KISWAHILI
KARATASI YA KWANZA
INSHA
MUDA: SAA 1 ¾
MAAGIZO
- Jibu maswali mawili
- Swali la kwanza ni la lazima
- Kisha chagua insha nyingine kutoka kwa maswali matatu yaliyosalia
- Kila insha isipungue maneno 400
- Kila insha ina alama 20
- Kila insha aindikwe kwa lugha ya Kiswahili.
MASWALI
- Umepata tangazo la nafasi ya kazi ya uhariri katika shirika la uchapishaji vitabu vya fasihi andishi kwenye gazeti la Taifa Leo.
Andika barua ya kuomba nafasi hii na uiambatanishe na wasifu kazi wako kwa maelezo zaidi. - Jukumu la kuzuia msambao wa virusi vya korona ni la mtu binafsi. Jadili.
- Andika insha itakyothibitisha ukweli wa methali:
Mchelea mwana kulia, hulia mwenyewe. - Anza kwa.
"Mwanangu, dunia imebadilika pakubwa lakini chunga mabadiliko hayo yasikuzuzue…."
MAAKIZO
- Barua
- Muundo wa barua rasmi – yenye anwani mbili
- Ina anwani ya kwanza: Mwandishi. (Mtahiniwa) abuni anwani yake – iwe wima Al.1
- Tarehe : Chini ya anwani ya kwanza Al. ½
- Anwani ya pili: Mwandikiwa – Mkurugenzi wa shirika la uchapishaji. Al.1
- Maamkizi : kwa Bw/Bi Al. ½
- Mtajo/mada: KUH/MINT – KUOMBA KAZI YA UHARIRI Al.2
- Mwili wa barua
- Utangulizi
- Maelezo ya kibinafsi kwa ufupi
- Ufaafu wake katika hiyo nafasi
- Maelekezo ya wasifu kazi kwa maelezo zaidi Al.4
- Hitimisho: sahihi ya mwandishi, jina na cheo kama anacho. Al.1
- Wasifu kazi/wasifu Taala
- Habari za kinafsi
- Jina
- Jinsia
- Umri/Tarehe ya kuzaliwa
- Ndoa/Hadhi
- Anwani – Barua pepe/nambari ya simu
- Dini
- Lugha azijuazo.
(Al.2)
- Elimu
- Orodha ya shule – aanze kwa kiwango cha juu zaidi.
- Ataje cheti alichohitimu.
(Al.2)
- Tajriba – Ujuzi wa kikazi/maarifa. Al.2
- Ufanisi – Ataja na aeleze ufanisi wake. Al.1
- Uraibu – Mambo anayopenda kufanya Al.1
- Wadhamini/Warejelewa wawili au zaidi;
- Jina la dhamini
- Vyeo/cheo cha mdhamini
- Anwani
- Nambari ya simu
- Barua pepe
- Habari za kinafsi
- Muundo wa barua rasmi – yenye anwani mbili
- Mikakati ya kuzuia virusi vya korona
- Kunawa mikono
- Kutosalimiana
- Kuvaa barakoa
- Kutokohoa au kupiga chafya kiholela/kutumia karatasi shashi au kiwiko unapokohoa au kupiga chafya.
- Kukaa mbali na watu wengine
- Kukaa nyumbani wakati ambapo mtu hana shughuli muhimu ya kufanya nje.
- Kuepuka mahali paolip na umati wa watu.
- Kutotumia pesa taslimu na badala yake atumie njia za kieletroniki kulipia
- Kutumia kieuzi wakati ambapo kuna ukosefu/uhaba wa maji
- Kujitenga/kutafuta matibabu wakati ambapo viwango vya joto viko juu au anaonyesha dalili za maradhi.
(Al.20)
- Mtu asiyetaka mwanawe alie huishia kulia yeye mwenyewe.
- Huwanasihi wazazi wasichelee kuuaadhibu watoto wao wanapokosea ili waishie kuwa na tabia na menendo mizuri.
- Mwanafunzi aweze kutunga kisa ambacho kinaonyesha ambacho kinaonyesha ni mambo gani ambayo yamefanya dunia kubadilika
- Ni nani aliyekuwa akimpa ushauri na sababu za kumpa ushauri huo.
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 4 End Term 2 2021.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates