Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - BSJE Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

LAZIMA

 1. Wewe ni Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Tia Fora. Wateja wa kampuni yako wamekuwa wakilalamikia huduma duni kutoka kwa kampuni yako. Imebainika kuwa wafanyakazi katika kampuni yako wanahusika katika hulka hizi duni. Andika arifa/memo ukiwaonya dhidi ya jambo hili.
 2. Jadili jinsi wanafunzi wanavyoweza kuimarisha matokeo katika masomo ya sayansi.
 3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali: Mchimba kisima huingia mwenyewe.
 4. Andika kisa kitakachoanza kwa maneno haya: Niliyafuta machozi. Uchungu uliokuwa moyoni uliyeyuka ghafla,tabasamu ikanivaa,nikawa tayari kukabiliana na hali yangu mpya liwe liwalo…..

                                                               MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. Insha hii ina sehemu mbili kuu
  1. Muundo
   Hii ni arifa
   Iwe na sehemu zifuatazo:
   • Neno Memo/Arifa
   • Jina la kampuni
   • Tarehe
   • Nambari ya rejea
   • Kutoka kwa
   • Kuelekea kwa
   • KUH:Mada
   • Mwili - mpangilio wa kiaya uzingatiwe katika kuelezea mada.
   • Kitambulishi - Sahihi
                        - Jina
                        - Cheo cha mwandishi
    Kwa mfano:
                                         MEMO                             
                            KAMPUNI YA TIA FORA
    Tarehe: 8/6/2023
    Nambari ya rejea: KYT/2/2023
    Kutoka kwa: Mkurugenzi mkuu
    Kwa: Wafanyakazi wote
    KUH: HUDUMA DUNI ZINAZOTOLEWA NA WAFANYAKAZI
    Kutokana na malalamishi ya wateja wetu kuwa kampuni inatoa huduma duni, uchunguzi wa ndani umefanywa ili kubaini chanzo cha malalamishi yao. Imebainika kuwa baadhi yenu mnahusika na jambo hili ambalo limetupunguzia wateja na kuanza kuteletea hasara.

    Kampuni haitakubali mwenendo huu kuendelea
    Asanteni
    Sahihi
    Sisitiza Mema,
    Mkurugenzi Mkuu.
  2. Maudhui
   Yalenge
   1. Kuelezea huduma hasi zinavyotekelezwa.
   2. Madhara ya huduma hizi kwa kampuni.
   3. Adhabu kwa wanaoendeleza huduma hizi.
    Mifano ya maudhui
    1. Kuchukua muda mrefu kabla ya kutoa huduma.
    2. Kuchukua muda mrefu katika kutoa huduma.
    3. Bidhaa kupakiwa vibaya.
    4. Bidhaa hazifiki viwango tarajiwa.
    5. Wateja kurundikana mahali pa mauzo.
    6. Hesabu zenye makosa (bidhaa au pesa).
    7. Hakuna mahali pa kungoja kabla ya kuhudumiwa.
    8. Wenye matatizo kama vile walemavu hawazingatiwi.
    9. Kelele za mashine mahali pa huduma.
    10. Sehemu za mauzo kufungwa ovyo ovyo hasa wakati wa chamcha.
    11. Lugha isiyofaa kwa wateja.
    12. Wateja kupuuzwa.
    13. Baadhi ya wateja kupendelewa.
    14. Kutoa maelezo yasiyo sahihi kuhusu matumizi ya bidhaa
    15. Kukosa utaratibu mwafaka wa kutoa huduma kwa mfano wanaokuja mwisho wanahudumiwa kwanza.
    16. Kukosa mwelekezi wa kuonyesha wateja mahali pa huduma.
    17. Vyumba vya kuenda haja ni vichafu /havipo.
    18. Vikwazo/itifaki zisizofaa au za kujitungia kabla ya kuruhusiwa kuingia au kuondoka kwenye kampuni.
    19. Kuagiza bidhaa fulani lakini kuishia kupewa bidhaa tofauti.
    20. Malalamishi yao kupuuzwa.
    21. Mahitaji yao hayarekodiwi hivyo inabidi mtu ajirudierudie katika kila ofisi.
    22. Kukosa kutoa mwelekeo wa hatua za kufuata aidha kwa mabango au maandishi ya aina yoyote.
 2.  
  1. Kushiriki kikamilifu darasani.
  2. Kuunda vikundi vya mjadala.
  3. Kufanya utafiti.
  4. Kusoma kwa undani/mapana na marefu.
  5. Kujibu maswali baada ya kila mada.
  6. Kujibu maswali ya mitihani mbalimbali.
  7. Kujiunga na masomo ya mtandaoni.
  8. Kufanya majaribio ya sayansi mara kwa mara.
  9. Kuandaa makongamano ya ndani kwa ndani.
  10. Kuandaa makongamano na shule zingine.
  11. Kuandaa mashindano ya ndani kwa ndani.
  12. Kuandaa mashindano na shule zingine.
  13. Kuwa na siku ya sayansi ambayo itatumiwa kujadili maswali na mada tata.
  14. Kutenga vipindi vya ziada vya kujadili maswali na mada tata.
  15. Kuwa na viranja wa sayansi ambao watahakikisha kuwa mambo haya yanatekelezwa.
  16. Kufanya mazoezi ya mara kwa mara.
  17. Kuwa na ukuta wa sayansi katika jengo/majengo ambapo magwiji wa sayansi watatunga maswali na kuwapa nafasi wenzao kuyajibu.
  18. Kupata ushauri wa walimu.
  19. Kujenga mwelekeo chanya kuhusu masomo ya sayansi.
 3.  
  • Anayemtafutia mwenzako maafa au kumtakia mabaya, hayo maafa au mabaya humfikia yeye au watu wake.
  • Kuna pande mbili: Kuchimba kisima-kumtafutia mwenzake mabaya
                               : Kuingia mwenyewe-madhara kumpata
  • Mifano:
   1. Mwanafunzi anayepanga kuwachoma wenzake shuleni, mwishowe vitu vyake vichomeke, afukuzwe shule au rafiki/ndugu yake achomeke.
   2. Mtu anayepanga kumsumisha mwenzake kwa chakula, badala ya huyo mwenzake kula chakula hicho, ale yeye au rifikiye na jamaa wake wa karibu kisha afe au adhurike vibaya.
   3. Anayepangia mwenzake wakora wamdhuru badala yake wamdhuru yeye au jamaa wake.
   4. Anayempangia mwenzake njama ya kufutwa kazi badala yake yeye apatikane na makosa afutwe.
   5. Anayetoa habari za uongo kuhusu mwenzake ili mwenzake afutwe kazi/afukuzwe shule/apoteze nafasi muhimu katika jamii badala yake apoteze yeye.
    TANBIHI: Anayezungumzia upande mmoja asipite kiwango cha C+
 4.  
  • Msimulizi anafaa asimulie hali mpya aliyoingia baada ya kutoka kwa hali nyingine.
  • Hali mpya iwe inahitaji kujitolea ( ndiposa neno kukabiliana).
  • Kuna matumaini ya hali nzuri au kuna hali nzuri (tabasamu na uchungu kuyeyuka.)
  • Hali ya awali haikuwa nzuri.
  • Masimulizi yanayoashiria yafuatayo yaweza kujitokeza.
   1. Msimulizi anaweza kuendeleza kisa kwa kusimulia alivyokabiliana na hali mpya na katika masimulizi aonyeshe hali ya zamani.
   2. Msimulizi anaweza kutumia mbinu rejeshi kuonyesha hali ya awali kisha asimulie jinsi alivyokabiliana na hali mpya.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - BSJE Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?