 

Kuanzia swali la 21 hadi 30, chagua jibu sahihi.

Vivumishi vifutavyo ni vya aina gani?

  1. Mtoto yule ni mcheshi.
    1. viulizi
    2. viashiria
    3. visisitizi
    4. namna
  2. Mwanafunzi hodari ni yule.
    1. namna
    2. wingi
    3. sifa
    4. wakati
  3. Mkulima yupi alituzwa?
    1. Radidi
    2. Kisisitizi
    3. Kiulizi
    4. Sifa
  4. Nomino 'kucheka' lipo katika kundi lipi la nomino?
    1. Mahususi
    2. Pekee
    3. Wingi
    4. Kitenzi jina
  5. Barua rasmi huwa na anwani ngapi?
    1. 2
    2. 3
    3. 4
    4. 5
  6. Kipande cha pili katika ubeti wa shairi huwa
    1. utao
    2. ubeti
    3. kipande
    4. mshororo
  7. Ni kipi kiwakilishi cha nafsi kati ya haya uliyopewa?
    Yeye ni mpole sana.
    1. ni
    2. yeye
    3. mpole
    4. sana
  8. Neno lipi liko katika ngeli ya U-U?
    1. Ugali
    2. Uzi
    3. Nguo
    4. Ukuta
  9. Kanusha:-
    Mimi nilianika nguo.
    1. Mimi nilianua nguo.
    2. Mimi sikuanua nguo.
    3. Mimi sikuanika nguo.
    4. Mimi nilianika nguo.
  10. Kamilisha kwa kutumia 'amba':-
    Duka _________________lilifunguliwa ni langu
    1. ambaye
    2. ambayo
    3. ambacho
    4. ambalo

INSHA  

Andika insha kuhusu:-

"NCHI YANGU FAHARI YANGU"

MARKING SCHEME

  1. B
  2. C
  3. A
  4. D
  5. A
  6. A
  7. C
  8. B
  9. D
  10. C
  11. A
  12. C
  13. B
  14. A
  15. B
  16. B
  17. C
  18. D
  19. A
  20. B
  21. B
  22. C
  23. C
  24. D
  25. A
  26. A
  27. B
  28. A
  29. C
  30. D

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5

(Mwasia anapiga gumzo na babu yake. Mazungumzo yanakuwa hivi)
Mwasia:   Shikamoo babu?
Babu:       Marahaba. Umeshindaje mjukuu wangu?
Mwasia:   Nimeshinda vyema. Nashukuru kwa kunijulia hali. Jana ulisema kwamba leo tutazungumzia suala fulani. Ikiwa unayo                     nafasi tunaweza kuzungumza badala ya kuyaweka mambo kiporo.
Babu:       Sawa, kaa kitako tuzungumze. Nilitaka uniambie ni nini kiini cha vijana wa siku hizi kukaidi mila zetu. Kwani                                     mmesahau kwamba mwacha mila ni mtumwa?
Mwasia:   Ni kweli kwamba baadhi ya vijana wameonyesha maasi hasa kwa kuiga utamaduni wa kigeni usiofaa. Inasikitisha                           kuwaona wengine wakivaa mavazi ya aibu, kutumia lugha ya kuudhi na kushiriki ndoa za jinsia moja.
Babu:      (Akatikisa kichwa kwa masikitiko). Haya ni baadhi ya mambo yanayotukera sisi wazee. Suala la mapenzi ya kiholela                       halionekani kama mwiko siku hizi.
Mwasia:   Vijana hawa wanafaa wajirekebishe. Hata hivyo kuna mila ambazo zinafaa kuachwa nyuma kwani haziongezi thamani                   katika maisha ya jamii.
Babu:       Zipi hizo?
Mwasia:   Mila kama kurithi wajane, ukeketaji, kafara ya damu ya binadamu na kuwanyima wasichana urithi zimepitwa na wakati.
Babu:      Sisi wazee tulijiendea tu kama gari lisilo na taa wala kidhibiti mwendo. Mnapaswa kutumia elimu yenu kubadili mkondo                  wa maisha katika jamii.
Mwasia:  Hayo ni kweli babu. Pia vijana lazima watumie akili vizuri wasiwe kama ng'ombe asiye na nadhari. (Wanaendeleza                           mazungumzo kwa muda kisha wanaagana)

  1. Maneno 'kuyaweka mambo kiporo' yana maana gani?
    1. Kupuuza mambo muhimu.
    2. Kushughulikia jambo mapema. 
    3. Kuacha jambo ili lishughulikiwe baadaye.
    4. Kula chakula kilicholala.
  2. Vijana wanapotoshwa na nini kulingana na mazungumzo haya?
    1. Kuiga utamaduni wa kigeni.
    2. Kufuata sana utamaduni wao.
    3. Teknolojia inayoonyesha mambo yasiyofaa.
    4. Kuandamana na wageni wabaya.
  3. Kwa nini watu wa zamani walizingatia mila ambazo hazikuwa na manufaa?
    1. Hawakufanya mambo kwa kufikiria.
    2. Vijana walikuwa watiifu.
    3. Hawakuwa na utamaduni wa kigeni.
    4. Hawakuwa na climu ifaayo ya kuwaongoza.
  4. Mila potovu zilizotajwa si pamoja na; .
    1. tohara ya wasichana.
    2. utiifu na unyenyekevu.
    3. kurithi wake.
    4. kuwatoa watu kafara.
  5. Baba analinganisha maisha ya kale na;
    1. gari bovu barabarani.
    2. gari la zamani.
    3. gari lisilo na taa.
    4. gari lisilo na dereva.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 - 9  

Kuku na mwewe walikuwa marafiki wa chanda na petc. Walijitahidi sana kuwalea na kuwaelekeza wana wao kwa njia iliyofaa. Yamkini, walimaizi kuwa mtoto umleavyo ndiyo akuavyo. Aghalabu mwewe aliamka mapema akaanza shughuli ya kusaka riziki. Zipo nyakati, japo kwa nadra sana, ambapo kuku alijitwika jukumu la kutafuta chakula. Chochote walichopata walitumia pamoja, jambo ambalo liliwavutia sana ndege wengine.

Wakati fulani, kiangazi kikali kilivamia enco lile ikawa kwamba mwewe akitoka angekawia hata kwa juma zima kabla ya kurudi na chakula. Wakati mwingine, hata hakuwaona watoto wake kwani alifika usiku na kuamkia kazi mapema. Hata hivyo, hakuwa na wahaka kwani alijua rafikiye kuku alimtunzia wana kama ndugu. Laiti angalijua! Jambo usilolijua ni usiku wa giza totoro.

Mwewe alipitisha majuma mawili bila kuwaona wanawe. Asubuhi moja, alijihisi mchovu akashindwa kufuata shughuli zake za kawaida. Kuku alidhani kuwamwenzake ameshaelekea mawindoni. Mwewe akiwa nje kwenye mti mmoja alimwona kuku akiwapa wanawe kiamshakinywa. Watoto wa mwewe waliodhoofika kupita kiasi waliambiwa kuwa hapakuwa na chakula chao.

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi Mwewe aliteremka kwa ghadhabu, akamshika mtoto mmoja wa kuku na kumrarua vipandevipande. Kuku alipoona hayo, aliwachukua wanawe waliosalia akatorokea kwa binadamu kuomba hifadhi. Usuhuba wao ulifikia kikomo papo hapo.

  1. Chagua maelezo sahihi kuhusu kuku na mwewe.
    1. Walikaa na kulala pamoja.
    2. Walitafuta chakula pamoja.
    3. Walizingatia malezi bora ya wanao.
    4. Walipendezwa na urafiki wa wenzao.
  2. Ni kweli kusema kwamba,
    1. haikuwa kawaida ya kuku kutafuta chakula.
    2. mwewe alibaki na watoto mara kwa mara.
    3. kuku aliwatunza watoto vizuri kuliko mwewe.
    4. jukumu la kutafuta chakula ni muhimu kuliko ulezi
  3. Kwa nini mwewe hakujua hali ya wanawe mapema?
    1. Kuku alimnyima nafasi ya kuwaona wanawe.
    2. Hakuweza kutangamana nao mara kwa mara.
    3. Hakuwajali watoto wake hata kidogo.
    4. Watoto walilelewa mbali na pale alipoishi.
  4. Urafiki wa kuku na mwewe ulivunjwa na nini hasa?
    1. Ukatili wa mwewe. mwewe.
    2. Uchochezi wa majirani.
    3. Tamaa ya watoto wa mwewe.
    4. Ubinafsi wa kuku na wanawe.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 - 12  

Nchi iliyo na misitu hunufaika kwa njia nyingi. Mbali na kuwa makao ya wanyama walio kivutio cha watalii, pia hutupa mvua ya kutosha. Kilimo huendeshwa msimu baada ya msimu hivyo kukabiliana na uhitaji wa chakula. Wakazi wanaweza kutumia miti iliyojikaukia kupata kuni au kuchomea makaa. Isitoshe, wanaweza kupata mbao za kujengea na kuundia samani almradi ukataji wa miti uandamane sambamba na upanzi wa mingine.

Uharibifu wa misitu huwaacha wenyeji wakisaga meno kwa masikitiko. Vyanzo vya maji hukauka. Vivuli vya kujikinga na jua huadimika kama kaburi la baniani. Upepo nao huvuma bila kizuizi, jambo ambalo hupelekea kung'olewa kwa mimea na mapaa ya majengo. Upepo uo huo huwa na mavumbi yanayowachafua watu na kuwasabibishia shida za macho. Sote hatuna budi kuitikia mwito wa serikali wa kuilinda misitu yetu.

  1. Manufaa ya misitu kulingana na kifungu hiki ni:
    1. Kuhifadhi mvua na kuzuia upepo.
    2. Kivutio cha watalii na kuni.
    3. Makao ya wanyama na mbao za ujenzi.
    4. Kuundia samani na dawa.
  2. Si kweli kuwa nchi yenye misitu;
    1. hukabiliwa na baa la njaa.
    2. hupunguza athari za upepo mkali.
    3. wakazi hupata mahali pa kujiburudisha.
    4. wenyeji hawasumbuliwi na mavumbi.
  3. Mwito wa mwandishi ni kuwa:
    1. Tukate miti ili tupande mingine. 
    2. Tutumie kuni na makaa ya msituni. 
    3. Tuepuke sehemu zilizo na misitu.
    4. Tuitikie mwito wa serikali.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 - 15  

Usalama ni uwepo wa amani, bila tishio wala hatari yoyote. Kila mmoja hupenda kukaa palipo na usalama. Mtoto akilelewa katika hali ya vurugu maisha yake huathirika vibaya. Yeye hukosa kujiamini na akiwa mbele ya watu hugeuka bubu. Ni rahisi kumtambua mtoto kama huyo akiwa shuleni. Mara nyingi hujitenga na shughuli wanazoshiriki wenzake hasa michezo, majadiliano na shughuli za vyama vya wanafunzi shuleni.

Ni muhimu kuelewa kuwa wakati mwingine, matendo ya mtu yanaweza kumsababishia utovu wa usalama. Mifano ni wale wanaojipalia makaa kwa kudandia magari yapitayo kwa kasi, kuchezea karibu na barabara au visima vya maji. Wengine huchezeana michezo inayowaweka katika hatari ya kujeruhiana.

Jukumu la kudumisha usalama halifai kuachiwa wazazi na walezi pekee. Lazima tujaliane maslahi popote tulipo. Ukihisi kwamba unakabiliwa na tishio la aina yoyote, mjulishe mzazi, mwalimu au mtu mzima unayemthamini.

  1. Usalama ni nini?
    1. Kupata utulivu palipo na hatari,
    2. Malezi mema katika hali ya vurugu.
    3. Taarifa zinazohusiana na mambo yasiyo ya hatari.
    4. Kuwepo hali ya utulivu mahali alipo mtu.
  2. Maana ya 'hugeuka bubu' ni kuwa
    1. hupoteza uwezo wa kuongea.
    2. huwa na mazoea ya kunyamaza.
    3. huongea kwa lugha ya ishara. 
    4. huzungumza kwa sauti ya chini.
  3. Jambo lipi si tishio kwa usalama wa mtoto? A
    1. Kuchezea pale yanapopitia magari.
    2. Michezo inayosababisha majeraha.
    3. Kucheza na wenzake mbali na kwao.
    4. Vitisho na ukatili katika malezi.

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 mpaka 20. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa jibu sahihi.

Kuna aina nyingi ___16___ ndege wa porini. Ndege mmojawapo ___17___ sana na watu ni ___18___. Hii ni kwa sababu ___19___ kuyaiga maneno ___20___ na watu

   A   B   C   D 
 16.   ya   wa   za   kwa 
 17.  anayejulikana   wanaojulikana   anaojulikana   wanajulikana 
 18.  njiwa  kasuku   heroe   ninga 
 19.  ameweza  angeweza   ataweza   anaweza 
 20.  yanayosema  anayosema   yanayosemwa   wanaosema 

 

Kuanzia nambari 21 mpaka 30,chagua jibu sahihi.  

  1. Ni jozi ipi ya maneno iliyo tofauti?
    1. baba - abu
    2. barua - waraka
    3. adui - hasimu
    4. furaha - huzuni
  2. Andika kauli ya kutendea ya sentensi.
    Baba alileta zawadi akampa mwanawe.
    1. Mwana aliletewa zawadi na babaye. 
    2. Baba alimletea mwanawe zawadi
    3. Zawadi ililetwa na baba kwa mwana.
    4. Baba alileta zawadi ya mwanawe
  3. Chagua sentensi iliyo sahihi.
    1. Darasani lililofagiliwa ni zuri.
    2. Darasani mlimofagiliwa ni pazuri. 
    3. Darasani mlimofagiliwa ni mzuri.
    4. Darasani palipofagiliwa ni kuzuri.
  4. __________________ ni ugonjwa wa kutabawali damu unaosababishwa na vidudu vya konokono.
    1. Kichocho
    2. Tauni
    3. Utapiamlo
    4. Waba
  5. Andika wingi wa:
    Jani hilo lilianguka karibu na ua wak
    1. oJani hizo zilianguka karibu na maua ya
    2. Majani hayo yalianguka karibu na nyua zako.
    3. Majani hayo yalianguka karibu na nyua zao.
    4. Majani hayo yalianguka karibu na maua yao.
  6. Ni sentensi ipi iliyo katika hali ya mazoea?
    1. Shawe alimsaidia mzee kuvuka barabara.
    2. Mjomba anaipalilia miche shambani.
    3. Kamau amempelekea bibi maziwa.
    4. Mimi hula matunda siku zote.
  7. Tashbihi gani inaonyesha sifa ya mchwa?
    1. Mlafi kama mchwa.
    2. Bidii mithili ya mchwa.
    3. Mkali kama mchwa.
    4. Mwaminifu kama mchwa.
  8. Chagua methali inayohimiza ushirikiano. 
    1. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
    2. Mtoto umlcavyo ndivyo akuavyo.
    3. Mwenye nguvu mpishe.
    4. Kikulacho ki nguoni mwako.
  9. Tambua maneno yaliyoangaziwa katika sentensi ifuatayo:
    Vijana waadilifu wametuzwa na mwalimu wao.
    1. kivumishi, nomino
    2. kivumishi, kitenzi
    3. nomino, kitenzi
    4. kivumishi, kiwakilishi
  10. Chagua sentensi iliyoaki fishwa ipasavyo.
    1. Mwaye, anaishi, wapi?
    2. Mtoto yule. ni mtiifu.
    3. Je? Unaenda wapi?
    4. Nilipomwona jana, alikuwa akitoka sokoni.

INSHA   

Andika insha ya maelezo kuhusu:

SIKU YA MICHEZO SHULENI  

MARKING SCHEME

  1. C
  2. A
  3. D
  4. B
  5. C
  6. C
  7. A
  8. B
  9. D
  10. C
  11. A
  12. D
  13. D
  14. B
  15. C
  16. C
  17. A
  18. B
  19. D
  20. A
  21. D
  22. B
  23. C
  24. A
  25. C
  26. D
  27. B
  28. A
  29. A
  30. D

Soma mazungumzo haya kisha ujibu swali la 1 hadi la 5.  

G6SwaT1SB23002P1

(Ni hotelini ambapo Roda na Hamisi wanakutana kunywa staftahi)

 
Roda:           Hujambo rafiki yangu.U hali gani?
Hamisi:        Sijambo,hali yangu ni njema.Nashukuru Maulana kwa afya njema.Je, u mzima?
Roda:           Naam,mimi ni mzima kama kigongo.Nimekuja kunywa kiamshakinywa.
Hamisi:        Mimi pia, wazazi wako vipi?Natumai wako salama salimini.
Roda:           Ni wazima japo mama alienda mjini kumwona bibi ambaye ni mgonjwa.
Hamisi:        Lo! Poleni sana.Atapata afueni.Mungu halali.
Roda:           Asante sana msena wangu.Bila shaka hapo umenena.Atapona.
                     (Mhudumu anawakata kauli kuwaomba waagize vyakula ama vinywaji)
Mhudumu:   Karibuni sana wateja wapendwa.Niwaletee nini?
Hamisi:        Kawaida ndugu yangu. Chai na chapati. Tutashukuru.
                     (Mhudumu anaondoka upesi,muda si muda anarudi akiwa amebeba sinia kubwa)
Mhudumu:   Karibuni sana.
Hamisi:         Starehe.

  1. Ni kweli kusema kuwa Roda na Hamisi walikuwa
    1. maadui
    2. marafiki
    3. wahudumu
    4. wacheshi
  2. Hamisi alitaka nini hotelini?
    1. Kusalimia mhudumu
    2. Kusalimia Roda
    3. Kuwajulia hali
    4. Kupata mlo
  3. Neno bibi lina maana sawa na
    1. nyanya
    2. mke
    3. mume
    4. mzee
  4. Ni nini maana ya msemo kata kauli?
    1. Kukatiza mtu maneno
    2. Kumwamkua mtu
    3. Kumshauri mtu
    4. Kuamulia mtu
  5. Unafikiri sinia ilibeba nini?
    1. Vyakula na vinywaji
    2. Vyakula pekee
    3. Vinywaji pekee
    4. Vikombe na birika

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 6 hadi la 9

G6SwaT1SB23002P2

Tulikuwa tumeingoja siku hiyo kwa hamu na ghamu. Ilikuwa ni siku ambayo mimi na sahibu yangu wa kufa kuzikana Yona tulikuwa tumepanga kuenda kuvua samaki. Tulitengeneza ndoana zetu na sisi hao! Tukang'oa nanga na kubandua nyayo mpaka mto Lusumu ambao haupo mbali sana na nyumbani kwetu. Haikuchukua muda mrefu kabla ya kufika mto Lusumu.

Moja kwa moja, tulianza kazi yetu. Billy ndiye aliyekuwa wa kwanza kubahatika. Alimvua mkunga mkubwa na mweusi tititi kama makaa. Alifanana sana na joka kiasi cha kwamba nusura tutundike miguu mabegani. Jisamaki hilo liligaragara huku na huko kwa dakika sita hivi mwishowe likatulia.

Tuliendelea na uvuvi wetu huku tukipiga soga kwa bashasha ghaya. Mara lo! Katika hizo harakati za kuvua samaki zaidi, nilitupa jicho juu ya mti. Mtini, palikuwa na joka jeusi na nono kupindukia. Lilikuwa limetukodolea macho kana kwamba lilitaka kutumeza wazima wazima. Macho yalitutoka pima huku tukigwaya kwa hofu. Punde si punde, tukawa miguu nibebe ili kuepukana na hatari hiyo.

  1. Yona walitaka kwenda wapi?
    1. Kufua nguo
    2. Kunasa samaki
    3. Kuona mto
    4. Kutembea Lusumu
  2. Ni kweli kusema kuwa mto Lusumu
    1. ulikuwa karibu
    2. ulikuwa na nyoka
    3. haukuwa na samaki
    4. ulikuwa mbali
  3. Kulingana na kifungu hiki,mkunga ni aina ya
    1. nyoka
    2. ndege
    3. samaki
    4. mamba
  4. Ni hatari gani Yona walipata?
    1. Kushika samaki
    2. Kushika nyoka
    3. Kutupa macho juu
    4. Kumwona nyoka

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 10 hadi la 12.   

Mtaa wetu huwa na maduka matano.Maduka haya huuza bidhaa pia za aina mbalimbali, Maria, Kendi, Sang na Oloo waliandamana kwenda kununua bidhaa. Sang alitaka vyakula, Kendi alitaka vifaa vya kielektroniki, Oloo alitaka simu na shati. Naye Maria alitaka kutembea tu madukani kujionea bidhaa. Soma jedwali lifuatalo kisha ujibu maswali.

 Jina la duka   Bidhaa 
 FAIDA  Unga, sukari, mboga, matunda
 JAMAA  Mboga, matunda, nguo, simu 
 FURAHA  Televisheni, tabuleti, rununu, kompyuta 
 DOLA  Matunda, mboga, mavazi, simu 

 

  1. Kendi angeenda duka gani?
    1. DOLA na FAIDA
    2. JAMAA na FURAHA
    3. FURAHA na FAIDA
    4. JAMAA na FAIDA
  2. Ni nani hakununua chochote?
    1. Sang
    2. Maria
    3. Oloo 
    4. Kendi
  3. Ni kweli kusema kuwa
    1. Oloo alinunua mavazi
    2. Maria alinunua simu
    3. Sang alinunua tabuleti
    4. Kendi alinunua vyakula

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 13 hadi la 15. 

Siku moja wanyama wa jamii ya simba, yaani walanyama waliungana pamoja. Azima ya mkutano ilikuwa kubuni mbinu za kuwinda Walamea. Walamea nao walikutana. Walijadili kuhusu mipango na mbinu za kujificha. Walionekana kuwa na wasiwasi wa mwasi. Kwa pamoja swara na wenzake waliamua kuhamia msitu uliokuwa na vichaka na mashimo mengi ya mhanga.

Waling'oa nanga na kuenda kasi kabla ya mkutano wa maadui kuisha. Mfalme simba alipotamatisha mkutano, wenzake waliingia vichakani kuwinda. Lo! Hawakupata mlo wowote. Njaa iliwatesa sana kwa siku nyingi. Baadaye waligundua kuwa wanyama waliopangiwa kuwindwa wamehama.

  1. Ni kweli kusema kuwa
    1. mikutano ilikuwa mingi
    2. mikutano ilikuwa miwili
    3. mkutano ulikuwa mmoja
    4. hakukuwa na mikutano
  2. Ni kwa nini wanyama walikuwa na wasiwasi?
    1. Woga
    2. Ujasiri
    3. Baridi
    4. Muda
  3. Ni nini maana ya msemo waling'oa nanga?
    1. Kumaliza safari
    2. Kwenda mbio
    3. Kutifua vumbi
    4. Kuanza safari

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya vale uliyopewa.

Siku moja nilikuwa ___16___ mpira wa miguu yaani ___17___ na rafiki yangu ambayetulipendana na yeye kama chanda na ___18___. ___19___ tuliamua kupumzika chini ya mti ___20___ mwembe ambao ulikuwa na matunda matamu.

   A   B   C   D 
 16.   nachezwa   nikicheza   ninacheza   nimecheza 
 17.  boli  voliboli   kandanda   pete 
 18.  pete  kidole  arusi   mkono 
 19.  Zote  Nyote   Wote  Sote 
 20.  ya  wa  la  cha 


Kutoka swali la 21 hadi la 30. Chagua jibu sahihi. 

  1. Jaza mapengo kwa maneno yanayofaa: Waimbaji wali____________ kupiga ______________
    1. koma, gona
    2. piga, pinga
    3. goma, ngoma
    4. aga, anga
  2. Chagua maelezo yaliyo sahihi.
    1. Meno husaidia kuonjea chakula.
    2. Moyo husaidia kusukuma damu.
    3. Figo husaidia kuhifadhi mkojo.
    4. Pafu husaidia kusaga chakula.
  3. Jaza pengo kwa kivumishi cha sifa: Madawati ______________________ hufurahisha mwalimu.
    1. masafi
    2. chafu 
    3. safi
    4. yote
  4. Jibu maagano haya: Buriani
    1. buriani dawa
    2. binuru
    3. aheri
    4. pia nawe
  5. Tegua kitendawili hiki: Chakula kikuu cha mtoto
    1. maziwa
    2. usingizi
    3. ndizi
    4. uji
  6. Chagua wingi wa sentensi hii: Soko lile lina tunda.
    1. Soko lile lina matunda
    2. Masoko yale yana tunda
    3. Masoko yale yana matunda
    4. Soko lile lina matunda
  7. Je, nomino mbu ni katika ngeli gani?
    1. U-I
    2. A-WA
    3. I-ZI
    4. LI-YA
  8. Ipi si sehemu ya kompyuta?
    1. Kiwambo
    2. Bodidota
    3. Kipanya
    4. Mitini
  9. Tambua kielezi katika sentensi hii: Mwanafunzi mzuri alicheza vizuri.
    1. vizuri
    2. mzuri
    3. alicheza
    4. mwanafunzi
  10. Chagua kinyume cha: Bandika picha nje.
    1. Bandua picha nje
    2. Bandika picha ndani
    3. Bandua picha ndani
    4. Usibandue picha nje

INSHA

Andika insha ya kusisimua ukurasa mmoja nanusu kuhusu:

MECHI YA KUSISIMUA

MARKING SCHEME

  1. B
  2. D
  3. A
  4. A
  5. A
  6. B
  7. A
  8. C
  9. D
  10. B
  11. B
  12. A
  13. B
  14. A
  15. D
  16. B
  17. C
  18. A
  19. D
  20. B
  21. C
  22. B
  23. C
  24. A
  25. B
  26. C
  27. B
  28. D
  29. A
  30. C

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA  

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali  

G5SWAT1TW23002P1

(Sofi na Patu wako darasani wakifanya shughuli ya wawili wawili katika kipindi cha Kiswahili)
Sofi:  Patu, sogeza dawati lako upande huu tuanze kazi yetu.
Patu: Naam Patu. Chelewa chelewa utapata mwana si wako.
Sofi:  Tutajadiliana kuhusu:Aina za vyakula, viungo vya mapishi, njia za mapishi na vifaa vya upishi.
Patu: Nitaandika tutakayoyajadili nawe utayawasilisha mbele ya wanafunzi wengine.
Sofi: Naam! Tuanze na aina mbalimbali za vyakula.
Patu: (akijikuna kichwa) Kuna wali, pure, ugali na mchuzi...
Sofi:  (akimkatiza) ongeza chapati, nyama, pilau, mahamri na viazi.
Patu: Mifano hiyo inatosha sasa. Tujadili viungo vya kupikia. Anza
Sofi:  (Huku akiwaza) nyanya, dania, tangawizi, pilipili na boga.
Patu:  Pia kuna iliki, pilipili hoho, kitunguu saumu, chumvi na mdalasini.
Sofi: Vizuri sana sahibu. Nazo njia za kupika ni gani?
Patu: (kwa upesi) Kuna kutokosa, kuchemsha, kuoka, kukaanga, kuchoma na kusonga.
Sofi: (kwa mshangao) Inaonekana wewe ni mpishi wa wapishi! Mimi na upishi ni kama samaki na maji.
Sofi: Nakubali. Mimi sasa nitataja vifaa vya kupikia. Kuna sufuria, nyungu, legeni, kikaango, mwiko na...
Patu: (akimsaidia) kinu, mchi, upawa na joko.
Sofi: Ninaona kama tumekamilisha shughuli yetu ya wawili wawili. Naona mwalimu akitaka kutupatia nafasi ya kuwasilisha kazi                yetu.
Patu: Niko tayari.
Sofi:  Kila la heri!

  1. Mazungumzo uliyoyasoma yalifanyika katika somo gani?
    1. Kiingereza
    2. Mapishi
    3. Kiswahili
    4. Sayansi
  2. Ni jambo gani ambalo Sofi na Patu hawakujadiliana?
    1. Aina za vyakula
    2. Njia za kupika
    3. Vifaa vya kupikia
    4. Viunganishi
  3. Ni kweli kusema kuwa :
    1. Sofi na Patu hawaelewi umuhimu wa kufanya kazi pamoja.
    2. Patu anaelewa msamiati wa mapishi kuliko Sofi.
    3. Sofi na Patu hawako katika darasa moja.
    4. Sofi aliwasilisha kazi aliyoiandika mbele ya wanafunzi wenzake.
  4. Mazungumzo haya yanatufunza maadili gani hasa?
    1. Ushirikiano
    2. Bidii
    3. Utengano
    4. Nidhamu
  5. Baada ya Sofi kumwambia Patu kila la heri, angemjibu vipi?
    1. Aleikum salaam
    2. Ya kuonana
    3. Asante
    4. Binuru

Swali la 6 hadi la 9

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

G5SWAT1TW23002P2

Katika kijiji cha Samaki paliishi mvuvi mmoja kwa jina Adili. Å iku moja alimpa rafiki yake Wema kazi ya kuipaka boti rangi. Wema alikuja na rangi na brashi kama alivyoagizwa na Adili. Alipokuwa akipaka rangi aliona shimo dogo chini ya boti na akaamua kuliziba.

Alipomaliza kazi yake alilipwa ujira wake na akaenda zake.Siku iliyofuata Adili alienda kwa Wema na kumpatia kitita cha pesa. Pesa hizi zilikuwa zaidi ya malipo ya kupaka rangi. Wema alishangaa na kumwambia Adili kuwa alikuwa ameshamlipa pesa zake. Wema alimwambia kuwa pesa hizo zilikuwa za kuziba shimo lililokuwa chini ya boti.

Wema alimwambia Adili kuwa hakufaa kumlipa tena kwani hiyo ilikuwa huduma ndogo sana ambayo haikufaa kulipwa pesa hizo zote. Adili alimwambia kuwa hakujua alichomfanyia. Alimwambia kuwa alisahau kumpa kazi ya kuziba shimo. Boti ilipokauka watoto wake waliichukua na kwenda kuvua na hawakujua kuwa kulikuwa na shimo naye hakuwa nyumbani. Aliporudi alishtuka kuona wamechukua boti. Alifikiri wangezama ziwani.

Alipowaona wamerudi moyo wake ulijawa na furaha kubwa. Alikagua boti na kuona hakukuwa na shimo. Wema alikuwa ameokoa maisha ya watoto wake. Alimwambia hivi akitokwa na machozi ya furaha.

Kusema kweli ni vizuri kuwafanyia wengine mema hata kama ni jambo dogo. Inaweza kuokoa maisha ya wengi bila wewe kujua. Mungu pia huona wema huu na kutulipa kwa Baraka kubwa.

  1. Adili alikuwa akifanya kazi gani?
    1. Kufua
    2. Kuvua
    3. Kurekebisha boti.
    4. Kupaka boti rangi
  2. Baada ya kazi yake, Wema alipata mapato ambayo yanaitwa ________________________
    1. pesa
    2. ujira
    3. mshahara
    4. nauli
  3. Nini maana ya kitita cha pesa kulingana na kifungu? 
    1. Pesa kidogo
    2. Noti
    3. Pesa nyingi
    4. Malipo madogo
  4. Kulingana na kifungu tunajifunza kuwa _____________________________
    1. tusipuuze kufanya wema kwa wengine.
    2. tufanye wema tukitarajia kulipwa.
    3. tufanye wema kwa marafiki zetu pekee.
    4. mtu akifanya wema hulipwa pesa nyingi.

Swali la 10 hadi la 12  

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. 

G5SWAT1TW23002P3
Mwaka uliopita, Stevo alikuwa amepata ajali uwanjani akicheza kandanda. Alikuwa ameumia kichwa na goti. Baada ya kutibiwa na kurudi shuleni, mwalimu alimpa nafasi aelezee hatua zilizochukuliwa na walimu na maskauti wakimpa huduma ya kwanza. Alielezea yafuatayo:

  1. Walichunguza kubaini jinsi nilivyoumia na iwapo wangeweza kunibeba.
  2. Nilibebwa na kupelekwa kwenye hema ya kufanyia huduma ya kwanza.
  3. Nililazwa chini na kuhakikishiwa kuwa niko sawa.
  4. Mwalimu alivaa glovu na kuniosha goti na kichwa kwa dawa ya kuua viini.
  5. Baadaye nilifungwa bandeji gotini na kichwani.
  6. Bila kupoteza wakati mwalimu aliagiza ambulensi nikapelekwa hospitalini na kufanyiwa uchunguzi zaidi.
  7. Nilitibiwa majeraha yale, nikapewa dawa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.
    Baada ya maelezo hayo mwalimu na wanafunzi walimpigia makofi kwa kueleza
  1. Kulingana na hatua ambazo Stevo alielezea ni kweli kusema kuwa:
    1. Mtu akiumia hafai kubebwa.
    2. Ni lazima tuwe waangalifu tunapotoa huduma ya kwanza. 
    3. Huduma ya kwanza hufanyiwa hospitalini.
    4. Baada ya huduma ya kwanza majeruhi hupelekwa nyumbani.
  2. Kwa nini mtu hupewa huduma ya kwanza?
    1. Kutibu viungo vilivyovunjika.
    2. Ili kumwezesha kufika hospitalini kupata matibabu.
    3. Ili apone.
    4. Ili aweze kurudi uwanjani acheze.
  3. Tunajifunza nini kutokana na kifungu?
    1. Utaratibu wa kumpa majeruhi huduma ya kwanza 
    2. Jinsi ya kumtibu mtu.
    3. Matibabu ya uwanjani.
    4. Ajali uwanjani.

Swali la 13 hadi la 15

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

G5SWAT1TW23002P4

Siku ya maonyesho ya mapambo shuleni kwetu ilikuwa ya kufana mno. Kila mwanafunzi alikuwa na pambo au mapambo yake ya kuonyesha. Katika maonyesho haya yaliyofanyika katika ukumbi wa shule yetu tulikuwa tukipigwa picha na kuchukuliwa video.

Baadhi ya wanafunzi hasa wasichana walichukua zamu kuonyesha mapambo ya kichwani. Walikuwa wamefunga vibanio nyweleni, wengine walikuwa wamezipaka wanja na wengine kuvaa taji. Masikioni walikuwa na vipuli. Kwenye upande wa pua walivaa vishaufu na kwenye uti wa pua wakavaa vipini. Kuna wengine waliovaa jebu videvuni na kupaka mduwaa midomoni. Baadhi yao walikuwa wamevaa vikuba, mikufu na vidani shingoni.

Wanafunzi wengine walionyesha mapambo ya mikononi, miguuni na kiunoni. Kuna wale waliovalia bangili na saa kwenye viwiko vya mikono, mishipi viunoni na kugesi miguuni. Wengine walikuwa wamejipaka hina mikononi na miguuni. Kama ungewaona wanafunzi siku hiyo hata wewe ungewamezea mate.

  1. Siku inayoelezewa ilikuwa na shughuli gani?
    1. Kupigwa picha.
    2. Maonyesho ya mapambo.
    3. Wasichana kujipamba.
    4. Wavulana kuonyesha mapambo.
  2. Ni pambo gani limeambatanishwa sawasawa na mahali linapovaliwa?
    1. Kipuli - mguuni
    2. Kikuba - mkononi
    3. Kishaufu - puani
    4. Bangili - shingoni
  3. Ungewamezea mate inamaanisha:
    1. Ungefurahia
    2. Ungekasirishwa nao
    3. Ungevaa kama wao
    4. Ungevutiwa nao

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Juma ___16___ nilienda dukani ___17___ mkate.  Mimi kama ___18___ nilimpa muuzaji ___19___ mia moja. Nilipewa mkate ___20___ na kuelekea nyumbani.

   A   B   C   D 
 16.   iliyopita   Lililopita   Kilichopita   aliyepita 
 17.  kununua   kuuza   kuwekeza   kulipa 
 18.  mtaji  bidhaa   mteja   mwekezaji 
 19.  pesa  shilingi   noti   sarafu 
 20.  changu  langu  yangu  wangu

 

Swali la 21-30

SARUFI

  1. Neema amekutana na shangazi yake barabarani asubuhi akielekea shuleni. Je,  atamwamkuaje?
    1. Hujambo
    2. Sabalkheri
    3. Shikamoo
    4. Umeamkaje?
  2. Kati ya nomino hizi ni gani nomino ya pekee?
    1. Kenya
    2. Maji
    3. Uzuri
    4. Meza
  3. Ni kitendawili gani kinalingana na picha hii?
    G5SWAT1TW23002P5
    1. Wafaa lakini wavaliwa bila matumizi maalum.
    2. Ananitazama hasemi hasikii.
    3. Lapendeza rangi lakini halidumu.
    4. Dhahabu yangu ya thamani haisimami.
  4. Ni sehemu gani ya kompyuta imeambatanishwa vizuri na jina lake?
    G5SWAT1TW23002P6
  5. Ni maneno gani yaliyopangwa vizuri kialfabeti?
    1. Saa,saumu, saidia na samaki
    2. Kalamu, karamu, karimu na kaumu
    3. Paa, pesa,pata na pia
    4. Tua, tuzo, tuza na tunu
  6. Kamilisha sentensi hii kwa tashbihi ifaayo: Mjomba alipokuwa akiingia kwenye mlango wa nyumba yetu aliinama kwa sababu yeye ni _______________________
    1. mrefu kama twiga.
    2. mfupi kama nyundo.
    3. mwembamba kama sindano.
    4. mkondefu kama ng'onda.
  7. Badilisha sentensi hii katika ukubwa. Mti uko karibu na mto.
    1. Kijiti kiko karibu na kijito.
    2. MTI UKO KARIBU NA MTO.
    3. Jiti liko karibu na jito.
    4. Miti iko karibu na mito.
  8. Sentensi kama hii huitwaje? " Shirika la reli la Rwanda larejelea shughuli zake rasmi.
    1. Silabi
    2. Konsonanti
    3. Irabu
    4. Kitanzandimi
  9. Kanusha sentensi hii: Umepewa huduma ya kwanza.
    1. Hujapewa huduma ya kwanza.
    2. Mmepewa huduma ya kwanza.
    3. Hutapewa huduma ya kwanza.
    4. Hukupewa huduma ya kwanza.
  10. Kati ya methali hizi ni gani haihusu malezi?
    1. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
    2. Mtoto wa nyoka ni nyoka.
    3. Mtoto hutazama kisogo cha nina.
    4. Haraka haraka haina baraka.

MARKING SCHEME

  1. C
  2. D
  3. B
  4. A
  5. C
  6. B
  7. B
  8. C
  9. A
  10. B
  11. B
  12. A
  13. B
  14. C
  15. D
  16. B
  17. A
  18. C
  19. B
  20. D
  21. D
  22. A
  23. D
  24. C
  25. B
  26. A
  27. C
  28. D
  29. A
  30. D

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5  

Asanyo: Hujambo Matoke? Naqna una haraka ama vipi?
Matoke:  Sijambo. Ndiyo nina haraka. Naelekea sokoni na kazi ya kuwalisha kuku yaningoja nyumbani
Asanyo: Ina maana kuwa unapata pesa nyingi sana.
Matoke:  Pesa zatoka wapi? Nimetumwa mboga sokoni na pia viungo vingine.
Asanyo: Nikifanya kazi yoyote nyumbani lazima nilipwe. Nikitumwa nalipwa. Kama silipwi naenda kurandaranda mtaani.
Matoke:  Huko ni kukosa busara na wavyele wako husemaje?
Asanyo: Hawana neno. Nikifanya kosa lolote hawawezi kuniadhibu.
Matoke:  Laiti wavyele wako wangalijua kuwa mchelea mwana kulia, hulia mwenyewe kwaheri.

  1. Matoke alikuwa anaelekea wapi?
    1. Dukani
    2. Nyumbani
    3. Sokoni
    4. Mtaani
  2. Kulingana na mazungumzo haya
    1. Asanyo ni mtoto mchafu
    2. wavyele wa Asanyo wanampenda
    3. matoke huwatii wavyele wake
    4. matoke hapendi kufanya kazi
  3. Neno wavyele limetumika kwenye kifungu lina maana gani?
    1. Wazazi
    2. Ndugu
    3. Marafiki
    4. Familia
  4. "Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe" huu ni mfano wa?
    1. Msemo
    2. Kitendawili
    3. Fimbo
    4. Methali
  5. Ni sahihi kusema _______________________
    1. pesa hufanya mtoto afanye kazi nyumbani
    2. wavyele wanastahili kuwaadhibu wanao
    3. kurandaranda mitaani ni jambo muhimu
    4. kukosa busara ni jambo muhimu

Soma shairi hili kisha ujibu maswali

Nakupongeza mlezi, shuleni kunipeleka
Chakula nacho kanipa, karo pia kalipa
Mpendwa watapatapa, mimi hapa nikicheka
Pongezi mlezi wangu, kazi njema waifanya

Kanionya kaonyeka, za kulevya nikahepa,
Mbaya tabia nikaacha, masomoni, nikangara
Jukumu nilijitweka, ushauri ulionipa
Pongezi mlezi wangu, kazi njema waifanya

  1. Hili ni shairi la aina gani?
    1. Tarbia
    2. Tathlitha
    3. Tasdisa
    4. Takhmisa
  2. Shairi hili lina beti ngapi?
    1. Tatu
    2. Nane
    3. Nne
    4. Mbili
  3. Kila ubeti una mishororo mingapi?
    1. Miwili
    2. Mitatu
    3. Mmoja
    4. Minne
  4. Shairi hili linatufunza kuwa
    1. tuwalaani wazazi
    2. tupongeze wazazi
    3. tusome kwa bidii
    4. tupate mihadarati
  5. Kibwagizo cha shairi hili ni
    1. Nakupongeza mlezi, shuleni kanipeleka
    2. Kanionya kaonyeka, za kulevya nikahepa C
    3. Pongezi mlezi wangu, kazi njema waifanya
    4. Mbaya tabia nikaacha, masomoni nikangara.

Soma mtungo ufuatao kisha ujaze nafasi zilizoachwa 11-15.

Kaka ___11___ ni mzuri. Yeye ni ___12___.Anapenda kuvaa nguo ___13___ na viatu vyeusi. Kwake viatu vyote ni vizuri. Mimi huvaa viatu vikubwa ___14___ kuviweka pahali ___15___ hawezi kufikia viatu vikubwa vinaweza kuumiza vibaya.

   A   B   C   D 
 11.    yangu   zangu   wetu   wangu 
 12.  mupole   pole   mpole   mbole 
 13.  zeupe  nyeupe   eupe    mweupe 
 14.  na  pa   ya   za 
 15.  ambapo   ambao  ambazo   ambayo

 

Chagua jibu sahihi kujibu maswali 16-30.

  1. Kamilisha methali: Kinga na kinga __________________________
    1. hukingana
    2. ndio ujao
    3. ndipo moto uwakapo
    4. huona makuu
  2. Yeye ni mwenye maringo kama 
    1. samaki
    2. tausi
    3. kunguru
    4. malaika
  3. Wingi wa sentensi hii ni. Tunda hili ni tamu
    1. Tunda haya ni matamu
    2. Matunda haya ni yamu
    3. Matunda haya ni matamu
    4. Matunda hizi ni tamu
  4. Bibi harusi alikuwa amebeba __________________ la maua.
    1. shada
    2. kipeto
    3. shungi
    4. doti
  5. Kanusha. Mama atapika wali kesho
    1. Mama hakupika wali kesho
    2. Mama hatapika leo
    3. Mama hatapika wali kesho
    4. Mama hakupika wali kesho
  6. Tegua kitendawili: Huku ngo na huko ng'o
    1. Giza
    2. Uyoga
    3. Ndoto
    4. Fua
  7. Neno jino liko katika ngeli ya
    1. A - WA
    2. LI - YA
    3. U - ZI
    4. U - U
  8. Wao ________________ waliocheza na kutuzwa.
    1. ndio
    2. ndiye
    3. ndiyo
    4. ndizo
  9. Jibu la salamu 'Alamsiki' ni ____________________
    1. binuru
    2. tunayo
    3. nawe pia
    4. ya kuonana
  10. Ukubwa wa neno mlango ni
    1. jilango
    2. kilango
    3. lango
    4. kijilango
  11. Umbo lifuatalo huitwa ______________________________
    G4SWAT1SF23002Q25
    1. pia
    2. mche
    3. duara
    4. duaradufu
  12. Chagua nomino ambata
    1. Mweka hazina
    2. Mwanambee
    3. Sungura
    4. Mchezaji
  13. Tumia amba ipasavyo
    Mwanafunzi _________________ hufaulu huwa na bidii
    1. ambao
    2. ambaye
    3. ambayo
    4. ambazo
  14. Jua hutua wakati wa ______________________
    1. mashariki
    2. magharibi
    3. alasiri
    4. adhuhuri
  15. Mnene kama _____________________
    1. nyundo
    2. sindano
    3. nguruwe
    4. ndovu

SEHEMU YA B: INSHA   

Andika insha ya kusisimua kuhusu mada ifuatayo.

SAFARI ILIYOPENDEZA   

MARKING SCHEME

  1. C
  2. C
  3. A
  4. D
  5. B
  6. A
  7. D
  8. D
  9. B
  10. C
  11. A
  12. C
  13. B
  14. A
  15. A
  16. C
  17. B
  18. C
  19. A
  20. C
  21. A
  22. B
  23. A
  24. A
  25. C
  26. D
  27. A
  28. B
  29. B
  30. C

Jaza pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi kutoka nambari 1 mpaka 5. 

Siku ___1___ mwalimu aliingia ___2___ mwetu ili atufunze somo tulipendalo ___3___ Kiswahili. Kila mwanafunzi alitoa ___4___ yake ili aangalie jinsi maneno yanavyofuatana na yanavyoendelezwa ___5___ ya somo mwalimu aliondoka na kuelekea majilisini. 

   A   B   C   D 
 1.   moja   mmoja   pamoja   kimoja 
 2.  nyumbani   kanisani   darasani   majilisini 
 3.  cha  la  na  kwa
 4.  penseli  sare  dawati  kamusi
 5.  Baada  Kabla  Chini  Kando


Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6- 10 

Nchi yetu ya Kenya ina Kaunti 47. Kaunti hizo ni kama vile Nyandarua, Kisumu, Taita Taveta na Garissa. Kila kaunti huongozwa na Gavana pamoja na naibu wake. Kila kaunti huwa na bendera tofauti na nyingine lakini bendera ya taifa hupeperushwa kwenye kaunti zote. Bendera ya taifa letu ina rangi nne. Rangi inayopatikana juu kwenye bendera ni nyeusi ambayo ni ya ngozi yetu. Rangi nyeupe hutenganisha rangi nyeusi, nyekundu na kijani. Nyekundu ardhi hutukumbusha damu iliyomwagwa na wapigania uhuru, nayo kijani ni ya ardhi yenye mimea. Rangi nyeupe ni ya amani. Tulipopata uhuru, Mkenya mmoja kutoka kaunti ya Makueni aliipandisha bendera kwenye Mlima Kenya kama njia mojawapo ya kusherehekea uhuru. Alituzwa na serikali kwa ushujaa na uzalendo wake kwani haikuwa rahisi kuipandisha bendera. Mkenya huyo alikuwa akiitwa Kisoi Munyao. 

  1. Mkenya aliyeipandisha bendera kileleni mwa Mlima Kenya alikuwa mzaliwa wa kaunti gani?
    1. Garissa
    2. Makueni 
    3. Nairobi
    4. Nyandarua
  2. Ni rangi gani ya bendera inayotenganisha rangi ya kijani na nyekundu kwenye bendera ya taifa la Kenya?
    1. Manjano
    2. Nyeusi 
    3. Samawati
    4. Nyeupe
  3. Nchi ya Kenya ina kaunti ngapi kulingana na taarifa uliyoisoma?
    1. Sabini na saba 
    2. Arubaine na sita.
    3. Arobaine na saba. 
    4. Nne
  4. Kwa nini Kisoi Munyao aliipandisha bendera kwenye kilele cha Mlima Kenya?
    1. Ili atuzwe na serikali. 
    2. Alikuwa mzalendo. 
    3. Ilikuwa njia ya kusherehekea uhuru.
    4. Ili awe shujaa.
  5. Ni kweli kusema,
    1. Kisoi Munyao alikuwa mpigania uhuru.
    2. Kila Kaunti nchini Kenya ina bendera yake.
    3. Bendera ya Kenya hutukumbusha kuhusu Mlima Kenya.
    4. Serikali ya Kenya haikumtuza Mkenya aliyeipandisha bendera mlimani.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 11 - 15 

Hapo zamani za kale Twiga na Fisi walikuwa marafiki wa dhati. Walisaidiana kwa kila hali. Watoto wao walicheza na kutembeleana bila pingamizi zozote. Siku moja mwanawe Twiga aliugua homa ya mapafu. Fisi aliamua kumpa mtoto wa Twiga dawa za kienyeji ili apone. Kwa bahati mbaya mtoto huyo alikufa. Fisi alishikwa na tamaa na akamla mtoto aliyekufa baada ya kumdanganya Twiga ya kwamba amemzika kaburini. Baada ya uchunguzi kufanywa, ilibainika wazi kuwa fisi alimpa mtoto wa Twiga dawa mbaya ili afe naye amle. Bweha aliyekuwa kiongozi wa mashtaka alimhukumu Fisi kifungo cha maisha gerezani. Tangu siku hiyo urafiki wa Fisi na Twiga uliisha na wakawa maadui. 

  1. Kwa nini Fisi alipanga njama ya kumuua mtoto wa Twiga? Ili 
    1. urafiki wake na Twiga uishe. 
    2. afe naye amle. 
    3. ahukumiwe na Bweha. 
    4. augue homa ya mapafu. 
  2. Ni nani aliyetoa hukumu? 
    1. Fisi 
    2. Twiga 
    3. Mwanawe Twiga 
    4. Bweha 
  3. Wanyama wangapi wametajwa kwenye hadithi
    1. 3
    2. 5
    3. 4
    4. 2
  4. Kulingana na kifungu ulichokisoma, Fisi ana tabia zifuatazo isipokuwa 
    1. mlafi 
    2. mdanganyifu
    3. mwenye tamaa
    4. mwaminifu.
  5. Hadithi hii inatufunza nini?
    1. Tuwatibu wagonjwa.
    2. Tucheze na watoto wengine.
    3. Tujihadhari na marafiki waovu.
    4. Tuwe maadui kwa watu wote. 

KutokÄ… swali la 16 hadi la 28 chagua jibu lifaalo zaidi kulingana na maagizo uliyopewa

  1. Andika katika hali ya ukubwa.
    Mti:
    1. Kijiti
    2. Vijiti
    3. Jiti
    4. Miti
  2. Andika katika hali ya kukanusha: Ameadhibiwa na mwalimu.
    1. Wameadhibiwa na walimu.
    2. Hajaadhibiwa na mwalimu.
    3. Hataadhibiwa na mwalimu.
    4. Hakuadhibiwa na mwalimu.
  3. Kamilisha tashbihi hii:  Nyeupe kama
    1. nguruwe.
    2. mlingoti
    3. karatasi.
    4. theluji.
  4. Jaza nafasi kwa kutumia kinyume cha nomino iliyopigiwa mstari.
    Joto na _________________ nyingi zinaweza kusababisha magonjwa kwa watoto
    1. mwangaza
    2. baridi
    3. upepo
    4. vumbi
  5. Geuza kitenzi hiki katika hali ya kutendwa. Batiza
    1. batizika. 
    2. kubatiza
    3. batizwa. 
    4. kutobatiza. 
  6. Kisawe cha neno barua ni 
    1. ishara. 
    2. tarakilishi
    3. baraste. 
    4. waraka. 
  7. Tambua kitenzi katika sentensi hii:
    Beba mzigo huo jioni. 
    1. mzigo
    2. huo
    3. beba
    4. jioni
  8. Badala ya kusema "Mtoto anahara tunafaa kusema: Mtoto
    1. ameenda msalani. 
    2. anaendesha. 
    3. ni mja mzito.
    4. amepoa. 
  9. Tegua kitendawili:
    Nyanya anapepeta mpunga.
    1. Jua
    2. Kaptura.
    3. Upepo. 
    4. Kope
  10. Jibu salamu hizi:
    Waambaje?
    1. Marahaba. 
    2. Sina la kuamba
    3. Vizuri.
    4. Sabalkheri.
  11. Nomino gani inapatikana katika ngeli ya LI-LI 
    1. Jengo
    2. Giza
    3. Jiwe
    4. Yai
  12. Pete ni kwa kidole kama vile __________________________ ni kichwani.
    1. kipuli
    2. hina
    3. mkufu
    4. taji
  13. Tumia nomino za makundi kujaza nafasi. 
    Mama amenunua  ____________________ la maembe sokoni.
    1. pakacha
    2. tita
    3. jozi 
    4. biwi 

Soma barua hili kisha ujibu maswali 29-30 

Kisa Hadija
S.L.P. 34
KIBANZI 
14/02/2023 

Kwa rafiki Musa, 

Pokea salamu nyingi kutoka kwangu na marafiki zangu. Natumai u mzima. Nakuandikia barua hii kukujulisha kwamba mjomba Kioko amepata nafuu. Daktari amemshauri ale chakula chenye lishe bora ili mwili wake upate nguvu. Wajulishe wazazi wako habari hii njema. Kwaheri ya kuonana. Wasalimie ndugu zako Sankare na Bosco. 

Wako umpendaye,
Kisa Hadija.

  1. Nani mwandishi wa barua hii? 
    1. Musa
    2. Kisa Hadija
    3. Sankare
    4. Kioko
  2. Barua hii ina anwani ngapi?
    1. Moja.
    2. Nne
    3. Tatu.
    4. Mbili 

INSHA 

Andika insha ya kuhusisimua kuhusu

SAFARI YA MJINI. 

MARKING SCHEME

  1. A
  2. C
  3. B
  4. D
  5. A
  6. B
  7. D
  8. C
  9. D
  10. C
  11. B
  12. D
  13. C
  14. D
  15. C
  16. C
  17. B
  18. D
  19. B
  20. C
  21. D
  22. C
  23. B
  24. D
  25. B
  26. B
  27. D
  28. A
  29. B
  30. D

Jaza mapengo kwa kutumia jibu sahihi.

Kadala ni mwanafunzi ___1___. Badala ___2___ kuwasikiliza walimu ___3___, yeye hupendelea kufanya utukutu. Jana mwalimu mkuu alimpa onyo ___4___ mwisho. Alimwambia aende nyumbani akamlete baba ___5___.

   A   B   C   D 
 1.   mtukutu   kitukutu   litukutu   matukutu 
 2.  za  cha  la  ya
 3.  yake  wake  chake  lake
 4.  ya  za  cha  la
 5.  zake  chake  lake  yake

 

Andika sentensi zifuatazo kwa wingi.

  1. Mtu amenunua chungu kingine.
  2. Mkate utaliwa na mtoto.
  3. Kiatu cha mtoto kimeshonwa.

Andika kinyume cha maneno haya.

  1. Kijana
  2. Maskini
  3. Baba

Tunga sentensi ukitumia majina uliyopewa.

  1. kalamu yake __________________
  2. mbegu _________________

Jaza mapengo kwa usahihi.

  1. Yupi kati ya hawa si mnyama wa porini? _______________________________
    (Tembo, Ngedere, Punda)
  2. Chagua neno lisilo tunda.
    _________________________
    (Parachichi, Tikitimaji, Zabibu, Viazi)
  3. Tunatumia kinu na ___________________ kutwangia nafaka. (mchi, mafiga, mwiko)

UFAHAMU
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali.

Hadija si tabia yake kufuatana na watu wenye tabia mbaya. Lakini siku moja alikata kauli kwenda katika sherehe za sikukuu ya Madaraka. Aliaandamana na watu vichwa maji. Watu hao walimcheka kila mahali. Wengine walisukumana hata na mama wajawazito waliwatisha watoto wadogo na kuwangurumia kama simba. Watoto walilia na kukimbia ovyo. Watu wengine walitoa sigara walizozificha mifukoni wakavuta. Hadija alichukia kile kitendo cha watu hao. Alichukia nywele zao chafu zilizosokotana kama manyoya ya kondoo. Aliyachukia mavazi yao yasiyo na adabu. Baada ya sherehe wanafunzi hao walirudi shuleni. Hadija alienda moja kwa moja hadi kwa mwalimu mkuu. Uchunguzi ulifanywa na ukweli wote ulipatikana, watukutu, wajeuri na vichwa maji waliadhibiwa.

  1. Hadija alipatana wapi na watu wenye tabia mbaya?
    1. Shuleni.
    2. Akjenda nyumbani.
    3. Sherehe za sikukuu.
    4. Nyumbani wakicheza.
  2. Hadija aliandamana na watu
    1. wazuri
    2. wenye bidii
    3. vichwa maji
    4. watiifu

Andika tabia mbili mbaya watu hawa walifanya.

  1. ____________________________
  2. ____________________________
  3. Watu wengine walitoa sigara walizoficha mifukoni na
    1. kuficha
    2. kuvuta
    3. kutupa
    4. kumpa Hadija.
  4. Kwa nini Hadija alienda kwa mwalimu mkuu? 
  5. Je, wafikiria maana ya vichwa maji ni gani?

UFAHAMU
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali.

MUGUMO

Miti ina faida nyingi kwetu sisi wanadamu. Hutupatia matunda, mbao, kivuli na hata kuvuta mvua. Nchi isiyokuwa na miti hubadilika na kuwa jangwa. Hii ndiyo sababu ya kuwa na siku maalumu ya kupanda miti kila mwaka.

Babu zetu walikuwa na njia yao ya kuzuia ukataji wa miti. Watoto wadogo walitolewa hadithi za kuwafanya waogope kuikata miti fulani. Miti kama mugumo una hadithi nyingi kama hizo. Hii ni kwa sababu ulitumiwa na makabila mengi kutolea sadaka kwa Mungu.

Hadithi moja inahusu mtu mmoja aliyeishi katika kijiji kilichoitwa Makongo. Jina lake lilikuwa Tangawizi. Watu wa kijiji cha Makongo walimchukia Tangawizi kwa sababu ya kukata miti ovyo. Walijaribu kumzungumzia lakini aliendelea kuikata miti.

"Miti ni mali ya Mungu," aliwaambia. Siku moja, Tangawizi aliondoka nyumbani kulipopambazuka, shoka mkononi na kuuendea mugumo uliotumiwa na watu wa kijiji cha Makongo kutolea sadaka kwa Mungu.

"Watatafuta mahali pengine pa kutolea sadaka," alisema na kuanza kuukata. Lakini kabla ya kuendelea sana, damu ilianza kutoka katika sehemu aliyoikata. Mara aliisikia sauti kubwa kutoka kwa mugumo huo.
Tangawizi!.... Tangawizi!...... Tangawizi!
Kwa vile wataka kuniua, mimi nitakuadhibu.
Kutoka leo, utakuwa kipofu hadi kufa.
Macho ya Tangawizi yalijifunga na akawa kipofu hadi kufa kwake.

  1. Taja faida moja ya miti kama zilivyozungumziwa katika hadithi.
  2. Nchi isiyokuwa na miti hubadilika na kuwa nini?
  3. Muguro una hadithi nyingi kwa sababu gani?
    1. Ni mti mkubwa sana.
    2. Ni mti unaoweza kuongea.
    3. Ulitumiwa kutolewa sadaka kwa Mungu.
    4. Uliwapa watu matunda.
  4. Aliyekwenda kuukata Mugumo alikuwa na nini?
    Taja vitu viwili vilivyofanyika mti ulipoanza kukatwa.
  5. _________________________________
  6. _________________________________
  7. Tangawizi aliadhibiwa aje na mugumo?
    1. Alichapwa.
    2. Alikatwa mkono.
    3. Alikuwa zuzu.
    4. Alikuwa kipofu

INSHA  

Andika Insha kuhusu:

NYUMBANI KWETU   

MARKING SCHEME

  1. A
  2. D
  3. B
  4. D
  5. D
  6. Watu wamenunua vyungu vingine.
  7. Mikate italiwa na watoto.
  8. Viatu vya watoto vimeshonwa.
  9. mzee
  10. Tajiri
  11. mama
  12. Sentensi sahihi
  13. Sentensi sahihi
  14. punda
  15. viazi
  16. mchi
  17. C
  18. C
  19. Wato hao walimcheka kila mahali.
  20. Watu wengine walitoa sigara walizozificha mifukoni wakavuta
  21. B
  22. Kupiga ripoti
  23. Watu wenye tabia mbaya.
  24. Hutupatia matunda, mbao, kivuli na hata kuvuta mvua.
  25. jangwa
  26. C
  27. Tangawizi
  28. Damu ilianza kutoka
  29. Alisikia sauti kubwa
  30. D

MASWALI

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne
Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Kusikiliza na kuongea ni stadi muhimu____1____kwa mwanafunzi__2__zinaimarisha usikivu na uelewaji mzuri wa mambo mbalimbali __3__hizi pia humtayarisha mwanafunzi ___4___ na kuyaendeleza maneno ya lugha hii ___5___Zinakusudiwa kumpa mwanafunzi ___6___ wa kujieleza bila woga. ___7___, ni sharti zifundishwe ____8____.

  1.                            
    1. katika
    2. kwa
    3. kwenye
    4. ndani ya
  2.                
    1. kwa kuwa
    2. sana sana
    3. ama kweli
    4. kwa kweli
  3.                      
    1. Maoni
    2. MienendoMbinu
    3. Uerevu
  4.                
    1. kuandika
    2. kutamka
    3. kusemewa
    4. kusoma
  5.              
    1. vizuri
    2. nzuri
    3. mzuri
    4. wazuri
  6.              
    1. bidii
    2. ujasiri
    3. uzembe
    4. mbinu
  7.                
    1. Kwa hivyo
    2. Hata hivyo
    3. Mbali na hayo
    4. Kinyume na hivyo
  8.                    
    1. wanavyofaa
    2. wanavyohitajika
    3. vile inahitajika
    4. Kinavyohitajika

Gari___9___aina ya Mwamba ___10___ kwenye maskani ya kina Asmini, wengi wa wakazi waliingiwa na ___11___ wasijue la kufanya. Waama, wasiwasi huo wote ulitokana na jinsi ___12___ kuwa duni kiasi cha ____13___ na wakwasi wanaonuka pesa. Wasichokijua kilikuwa ni kwamba Asmini alikuwa kampata mfadhili wa kuyagharimia maradhi yaliyomzonga tangu zama za ___14___ hadi siku hiyo. Wallahi, ___15___.

  1.                                            
    1. nyeupe
    2. leupe
    3. jeupe
    4. cheupe
  2.                    
    1. likaingia 
    2. liliingia
    3. lilipoingia
    4. likiingia
  3.                
    1. furaha kuu
    2. huzuni nyingi
    3. aibu kubwa
    4. tumbo joto
  4.                  
    1. walivyojichukua
    2. walichukulia
    3. walivyo
  5.                      
    1. kutembelewa
    2. kutotembeleana
    3. kutembeleana
    4. kutotembelewa
  6.                                            
    1. kali
    2. zamani
    3. kitambo
    4. zama
  7.                                
    1. Mungu hamsahau mja wake
    2. siku ya nyani kufa miti yote huteleza
    3. mficha uchi hazai
    4. pole pole ndio mwendo 

Kutoka swall la 16 hadi 30. Jibu kulingana na maagizo

  1. Vivumishi halisi pia huweza kuitwa vivumishi
    1. vya idadi.
    2. vya pekee.
    3. vimilikishi.
    4. vionyeshi.
  2. Mama ameenda sokoni katika hali ya wingi ni
    1. kina mama wameenda masokoni.
    2. mama wameenda sokoni.
    3. kina mama wameenda sokoni.
    4. mama wameenda masokoni.
  3. Kutokana na kitenzi andika, tunaweza kuunda nomino gani?
    1. Andika.
    2. Barua.
    3. Mwandishi.
    4. Insha.
  4. Chagua majina ya ngeli ya I-ZI pekee.
    1. Chuma, cheo, chupa.
    2. Rula, meza, kalamu,
    3. Nguo, ulimi, zeze.
    4. Darasa, shule, gwaride.
  5. Ni vazi gani kati ya haya huzuia mavazi ya ndani yasichafuke wakati wa kazi?
    1. Bombo.
    2. Kizibao.
    3. Buibui.
    4. Bwelasuti.
  6. Ni barua ya aina gani ambayo huwa na anwani moja? Barua ya
    1. kiofisi.
    2. kindugu.
    3. marafiki.
    4. kidugu.
  7. Teua sentensi yenye kivurishi cha sifa.
    1. Watu wanane wameangamia.
    2. Mwanafunzi yule ni mweledi.
    3. Maembe haya ni mabichi.
    4. Niletee kalamu nyingine.
  8. Tumia kiulizi ngapi. Marealiwa peremende
    1. mangapi?
    2. ngapi?
    3. mingapi?
    4. vingapi?
  9. Eleza matumizi ya ki.
    Sakina amekichapa kitoto chake.
    1. Masharti.
    2. Ngeli
    3. Udogo
    4. Kiwakilishi.
  10. Ni sehemu gani hupatikana shingoni?
    1. Ndewe.
    2. Kidakatonge
    3. Kiwiko.
    4. Kigasha.
  11. Jibu maamkizi yafuatayo:
    U mzima?
    1. Ni mzima.
    2. Tu mzima.
    3. Si wazima.
    4. Ni wazima.
  12. Akisami, 4/9 huitwaje kwa maneno?
    1. Robo tisa.
    2. Subui nne.
    3. Tusui nne.
    4. Sudusi nne.
  13. Kanusha sentensi ifuatayo:
    Yaya anapiga deki. Yaya
    1. hapigi deki.
    2. hajapiga deki.
    3. hakupiga deki.
    4. hatapiga deki.
  14. Dakika moja huwa na jumla ya sekunde ngapi?
    1. Sitini.
    2. Tisini.
    3. Arubaini na tano.
    4. Thelathini.
  15. Aliye na mtoto tumboni ni
    1. mtu mzito.
    2. mjamzito.
    3. mama.
    4. mimba

Soma kifungu kisha ujibu maswali 31 hadi 40.
Kila baada ya mtihani wa kitaifa kufanywa na matokeo kutangazwa rasmi na wanaohusika. huwa jambo la kawaida kuwaona wadau mbalimbali wakishangilia na kusherehekea matokeo ya bidii za wana wao na wanafunzi wao. Aghalabu, utawaona waliovuna pakubwa wakiinuliwa hanga hanga na kurushwarushwa hewani ovyo ovyo kwa kile ambacho kwa wakati huo huitwa shamrashamra za kusherehekea ubingwa wa wanafunzi.
Aidha, katika barabara za mengi ya majiji na hata viungani, ni kawaida kuyaona magari ya manjano yakiongozana kwa milolongo huku "abiria" wakishangilia kwa shangwe, vifijo na cherekochereko. Ni kawaida pia kuyaona majina ya mabingwa wa shule mbalimbali yakiwa yamebandikwa ubavuni pa magari hayo katika karatasi pana angavu. Hakika, wakati huo huwa wakati wa kuvuna alichokipanda mpanzi. Waama, ukipanda pantosha, utavuna pankwisha.
Iwapo waliotia fora hustahili kushangiliwa hivyo na kuinuliwa hainehaine, je, wenzao ambao walikuwa na matokeo ya wastani au wale waliokuwa na alama zisizoridhisha hustahili zawadi gani? Si nao waliufanya mtihani huo huo? Ifahamike kuwa wanafunzi mbalimbali kote nchini hufanya mtihani mkuu wa kitaifa katika mandhari tofauti tofauti. Ni kweli kuwa baadhi yao hufanya mtihani huo wakiwa wodini na hata vizuizini. Wakati mwanafunzi mmoja analifurahia joto la darasa na mapochopocho wakati wa mafunzo, mwengine kwingine anangurumwa na tumbo huku akivumilia baridi shadidi chini ya mti, sehemu anayoiita darasa, ilhali wote wanausubiri mtihani huo huo. Kuna uwezekano wa wanafunzi wanaosoma katika mazingira magumu kufanya vizuri iwapo hali ya maisha itakuwa sawa kwa watahiniwa wote.
Kwa upande mwingine, si jambo la kawaida kuwaona walimu waliowaandaa wanafunzi wanaofuzu wakiangaziwa katika vyombo vya habari. Ama wanafunzi hawa hujielimisha wenyewe? Aghalabu, shule zao, baadhi ya watu wa familia zao na wao wenyewe ndio wapatao umaarufu. Ajabu ni kuwa, umaarufu huu huwa kama moto wa karatasi ambao haukawii kuzima. Hivi ni kwa sababu, pindi wafikapo sekondari, umaarufu wao hupotea na kuzima mfano wa kibatari kilichotumbukizwa majini ghafla. Hakuna ajuaye hali ya elimu yao katika shule za upili. Mwisho, heko kwa serikali hii ya tano kupitia Wizara ya Elimu kuibua mtindo mpya wa kuyatangaza matokeo baada ya kuyafanyia kazi kwa kipindi kifupi cha muda. Siku hizi ni mshindi tu ndiye atangazwaye, tena bila jina lake bali alama zake tu, kinyume na hapo awali ambapo majina ya wanafunzi, shule zao na alama zao yaliwekwa wazi.
Kaa Salama-Nawa mikono na uvae barakoa!

  1. Kwa mujibu wa aya ya kwanza.
    1. sherehe hupamba moto wakati wa mtihani mkuu wa kitaifa.
    2. walimu huhusika katika kutangaza matokeo ya mtihani wa kitaifa
    3. ubingwa wa baadhi ya wanafunzi katika mtihani mkuu hushangiliwa.
    4. magari mengi hufuatana kama njia ya kusherehekea matokeo ya wanafunzi.
  2. Kwa maoni yako, wanaohusika ni kina nani?
    1. Wizara ya Elimu.
    2. Walimu wakuu katika shule zilizofuzu.
    3. Viongozi wakuu serikalini.
    4. Wanafunzi waliotia fora katika mtihani mkuu.
  3. Mwandishi ametaja namna ngapi za kuwashangilia wanafunzi waliofanya vizuri? 
    1. Tatu.
    2. Nne.
    3. Moja.
    4. Mbili.
  4. Methali iliyotumika mwishoni mwa paragrafu ya pili inamlenga nani hasa?
    1. Mwanafunzi katika shule ya msingi.
    2. Walimu waliofanya bidii kuwafunza wanafunzi waliotia fora.
    3. Mwanafunzi ambaye ameukamilisha mtihani mkuu.
    4. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
  5. Mwandishi anatudokezea kuwa wanafunzi waishio katika mandhari duni wakipata mandhari nafuu,
    1. ushindani utaimarika baina ya makundi haya mawili.
    2. wanaweza kufanya vyema zaidi katika mitihani.
    3. watawashinda wale wanaioshi katika mazingira salama.
    4. hali ya kielimu inaweza kuimarika maradufu.
  6. Taarifa imeweka wazi kuwa si jambo la kawaida
    1. walimu wa wanafunzi waliofuzu kuangaziwa.
    2. wazazi wa wanafunzi waliofaulu kuangaziwa.
    3. wanafunzi waliotia fora kuangaziwa.
    4. shule za wanafunzi waliofaulu kuangaziwa.
  7. Inawezekana kuwa wanafunzi wanaofanya mtihani mkuu wakiwa wodini huwa
    1. wauguzi.
    2. wahalifu.
    3. wagonjwa.
    4. washukiwa.
  8. Kidokezi ngarafu huu huwa kama mote wakeratasi ambao haukawii kuzima kinatoa wazo gani?
    1. Wanafunzi wanaofanya vizuri katika shule za msingi hupotea pindi wafikapo sekondari
    2. Baadhi ya wanafunzi huwa hawafanyi vizuri sekondari ama walivyofanya katika shule za msingi.
    3. Majina ya wanafunzi waliofuzu katika shule za msingi husahaulika wavukapo daraja.
    4. Wanafunzi waliotia fura katika shule za msingi huanza kuwa mazuzu.
  9. Msimulizi anaipa serikali ya tano mkono wa tahania kwa
    1. kuorodhesha majina ya wanafunzi waliotia fora.
    2. kuongeza muda wa kuhakiki matokeo ya mtihani mkuu.
    3. kuzua namna mpya ya kupeperusha matangazo ya matokeo ya mtihani mkuu.
    4. kupanga matokeo ya mtihani mkuu kulingana na kaunti.
  10. Hapo awali
    1. matokeo ya mtihani mkuu yalishughulikiwa kwa muda mfupi.
    2. majina na shule za wanafunzi yaliorodheshwa sambamba na alama zao.
    3. alama za mwanafunzi bora tu ndizo zilizotangazwa.
    4. wanafunzi wote waliofanya mtihani nchini waliangaziwa 

Soma kifungu kisha ujibu maswali 41 hadi 50.
Sherehe nyingi kupita kiasi na anasa yalikuwa yamepita mpaka katika mji wa Peponi. Ingawa walikuwa na bidii kuliko za mchwa, mapato yao na mali waliyochuma yaliishia katika vileo haramu na sehemu nyinginezo za anasa.
Si hayo tu, mjini humo alitokea kidosho mmoja aliyekuwa na aina mpya ya kileo alichokiuza kisirisiri kwani kilikuwa haramu. Kileo hicho kiliwavutia sana wengi hususan wanaume ambao kila wakati walimwita kando ili awauzie pombe hiyo mpya. Siku zilizidi kusonga huku waliokionja kileo hicho wakawaita wenzao nao wapate kukionja bila kujua kuwa kileo hicho kilikuwa haramu na chenye sumu. Daima walijipa moyo kwa ule usemi usemao, kiingiacho mjini si haramu. Ole
wao!
Wave's wachanga walipopata ripoti kuhusu pombe ile mpya na kile walichokiita utamu wake, walijaribu kadiri walivyoweza ili angalau wapate fursa ya kuionja. Waliifurahia mno. Nyumbani kowe Bwana Chachandu, alikuwapo mwanawe aliyeitwa Sheshe na yaya aliyekuwa na jukumu la kumshughulikia kitindamimba katika familia hiyo, Majaliwa. Daima, Puza alimshughulikia Majaliwa bila kununa. Bwana Chachandu alipopata habari za kileo kile kipya, hakutaka kuachwa nyuma. Naye alipata fursa ya kukionja na hata kujibebea kiasi katika chupa ndogo ya plastiki. Si hunenwa kuwa akiba haiozi! Chachandu alilifahamu hili barabara.
Chachandu alipofika nyumbani, alimlazimisha Puza kukionja kileo kile. Ingawa Puza alijaribu kukataa, alitishiwa kuadhibiwa ikambidi naye apate kukionja kileo kile. Angurumapo simba hucheza nani? Siku mbili tatu, Puza alinyatia na kuichukua pombe iliyosalia chupani na kumwonjesha Sheshe. Bwamdogo alipokionja kileo kile, alifurahia mno.
Baada ya muda, ilifahamika kuwa pombe yenyewe haikuwa salama mwilini. Walioshiriki pombe hiyo walianza kufariki mmoja mmoja. Mama wa Majaliwa alipopata habari hizo, aliamua kuwaita waganga na waganguzi maana dalili mbaya zilianza kuonekana kwake nyumbani. Baada ya mama wa Majaliwa kushawishiwa na mumewe, naye akaonjeshwa kileo kidogo kilichokuwa kimebaki.
Baada ya kipindi cha muda, madhara ya pombe ile yalikuwa yamekolea mno mjini mote. Maskini nyumbani mwa Bwana Chachandu akabakia mmoja tu. Wengine wakasafiri jongomeo.

  1. Licha ya yaya, familia ya kina Majaliwa ilikuwa na watu wangapi?
    1. Watano
    2. Watatu
    3. Sita
    4. Wanne
  2. Kulingana na taarifa, ni kauli gani ni ya kweli?
    1. Mzee Chachandu alipewa pombe n mjakazi.
    2. Mjakazi alimpa S..she kileo hatari.
    3. Puza alipewa kileo hatari ne kidosho.
    4. Bi. Chachandu alijaribu kukataa kunywa pombe akalazimishwa.
  3. Wakazi wengi wa Peponi
    1. hawakuwahi kupatikana baani.
    2. hawakuwa walevi.
    3. hawakushiriki michezo sana sana.
    4. hawakupenda raha kupita kiasi.
  4. Ni kwa nini Puza alikipokea kileo cha sumu?
    1. Alitishiwa.
    2. Aliadhibiwa.
    3. Alikuwa akikitaka.
    4. Alikuwa akikitamani.
  5. Ni kundi gani kati ya haya lilifurahi mno baada ya kupata taarifa kuhusu pombe ya kigeni? Vijana
    1. wote.
    2. wa kike.
    3. wa kiume.
    4. kwa wazee.
  6. Mtoto wa mwisho katika familia ya Bwana Chachandu alikuwa nani?
    1. Sheshe.
    2. Puza.
    3. Kidosho.
    4. Majaliwa.
  7. Kulingana na makala haya, ni yupi alikuwa yaya?
    1. Sheshe.
    2. Puza.
    3. Majaliwa.
    4. Kidosho.
  8. Ni bwamdogo gani aliyerejelewa katika ufahamu?
    1. Sheshe.
    2. Puza.
    3. Majaliwa.
    4. Chachandu.
  9. Kwa maoni yako, ni yupi kati ya hawa hakufariki kutokana na kileo hatari?
    1. Puza.
    2. Chachandu.
    3. Mama wa Majaliwa.
    4. Majaliwa.
  10. Mwishoni, mwandishi anatueleza kuwa, licha ya mmoja, wengine wote
    1. walienda safari ya mbali.
    2. waliugua sana.
    3. waliaga dunia.
    4. waliathirika zaidi.

MARKING SCHEME

swa addada

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.
Endeleza insha ifuatayo kwa maneno yake mwenyewe na ulfanye iwe va kusisimua.
Sote tulikuwa na furaha mpwitompwito kutia guni katika darasa la nane. Asubuhi hiyo, kipindi cha kwanza kilikuwa cha Kiswahili. Mwalimu alipoingia darasani........................................................................

 

Tagged under

Jaza nafasi zilizoachwa wazi kuanzia 1 - 15 kukamilisha vifungu vifuatavyo:-

Nina uhakika __1__ mwendo wa usiku wa manane hivi. Mlio wa __2__ yangu ndio ulionigutusha. Niliinua __3__. Lo! Ilikuwa ni sauti ya Mluna wangu aliyekuwa akizimbua __4__ huko ughaibuni. Baada ya maamkizi, alitaka, bila kupoteza mwia, ni atumie maelezo fulani kwa njia ya faksi. Nami kwa kuwa sikuwa na huduma hiyo ya __5__, nilimweleza ningetuma kwa __6__ "Haidhuru." alisema. Kutokana na ukosefu wa __7__ simu ilikatika. Hata hivyo, ujumbe ulikuwa umewasilishwa. Bila kupoteza wakati, nilichukua __8__ na
kuanza kuandika maelezo yale. Kwa ndege nzuri, tarakilishi hiyo ilikuwa imeunganishwa na __9__. Papo hapo nikamtumia ujumbe.

   A   B   C   D 
 1.   ilikuwa   ulikuwa   nilikuwa   mlikuwa 
 2.  rununu   satalaiti  nukulishi   redio
 3.  kuichuna   kupiga  kuibonyeza   kujibu
 4.  unga  maisha  mali  riziki
 5.  kipepesi  satalaiti  arafa  barua meme
 6.  nukulishi  huduma za mhadalishi   runinga  redio
 7.  utandawazi   njia ya mhadili  njia ya mhadihi   barua pepe
 8.  runinga  jokofu  tarakilishi  panka
 9.  wavuti  kidaka  waraka  simu


Kukutana __10__ naye kulikuwa kwa sadfa. Nilikuwa __11__ kondeni __12__. __13__. Mara nikamwona kijana Skambe __14__
barasteni. Hali yake ilisikitisha kutokana na __15__ ulevi haramu

   A   B    C   D  
 10.  kwetu   kwangu   kwao   kwenu 
 11.   ninaelekea   naelekea   nikielekea   kuelekea 
 12.  kunadi   kupalilia   kuinjika   kuabudu 
 13.  Kulikuwa kukinyesha   Mvua ulikuwa ukinyesha   Kulikua kukinyesha   Mvua ilikuwa ikinyesha 
 14.  akipepesuka  akihohosa   akiweweruka   akikweta 
 15.  kunywa   kulewa   kushiriki   kutopea 


Kutoka swali la 16 mpaka 30, jibu kila swali kulingana na maagizo yake:-

  1. Nyambua kitenzi kilichopigwa mstari katika kauli ya kufanyiwa. KUFA
    1. Hapo ndipo alipofiliwa
    2. Hapo ndipo alipofia
    3. Hapo ndipo alipokufiwa
    4. Hapo ndipo alipofiwa
  2. Tambulisha nomino tadunisha na nomino kuza ya neno kiti ni
    1. Kijiti - Jiti
    2. Kikiti - Jikiti
    3. Kijikiti - Jikiti
    4. Kijikikiti - kiti
  3. Chagua sentensi moja yenye maana sawa na ile uliyopewa katika sentensi iliyo hapo chini
    Ni heri nivumilie shida kuliko kuiba
    1. Ni bora niibe nikiwa na shida
    2. Afadhali nisiibe hata nikiwa na shida
    3. Nisingekuwa na njaa nisingeiba
    4. Niliiba kwa vile nilikuwa na njaa
  4. Tumia kilinganishi sahihi
    Matilda-
    1. Anafanana na dada yangu
    2. Anakaa kama dada yangu
    3. Anafanana kama dada yangu 
    4. Analingana kama dada yangu
  5. Mbio za farasi ni _________________________
    1. kupupira
    2. kutekela
    3. kuparakasa
    4. kunyiririka
  6. Mzazi wa mke humwita mume wa binti
    1. mlamu
    2. mkaza
    3. mwana
    4. mkwerima
  7. Taja kiwakilishi katika sentensi
    Ninakipenda chakula hiki kwa sababu chenyewe ni kitamu.
    1. chakula
    2. hiki
    3. chenyewe
    4. kitamu
  8. Taja neno moja tu linalosimamia fungu zima.
    Kabaila alizivua nguo akaosha mwili.
    1. Oga
    2. Osha
    3. Nawa
    4. Pangusa
  9. Eleza tofauti baina ya sentensi katika jozi (sawia)
    1. Mvua ilinyesha ndogo ndogo
    2. Mvua ilinyesha kidogo kidogo
      1. Mvua haikunyesha kwa wingi.
        Mvua ilikuwa kiasi kidogo.
      2. Mvua ilikuwa kiasi kidogo.
        Mvua ilikuwa matone madogo madogo 
      3. Mvua ilikuwa kiasi kidogo kidogo.
        Mvua ilikuwa chache
      4. Mvua ilikuwa matone madogo madogo.
        Mvua ilikuwa kiasi kidogo kidogo.
  10. Andika jina la kitendo na mtenzi kutokana na KITENZI ulichopewa
    Rehemu __________________      _________________
    1. Rehemu - Rehema
    2. Rehema - Rahimu
    3. Rahimu - Rehema
    4. Rahimu - Rehemu
  11. Badilisha sentensi hii kwa wingi.
    Malkia wa kijiji ana macho ya kikon:be. 
    1. Malkia wa vijiji wana macho ya kikon:be 
    2. Malkia wa vijiji wana macho ya vikombe 
    3. Malkia wa kijiji ana jicho la vikombe 
    4. Mamalkia wa vijiji wana macho ya vikombe
  12. Kumramba mtu kisogo ni
    1. kulamba kisogo chake
    2. kumdharau
    3. kumwangalia kwa dharau
    4. kumsema vibaya asipokuwepo
  13. Badilisha sentensi ifuatayo katika wakati RUDUFU 
    Mgeni anakuja kwangu
    A. Mgeni akaja kwangu
    B. Mgeni yuaja kwangu
    C. Mgeni huja kwangu
    D. Mgeni aja kwangu
  14. Ni kikundi kipi kilicho na viarifa pekee?
    1. Angua, chomoa, zana, vizuri
    2. Vunja, sana, chora, lia
    3. Polepole, upesi upesi, mbiombio
    4. La, pa, ita, ona
  15. Kamilisha methali ifuatayo:Asiyeona nafsiye _____________________________
    1. haoni akionyeshwa
    2. hana ajifunzalo
    3. ni malaika
    4. hanong'onezewi neno

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 31-40:-

Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka miwili awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari.

Mwezi mmoja ukawa umepita tangu nipewe pesa za kiinua mgongo. Mwezi mmoja mzima nilkuwa katika shughuli za kulipa karo huku. Kuwekeza kwenye mradi ule na kununua hili. Sasa shilingi laki mbili tu zilikuwa zimesalia katika benki.

Watu wengi walinishawishi nijaribu kilimo cha mahindi. Bei ilikuwa imeanza kuimarika. Katika taarifa ya habari jioni hiyo, Waziri wa Kilimo alitangaza bei mpya. Shilingi 1,500 kwa kila gunia. Nami nilikuwa naaza kuumakinikia mradi huu.

Baada ya taarifa, nilikoga, nikala na nikaenda kulala. Kwa sababu ya uchovu, usingizi ulinichukua mara moja. Usingizini niliota. Katika ndoto niliutekeleza mradi wangu. Msimu huo wa kulima nilitenga ekari kumi za shamba langu. Wataalamu walinishauri kuwa wakati mzuri wa kulima ni wa kiangazi. Mwezi wa Januari ulipoanza tu nilitafuta trekta na kulima. Malipo yalikuwa shilingi 1,200 kila ekari. Katikati ya mwezi wa Machi, nilitafuta treka la kutifua shamba tena kwa gharama ya shilingi 15,000 ekari zote kumi. Kufuatia ushauri wa manyakanga wa kilimo, nililipa shilingi elfu kumi na tatu kupiga shamba lote haro.

Mwishoni mwa mwezi huo, nilienda mjini kutafuta pembejeo. Kwanza, nililipa shilingi 20,500 kwa magunia 15 ya mbolea. Kisha nilinunua magunia manne ya mbegu ya mahindi yenye uzani wa kilo 25 kwa shilingi 3,300 kila gunia. Mwezi wa Aprili ulipotimia tu, niliamua kupanda. Ili nipate mazao bora, nilipanda kwa tandazi. Gharama ilikuwa shilingi 1,000 kila ekari. Mvua ilinyesha vizuri na baada ya siku saba, mahindi yalianza kuota. Ilifurahisha kuhesabu mistari ya kijani iliyonyooka. Hali hii iliwezekana tu baada ya kuajiri vijana wa kuwafukuza korongo na vidiri ili wasifukue mbegu mchangani.

Baada ya mwezi mmoja, hatua ya kupalilia ilifika. Nilitafuta vibarua wa kupalilia. Malipo yalikuwa shilingi 700 kila ekari. Kumbe kupalilia kulichochea mtifuko wa mahindi. Punde yakawa yananifikia magotini, Hii ikawa ishara kuwa yanahitaji kumwagiwa mbolea ya kunawirisha iitwayo 'amonia'. Gharama yake ikawa shilingi 1,300 kila gunia. Hivyo, nikalipa shilingi 19,500 kwa magunia kumi na matano.

Mahindi yalibadilika kimiujiza. Ghafla tu yalirefuka na kunenepa mashina. Yalibadilika rangi yakapiga weusi. Shamba liligeuka likawa kama msitu wa rangi ya kijani iliyokolea. Wapita njia walistajabia mimea na juhudi zangu. Shamba langu sasa likawa kielelezo. Maafisa wa kilimo wakawa kila siku wanawaleta wakulima wengine kujifunza siri ya ufanisi wangu. Hapo nikaanza kuhesabu mavuno nitakayopata na kukadiria faida. Nilipuuza kabisa ushauri wa wahenga kuwa 'Usikate majani, mnyama hajauawa.

Bila taarifa wala tahadhari mvua ilitoweka. Hayakupita majuma mawili mahindi yakaanza kubadilika. Juma moja baadaye mahindi yalinyauka. Badala ya mahindi, shamba likageuka la vitunguu vilivyochomwa na jua. Makisio yangu ya faida yaliyeyuka jinsi ufanyavyo moshi.

Lakini 'Muumba ndiye Muumbua.' Siku moja mawingu yalitanda na mvua ikanyesha. Muda si muda mahindi yalianza kunawiri. Kumbe tukio lililonivunja moyo lilikuwa laja. Siku moja mvua kubwa ilinyesha. Asubuhi nilipotoka nje nilipigwa na butwaa. Barafu ilitapakaa pote. Shamba lilikuwa limetapakaa barafu huku majani ya mahindi yamechanika kama nyuzi. Niliugua. Baada ya wiki moja, nilipata nafuu. Nilipotazama upande wa shamba niliona dalili za majani mapya ya mahindi yakianza kuchomoza. Maumbile ni kitu cha ajabu kweli.

Muda si mrefu mahindi yalirudia hali yake tena, kisha yakakomaa. Harakati za kutafuta watu wa kuyakata na kuyakusanya zilianza. Gharama ya shughuli hii ikawa shilingi 5,000. Kuvuna, kusafirisha kutoka shamba na kukoboa kwa mashine magunia 200 yakachukua shilingi 20,500. Kufikia hapo nilikuwa nimetumia takribani shilingi 192,700. Gharama nyingine zilikuwa za usafiri, gharama ya dharura na usimamizi, usumbufu wangu binafsi, gharama ya magunia na kadhalika. Mahindi yalipokuwa tayari kwenye magunia, nilifunga safari kwenda mjini kutafuta soko.. Niliposhuka tu niliona gazeti. Habari motomoto siku hiyo ilikuwa: 'MAHINDI GUNIA 900/= Niligutuka usingizini

  1. Andika kichwa mwafaka kwa kifungu hiki
    1. Mahindi gunia
    2. Mashaka ya kilimo cha gunia
    3. Kiinua mgongo
    4. Usingizi
  2. Msimulizi alikuwa na kiasi gani cha fulusi baada ya mradi kukamilika?
    1. Elfu mbili tu
    2. Laki mbili tu
    3. Elfu saba mia tatu
    4. Laki moja mia tisa, mia saba
  3. Kwa mujibu wa kifungu hiki msimulizi alikuwa na matatizo matatu makuu katika zaraa ila
    1. tishio la korongo
    2. tishio la kiangazi
    3. mvua ya barafu
    4. gharama ndogo
  4. Kwa mujibu wa kifungu methali "Muumba ndiye muumba" imetumika. Ni methali ipi iliyo na maana sawa na hiyo?
    1. Aliyekupa wewe kiti ndiye aliyenipa kumbi 
    2. Hulka njema sawa na mali
    3. Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi
    4. Baada ya dhiki faraja
  5. Pamoja na kiwango cha chini cha mavuno ni jambo lipi jingine lililosababisha msimulizi kutopata faida?
    1. Gharama ya kilimo
    2. Kushuka kwa bei
    3. Kutoweka kwa mvua
    4. Tangazo lililokuwa gazetini
  6. Eleza maana ya kiinua mgongo kama lilivyotumika katika kifungu
    1. Mshahara wa mwezi
    2. Mkopo wa kilimo.
    3. Malipo ya kustaafu
    4. Kuinuliwa mgongo juu
  7. Kwa mujibu wa aya ya tano jambo lipi ambalo lilikuwa la mwisho kutendewa na msimulizi
    1. Kuhesabu mistari ya kijani iliyonyoka 
    2. Kuenda mjini kutafuta pembejeo
    3. Kuajiri vijana kuwafukuza vidiri na korongo
    4. Kupanda kwa tandazi ili apate mazao bora
  8. Maana ya yalinyauka ni
    1. kauka
    2. kufa
    3. nawiri
    4. stawi
  9. Katika aya ya nane maoni ya msimulizi ni kuwa faida yaliyeyuka ufanyavyo moshi. Huu ni mfano wa
    1. tashbihi
    2. tashdidi
    3. istiari
    4. tanakali
  10. Kulingana na kifungu ni kweli kusema kuwa
    1. mavuno hayakuwa mema
    2. mavuno yalikuwa haba
    3. msimulizi hakutumia ngwenje nyingi
    4. msimulizi alikuwa amestaafu

Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali 41 - 50:-  

Ama kwa hakika, dunia uwanja wa fujo. Vituko vya ulimwengu haviishi. Huzuka kama mizuka kila kunapokucha. Maajabu yaja yakienda. Yote hayo ni mawimbi ya maisha yanayomkumba mwanadamu katika kuishi na kuisha kwake. Lo! Hayo ndiyo malimwengu ulimwenguni.

Nikikaa na kutafakari, huku nikivuta taswira ya mambo kuhusu haya na yale nywele hunisimama, moyo hunidunda, mifupa hunikengeta, nayo damu hunisisimka. Na damu isipowasha hunyeza! Lakini tufanyeje sisi waja wa Mungu ilhali tunajua na kuelewa fika kuwa mja hana hiari na liandikwalo ndilo liwalo? Tunaishi na tuishi kwa rehema na majaliwa ya Jalali. Ewe Mola tunakuhimidi!

Kisa na maana? Hebu nikukumbushe machache tu. Akali ya vituko na vitushi vya hivi karibuni. Bila shaka
nitakuwa nimekusaidia na kukufaa ushughulishe kumbukumbu zako nawe urejee nyuma kidogo. Wazee hukumbuka,
vijana hukumbushwa.

Si miaka mingi sana ulimwengu wetu ulipokumbwa na mvua za mafuriko ya Elnino. Maafa mangapi kama si misiba iliyotusibu. Baadaye tukakumbwa na uhasama wa Osama! Roho nyonge zikanyongwa. Yakaja mawimbi ya kabobo, nyinyi mnayaita Sunami! Vifo vilifisha wengi. Baada ya kidonda moyoni, msumari wa moto juu ya dondandugu. Kabla ya kupona wakazuka ndugu wawili Artur magariani na mwenzake. Nyinyi mkawaita mamluki. Shangaa. Kesho yatazuka yapi? Tahadhari iko wapi? Roho mikononi. Ndugu amkeni tulale tukiwa macho.

  1. Dunia imemithilishwa na uwanja wa fujo kwa nini?  Kwa sababu
    1. Kuna vituko vingi mno vya kushangaza
    2. Fujo hutokea duniani
    3. Watu wanafurahishwa na fujo za dunia
    4. Furaha za watu ni kufanya fujo
  2. Tunaambiwa kuwa
    1. vituko vina mwisho, vimeisha
    2. maajabu hayana mwisho, huja yakienda
    3. maajabu ni malimwengu
    4. vituko vya dunia havimtishi mwanadamu
  3. "Kuishi na kuisha" kuna mantiki gani?
    1. Kufurahia kuishi na kuisha
    2. Huwezi kuisha bila kuishi
    3. Ukiisha utaishi
    4. Watu wanakuwa hai huku wengine wakifa.
  4. Kulingana na kifungu, nini maana kuvuta taswira?
    1. Kuona picha
    2. Kupiga mambo picha
    3. Kusoma na kuelewa
    4. Kuyakumbuka matukio kwa makini
  5. Nywele husimama, moyo hudunda. Kichwa _________________ ilhali tumbo __________________
    1. huvuma, hudorota
    2. hutafuna, huzunguka
    3. huwanga, husokota
    4. huruka, huchanganya
  6. Taarifa inatuambia kwamba tunaishi
    1. kwa kudra za Mwenyezi Mungu 
    2. kwa kuwa tuna nguvu nyingi
    3. kwa kutumia ujanja
    4. ili Mungu atusaidie
  7. Baadhi ya maafa yaliyowahi kutokea ni pamoja na
    1. yote yaliyosababishwa na uzembe wetu
    2. yaliyo zaidi ya uwezo wetu kuzuia
    3. mengi ambayo tungezuia
    4. dhambi za wanadamu wenyewe
  8. Maafa yaliyosababishwa na nguvu za maji ni kama vile
    1. Elnino na uhasama
    2. Kabobo na Artur
    3. Osama na Artur
    4. Kabobo na Elnino
  9. Miongoni mwa walioaga dunia walikuwepo
    1. Mamluki
    2. Wenye hatia
    3. Wasio na hatia
    4. Waliosababisha kabobo
  10. Bila shaka taarifa hii ni
    1. Kuhusu msiba na huzuni ya maafa
    2. ya kuchekesha
    3. hadithi ya porojo tu
    4. mambo yaliyopita ambayo hayana umuhimu.

MARKING SCHEME

  1. B
  2. A
  3. C
  4. D
  5. A
  6. B
  7. C
  8. D
  9. A
  10. A
  11. C
  12. B
  13. D
  14. A
  15. C
  16. D
  17. C
  18. B
  19. A
  20. C
  21. D
  22. C
  23. A
  24. D
  25. B
  26. A
  27. D
  28. C
  29. D
  30. A
  31. B
  32. C
  33. D
  34. A
  35. B
  36. C
  37. C
  38. A
  39. A
  40. D
  41. C
  42. B
  43. B
  44. B
  45. C
  46. D
  47. A
  48. A
  49. B
  50. A

QUESTIONS

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi kutoka 1-15. Kwa kila nafasi, umepewa majibu manns.
Chagua jibu sahihi kati ya yale aliyopewa

__1__jamii humu nchini zilikuwa__2__majira ya mwaka badala ya miezi. Kwa mfano,majira ya mvua kubwa yaani__3__jua kali, upanzi na mavuno. Jamii zingine nazo ziliweka__4__ ya matukio maalum kama vile tohara, njaa, vita, mafuriko na uvamizi wa nzige. Yasemekana kuwa jamii moja __5__ikiishi Kusini __6__ukanda wa Ikweta __7__ mwezi wa __8__ "Jua kali" na mwezi wa Desemba ukaitwa mpe mjombako maji.

  1.                        
    1. Baadhi ya
    2. Baina ya
    3. Fauka ya
    4. Licha ya
  2.                    
    1. zinatumia
    2. zimetumia
    3. zikitumia
    4. zilitumia
  3.                
    1. mchoo
    2. vuli
    3. kipupwe
    4. kifuku
  4.              
    1. kumbusho
    2. kumbukumbu
    3. mafanikio
    4. madaftari
  5.                  
    1. iliyokuwa
    2. iliokwa
    3. waliyokuwa
    4. waliokuwa
  6.                      
    1. ya
    2. mwa
    3. na
    4. la
  7.                    
    1. waliuita
    2. iliita
    3. iitwa
    4. iliuita
  8.                
    1. Oktoba
    2. Octomba
    3. Oktomba
    4. Octobe

Hapo zamani za kale, __9__mtumwa mmoja ambaye alidhulumiwa sana na tajiri wake. Licha ya__10__kazi za sulubu kutwa kucha, alicharazwa__11__mijeledi. Mtumwa__12__kwa jina. Hasimu, hakuweza __13__tena mateso hayo.__14__akaamua kutorokea__15__kule, na liwe liwalo.

  1.                          
    1. kuliishi
    2. mliishi
    3. muliishi
    4. paliishi
  2.                
    1. kufanyishwa
    2. kufanyizwa
    3. kufanyia
    4. kufanyika
  3.                
    1. na
    2. ni
    3. kwa
    4. bila
  4.                
    1. buyo
    2. huu
    3. huo
    4. huyu
  5.                  
    1. kustahimili
    2. kudhamini
    3. kukabiliwa
    4. kukabidhi
  6.            
    1. Alipiga jeki
    2. Alipiga moyo konde
    3. Alipiga chafya
    4. Alipiga domo
  7.                
    1. kokote
    2. kwakwote
    3. popote
    4. momote

Kutoka swali la 16-10. jibu kila swali kulingana na maagizo uliyopewa

  1. Ni uunganishi upi unaofaa zaidi wa sentensi hizi mbili?
    Mimi nitakuwapo. Wewe hutaniona.
    1. Mimi nitakuwapo halafu wewe hutaniona.
    2. Mimi nitakuwapo lakini wewe hutaniona.
    3. Wewe utakuwapo halafu mimi sitakuona
    4. Wewe utakuwepo lakini mimi sitakuona.
  2. Ki katika sentensi "Wageni wakifika watavalia kitamaduni," imetumiwa kuonyesha
    1. masharti, namna
    2. wakati, udogo
    3. masharti, nomino
    4. namna, nomino
  3. Ikiwa jana ilikuwa Jumapili, kesho kutwa itakuwa
    1. Jumatano
    2. Jumamosi
    3. Jumatatu
    4. Jumanne
  4. Kalamu ni kwa kuandikia, meno ni kwa
    1. kulia chakula
    2. kusagia chakula
    3. kutafunia chakula
    4. kukatia chakula
  5. Ni sentensi ipi sahihi?
    1. Huree! Tumeshindwa.
    2. Ng'o! Naomba maji.
    3. Hamadi! Amefaulu.
    4. Wallah! Watoto hawa wataadhibiwa
  6. Kamilisha: Baidika kama
    1. ardhi na mbingu
    2. mchuzi na ugali
    3. maziwa na tui
    4. pua na mdomo
  7. Chagua maelezo sahihi
    1. Susu-kifuniko cha chungu
    2. Ufu-nazi iliyokunwa
    3. Ukoko-chakula kilicholala mpaka asubuhi
    4. Bariyo-chakula kilichoganda kwenye chombo
  8. Chagua sentensi yenye kiwakilishi.
    1. Mwalimu anatembea kijeshi.
    2. Gari limeegeshwa kando ya barabara.
    3. Cha mlevi huliwa na mgema
    4. Watoto hawa ni watiifu
  9. Joka la mdimu ni kwa inda ilhali kutokuwa mwaminifu katika ndoa ni kuwa na
    1. mpango wa kawaida
    2. kisebusebu
    3. mkono mrefu
    4. jicho la nje
  10. Mtu anayehamia nchi nyingine na kuifanya makao yake huitwa
    1. mlowezi
    2. mkimbizi
    3. Mmtoro
    4. kibaraka
  11. Nyambua kitenzi 'tokota' katika hali ya kutendesha
    1. tokoza
    2. tokosha
    3. tokosa
    4. tokesha
  12. Akisami, kwa maneno ni
    1. subui kumi
    2. ushuri saba
    3. ushuru saba
    4. subui saba
  13. Chagua sentensi yenye kivumishi cha idadi katika orodha
    1. Mgeni wa mwisho amewasili.
    2. Daktari amewatibu wagonjwa watano.
    3. Waliingia wawili wawili kwenye jukwaa
    4. Vitabu vingi vimechafuka.
  14. Geuza sentensi katika kauli ya taarifa: Mwalimu aliwaambia wanafunzi, "Viwekeni vitabu vyenu safi kila siku."
    1. Mwalimu aliwamuru wanafunzi kuviweka vitabu vyao safi kila siku.
    2. Mwalimu aliwaambia wanafunzi kuwa anataka waviweke vitabu vyao safi kila siku.
    3. Mwalimu aliwaambia wanafunzi kuwa angetaka waviweke vitabu vyao safi siku zote.
    4. Mwalimu aliwaambia wanafunzi kuwa yeye hutaka waviweke vitabu vyao safi kila siku.
  15. Chagua kundi lenye wadudu pekee.
    1. Kipepeo, sigi, mende, panzi
    2. Bandi,nzige,nzi, njiwa
    3. Kiwavi, nyigu, kumbukumbi, kiroboto
    4. Mbu, utitiri, mkunga, kipepeo 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40
Nyangi alikuwa na furaha isiyo na kifani. Alikuwa ameyakamilisha masomo yake ya uzamifu huko Uingereza. Alikuwa mwenye buraha na furaha kwani ndiye aliyekuwa kijana wa kipekee katika familia yao aliyesoma.
Siku ya kurudi kwake humu nchini, jamaa yake na marafiki wachache walijitokeza kumlaki katika uwanja wa ndege. Hakuna aliyempa Nyangi raha kumwona kama Farida aliyekuwa mchumba wake ambaye hawakuwa wameonana kwa miaka sita mtawalia. Ndoa yao ilikuwa imepangwa kufanyika mwezi wa Agosti baada ya Nyangi kupumzika siku sitini na tano. Farida alikuwa amemsubiri mpenzi wake kwa ustahimilivu kweli, mara nyingi alikuwa na wasiwasi kuwa angepata mchumba mwingereza. Sasa alipata uhakika na kuamini ya wahenga subira huvyaa mwana. Aidha, subira ni ufunguo wa faraja. Sheria ya kanisa lao ilihitaji kwanza wafanyiwe uchunguzi wa ukimwi. Hakuna kati yao aliyekuwa na tashwishi kwa kuwa walikuwa waaminifu. Kwa hivyo, walichangamka vilivyo pale walipoendea matokeo na cheti cha kupimwa. Farida ndiye aliyepatiwa matokeo kwanza na kama walivyotarajia, yalikuwa sawa kabisa. Wakati wa matokeo ya Nyangi, daktari alisitasita, "Samahani, sina habari njema kwako!" "Unamaanisha nini daktari?" Nyangi aliuliza kwa mshangao. Alipoarifiwa eti alikuwa na virusi vya ukimwi, alikataa katakata.
Farida alibaki kuduwaa. Walitoka pale bila maongezi. Hata walipoachana, Nyangi alizidiwa na mawazo chungu nzima, kuwa na ukimwi kwake lilikuwa fumbo ililohitaji kufumbuliwa. Alijijun mwenye nidhamu ya hali ya juu. Mara wazo likamjia. Lazima ilikuwa simimi. Alikumbuka vyema walikuwa pamoja kitambo sana. Alijiuliza maswali yasiyo na majibu. Mbona mabaya yalikuwa yakimlenga yeye ambaye aliishi maisha ya uaminifu na kujinyima raha akiogopa karaha? Lilikuwa jambo la kumkera kuona kuwa wengi ambao waliishi maisha ya kiholela na anasa walikuwa wazima kama vigongo wakitembea mzofafa bila athari yoyote. Laiti angalijua! Angalikuwa mbembe na kuzini kama vijana wengine pengine asingalijuta hivyo! Mawazo yake hata yalimwongoza aanzie pal kasambazia wengine, ili asife peke yake, lakini fikra za kuwa tabibu zikamwambia hivyo ni vibaya.
Asubuhi iliyofuata wakati wa staflahi, hakuwa ameamka. Ilibidi aitwe lakini hakujibu. Mlango wake ulibishwa kwa nguvu, lakini hakufungua. Ulipovunjwa, kila mmoja alishangaa kumpata ni maiti. Alikuwa amejitia kitanzi. Hakuna aliyeelewa hadi walipoisoma barua aliyoandika kusema "Poleni wavyele wangu, siwezi kuishi katika hali hii. Singeweza kumchukua mchumba wanga akiwa anajua ninaishi na ukimwi. Nilitenda kosa moja tu, nalo limeniua. Nawaomba radhi. Ninawapenda!
Vilio vilitanda kote. Daktari yule aliyewapima naye alishindwa kufungua kinywa alipofika pale kutaka kuongea naye. Alikuwa ameenda huko kwao kumweleza kuwa alikuwa amefanya makosa. Jibu alilokuwa amepeana awali kuwa la Nyangi kumbe lilikuwa la mgonjwa mwingine! Afanalek!

  1. Kulingana na aya ya kwanza, Nyangi
    1. alienda Uingereza kusomea shahada ya pili
    2. alienda Uingereza kusomea shahada ya tatu
    3. alienda Uingereza kusomea shahada ya kwanza
    4. alienda Uingereza kusomea stashahada
  2. Ni kweli kusema kuwa
    1. Nyangi alikuwa kijana wa kipekee katika familia yao
    2. familia ya Nyangi haikuwa na mtoto mwengine kijana
    3. wazazi wa Nyangi hawakuwa na karo ya kuwalipia watoto hao wengine
    4. Nyangi ndiye tu aliyesoma katika familia yao
  3. Kwa nini Nyangi alifurahi alipomwona Farida?
    1. Walikuwa wamekaa miaka sita bila kuonana
    2. Alifurahi kurudi nchini
    3. Alikuwa mpenzi wake
    4. Aliandamana na wazazi wake
  4. Kulingana na kifungu, Nyangi alirudi mwezi wa
    1. Juni
    2. Mei
    3. Julai
    4. Agesti
  5. Methali 'subira havyaa mwana" mwema hailingani kimaana na
    1. mkono mmoja haupigi kofi
    2. papo kwa papo kamba hakata jiwe
    3. Zito hufuatwa na jepesi
    4. Baada ya dhiki faraja
  6. Neno mbembe limetumika kumaanisha nini?
    1. Mahindi ya kuchoma yaliyoza
    2. Kufutia hali aliyonayo mtu
    3. Mtu anayependwa sana na wengine
    4. Mtu msherati
  7. Ni sahihi kusema kuwa
    1. Simimi alimwambukiza Nyangi ukimwi
    2. Nyangi na Farida walioana
    3. Nyangi hakuwa na ukimwi
    4. Matokeo ya ukimwi ya Nyangi hayakuwa na makosa
  8. Nyangi alikuwa ameenda Uingereaza kusomea
    1. urubani
    2. uhasibu
    3. udaktari
    4. uhazigi
  9. Kwa nini Nyangi alijitia kitanzi?
    1. Hakuwa na ukimwi
    2. Simimi alimwambukiza ukimwi
    3. Aliamini alikuwa na ukimwi
    4. Alikuwa na ukimwi
  10. Kichwa mwafaka cha kifungu hiki ni
    1. Arusi ya Nyangi na Farida
    2. Kosa la daktari
    3. Simimi kumwambukiza Nyangi ukimwi
    4. Urafiki wa Nyangi na Farida 

Sama kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50
Kuwa na elimu ni jambo la busara. Tumefunzwa kwa kina hadi tukaelewa kinagaubaga kuwa masomo ni taa ambayo huangaza gizani. Aidha, elimu ndiyo ufunguo wa maisha mema ya mustakabali. Kutokana na ujuzi huu, wanafunzi wengine hujikaza kisabuni na kusoma kutwa kucha ili wafaulu katika mitihani yao.
Wazazi nao wametekeleza wajibu wao wa ulezi wa kuhakikisha wana wao wamezima kiu yao ya masomo. Wengi wamechukua mikopo minono kwenye benki huku wengine wakiuza mali na mashamba yao ili kulipa karo ambayo si mchezo siku hizi. Walimu kwa upande mwingine wanajizatiti kuwapa wanafunzi wao masomo ya kiwango cha juu.
Serikali haijasazwa. Masomo bila malipo ya msingi yametolewa kwa watoto wote maskini kwa matajiri. Kwa sasa, ni hatia kutompeleka mwana shuleni hata kama wewe ni maskini hohehahe.. Jukumu la watoto nao ni kusoma. Wengi wameyatwaa masomo na kuyakumbatia kiasi cha kualikwa katika vyuo vikuu kusomea taaluma mbalimbali. Kuna wale huendeleza masomo yao kwa bidii ya mchwa lakini kunao wakifika huko husahau kabisa kilichowapeleka chuoni.
Ni juzi tu kijana barobaro wa chuo kikuu alifyatuliwa risasi na kufa papo hapo baada ya kushiriki utekaji nyara wa mkuu mmoja wa polisi. Alipatikana chumbani mwa mwanafunzi huyu akiwa amefungwa miguu na mikono kwa kamba. Nao mdomo ulikuwa umezibwa kwa kitambaa. Polisi mwenyewe alikuwa na bahati ya mtende kuokolewa na mwanafunzi mwengine aliyemshuku kijana huyo baada ya kugundua hakutaka yeyote akaribie chumba hicho. Ilibainika kuwa kijana pamoja na genge lake walikuwa wakidai kulipwa shilingi milioni tano na familia ya polisi ili wamwachilie huru. Aibu iliyoje! Kikawa kisa cha tamaa mbele mauti nyuma.

  1. Wanafunzi wengine hujikaza kisabuni kusoma kutwa kucha. Hii inamaanisha kuwa
    1. wanafunzi husoma mchana na usiku 
    2. wanafunzi husoma usiku na mchana
    3. wanafunzi husoma asubuhi na mchana
    4. wanafunzi husoma jioni na asubuhi
  2. Neno 'mustakabali' kama lilivyotumika linamaanisha
    1. maisha ya kisogoni
    2. maisha ya baadaye
    3. maisha ya raha
    4. maisha ya utosini
  3. Ni nini maana ya "serikali haijasazwa?"
    1. Serikali haijabaki nyuma kimasomo
    2. Serikali imejitia hamnazo
    3. Serikali inachunguza masomo
    4. Serikali ina hatia kimasomo
  4. Kilichomfanya mwanafunzi kumshuku kijana ni
    1. tabia yake ya utekaji nyara
    2. tabia yake ya uongo
    3. tabia yake ya ukali
    4. tabia yake ya usiri
  5. Wajibu mkuu wa wazazi uliotajwa ni
    1. kuwaelea wanao, kuuza mashamba
    2. kuuza mashamba, kuchukua mikopo benkini
    3. kuwalea watoto, kugharamia masomo yao
    4. kugharamia elimu ya wanao, kuchukua mikopo benkini
  6. Kulipa karo si mchezo siku hizi kwa sababu
    1. si lazima mtu acheze ili aweze kulipa karo
    2. kulipa karo kwahitaji kujitolea
    3. ni lazima mtu acheze ili aweze kulipa karo
    4. kulipa karo na kucheza ni sawa
  7. Kulingana na kifungu, si sahihi kusema kuwa
    1. kijana na genge lake walilipwa milioni tano
    2. vyuo vikuu hufundisha mambo mbalimbali
    3. wana wengine hulaza damu chuoni
    4. kijana na genge lake hawakulipwa milioni tano
  8. Kwa mujibu wa kifungu
    1. si hatia watoto wa maskini wakikosa kusoma
    2. wazazi wanapenda kuuza mashamba na kuchukua mikopo
    3. walimu wanazuia wanafunzi kusoma vizuri
    4. watoto wa mkata wanafaa kusoma sawa na wa kizito
  9. Waliotajwa kushiriki masomo ni
    1. serikali, walimu, wavyele, wazazi
    2. watoto, serikali, wafanyikazi, askari
    3. watoto, wavyele, walimu, serikali
    4. askari, polisi, wazazi, watoto
  10. Methali iliyotumiwa mwisho ni mwa kifungu inaweza kulinganishwa na
    1. Yote yang'aayo si dhahabu
    2. Penye mawimbi na milango i papo
    3. Mwenye pupa hadriki kula tamu
    4. Kilicho baharini kakingoje pwani

Insha

Andika insha ya kusisimua isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukimalizia kwa maneno haya

................................................................................tulinadi kwa vicheko na bashasha.

 

 

Tagged under
Page 6 of 14