Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Asumbi Girls Pre Mock Examinations 2023

Share via Whatsapp
  1. LAZIMA
    Kumekuwa na visa vingi vya dhuluma kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kutoka kwa wenzao. Wewe kama kiranja mkuu katika shule yako, mwandikie mwalimu mkuu barua ukimwelezea chanzo na kupendekeza hatua zinazofaa kuchukuliwa dhidi ya maovu haya.
  2. Wazazi ni wa kulaumiwa kwa kupotoka kwa maadili miongoni mwa kizazi kichanga.
    Jadili.
  3. Tunga kisa kinachodhihirisha maana ya methali ifuatayo:
    Mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani.
  4. Andika insha itakayomalizia maneno yafuatayo;
    ............ Baada ya tukio hilo, nilipiga dua kwa Mola ili kumpa shukrani kwa kuniepusha na janga hilo.


MARKINGS SCHEME 

SWALI LA LAZIMA

  1. Hii ni barua rasmi. Sura ya barua rasmi izingatiwe kikamilifu.
  2.  Itakuwa na anwani mbili:
    1. Anwani ya mwandishi
    2.  Anwani ya mwandikiwa
  3. Sehemu nyingine za barua rasmi ziwepo
    1. Mtajo
    2. Mada
    3. Mwili
    4. Sahihi ya mwandishi
  4. Mtahiniwa anaweza kutumia mtindo wowote (wima au mlazo) lakini asichanganye mitindo.
  5. Barua ishughulikie pande zote mbili za swali.
    1. Vyanzo vya dhuluma kwa wanafunzi
    2. Mapendekezo/hatua za kuchukuliwa
  6. Barua imlenge mwalimu mkuu wa shule yako.

Baadhi ya hoja za kuzingatiwa.

  1. Vyanzo vya dhuluma kwa wanafunzi.
    1. Mapendeleo kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza - mabweni, vyakula, mavazi.
    2. Wananfunzi wengine hutaka kulipiza kisasi kwa namna walivyodhulumiwa walipokuwa kidato cha kwanza.
    3. Wanafunzi wa kidato cha kwanza wanapokataa kushirikiana na watenda maovu, k.v. kutumia dawa za kulevya.
    4. Mchipuko wa uasi kutoka kwa wanakidato cha kwanza k.v kuwa na kiburi.
    5. Wanakidato cha kwanza kupewa hela nyingi za masurufu hali inayowafanya kuonewa ngoa.
    6. Usingiziaji/usaliti. Vidato vingine kuwalaumu kuwa ni wasaliti.

Hatua za kuchukuliwa/Mapendekezo

  1. Wanafunzi wote washauriwe kuhusu umuhimu wa utangamano.
  2. Wavunja sharia/kanuni za shule waadhibiwe bila mapendeleo.
  3. Usawa udumishwe katika viwango vyote shuleni.
  4. Kiwango cha hela za masurufu kidhibitiwe ili kusiwe na wanafunzi walio na pesa nyingi kuliko wengine.
  5. Wanafunzi wote washirikishwe katika michezo mbalimbali ili kudumisha utangamano.

Utuzaji

  1. Asiyezingatia sura ya barua rasmi aondolewe alama (45) za sura.
  2. Atakayeshughulikia upande mmoja tu wa swali asipite alama C+1
  3. Alama/mkwaju wa hoja za nyanzo uwe kamili (V). Ule wa mapendekezo uwe na kikia (√)
    Tanbihi: Urefu wa insha uzingatiwe vilivo.
    1. Insha robotatu-asipite alama 15
    2.  Insha nusu - asipite alama 10
    3. Insha robo- asipite alama 05.

Kiswahili Paper 2

UFAHAMU.

  1. Eleza sifa mbili mbili za wahusika wafuatao: (alama 4)
    1. Kasim
      • Mwenye matusi
      • Mwenye dharau
      • Mwenye majuto
    2. Bi Mwajuma
      • Mwenye heshima
      • Mwenye shukrani
      • Msema kweli (4x1 = 4)
  2. Fafanua maovu aliyotenda Kasim kulingana na kifungu. (alama 3)
    1. Alifanya mpango na wezi wengine ili kuvunja sefu na kumwibia Bwana Hakimu fedha zake.
    2. Alimkaba roho Bwana Hakimu alipokuwa akisali.
    3. Alimtusi Bwana Musa
    4. Aliwadharau wengine kwa kuwaita ghabeni. (3x1 = 3)
  3. Eleza sababu za Kasim kughairi nia yake. (alama 2)
    1. Aligundua kuwa Bwana Hakimu hakuwa babake wa kweli.
    2. Hakuona haja ya kudai urithi usiokuwa wake. (2x1 = 2)
  4. Andika methali moja inayofupisha masimulizi haya.
    • Fadhila za Punda ni mateke.(alama 1) (1x1 = 1)
  5. Eleza uhusiano uliopo kati ya Kasim na Bw. Hakimu.
    • Kasim ni mtoto wa kupanga wa Bwana Hakimu. (1x2 = 2) (alama 2)
  6. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika kwenye kifungu; (alama 3)
    1. Wamemshabihi - Wamemfanana (1x1 = 1)
    2. Dunia inapomkunjia uso - Watu wanapomshangaa (1x1 = 1)
    3. Kutiwa ufunguo wa kufanya hivyo - Kuambiwa aanze/kupewa idhini (1x1 =1)
      Sarufi - Alama nusu iondolewe kwa kila kosa la sarufi.
      Hijai - Alama nuşu iondolewe kwa kila kosa la hijai.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Asumbi Girls Pre Mock Examinations 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?