Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Bungoma Diocese Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

Instructionns to students

 •  Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
 • Kisha chagua insha moja nyingine kutoka kwa hizo tatu zilizobakia.
 • Kila insha isipungue maneno 400.
 • Kila insha ina alama 20.
 1. Umechaguliwa kuwa katibu wa Chama cha Kiswahili shuleni. Andaa kumbukumbu za mkutano uliofanyika hivi majuzi ili kupanga mikakati ya kukiendeleza Kiswahili ndani na nje ya shule yenu.
 2. Vijana wa sasa wanakumbwa na changamoto nyingi za maisha. Thibitisha kauli hii huku ukieleza namna wanavyoweza kuzishughulikia.
 3. Ngozi ivute ili maji.
 4. Andika insha itakayomalizikia kwa kifungu hiki:-
  …….. ndivyo wahenga kuwa aliye juu mngojee chini. Hii ni zamu yao sasa. Wamewadhulumu wanawake kwa miaka na miaka. Wacha wapate kichapo cha kisasi.


MARKING SCHEME

 1.  
  1. Muundo wa kumbukumbu.
   1. Kichwa/mada
  2. Rekodi ya mahudhurio.
   1. Waliohudhuria
   2. Waliotuma udhuru
   3. Waliokosa kuhudhuria bila udhuru
   4. Mahudhurio
  3. Rekodi ya Ajenda.
   1. Kusoma kumnukumbu za mkutano uliopita
   2. Masuala yanayoibuka kutokana na kumbukumbu za mkutano uliopita
   3. Mambo yatakayozungumziwa.
    Huandikwa kwa muhtasari
    Kila ajenda hueleza kwa ufupi
  4. Kufunga mkutano
  5. Mkutano mwingine (si lazima)
  6. Mwisho/hitimisho
   Nafasi ya sahihi ya Mwenyekiti na Katibu kuidhinisha kumbukumbu.
 2. Hii ni insha ya maelezo
  Changamoto:_
  1. Magonjwa sugu (ukimwi)
  2. Dawa za kulevya
  3. Ukosefu wa ajira
  4. Umaskini uliokithiri
  5. Uigaji wa tamaduni za kigeni
  6. Athari za utandawazi
  7. uchumi kudoroa (Kustaafishwa mapema)
  8. Kuibuka kwa lugha ya vijana isiyoeleweka na wavyele wao, basi kukosa maongozi bora.
  9. Shinikizo la hirimu (marika)
  10. Ujana (Ushababi)
   Taja zozote 5 (changamoto na pendekezo la kusuluhisha)
 3. Swali la methali
  Methali: Ngozi ivute ili maji
  Methali nyingine yenye maana sawa na hii ni
  Samaki mkunje angali mbichi
  Maana: Ngozi huvutika vizuri inapokuwa mbichi kabla haijakauka, ikaukapo haivutiki.
  Matumizi. Methali hii inatufunza umuhimu wa kulirekebisha jambo kabla halijaharibika kabisa.
  • Mtahiniwa anaweza kuandika ufafanuzi wa maana ya juu, pamoja na matumizi ya methali au ayapuuze.
  • Mtahiniwa aandike kisa (visa) kinachooana na methali hii.
  • Mtahiniwa akiandika kisa kinachopingana na methali hii atakuwa amejitungia swali apewe bakshishi (01-02)
 4. Insha ya maelezo: Dhuluma dhidi ya wanaume:
  1. Kupigwa
  2. Kufanyizwa kazi nzito za kinyumbani.
  3. Kutusiwa/kukashifiwa.
  4. Kunyimwa haki za ndoa.
  5. Kukejeliwa (wakosapo ajira)
  6. Kushurutishwa kutoa pesa zote.
  7. Kunyimwa uhuru wa kutoa maoni.
  8. Kunyimwa chakula (wafikapo nyumbani kuchelewa/walevi).
   Tanbihi
   1. Mtahiniwa akipachika kimalizio, atakuwa amepotoka.
   2. asiyeweka kimalizio, amejitungia swali

KIWANGO CHA D
MAKI 01 – 05

 1. Insha ya aina hii haieleweki kwa vyovyote, ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana,
  hivi kwamba mtahini lazima afikirie kile anachojaribu kuandika.
 2. Mtahiniwa hana uwezo wa kutmia maneno ya Kiswahili kwa njia inayofaa.
 3. Lugha imevurugika, uakifishaji haufai na insha ina makosa ya kila aina; kisarufi, kimaendelezo, kimtindo n.k.

VIWANGO TOFAUTI VYA D.
D- (KIWANGO CHA CHINI) MAKI 01-02

 1. Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile kwa vyovyote vile. Kwa mfano, kunakili
  swali au kujitungia swali tofauti na kulijibu.
 2. Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili.
 3. Insha za aina hii zifanywe uamuzi na kiongozi wa kikundi.
 4. Yule anayenakili kichwa kutoka karatasi ya maswali lakini hakushughulikia mada inayokusudiwa atakuwa amejitungia swali.

D (KIWANGO CHA WASTANI) MAKI 03

 1. Utiriko wa mawazo haupo.
 2. Insha haieleweki.
 3. Hoja hazikuelezwa kikamilifu / mada haikukuzwa vilivyo.
 4. Mtahiniwa amepotoka kimaudhui. hakuzingatia urefu.
 5. kuna makosa mengi ya kila aina.

D+ (KIWANGO CHA JUU) MAKI 04 - 05

 1. Insha hii ina makosa mengi ya kila aina. Lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kusema.
 2. Insha ina lugha dhaifu ya Kiswahili na haina mpangilio.
 3. Anawasilisha ujumbe kwa njia isiyoeleweka kikamilifu.
 4. hana uhakika wa matumizi ya lugha na hupotoka hapa na pale.
 5. mpangilio wa kazi ni dhaifu na mtahiniwa hujirudiarudia.
 6. mtahiniwa ana athari za lugha ya kwanza k.m. papa, badala ya baba, karamu badala ya kalamu n.k.

KIWANGO CHA C – MAKI 06 – 10
Kiwango hiki kina makosa yafuatayo:

 1. Mada haijakuzwa na kuendelezwa.
 2. Anawasilisha ujumbe kwa njia isiyovutia.
 3. Hana ubunifu wa kutosha.
 4. Anaakifisha sentensi vibaya.
 5. Hana mstamiati wa kuvutia wala msamiati mwafaka.
 6. Kuna makosa mengi ya sarufi, msamiati na hijai (tahajia).

VIWANGO TOFAUTI VYA C
C- (KIWANGO CHA CHINI) MAKI 06 – 07

 1. Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha mawazo yake.
 2. Hana msamiati wa kutosha wala muundo wa sentensi ufaao.
 3. Mada haijakuzwa na kuendelezwa kwa njia ifaayo.
 4. Ana makosa mengi ya sarufi, tahajia na msamiati.

C (KIWANGO CHA WASTANI) MAKI 08

 1. Anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu.
 2. Hana ubunifu wa kutosha na dhana tofauti tofauti hazijotekzi wazi.
 3. Uakifishaji wa sentensi zake si mzuri.
 4. Amejaribu kushunghulikia mada aliyopewa.
 5. Ana makosa ya hijai, sarufi na mswamiati.

C+ (KIWANGO CHA JUU) MAKI 09 – 10

 1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri lakini kwa njia isiyo na mvuto.
 2. dhana tofauti tofauti zimeanza kujitokeza kwa njia hafifu.
 3. kuna utiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa.
 4. misemo, methali na tanakali za sauti zimetumiwa kwa njia hafifu.
 5. Anashughulikia mada aliyopewa kwa utiririko mzuri.
 6. Kuna makosa ya sarufi, msamiati na hijai lakini bado insha inaeleweka.

KIWANGO CHA B, MAKI 11 – 15

 1. Katika kiwango hiki mtahiniwa anaonyesha kuimudu lugha vilivyo.
 2. Mtahiniwa anadhihirisha kwamba anaweza kutumia lugha kwa urahisi katika kuieleza.
 3. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi.
 4. Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha kama vile kuandika sentensi kwa njia tofauti na zikaleta maana sawa.
 5. Mada huwa imekuzwa na kuendelezwa kikamilifu.

VIWANGO TOFAUTI VYA B
B- (KIWANGO CHA CHINI) MAKI 11 – 12

 1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe wake kwa kuonyesha hoja tofauti tofauti, akizingatia mada.
 2. Ana utiririko mzuri wa mawazo.
 3. Ana uwezo wa kutumia miundo tofauti tofauti ya sentensi.
 4. Makosa ni ya hapa na pale.

B (KIWANGO CHA WASTANI) MAKI 13

 1. Mtahiniwa anadhihirisha hali ya kuimudu lugha.
 2. Anawasilisha ujumbe wake waziwazi kwa mawazo yanayodhihirika.
 3. Matumizi ya lugha ya mnato yamejitokeza.
 4. Anatumia mifano michache ya msamiati mwafaka.
 5. Matumizi ya tamathali za semi yanaanza kudhihirika.
 6. Kuna makosa machache ya hapa na pale.

B+ (KIWANGO CHA JUU) MAKI 14 – 15

 1. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika – kujitokeza waziwazi.
 2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe wake kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada.
 3. Uteuzi wake wa msamiati ni mzuri – mchanganyiko wa msamiati.
 4. sarufi yake ni nzuri.
 5. Uakifishaji wake ni mzuri.
 6. Makosa yanaweza kutokea ya hapa na pale.

A KIWANGO CHA MAKI 16 – 20

 1. Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato. Ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka.
 2. Ana uwezo wa kutumia tamathali za lugha ili kutoa hisia zake kwa njia bora na kwa urahisi.
 3. Umbuji wake nadhihirisha ukakamavu wake kimawazo na mpangilio mzuri na hali ya kumvutia msomaji wake.
 4. Kazi ya mtahiniwa ni nadhifu na hati nzuri.

VIWANGO TOFAUTI VYA A
A- (KIWANGO CHA CHINI) MAKI 16 - 17

 1. Mtahiniwa anadhihirisha ukomavu wa lugha.
 2. Ana utiririko mzuri wa mawazo kulingana na mada.
 3. Anapamba lugha kwa kutumia tamathali za usemi.
 4. Anazingatia matumizi mazuri ya msamiati na sarufi.
 5. Uakifishaji wake ni mzuri zaidi.
 6. Makosa machache yasiyokusudiwa.

A (KIWANGO CHA JUU) MAKI 19 – 20

 1. Mawazo yanadhihirika na anashughulikia mada aliyopewa.
 2. anatumia lugha ya mnato.
 3. Anatumia msamiati wa hali ya juu na unavutia.
 4. Sarufi yake ni nzuri zaidi.
 5. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi.
 6. Anajieleza kikamilifu
 7. makosa ni ndra kupatikana.

A+ (KIWANGO CHA JUU) MAKI 19 – 20

 1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kulingana na mada.
 2. Anadhihirisha mawazo yake vizuri zaidi.
 3. Anajieleza kikamilifu bila shida.
 4. Anatoa hoja zilizokomaa.
 5. Msamiati wake ni wa hali ya juu.
 6. Makosa yote yasizidi matano.

JINSI YA KUTUZA INSHA MBALI MBALI

 1. Mtahiniwa asipozingatia sura ya insha aondolewe maki 4 (nne) baada ya kutuzwa (4 sura).
 2. Insha isiyotosheleza idadi ya maneno ataondolwea maki 2 (mbili) badala ya kutuzwa (2U).

SARUFI
Sahihisha kwa makini sana ukionyesha makosa yote yanayotokea. Makosa ya sarufi huwa katika:
Kuakifisha vibaya; mifano, vikomo, vituo, alama ya kuuliza n.k.

 1. Kutumia herufi ndogo au kubwa mahali si pake.
 2. Matumizi mabaya ya ngeli na viambishi, nyakati, vihusiano, muundo mbaya wa sentensi na mnyambuliko wa vitenzi na majina.
 3. Kuacha au kuongeza neno katika sentensi kwa mfano, kwa kwa.
 4. Matumizi ya herufi kubwa.
  Tazama: Matumizi ya herufi kubwa.
  1. Mwanzo wa sentensi.
  2. Majina ya pekee.
  3. Majina ya mahali, miji, nchi n.k.
  4. Siku za juma, miezi n.k.
  5. Mashirika, masomo, vitaub n.k.
  6. Makabila, lugha n.k.
  7. Jina la Mungu.
  8. Majina ya kutambulisha k.m. majina ya mbwa,

MAKOSA YA HIJAI/TAHAJIA

Haya ni makosa ya maendelezo. Sahihisha huku ukiyaonyesha yanapotokea. Makosa ya tahajia huwa katika:

 1. Kutenganisha neno kama vile ‘aliyekuwa.’
 2. Kuunganisha maneno kama vile ‘kwasababu.’
 3. Kukata silabi vibaya kama vile ‘ngan-o.’
 4. Kuandika herufi isiyofaa katika neno kama ‘mahari ‘ badala ya ‘mahali.’
 5. Kuacha herufi katika neno kama ‘aliekuja’ badala ya ‘aliyekuja’.
 6. Kuongeza herufi isiyofaa katika neno kama piya badala ya pia..
 7. Kuacha alama inayotarajiwa kuwepo katika herufi.
 8. Kutoandika kistari cha kuunganisha neno ufikiapo pambazo au mwisho au kuandika mahali si pake.
 9. Kuacha ritifaa au kuiweka pasipofaa, ng’ombe, ng’ombe, ng’ombe.
 10. Kuandika maneno kwa kifupi km. v.v.

MTINDO
Mambo yatakayovunguzwa:

 1. Mpangilio wa kazi kiaya.
 2. Utiririko wa mawazo.
 3. Hati nzuri inayosomeka kwa urahisi.
 4. Namna anavyotumia methali, misemo, tamathali za usemi na mengineyo.
 5. Unadhifu wa kazi.
 6. Kuandika herufi vizuri, k.m Jj Pp Uu n.k.
 7. Sura ya Insha.

MSAMIATI
Jumla ya maneno yaliyotumiwa kuafikiana na mada au kichwa kilichopendekezwa.
MAUDHUI NA MSAMIATI
Baada ya kusoma mtungo utafikiria maudhui na msamiati uliomo kwa jumla.

ALAMA ZA KUSAHIHISHA
= Hupigwa chini ya sehemu ambayo kosa la sarufi
Limetokeza kwa mara ya kwanza.
- Hupigwa chini ya sehemu au neno ambako kosa la hijai limetokeza kwa mara ya kwanza tu.
∧ Hutumiwa kuonyesha kuachwa kwa neno
✓ Hutumiwa kuonyesha msamiati bora. Alama hii hutiwa juu ya neno lenyewe.
X Hutumiwa kuonyesha msamiati usiofaa. Alama hutiwa juu ya neno lenyewe.

Maelezo mafupi kuhusu tuzo la mtahini yanahitajika. Kila ukurasa uwe na alama ya chini katikati kuonyesha
kuwa mtahini ameupitia ukurasa huo.

MANENO
Maneno 8 - kurasa 1¾
Maneno 7 - kurasa 2
Maneno 6 - kurasa 2¼
Maneno 5 - kurasa 2¾
Maneno 4 - kurasa 3¾
Maneno 3 - kurasa 4½

001 – 174 – Robo
175 – 274 – Nusu
275 – 374 – Robo tatu
375 – 400 - Kamili


Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Bungoma Diocese Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest