Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Arise and Shine Mock Exams 2022

Share via Whatsapp
Maagizo
 1. Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 2. Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 3. Andika insha mbili.  Insha ya kwanza ni ya lazima kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
 4. Kila insha isipungue maneno 400.
 5. Kila insha ina alama 20.
 6. Karatasi hii ina kurasa 2 zilizopigwa chapa. 
 7. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa.
 8. Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
Matumizi ya Mtahini Pekee

SWALI

UPEO

ALAMA

1

20

 
 

20

 

Jumla

40

 

MASWALI

 1. Suala la umoja wa kitaifa wakati huu wa kampeni za uchaguzi limekuwa katika vinywa vya wananchi wengi.  Andika tahariri katika gazeti la MWANANCHI, kuhusu namna ya kustawisha umoja wa kitaifa.
 2. Magonjwa mengi yanasababishwa na mitindo ya kisasa ya maisha. Jadili.
 3. Andika insha inayoafiki methali; Asiyejua faida ya mwangaza aingie gizani.
 4. Andika insha itakayomalizika kwa; ... nilipojitazama, nilijidharau kwa aibu niliyopata. Niliapa kutorudia kitendo hicho maishani mwangu.

MWONGOZO WA INSHA - 2022

 1. Suala la umoja wa kitaifa wakati huu wa kampeni za uchaguzi  limekuwa katika vinywa vya wananchi wengi. Andika tahariri katika gazeti la MWANANCHI, kuhusu namna ya kustawisha umoja wa kitaifa.
  • Hii ni insha ya kiuamilifu.
  • Sura ya tahariri izingatiwe. Tahariri iwe na:
   1. Jina la gazeti: Mwananchi liandikwe
   2. Tarehe na siku  iandikwe
   3. Kichwa / anwani ya tahariri iandikwe
   4. Maudhui ya kujenga mada husika:namna ya kustawisha umaja wa kitaifa kama vile;
  • Kujiepusha na matamshi ya uchochezi katika mikutano ya kisiasa
  • Kutiwa mbaroni na kuchukuliwa hatua  wale wote wanatishia utangamano wa jamii mbalimbali.
  • Watu kutoka jamii/ mirengo ya kisiasa mbalimbali kushirikiana kuhimiza watu kuishi kama ndugu na dada.
  • Wanaoeneza ujumbe wa uchochezi katika mitandao ya kijamii wachukuliwe hatua na vyombo husika vya dola.
  • Watu wakubaliwe kuishi na kufanya biashara katika sehemu yoyote nchi bila kujali wanakotoka.
  • Shule ziwasajili wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali za jamhuri ili waweze kutangamana katika shughuli zote.
  • Miradhi ya maendeleo isambazwe katika kila sehemu ya nchi bila ubaguzi wowote.
  • Viongozi wa kidini  waendelee kuhubiri matakwa ya dini  mbalimbali kumpenda jirani unavyojipenda.
  • Watu wahimizwe kutembeleana katika maeneo yao mbalimbali.
  • Mitaala katika taasisi za elimu izingatie umoja umoja wa kitaifa kama mojawapo ya maswala muhimu katika masomo.
  • Ndoa kati ya watu wa jamii mbalimbali zihimizwe.
  • Tamasha za watu wa tamaduni mbalimbali ziandaliwe na kuhudhuriwa na watu wote.
   Tanbihi:  Mwalimu akadirie majibu ya mtahiniwa.
 2. Magonjwa mengi yanasababishwa na mitindo ya kisasa ya maisha. Jadili.
  • Mtahiniwa aandike insha ya hoja.
  • Lazima ataje hoja, kuifafanua na kuitolea mifano.
  • Sharti aunge mkono hoja aliyopewa.
  • Pia aonyeshe upande wa pili wa hoja aliyopewa. Akiangazia upande mmoja asipite alama 10/20 (C+)
  • Aeleze mitindo ya maisha ya kisasa.
  • Hoja zake ziwe tano au zaidi.
Kuunga Mkono
 1. Baadhi ya vyakulaa hasa vyenye mafuta, madini, sukari na chumvi husababisha magonjwa kama vile msukumo wa damu na kisukari.
 2. Kukosa mazoezi ya mwili kwa sababu ya matumizi ya magari ya usafiri nay a kibinafsi na watu hawatembei kwa mguu.
 3. Matumizi ya pombe huleta madhara mengi kwa mwili yanayosababisha magonjwa ya akili, ini na kansa.
 4. Mienendo mibaya hasa kushiriki mapenzi ovyo ovyo husababisha magonjwa ya ukimwi,kisonono na magonjwa mengine ya zinaa.
 5. Uchafuzi wa mazingira husababisha magonjwa kama vile ya pumu, malaria, kipindupindu n.k.
 6. Teknolojia kama vile uyoga husababisha ugonjwa wa kansa.
 7. Kujumuika ovyo bila kujali ukuruba hueneza magonjwa kama vile korona na homa.
            Tanbihi: Mwalimu akadirie hoja za mtahiniwa.
Hoja za Kupinga:
Magonjwa hayasababishwi tu na mitindo ya kisasa pekee;
 1. Baadhi ya magonjwa huritishwa katika familia.
 2. Kuna magonjwa yanayoletwa na wanyama na wadudu kama vile mbu konokono, nyani na kadhalika.
 3. Magonjwa kama vile mafua husababishwa na hali ya anga na si hali ya maisha
 4. Hali za kimaumbile kama vile mafuriko husababisha magonjwa kama vile kipindupindu.
3. Andika insha inyoafiki methali: Asiyejua faida ya mwangaza aingie gizani.
Mtahiniwa aelewe maana ya methali.
Kisa cha mtahiniwa kionyeshe mapuuza kuhusu jambo, kitu au mtu fulani. Baada ya mtu yule kuondoka, umuhimu wake uweze kutambulika.
 
Azingatie pande zote mbili za methali.
 
Hali mbalimbali zinaweza kudhihirika: kwa mfano;
 • Mwanafunzi apuuze mawaidha ya wakuu wake k.v walimu, wazazi, n.k. baadaye afeli mtihani na aishie kujuta.
 • Mkulima aliyeghairi kufuata uelekezi wa watabiri wa hali ya anga na wataalamu wa kilimo na baadaye akapata mazao duni.n.k. 
Tanbihi: Mtahiniwa LAZIMA aonyeshe mapuuza la sivyo asipate alama 08/20 C
 
4. Andika insha itakayomalizika kwa; ... nilipojitazama, nilijidharau kwa aibu niliyopata. Niliapa kutorudia kitendo hicho maishani mwangu.
 • Hii ni insha ya kumalizia.
 • Taharuki ijitokeze vilivyo.
 • Lazima mtahiniwa akamilishe kwa maneno haya.
 • Asipokamilisha kwa maneno haya, ataadhibiwa kimtindo.
 • Atumie nafsi ya kwanza.
 • Mwanafunzi abuni kisa kitakachodhihirisha hali ya kujuta sana kutokana na kitendo hicho. Asipofanya hivyo, atakuwa amepotoka kimaudhui.

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Arise and Shine Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?