Kiswahili Questions - Alliance Boys High School Post Mock KCSE 2020

Share via Whatsapp

MAAGIZO
JIBU MASWALI YOTE KATIKA KILA SEHEMU

Swali/Sehemu Alama Alama za Mwanafunzi 
Insha   20  
Ufahamu  15  
Matumizi ya Lugha  20  
Ufupisho  10  
Isimu Jamii  10  
Fasihi Simulizi  10  
Ushairi  15  
JUMLA 100  

INSHA
Wewe ni mwenyekiti wa Kamati ya Dharura ya kushughulikia janga la Korona. Mwandikie barua mhariri wa Gazeti la Pilipili ukieleza athari ya janga hili kwa jamii nzima. (Alama 20)

UFAHAMU
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
(Alama 15)
Siku moja nilifika kumwona babu yangu kule kwetu kijijini bila kumtolea taarifa mbele. Nilipofika nilimkuta amevaa magwanda yake yaliyokula chumvi hadi yakakinai. Alinitazama huku akitabasamu akisema, "Tabia hii ya kuja kwako bila taarifa utaikoma. Ukiendelea hivi utakuja kwenda kwa wakwe wako upate ndio wanakwenda uchi"
Kauli hii ya babu ilinifanya kucheka. Tulisalimiana huku tunapigana pambaja. Harufu ya manukato niliyojirashia asubuhi hiyo ilikutana na kuchanganyika na harufu ya jasho lake. Baadaye tuliingia ndani, tukaketi kwenye makochi yaliyokuwa yameanza kuonyesha dalili za kuchoka, Baada ya kuulizana habari za kimsingi nilitaka kujua alipokuwa nyanya.
"Nyanyako ameenda kumwona jirani yetu mgonjwa. Amepata ajali akitoka mjini alikokuwa ameenda kuwatembelea wajukuu wake. Raha yote ya kuwaona iligeuka karaha." Alinyamaza kidogo, akaguna, kisha akaendelea, "Barabara hizi,sijui mwaziita "haibei', zimewala watu wetu. Huwezi kuwahesabia vidole tena."
Kwa muda nilikosa la kusema. Niliona niubadili mkondo wa mazungumzo. Nilianza kwa kumweleza kuwa mazingira ya kijijini yalipendeza. Kwa kweli mandhari yale ya kijani kote hadi upeo wa macho yalinisisimua sana. Sauti za ndege zilikuwa mfano wa muziki wa chini uliochezwa ili kuyapamba mazungumzo yetu. Mara mojamoja nilitekwa na sarakasi ya jogoo aliyetanua mabawa yake na kukaribia kuzungumza, utadhani ni sauti ya mwanadamu. Nilipokuwa ninamtazama yule jogoo, nilishtukia mkono wa babu ukiushika wangu, akaniongoza nje akisema, "Haina haja kuyamezameza mate. Huyu jogoo ni wako. Leo tutamfanya kitoweokwa ajili yako, Najua kule mjini mnakula kuku wa miigizo tu. Faida yao kwa mwili ni duni."
Tulishirikiana kumkamata yule jogoo lakini baada ya muda nilicho ka. Moyo wangu ulikuwa unapiga kwa nguvu ajabu. Niliona kisunzi, nikakaa. Nikiwa ninajipumzisha chini ya kivuli cha mpera nilisikia sauti za watoto waliokuwa wamejiunga na babu kumkamata yule jogoo.
Tukiwa tunasubiri chakula cha mchana, niliona hii kuwa fursa mufti kumweleza babu kwamba nilifika kusudi niende naye mjini. Nilipo litamka tu hili alicheka sana. Aliniambia, "Mji ni wenu nyinyi. Sisi watu wa shamba raha yetu ni kufukuzana na kazi hizi za sulubu. Kwendakukaa mjini na nguvu zote hizi faida yake nini? Nasikia siku hizi huko mjini kuna misongamano ya magari isiyoisha. Kuna haja gani kwenda kushinda kwenye gari kuharibu muda wako kwa sababu ya msongamano? Mimi hapa kwangu nikitaka kwenda kuzitekeleza shughuli zangu sipati kizuizi. Ninakwenda tu."
"Sikiliza babu," nilimwambia, "mji una raha yake. Wingi wa magari ni ishara ya maendeleo. Uwezo wa kifedha wa watu uko juu kuliko wa hapa kijijini. Leo hii mtu akipatwa na dharura ya ugonjwa hapa, kijiji kitafanya takilifu kumfikisha hospitalini. Mjini usafiri upo kila
mahali wakati wowote."
"Kule mjini mnadai kuona mwanga na kuujua ustaarabu ila mmenoa," alisema babu, "maisha yenu, afadhali ndege warukao angani. Ni kama mnachupa kutoka upande mmoja hadi mwingine, kana kwamba mnaendeshwa kwa nguvu za mtambo usioonekana. Jamaa hawajuani tena. Mizizi yenu hamuitambui. Mmekuwa mithili ya miti inayopendeza lakini isiyo na mizizi ya kutosha. Upepo hafifu uvumapo inalemewa na kujibwaga chini. Je, huo ndio ustaarabu?
Ustaarabu kwetu sisi watu wa hapa kijijini ni mtu kuwaamkua wenzake kila kukicha. Ni kujuliana hali. Ni kuombana kibaba cha unga au kibakuli cha mboga. Tunaishi tukijuana, si majina na sura tu, bali pia hata upishi wetu. Nyinyi mnaishi pasi na kujua majirani wenu. Je, wgwe hukuona hata kuku wangu hawa wanatangamana?"
Swali hili lilipoachiliwa nilihisi kama aliyetwikwa nanga. Kijasho chembamba kilinitoka. Kwa bahati nzuri meza ilikuwa imeisha kuandaliwa; kipindi cha kupambana mezani kikawadia.
Nilipokuwa nikila nilitambua kitu kimoja; yule kuku alikuwa na ladha ya kupendeza, tofauti na tuliozoea kuwala kule mjini. Ila nililoliona tu ni kuwa alikuwa mgumu kidogo. Nilipokuwa nikilifikiria hili niliisikia sauti ya babu tena.
"Chunga asikung'oe meno. Huyu ni kuku hasa. Atakusaidia kuimarisha meno. Hutakuwa na haja ya kwenda kumwona daktari wa meno. Sisi hapa hata kushiriki chakula kunatukumbusha kuwa kila shughuli ni kazi tosha. Hatuna muda wa kulaza damu." Alichukua bilauri ya maji, akapiga tama, kisha akaendelea kuinyofoa sima yake ya bada.

Maswali

 1. Huku ukirejelea kifungu, fafanua faida sita utakazopata ukiishi shambani. (Alama 6)
 2. Eleza mtazamo wa wahusika wafuatao kuhusu mji: (Alama 3)
  Msimulizi
  .........................
  Babu
  ..............(Alama 4)
 3. Andika maana ya fungu lifuatalo la maneno kwa mujibu wa taarifa (Alama 1)
  kwenda kwa wakwe wako upate ndio wanakwenda uchi.
  ..........................
 4. Andika kisawe cha: (Alama 1)
  Niliona kisunzi
  ................................

MATUMIZI YA LUGHA (Alama 20) 

 1. Taja sauti moja ambayo ni: (Alama 1)
  Kituo ghuna cha midomo.
  ....................
  King'ong'o cha kaakaa gumu.
  ...................
 2. Ainisha viambishi katika kitenzi. (Alama 1)
  Waliowaandalia
  .........................
 3. Changanua sentensi ifuatayo ukitumia mchoro wa matawi (Alama 2 )
  Mdarisi aliyewafundisha insha tano amepewa tuzo bora.
  ........................
 4. Tambua aina za shamirisho katika sentensi hii. (Alama 1 )
  Busara alimbebea mzazi wake mzigo kwa gari.
  ........................
 5. Unda nomino moja inayorejelea kitendo kutokana na kitenzi. (Alama 1)
  Cheza
  ..........................
 6. Andika kwa usemi wa taarifa (Alama 1)
  "Mbona ulimfanyia mzazi ujeuri? Jo, utaenda kumwomba radhi?" Nasaha alimwuliza Katili.
  ........................
 7. Eleza matumizi ya 'na' katika sentensi hii. (Alama 1)
  Mwanafunzi anayesoma vizuri alielekezwa na mwalimu wake.
  ........................................
 8. Andika wingi wa ukubwa wa sentensi hii. (Alama 1)
  Mbuzi alipigwa kwa jiti akatoroka.
  .........................
 9. Andika sentensi mojamoja kuonyesha matumizi ya: (Alama 1)
  Kinyota
  .................
  Kibainishi
  .................
 10. Nomino'mijusi' iko katika ngeli gani?
  .............. (Alama ½)
 11. Yakinisha sentensi hii. (Alama 1)
  Sitaandika insha murwa na mufti leo.
  ........................................
 12. Onyesha vishazi katika sentensi hii. (Alama 1)
  Mwanafunzi hodari aliyepita mtihani amesifiwa.
  ........................................
 13. Tambua kijalizo katika sentensi hii. (Alama 1)
  Mgeni aliyefika jana jioni ni mtaalam.
  ........................................
 14. Onyesha virai katika sentensi hii huku ukieleza ni vya aina gani (Alama 1)
  Maria anapenda kusoma vitabu vyenye mvuto halisi.
  ........................................
 15. kwa kutolea mfano faafu tofautisha kati ya kiima na kiarifa (Alama 2)
  ........................................
 16. Andika sentensi hii upya ukitumia vinyume vya maneno yaliyopigiwa mstari (Alama 1)
  Kazana amefaulu kuhifadhi pesa zake, kwa hivyo ametajirika.
  ........................................
 17. Andika sentensi hii katika hali isiyodhihirika. (Alama ½)
  Alianguka akicheza
  ........................................
 18. Tunga sentensi ya neno moja yenye visehemu hivi vya sarufi. (Alama 1)
  Kiambishi kiwakilishi cha kiima.
  Kiambishi kiwakilishi cha wakati ujao Kiambishi kiwakilishi cha mtendewa.
  Mzizi.
  Kiambishi cha kauli ya kutendesha
  Kiishio
  ................................................................................
  ................................................................................

UFUPISHO
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Wakenya walipoipitisha katiba mpya waliidhinisha mfumo wa ugatuzi. Katika mfumo huu, mamlaka ya serikali kuu katika uongozi, usimamizi na utumiaji wa rasilimali za nchi hupunguzwa. Kiasi fulani cha mamlaka hutwaliwa na maeneo ya ugatuzi. Suala hili halikuzingatiwa katika katiba ya awali ambapo mamlaka yote yalikuwa mikononi mwa serikali kuu. Kutokana na upana na wingi wa maeneo nchini, iliiwia vigumu serikali kuu kuhakikisha kwamba kulikuwa na usawa wa kimaendeleo katika sehemu zote nchini.
Kwa mujibu wa katiba mpya, serikali kuu haina budi kuyasaidia maeneo yote ya ugatuzi ili yaweze kujinyanyua kiuchumi na kuboresha hali za maisha za wakazi wake. Vilevile ni jukumu la kila eneo la ugatuzi kuweka mikakati madhubuti ili kuchunguza na kubainisha rasilimali zote katika maeneo husika. Hili litasaidia kuvumbua rasilimali ambazo zinaweza kuchangia katika ustawishaji wa maeneo haya. Maeneo haya pia yanatakiwa kutafuta mbinu zitakazofanikisha uzalishaji na utumiaji wa rasilimali hizi kwa njia endelevu. Mojawapo ya mbinu hizi ni uongezaji thamani katika rasilimali yoyote inayozalishwa kwenye eneo mahususi.
Maeneo mengi ya ugatuzi nchini humu yanategemea kilimo cha ufugaji kama mhimili wa uchumi. Licha ya kuwa nguzo, kilimo hiki hakijawahi kupigiwa darubini vizuri kwa lengo la kukiimarisha ili kiwanufaishe wenyeji kikamilifu. Aghalabu wafugaji wengi huandama mbinu za jadi za ufugaji ambazo haziwahakikishii ongezeko la mapato. Isitoshe, wafugaji hawa wanakabiliwa na tatizo katika soko la mifugo ambapo wengi hupunjwa na matapeli. Pamoja na haya, baadhi ya wakazi huuza mifugo nje ya nchi wakiwa wazimawazima bila kuwazia matokeo ya kitendo hiki.Si ajabu kuwaona ng'ombe, ngamia, mbuzi na kondoo wakipakiwa kwenye malori na kusafirishwa nje ya nchi. Ukweli ni kwamba jambo hili ni hatari sana, si kwa uchumi wa maeneo husika tu, bali pia kwa Kenya kwa jumla. Hii ni kwa kuwa walionunua mifugo wazimawazima wanaweza kuhiari kutowachinja na badala yake kuwatumia kama mbegu za kuzalisha mifugo wao. Hapa pana hatari ya maeneo haya kupoteza wateja kwani baada ya muda huenda wanaonunua mifugo wakajitosheleza na kukosa kuja kununua mifugo wengine. Hali ikiwa hivyo, maeneo yaliyotegemea soko hili huenda yakalipoteza taratibu, na bila shaka kupoteza natija inayotokanana soko lenyewe.
Ili kudhibiti hali hii, itakuwa bora ikiwa viwanda vya kuchinjia mifugo na kupakia nyama vitajengwa katika maeneo haya ya ugatuzi. Hili litawawezesha wakazi kuuza nyama badala ya kuuza mifugo wazimawazima. Fauka ya haya, maeneo haya yatajikinga dhidi ya kupoteza bidhaa zinazotokana na mifugo. Hizi ni kama vile ngozi, kwato na pembe ambazo bila shaka zina natija kuu. Ngozi kwa mfano, ni bidhaa muhimu sana katika sekta ya utengenezaji wa mavazi na mifuko. Viwanda vinavyotumia ngozi kama malighafi vikijengwa katika maeneo haya, wakazi wake watanufaika si haba. Mathalani, viwanda vya kutengenezea viatu, mishipi, mifuko na nguo vikianzishwa, wawekezaji watalazimika kuanzisha viwanda vingine vitegemezi. Kadhalika, ni dhahiri kwamba bidhaa zinazotokana na ngozi huhitaji kutiwa nakshi. Kuanzishwa kwa viwanda hivi basi kutazua haja ya kuanzishwa kwa viwanda vya kutengenezea rangi pamoja na maduka ya kuuza bidhaa yenyewe. Isitoshe, gundi ya kugandisha bidhaa hizi itahitajika, hivyo kusababishahaja ya kuanzishwa kwa kiwanda cha gundi. Matokeo ya shughuli hizi zote ni kuzalishwa kwa nafasi anuwai za kazi kwa wakazi. Hili litakuwa na matokeo zaidi chanya, hususan kwa vijana. Badala ya kushiriki ulevi na burudani zinazowahatarisha, wataweza kujitafutia riziki katika viwanda hivi.
Juu ya hayo, mfumo wa ugatuzi utayawezesha maeneo husika kuongezea thamani utoaji wa huduma za kijamii na kiutawala kulingana na mahitaji ya maeneo haya. Ni muhimu hata hivyokuzingatia kwamba kila eneo la ugatuzi lina upekee wake, navyo vipaumbele hutofautiana kulingana na maeneo. Kuna yale ambayo yatasisitiza usalama, mengine ujenzi na uimarishaji wa miundomsingi kama vile barabara, vituo vya afya na hata taasisi za elimu. La muhimu ni wakazi wa maeneo husika kubainisha ni lipi litatekelezwa kwanza.
Kinga na kinga ndipo moto uwakapo. Kufanikiwa kwa mfumo wa ugatuzi kutategemea juhudi za kila mkazi wa eneo husika. Ni muhimu kila mkazi kujiona kuwa mmiliki wa eneo zima la ugatuzi na kuwajibika katika kuliendeleza kwa hali na mali. Uwajibikaji huu unajumuisha uteuzi wa viongozi wenye muono mzuri na ambao watawawezesha kuyafikia malengo yao ya kimaendeleo. Hakika, mustakabali na uwepo wa eneo la ugatuzi utakuwa zao la maamuzi ya wanaenco. Vilevile ufanisi wa maeneo ya ugatuzi utakuwa msingi wa ufanisi wa taifa kwa jumla

 1. Fupisha ujumbe wa aya tatu za mwanzo kwa maneno 85-90. (Alama 5)
  Matayarisho:
  Jibu:
  ........................................
 2. Kwa kutumia maneno 75-80, bainisha masuala ambayo mwandishi anaibua katika aya tatu za mwisho. (Alama 5)
  Matayarisho:
  Jibu:
  ........................................

ISIMUJAMII
Fafanua maana ya istilahi zifuatazo. (Alama 10)
Viziada Lugha
........................................
Kaida za Lugha
........................................
Kubadili msimbo
........................................
Sifa bia za Lugha
........................................
Pijini
........................................
Lingua franka
........................................
Lahaja
........................................
Sajili
........................................
Maenezi ya Kiswahili
........................................
Wingi lugha
........................................

FASIHI SIMULIZI
Fafanua vipera vifuatavyo: (Alama 10)
Ngomezi
........................................
Mivigha
........................................
Maapizo
........................................
Matambiko
........................................
Ngano za mtanziko
........................................
Soga
........................................
Hodiya
........................................
Vivugo
........................................
Misimu
........................................
Vitanzandimi
........................................

USHAIRI
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali (Alama 10)
Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na kotama
Katika njia iendayo Kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani;
Nimuonapo huwa anatabasamu
Kama mtu aliye na hamu
Kushika mpini na kutokwa jasho
Ili kujikimu kupata malisho.
Anapotembea anasikiliza
Videge vya anga vinavyotumbuiza
Utadhani huwa vimemngojea
Kwa usiku kucha kuja kumwimbia
Pia pepo baridi kumpepea Rihi ya maua zikimtetea
Nao umande kumbusu miguuni;
Na miti yote hujipinda migogo
Kumpapasa, kumtoa matongo:
Na yeye kundelea kwa furaha
Kuliko yeyote ninayemjua
Akichekelea ha ha ha ha ha ha ...
Na mimi kubaki kujiuliza
Kuna siri gani inayomliwaza?
Au ni kujua au kutojua?
Furaha ya mtu ni furaha gani?
Katika dunia inayomhini?
Ukali wa jua wamnyima zao
Soko la dunia lamkaba koo;
Dini za kudhani zamsonga roho
Ayalimia matumbo ya waroho.
Kuna jambo gani linalomridhisha?
Kama si kujua ni kutojua
Laiti angalijua, laiti angalijua!

Maswali:

 1. Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili. (Alama 1)
 2. Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili (Alama 2)
 3. Fafanua aina tatu za taswira ukirejelea ubeti wa pili (Alama 3)
 4. Maswali ya balagha katika shairi hili yanasisitiza maudhui yapi? (Alama 2)
 5. Kwa kutoa mifano, bainisha vipengele vitatu vya kimtindo katika shairi hili (Alama 3)
 6. Eleza toni ya shairi hili (Alama 1)
 7. Bainisha nafsineni katika shairi hili (Alama 1)
 8. Eleza muundo wa shairi hili (Alama 2)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions - Alliance Boys High School Post Mock KCSE 2020.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest