Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Momaliche Post Mock 2020 Exam

Share via Whatsapp

MAAGIZO

 • Andika insha mbili: insha ya kwanza ni ya lazima
 • Chagua insha moja nyingine kutoka kwa hizo tatu zilizobakia.
 • Kila insha isipungue maneno 400.
 • Kila insha ina alama 20.
 • Zingatia sarufi.
 • Onyesha nambari ya insha unayoandika.
 1. Andika tahariri kuhusu sababu za kudorora kwa usalama katika gatuzi lako.
 2. Fafanua hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa nchini kukabiliana na umaskini nchini.
 3. Andika insha inayooana na methali mchuma janga hula na wa kwao.
 4. Andika insha itakayomalizia kwa maneno yafuatayo.
  ...niliyagugumia maji hayo kwa pupa na kung’amua kuwa maji ni uhai.


MARKING SCHEME

 1. Kichwa
  jina la gazeti
  Siku na tarehe
  Mada
  Utangulizi – aya ya kwanza itoe maelezo ya jumla kuhusu suala la kudorora kwa usalama
  Maudhui
  1. Kuwepo kwa makundi haramu/makundi ya kigaidi
  2. Uhaba wa kazi kwa vijana
  3. Watu kumiliki silaha kinyume na sheria
  4. Uchochezi wa wanasiasa/siasa za migawanyiko
  5. Ukabila
  6. Wizi wa mifugo baina ya jamii mbalimbali
  7. Kuzembea kwa vyombo vya usalama
  8. Uhusiano mbaya kati ya polisi na raia
  9. Athari hasi za dawa za kulevya/vileo
  10. Giza/kukosekana kwa taa za usalama mijini
  11. Idadi ndogo ya polilsi/walinda usalama
  12. Kisasi cha ukatili wa kitambo
  13. Kutoaminiana kwa wanandoa
  14. Kudorora kwa usalama mipakani
  15. Ushindani wa kupata mamlaka
  16. Misongamano ya watu mijini
   Aya ya mwisho iwe ya hitimisho. Mtahiniwa atoe kauli yake ya mwisho labda kwa kufupisha maelezo yake ya hapo juu.
   • Jina la mwandishi
   • Cheo chake
 2. Kichwa
  Hoja/maudhui
  • Kuhimiza upangaji uzazi
  • Kuwapa watu ajira
  • Kufanya biashara
  • Kuwa na maendeleo endelevu nchini
  • Kudhibiti ufisadi
  • Kupunguza mikopo/ukopaji kutoka ughaibuni
  • Kuboresha usalama katika kila janibu ya nchi
  • Kufanya maendeleo mashambani
  • Kuboresha kilimo ili kuwa na utoshelezaji wa chakula
  • Kuhimiza uwekezaji utaohakikisha maendeleo na nafasi za kazi
  • Kuwapa watu mishahara inayolingana na gharama za maisha
  • Kuweka mtalaa wa elimu unaoona na mahitaji/gharama ya maisha.
 3. Mchuma janga hula na wa kwao
  Hii ni insha ya methali
  Chuma ni kufanya kazi na kupata faida/ tungua matunda kutoka mtini.
  Janga-balaa /baa /mataka / shida / hatari / taabu
  Ajitafutiaye shida huathirika na jamii / jamaa yake .
  Mtahiniwa asimulie kisa /visa vitakavyoafikiana na methali.
  Asipinge methali.
  Ruwaza zifuatazo zinaweza kujitokeza;
  • Mhusika kushiriki raha za kilimwengu, akaambukizwa magonjwa yasotibika,hatimaye anarejea nyumbani anakogua , mzigo wa kumtunza unakuwa kwa familia yake.
  • Mhusika aliyekuwa akifanya kazi katika kampuni au shirika fulani, anacheketwa labda kutokana na uzembe au utovu wa maadili ya kikazi,anarejea nyumbani kwa familia yake; kule hana chochote hivyo basi anaishia kutegemea jamma zake, huu unakuwa mzigo mkubwa kwa watu wake.
  • Mtoto ambaye anatokea kuwa mhalifu, anafikishwa kortini na kutozwa faini kubwa.Hii inakuwa gharama kwa familia yake kwa vile ndio wanaotakiwa kulipia.
  • Mwanafunzi ambaye anakosa kuwajibika masomoni shuleni , anafeli mtihani, maisha ya halafu yanakuwa magumu kwa hivyo jamaa zake wanalazimika kuingilia kati ili kumuauni kwa mahitaji ya kila siku
 4.  
  • Mtahiniwa aandike kisa kinachoonyesha mtu ambaye anateseka sana labda kutokana na kutekwa nyara.
  • Mtu huyu asawiriwe kama ambaye alikuwa karibu kufa/kukata tamaa na baadaye kwa bahati nzuri anapata maji.
   (Alama zituzwe kutokana na mwongozo wa kudumu wa kusahihisha insha kama inavyopendekezwa na Baraza la Mitihani ya Kitaifa Nchini (KNEC) )
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Momaliche Post Mock 2020 Exam.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest