Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End Term 2 Exams 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

UFAHAMU: (ALAMA 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali:
Takwimu zilizothibitishwa zaonyesha kuwa kila sekunde nane mtu mmoja hufa duniani kutokana na utumiaji wa tumbako. Kwa siku basi, watu 10,800 hufa. Wengi wa wavuta sigara huanza katika umri kati ya miaka kumi na mitatu hadi kumi na tisa. Takwimu zaonyesha kuwa mtu akivuta sigara kwa zaidi ya miaka ishirini huupunguza umri wake kwa kati ya miaka 20 hadi 25 zaidi ya ambaye hajawahi kuvuta. Hii ni kwa kuwa tumbako ina zaidi ya kemikali 4,000 zinazodhuru afya.
Mojawapo ya madhara makuu zaidi yanayosababishwa na sigara ni saratani. Kunayo saratani ya ngozi – vidonda visivyopona huchubuka ngozini na baada ya muda hugeuka na kuwa kansa. Iri ya mapafu hutokea vifuko vya hewa vinapopasuka na hivyo kutatiza uvutaji wa oksijeni na utoaji wa kabondayoksaidi. Moshi pia husababisha madhara kwa njia ya kupitisha hewa, yaani umio, ambapo njia hii yaweza hata kuzibika hivyo kulazimu tundu kutobolewa kooni ili mgonjwa aweze kupumua. Kabla ya kufika kooni na mapafuni, moshi hupitia mdomoni. Saratani ya mdomo na ulimi basi hupatikana zaidi miongoni mwa wavuta sigara. Pia kidonda chochote, kwa mfano baada ya kung’olewa jino, huwa vigumu kupona kwa mvutaji sigara.
Kwa wanawake, kuna hatari ya kupatwa na iri ya fuko la uzazi. Madhara kwenye njia nzima ya uzazi huifanya iwe vigumu kwa wanawake wavuta sigara kuhimili. Ni rahisi pia kuzaa njiti. Mtoto wa mvutaji huzaliwa akiwa mwepesi zaidi ya kawaida. Hii husababishwa na kabonimonoksaidi kutoka kwa sigara inayomdhuru mtoto tumboni. Saratani hii husababisha hata kifo cha mtoto aliye tumboni. Wengine wazaliwapo huwa na hatari ya kupatwa na saratani zaidi ya waliozaliwa na akina mama wasiovuta sigara.
Aina zaidi za saratani zinazowakumba wavuta sigara ni kama vile saratani ya pua, ya tumbo, ya figo, ya kibofu cha mkojo, ya kongosho, ya njia ya kinyesi na hata saratani ya matiti inayowaathiri zaidi wanawake.
Shida za sigara sio saratani pekee; sigara husababisha shida za macho na masikio kwa kiasi kikubwa. Mboni ya jicho yaweza kufunikwa na utando, hali inayoweza kusababisha hata upofu. Macho yaweza kuwashwa na moshi mkali wa sigara au mishipa ya macho iathirike na kemikali zinazofika kwayo kupitia kwa mishipa mapafu yanapoathirika. Masikio nayo huathiriwa na uchafu wa tumbako unaoganda kwenye mishipa hadi sehemu za ndani za masikio. Damu hupunguza mwendo ufaao masikioni hivyo yanaugua. Moshi na kemikali za tumbako pia hujeruhi sehemu za ndani na athari hii yaweza kuenea hadi ubongoni na kusababisha utando unaofunika ubongo. Hali hizi zaweza kusababisha uziwi.
Mifupa na meno huathirika pia. Mifupa huwa myepesi, hukosa nguvu na kuwa rahisi kuvunjika. Mvuta sigara akivunjika mfupa huchukua muda wa asilimia themanini (80%) kupona zaidi ya mtu asiyevuta. Meno nayo hutatizika katika ukuaji wake kutokana na kugandwa na moshi wenye kemikali. Hali hii husababisha harufu mbaya, uchafu pamoja na kuoza kwa meno.
Ngozi ya mvuta sigara hukaushwa na kemikali kwa sahabu uwezo wake wa kujirekebisha na kujilainisha hupunguzwa pakubwa. Hali hii husababisha ukavu unaoonekana pamoja na makunyanzi yanayomfanya mvuta sigara aonekane mzee zaidi ya umri wake. Vidole navyo vilevile hugandwa na kutu ya sigara, nazo kucha na vidole hugeuka rangi vikawa vya manjano, hudhurungi au maji ya kunde. Vidole pia hukaushwa na moto na kemikali ya sigara. Nywele za mvuta sigara pia huathirika kwa kuwa kemikali huipunguza kinga ya mwili hivyo mizizi ya nywele kukosa nguvu. Nywele za mvuta sigara zaweza kung’oka mapema.
Sigara husababisha magonjwa ya moyo na vidonda vya tumbo. Kwa moyo, sigara husababisha shinikizo la damu na hatimaye mshtuko wa moyo waweza kutokea na kusababisha hata kifo. Kwa tumbo, sigara hupunguza uwezo wa kinga zake wa kuikinga dhidi ya asidi zinazosaga chakula. Pia hupunguza uwezo wa mwili wa kujikinga dhidi ya vidonda vya tumboni. Vidonda vya tumbo vya mvuta sigara huwa vigumu kupona na, ni rahisi kutokea tena baada ya kupona.
Kwa mwanamume, mpigo wa damu kwenye sehemu za uzazi huathiriwa. Hali hii ikizidi husababisha hata upungufu wa nguvu ya mbegu kwenye shahawa. Hata ugumba waweza kutokea. Pia watoto wa mwanamke mvuta sigara waweza kuzaliwa wakiwa na kasoro. Mimba zingine zilizotungwa na wanawake wavuta sigara pia hutunguka. Na si hayo tu; madhara ya sigara ni mengi zaidi.
Maswali

  1. Yape makala haya kichwa. (alama 2)
  2. Mbali na athari kwa uzazi kwa wanawake na wanaume na sura/umbo la binadamu, taja madhara mengine ya uvutaji sigara kwa binadamu. (alama3)
  3. Kwa kurejelea kifungu onyesha kwamba sigara kwa wanawake hasa ni hatari mno.
    (alama 4)
  4. Je, ni kweli kuwa vifo vingi hutokea kwa sababu ya uvutaji sigara? Toa sababu. (alama 2)
  5. Eleza namna ambavyo uvutaji sigara huathiri sura ya mhusika. (alama 3)
  6. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa kwenye taarifa. (alama 1)
    Gandwa _______________________________________________________________________

MATUMIZI YA LUGHA. AL 35

  1. Eleza maana ya ishali zifuatazo. (al 2)
    1. Mofimu
    2. Viambishi
  2. Andika kwa wingi sentensi hii; (al 1)
    1. Goti la mtoto liliumia –––––––––––––––––––––––––––--–––––––––––––––––––
  3. Bainisha nomino hizi ni za aina gani. (al 1)
    1. Mzee
    2. Oduori
  4. Tumia vivumishi vya sifa katika mabano kukamilisha sentensi zifuatazo. (al 2)
    1. Mtoto yule ni –––––––––––––––––––––– (nene)
    2. Kiberiti si kifaa ––––––––––––––––––––– kubeba. (zito)
  5. Kamilisha sentensi zifuatazo kwa kuchaza viambishi vya upatanisho vya ––ingine. (al 2)
    1. Mahali ––––––––––––––––––––––––––kulikobaki ni kwao.
    2. Mwizi huyo –––––––––––––––––––––––––hakupigwa risasi.
  6. Ziandike upya sentensi zifuatazo ukitumia ‘O’rejeshi. (al 2)
    1. Meno ambayo yanamuuma yatatiwa dawa.
    2. Kioo ambacho kilinunuliwa ni kipya.
  7. Tambulisha vitenzi visaidizi katika sentensi hizi. (al 2)
    1. Hajaenda kusoma
    2. Niliwahi kumweleza.
  8. Sahihisha sentensi zifuatazo kimapokeo. (al 2)
    1. Zizi tuna sisi la ng’ombe kwetu.
    2. Kiza cha abunuwasi kwenye kisa kinazikitisha.
  9. Andika sentensi zifuatazo kwa wingi. (al 2)
    1. Nitaenda alasiri kumwangalia alikoenda.
    2. Atamwinda mnyama huyo kisirisiri.
  10. Tumia kihusishi kifaacho katika sentensi zifuatazo. (al 3)
    1. Amechuma matunda –––––––––––––rafiki yake
    2. Walikimbia ––––––––––––––swara.
    3. Tutafanya kazi ––––––––––wenzetu.
  11. Tunga sentensi ukitumia vihisishi ukionyesha hisia zifuatazo. (al 2)
    1. Furaha.
    2. Dharau.
  12. Andika kinyume cha vitenzi vifuatavyo. (al 2)
    1. Tandika
    2. Unga
  13. Kamilisha methali zifuatazo. (al 2)
    1. Kawia–––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––
    2. Chovya chovya ––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––
    3. Isipowasha––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––
    4. Cha kuzama–––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––––
  14. Kanusha sentensi zifuatazo. (al 2)
    1. Nilimwona akicheza
    2. Ningalienda kwake ningalimpata.
  15. Tambua kikundi Nomino na kikundi Tenzi katika sentensi zifuatazo. (al 2)
    1. Mwanafunzi amevaa sare safi mno
    2. Sakafu ile inateleza sana
  16. Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa. (al 2)
    "Njoo hapa” Asksri alimwita Juma.
  17. Unda nomino mbili kutokana na kitenzi safari. (al 2)
  18. Andika kitenzi kifuatacho katika kauli ya kutendeswa. (al 1)
    Panga

FASIHI SIMULIZI AL 10

  1.                          
    1. Eleza maana ya methali (al 2)
    2. Fafanua sifa nne za methali (al 8) 

ISIMU JAMII AL 10

  1.                            
    1. Eleza maana ya sajili ya bungeni. (al 2)
    2. Taja sifa nane za sajili ya bungeni. (al 8)

MWONGOZO

UFAHAMU

  1. Uvutaji sigara/tumbaku.
    Madhara ya uvutaji sigara/tumbaku 1x2=2
  2.                  
    1. Husababisha saratani
    2. Husababisha shida za macho na masikio.
    3. Huathiri mifupa na meno.
    4. Husababisha magonjwa ya moyo na vidonda vya tumbo. 3 x 1
  3.                        
    • Madhara kwa njia ya uzazi huifanya iwe vigumu kuhimili.
    • Ni rahisi kwao kuzaa njiti.
    • Huzaa watoto wepesi
    • Huweza kusababisha kifo cha mtoto aliye tumboni.
    • Mtoto huweza kuzaliwa akiwa na kasoro.
    • Mimba huweza kutunguka. 4 x 1
  4. Ndio: Kwa kila sekunde nane mtu mmoja hufa duniani kwa sababu ya kutumia tumbaku/kwa siku watu 10,800 hufa. 1 x 2
  5.                            
    • Ngozi ya mvutaji hukauka/fanya mtu kuonekana mzee.
    • Vidole hugandwa na kutu ya sigara.
    • Kucha za vidole hugeuka rangi vikawa vya manjano/hudhurungi.
    • Nywele hukosa nguvu
    • Nywele hung’oka mapema. Zozote 3 x 1
  6. Kwamiliwa/kataliwa.

MATUMIZI YA LUGHA. AL 35

  1. Eleza maana ya ishali zifuatazo. (al 2)
    1. Mofimu
      • Mofimu ni ile sehemu ndogo sana ya neon inayowasilisha maana
    2. Viambishi
      • Kiambishi ni mofimu inayowekwa kwenye shina la neno ili kuwasilisha maana tofauti za kisarufi.
  2. Andika kwa wingi sentensi hii; (al 1)
    1. Goti la mtoto liliumia - Goti la mtoto liliumia
  3. Bainisha nomino hizi ni za aina gani. (al 1)
    1. Mzee – Nomino ya kawaida
    2. Oduori – Nomino ya pekee
  4. Tumia vivumishi vya sifa katika mabano kukamilisha sentensi zifuatazo. (al 2)
    1. Mtoto yule ni - Mnene (nene)
    2. Kiberiti si kifaa - Kizito kubeba. (zito)
  5. Kamilisha sentensi zifuatazo kwa kuchaza viambishi vya upatanisho vya ––ingine. (al 2)
    1. Mahali - Kwingine kulikobaki ni kwao.
    2. Mwizi huyo – Mwingine hakupigwa risasi.
  6. Ziandike upya sentensi zifuatazo ukitumia ‘O’rejeshi. (al 2)
    1. Meno ambayo yanamuuma yatatiwa dawa.
      • Meno yamuumayo yatatiwa dawa
    2. Kioo ambacho kilinunuliwa ni kipya.
      • Kioo kinunuliwacho ni kipya
  7. Tambulisha vitenzi visaidizi katika sentensi hizi. (al 2)
    1. Hajaenda kusoma
      • Hajaenda
    2. Niliwahi kumweleza.
      • Niliwahi
  8. Sahihisha sentensi zifuatazo kimapokeo. (al 2)
    1. Zizi tuna sisi la ng’ombe kwetu.
      • Sisi tuna zizi la ng’ombe kwetu
    2. Kiza cha abunuwasi kwenye kisa kinazikitisha.
      • Kisa cha abunuwasi kwenye kiza kinazikitisha.
  9. Andika sentensi zifuatazo kwa wingi. (al 2)
    1. Nitaenda alasiri kumwangalia alikoenda.
      • Tutaenda alasiri kuwaangalia walikoenda
    2. Atamwinda mnyama huyo kisirisiri.
      • Watawawinda wanyama hao kisirisiri
  10. Tumia kihusishi kifaacho katika sentensi zifuatazo. (al 3)
    1. Amechuma matunda Zaidi ya rafiki yake
    2. Walikimbia Mithili ya swara.
    3. Tutafanya kazi sawasawa na / pamoja na wenzetu.
  11. Tunga sentensi ukitumia vihisishi ukionyesha hisia zifuatazo. (al 2)
    1. Furaha.
      • Alhamdulilahi! Sikutarajia mwanangu angefanikiwa kesi ile haraka hivi.
    2. Dharau.
      • Ebo! Msinizungushe mambo hapa, niambieni mliloniitia haraka.
  12. Andika kinyume cha vitenzi vifuatavyo. (al 2)
    1. Tandika - Tandua
    2. Unga - Kata
  13. Kamilisha methali zifuatazo. (al 2)
    1. Chovya chovya humaliza buyu la asali
    2. Isipowasha hunyesha
    3. Cha kuzama hakina rubani
  14. Kanusha sentensi zifuatazo. (al 2)
    1. Nilimwona akicheza
      • Sikumwona akicheza
    2. Ningalienda kwake ningalimpata.
      • Nisingalienda kwake nisingalimpata
  15. Tambua kikundi Nomino na kikundi Tenzi katika sentensi zifuatazo. (al 2)
    1. Mwanafunzi amevaa sare safi mno
      • KN – Mwanafunzi KT – amevaa sare safi mno
    2. Sakafu ile inateleza sana
      • KN – Sakafu ile KT – Inateleza sana
  16. Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa. (al 2)
    “Njoo hapa” Askari alimwita Juma.
    • Askari alimwita Juma aende kule
  17. Unda nomino mbili kutokana na kitenzi safari. (al 2)
    1. Safari
    2. Msafiri
    3. Msafara
    4. Kusafiri
  18. Andika kitenzi kifuatacho katika kauli ya kutendeswa. (al 1)
    Panga
    1. Pangishwa

FASIHI SIMULIZI AL 10

  1.                        
    1. Eleza maana ya methali (al 2)
      • Semi fupi ambazo hueleza kwa muhtasari au mafumbo ukweli fulani wa kimaisha.
    2. Fafanua sifa nne za methali (al 8)
      • Huwa fupi k.m. ‘Msafiri kafiri.’
      • Hutumia tamathali za usemi.
      • Hutumkia lugha ya kimafumbo.
      • Huwa na maana ya ndani na nje.
      • Kunazo hufanana kimaana k.m. ‘Haraka haraka haina baraka’ na ‘Polepole ndio mwendo.’
      • Hupingana zenyewe k.m ‘Polepole ndio mwendo’ na ‘Chelewa chelewa utamkuta mwana si wako.’
      • Huwa na sifa za kishairi k.v. ukwapi, utao na vina -Haba na haba, hujaza kibaba.
      • Sifa za utegemezi kwa kuingiliana na tanzu nyingine za fasihi.
      • Huwa na muundo maalum wa sehemu mbili:

ISIMU JAMII AL 10

  1.                      
    1. Eleza maana ya sajili ya bungeni . (al 2)
      • Haya ni matumizi ya lugha katika muktadha wa bunge.
    2. Taja sifa nane za sajili ya bungeni. (al 8)
      Kuchanganya msimbo/ndimi katika mijadala, ili kujieleza vyema – waziri wa Finance.
      • Lugha ya adabu – naingependa kumkosoa.
      • Msamiati na istilahi huhusiana na bungeni k.m. vikao vya bunge, spika, mesi, karani –
      • hoja, kifungu nambari n.k.
      •  Hurejelea sheria za nchi au katiba katika kutetea hoja fulani inayojadliwa.
      • Lugha ya heshima katika mawasiliano na majadiliano-Mheshimiwa spika
      • Wabunge hutaja msamiati unaorejelea sheria na kanuni za bunge wanapojadiliana
      • kuhusiana na maswala mbali mbali, hasa shughuli za kinidhamu.
      • Lugha huwa sanifu.
      •  Huwa na urudiaji wa maneno mfano. Bwana Spika.
      • Huwa na kukatizana usemi mfano pale ambapo mbunge husimama kwa hoja ya nidhamu.
      • Mara nyingi huwa na sentensi ndefu ndefu.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End Term 2 Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest