Displaying items by tag: kiswahili
Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 1 2023 Set 8
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati va vale uliyopewa
Sikukuu ya Krismasi ilishangiliwa __1__. Makundi ya wakristo __2__ makanisani ili __3__. Ndugu na jamaa __4__ waliziwahi sehemu__5__ burudani ili kuburudika kwa furaha na buraha. Watu wengine __6__ ili kuwapa mkono waliokuwa hawajiwezi __7__
walizingatia kwamba __8__.
A. | B. | C. | D. | |
1. | kwa hamu na ghamu | kwa uti wala mauti | kwa shangwe na nderemo | kwa udi na uvumba |
2. | walimiminika | yalimiminika | watamiminika | yatamiminika |
3. | kusheherekea | kushehekea | kureshehekea | kusherehekea |
4. | pia | ilhali | madhali | angalau |
5. | ya | kwa | za | wa |
6. | walijitolea kibwebwe | walijitolea mhanga | walijitolea kingoto | walijitolea kiguu |
7. | Kwa kwamba | kwa ajili | Kwa hakika | Kwa moja |
8. | kutoa ni moyo, usambe ni utajiri | cha mfupi huliwa na mrefu | mtegemea cha nduguye hufa maskini | fimbo ya mbali haiui nyoka |
Kiswahili ni lugha mojawapo __9__ katika mazungumzo ya kawaida. Lugha hii __10__ sana __11__ nyanja anuwai. Wanafunzi shuleni hufundishwa __12__ thelathini.
Aidha, kuna sauti ghuna ambazo pia huitwa __13__. Sauti hizi huunda __14__. Mathalani, neno 'kilichoundwa' lina silabi __15__
A | B | C | D | |
9. | zilizotumika | iliyotumika | zinazotumika | inayotumika |
10. | inadhaminiwa | kinathaminiwa | inathaminiwa | kinadhaminiwa |
11. | katika | kati ya | kwenye | katikati ya |
12. | konsonati | alfabeti | vokali | irabu |
13. | nyepesi | sighuna | kwaruzo | mwambatano |
14. | neno | sentensi | silabi | aya |
15. | sita | tano | kumi na mbili | nane |
Kutoka swali la 16-30. jibu swali kulingana maagizo uliyopewa.
- Chagua matumizi ya 'kwa' kurejelea mchanganyiko
- Walitembea kwa miguu hadi shuleni.
- Wazee kwa vijana walihudhuria sherehe hizo.
- Timu hizo zilifungana mabao matano kwa sita.
- Aliadhibiwakva utundu wake.
- Hazama ni kwa puani kama vile _________________________ ni kwa sikio.
- mkufu
- kidani
- kipete
- mapete
- Chagua wingi wa sentensi hii
Ua wa dobi ulinivutia sana- Maua ya madobi yalituvutia sana.
- Nyua za madobi zilinivutia sana.
- Maua ya dobi yalituvutia sana.
- Nyua za madobi zilituvutia sana.
- Chagua kiambishi 'ku' cha ukanusho
- Kusoma huku kunafurahisha
- Hakusoma kitabu hicho cha hadithi
- Aliyekupiga ametiwa mbaroni
- Mchezo huo ulichezwa kule.
- Fidia ni _______________________
- malipo ya kumvunjia mtu heshima
- malipo ya kwanza ya kumshika mtoto
- malipo kwa ajili ya hasara au maumivu
- malipo ya kwanza ya kukinunua kitu dukani.
- Kanusha:
Jengo lililojengwa kwa uhafifu limebomolewa- Jengo lisilojengwa kwa uhafifu limebomolewa
- Jengo lililojengwa kwa uhafifu halijabomolewa
- Jengo halikujengwa kwa uhafifu limebomolewa
- Jengo lisilojengwa kwa uhafifu halijabomolewa.
- Ni nini maana ya msemo huu?
Kumvisha mtu kilemba cha ukoka- Kumtegemea mtu kwa kila jambo.
- Kumsema mtu katika mafumbo.
- Kumweka mtu katika hatari.
- Kumdanganya mtu kumhusu.
- Chagua jibu lenye ala za muziki pekee
- Filimbi, udi, mvukuto, chapuo.
- Siwa, zeze, upatu, nembo.
- Njuga, tari, kinubi, fidla.
- Harimuni, marimba, msondo, maleba.
- 5/6 kwa maneno ni
- sudusi sita
- humusi sita
- sudusi tano
- humusi tano.
- Ni kundi lipi la nomino ambalo lipo katika ngeli ya LI-YA?
- Maji, marashi.
- Gitaa, povu.
- Maskani, mavazi.
- Maagizo, maarifa.
- Onyesha sentensi yenye kielezi cha mahali
- Mwajuma alisafisha nyumba alfajiri.
- Kule kuna miti mirefu.
- Wawili walisajiliwa chuoni.
- Gari limefika asubuhi.
- Chagua jibu lenye nomino ya makundi isiyofaa
- Mzengwe wa wagomaji.
- Numbi ya nyuki.
- Shungi la moto.
- Thurea ya nyota.
- Kauli, 'Jedi ni sungura maishani; imetumia tamathali gani ya usemi?
- Jazanda.
- Kinaya.
- Tashhisi.
- Nahau.
- Ikiwa juzi ilikuwa Jumanne, mtondo itakuwa
- Ijumaa.
- Jumatatu.
- Jumapili.
- Jumamosi.
- Chagua jibu lenye kivumishi kilichoundwa kutokana na kitenzi.
- Ita - mwito
- Vumilia - uvumilivu
- Agiza - maagizo
- Sahau - sahaulifu.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 - 40.
Kuku aliketi nje ya nyumba yake huku amejishika tama. Moyo wake ulijawa na huzuni mpwitopwito. Je, angewezaje kuujenga urafiki wake upya na mwewe mwandani wake wa chanda na pete? Tatizo sugu lililokuwa limeubomoa urafiki wao wa kufa kuzikana ni wembe. Kuku alishangaa namna ambavyo kitu kidogo kama hicho kingesababisha mgogoro kama huo mkubwa. Mawazo kedekede
yalizidi kumzunguka akilini mithili ya pia.
Mwewe naye kwa upande wake pale kiotani alitabasamu kwa furaha mzomzo. Aliurarua mnofu wa nyama wake kifaranga mtoto wa kuku. Kwake alijiambia kuwa, "Sasa ninazidi kujilipa deni langu la wembe. Mtu hawezi kuwa ananipotezea rasilimali zangu pasipo kuzingatia hisia zangu pia. Bado atakuja kunitambua! Atabaki mzazi bila vikembe hadi atakapolipa deni lote!"
Giza la usiku lilikumbatia siku yenyewe. Sauti za mbwa zikawa zinasikika kwa umbali. Bado kuku pamoja na vifaranga wake watatu walikuwa hawajalala. Biwi la simanzi liliwaangukia kuku. Mtoto wake wa kiume alikuwa amenyakuliwa na mwewe. Mwewe asiye na utu wala msamaha. Mbona asingengoja hata siku moja imalizike kabla ya kuanza kujilipa yeye mwenyewe? Kwa nini basi asingekuja wapange mikakati namna ya kulipwa? Utitiri wa mawazo ulimtembea akilini mwake bighairi ya kuwa na mwisho.
Hatimaye, kuku aliwageukia wana wake ambao ndio chanzo cha kupotea kwa wembe wake mwewe. Aghalabu, alikuwa amewakanya dhidi ya kuchezea vitu vya wenyewe bila ya ruhusa. Kuku alijua siku moja mchezo wao huo ungewatumbukiza katika kidimbwi cha moto. Sasa moto huo ulikuwa umeanza kuwateketeza mno. Kuku akaishia laiti ningalijua na vyanda vi mkononi. Hata hivyo, akaamua
kulitafuta suluhisho la kudumu ifikapo asubuhi.
Jua la asubuhi liliramba umande wa alfajiri huku likimzizimua kobe ambaye alitoka nyumbani mwake asteaste. Mzee kobe alisifika sana kwa maarifa yake na akili tambuzi alizokuwa nazo hasa katika kuyatatua mambo baina ya wenzake. Aliketi pale nje huku akibukua tabu kubwa kuhusu migogoro. Kuku jirani yake aliwasili kwake kwa kishindo. Hapo kobe akatambua ya kwamba lazima kuna jambo. Huku amenyong'onyea kama mkufu. Kuku alimpasulia mbarika mzee kobe kuhusu tatizo lake.
Jungu kuu halikosi ukoko. Baada ya kikao hicho cha saa tatu naye mzee kobe, kuku alirudi nyumbani akiwa na matumaini kwamba suluhu limepatikana. Mzee kobe alibaki katika kina kirefu cha fikra ili kulipata suluhisho hilo la kudumu na kumpiga jeki jirani yake. Kwa hakika, ni heri jirani kuliko ndugu yako wa toka nitoke wa mbali.
- Chagua maana ya 'kushika tama' kwa mujibu wa kifungu.
- kuhangaika
- kuhuzunika
- kunung'unika
- kukasirika
- Kulingana na aya ya kwanza, kuku
- aliketi ndani ya kiambo chake
- alikuwa jasiri na mkakamavu
- aliwazia kiini cha ufa uliokuwa umetokea
- hakushangaa kiini cha mgogoro.
- Kulingana na aya ya pili, mwewe anaonekana kuwa
- mwenye ubinafsi
- mwenye urafiki wa dhati
- mwenye huzuni nyingi
- mwenye maarifa chungu nzima.
- Kitendo cha mwewe kuamua kujilipishia deni lake kinaweza kulinganishwa na methali gani?
- Asante ya punda ni mateke.
- Tamaa mbele mauti nyuma.
- Mtu ni watu.
- Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti.
- "Biwi la simanzi lilimwangukia kuku,"
imetumia tamathali gani ya usemi?- Ishara.
- Sitiari.
- Chuku.
- Tashhisi.
- Kwa nini mzee kobe alisifika?
- Kwa sababu alipenda kusoma mabuku.
- Kwa sababu alikuwa mstahimilivu.
- Kwa sababu alikuwa mwenye akili pevu.
- Kwa sababu alipenda kuliota jua.
- Kulingana na aya ya mwisho si sahihi kusema
- kikao hakikuzalisha matunda.
- jirani anaonekana kuwa na umuhimu.
- mzee Kobe aliwazia jambo hilo.
- kikao kilichukua saa tatu.
- Kifungu kinabainisha kwamba
- mwewe alikuwa mwandani wa dhati.
- kuku hakuwajali watoto wake.
- mzee kobe hakupenda kisomo kwa dhati.
- kuku alimwelezea kobe mambo dhahiri.
- Maana ya, "biwi la simanzi' kulingana na kifungu ni
- mkusanyiko wa hasira
- mkusanyiko wa taka
- kuwa na kiasi kikubwa cha huzuni
- kuwa na kiasi kikubwa cha taka.
- Kichwa kifaacho kifungu hiki ni sana ni
- Mzee Kobe mwenye magamba.
- Elimu nyingi huondoa maarifa.
- Urafiki wenye unafiki.
- Vifaranga vya kompyuta.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 - 50.
Afya au siha ni hali ya kutokuwa na maradhi. Hali hii humwezesha mtu kuhifadhi nguvu zake za mwili na kumwezesha kufanya kazi katika mawanda mbalimbali. Mtu mwenye afya bora huweza kutekeleza mengi bila masumbuko. Kwa mfano, yeye huweza kujirausha na kujishughulisha hadi jioni bila kuhisi uchovu mwingi.
Chombo hakiendi ila kwa makasia, nayo afya nzuri haimjii tu mtu. Afya hustahili kupaliliwa na kutunzwa kwa namna anuwai kama vile kula vyakula vyenye viinilishe, kufanya mazoezi na kuandama mienendo miadilifu. Usafi wa mv ili na mazingira pia huchangika katika kuimarisha afya. Ni bayana kwamba mazingira yakiwa machafu hukosa kuvutia na kusababisha kusambaa kwa harufu inayokirihisha. Isitoshe, uchafu huwa hali mufti ya kuzaana kwa wadudu kama vile chawa, nzi, kunguni na mbu ambao ni maadui wakuu wa afya.
Tabia ya binadamu huathiri afya yake. Wapo watu ambao wameambulia magonjwa kama vile saratani ya mapafu na kifua kikuu kutokana na mazoea ya pombe, sigara na dawa za kulevya. Wengine hujiponza kwa kuingilia vitendo viovų kama vile kushiriki mapenzi kiholela na kujisababishia magonjwa. Magonjwa haya ni kama vile kisonono na ukimwi ambao umewapukutisha watu kama majani makovu kutoka mtini.
Aidha, watu hujiharibia afya kwa kufanya kazi mfululizo bila kupumzika. Licha ya kwamba bidii ni muhimu katika maendeleo ya jamii yoyote ile, utendaji kazi pasipo kupumzika huweza kuwa na athari hasi. Kuna baadhi ya watu ambao wamewahi kupata maradhi ya moyo, ya kiakili na hata shinikizo la damu kutokana na hali kama hii. Wengine hujihasiri kwa kula vyakula vingi kupindukia. Kadhalika, wapo wengine ambao hupata magonjwa kwa kula vyakula visivyofaa katika kundi hili kwa wale ambao hawadiriki kufanya kazi wala mazoezi. Hawa hujinenepea na kudhoofisha utendakazi wao.
Hali ya umaskini pia huchochea kuzoroteka kwa afya. Asilimia kubwa ya watu nchini humu haimudu huduma bora za afya na lishe bora kutokana na hali ya ufukara. Wengine, kwa kukosa fedha hawapati elimu ya kimsingi kuhusu afya. Hawa huweza kujizulia magonjwa kwa kutojua na kutofuata sheria za afya. Pamoja na hayo, kuna wale ambao wanarithi magonjwa ya kiukoo kama vile bolisukari kutoka kwa wazazi wao.
Umuhimu wa afya hauwezi kupuuzwa. Nchi yenye kizazi chenye afya hustawi kiuchumi. Afya ikidumishwa wanajamii huweza kutumia fedha zao kuwekeza katika miradi badala ya kuzitumia kujiunga na kuwauguza wenzao. Ni jukumu la kila raia kuhakikisha kwamba anailinda afya yake na ya wengine kwa vyovyote vile. Walio na mazoea ya kupuuza ushauri wa wanaotoa huduma za afya na lishe wajiase, la sivyo watakuja kujiuma vidole.
- Kulingana na aya ya kwanza siha
- hukuza maendeleo katika maeneo mbalimbali
- humwondolea mtu matatizo mwilini
- humpunguzia mtu mazoea ya uchovu
- huimarisha matokeo ya utendakazi.
- Ni muhimu kutunza mazingira kwa kuwa
- tutamaliza vikwazo tofauti tofauti vya afya
- tutazuia ongezeko la wadudu waharibifu
- tutaepuka kuenea kwa harufu
- tutarudisha hali ya kupendeza.
- Mwandishi anapinga hali gani hasa katika aya ya tatu?
- Uambukizaji wa magonjwa.
- Kuhusiana bila mpango.
- Vifo vya watu wengi.
- Matumizi mabaya ya mihadarati.
- Chagua jibu ambalo ni sahihi kulingana na aya ya nne
- Jambo jema husababisha maradhi
- Kazi nyingi husababisha moyo kuharibika
- Mazoezi hayawezi kudhibiti afya.
- Mapumziko huimarisha hali ya mtu kiakili.
- Kufanya kazi kidindia
- huboresha maendeleo ya taifa
- huweza kusababisha uharibifu wa afya
- huwa na athari chanya
- hupunguza shinikizo la damu.
- Maana ya 'inayokirihisha' ni
- inayochukiza
- inayoenea
- inayoaibisha
- inayodhuru.
- Maana ya "chombo hakiendi bila ya makasia' imejitokeza vipi katika kifungu?
- Wanaonyoosha viungo vyao huwa wakakamavu.
- Wanaozingatia mienendo mizuri hudumisha afya.
- Wanaoepuka kazi hawapati shinikizo la damu
- Wanaokula vyakula vyenye viinilishe huzuia kunenepa.
- Chagua funzo linalojitokeza katika aya ya mwisho
- Wanaokosa kuzingatia maelekezi hupata majuto.
- Mtu hawezi kufaidika kiafya bila kupata ushauri.
- Wanaodharau watu wenye hekima hupata magonjwa.
- Nchi haiwezi kupiga hatua bila raia wote kuzingatia maradhi.
- Umuhimu wa afya hauwezi kupuuzwa kwa vile
- mipango nchini hukwama wahudumu wakikosekana
- watu wagonjwa hawawezi kuizalisha mali
- maradhi husababisha kuzorota kwa maendeleo
- pesa nyingi hutumiwa kuwatunza walio hospitalini.
- Kisawe cha 'kujiuma vidole" ni
- kupiga vijembe
- kutia nanga.
- kupigwa butwaa.
- kujuta hatimaye.
INSHA
Una dakika 40 kuandika insha yako
Andika insha ya kusisimua ukiendeleza kwa maneno haya:
Nilikuwa nimeketi sebuleni nikisoma kitabu cha hadithi.........
MARKING SCHEME
- C
- B
- D
- A
- C
- B
- C
- A
- D
- C
- A
- B
- C
- C
- B
- B
- D
- D
- B
- C
- B
- D
- C
- C
- B
- C
- B
- A
- C
- D
- B
- C
- A
- D
- D
- C
- A
- D
- C
- C
- D
- A
- D
- D
- B
- A
- B
- A
- C
- D
Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 1 2023 Set 7
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Wahenga na wahenguzi hawakukanyaga chechele walipolonga kuwa Mungu __1__. Ama kwa __2__ Mungu si mtovu. Yeyote anayemwamini atajibiwa __3__ yake. Mara nyingi tumewasikia watu wakitoa __4__ kuhusu nasaha waliyokwisha kupokea kutoka kwa wajuzi wa nyanja mbalimbali.Ukweli ni kwamba, wenye __5__, wote huishia kubarikiwa. Yote tuyafanyayo bila kumtegemea
Rabuka huwa ni kazi __6__ hata ingawa tutatia bidii ya mchwa.
A | B | C | D | |
1. | hamwachi mja wake | huwabariki waja wake | hawaachi waja wao | humwacha mja wake |
2. | yamkini | lakini | yakini | makini |
3. | ombi | dau | doa | dua |
4. | ushahidi | shahidi | ushuhuda | shahada |
5. | amani | amana | dhamana | imani |
6. | bure bilashi | kuntu kabisa | nzuri zaidi | nyingi mno |
Siku __7__ sote tulibakia uwanjani huku tukicheza mchezo wa __8__ yaani kibe. Mara tulimwona akiwa amesimama mlangoni. Mmoja wetu alitudokezea tukakimbia, tukaingia darasani na __9__. Tulijua kuwa mambo yalikuwa __10__. Tulingojea huku tukiwa na huzuni __11__ sisemi wasiwasi. __12__ kuhusu makosa yetu na __13__ kuwa tulikuwa tumemkosea mwalimu wetu. Mdarisi alipoingia tulisimama tisti na kumwomba msamaha. Mwalimu alifurahi na kutufunza __14__ badala ya kipindi cha Kiswahili alichokiandaa. Alitukumbusha kuwa heshima __15__.
A | B | C | D | |
7. | hilo | hio | hizo | hiyo |
8. | kukimbizana na kuangushana | kuiga na kuigiza majukumu ya wazazi nyumbani | watoto wa kujificha na kutafutana | kuvuta kamba kwa kushindania |
9. | kukimya | kunyamzana | kunyamaza | kuropokwa |
10. | yamezidi unga | yametumbukia nyongo | yametengenea sana | yameimarika zaidi |
11. | mwingi | mingi | wingi | nyingi |
12. | Tulichunguzwa | Tulikumbuka | Tulitafakari | Tulisahau |
13. | kukiri | kukana | kukanusha | kukataa |
14. | maadili | madili | adhabu | utundu |
15. | utumwa | haidumu kamwe | si utumwa | inadumu daima |
Kuanzia swali la 16 hadi la 30, jibu kulingana na maagizo.
- Maneno yafuatayo yatapangwaje katika kamusi?
- Pasa
- Paka
- Pakua
- Paku
- ii, iv, iii, i
- i, iii, iv, ii
- iii, i, ii, iv
- iv, ii, iii, i
- Kamilisha sentensi ifuatayo kwa maneno yafaayo.
__________wake amemnunulia _________ __________ nguvu _______________- Mzazi, fahali, enye, malindandi
- Msasi, fahari, mwenye, malidandi
- Mzazi, fahali, mwenye, maridadi
- Mzazi, fahari, enye, maridadi
- Chagua wingi wa sentensi ifuatayo.
Hakuelewa kuwa ningechelewa.- Hawakuelewa kuwa tungechelewa
- Hamkuelewa kuwa tungechelewa.
- Hamkuelewa kuwa ningechelewa.
- Hawakuelewa kuwa ningechelewa.
- Tambua sentensi sanifu inayolinganisha hizi.
Utubora alifaulu.
Utubora hakufurahi.- Lau Utubora alifaulu hakufurahi.
- Utubora hakufurahi aghalabu alifaulu.
- Utubora hakufurahi licha ya kufaulu.
- Maadamu Utubora hakufurahi alifaulu.
- 3051660 kwa maneno ni
- Milioni tatu, laki hamsini na moja mia sita sitini
- Milioni tatu elfu hamsini na moja mia sita na sita
- Milioni tatu hamsini na moja elfu, mia sita na sitini
- Milioni tatu hamsini elfu na moja mia sita na tisini
- Ni nini maana ya 'kutia masikio nta"?
- Kutojali yasemwayo.
- Kujali yasemwayo.
- Kuweka masikio vipuli.
- Kutia masikio pamba.
- Mwasaru alinipigia simu, nami nikampigia simu. Kwa hivyo sote wawili __________________________
- tulipigiana pigiana simu
- tulipigiwa simu
- tulipigana simu
- tulipigiana simu
- Ni methali gani iliyo na maana sawa na "polepole ndio mwendo"?
- Chelewa chelewa utapata mwana si wako.
- Haraka haraka haina baraka.
- Chovya chovya humaliza buyu la asali.
- Heri kenda kuliko kumi nenda rudi.
- Ni sentensi gani iliyo na kivumishi cha pekee?
- Kusafiri kwa gari moshi ni kuzuri
- Chakula hiki ni kitamu sana.
- Ukucha wangu umekatika.
- Nyumba yote iliteketea moto.
- Chagua ukubwa wa sentensi hii
Gari hili zuri, lina dirisha kubwa navmlango wa kupendeza.- Kigari hiki ni kizuri, kina kijidirisha kikubwa na kijilango cha kupendeza.
- Jigari hili ni zuri, lina jidirisha kubwa na lango la kupendeza.
- Jigari hili ni mzuri, lina dirisha kubwa na lango la kupendeza.
- Ligari hili ni zuri, lina dirisha kubwa na lango la kupendeza.
- Fuma ni kusuka nyusi. Vile vile fuma ni ____________________
- kudunga kwa kifaa chenye makali.
- kudunga kwa mtutu wa bunduki.
- kushona nguo paliporaruka.
- kupachika nguo kiraka kipya.
- Umbo lifuatalo ni
- Mstari sulubu
- Pembe butu
- Pembe kali
- Pembe nyoofu
- Chagua sentensi inayoonyesha ‘ji' ya nafsi.
- Uimbaji wake uliwatumbuiza wageni.
- Jibwa limefungiwa chumbani.
- Msomaji wa taarifa alisikika vizuri.
- Nilijisomea Riwaya ya Siku Njema.
- Ikiwa mtondogoo itakuwa Jumamosi Machi tarehe mbili 2023, jana ilikuwa lini?
- Jumatatu Februari tarehe ishirini na tatu
- Jumatatu Februari tarehe ishirini na saba.
- Jumatatu Februari tarehe ishirini na sita.
- Jumatatu Februari tarehe ishirini na tano.
- Mzee Weru ameishi miaka mingi sana. Yaani
- amekula siku zake
- ameona mambo mengi
- amekula tarehe
- amekula chumvi nyingi
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40
Waswahili husema kuwa safari ya kesho hupangwa leo. Waaidha, msafiri ni aliye bandarini. Mwanadamu anatakiwa awe na mpango madhubuti wakati anapohitaji kufanya jambo lolote; liwe jambo dogo au kubwa. Kimsingi ni kwamba, mtu hawezi akafyeka kichaka akalima, akapanda, akapalilia na kufaidi matunda kwa siku moja. Ni sharti mtu kujua kwamba mambo hutayarishwa hatua kwa hatua na kupatiwa muda ili yatengenee.
Mtahiniwa yeyote anafaa kujiandaa barabara wakati ambapo anaungojea mtihani wowote. Mtu hupata kufahamu wakati wa mtihani mapema zaidi. Kwa hivyo si vyema hata kidogo mtu kungojea hadi siku ya siku kuwa pua karibu na mdomo ili aweze kuanza kujiandaa. Mwanzo kabisa, ni sharti awe na ratiba yake binafsi. Ratiba huwa kama dira na rubani. Rubani anapokosa dira bila shaka atasalia pale hewani na wala hataweza kutua hata kidogo. Hivyo ndivyo ilivyo kwa mwanafunzi pia. Hakuna vile unaweza kuketi tu na kuchomoa kitabu na kuanza kusoma. Mwanafunzi anapofanya hivyo atajipata kuwa amesoma masomo anayoyapenda huku akiyasahau yale ambayo yanampa changamoto.
Mtahiniwa anapodurusu, afanye udadisi wa kutosha. Asichukue vitabu tu bila kufahamu kinachohitajika ili kujiandaa vyema ni lazima asome mwanzo akili ya mtahini. Atafanya hivi kwa kutazama karatasi zilizofanywa awali. Hili litamsaidia kusoma tu yale muhimu kwa mujibu wa kuupasi mtihani huo. Mtu anaposomasoma kila kitu hata kisichomhusu atamalizia kuyajua mambo mengi zaidi ambayo hayamhusu ndewe wala sikio. Huu ndio unaoitwa ukasuku katika kusoma. Hebu nikuulize, je, mwanafunzi anaweza kufaulu kwa kusoma magazeti tokea asubuhi hadi jioni? Hapo nafikiri hatafua dafu mtihanini.
Aidha, mwanafunzi anashauriwa kuwa pahali pake pa kusomea pasiwe karakana. Yaani pasiwe na kelele wala vitu vinavyoweza kumchachawiza msomaji akaacha kusoma. Ijapokuwa wengine hupenda kudurusu huku wakisikiliza muziki, ni bora kuwe kutulivu na shwari kwa uelewa aula. Vile vile, sehemu hiyo iwe na hewa safi; madirisha yafunguliwe, pasiwe baridi sana au joto kupita kiasi. Licha ya hayo, aandae vifaa vyake mapema, mathalan meza, kiti, vitabu, kalamu, karatasi na vingine vingi vinavyohitajika. Fauka ya hayo, awe na saa ili aweze kuyapatia masomo yake wakati maalum.
Kusoma pia kuna mipaka. Mwanafunzi asijilazimishe na kujipagaza bure hasa anapoona kwamba anasinzia. Inafaa ajipumzishe kidogo au atembee kidogo ili kupata hewa safi, halafu arudie kusoma. Ikiwa ni usiku, anaweza hata akaenda kulala ili aamke alfajiri kuendelea na masomo wakati hana chelewa ya usingizi. Ifahamike kwamba binadamu anapaswa angalau kulala muda wa saa sita na saa nane ili akili na mwili viweze kufanya kazi vyema. Pia, anaposoma, ahakikishe kwamba hana njaa wala kushiba sana kupita kiasi.
Wakati wa mtihani, mtahiniwa anafaa kuamka mapema kama kawaida. Afike darasani kabla ya muda rasmi wa kuanza mtihani. Apatiwapo karatasi ya maswali, asome maagizo kwa makini na ayaelewe vizuri kabla ya kuanza kujibu maswali. Kufuata maagizo aliyopewa pia ni sehemu ya mtihani. Asilimia kubwa ya watahiniwa hufeli mtihani kwa kuyapuuza maagizo yaliyotolewa. Kumbuka kuwa mtu hutungiwa mtihani, hajitungii mwenyewe.
- Mwandishi anazingatia nini katika aya ya kwanza?
- Mtu akifanya maandalizi vyema anaweza kuvuna siku hiyo hiyo
- Hakuna haja ya kuyafanya mambo hatua kwa hatua ila kwa mkupuo
- Ili jambo lolote kufanikiwa linahitaji kupewa subira
- Wakulima ndio watu wanaotakikana kuwa na subira
- "...akafyeka kichaka, akalima, akapanda, akapalilia..." 'ka' imetumikaje katika muktadha huu?
- Mfululizo wa matukio
- Kuradidi kwa matukio
- Usisitizo wa matukio
- Mkururo wa matukio
- Ratiba kwa mwanafunzi imemithilishwa na
- ndege kwa rubani
- mwanafunzi na bidii
- mtahiniwa na mtihani
- dira kwa rubani
- Mwanafunzi anayesomasoma tu bila kuwa na ratiba hutokewa na nini?
- Kufeli katika mitihani yake kila mara
- Kuyasoma masomo anayoyahenzi pekee
- Kuyadurusu hata yale masomo asiyoyapenda
- Hujiandaa barabara dhidi ya mitihani ijayo
- 'Ukasuku katika kusoma' unamaanisha nini kulingana na mwandishi?
- Kusomasoma mambo mengi ambayo hayakuhusu
- Kusomasoma kwa kukariri tu bila kuelewa
- Kusoma jinsi kasuku anavyosoma
- Kusoma na kuropokwa kwa kuiga kasuku
- Ni kwa nini mwanafunzi anafaa kusomea mahali patulivu?
- Ili aweze kuwa na vitu vinavyohitajika
- Kuna wengine wanaopenda kusoma huku muziki ukidunda
- Ili yanayosomwa yaweze kueleweka bila shida yoyote
- Kwa kuwa muziki hautahiniwi katika mtihani wowote
- Mwanafunzi anayesoma tu somo moja kila wakati hatimaye
- hupita vizuri mitihani yake
- hujiburudisha
- huchoka akili
- hafaulu mtihani wake
- Ni mambo gani mwanafunzi hafai kufanya anapodurusu ili kujiandaa kufanya mtihani?
- Asome mchana na usiku bila kupumzika
- Ale lakini asishibe kupita kiasi
- Asisome huku akiwa na chelewa yamusingizi
- Asiendelee kusoma iwapo anahisi uchovu
- Mwanafunzi anapofanya mtihani bila kusoma na kufuata maagizo ni sawa na
- anayefanya mtihani akipanga kufeli
- anayejitahini na kuyajibu maswali yake mwenyewe
- wanafunzi wale werevu wanaoanguka mtihani
- anayechelewa kufika kwenye chumba cha mtihani
- Baadhi ya wanafunzi waliojiandaa vyema hufeli mtihani kwa
- kufanya mtihani pasi kusoma maagizo
- kufanya mtihani palipo na kelele nyingi
- kuanza kujibu maswali pasi kusoma na kuelewa maagizo
- kufanya asilimia kubwa ya maswali kwa papara
Soma habari inayofuata kisha ujibu maswali 41-50
Nilikuwa nimeungojea wakati huo kwa hamu na ghamu. Japo niliona kuwa siku hiyo ilikuwa mbali, hauchi hauchi unakucha, hatimaye iliwadia. Mwalimu wetu alikuwa anasisitiza kuwa achanikaye kwenye mpini hafi njaa; waaidha, mchumia juani hulia kivulini. Wahaka usio na kifani ulinivaa kwani nilifahamu kuwa ni vyema kujiandaa mapema ili niende kupokea Hidaya yangu. Furaha mpwitompwito ilinivaa kwelikweli.
Niliondoka kitandani huku nikiimba nyimbo za furaha. Nilijua kuwa safari yangu ingechukua takriban saa tatu unusu. Tayari ilikuwa saa thenashara na sherehe ingeanza mida ya saa nane. Kwa pupa nilivalia sare zangu za shule yangu ya awali. Mwalimu mkuu ambaye angeandamana nami alikuwa amenishauri niweze kuvalia sare hizo. Hafla hiyo yote ingeonekana kwenye televisheni zote nchini. Alikuwa akitaka sare hiyo ipate kunadi shule yake ambayo ilikuwa haijatia fora kwa mwongo mmoja mtawalia. “Shule ya upili ya Busara itatambuliwa leo na dunia nzima," nilijisemea kimoyomoyo. Niliwaza na kuwazua kuhusu maisha ya chuo.
Baada ya kujiandaa, niliharakisha kufika katika kituo cha mabasi. Inshallah, nipate basi bado halijaondoka. Mwalimu mkuu alikuwa tayari amekata nauli ya watu wawili. Basi lenyewe lilikuwa jipya. Mlikuwa na abiria wengi ambao walikuwa wameabiri. Basini mlikuwa na viti vinne ambavyo havikuwa na abiria. Mwalimu aliniambia kuwa twende kutafuta staftahi. Tuliandamana naye kuelekea kwenye mkahawa tukanywa chai kwa mahamri. Japo mwalimu alitaka tunywe kwa haraka, chai ile ilikuwa moto ajabu. Hata hivyo, tulijikaza tukaimaliza. Tulirudi kituoni huku tukihema na kutweta. Tulifahamishwa kuwa basi lilikuwa limeondoka. Kwa hivyo ilitulazimu kusubiri saa moja kabla ya basi jingine kufika. Nilitekwa na hisia za huzuni lakini nikajizuia kulia. Hapo ndipo nilianza kusinzia na kukumbuka maisha yangu yalivyokuwa.
Nilikuwa nimezaliwa katika familia ya ukata. Mazingira niliyokulia yalikuwa yenye matatizo chungu nzima. Haya ndiyo yaliyonifanya kusoma kwa bidii ili niinusuru familia yetu kutokana na uchochole. Nilipopelekwa katika shule ya msingi nilitia fora masomoni nikaweza kujiunga na shule ya sekondari ya kutwa pale karibu na kwetu. Kupitia wadhamini wenye ukarimu si haba niliweza kukamilisha masomo yangu na kupata alama ya A iliyonipa hadhi niliyokuwa nayo.
Mawazo yangu yalikatizwa na milio ya hofu. Mwalimu wangu aliniashiria kitu. Nilipotazama upande wangu wa kulia niliona basi ambalo nilikuwa nikilisubiri likigongana na lori la takataka. Niliharakisha kwenda kuwasaidia watu waliokuwa wamejeruhiwa. Kwa nyota ya jaha, wote walikuwa salama salimini. Lakini tatizo la usafiri likatokea tena. Basi hilo lilihitajika kukarabatiwa tena kabla ya kuendelea na safari. Pasipo budi hubidi.
Punde si punde, simu ya mwalimu ilitoa mlio. Alitazama kidogo kisha akaanza kutetemeka kama aliyetoka kwenye friji. "Wamepiga simu" alisema. Aliichukua, akazungumza nayo kisha nikaona akitabasamu. Baada ya kumaliza, alinifahamisha kuwa sherehe ile ilihairishwa hadi wiki ambayo ingefuata. Nilifurahia sana kwa kuwa nilikuwa nimekata tamaa-muda wetu ulikuwa umekwisha. Tuliamua kurudi nyumbani japo tulikuwa tumechoka hoi bin tiki.
- Ni kwa nini mwandishi wa makala haya alikuwa na furaha?
- Siku yenyewe ilikuwa imengojewa kwa hamu na ghamu
- Jitihada zake masomoni zingetambuliwa siku hiyo
- Alikuwa ametuzwa kwa bidii zake
- Maisha yake yangebadilika siku hiyo
- Kulingana na aya ya pili ni kweli kusema kuwa
- mwandishi alikuwa amefaulu katika mtihani wa shule ya msingi
- shule ya Busara ilikuwa na utamaduni wa kung'aa mtihanini
- mwandishi hakutarajiwa kuvalia sare ya shule ya awali
- hafla hiyo ilitarajiwa kuonyeshwa kwenye televisheni za kitaifa
- Msimulizi alivalia sare
- kwa kuwa alinuia kuitumia kunadi umaarufu mpya wa shule hiyo
- alikuwa amefanya vizuri katika mtihani uliotangulia
- kwa kuwa alikuwa na furaha mpwitompwito
- kwa kuwa walikuwa waandamane na mwalimu mkuu
- Mwandishi wa makala haya alitarajiwa kufika shereheni saa ngapi?
- Saa thenashara
- Saa nane mchana
- Saa saba za asubuhi
- Saa kumi na mbili
- Lengo la kujitahidi masomoni ilikuwa
- kuinua hali ya jamii aliyoishi
- kujipatia shahada na kazi bora
- kuimarisha hali ya jamaa yake
- kupata tunu maridhawa
- Kuachwa na basi kwa mwandishi
- kulimkumbusha shida alizokulia kijijini
- kulimfanya akate tamaa kuhusu zawadi yake
- kulimfanya aende kutafuta staftahi
- kulimfanya afanye bidii masomoni
- Taarifa hii inatoa sifa gani kwa mwandishi wa makala haya?
- Mkakamavu, mwenye moyo mwepesi
- Mkakamavu, mwenye moyo thabiti
- Mchochole, mwenye moyo thabiti
- Mlegevu, mwenye mori kubwa
- Tunajifunza nini kuhusiana na maisha ya mwandishi?
- Mafanikio hupatikana tu wadhamini wakijitolea
- Wanaojiunga na shule za kutwa hujiunga na vyuo vikuu
- Wenye elimu ya juu hupata tunu masomoni
- Mafanikio huweza kupatikana hata na walio na uwezo duni wa kifedha
- Mwandishi alitabasamu katika aya ya mwisho kwa kuwa
- alikuwa na nafasi nyingine ya kuhudhuria sherehe
- alimwona mwalimu wake akitabasamu
- aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kuchoka
- hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali iliyotendeka
- "... kutetemeka kama aliyetoka kwenye friji." Ni tamathali gani ya lugha iliyotumiwa kwenye kifungu hiki?
- Methali
- Istiari
- Tashbihi
- Msemo
INSHA
Andika insha ya kusisimua isiyopungua ukurasa mmoja na nusu huku ukimalizia kwa kifungu kifuatacho:-
..................................................................nilifurahishwa na tabia ya utu wema wa rafiki yangu.
MARKING SCHEME
- A
- C
- D
- C
- D
- A
- D
- C
- A
- B
- D
- C
- A
- A
- C
- A
- C
- A
- C
- C
- A
- D
- B
- D
- B
- A
- D
- D
- D
- D
- C
- A
- D
- B
- A
- C
- C
- A
- B
- C
- B
- D
- A
- B
- C
- A
- B
- D
- A
- C
Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 1 Exams 2023 Set 7
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 1-5
Katee alimwalika rafiki Kilo wanywe chai mjini. Kilo aliomba waandamane na binamu yake koko. Basi Kilo alimwambia Koko ajiandae waende mjini Koko alifurahi sana na akajiandaa upesi.
Walipofika mjini, walimkuta Katee akiwasubiri katika hoteli iliyoitwa Fahari. Waliagiza chai na mandazi. Wakaletewa vikombe, sukari kwenye kikopo na vifuko vya majani.
Koko alichukua kifuko cha majani alikuwa tayari kukirarua ili ayatie majani kwenye kikombe Kilo alipoona vile alishtuka sana. Akashika bega na kumtuliza.
"Kaka kwanza tuiombee chai" Kilo alimsihi kwa sauti ya chini. Badala ya kuomba Kilo alimshauri Koko kwa lugha ya mama kuhusu jinsi ya kutumia kifuko kile cha majani. Hakutaka Koko awatie aibu pale hotelini.
- Kwa nini Koko alifurahi?
- Kwa sababu alikuwa aende mjini
- Alikuwa amepita mtihani wake
- Alikuwa ametumwa mjini
- Alikuwa amepewa zawadi na Kilo
- Vyote hivi vililetwa mezani kule mkahani ila
- sukari
- majani
- mandazi
- sharubati
- Neno hoteli liko katika ngeli ya
- I-I
- I-ZI
- LI-YA
- U-ZI
- Ni kweli kusema kuwa
- Katee na Kilo walimchukia Koko
- Koko hakufahamu jinsi ya kutumia kifuku. cha majani
- Koko ndiye aliombea chai
- Watatu hawa hawakupenda chai
- Kwani nini Kilo alimshauri Koko kwa lugha ya mama? Kwa sababu
- ndiyo lugha tu angeelewa
- hakufahamu vyema Kiswahili
- alitaka watu wengi wasisikize alivyomweleza jinsi ya kutumia mayai
- ndiyo lugha ya taifa
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu swali 6-10.
Nina rafiki mmoja, mwenye mguu mmoja
Tunapokuwa pamoja, mimi huona kioja
Anasema ngoja haja, napiga hatua moja
Fumbo hili ni la haja, jibu lake hilo laja.
Rafiki huyo mmoja, mwenye muundi mmoja
Ana jina lake moja, ni uyoga nalitaja
Nilimla siku moja, alipikwa na Khadja
Fumbo hili ni la haja, jibu lake hilo laja
Nina rafiki wa pili, nikila anajongea
Japo yeye hali, mezani amezoea
Rafiki huyo mkali machozi ananitoa
Matega kitendwali, fumbo ninakufumbia
Huyo rafiki wa pili, sasa namueleza
Ni kiungo cha halali, wengi wamekizoea
Kinaitwa pilipili, machoni kinasumbua
Nategua fumbo hili, jibu nimekupatia
- Mshairi ana rafiki mmoja mwenye mguu mmoja, rafiki huyo anaitwa?
- Bendera
- Uyoga
- Pilipili
- Kiungo
- Ni ipi ni sifa ya rafiki wa pili wa mshairi?
- Yeye humfanya atabasamu
- Humtoa machozi machoni
- Humtoa neno kinywani
- Ni mtamu kama hatua
- Shairi hili lina beti ngapi?
- Tano
- tatu
- Sita
- Nne
- Vina vya kati katika ubeti wa mwisho ni?
- a
- li
- u
- ja
- Neno kioja lina silabi ngapi?
- Tatu
- Nne
- Tano
- Mbili
Soma kifungu hiki kwa makini kisha uchagua jibu bora zaidi kujazia mapengo yaliyoachwa 11-15.
Katika shule ___11___ kuna duka. Duka hili ___12___ na wanaskauti. Bidhaa ___13___ huuzwa dukani humo ni ___14___ kalamu, madaftari, vichongeo na vifutio. Wanaskauti hutumia ___15___ inayotokana na maunzo ya bidhaa hizi kuwasaidia watoto wenye mahitaji ya kimsingi.
A | B | C | D | |
11. | yetu | kwetu | sababu | petu |
12. | linaposimamia | linasimamisha | linasimamiwa | linasimamika |
13. | ambayo | ambazo | ambako | ambamo |
14. | , | ! | ; | ? |
15. | riba | hisa | kodi | faida |
Kuanzia swali la 16-30. Jibu kulingana na maagizo.
- Kati ya maneno haya chagua neno linalopatikana kati ngeli ya U-I
- mali
- nywele
- mpera
- kucheza
- Maneno yafuatayo hupangwa vipi kwenye kamusi gonga, ganda, gamba, godoro.
- ganda, gamba, godoro, gonga
- gamba, gonga, ganda, godoro
- ganda, gamba, gonga, godoro
- gamba, ganda, godoro, gonga
- Andika kwa wingi
Wavu wa mvuvi unastahili kuwa na shimo kubwa- Nyavu za mvuvi zinastahili kuwa na shimo kubwa
- Nyavu za wavuvi zinastahili kuwa na mashimo makubwa
- Nyavu za wavuvi zinastahili kuwa na shimo kubwa
- Wavu za wavuvi zinastili kuna na mashimo makubwa
- Kanusha:
Maseremala walitutengenezea madawati- Maseremala hawakututengenezea madawati
- Maseremala hakutengeneza madawati
- Seremala alitulengenezea dawati
- Maseremala waliharibu madawati
- Ukubwa wa neno mlango ni
- Kilango
- jilango
- mlango
- lango
- Umesimuliwa hadithi na mlezi wako sasa ni wakati wa kulala. Chagua maagano utakayotumia kumwaga mlezi wako
- kwaheri
- alamsiki
- masalkheri
- buriani
- Changua methali inayotoa maana na maelezo kuwa mtoto huchukua tabia za walezi na watu walio karibu naye
- Mwana hutazama kisogo cha mamaye
- Mchelea mwana hulia mwenyewe
- Asiyesikia la mkuu huvunjika guu
- Mchimba kisima huingia mwenyewe
- Wachezaji wana nidhamu _______________________ huheshimu refarii.
- wao
- wewe
- yeye
- nyinyi
- Tunasema thureya ni kwa nyota. Tutasema ______________________ ni kwa nyuki.
- bunda
- bumba
- wingu
- mkusanyiko
- Levi ni wembe masomoni. Hii ina maana kuwa yeye ni _________________________
- mwenye subira
- jasili
- mwenye bidii
- mwerevu
- Ni sentensi ipi sahihi.
- Palipo na siafu hakukaliki
- Palipo na siafu hamukaliki
- Mlimo na siafu hapakaliki
- Kuliko na siafu hakukaliki
- Tegua kitendawili
Niendapo hinifuata _______________________- mauti
- kivuli
- jua
- nzi
- Kipi si kiungo cha mapishi?
- Sukari
- Bizari
- Unga
- Nyanya
- Kitenzi nawa katika kauli ya kutendesha ni
- navya
- nawisha
- nawishia
- nawia
- Tunda lilianguka sakafuni
- kacha!
- chubwi!
- pu!
- tifu!
MARKING SCHEME
- A
- D
- B
- B
- C
- B
- C
- D
- B
- A
- A
- C
- B
- C
- D
- C
- D
- B
- A
- D
- B
- A
- A
- B
- D
- D
- B
- C
- A
- C
Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 1 Exams 2023 Set 6
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali yafuatayo.
Akilibora Ujingakutu ni mwenye heshima na busara. Alijitahidi asikasirike ovyoovyo hadharani. Kukasirika ovyo kunamfanya mtu aonekane baradhuli. Mtu huyu hakukasirika hata kama ungemwudhi kiasi gani. Labda alizificha hamaki zake kwa sababu mwungwana hakasiriki usoni, hukasirika moyoni.
Alipoitwa shuleni Hekimautu kuongea na wanafunzi, hakutarajia kuzungumza kwa muda mrefu. Alikuwa na maneno machache tu ya kuwaeleza wanafunzi wote ukumbini. Alinena kuhusu umuhimu wa kurauka na kuenda shuleni kusoma. Pia alieleza kuwa darasani ni mahali pa kukipa kichwa nafasi, wakati na uwezo wa kuchora mambo na kuyaweka kichwani ili yatumike katika maisha ya baadaye.
Maswali
- Akilibora Ujingakutu alikuwa ________________________________
- mwungwana
- mjinga
- mwalimu
- mkali
- Kisawe cha heshima ni ________________________________
- hekima
- taadhima
- huruma
- akili
- Akilibora alialikwa kumaanisha alipatiwa:-
- mwaliko
- wito
- mwali
- uwakilishi
- Sifa za mwungwana ni __________________________________
- kuhamaki
- kuficha hasira.
- kununa
- kufunza
- Bwana Ujingakutu hakuwafunza wanafunzi kuhusu:-
- wakati wa kuenda shuleni kusoma.
- umuhimu wa kufika shuleni mapema.
- umuhimu wa darasa.
- manufaa ya kuenda shuleni.
Jibu maswali kulingana na kisa hiki.
Siku moja ndovu alikuwa akipita kwenye msafara wa siafu. Aliwakanyaga bila kujali kuwa siafu waliumia. Siafu walijaribu sana kumwuma ndovu kwa nguvu zao zote lakini ndovu hakuhisi uchungu. Alizidi kuwakanyaga siafu. Siafu walizidi kuumia na kulalamika ila hakuna aliyewasaidia. Siafu mmoja aliamua kutambaa polepole hadi kwenye mwiro wa ndovu. Aliingia ndani na kutulia tuli! Ndovu hakujua chochote. Mara alianza kumwuma ndani kwa ndani kwenye mwiro wake.Ndovu alihisi uchungu mwingi. Aliendelea
kumwuma kwa muda mrefu. Ndovu alijaribu kupiga chafya lakini siafu yule hakutoka. Ndovu akaenda penye mti mkubwa. Akaanza kuuchapa mwiro kwenye mti hadi ukatoka damu. Siafu hakutoka. Aliendelea kujiumiza kwenye mti ule hadi akafa. Hatimaye siafu alienda zake.
Maswali
- Ndovu alipokuwa akipita alikanyaga __________________________
- msafara
- siafu
- nyasi
- mwiro
- Msafara wa siafu ni siafu _________________________
- wakali
- wadogo
- wanyonge
- wengi
- Siafu walipokanyagwa ___________________________
- walilia
- waliumia
- waliamka
- walikimbia
- Siafu aliyemwuma ndovu aliingia wapi? Kwenye:-
- pembe
- mkonga
- jicho
- mdomo
- Ndovu alijaribu kumtoa siafu kwa kuupiga mwiro mtini na _____________________
- kupiga mayowe
- kulia
- kuenda miayo
- kupiga chafya.
Soma kifungu kisha ujibu maswali barabara.
Jina la mjomba wangu ni Simu Sumu. Ana simu nzuri sana. Anakipenda kifaa hiki sana na mara nyingi hukisifia kuwa kimeifanya dunia kuwa kimoja au vitu viwili vilivyounganishwa kwa sauti moja. Lakini kwa upande mmoja,mjomba anachukia zaidi jinsi watu wanavyotumia simu kuwadanganya wengine. Watu hudanganya kuwa hawapo karibu kumbe wapo! Wabaya zaidi ni matapeli wanaowaibia wengine kupitia rununu.
Mjomba alitumiwa pesa hewa shilingi elfu kumi. Ndani ya simu yake alikuwa na pesa zake zaidi ya shilingi elfu kumi. Tapeli akamwandikia arafa kuwa amemtumia shilingi elfu kumi. Kabla ya mjomba kutulia akili, alipigiwa simu kuwa pesa hizo alitumiwa kwa bahati mbaya. Akaombwa azirudishe pesa zile kwa mtumaji. Mjomba kwa huruma, akatuma pesa alizoulizwa. Alipoangalia salio la akiba yake, alipata kuwa imepungua. Akagundua kuwa alimtumia tapeli pesa zake. Kuanzia siku hiyo, mjomba anazichukia simu zote za matapeli. Hizo ndizo anazoita simu sumu!
Maswali
- Mjomba wangu ana simu __________________________
- kubwa
- sumu
- nzuri
- ghali
- Mjomba anachukia zaidi watu gani?
- Matapeli wa kutumia simu.
- Wateja wasiopatikana.
- Wadanganyifu kwa simu.
- Wanaoandika arafa.
- Pesa hewa ni pesa zipi?
- Za kuiba
- Nyingi
- Bandia
- Ambazo hazipo.
- Mjomba anaziona simu za udanganyifu kama _____________________________
- simu
- wazimu
- sumu
- sima
- Maandishi yanayotumwa kwenye simu ni ________________________________
- arifa
- arifu
- taarifa
- arafa
Jaza mapengo kwa majibu mwafaka.
Taa ___16___ umeme ___17___ mwangaza ___18___kutosha. Giza ___19___ usiku hutoweka mpaka usiku ___20___ kama mchana.
A | B | C | D | |
16. | ya | la | wa | cha |
17. | una | ina | zina | yana |
18. | za | la | wa | ya |
19. | ya | za | la | cha |
20. | ikiwa | yakawa | ukawa | zikawa |
Kamilisha kwa kufuata maagizo.
- Mfupa unaoshikilia meno kinywani unaitwa ___________________________-
- ufizi
- ulimi
- utaya
- midomo.
- Jozi ipi isiyo na maneno yenye sauti tata?
- kacha- kasha
- ponda - poda
- chuma - chama
- piga - pinga
- Maneno haya yatafuatana vipi katika kamusi?
- chunga
- chupa
- chanda
- changa
- iii, iv, ii, i
- i, iv, iii, ii
- iii, i, iv, ii
- iii, iv, i, ii
- Mtoto yule mzembe haandiki vizuri. Kivumishi kionyeshi ni kipi?
- mtoto
- mzembe
- yule
- vizuri
- Kamilisha: Mfupa ______________________________
- mkubwa
- kubwa
- mikubwa
- makubwa.
- Sentensi ipi iliyo na kiashiria cha mbali kidogo?
- Mzee yule amelala.
- Mti huo utakatwa.
- Kalamu hizi haziandiki.
- Ndoo zao zinavuja.
- Neno hoki ni aina gani ya neno?
- Kitenzi
- Nomino
- Tahajia
- Ngeli.
- Sentensi: Maji mengi yamemwagika chini ina kivumishi kipi cha idadi?
- jumla
- kamili
- wingi
- katika orodha.
- Mchezo wa kuvutana kamba huitwa:-
- sataranji
- raga
- jugwe
- mwereka.
- Endeleza:
Ulinunua vitabu _______________________________________?- ngapi
- vigani
- zipi
- vingapi
INSHA.
Andika insha ya wasifu kuhusu 'MWILI WANGU'
MARKING SCHEME
- A
- B
- A
- B
- A
- B
- D
- B
- B
- D
- C
- A
- D
- C
- D
- A
- B
- C
- C
- C
- C
- C
- D
- C
- A
- B
- B
- A
- C
- D
Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 1 Exams 2023 Set 5
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 1-5.
Tuta na Twita walikuwa wavulana. Walipendana kama chanda na pete. Walisoma katika shule moja.
Ajabu ni kwamba wote walikuwa na umri sawa. Walikuwa wakisoma kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.
Jumamosi na Jumapili walipumzika nyumbani kwao na kufanya kazi za ziada kutoka shuleni. Baada ya
kumaliza kazi za ziada, walipendelea kuenda kucheza.
Siku moja Tuta na Twita waliamua kwenda msituni kuwinda ndege kwa manati. Ilikuwa siku ya
Jumapilii. Walipofika msituni, waliendelea kuwawinda ndege. Waliendelea na mchezo wao hadi masaa ya
adhuhuri. Tuta akamwuliza Twita," Rafiki yangu,tutakula nini? Mimi ninahisi njaa!" Twita akasema "Mimi
nina kiporo ndani ya mfuko wa kaptura yangu. Sina wasiwasi!"
Maswali
- Tuta na Twita walikuwa wavulana ndiko kusema
- walikuwa vijana
- walikuwa watoto wa kiume
- walikuwa duma
- walikuwa wanaume.
- Walipendana kama chanda na pete inamaanisha
- walipendana sana
- walipendana kidogo tu
- walipenda pete na chanda
- walikuwa wapenzi.
- Wote wawili walikuwa na umri sawa. Kumaanisha walikuwa
- pacha
- ndugu
- marika
- kaka.
- Ni yupi aliyehisi njaa walipokuwa msituni?
- Hatujaambiwa
- Twita
- Tuta
- Rafiki.
- Twita alikuwa na kiporo. Hiki ni chakula
- cha nyama
- cha ugali
- kilicholala
- cha msituni.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 6-10.
Mama aliniacha nyumbani na mtoto wetu mdogo. Nilimpenda sana mtoto wetu Nurika. Tulicheza na kucheka pamoja. Nilimwimbia wimbo mzuri. Nurika alikuwa mtoto mwenye furaha. Mara nilisikia mlango wa nyumba ukigongwa. Nikaitikia, "karibu!" Nilidhani ni rafiki yangu Sifu aliyekuja kwetu kucheza
nami.
Nilipoufungua mlango, nilimwona mtu mgeni kabisa Akaniuliza, "Mama yako yuko wapi?" Nilimjibu, "Ameenda sokoni." Mgeni aliketi hata kabla nimwambie aketi.Akaniambia:"Mimi ni rafiki ya mama yako. Nitamngoja mpaka aje kutoka sokoni. Nenda dukani ukaniletee soda ninywe nikimsubiri, Nina kiu sana!" Alinipa pesa.Nikakimbia dukani kumletea soda.
Nilipotoka dukani, sikumkuta. Alitoweka na mtoto wetu Nurika. Polisi bado wanamtafuta mama huyo.
Maswali.
- Mwandishi alipoondoka alimwachia nani mtoto?
- Mama yangu
- Mama mgeni
- Nyanya
- Nurika.
- Aliyebisha mlango bila shaka alisema nini?
- Karibu
- Hodi
- Niingie
- Nani yupo?
- Mgeni aliyeingia alikuwa
- mwanamke
- rafiki
- askari
- mwanamume.
- Mgeni alimtuma mwandishi soda ili
- akunywe
- anywe
- akule
- ya kukunywa.
- Kulingana na kisa hiki mgeni alikuwa na tabia gani?
- Mkweli
- Mzalendo
- Mwema
- Mwenye mkono mrefu.
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 11-15.
Magari yoyote ya kuwabebea abiria huitwa matwana. Katika matwana mna mabasi au kwa umoja basi. zipo matatu au kwa jina jingine ni daladala. Magari yote haya hulipisha nauli ndipo yatoe huduma za usafiri. Anayelipa nauli ili asafiri huitwa abiria. Mahali ambapo magari yote huegeshwa ili yaanze safari tena upya huitwa kituoni au stesheni ya mabasi au kituo cha matwana.
`Anayeendesha gari huitwa dereva. Anayemsaidia dereva kupanga abiria ni utingo. Yeye ndiye
anayepokea nauli. Hulipisha abiria kulingana na mahali wanapoenda iwapo ni mbali au karibu. Matwana
husimama kwa muda mfupi stanini ili kushusha au kubeba abiria. Madereva wanafaa kuyaendesha magari kwa utaratibu mkubwa ili kuzuia ajali.
Maswali
- Magari ya kuwabeba abiria kwa jina maalum ni
- matwana
- matatu
- mabasi
- daladala.
- Malipo anayotozwa abiria ili asafiri ni
- tikiti
- ada
- risiti
- nauli.
- Watu wanaotumia magari kusafiri wanaitwa
- wasafiri
- wafanyikazi
- abiria
- utingo.
- Dereva ni mtu ambaye ________________________________ gari.
- huongoza
- huendesha
- hupeleka
- huchukua
- Ajali nyingi husababishwa na madereva
- wasiomakinika
- wenye utaratibu
- wanaomakinika
- waangalifu.
Jaza mapengo kwa majibu sahihi.
Chakula ___16___ kitamu watu hufurahia. Mimi hupenda chakula ___17___ na ___18___. Sitaki ___19___
chakula ___20___kwa sababu husababisha maradhi ya tumbo
A | B | C | D | |
16. | kikiwa | ikiwa | ukiwa | yakiwa |
17. | nzuri | mzuri | tamu | kitamu |
18. | kisa | safi | mzuri | nyingi |
19. | nile | nikule | kukula | kuikula |
20. | chafu | kichafu | mchafu | uchafu |
Chagua jibu mwafaka kulingana na maagizo.
- Kiungo cha kusafisha hewa ni
- maini
- figo
- moyo
- pafu.
- Miti _________________________ ilikatwa ni hii.
- ambao
- ambaye
- ambayo
- ambazo
- Mchezo wa kuvutana kwa kamba ni
- ndondi
- njugwe
- jugwe
- mwereka
- Ukubwa wa nguo ni
- manguo
- guo
- kiguo
- vinguo
- Kitenzi 'cheza' katika hali ya mazoea ni
- hucheza
- amecheza
- hajacheza
- atacheza.
- Kivumishi kionyeshi ni kipi katika sentensi ifuatayo?
Watoto hao watacheza vizuri sana- Sana
- Vizuri
- Hao
- Watoto.
- Kiambishi cha nafsi ya pili katika wingi ni
- yeye
- wewe
- wao
- nyinyi.
- Akifisha sentensi ifuatayo.
Mbona unatembea polepole- !
- ?
- :
- ,
- Chagua jozi ya vitate.
- cheka - chora
- fika - pika
- buda - bunda
- gamba - gumba
- Msimu wa baridi kali ni
- kipupwe
- kiangazi
- vuli
- masika.
INSHA
Mwandikie rafiki yako barua ukimshauri jinsi ya kufaulu katika masomo.
MARKING SCHEME
- B
- A
- C
- B
- C
- B
- B
- A
- B
- D
- A
- D
- C
- B
- A
- A
- D
- B
- A
- B
- D
- C
- B
- B
- A
- C
- D
- B
- C
- A
Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 9
MASWALI
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umpewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi.
Visa vya uhalifu vinaweza kugeuka na kuwa .............1................ la kitaifa iwapo .............2............... na serikali. Wananchi wengi ...............3............. nchini mwetu .............4............... na ..............5.............. mali ..............6.............. hususan katika miji yetu. Mikakati madhubuti inapaswa kuwekwa ili ............7................ wahalifu ..............8.............. maendeleo. Ikumbukwe kuwa idadi kubwa ya vijana .............9............... watu huishi pamoja na raia wa kawaida kwani .............10.................
-
- tabu
- shida
- mkasa
- janga
-
- havitathibitiwa
- havitadhibitiwa
- havitadibithiwa
- havitathaminiwa
-
- huku
- humo
- humu
- mle
-
- huvamiwa
- huvamia
- hukabiliana
- hukumbana
-
- kuibwa
- kunyang'anywa
- kukabidhiwa
- kukabwa
-
- wao
- lao
- zao
- yao
-
- kuwatia mbaroni
- kuwatia kiwi
- kuwatia hamasa
- kuwatia kiwewe
-
- wanaoduwaza
- wanaoshurutisha
- wanaodidimiza
- wanaoandamana
-
- inayohangaisha
- wanaohangaisha
- wanahangaisha
- inahangaisha
-
- kinga na kinga ndipo moto uwakapo
- kikulacho ki nguoni mwako
- usipoziba ufa utajenga ukuta
- pwagu hupata pwaguzi
Likizo ..............11............... tulimzuru nyanya mashambani. Wakati ...............12.............. alitupokea kwa furaha tele. Babu alikuwa ...............13.............. kivuli chini ya mbuyu. Tulimkabidhi nyanya mzigo uliojaa. .............14................ matunda, sukari, unga na kilo tano za mchele. ...............15.............. kuingia chumbani, nyanya aliomba na kumshukuru Mungu. Tukajiunga na babu chini ya mbuyu.
-
- iliopita
- ilipopita
- iliyopita
- ilikopoita
-
- tulipofika
- tutakapofika
- tunafika
- tulifika
-
- katikati
- kati ya
- chini ya
- kwenye
-
- !
- :
- ;
- ,
-
- Kabla ya
- Baada ya
- Sembuse
- Mradi
Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi
- Kukanusha kwa: "Mti ambao ulikatwa umeanza kukauka, 'ni:
- Mti ambao ulikatwa haukuanza kukauka
- Mti ambao haukukatwa haujaanza kukauka
- Mti ambao ulikatwa haujaanza kukauka
- Mti ambao haukukatwa haujaanza kukauka
- Ni sentensi ipi ambayo ina matumizi ya kiambishi "ki' cha wakati pekee?
- Chakula kikipikwa nitafurahi sana
- Dereva alipoingia garini alimpata akilala
- Kitabu hiki kina picha za kupendeza
- Shangazi anatembea kijeshi
- Ikiwa keshokutwa itakuwa Alhamisi, juzi ilikuwa:
- Jumatatu
- Jumamosi
- Ijumaa
- Jumapili
- Somi ameolewa na Hamisi. Dada yake Somi ameolewa na Charo. Hamisi na Charo wataitana:
- Mwanyumba
- Mavyaa
- Kivyele
- Mkwe
- Sentensi inayounganisha sentensi: "Kirui ni mzee. Kirui anatembea bila mkongojo." ni
- Kirui anatembea bila mkongojo minghairi ya yeye kuwa mzee.
- Kirui ni mzee madhali anatembea bila mkongojo
- Kirui anatembea bila mkongojo licha ya kuwa yeye ni mzee.
- Kirui ni mzee maadamu anatembea bila mkongojo.
- Chagua nomino isiyoafikiana na nyingine.
- Werevu
- Ushindi
- Amani
- Unga
- Johari hapendi kufanya kazi. Anazembea kwa kila jambo. Ni nahau gani iliyoafikiana na tabia yake?
- Kupiga zohali
- Kufanya inda
- Kujifunga kibwebwe
- Kupiga chuku
- Kauli, 'Sinyorita ni ninga' imetumia tamathali gani ya usemi?
- Nahau
- Tashbihi
- Istiara
- Kinaya
- Onyesha sentensi yenye kivumishi.
- Omondi alilima shamba juzi
- Pale pana madawati machache
- Ndege imeondoka mapema
- Watatu waliumia uwanjani
- Chagua jibu ambalo lina vihusishi pekee.
- Mno, tena, baadaye
- Kati ya, labda, ama
- Kama, kwa haraka, vizuri
- Katika, kando ya, tangu
- Chagua wingi wa: Hukujua kuwa seremala angemnunulia bata mkubwa.
- Hawakujua kuwa seremala angewanunulia mabata wakubwa.
- Hamkujua kuwa maseremala wangewanunulia mabata wakubwa
- Hamkujua kuwa maseremala wangemnunulia mabata wakubwa
- Hawakujua kuwa maseremala wangemnunulia mabata wakubwa
- Neno, Mkalimani lina silabi ngapi?
- Nne
- Sita
- Tano
- Tisa
- Maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo ni:
Babu yangu amerudi nyumbani lakini wake ataondoka kesho.- Kivumishi, kiwakilishi, kielezi
- Kimilikishi, kielezi, nomino
- Kivumishi, kielezi, kiwakilishi
- Kielezi, kivumishi, kiwakilishi
- Tegua kitendawili:
Kikigongwagongwa wanawe hutoka nje- hindi
- ngoma
- mgomba
- kichuguu
- Chagua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo.
- Je? Ulifika shuleni saa ngapi?
- Kaka alinunua; kitabu, rula na kalamu.
- Mwalimu wetu(Bi. Mona) anapenda michezo.
- lahaula unamfahamu mama yangu!
Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.
Wengi wetu tumewahi kusikia kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu. Hata hivyo, sio wote wanaoelewa hatari ya ugonjwa huu. Kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na bakteria. Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kuwadhuru watu hata kusababisha vifo katika nchi maskini. Kenya ni mojawapo ya nchi zilizo na mzigo mkubwa wa kifua kikuu kote ulimwenguni huku zaidi ya Wakenya laki moja wakiambukizwa ugonjwa huu kila mwaka.
Kifua kikuu ni ugonjwa ambukizi ambao huchukua miezi kadhaa kuutibu, usipogunduliwa na kutibiwa mapema, unaweza kusababisha madhara kadhaa mwilini kama vile kupoteza mapafu na uwezo wa kusikia. Aidha unaweza kusababisha kiharusi. Hata hivyo, ugonjwa huu una tiba. Wagonjwa wengi hupata nafuu na kupona na miili yao kuanza kufanya kazi vizuri tena baada ya mgonjwa kukamilisha matibabu.
Ugonjwa huu husambaa mgonjwa anapokohoa, kupiga chafya au anapozungumza na mtu anapopumua hewa iliyo na viini vya ugonjwa huu. Ingawa hivyo sio kila mmoja anayepumua hewa yenye viini anayepata kifua kikuu. Watu wengi walio na kinga imara ya mwili hupambana na viini vya ugonjwa huu na kuvishinda.
Watoto wachanga na watu waliozeeka ndio walio na hatari zaidi ya kupata maambukizi ya ugonjwa huu kutokana na kinga yao dhaifu ya mwili. Matibabu ya saratani na ukimwi hupunguza kinga ya mwili na kuhatarisha maisha ya wagonjwa hao ambao hunyemelewa kwa urahisi na kifua kikuu. walio tena kwenye hatari ya maambukizi ya kifua kikuu ni watu wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda iliyo na msongamano mkubwa wa watu. walio kwenye magereza, wanaofanya kazi maeneo yaliyo na maambukizi mengi ya kifua kikuu hasa wafanyakazi katika hospitali zetu na wanaoishi kwenye chumba kimoja na mgonjwa wa kifua kikuu.
Baadhi ya dalili za kifua kikuu ni pamoja na joto jingi mwilini, kupunguka kwa uzani, kutoka jasho usiku na kikohozi. Ugonjwa wa kifua kikuu una tiba. Tiba bila malipo inapatikana katika hospitali zote za umma na zahanati Tiba ya dezo pia inapatikana katika kliniki kadhaa za umma nchini. Dawa hutumiwa kwa takribani miezi sita na baadaye mgonjwa hukaguliwa na kuwekwa chini ya uangalizi wa karibu.
Kwa kweli mti hauendi ila kwa nyenzo. Hatuwezi kujipakatia mikono na afya nzuri ije kwetu. Ili kupunguza maambukizi, epuka sehemu zilizo na misongamano mikubwa ya watu, hakikisha makazi yana mzunguko mzuri wa hewa hasa palipo na msongamano; hakikisha kuwa walio na kifua kikuu wamepata matibabu.
- Kulingana na aya ya kwanza:
- Watu wote wana habari kuhusu kifua kikuu
- Baadhi ya watu wanaelewa hatari ya kifua kikuu
- Kifua kikuu ni ugonjwa unaoua watu wengi zaidi ulimwenguni.
- Kifua kikuu ni ugonjwa unaosambazwa na bakteria
- Kifua kikuu;
- hupatikana nchini Kenya pekee
- husababisha vifo vya watu laki moja kila mwaka katika nchi maskini
- ni ugonjwa usiokuwa na tiba
- ni chanzo cha kifo katika nchi nyingi maskini
- "Kifua kikuu ni ugonjwa ambukizi" inamaanisha:
- Mtu huchukua muda mrefu kupona ugonjwa huu
- Husababisha kiharusi
- Unaweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine
- Ugonjwa huu unatibika
- Chagua kundi lisilokuwa kwenye hatari ya kuambukizwa kifua kikuu kwa mujibu wa kifungu.
- Wakazi wa mitaa ya mabanda
- Wafungwa gerezani
- Madaktari wanaotibu wagonjwa wa kifua kikuu
- Wagonjwa wote wanaougua kansa
- Kifua kikuu ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia zifuatazo isipokuwa:
- Wakati mtu mwenye afya hupumua
- Kupitia kikohozi cha anayeugua kifua kikuu
- Mgonjwa wa kifua kikuu anapopiga chafya
- Mtu anapopumua hewa viini vinavyosababisha kifua kikuu
- Kulingana na kifungu, ni nani asiyeweza kuugua kifua kikuu hata baada ya kupumua hewa yenye viini vya ugonjwa huo?
- Watu wenye afya bora
- Wenye kinga ya mwili iliyo madhubuti
- Watu waliozeeka sana
- Wagonjwa wa ukimwi
- Maana ya methali, 'Mri hauendi ila kwa nyenzi imedhihirika namna gani katika kifungu?
- Wanaopata matibabu ya kifua kikuu hupona
- Watoto wachanga na wazee hukumbwana maambukizi.
- Wanaochukua tahadhari huepuka ugonjwa wa kifua kikuu.
- Wahudumu wa afya hospitalini huweza kuambukizwa kifua kikuu.
- Tiba ya dezo ni tiba gani?
- Isiyokuwa na malipo
- Ya malipo yaliyopunguzwa
- Ya lazima
- Isiyoepukika kabisa
- Kulingana na kifungu, tiba ya kifua kikuu huchukua muda gani?
- Zaidi ya miezi sita
- Miezi sita
- Mwaka mmoja
- Karibu miezi sita
- Yafuatayo ni madhara ya kifua kikuu ila:
- Keathiriwa mapafu
- Kupoteza uwezo wa kusikia
- Kupungua kwa uzani wa mwili
- Kusababisha kiharusi
Soma ufahamu huu kisha ujibu maswali 41-50.
Punda na nguruwe waliumbwa kuwa marafiki wa dhati daima. Hata hivyo, urafiki wao uliosambaratika siku moja Nguruwe alipozuru kwa rafikiye. Wasemao husema kuwa mambo ni kangaja huenda yakaja.
Ndugu hawa wawili walikuwa wazawa wa kijiji kimoja. Wazazi wao walikuwa marafiki wa kufa kuzikana jambo lililosababisha wawili hao kuishi na kukua pamoja kama ndugu wa mzazi mmoja. Kifo kilinyemelea familia hizi na kuacha wafaruku wakiyahangaikia maisha. Wote wakiwa na moto wa kiume wa kulea. Walijifunga kibwebwe kazini ili kuwakidhia wana wao mahitaji ya kimsingi.
Punda na nguruwe walikua na kuwa mabarobaro na hata kujijengea makazi yao. Hata hivyo, waliwategemea wazazi waliobaki kujipatia riziki ya kila siku. Ndugu hao wawili kila walipokutana ugani, wangemenyana miereka ili kubainisha mwenye nguvu japo walifanya hivyo kupitisha wakati. Mara nyingi nguruwe angeibuka mshindi kwa hisani ya mamaye. Jambo hili lilimkera punda ambaye alikuwa dhaifu kutokana na ukosefu wa lishe bora.
"Rafiki yangu," Punda alimwambia Nguruwe, "Nasadiki kuwa sasa tunaweza kujikidhia mahitaji yetu. yafan tuwasafirishe abera wazazi wetu maadamu wamekula chumvi nyingi. Sisi tu wapishi hodari."
Kutokana na madai kwamba walikuwa wapishi stadi, nguruwe aliyavalia maneno na ushauri wa nduguye njuga. Bila kuwazia zaidi, wawili hao walisuka mpango wa kuyatatiza maisha ya wazazi wao.
"Hili ni jambo rahisi," punda alisema, "Wanahitaji kichapo na kuwasafirisha kaburini," alishauri huku akitabasama kichinichini.
Baada ya maandalizi ya mada, wawili hao walikuwa tayari kutimiza mpango wao walivyokubaliana. Punda alitoa amri. 'Gonga' na wote wakaanza kuwachapa wazazi wao.
Nguruwe alimpondaponda mama yake hadi akamsafirisha jongomeo. Kwa upande mwingine punda aligongagonga ngoma huku akipiga mayowe na kuiga kilio cha mwanamke. Alijitoma kwenye nyumba ya nguruwe machozi yakimdondoka njia mbilimbili. "Nimemaliza" Punda alisema. Nguruwe naye akamwambia, "Wangu anapumzika kaburini.
Baada ya miezi kadhaa walikutana mahali paopa kawaida na kupiga gumzo kuhusu maisha bila wazazi. Punda alikuwa amenenepa lakini nguruwe alikuwa mkondefu kama mwiko wa pilau. Wakaelewana kupunguza ziara za kutembeleana kutokana na kazi iliyowabana. Nguruwe alikuwa amepigwa mafamba vilivyo.
Siku moja nguruwe alipokuwa kwenye pitapita zake karibu na nyumba ya punda akitafuta chakula, alishtuka kumwona mamaye punda akinywa uji huku akiota jua. Nguruwe alitaka kulia, akakata shauri kuachana na usuhuba wa punda.
- Kulingana na aya ya kwanza, urafiki kati ya punda na nguruwe unaweza kuelezwa kuwani wa:
- Kudumu
- Kujitolea
- Kusambaratika
- Unafiki
- Aya ya pili imebainisha kuwa:
- Punda na nguruwe walizaliwa na mzazi mmoja
- Punda na nguruwe walikuwa na tabia zilizofanana
- Wazazi wa kike wa punda na nguruwe walifariki kwanza
- Urafiki wa wazazi ulisababisha malezi ya pamoja ya punda na nguruwe
- Sentensi, kifo kilinyemelea familia hizi na kuacha wafaruku wakiyahangaikia maisha" imetumia tamathali gani ya usemi?
- Tashhisi
- Nahau
- Istiara
- Kinaya
- Ni jambo gani linaloonyesha kuwa wazazi wa punda na nguruwe waliwajibikia majukumu yao?
- Kuwazaa wana wao katika kijiji kimoja
- Kutimizia haja familia zao
- Kuwalea wana wao katika mazingira sawa
- Kuishi pamoja na kuwa marafiki wa kufa kuzikana
- Miereka ni
- mchezo wa kushindana na kuvuta kamba
- michezo ya kujificha na kutafutana
- michezo ya kushikana na kuvamiana kwa lengo la kuangushana
- michezo ya mazoezi ya viungo vya mwili
- Baada ya punda kushindwa na nguruwe;
- punda alilalamikia mamaye
- aligundua kuwa alikosa lishe bora
- alifurahishwa na ushindi wa nduguye
- alikasirishwa na kushindwa kwake.
- Punda alimshauri nguruwe kuwaua wazazi kutokana na sababu zifuatazo isipokuwa:
- Walikuwa na uwezo wa kujikidhia mahitaji yao
- Walishakuwa mabarobaro na hata kujijengea makazi
- Walikuwa na uzoefu wa kujipikia
- Wazazi wao walikuwa wamezecka
- Wazazi wa punda na nguruwe walipoanza kupata kichapo
- walikuwa wamefahamu mpango wa wanao
- nguruwe alimchapa mama yake hadi akafa
- hakuna mwana aliyekusudia kuua mzazi wake
- punda hakupoteza muda, aliua mama yake
- Chagua jawabu lisilokuwa sahihi; Baada ya vifo vya wazazi:
- Nguruwe alijipata na shughuli nyingi za kujitafutia riziki
- Marafiki hao wawili walisimuliana kuhusu maisha yao.
- Hatimaye siri ya punda ilifichuka
- Nguruwe alianza kumtembelea punda mara kwa mara.
- Funzo linalotokana na kisa hiki hasa ni: Yafaa
- tujiamini
- kuwasiliana kwa njia nzuri
- tufikiri kabla ya kutenda
- tuwe wabunifu
Insha
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako
Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa: Andika insha itakayomalizika kwa maneno yafuatayo:
.............................................................................................Hapo ndipo nilipogundua kuwa hatupaswi kukata tamaa maishani.
MAJIBU
Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 8
MASWALI
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila pengo umepewa majibu manne. Chagua jawabu lifaalo zaidi.
Matumizi mabaya ya mihadarati..................1..................maisha ya watu wengi...................2.................Yakini, yaani...................3.................kuna watu ..................4................kiafya huku wengine..................5................hoi, hawamjui aingiaye..................6................atokaye. Vijana wanastahili ..................7................ dhidi ya uraibu huo lau sivyo jamii..................8................warithi.
-
- yamewasababisha
- imeyasababisha
- yameyasababisha
- imewasababisha
-
- kutumbukia nyongo
- kuenda joshi
- kula mwata
- kufa moyo
-
- huenda
- labda
- yamkini
- kwa hakika
-
- waliodhoofisha
- waliodhoofika
- waliodhoofia
- waliodhoofiwa
-
- wamebaki
- wanabaki
- wangebaki
- wakibaki
-
- ila
- kama
- wala
- ilhali
-
- kuusiwa
- kuhusishwa
- kuhasiwa
- kudhulumiwa
-
- watakosa
- itakosa
- litakosa
- mtakosa
Juhudi alijitahidi kadri...................9..................ili afanikiwe masomoni...................10..................Moyoni, alijawa na shukrani kwa, ...................11.................. aliyejitolea ...................12.................. licha ya kuwa ...................13.................. Kama walivyosema wahenga...................14.................. Juhudi zake zilizaa matunda kwani alifuzu ...................15..................na shule ya kitaifa.
-
- alioweza
- alipoweza
- alivyoweza
- aliyoweza
-
- yake
- yao
- mwao
- mwake
-
- mhisani
- mwadhini
- mlanguzi
- msaliti
-
- kumdhamini masomo yake
- kuyadhamini masomo yake
- kumthamini masomo yake
- kuithamini masomo yake
-
- hawakuhusiana kwa damu wala usaha
- walibaidika kama ardhi na mbingu
- alijitia kati kama mchuzi
- alikula huu na hasara juu
-
- juhudi si pato
- upweke ni uvundo
- bahati ni chudi
- mpanda ngazi hushuka
-
- akaungana
- akaungia
- akajiunga
- akaungwa
Kutoka swali 16-30, chagua jibu sahihi kulingana na maagizo.
- Tambua maneno yaliyoangaziwa katika sentensi ifuatayo.
Aghalabu watu warefu hutembea haraka kuliko wafupi.- Kiunganishi, kivumishi, kivumishi.
- Kielezi, kiwakilishi, kivumishi.
- Kiunganishi, kiwakilishi, kiwakilishi.
- Kielezi, kivumishi, kiwakilishi.
- Andika sentensi ifuatayo katika umoja. Nyua hizo ndizo zilizopaliliwa na vibarua wale.
- Ua hilo ndilo lililopaliliwa na kibarua huyu.
- Ua huo ndio uliopaliliwa na kibarua yule.
- Nyua hiyo ndiyo iliyopaliliwa na kibarua huyu.
- Nyua hiyo ndiyo iliyopaliliwa na vibarua wale.
- Fuawe ni kwa mhunzi kama ilivyo timazi kwa
- mwashi
- sonara
- seremala
- mjumu.
- Chagua sentensi iliyo katika wakati uliopo hali isiyodhihirika.
- Mama anawalisha ng'ombe majani.
- Mwelu amefanya vizuri katika mtihani huu.
- Nawapa wenzangu nasaha kuhusu maisha.
- Balozi wetu atakuwa akitutetea huko. ugenini.
- Kati ya wadudu wafuatao yupi si kimelea?
- Pange
- Nondo
- Mbu
- Utitiri
- Chagua sentensi yenye kivumishi kisichochukua kiambishi ngeli.
- Mwembe mrefu ulikuwa shambani. mwao.
- Kiatu kile ndicho alichokushonea.
- Muziki ninaoupenda unazingatia maadili.
- Mchezaji stadi amefunga bao jingine.
- Tegua kitendawili kifuatacho. Kondoo wangu mnene huchafua njia nzima.
- Konokono
- Mvua
- Kobe
- Ndovu
- Kiambishi 'ka' kimetumiwa kuonyesha nini katika sentensi ifuatayo?
Ametumwa nyumbani akamlete mzazi wake.- Kuonyesha amri.
- Kuonyesha kusudi.
- Mfululizo wa matukio.
- Kukamilika kwa jambo.
- Chagua methali yenye maana sawa na hii.
Afadhali dooteni kama ambari kutanda.- Bura yangu sibadili na rehani.
- Usiache mbachao kwa msala upitao.
- Moja shika si kenda nenda urudi.
- Heri kujikwaa dole kuliko kujikwaa ulimi.
- Chagua maelezo yasiyoonyesha maana ya neno 'kinga'.
- Kumlinda mtu kutokana na madhara.
- Kipande cha ukuni chenye moto.
- Ubao wa chini ya mlango.
- Tayarisha mikono ili kupokea kitu.
- Kanusha sentensi ifuatayo,
Shamba lililolimwa limepandwa mahindi.- Shamba lisilolimwa halikupandwa mahindi.
- Shamba lililolimwa halijapandwa mahindi.
- Shamba ambalo halikulimwa halipandwi mahindi.
- Shamba lililolimwa halipandwi mahindi.
- Ikiwa leo ni Jumanne, mtondogoo itakuwa hini?
- Ijumaa
- Jumapili
- Jumatatu
- Jumamosi
- Kauli 'mkono wangu ulikufa ganzi' imetumia tamathali gani ya usemi?
- Nahau
- Chuku
- Tashhisi
- Kinaya
- Bainisha nomino iliyoundwa kutokana na kitenzi.
- Mcheshi-Cheka
- Kataa-Kataza
- Aminika Uaminifu
- Kicheko Mcheshi
- Badilisha sentensi ifuatayo katika hali ya udogo.
Nyumba hiyo imejengwa papa hapa mjini.- Jumba hilo limejengwa papa hapa mjini.
- Kijumba hicho kimejengwa papa hapa. jijini.
- Jumba hilo limejengwa papa hapa kijijini.
- Kijumba hicho kimejengwa papa hapa kijijini.
Soma ufahamu kwa makini kisha ujibu maswali 31-40.
Fanaka alikuwa ghulamu mcheshi aliyependwa sana na wanafunzi wengine darasani mwetu. Katika shughuli za vikundi, tulipendelea kujiunga naye kutokana na weledi wake wa masuala mbalimbali. Jingine lililotuvutia kwake ni jinsi alivyoonekana nadhifu siku yoyote, wakati wowote. Ama kweli, alikuwa kipenzi na kielelezo kwa wengi.
Siku moja, mwalimu alitupangia somo kuhusu usafi wa kibinafsi. Alituonyesha vitu vinavyohitajika kudumisha usafi wa kibinafsi mathalani sabuni, mswaki, dawa ya meno na kitana. Baadhi ya vitu vilikuwa vifaa halisi na picha za vingine. Isitoshe, alitumia projekta kuonyesha video za vijana mbalimbali wakitekeleza shughuli za usafi wa kibinafsi. Baadaye, alitupa nafasi ya kuwaelezea wenzetu jinsi tunavyoshughulikia usafi wetu wa kibinafsi. Hapo Fanaka alijitolea kulishughulikia darasa.
Alianza kwa kutujulisha jinsi wavyele wake walivyomhimiza kudumisha usafi tangu utotoni. Walielewa umuhimu wa kumkunja kambare angali mbichi. Mazoea haya yalimwepushia matatizo ya kiafya na kumwezesha kuhudhuria masomo yake bila shida.
Fanaka alisema kuwa ilikuwa ada yake kuoga kila asubuhi na jioni. Mtu anapoendelea na shughuli zake za kila siku, huenda akadondokwa na jasho, akatifuliwa vumbi au uchafu mwingine ambao huenda hata hauonekani. Joto la usiku nalo humfanya aliyelala kulowa jasho rovurovu hususan ikiwa anatumia mablanketi mazito. Uchafu huu hauna budi kuondolewa kwa kuoga lau sivyo mtu atanuka gugumo asubuhi na jioni.
Tuliendelea kumtegea Fanaka masikio yetu ndi. Alitueleza kwamba alikuwa na mazoea ya kupiga mswaki kuondoa mabaki ya vyakula ambayo yanaweza kufanya meno kuoza. Hapo tulielewa kiini cha meno ya Fanaka kuwa meupe mithili ya tui la kasimile.
Jingine alilotukumbusha Fanaka ni kujiepusha na uraibu wa pombe na uvutaji sigara. Hata mtu akioga namna gani, uvundo wa dawa hizi za kulevya huwaghasi wale walio karibu naye. Ni vyema mja ajitanibu kabisa na dawa hizi. Nilipoyasikia hayo nilijikumbusha kimoyomoyo kuwa uraibu wa mihadarati huathiri utendakazi wa mwanafunzi kiasi cha kukosa makini katika shughuli za kielimu miongoni mwa nyingine.
Kabla ya kuketi, Fanaka alitukumbusha tusipuuze mambo yanayoonekana madogomadogo kama vile kuzifua lebasi zetu, kunyolewa au kusukwa ikiwa ni wasichana, kunawa mikono na kuangua kucha. Mtu akizingatia hayo na mengine kisha aishi katika mazingira safi, ataonekana mwenye bashasha wakati wote.
Tulimpigia Fanaka makofi kwa ushauri wake. Yamkini, kila mmoja wetu alikuwa akijiahidi kimoyomoyo kumwiga Fanaka katika yale aliyotueleza. Alipojiunga nami pale nilipoketi, nilijua kuwa yote aliyoyasema yalikuwa ukweli mtupu. Nilijivunia uhusiano wetu wa karibu kwani nilikuwa nimeathiriwa vyema.
- Kulingana na aya ya kwanza
- Fanaka alipendelea ucheshi wa vikundi darasani
- Fanaka alivutiwa zaidi na kikundi cha mwandishi
- Fanaka alikuwa kijana mwenye kichwa chepesi
- Fanaka alipendwa na mwalimu kuliko wenzake.
- Kulingana na ufahamu, mwalimu
- aliwaonyesha wanafunzi jinsi ya kutekeleza usafi wa kibinafsi
- alitumia mbinu mbalimbali kufanikisha masomo darasani
- ndiye aliyefunza kila kitu kuhusu usafi wa kibinafsi
- alimpa msimulizi nafasi ya kuwaeleza wenzake kuhusu usafi wa kibinafsi.
- Nimethali gani inayofaa zaidi kueleza ujumbe katika aya ya tatu?
- Mtoto akibebwa hutazama kisogo cha nina.
- Mwana mui ni dawa ya mlango.
- Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
- Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
- Eleza manufaa ya usafi kulingana na kifungu
- Kudumisha afya na kufanikisha utendakazi nyumbani.
- Kuepuka vimelea na uchafu wa mavazi.
- Kuvuta urafiki na kuondoa mabaki ya vyakula.
- Kutunza siha na kuondoa uvundo.
- Mtu anapaswa kuoga kila usubuhi. Ni uchafu upi unaoondolewa kwa kufanya hivyo?
- Jasho, matongo
- Vumbi, jasho
- Matongo, vumbi
- Nta, vumbi.
- Kauli meupe mithili ya tui la kasimile' imetumia tamathali gani ya usemi?
- Sitiari
- Chuku
- Kinaya
- Tashbihi.
- Fanaka hakuwaambia wenzake kuwa
- mtu anapaswa kuoga angaa mara mbili kwa siku
- wanaotumia dawa za kulevya hutoa uvundo unaokirihi
- mtu asipopiga mswaki meno yake huoza
- matumizi ya mihadarati huvuruga utendaji wa wanafunzi.
- Usafi wa kibinafsi si pamoja na
- kunyoa nywele
- kukata kucha
- kupiga deki
- kufua nguo.
- Kulingana na aya ya mwisho
- Fanaka aliwaathiri vyema wenzake darasani
- wanafunzi walimwahidi Fanaka kufuata ushauri wake
- ilikuwa mara ya kwanza kwa mwandishi na Fanaka kukaa pamoja
- wengine waliyatilia shaka maneno ya Fanaka.
- Neno lebasi lina maana sawa na
- malazi
- mavazi
- mapambo
- mazingira.
Soma kifungukifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia 41 hadi 50.
Matumizi ya mitandao ya kijamii yamefikia upeo wa juu katika miaka ya hivi karibuni. Si ajabu kuwaona waja wanaotumia simu zao, tabuleti au vipakatalishi katika magari ya uchukuzi wa umma, ofisini, nyumbani na katika bustani mbalimbali. Utawapata watu wenyewe wakionyesha hisia mbalimbali kwa kutegemea picha, jumbe au video wanazotazama kwenye mitandao hiyo.
Watu wengi hutumia mitandao hii kujiburudisha. Wao hutazama video zinazohusiana na nyimbo, michezo, mitindo ya mavazi na ya nywelle. Aghalabu utawaona wakibadilisha mitindo yao kuambatana na vigezo wanavyovipata mitandaoni. Video hizi zinapopata idadi kubwa ya watazamaji, wanaozipakia huanza kujipatia kipato. Kuna watu walioimarika sana kiuchumi
kutokana na video kama hizi.
Mumo humo mitandaoni huwa soko la huduma na bidhaa mbalimbali. Wawekezaji hutumia njia hii kunadi biashara zao hivyo basi kujiongezea idadi ya wateja. Gharama ya utangazaji huu ni nafuu ikilinganishwa na matangazo mbadala kama vile ya redio, runinga, magezeti na maonyesho. Mteja naye hurahisishiwa kazi ya kusaka bidhaa kwani analinganisha maelezo na bei za bidhaa mbalimbali pasipo kusumbuka sana. Akifikia uamuzi wa kununua bidhaa au huduma fulani, atawasiliana naye kwa simu au mitandao iyo hiyo, kisha hupelekewa bidhaa popote alipo kwa ada nafuu.
Watu wengi hasa vijana huwa na marafiki wengi katika mitandao ya kijamii. Urafiki huu unaweza kumfaa mtu kiuchumi, kisaikolojia na kisosholojia. Wengine wamewahi hata kupata wachumba na wenzi wao katika ndoa kupitia mitandao hii.
Elimu ni bahari. Kupitia mitandao ya kijamii, tunaweza kupata maarifa ya kielimu, kidini, uwekezaji, utamaduni na mengine mengi. Wanaotumia maarifa haya kwa njia ifaayo huongeza thamani katika maisha yao. Wao hufanya hivi kwa kuanzisha biashara zao, kazi za kiufundi, vilabu vya mazoezi, upishi na uokaji wa keki. Almradi, kila mmoja hufaidika kivyake na maarifa ya mtandaoni.
Chambilecho wahenga, hakuna bamvua lisilokuwa na usubi. Kuna watu waliowahi kuhasirika kutokana na mitandao hii. Uhalifu wa mitandaoni umekuwa tatizo sugu hivi kwamba serikali imeapa kulivalia njuga. Wapo waja wanaotumia mitandao hii kuwatishia wengine wawape kiwango kikubwa cha fedha lau sivyo wafichue siri zao au kuweka picha zao za kuaibisha. Ajabu ni kuwa wanaofanya hivyo aghalabu waliwahi kuwa marafiki wa wahasiriwa. Matukio ya aina hii yamewahi kuwaletea wengi mzongo wa mawazo huku baadhi yao wakijitia kitanzi.
Utapeli ni uhalifu mwingine unaotekelezwa mitandaoni. Wapo wanaojifanya kuuza huduma au bidhaa ambazo hazipo. Nyingine nazo hupambwa kwa picha nzuri nzuri wateja wakaziagiza kwa wingi pasipo kujua kwamba hazifikii viwango. Waliofikia viwango vya juu vya uhalifu huu hudukua akaunti za wengine na kuzitumia kuwalaghai marafiki zao ili wawatumie pesa.
Mitandao hii ikitumika vizuri, italeta manufaa kochokocho. Wanajamii hawana budi kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuwafichua wanaotumia mitandao ya kijamii kueneza porojo, kufaidi jasho la wengine au kuvuruga mahusiano ya kijamii. Serikali pekee haiwezi kufanikiwa kukomesha uhalifu huu maadamu kofi hazilii ila kwa viganja viwili.
- Chagua maelezo yaliyo sahihi.
- Mitandao ya kijamii huwaathiri watumiaji kwa njia zinazohitilafiana.
- Uchukuzi wa magari ya umma umeifanya mitandao ya kijamii kupata umaarufu.
- Mitandao ya kijamii hutumiwa na vijana peke yao.
- Hisia mbalimbali huwatambulisha wanaotumia mitandao ya kijamii.
- Aya ya pili inaonyesha kuwa
- watu hubadilishiwa mitindo yao ya mavazi mitandaoni
- watu wengi walianza kujipamba walipojiunga na mitandao
- mazoea ya mtu huathiriwa na yale anayoshuhudia mitandaoni
- mitindo bora zaidi ya nywele ni ile ishuhudiwayo mtandaoni.
- Ni kweli kusema kuwa
- wanaotazama video nyingi mitandaoni hupokea malipo
- mitandao ya kijamii inaweza kumwimarisha mtu kiuchumi
- bidhaa hununuliwa na kusafirishwa mumo humo mitandaoni
- wafanyabiashara wengi wana maduka yao mitandaoni.
- Jambo lipi ni sahihi kuhusu matangazo mitandaoni?
- Bei yake ni rafi.
- Bei yake ni ya kuruka.
- Bidhaa huwa bora zaidi.
- Mengine yametiwa chumvi.
- Manufaa ya urafiki kulingana na kifungu hiki ni
- kumpunguzia mtu matatizo ya kiakili
- kumwezesha kuepuka hila za matapeli
- kupata umaarufu kitaifa na kimataifa
- kupata video mbalimbali mitandaoni.
- Wanaoanzisha miradi ya kujifaidi kutokana na mitandao ni wale
- wanaotumia mitandao kujiburudisha
- wanaotumia mitandao kwa wingi zaidi
- wanaotumia mitandao kutafuta maarifa
- wanaopitisha maarifa kwa wenzao mitandaoni.
- Kauli 'kulivalia njuga' ina maana gani?
- Kulivalia viatu.
- Kulishughulikia sawasawa.
- Kulipuuza kwa vyovyote.
- Kuliwazia kwa kina.
- Ili kukomesha uhalifu wa mitandaoni, mwandishi anahimiza kuwa na
- uaminifu
- uvumilivu
- utangamano
- ushirikiano.
- "Wanaofanya hivyo aghalabu waliwahi kuwa marafiki wa wahasiriwa." Kauli hii inaonyesha kuwa
- mtu hughulumiwa zaidi na mahasimu wake
- wale tuliowaamini wanaweza kusaliti uhusiano wetu
- hatufai kumwamini mtu yeyote maishani
- mtu akikufanyia mabaya mlipe kwa ubaya uo huo.
- Maana ya neno 'kunadi' ni
- kusifu
- kuuza
- kutangaza
- kuonyesha.
MAJIBU
Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 7
MASWALI
Vihosho vifuatavyo vina nafasi 1-15. Vikamilishe ukitumia kiteuzi mwafaka.
Kuna sauti kadhaa za Kiswahili. Sauti za Kiswahili...................1......................na...................2......................zinazopatikana katika ...................3...................... yenyewe. Konsonanti moja ikiambatanishwa na ...................4...................... moja huunda silabi ...................5...................... Wakati ...................6...................... silabi zinaunganishwa, zinaunda neno. Mwanafunzi ..................7...................... kuhusu utaratibu huu ni ..................8......................anoe swali kuhusu mada inayorejelewa.
-
- zinatokana
- zinatoka
- zikitoka
- inatokana
-
- mizani
- silabi
- mapigo
- herufi
-
- akrabu
- abjadi
- akraba
- abadi
-
- neno
- sauti
- vokali
- tamko
-
- sahili
- mwambatano
- changamano
- soghuna
-
- ambalo
- ambapo
- ambayo
- ambao
-
- akieleweka
- aliyeeleweshwa
- alielewa
- anayejielewa
-
- mgumu
- ngumu
- sharti
- vigumu
Mwalimu alipotuomba ..................9.....................katika makundi..................10......................nilitatizika sana. Alisema kuwa alitaka ..................11......................au kuimba shairi la majibizano..................12......................kama ..................13...................... Nilitatizika mawazoni ..................14...................... sijawahi kuwa na ujasiri wa kusimama kadamnasi ..................15......................watu.
-
- tugawanwe
- tujigawe
- tugawanyishwe
- tutengane
-
- viwili
- mbili
- mawili
- ya pili.
-
- tukariri
- tughani
- tusome
- tujifunze
-
- inayojulikana
- Unayojulikana
- inaojulikana
- linalojulikana
-
- ngonjera
- tarbia
- utenzi
- thuluthi
-
- ilhali
- wala
- maadamu
- yaani
-
- kwa.
- ya
- mwa
- la
Kuanzia swali la 16 hadi 30, jibu kulingana na maagizo
- "Mlango ulinikodolea macho." Eleza tamathali ya lugha iliyotumika katika kauli hii.
- Utohozi
- Tashihisi
- Kinaya
- Chuku
- Kaka ni, ganda tupu la yai au konokono.
Kaka pia ni;- ndugu yangu wa kiume
- sehemu ya juu ya mdomo huko ndani
- kifaa cha kutobolea mashimo kwenye mbao au chuma
- mbwa asiyekuwa na mahali maalumu pa kuishi
- Jiriwa ni kwa seremala kama vile chungu ni kwa:-
- mfinyanzi
- sonara
- mnajimu
- mkalimani
- Ni ipi kati ya sentensi zifuatazo imeakifishwa vizuri?
- Unajua kusoma vizuri!
- Unajua kusoma vizuri.
- Unajua kusoma, vizuri.
- Unajua kusoma vizuri
- Ukizidisha nusu kwa thuluthi utapata nini.
- Sudusi
- Ushuri
- Humusi
- Tusui
- Chagua malipo yenye maelezo sahi
- Malipo ya kuoa ni fola.
- Malipo ya kuingia kweny, sherehe ni mahari.
- Malipo ya kuokota itu kilichopotea ni kosi.
- Malipo ya kiyesha shukrani ni duhuli.
- Baba yangu atamwitaje dada wa mama yangu?
- Mlamu
- Shemeji
- Mwanyumba
- Mkwemwana
- Chagua sentensi iliyotumia kiingizi kwa usahihi.
- Shime! Wamefiwa na nyanya yao wampendaye mno!
- Simile! Ama nitakuangukia na mzigo!
- Maskini! Amezoa alama sheshe mtihanini!
- Naam! Hatimaye anaugua kifuakikuu!
- Ni kauli gani inaonyesha kwamba mtu hachagui?
- Naomba tunda jingine tamu nilile
- Maisha yenyewe yamekuwa magumu siyamudu
- Kitabu chochote cha hadithi kikisomwa kitafaidi
- Moyo wake wote ulijaa baridi ukahaki harafu
- Chagua jozi ambayo haina visawe
- Asali uki
- Kilimo zaraa
- Barabara taliki
- Wasiwasi wahaka
- Kanusha kauli hii. Mama aliyejifungulia barasteni amelazwa katika hospitali ya rufaa.
- Mama aliyejifungulia barasteni hatalazwa katika hospitali ya rufaa
- Mama asiyejifungulia barasteni hatalazwa katika hospitali ya rufaa
- Mama aliyejifungulia barasteni hakulazwa katika hospitali ya rufaa
- Mama asiyejifungulia barasteni hakulazwa katika hospitali ya rufaa
- Chagua sentensi ambayo inaonyesha majuto.
- Mama alikuja akala akatazama taarifa akaingia chumbani.
- Wasichana hawajamudu kusukwa maana hawana pesa
- Ukiinama ovyooovyo utauumiza mgongo wako tena
- Lucia angalijiandikisha angaliibuka mshindi
- Onyesha mahali ambapo kiambishi 'wa' kimetumika kuonyesha kutendewa.
- Wamefua nguo
- Wamefuliana nguo
- Wamefuliwa nguo
- Wamewafulia nguo
- Chagua Kiunganishi ambacho kimetumika kwa usahihi katika sentensi.
- Wasichana wala wavulana wamekula matunda
- Walimu ila wanafunzi wamechelewa
- Walimu na wanafunzi wameenda ziarani
- Wanafunzi isipokuwa walimu wanakula wali.
- Andika katika hali ya wingi. Mtume ametumwa dukani kununua yai.
- Mime wametumwa dukani kunum mayai.
- Watume wametumwa madukani kununua mays
- Watume wametun, wa dukani kununua mayai.
- Mitume wametumwa madukani kununua mayai.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 31-40,
Mwanafunzi asiyeelewa kile ambacho mwalimu anafunza darasani hupatwa na mzongo sana. Saa nyingine huhisi kukata tamaa asiendelee kujishughulisha na somo hilo tena. Hata akianguka hajali tena. Mwalimu naye asipomwelewa amvumilie na kumfunza mwanafunzi huyo taratibu, kwa kweli mtoto huyo atapotea kabisa. Pengine hata atakamilisha masomo ya shule ya msingi bila kujua utaratibu wa ngeli. Ina maana kwamba akipata maswali kuhusiana na sehemu asiyoielewa ataanguka mtihani huo.
Lakini kwa nini mwanafunzi asielewe mwalimu anapofunza? Sababu ni kochokocho kama mchanga ufuoni pa bahari. Pengine kuna matatizo ya kinyumbani ambayo humjia mawazoni mwalimu anapofunza. Labda wazazi wanazozana, kuna mtu mgonjwa, kufiwa na mpendwa au pengine mmoja wa wazazi ni mlevi aletaye vurugu nyumbani kila siku. Sababu nyingine ni njia ya walimu kufundisha. Walimu wengine hufunza vibayavihaya hata mwanafunzi haelewi lolote. Walimu wanaopenda kuwachekesha tu wanafunzi darasani, ama wana athari ya lugiiamama ama wanazembea tu darasani, hawawezi kuwafaa wanafunzi.
Kuna wanafunzi ambao hali haiwaruhusu kupata vitabu vya kiada na madaftari ya kufanya ziada zao. Wanategemea wenzao wenye vitabu ambao saa nyingine huwanyima. Mwanafunzi kama huyu hataweza kujisomea zaidi katika muda wake wa ziada. Kama mwalimu hakumpa nakala za kurejelea, atadurusa vipi? Vilevile kuna wanafunzi ambao hawakujaliwa na akili nyepesi ya kuyaelewa mamb, haraka. Hata kama mwalimu atarudia masa mia na moja, bado hawataambua chochote! Walimu wasiotumia vifaa halisi kufundisha pia hutati kuelewa kwa wanafunzi. Mara nyingi wakiona unachozungumzia na kukigusa, kusahau kutakuwa vigumu.
Pia kuna wanafunzi walio na mtazamo hasi kuhusu somo fulani. Utawasikia wakisema, "sisi kwetu hatupiti Hisabati, au Kiswahili." Nami nauliza, kuna watu ambao wameandikiwa kuwa hawawezi kulipita somo fulani kwa sababu fulani? Ninaamini kwamba yeyote akijitolea, anaweza kufaulu katika chochote akifanyacho.
- Kwa kawaida, ikiwa mwanafunzi haelewi kile ambacho anafunzwa:-
- anamchukia mwalimu anayemfunza
- anaenda kutafuta ushauri kwa mwalimu
- anatatizika kimawazo na kukosa utulivu
- anahofia kuchukiwa na mwalimu wake
- Ikiwa mwanafunzi anashindwa kuelewa kile ambacho amefunzwa, mwalimu:-
- anafaa kubadilisha vitabu anavyovitumia
- anafaa kumvumila na kumfunza tena polepole
- anafaa kumwadhibu ili aelewe
- kumkalisha karibu na ubao na kumpa kazi nyingi ya ziada
- Ni yapi si matatizo ya kinyumbani?
- Kuugua kwa mtu wa jamaa.
- Baadhi ya wazazi kutumia mihadarati.
- Migogoro baina ya wazazi
- Akili inayochukua muda kuelewa mambo
- Ni kweli kwamba mwanafunzi ataambulia alama mbaya iwapo mwalimu:-
- hafanyi uzembe darasani
- hatumii muda wa masomo kuwaburudisha wanafunzi
- anaepuka athari za lughamama
- hatajibidiisha katika kuyatekeleza majukumu yake ipasavyo
- Badala ya kutamka 'sasa' mtu akitamka 'thatha' husemwa kwamba ana;
- kigugumizi
- kithembe
- ububu
- zusitasita
- Kukataa kumwazima mwenzako kitabu anapokuomba
- tukatika kutunza bidhaa zako zisipotee
- ni dalili ya uchoyo na ubinafsi
- humtia moyo kujikaza na kidogo alicho nacho
- kunawafanya wazazi wake wamnunulie vitabu vingine
- Ni kweli kwa mujibu wa habari kwamba:-
- mwanafunzi anafaa kujitengenezea nakala baada ya kufunzwa
- mwanafunzi hahitaji vitabu au nakala ili kufaulu masomoni
- mwanafunzi akiwa na nakala, zinaweza kumfaa kudurusu akapita mtihani wake
- kama mwalimu amefunza, si lazima awape wanafunzi nakala
- Mwalimu anapendekezewa kutumia nyenzo kufunza ili;
- asisumbuke kuandikia wanafunzi nakala
- kurahisisha kuelewa na kutosahau kwa wanafunzi
- kuweza kufundisha haraka bila shida
- watoto wasiokuwa na vitabu vya ziada na kiada wafaidike
- Mtazamo hasi ni kinyume cha mtazamo
- chanya
- tasa
- shufwa
- witiri
- "Ninaamini kwamba yeyote akijitolea, anaweza kufaulu katika chochote akifanyacho." Kauli hii inaunga mkono usemi kwamba:-
- penye nia pana njia.
- mchagua jembe si mkulima.
- lisemwalo lipo njiani laja.
- asiyejali hupata hatari.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50
Je umewahi kujiuliza, ama unajua mwandani ni nani? Mwandani ni mtu wa ndani, rafiki ambaye pia huitwa msena au msiri. Ni mtu wa kuambia mambo ya siri au pengine mambo ya ndani ambayo hayafai kuambiwa mtu mwingine hivihivi. Ni mtu ambaye kwa muda umemkagua na kumjua kuwa mtu wa kuaminika. Kufikia kumfungulia mambo yako ya ndani ina maana kwamba umemsoma kama msahafu na kuwa na Imani kuwa hutakuwa umekosea kuchukua funguo za moyo wako ukamwekea wazi mambo ya ndani kabisa.
Hata hivyo siku hizi dunia i...ebadilika kabisa! Imebadilika kama hali ya anga ilivyobadilika, kiangazi kikageuka kipupwe au pengine masika yakageuka vuli! Ni vigumu kumpata mtu wa kumwamini hasa ikizingatiwa ile methali ya wahenga kwamba hapana siri ya watu wawili. Ukitaka iwe siri, basi heri uizike katika moyo wako na kuifunikia hadi kifo. Marafiki wa siku hizi ni kama wanawashwa na midomo, ukiwaambia jambo, mara tu watokapo kadamnasi yako, wanamtafuta mtu wa kumpasha habari motomoto.
Habari hizo sharti wanazitia chumvi ili ziwe tamu masikioni mwa yule anayepokezwa! Sasa chukulia kwa mfano umemweleza rafiki yako kuhusu migogoro inayoendelea katika familia yako. Pengine wazazi wako wanazozana au pengine mmoja katika familia yenu anaugua ugonjwa wa UKIMWI. Ama pengine mmefungiwa nyumba kwa sababu ya kukawia kulipa pango. Halafu keshoye ukifika shuleni unashangaa kuona waangaliwa na kuchekwa kisirisiri. Ukichunguza unapata kwamba tayari siri yako imetembea kama moto kwenye kichaka kikavu, Je hilo litakuchoma maini kiasi gani?
Wosia wangu kwa marafiki ni kwamba, wanafaa kuwa wa ukweli, ama waache kabisa kujiita marafiki ilhali mioyo yao imejaa uadui. Kumbuka kuujenga urafiki huchukua muda mrefu lakini kuuvunja ni kazi ya chini ya sekunde tano. Nani angependa kuchukua muda kujenga uhusiano ambao hautadumu? Hata watu wakikusikia kuwa u mtu wa sampuli hiyo, unafikiri yupo ambaye angependa kuhusiana na wewe? Hakutakuwa na haja ya wewe kuhesabiwa kama rafiki maana utakuwa hufai lolote la haja. Akufaaye kwa dhiki ndiye awezaye tu kuitwa rafiki.
- Kabla ya kumchagua rafiki:-
- unakuwa umesifiwa na wengine kumhusu
- unakuwa umesikia kuhusu wema wake
- unakuwa umemchunguza na kumkagua
- anakuwa amejipendekeza sana kwako
- Kwa kawaida rafiki:-
- huambiwa mambo wanayoambiwa wenzake
- haambiwi mambo wanayoambiwa wenzake
- hana tofauti na watu wengine wa kawaida
- hufunuliwa mambo waliyofichwa wengine
- Neno msahafu kama lilivyotumika katika ufahamu liria maana ya:-
- gazeti lililoandikiwa watu kusoma
- daftari lenye maneno mengi ya kusomwa
- kitabu kitakatifu
- kitabu kinachopendwa na wengi
- Ni msimu gani uliolinganishwa sawa na maelezo yake?
- Vuli - Majira ya joto jingi
- Kiangazi - Wakati wa matope mengi
- Kipupwe - Msimu wa baridi kali
- Masika - Msimu wa rasharasha za mvua
- Ukilinganisha siku hizi na za zamani, ni wazi kwamba:-
- hapo zamani ilikuwa vigumu kupata mtu wa kukutunzia siri.
- watu wengi siku hizi wamejifunza kuwa wasiri kama usiku.
- si rahisi kupata mtu wa kumwamini na mambo yako siku hizi.
- watu wa zamani walitangaza sana mambo ya wenzao.
- Rafiki anapotoboa siri yako kwa wengine:-
- hakosi kuiongeza utamu kwa maneno yasiyokuwa kweli
- humwambia huyo anayeambiwa aitunze siri hiyo
- huwa lengo lake ni kukuaibisha usiwahi kumpa siri nyingine
- anapata sifa na marafiki wapya
- Mara nyingi siri zinazoambiwa wengine
- hazihusiani na vurugu katika jamaa
- hazihusiani na mafanikio au ushindi nyumbani
- si kuhusu maradhi ya aibu
- hazina lolote la kweli bali uongo mtupu tu
- Je, ni nini maana ya UKIMWI?
- Upungufu wa Kinga Mwilini
- Ukondefu wa Kinga Mwilini
- Usafi wa Kinga Mwilini
- Ukosefu wa Kinga Mwilini
- Mtu hujuaje kwamba siri yake. imewafikia wengine?
- Rafiki mwenyewe anaenda kujishtaki
- Wanaoambiwa wanakuja kumwambia
- Jinsi wanavyomwangalia wakimwona
- Anakisia tu bila kuwa na hakika
- Kauli ya mwandishi anapomalizia makala katika aya ya mwisho ni kwamba:-
- ni kazi ngumu kuuanza urafiki lakini kuuharibu hakuhitaji muda
- kujenga urafiki ni rahisi kuliko kuuvunja
- kuuanza na kuumaliza urafiki si kazi rahisi
- unapotangaza siri za wengine unajisaidia ili usiletewe umbeya Zaidi
INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika Insha yako.
Endeleza isha ifuatayo:-
Baada ya kufunga shule Novemba mwaka jana, nilienda mashambani kumtembelea nyanya yangu. Nilipofika huko......................................
MAJIBU
Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 6
MASWALI
Soma vifungu situatavyo. Vina nafasi I mpaka 15. Kva kila pengo umepeva majibu manne. Chagus jibu lifaalo zaidi.
Waba ni ......................1......................Maradhi haya huwaambukia hususan waja ambao......................2.....................usafi wa vyakulana maji katika ulaji wao. Ulaji wa vyakula vilivyopikwa vizuri na unywaji wa maji .......................3.................... ....................4.......................mara kwa mara lakini wengi wanaonekana ....................5....................... dhidi ya wazo hili. Mapuuza haya yamesababisha hasara kubwa. .........................6.................. kutapika na kuendesha sana ni hatari zaidi kwa maisha ya mwanadamu .......................7.................... Watu wasipochukua tahadhari hususan dhidi ya unywaji wa maji machafu ukongo huu.......................8.................... ya adinasi wengi.
-
- ugonjwa wa kuambukiza wa kuhara na kutapika sana
- ugonjwa wa kuambukiza kutokana na maji maji yanayomtoka mtu
- ugonjwa unaosababishwa na kuumwa na mbu wa kike
- ugonjwa wa kuambukiza unaomfanya mtu kukohoa na kutema damu
-
- wanatumia
- hawachachawizwi
- wanazingatia
- hawazingatii
-
- masafi
- machafu
- safi
- chafu
-
- kumekuwa kukisisitizwa
- umekuwa ukisisitizwa
- yamekuwa yakisisitizwa
- imekuwa ikisisitizwa
-
- kutiatia na kutoatoa
- kuvalia njuga
- kukata shauri
- kutia nta masikioni
-
- Hapa
- Hio
- Kule
- Hiyo
-
- yeyote
- wowote
- yoyote
- chochote
-
- yanawadhuru
- utawadhuru
- inawadhuru
- yatawadhuru
Mali yaliyokuwa .................9................ na bwana Bwale yalimfanya mwanawe ...............10.................. na kukataa kuendelea kusoma. Kijana huyu, kwa kulelewa katika ukwasi mkubwa, majivuno .................11................ Aliwadharau waadhiri na wale wa rika lake. Heshima kwake ilikuwa ................12................. Tabia hizi zilisababisha wana wa hirimu yake ................13................. kama mwasiriwa wa ukoma. Kwa kuwa hakuwa na manufaa yoyote .................14................Aligeuka na kuwa mkia wa mbuzi. Wazazi wake walijaribu kuficha ................15................. cha mwana wao bila kujua kuwa tunda likioza ni sharti linuke fee!
-
- yamepeana
- yametwaliwa
- yamekabidhiwa
- yamehodhiwa
-
- kuvimba kichwa
- kuasi ukapera
- kuuma uzi barabara
- kujikaza kisabuni
-
- yalimvaa kama liliwala
- yalimvaa kama kiko na digali
- yalimvaa na kinu bila mchi
- yalimvaa kama shetani
-
- mwiku
- mwiko
- desturi
- kawaida
-
- walimpendelea
- walimwambaa
- walimpenda
- walimkataa
-
- kwenu.
- kwetu
- kwake
- kwao
-
- mwendo
- kitiba
- mwenendo
- tabia
Kutoka swali la 16 hadi la 30. chagua jibu sahihi.
- Mbwa yule akikuona atabweka kishujaa.
'ki' katika sentensi imetumiwa kuonyesha ................................. na ............................... mtawalia.- masharti, nomino
- wakati, nomino
- masharti, namna
- wakati, namna
- Ni kundi lipi lenye sauti ghuna pekee?
- b, m, dh
- v, b, r
- gh, th, b
- sh, l, r
- Sentensi zifuatazo zinaweza kuunganishwa vipi kisahihi?
Masden ni mzungu.
Masden anazungumza Kiswahili sanifu.- Masden ni mzungu maadamu anazungumza Kiswahili sanifu.
- Masden anazungumza Kiswahili sanifu licha ya kuwa yeye ni mzungu
- Masden ni mzungu madhali anazungumza Kiswahili sanifu.
- Masden anazungumza Kiswahili sanifu mighairi ya yeye ni mzungu.
- Chagua sentensi yenye kiwakilishi kimilikishi.
- Mtoto wako alichelewa ilhali wangu alifika mapema.
- Shamba lao lililimwa vizuri lakini hili halikulimwa kabisa.
- Mwanafunzi wa kwanza alituzwa lakini wengine waliahidiwa.
- Rais wa kwanza aliupigania uhuru lakini huyu aliinua uchumi.
- Riba ni
- faida anayopata mtu aliyekopesha watu fedha ambayo ni ziada ya fedha aliyokopesha
- sehemu ya bei ya kitu inayotolewa mwanzoni.
- sehemu ya fidia anayolipwa mtu mwanzoni.
- sehemu ya malipo ya kukopea kitu mwanzoni.
- Chagua sentensi iliyo sahihi kisarufi
- Kibaka hicho ndicho kilichowatisha watu.
- Mabata wadogo waliyachezea maji.
- Kipepeo chochote chenye rangi hufurahisha.
- Shingo la Mwakideu linauma.
- Sehemu ya chini ya mguu kati ya vyanda na kisigino ni
- kisugudi
- utosi
- shavu
- wayo
- Tambua tashbihi inayofaa kukamilisha.
Mwajuma ni msiri kama...- giza
- mwizi
- kaburi
- kinyonga
- Akifisha ipasavyo
Mwalimu aliwauliza kwa nini hamkukamilisha kazi kwa wakati.- Mwalimu aliwauliza, "Kwanini hamkukamilisha kazi kwa wakati?"
- Mwalimu aliwauliza, "Kwanini hamkukamilisha kazi kwa wakati."
- Mwalimu aliwauliza "Kwanini hamkukamilisha kazi kwa wakati?"
- Mwalimu aliwauliza "kwa nini hamkukamilisha kazi kwa wakati."
- Ni nini kinyume cha sentensi ifuatayo? "Jua lilipozama msichana alianua nguo."
- Jua lilipopanda kijana alianika nguo.
- Jua lilipochomoza mvulana alianika nguo.
- Jua lilipozama kijana alianika nguo.
- Jua lilipochomoza msichana alianika nguo.
- Kitenzi 'lia' katika kauli ya kutendesha ni
- lilisha
- liliza
- lilishana
- liza
- Toti alikuwa akielekea upande wa kaskazini magharibi wakati wa asubuhi. Je, kivuli chake kilielekea upande gani?
- Kusini mashariki
- Magharibi
- Mashariki
- Kusini magharibi
- Ni sentensi gani kati ya zifuatazo imetumia kihisishi kifaacho?
- Poleni jamani! nyote mmekuwa washindi
- Aha! wewe usinikere hivyo
- Alhamdulilahi! Mterehemezi awajalie mema
- Acha! Umetuzwa tuzo bora zaidi
- Mtu anayezitoa siri za nchi yake kwa nchi adui ni
- mkimbizi
- msaliti
- mlowezi
- mtoro
- Jibu maagano yafuatayo.
"Buriani!"- Buriani dawa
- Alamsiki
- Nawe pia
- Binuru
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40
Katika jiji la Tuleraha palikuwa na asilimia kubwa ya watu ikilinganishwa na maeneo mengine katika nchi ya Wakonga. Hapakuwa na mila wala desturi katika jiji lile. Wakonga walikuwa wametangamana kutoka maeneo yote ambapo palikuwa na zaidi ya makabila arubaini na mawili. Kila mmoja alitengana na mila zake punde tu alipogura mashinani. Watu wa Tuleraha waliiga mila za wazungu na wakawafuata wazungu namna bendera ifuatavyo upepo. Mitandao ya kijamii ndiyo iliyokuwa walimu wa vijana wengi pale. Chochote ambacho mzungu alifanya kilikuwa kinaonekana sawa. Mavazi yao ya Kiafrika waliyatupilia mbali, sisemi vyakula na ustaarabu wao. Wale wazee wachache waliojaribu kukuza utamaduni walionekana kuwa na kubaki nyuma kimaendeleo.
Kwa sababu ya kuiga zaidi mambo ya magharibi, jiji hili lilikuwa maarufu sana kwa anasa. Watu wa pale walijulikana kwa kupenda raha kupindukia. Ingawa walikuwa wachapa kazi, sehemu kubwa ya pato lao liliishia kwenye maeneo ya burudani kama vile katika mabaa na madanguro. Wengi wa watu hawa walikuwa wasomi wa ajabu. Palikuwa na taaluma kibao jijini kama ville: waandisi, madaktari, wanasheria, walimu na wengine. Mtu atadhani kuwa kule kusoma kungewapatia ustaarabu kumbe ndio waliopotoka zaidi kuliko mazuzu waliozitazama tu shule kwa mbali. Shahada, shahada za uzamili, shahada za uzamifu na uprofesa wao ungetumiwa bora zaidi kama maadili yale yangezin gatiwa.
Katika mazingira yale, vileo na dawa nyingine za kulevya ndizo zilikuwa starehe kamili. Palitokea binti mmoja aliyekuwa na aina mpya ya kileo alichouza kisirisiri. Kiliwavutia sana wanaume kwani kila wakati walitaka kumwona pembeni ili wafaidi kileo hicho cha faragha na kipya. Waliokionja waliishia kuwapelekea wake zao ambao walikifurahia bila kujua kilikuwa haramu. Vijana wadogo waliposikia habari za kileo hiki na utamu wake, walifanya juu chini kuona kuwa walipata fursa ya kukionja. Mzee Mkarara alikuwa na barobaro kwa jina Maraha na mjakazi aliyeitwa Sijali. Mkarara alipitia pale na kupewa sehemu yake.
Babake Maraha alipofika akiwa mlevi, hakusita kumwita Sijali kwani mkewe alikuwa safarini kikazi. Alimshawishi Sijali kukionja kileo kile kidogo na alipokataa, alimtishia kumwachisha kazi ndipo maskini binti wa watu akaridhia kuonja kwa madai kuwa iwe mara ya mwisho. Siku iliyofuata Sijali alimwita Maraha na kumshawishi kuonja kileo alichomwachia baba yake. Maraha aliona raha kweli.
Haukupita muda mrefu ikabainika kuwa kileo kile kilikuwa na madhara makubwa kwa mtumizi. Wote waliokitumia walianza kulalamika na walipopimwa, walipatikana na sumu fulani mwilini ambayo ilianza kuwaua polepole. Mke wa Mkarara alipopata habari akaamua kuwaita madaktari kuipima familia yake. Ajabu ni kwamba ni binti yake tu aliyeonekana salama kwani kila mtu alikuwa na sumu ile mwilini.
Alipoulizia Maraha alikiri kuonjeshwa na Sijali baada ya kupewa na babake, mzee Mkarara. Hata mkewe pia aliugua kwa kuambukizwa na mumewe. Jamaa nzima iliangamia kwa sumu ila Makini, binti yao aliyekataa katakata kuwa bendera. Wafu hawa wa familia ya Mkarara walizikwa kwa mazishi ya pamoja. Wale madaktari waliotambua sumu ile walikuwa kwenye maombolezo. Walipata nafasi na kuelezea kilichoangamiza familia ile. Walinadi kuwa walikuwa wamekunywa kinywaji ambacho kilikuwa kimetiwa madini yanayotumiwa kuhifadhi maiti ufuoni. Walisema kuwa sumu hiyo ilipoingia mwilini iligandisha damu na kusababisha saratani ya damu. Watu wengi walianza kubabaika kwani idadi kubwa ilikuwa imekionja kileo kile. Daktari aliwashauri wote waende wakapate vipimo kamili ili kubaini hali yao ya afya.
Yule 'mgema' alipoipata taarifa ile alichana mbuga. Alijua kuwa angeshikwa angekula kalenda kwa kuwagemea watu sumu. Serikali ilipitisha sheria kali dhidi ya vileo vile visivyohalalishwa. Isitoshe, muda wa starehe za mvinyo ulifupishwa wala si wakati wote ilivyokuwa awali. Serikali iliwashauri wakazi wa mji huo mkuu kuwajibika na kurudisha maadili mema lau jamii yote ingekwisha.
- Kulingana na aya kwanza
- wakazi wa Tuleraha walitoka sehemu ambazo hazikuwa na mila wala desturi
- wazee wachache waliojua tamaduni waliruhusiwa kuwafunza wengine
- mambo mengi yaliyofanywa na wana Tuleraha yalichochewa na wazungu na uzungu
- tamaduni zilizotalikiwa si pamoja na mavazi, vyakula na ustaarabu
- "Mitandao ya kijamii ndiyo iliyokuwa walimu wa vijana wengi pale." Huku ni kumaanisha kuwa
- wanafunzi wengi walitumia mtandao kusoma
- nchi hiyo ilikuwa imepiga hatua kubwa kidijitali
- hapakuwa na walimu wa kufunza vijana katika nchi ile
- wakazi walitegemea na kuyafuata yaliyonadiwa mitandaoni
- Shahada ya uzamili ni shahada gani?
- Ni shahada ya pili baada ya kupata shahada ya kwanza
- Ni shahada ya mwisho zaidi katika masomo
- Ni shahada inayotwaliwa na waandisi pekee
- Ni shahada ya tatu inayompatia mtu udaktari
- Kinywaji kinachozungumziwa katika aya ya tatu kilipendwa zaidi kwa kuwa
- kilikuwa kikiuzwa kisirisiri
- kilikuwa katika ile hali ya kunoga
- kilitumiwa na wazee pamoja na vijana
- kilikuwa kinywaji kipya pale jijini
- Kijiji cha Tuleraha kilijulikana kwa sifa gani?
- Ulevi chakari
- Vileo chakari
- Raha chakari
- Madanguro chakari
- Ni ipi si sahihi kulingana na habari uliyoisoma?
- Watu wote waliangamia katika familia ile
- Binti wa mzee Mkarara ni Maraha
- Sijali alikionja kileo kile kwa kusurutishwa
- Maraha alionja kileo cha sumu
- Ni nani aliyemwonjesha Maraha kileo cha sumu?
- Karamka
- Makini
- Tuleraha
- Sijali
- Ni kipi kilichokuwa kilele cha madhara ya sumu ile inayozungumziwa?
- Kuwapofusha watumizi
- Kusababisha watu kugandishwa damu
- Kusababisha mauko baina ya jamii.
- Kusababisha maradhi ya saratani
- Kulingana na taarifa uliyoisoma
- ni familia nyingi zilizoathiriwa na sumu ile
- familia nyingi huenda ziliathiriwa na sumu ile
- serikali ilijitia hamnazo kuhusu suala la sumu
- ni uajibikaji wa serikali tu utakaoiokoa jamii ile
- Ni kichwa kipi kinachofaa ufahamu uliosoma?
- Bendera hufuata upepo
- Raha nyingi ni karaha
- Kila kilevyacho si tembo
- Ulevi unamfaidi mlevi
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50
Bila shaka umewahi kusikia watu wakimtaja mwenzao kuwa ni mhalifu. Mimi kwa kweli neno hili uhalifu sielewi maana yake hasa. Labda nisake ushauri wa wataalam kama Bwana Hussaini Khali ambaye amebobea na kutopea kwenye lindi la uswahili. Naam! Imara ya jembe ka ingoje shambani.
Ama kwa kweli, uhalifu ni hali ya uvunjaji sheria za nchi au jamii. Kwa mintarafu hii anayevunja sheria moja kwa moja hujibatiza jina la mhalifu. Mhalifu ni mtu asiyependwa na wengi kwani anaaminika kuwa mtu wa kuvuruga staha za wenzake. Mtu kama huyu aghalabu huelekea kukosa hata mtu wa kumnasihi kwa namna watu wacheleavyo kushirikiana naye.
Pwagu aidha ni mhalifu, yeye huvunja amri isemayo asiibe. Atakuja kukujulia hali ukakaramka kuwa pako kutokea ajinabi kumbe amekuja kuchunguza jinsi hali yako ilivyo. Baadaye akishapata ramani ya maskani yako, hutokomea kuandaa kikosi cha wageni wasioheshimu wenyeji, Kwa kupumbazika na kutekwa bakunja na ubinadamu ghushi aliokuonyesha, utashtukia pamejiri mikasa na wizi wa mabavu na huenda ukapoteza hata uhai. Naam! Mgeni kumpokea kumbe ni kujihasiri.
Watu wanaowaajiri watoto wanavunja sheria hususan wale wanaowaadhibu watoto kijeshi kwa mijeledi, fimbo na makofi. Wafahamu kuwa ni ukiukaji wa haki za watoto. Waelewe kwamba siku watakapotiwa mbaroni wataishia na kilio cha mbwa mdomo juu, ndipo watalazimika kutia akilini msemo, majuto ni mjukuu huja kinyume na mwiba wa kujidunga hauambiwi pole.
Wavyele wanaokataa katakata kuwapeleka wana wao shuleni watambue kuwa wamo katika uhalifu jinsi walivyo wahuni na wachopozi. Hata hivyo, yafaa waelewe kuwa mbio za sakafuni huishia ukingoni na nguvu ya mayonda huishia jangwani. Wanaoshuhudia uongo na kuwasingizia wenzao mambo ambayo hayana msingi madhubuti aidha wamevunja kanuni za nchi. Unaposhiriki porojo bila shaka una mshabaha na wanyang'anyi wa kutumia mabavu.
Abiria wawapo safarini kisha wakarakibu daladala, huhitajika kujisetiri kwa mikanda ya usalama. Watu wanaokosa kujifunga mikanda ya usalama hawatii sheria ambao wao aidha ni wahalifu. Fahamu kwamba asiyetii hutiwa. Ni jambo bora na mwanana endapo lusi razini watakuwa watiifu angalau kuepuka lawama na majuto. Bora kuzuia majuto tukifahamu kuwa kinga yashinda tiba.
- Mtu avunjaye amri za nchi au jamii bila shaka si
- mwadilifu
- maadili
- mwasi
- mzalendo
- Bwana Hussaini Khali anatajika kifunguni kama
- msomi
- mswahili mahiri
- mhandisi
- kandawala
- Ni usemi gani utakoingiana barabara na aya ya tatu?
- Mgeni aje mwenyeji apone.
- Mgeni hachomi chaza mtaani
- Mgeni kumpokea kumbe ni kujitongea
- Mgeni ni kama kengewa huruka akenda kwao
- Mhalifu si rahisi kutangamana na wenzake kwakuwa
- ana sura mbaya
- hana afya njema
- hana imani mwafaka
- ni mfano mbovu
- Ni kauli ipi kutokana na taarifa isiyo ya kweli?
- Mshabaha upo baina ya dini na sheria za nchi
- Sheria za nchi hazihusiki na dini yoyote
- Wafanyayo makosa yoyote ni wahalifu
- Lusu si mwasi
- Neno ajinabi lilivyotumika yamkini linia maana ya
- mgeni
- kigeni
- desturi
- sherehe
- Wageni wasioheshimu wenyeji... ni kina nani hawa?
- Majangili
- Majambazi
- Makaidi
- Wahalifu
- Kwenye aya ya tatu, mwandishi anatoa tahadhari kuhusu
- kukirimu wageni
- kutunza wageni
- kupokea wageni
- kushuku wageni
- Abiria aliye kwenye matwana aweza kuitwa mhalifu kwa
- kutolipa nauli
- kujifunga mkanda wa usalama
- kutovuta sigara
- kutulia garini
- Kwenye aya ya mwisho, mwandishi anatoa nasaha inayoandamana na msemo
- kuepukana na tatizo kuliko kusubiri balaa ikufike kwanza ni bora
- heri ungoje ujionee
- kujionea balaa ni vizuri
- heri kungoja maana utakuwa shujaa
INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako
Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu huku ukianza kwa kifungu ulichopewa.
Ilikuwa siku ya michezo ya riadha shuleni kwetu Bahati. Hivyo basi.......
MAJIBU
Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 5
MASWALI
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi, umepewa majibu manne.
Chagua jibu lifaalo zaidi.
Laiti angalimaizi, abadan katan ............1...............katika ............2............... ............3............... Ilikuwa ............4............... kwao wavyele wake kumhimiza ............5............... juhudi, ............6...............sikio la kufa halisikii ............7............... Kilio cha mtima ndicho ............8............... kila uchao. Alipanda pankwisha akavuna
............9...............
-
- angalizembea
- asingelizembea
- angezembea
- asingalizembea
-
- somo
- masomoni
- ujiva
- masomo
-
- zao
- yake
- yao
- wake
-
- mwelekeo
- kaida
- kusudi
- nia
-
- kutojali
- kujibali na
- kutoasi
- kuasi
-
- bali
- seuze
- mbali
- licha ya
-
- yeyote
- uneni
- madawa
- dawa
-
- anakiamkia
- wanachokilalia
- anakilalia
- anachokilalia
-
- pankwisha
- ayami
- pantosha
- kiishicho
Hakika misitu ............10...............umuhimu chungu ............11............... ............12...............uhifadhi ............13............... ni jambo ............14............... kuzungumziwa na kutiliwa mkazo ............15............... kumbi na mikutano iliyopangwa na itakayopangwa kote duniani.
-
- inazo
- inalo
- inao
- inayo
-
- mzima
- nzima
- zima
- nomi
-
- Kwa sababu
- Hata hivyo
- Kwa mintarafu
- Kwa hivyo
-
- wazo
- wayo
- wapo
- wao
-
- linalobidi
- linaobidi
- linaostahili
- lisilostahili
-
- kwa
- si
- pasipo
- katika
Kutoka swali la 16 mpaka 30, jibu kila swali ukifuata maagizo uliyopewa.
- Ni orodha gani ya nomino za ngeli ya U-YA pekee?
- Mabua, mauaji, mawele, maumbo
- Uuaji, ulezi, ubao, ugonjwa
- Upishi, malezi, mawele, makelele
- Magonjwa, maua, mapishi
- Ni sentensi gani kati ya hizi imetumia methali?
- Mtoto alilala fofofo
- Usipoziba ufa utajenga ukuta
- Swali hili lilikuwa mboga
- Amina ni mwoga kama kunguru
- Ipi si maana ya neno "chuma"?
- Pata pesa nyingi
- Toa matunda kutoka mtini
- Mtu asiye na nguvu
- Aina ya madini
- Tegua kitendawili:-
Kina mkono na uso lakini hakina uhai- jua
- Nyota
- saa
- sahani
- Kinyume cha sentensi:-
Shangazi anaondoka nje anarudi ndani ni- Mjomba anarudi ndani kutoka nje
- Shangazi anarudi ndani kutoka nje
- Mjomba anarudi nje kutoka ndani.
- Shangazi anarudi nje kutoka ndani
- Kulia ni kwa machozi, jeraha ni kwa
- kamasi
- matongo
- damu
- usaha
- Malipo anayopatiwa mtu aliyekwazwa ili kuondoa hasira yake ni
- kilemba
- honoraria
- mapoza
- marabaha
- Mwalimu yule aliyekuja jioni ni jirani yangu.
Maneno yaliyopigiwa mstari ni- kielezi, kiwakilishi, kivumishi
- kivumishi, kielezi, kiwakilishi
- kiwakilishi, kivumishi, kielezi
- kivumishi, kielezi, kivumishi
- Kati ya wafanyakazi hawa, ni yupi anayeuza bidhaa rejareja mnadani?
- Dalali
- Nokoa
- Hamali
- Mchuuzi
- Chagua sentensi ambayo ni sahihi kisarufi
- Wamezificha funguo kabatini ile
- Moshi anafuka chumbani mle penye wageni
- Barasteni penyewe kumelimwa tena
- Moyoni mwake ndimo mlimoficha siri
- Jaza vihasho kwa maneno sahihi:-
Alimwinda .....................................na jioni aka ...................................mchuzi mkali kama...................................- siki, unga, sigi
- sigi, uga, siki
- sigi, unga, siki
- unga, siki, sigi
- Andika kauli ya taarifa ya:-
"Mbona unayachafua mazingira hivi?” aliuliza- Alitaka kujua mbona ulikuwa ukichafua mazingira hivyo
- Alitaka kujua mbona alikuwa akichafua mazingira vile
- Aliuliza sababu ya kuchafua mazingira hivi
- Aliuliza mbona unachafua mazingira hivyo
- Chagua jibu lisilo sahihi
- Maktaba: YA-YA
- Nyanya: 1-ZI
- Uyoga: U-U
- Unyasi: U-ZI
- Kilinge ni cha wachawi ilhali .......................................ni kwa vitabu,
- bunda
- matopa
- furushi
- mtungo
- Kiingilio hutolewa kuingilia chumba cha burudani.
Malipo au zawadi inayotolewa kwa mtu aliyeona au kuokota kitu kilichopotea ni- ada
- fidia
- utotole
- kiokote
Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali 31-40.
Siku ya chete hungojewa kwa hamu na hamumu katika mji wa Leteraha. Hii ndiyo siku watu wa mbali na karibu hutangamana kwa madhumuni tofauti. Kunao wanaoleta bidhaa mbalimbali kuziuza. Kunao wengine ambao hutangaza huduma hizi au zile ilhali kunao wanaokuja kununua. Mara nyingi ununuzi si ununuzi tu bali ni ununuzi kwelikweli. Kwa vile wanunuzi wengi wanafahamu fika kuwa itawachukua siku saba ndipo wafike sokoni tena, inabidi basi wanunue bidhaa za kudumu siku zote hizo.
Nao wauzaji huhakikisha kwamba wanakidhi mahitaji ya wateja wao maana wasingependa wao waende mbali kutafuta bidhaa au huduma hizo. Basi mimi na sahibu yangu Mwendwa tulilizuru soko hilo la kwetu siku ya chete Jumamosi iliyopita. Baada ya pitapita za hapa na pale na ununuzi wa vitu hivi na vile tuliona tumeridhisha haja zetu. Tukawa tunajiandaa kuambua nyayo kurudi makwetu.
Ghafla ustahi ulisikika kutoka karibu na tulipokuwa tukifungia mzigo wetu. Ustahi huo ulitatiza na kutatiza kelele zilizokuwa zikiendelea pale sokoni. Wacha mtafuruku upande moto. Ni kupita kwa watu waliokuwa karibu mno na tukio la mkasa ndipo tulipata fununu ya mambo.
Mwendawazimu mmoja alitokea kudai kuwa mwanamume fulani aliyekuwa amevalia nadhifu kuwa ni mumewe. Yule mwanamke mwendawazimu aliyejulikana sana pale sokoni aliitwa Wamnara. Alimshika maskini mwanamume wa watu na kukatalia ungedhani dondora. Juhudi za mwanamume huyo kujaribu kujinasua zilimjadirisha tu Wamnara. Wehu ukampanda maradufu kama zaibaki kwenye kipimajoto. Sauti kali iliendelea kumtoka huku akitaka yule mwanamume amwambie mbona alimwacha pale sokoni na kutoweka.
Kioja hicho kilivuta na kuvutia lukuki ya watu. Baadhi yao walimwonea huruma mwanaume yule huku wengine wakimsihi Wamnara kumwacha.
- Watu wengi huitazamia siku ya chete kwa kuwa
- kunazo jamii zilizoendeleza elimu ua kujenga nyumba
- kila jamii ilifunza elimu ya kupaka kuta rangi
- ni siku ya kutangamana
- ni siku ya kuleta bidhaa tele sokoni
- Mnunuzi huitwa mteja au
- mhudumu
- mshitiri
- dalali
- mwuzaji
- Siku ya soko pale mjini Leteraha ilitanguliwa na
- Alhamisi
- Jumapili
- Ijumaa
- Jumanne
- Mwandishi na Mwendwa walidhamiria kufanya nini sokoni?
- kumwona mwendawazimu Namnara
- kununua bidhaa kadhaa pale sokoni
- kutongamana na wauzaji na wanunuzi
- kwenda kuuza bidhaa kadhaa
- Wanakidhi mahitaji ya wateja maana yake ni
- wanatosheleza matilaba ya wanunuzi
- wanaridhisha haja zao na za wateja pia
- wanawaudhi wanunuzi
- wanawapunja wanunuzi
- Kizaazaa kilisababishwa na nini pale sokoni?
- watu waliokuwa wakiambua nyayo
- tafrani za wanunuzi waliotaka kuhudumiwa haraka
- ukwenye uliotoka karibu na alikosimama Mwendwa
- moto ulioanza kuungaza vibanda sokoni
- Mwendwa na rafikiye hawakudhamiria
- kuwa miongoni mwa waliofika kutazama kioja cha sokoni
- kuona vioja vya pale sokoni
- kujua nini kilichotafirisha shughuli za sokoni
- kuabiri gari na kurudi makwao
- Kwa nini Wamnara alimganda mwanaume yule?
- Alidai kuwa mwanaume huyo alimrelekeza
- Alipendekezwa na jinsi alivyovalia maridadi
- Walijuana sana tangu zamani
- Alidai kuwa mwanamume huyo alikataa kununua bidhaa zake
- Vitimbi hivyo viliisha wakati
- polisi walifika na kumshika Namnara
- mwanamume alipofurukuta na kujinasua kisha akatoroka
- mwanamume huyo alimkubalia Namnara maombi yake
- watu waliingilia kati na kumsaidia mwanamume huyo
- Kichwa kipi kinafaa kwa habari hii?
- Vioja sokoni
- Mnunuzi ashikwa kwa kumwibia mwendawazimu
- Kila soko lina wendawazimu wake
- Wamnara na koti la mwungwana
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50.
Siku za hivi karibuni, mambo ni kana kwamba kaenda segemnege katika taifa fulani liitwalo Kenya. "Watazamaji leo tungependa kuanzia kwa habari za tanzia. Abiria watano kaitwa rehemani baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani. Wenzao manusura si hayati si mamati na wamo hospitalini" Runinga moja katika taifa hili ilipeperusha habari.
Wadau wa sekta ya uchukuzi katika taifa la Kenya kutwa kucha vichwa wajipata kongamanoni kukitegua kitendawili hiki sugu "Wakuu wa trafiki, wasimaminzi wa barabara na wahusika wengine, sabalkheri? Ningependa kunena kuwa ajali nyingi taifani zinasababishwa na baadhi ya haya. Madereva wengine baada ya kubugia ya mgema hujipata usukani. Magari mengine huwa ni yale ambayo spana ziwe tayari. Silatini si kwao kwema. Imemaizika kuwa magari mengine huendeshwa kwa kasi ghaya. Bila shaka kasi hii ya duma huyaleta maafa yaso kinaya. Baraste zingine huwa na mashimo yasokarabatiwa.
Magari yanapoyagonga pengine hujipata kabingiria bingiribingiri. Abiria" Wengine wasibahatike kutoyaona mauko." Ukumbi wote hakuna aliyesinasina wala kukohoa. Walimkazia macho aliyekuwa mkabala. Hoja zake ziliwaingia akilini na kuwapa kero. Basi tufanye nini kuyaokoa aushi ya maskini abiria na waendashaji wa magari, bodaboda na tuk-tuk?.......?
- Kwa mujibu wa aya ya kwanza
- mambo hayakuwa vyema
- risala za heri zilitumwa na mtangazaji
- habari runingani ilitamiwa
- utulivu kafurahiwa Kenya
- Tambua jibu lisilo na maana ya kwenda segemnege.
Kwenda- mvange
- kasi
- kombo
- mrama
- Kulingana na kifungu,
- nia yao ilikuwa kuvikuna vichwa
- wadau walikuwa ajizi
- walijitia hamnazo kuhusu ajali
- walichemsha bongo kuhusu kero lao
- Ni kweli kulingana na kifungu kuwa kongamano
- Lilitia nanga macheo
- Liling'oa nanga asubuhi
- Halikuanza katu
- Lilisitishwa asubuhi
- Ajali katika nchi husika
- ubugia tembo si hoja
- zaadimika
- ni nadra
- visababishi ni ayami
- Magari, spana ziwe tayari kama ilivyotumika katika ufahamu ina maana
- magari yenye spana
- spana kuwa tayari
- makanika wawe tayari
- magari mabovu
- Tambua neno lisilo kisawe cha silatini
- barabarani
- barasteni
- manzilini
- njiani
- Tambua matumizi ya............bingiribingiri.
- chuku
- nahau
- tanakali za sauti
- tashbihi
- Kulingana na kifungu, aya ya tatu ukumbini mwa kongamano
- hali ilikuwa shwari
- kimya kilitamalaki
- watu walifurika
- hatibu alisimama kando
- Tambua maana ya maskini kama iliyotumika kifunguni
- fakiri
- hohehahe
- akina yahe
- waathiriwa
MAJIBU
INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.
Andika insha ya kusisimua ukianzia kwa maneno haya :-
Ilikuwa siku ya ziara. Tulikuwa tumeingoja kwa hamu na ghamu.........................................................................................................................................................
..............................................................................................................................................................................................................................................................