Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End Term 2 Exams 2023

Share via Whatsapp

SEHEHU YA A: INSHA

Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali:

Nazi mbovu harabu ya nzima

 SEHEMU B UFAHAMU

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Mwalimu Mosi aliitwa Mwalimu Mosi kama alivyopenda mwenyewe. Mwalimu Mstaafu ambaye mikononi mwake wanafunzi walifinyangwa barabara mpaka hatimaye wakaisha kuwa madaktari, marubani, wabunge, mawaziri, wahandisi, wahasibu.

Wanafunzi wake wote hao wanafunzi wake hawamsahau kwa nasaha zake, kwa insafu yake, kwa huruma zake, kwa hekima yake, kwa ustaarabu wake, kwa uadilifu wake, kwa uajibikaji wake, kwa nemsi yake, kwa ucheshi wake, kwa ukaramshi wake – kwa yote na yote.
Hawamsahau mwalimu wao huyo wa shule ya msingi aliyelimbuka kuwashikisha kalamu,kuwafichulia siri ya tarakimu, abjadi, ramani, michoro, jedwali, Hisabati wake –Sayansi, Historia na Jiographia – na vyote na vyote.

Alijaaliwa mvi nyeupe zilizojianika kwenye kichwa chake kidogo kilichosimama jadidi kwenye shingo yake nyembamba. Alijaaliwa mvi kwa vile zilikuja mapema wakati alikuwa bado ana umri wa miaka thelathini. Watu wakasema wakati hekima hiyo, kutabasuri huko. Kwa hiyo, hakujisumbua kujipaka rangi nyeusi kuung’ang’ania ujana uliotishia kumwondoka mapema. Wakati wa kustaafu ulipotimu, mvi zimemkaa kwa haiba kama theluji
kwenye mlima Kilimanjaro.Zimempa haiba na staha na mvuto wa aina yake.

Anaikumbuka siku ya sherehe za kumuaga shuleni. Zilikuwa sherehe za ndovu kumla mwanawe. Wazazi na wanafunzi wa zamani na wapya walifurika kwenye kiambo cha shule kama mashabiki wa mchuano wa siku wa kuwania kombe la dunia. Baadhi ya wanafunzi wake waliokuwa watu
wa kutajika walifika kumzawidi mwalimu wao wa awali. Mwalimu aliyechangia pakubwa kuwafanya kuwa watu wa subira yake, shime yake, wasia wake na kielelezo chake.Kielelezo kisichomithilika. Wanafunzi wake wa zamani waliopewa kisogo na dunia, wakifika kuumiza roho zao kwa kuhesabu magari ya kifahari ya wenzao na kuhusudu masuti yao yaliyotoka ng’ambo, na kuwamezea mate wake za wenzao hao waliokuwa wamekuwa ‘watu; kwa vigezo hivi vya kupima utu kwa vitu.

Wanafunzi wake waliokuwa bado wanasoma kwenye shule hiyo waliimba lele, nyimbo za jamii mbalimbali, wakacheza zeze, marimba, lelemama, mdundiko, violini, vinubi. Sikwambii, kukariri mashairi na kucheza drama, na sarakasi. Watu walifurahi hadi ya kufurahi. Sherehe zilifana. Hotuba zilitolewa na Mstaafu Mosi alisifiwa. Alipaliwa sifa hasa. Aliposisimama kuzungumza, uwanja mzima ulizizima. Walijua kwamba Mwalimu Mosi nihatibu hodari, anayo maneno kuweza kumtoa nyoka pangoni. Akashika kipaza sauti. Akakohoa kama ishara ya kuosha koo.

‘SIwezi kuhutubu’ alisema ‘Mimi sikuwafundisha ubaguzi. Kwa nini mnabaguana? Kwa nini hamkuwapa watu wa matabaka yote nafasi ya kuzungumza? Kwa nini? Kwa nini nmafanya hali hii ya kuwa kuna watu na nusu watu? Naomba radhi mfawidhi wa sherehe lakini nadhani ni jambo la busara kutokitia mchanga kitumbua cha sherehe hii kwa kubagua. Kwa hivyo, naomba wazungumze pia wale ambao hawajakuja hapa kwa magari mazito. Nataka wazungumze wale ambao hawatusifu tu”.

Kimya.

‘Nasema nataka aje hapa mwanafunzi wangu wa sasa wa zamani ambaye hana nafasi ya hali au
dhamira yake si kusifu , naye pai hatubu’.

Kimya.

Kisha mtu mmoja alianza kuwasukuma kwa mkikimkiki watu akitaka wampishe. Baadhi walisonya au kutapika ufyosi kwa hasira huku wengine wakisihi aachiwe apite. Kichwa chake chenye upara kiling’aa utosini kama sufuria mpya kwenye duka la Baniani. Alipokaribia jukwaa
ilibainika kuwa alikuwa na furaha nyekundu iliyochanika vibayavibaya kana kwamba ndiyo mwanzo anatoka kupigana kiereka mieleka. Alipopanda jukwaa, nusura aanguke, ama kwa haraka zake au kwa kukosa makini au yote pamoja. Alikitwaa kipaza sauti kutoka kwa Mwalimu Mosi kana kwamba yalikuwa makosa makubwa kumruhusu mwalimu kuwa nacho watu walianza kucheka.

‘Hebu nitazameni vizuri’ aliguruma. ‘Mnasikia lakini? Sijawahi kusema kwenye kipaza sauti tangu nizaliwe sijawahi kuvaa kiatu mguuni, sijawahi kumiliki hata baiskeli, sikwambii haya madude makubwa waliyokuja kututisha nayo akina Baraka, Festo, Mshamba, Nangeto, na hali kadhalika. Hawa wote wanaojiita watu ambao tulikuwa nao hapa pamoja hatujui hata kupenga kamasi wala kuhesabu vidole vya mikono yetu, sijawahi kuruka kwa ndege wala kufika kwenye majiji ya ndani na nje ya nchi hii wanakoishi au kutembelea mabingwa hawa. Sijawahi kuona sura ya shule ya upili ila pale alipokuja rais kuchangisha pesa kwenye shule ya upili ya Wangwani. Pesa zilizoliwa na wakora kama hawa, sijawahi kuona raha ya
kuitwa mheshimiwa , sijawahi kuitwa, mtu, mtu wa maana, mtu bora wa halafu na wa sasa. Kisa na maana ni huyu Mwalimu Mosi ….?

Jibu maswali yafuatayo:

  1. Kipe anwani mwafaka kifungu hiki   (alama 1)
  2. Mwalimu Mosi aliwafinyanga wengi barabara.Thibitisha (alama 2)
  3. Ni nini ishara ya mvi nyeupe iliyojianika kwenye kichwa cha mwalimu Mosi kulingana na watu. (alama2)
  4. Sherehe za mwalimu Mosi zilikuwa za ndovu kumla mwanawe.Fafanua. (alama2)
  5. Kwa nini mtu yule alianza kusukuma watu kwa mkikimkiki nusura anguke? (alama2)
  6. Dondoa tashbihi zozote mbili ambazo zimetumika katika kifungu hiki .(alama2)
  7. Ni kwa jinsi gani mtu aliyekitwaa kipasa sauti anajiona duni ? (alama 2)
  8. Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumika katika kifungu hiki
    1. Mfawidhi
    2. Nemsi (alama2)

SEHEMU C YA SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA

  1. Taja sauti ambazo huwa na sifa zifuatazo (alama 3)
    1. irabu ya kati, chini
    2. konsonati sighuna ya menoni.
  2. Bainisha silabi zinazowekwa shadda katika maneno yafuatayo
    1. Mwalimu
    2. Ala (kihisishi) (alama 2)
  3. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha mstari :
    Wale waovu watalaaniwa hatimaye.           (alama2 )
  4. Nyanbua vitenzi vifuatavyo ukizingatia kauli kwenye mabano.
    1. Chota (kutendesha) _______________________
    2. Tembea (kutendea)________________________ (alama 2)
  5. Sentensi zifuatazo ni za aina gani?
    1. Mkurugenzi aliyeshiriki katika ufisadi ametiwa kortini.
    2. Mama anapika ilhali watoto wanacheza (alama 2)
  6. Eleza matumizi mawili ya kiakifishi .
    Kibainishi. (alama 2)
  7. Badilisha sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.
    “sitaweza kukusaidia leo’. Mfadhili akasema. (alama 2)
  8. Eleza matumizi ya kiambishi ‘po’ katika:
    Mwalimu alipofika alioneshwa walipokuwa wageni. (Alama 2)
  9. Tunga sentensi katika wakati uliopita hali timilifu (alama 2)
  10. Ainisha mofimu katika neno
    Kilichopikwa -
  11. Andika katika ukubwa wingi
    Ngozi ya mtoto ni laini sana . (alama 2)
  12. Tunga sentensi kwa kutumia .
    Kivumishi kionyeshi kisisitizi kimoja na nomino katika ngeli ya YA-YA. (alama 2)
  13. Onyesha miundo miwili inayojitokezea katika nomino za ngeli ya U-ZI (alama 2)
  14. Unda nomino dhahania kutokana na vitenzi
    1. lima
    2. Pika (alama 2)
  15. Kwa kutoa mifano eleza maana ya mzizi huru na mzizi funge. (alama 2)
  16. Yakinisha sentensi ifuatayo
    Usiposoma kwa bidii hutafaulu vyema (alama 2)
  17. Kwa kutunga sentensi onyesha maana ya vitate. (alama 2)
    Fua
    Vua
  18. Sahihisha sentensi (alama 2
    Mwanafunzi ambaye niliyemsomesha ameasi jamii
  19. Tambua na ueleze aina za vivumishi katika sentensi zifuatazo ( alama 2)
    • Mkulima mwenyewe analima shambani
    • Kazi yao inahitaji mjini.
  20. Kwa kutunga sentensi onyesha maana ya vitate. (alama 2)
    Fua
    Vua
  21. Choyo ni kwa karimu _______________ ni kwa sifu na _______________ ni kwa tawanya. (alama 2)

SEHEMU YA D: ISIMU JAMII

Soma makala yafuatayo kasha ujIbu maswali

Mhusika A: Njoo hapa! Ni saa ngapi? Unatenbea usiku.
Mhusika B: (akitetemekaNIsamehe afande, nimechelewa.
Mhusika A: Nani akusamehe. Piga magoti haraka! Toa kitambulisho!
Mhusika B: Nilisahau nyumbani
Mhusika A: Wewe unatembea bila numberplate. Nitakutia ndani saa hii.
Mhusika B: (kwa kunyenyekea) Nisamehe afande.
Mhusika A: Utajitetea na nani? Mkono mtupu haulambwi.
Mhusika B: Sina chochote
Mhusika A: leta hiyo mkono! Nikikutia hizi pingu utaongea sawasawa .

  1. Tambua sajili ya makala; uliyosoma (alama 2)
  2. Eleza sifa zinazojitokeza katika sajili uliyotaja hapo juu. (alama 8)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

  1. Eleza maana ya:
    1. Visasili ( al2)
    2. Visasili vina umuhimu gani? ( al5)
  2. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata
    Lala mtoto laala
    Lala mtoto laala
    Mama anakuja laala
    Akupe maziwa laala
    Maziwa matamu laala
    1. Tambua aina ya wimbo uliosoma (alama 2)
    2. Taja sifa za aina ya wimbo uliotambua hapo juu. (alama 3)
  3. Ni kwa njia gani hadhira katika fasihi simulizi inaweza kushirikishwa kwenye utambaji wa hadithi? (alama3 )

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

SEHEMU YA A: INSHA

Hii ni insha ya methali

Mtahiniwa atunge kisa ambacho kitadhihirisha maana ya methali hii.

Maana ya methali ni kuwa mtu mmoja akiwa na tabia mbovu, anaweza kuziambukiza kwa wengine.

Kisa unaweza kudhihirisha hali zifuatazo.

  1. Mwanafunzi mtovu wa nidhamu akiwa miongoni mwa wanafunzi wengine anaweza kuwaharibu.
  2. Mtu ambaye anatumia muhadarati katika jamii anaweza kuwafanya wajamii wengine kuanza kutumia mihadarati.
  3. Mwanafuzi mzembe anaweza kuwafanya wanafunzi wenzake kuwa wazembe.
    Kwa vyovyote vile insha iweze kuonyesha pande mbili za methali.
    Kwa mfnao tuone uozo wa mhusika fulani na jinsi alivyoambukiza wengine akiandika kisa ambacho hakioani na methali atakuwa amepotoka kimaudhui.


SEHEMU YA B

  1. Anwani
    Sherehe ya kumuaga Mwalimu Mosi   (alama 1)
  2. Kuna waliopita mkononi mwake na kuwa mdakatri, marubani, wabunge,
    mawaziri, mahadisi wahasibu na kadhalika. (alama 1)
  3. Ishara ya mvi nyeupe ni hekima na kutabasuri . (alama 2)
    1. Wazazi na wanafunzi wa zamani na wapya walifurika
    2. Baadhi ya wanafunzi wake waliokuwa tajika walifika kumzawidi. (alama 2)
    3. Wanafunzi waliokuwa bado wanasoma walitumbuiza (alama 2)
  4. Kwa sababu ya:
    1. Haraka
    2. Kukosa makini
    1. Zimekaa kwa haiba kama theluji ya mlima Kilimanjaro (alama 2)
    2. Kana kwamba ndivyo mwanzo anataka kupigana miereka (alama 2)
    1. Hajawahi kutumia kipaza sauiti tangu azaliwe (alama 2)
    2. Hajawahi kumilki hata baiskeli (alama 2)
    3. Hajawahi kuiona shule ya upili (alama 2)
    4. Hajawahi kuitwa mtu wa maana. (alama 2)
    5. Hajawahi kuona raha (alama 2)
    1. Mfawidhi – kiongozi wa sherehe
    2. Nemsi – heshima (alama 2)


SEHEMU C YA SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA

  1.  
    1. Irabu ‘a
    2. Kansonanti th    (alama 3)
  2.  
    1. Mwalimu (alama2)
    2. Ala
  3. Wale wouvu watalaaniwa hatimaye S – KN (W + V) + KT (T +E)
  4.  
    1. Chota - Chovya
    2. Tembea – Tembelea (alama2)
  5.  
    1. Sentensi changamano (alama2)
    2. Sentensi ambatano
  6. Kibainishi /ritifaa (alama 2)
    1. kuonyesha sehemu au maneno ambapo kuna herufi fulani zimeondolewea au kuachwa.
    2. Hutumwa kuonyesha tofauti kati ya ng na ng’ (alama 4)
  7. Usemi halisi
    Mfadhili alisema kuwa hangeweza kumsaidia siku hiyo. (alama 2)
  8. PO ya kwanza : wakati
    PO ya pili : mahali (alama 2)
  9. Wakati uliopita hali timilifu mfano
    Mwalimu alikuwa amefundisha (alama 2)
  10. KI  - Kiambishi awali                              KI- ngeli
    LI  - Kiambishi awali                               LI – wakati
    Cho - Kiambishi awali                            Cho – kerejeshi
    PIK                                                          PIK – mzizi
    W                                                             W – kauli
    A                                                              A – kiishio                                 (alama2)
  11. Ukubwa wingi              (alama 2)
    Magozi ya matoto ni laini sana
  12. mfano
    Maji yaya haya/yayo hayo/yale yale yatanywewa na wanafunzi.  (alama2)
  13. muendo ya u-zi
    Ulimi – ndimi –u zi
    Ukubwa – kuta – u – O
    Uzi – Nyuzi – u - ny
    Ubao – mbao - u –mb         (alama2)
  14. Nomino dhahamia
    1. lima – ukulima
    2. pika – upishi                  (alama2)
  15. Mzizi huru – mzizi unaojisimamia kimaana na hauhitaji kuongeza viambishi vingine ili utoe maana.km samehe,sahau.Sali.
    Mzizi funge – haujisimami kimaana.km pik,som.. (alama2)
  16. Ukisoma kwa bidii utafaulu vyema (alama2)
  17. fua – kuosha nguo
    Vua – kutoa nguo
    Kuwakamata samaki          (alama 2)
  18. mwanafunzi ambaye nilisomesha amlasi jamii
    Mwanafunzi niliyemsomesha amliasi jamii (alama 3)
  19.  
    1. mwenyewe – kivumishi cha pekee
    2. Yao – kivumishi kimilikishi (alama 2)
  20. sifu - kashifu
    kusanya - tawanya

SEHEMU D ISIMU JAMII

  1. Sajili ya polisi      (alama 2)
  2. Sifa za sajili ya polisi.   (alama8)
    1. Huwa matumizi ya kauli za kuamuru
    2. Kuna matumizi ya kauli za kuamuru
    3. Kuna kuchanganya ndimi
    4. Hutumia lugha legevu
    5. lugha ya unyenyekevu kwa mshukiwa
    6. Ni Lugha inayoeleweka kwa urahisi
    7. Lugha ya misimu


SEHEMU E FASIHI SIMULIZI

  1.  
    1. Visasili ni hadithi za kale ambazo huelezea imani na mtazamo wa jamii kuhusu asili ya ulimwengu na mwendo wake (alama 2)
    2. Sifa wa visasili   (alama5)
      1. Husimulia mambo ya kiimani au kidini kama yanayoaminiwa na jamii.
      2. hukubalika na jamii husika
      3. huwa na msingi wa kihistoria
      4. huweza kuwa na wahusika binadamu, muingu, wanyama mawe na vitu vingine.
      5. Matendo ya wahusika hukitwa katika ulimwengu wa asili
  2.  
    1. bembelezi   (alama2)
    2. Sifa za bembelezi   (alama3)
      1. Huanbiwa na walezi au wazazi wa watoto
      2. Huimbwa kwa sauti tamu
      3. Hutoa ahadi kwa watoto
      4. Huwa fupi kwa huimbiwa kwa kurudiwarudiwa
  3.  
    1. Kupiga makofi
    2. kuimba wimbo
    3. kuuliza maswali   (alama 3)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End Term 2 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest