KISWAHILI Paper 1 Questions and Answers - KCSE 2022 Past Papers

Share via Whatsapp

MASWALI ; 

  1. LAZIMA 
    1. Fadhila ni miongoni mwa wanafunzi waogombea nafasiya kiranja katika shule ya upili ya kumekucha . Hekima anamhoji kuhusu mikakati atakayoweka ili kuboresha hali ya maisha shuleni . Andika mahojiano hayo .
  2. Rafiki yako hapendi riadha . Andika barua kumshawishi kubadili mtazamo wake .
  3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali  ifuatayo ;Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe. 
  4. Tunga kisa  kitakachomalizikia kwa maneno yafuatayo;
    Hapo ndipo nilipotambua kwamba mtu akitia bidii katika jambo hata likiwa gumu vipi , hafanikiwa.

MARKING SCHEME

  1. Hii ni insha ya mahojiano.
    Vipengele vifuatavyo vijitokeze:
    1. Muundo
      Kichwa

      Kiandikwe kwa herufi kubwa.
      Kichwa kitaje ni mahojiano baina ya Fadhila na Hekima, yanafanyika wapi na yanahusu mada gani. Kwa mfano, MAHOJIANO KATI YA HEKIMA NA FADHILA KUHUSU MIKAKATI YA FADHILA YA KUBORESHA HALI YA MAISHA SHULENI.
      Utangulizi 
      1. Maamkuzi yajitokeze
      2. Makaribisho kutoka kwa mhoji - Hekima.
      3. Kiini cha mahojiano kijitokeze hapa.
      4. Mhoji anaweza kumhongera mhojiwa ama kwa kufika kwenye mahojiano au kwa kujitosa kwenye kinyang'anyiro.
        Mwili
        Hoja zijadiliwe hapa. Kila hoja kwenye aya.
        Hitimisho
        1. Kuhusu mada na wa kimuundo- ajumuishe mawazo yake.
        2. Mhoji anaweza kutoa muhtasari wa hoja zilizojadiliwa au msimamo wake kuhusu hoja zilizojadiliwa.
        3. Mhoji anaweza kumshukuru mhojiwa kwa kufika.
    2. Mtindo
      1. Hoja zijadiliwe kwa mtindo wa kimazungumzo.
      2. Upashanaji zamu ufaao udhibitiwe na mhoji.
      3. Mahojiano yazingatie lugha rasmi. Maneno ya misimu yanapotumiwa yatiwe kwenye
        nukuu.
      4. Mahojiano yawe na dayalojia ya kidrama; majina ya mhoji na mhojiwa yaandikwe pambizoni na kufuatwa na koloni kabla ya kauli halisi.
    3. Maudhui
      Baadhi ya hoja ni:
      1. Kuimarisha nidhamu shuleni kupitia kwa shughuli za ushauri nasaha.
      2. Kuleta mshikamano miongoni mwa wanafunzi.
      3. Kuboresha uhusiano kati ya wanafunzi na walimu.
      4. Kuhimiza kushiriki katika michezo na ukuzaji wa talanta.
      5. Kukuza uhusiano kati ya walimu, wafanyakazi na wanafunzi.
      6. Kuimarisha juhudi za usafi. Kwa mfano, kuweka ratiba ya kufanya usafi shuleni.
      7. Kuhimiza huduma kwa jamii kwa mfano, kutoa ufadhili/ kuwahudumia wenye uhitaji kwa kuanzisha mfuko wa kuchangia.
      8. Kuhimiza usimamizi wa shule kuzingatia lishe bora.
      9. Kuhimiza usimamaizi wa shule kuboresha miundomsingi.
      10. Kuimarisha mawasiliano shuleni.
      11. Kuboresha utendakazi wa viranja
      12. Kuhakikisha usalama shuleni kwa kuwahimiza wadau kuweka mikakati mwafaka. (xiii) Kupigania haki/ kuwatetea wanaodhulumiwa.
        Tanbihi
        1. Mtahiniwa anaweza kuzingatia mkakati mmoja kwa mapana na kufafanua vipengele vyake kama vile udumishaji wa nidhamu.
        2. Mtahiniwa atathminiwe kimaudhui kulingana na jinsi anavyojieleza.
        3. Vigezo vingine vya usahihishaji vizingatiwe kulingana na mwongozo wa kudumu.
  2. Hii ni insha ya barua ya kushawishi yenye muundo was kirafiki. Mtahiniwa anastahili kuandika insha ambayo inazingatia ukweli kuhusu manufaa ya riadha. Baadhi ya hoja ni:
    1. Ajira/kazi
    2. Kukuza vipawa
    3. Kutangamana/ kuimarisha utangamano
    4. Kuboresha afya
    5. Kujenga kukuza umoja au ushirikiano
    6. Kukuza uzalendo
    7. Ni kitambulisho cha jamii
    8. Kuimarisha uchumi
    9. Kukuza utalii
    10. Kujenga jina/ umaarufu
    11. Kudhibiti na kupunguza uhalifu
    12. Kujenga nidhamu
    13. Kujenga mwili
    14. Kuchangamsha bongo
    15. Burudani
    16. Kujenga ukakamavu ujasiri
  3.  
    1. Hii ni insha ya methali. Mtahiniwa anastahili kutunga insha ya masimulizi inayodhihirisha maana na matumizi ya methali hii.
    2. Mtahiniwa atunge kisa kinachodhihirisha kwamba anayechelea kumwadhibu mwana huishia kujuta.
    3. Hali zifuatazo zinaweza kujitokeza:
      1. Msimulizi anafahamu mzazi fulani/ familia iliyodekeza mwana wao ambaye anapotoka kimaadili, wazazi wanajuta kutomwadhibu mwana wao.
      2. Kuwepo kwa kiongozi ambaye alishindwa kuwakanya walio chini yake dhidi ya mienendo isiyofaa kisha akaingia mashakani mambo yalipoharibika.
        Tanbihi
        1. Lazima pande zote za methali zijitokeze
        2. Mtahiniwa aonyeshe mhusika anayeogopa kumwadhibu mdogo wake aliye chini yake kisha anajuta mabaya yanampomfika.
        3. Mwongozo wa kudumu urejelewe katika utuzaji.
  4. Mdokezo
    1. Hii ni insha ya mdokezo wa kumalizia.
    2. Ni insha ya masimulizi. Mtindo wa kimasimulizi utumiwe.
    3. Mtahiniwa atunge kisa ambacho kinaoana na kimalizio kilichotolewa.
    4. Kisa kionyeshe umuhimu wa kutia bidii maishani.
    5. Ruwaza ifuatayo inaweza kujitokeza:
      Mhusika aliyekabiliwa na jambo gumu kisha akajibidiisha bila kukata tamaa na hatimaye kufanikiwa.
      Tanbihi
      1. Hali ya kutia bidii sharti ijitokeze.
      2. Mwongozo wa kudumu urejelewe katika utuzaji.
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI Paper 1 Questions and Answers - KCSE 2022 Past Papers.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?