Kiswahili - KCPE 2021 Prediction Set 2 (Questions and Answers)

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi.

Ufisadi ni janga ___1___ tangu enzi za mababu zetu. Viongozi wa wakati huo ___2___ maana ya methali___3___ wangalikabiliana nao kabla ya visa hivyo vya ufisadi ___4___. Ufisadi ni uovu ___5___ kukemewa na kupigana nao kwa___6___, Tume ya kupambana na ufisadi ___7___fedha za kutosha ___8___ shughuli zake, huenda tukapiga hatua kukabiliana na tatizo hili sugu.

kiswa set 2 q1 8

Kristina aliamua____9____ shuleni. Juhudi za walimu kumshawishi afanye bidii hazikufanikiwa. Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane_ 10__ ajabu ni kuwa alizoa alama za ____11____. Alikitazama cheti chake kilichokuwa mikononi ____12____asiweze kuamini. Alivuta fikra na kuona jinsi ____13____ kwenye anasa na kupuuza masomo. Machozi ____14____ njia mbilimbili. Wazazi wake walimshauri arudi shuleni tena ____15____umri wake bado ulikuwa mdogo. Safari hii hakufanya ajizi.

kiswa set 2 q9 15

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi.

  1. "Ka' imetumiwaje katika sentensi;
    Mama alipika pilau, akala, akaosha vyombo, akaoga, akalala?
    A. Kuonyesha hali ya masharti.
    B. Kuonyesha hali ya kuendelea kwa matukio.
    C. Kuonyesha hali ya wakati uliopita.
    D. Kuonyesha hali ya mfuatano wa matukio.
  2. Chagua sentensi inayoonyesha matumizi sahihi ya lau?
    A. Lau mwalimu anapofundisha husimama.
    B. Nipe lau shilingi tano ninunue kaukau.
    C. Lau ungefika mapema ungekutana na mwalimu wetu.
    D. Lau mtu anapofunga ndoa watu husherehekea
  3. Sentensi, “karembo amekwenda kwao” ina maana mbili. Zichague
    A. (i) Amekwenda alikozaliwa
    (ii) Amekwenda mbali na kwao.
    B. (i) Amekwenda alikozaliwa,
    (ii) Amekwenda kwa watu wengine.
    C. (i) Amekwenda kwa watu wengine.
    (ii) Amekwenda mbali na kwao.
    D. (i) Amekwenda kwa mtu mwingine.
    (ii) Amekwenda mbali na kwao
  4. Maana ya 'ungalifika ungalinisaidia' ni
    A. ulifika lakini hukunisaidia.
    B. ulifika na ulinisaidia.
    C. hukufika wala hukunisaidia.
    D. hukufika ila ulinisaidia.
  5. Chagua usemi taarifa ufaao wa sentensi: “Ondoeni madaftari yenu hapa kila siku,” mwalimu aliwaambia wanafunzi.
    A. Mwalimu aliwaambia wanafunzi kuwa anataka wayaondoe madaftari yao hapo kila siku.
    B. Mwalimu aliwaambia wanafunzi kuwa angetaka wayaondoe madaftari yao hapo kila siku.
    C. Mwalimu aliwaambia wanafunzi kuwa yeye hutaka wayaondoe madaftari yao hapo kila siku. D. Mwalimu aliwaamuru wanafunzi wayaondoe madaftari yao hapo kila siku.
  6. Chagua jibu lenye vivumishi visivyochukua viambishi vya ngeli
    A. dhaifu, ghali, hodari.
    B. zuri, baya, safi.
    C. gumu, safi, karimu.
    D. bora, hodari, chema.
  7. Akisami 7/9 huitwa
    A. sudusi saba.
    B. subui saba.
    C. lusui saba.                     
    D. thumni tisa.
  8. Chagua neno lenye maana sawa na maadamu
    A. Mradi.
    B. Isipokuwa
    C. Pasipo                           
    D. Kwa kuwa
  9. Chagua jawabu lisilo sahihi
    A. Sura ni sehemu katika kitabu iliyogawanywa.
    B. Sura ni umbile la mtu au nyama lililo usoni.
    C. Sura ni mpango wa toatundisho ya elimu maalum.
    D. Sura ni kutoa ushuzi.
  10. Wingi wa ‘mtume amemtuma padri akaupeleke ujumbe’ ni?
    A. Mitume wamewatuma mapadri wakapeleke jumbe.
    B. Watume wamewatuma mapadri wakalipeleke ujumbe.
    C. Mitume wamewatuma padri wakazipeleke jumbe.
    D. Mitume wamewatuma mapadri wakazipeleke jumbe.
  11. Shaibu ni kwa ajuza kama vile mwanyumba ni kwa
    A.mkemwenza.
    B. mjakazi.
    C. mkazamwana                
    D. mwanamwali.
  12. Kitenzi, "soma” katika kauli ya kutendea ni
    A. somesha.
    B. somea.
    C. someka.                        
    D. somasoma.
  13. Kamilisha methali
    Siri ya mtungi
    A. aijuaye chungu.
    B. aijuaye debe
    C. aijuaye kopo.                 
    D. aijuaye kata.
  14. Jibu la kitendawili
    Nikicheka anacheka, nikinuna ananuna ni
    A. maji
    B. moto.
    C. kioo.                             
    D. picha.
  15. Bainisha matumizi ya 'karibu’ katika sentensi Geteri ameanguka karibu avunjike mguu.
    A. Kuonyesha makaribisho.
    B. Kuonyesha nusura.
    C. Kuonyesha kiasi
    D. Kuonyesha wakati.

Soma kifungu kifuatacho kisha wibu maswali 31 mpaka 40

Amani ni utulivu au hali ya kuwa na usalama bila ghasia au vita. Hali hii ya mtu binafsi kukaa kwa utulivu miongoni mwa watu wa aila moja au katika jamii pana ndilo alilokusudia Mungu. Alipowaweka Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni, wawili hawa walikaa kwa utulivu na viumbe wote, wadudu na nyuni wa angani, wala hakuna aliyemzoza mwenzake. Lau sio dhambi ya mwanadana iliyoleta mafarakano baina ya mtu na wanyama na hatimaye wivu wa Kaini dhidi ya nduguye Abeli, tungekuwa na aushi tulivu kabisa.

Utangamano baina ya binadamu huwezekana kwa sababu ya amani. Uelewano huu hutufanya tujue mengi kutoka kwa wenzetu. Maulana alituhuluku tukiwa na akili na uwezo wa viwango tofauti ili tufaane. Anayetangamana na wenzake hupata kuelewa mbinu wanazotumia ili kustawi, naye akazitumia na kupiga hatua. Haifai kuona gere au inda mtu anapokupiku katika hili na lile. Muhimu ni kujitahidi na labda kumwiga au kutumia mbinu zinazokaribiana na zake na ikiwezekana umkaribie katika ufanifu au hata kuwa bora kumshinda.

Kuingiliana na kufaana kwa kila jambo huletwa na amani. Binadamu aliyejitosheleza kwa kila kitu hajawahi kuonekana. Utangamano huwafanya watu kuhisi kama wana vyote wanavyohitaji. Huyu akimwazima mwenzake kinu, naye yule anayeazima kinu, mchi wake unaweza kuvunjika kesho, amwazime mwenzake. Mradi itakuwa hali ya kufaana kwa la jua na kwa la mvua. Hii ndiyo huwafanya waja wasio na vyote wanavyohitaji kukaa maisha ya utele; cha huyu kinakuwa cha yule na cha yule kuwa cha huyu. Amani huwafanya watu hatimaye kuonekana wakiwa na usawa. Ukipata mwapata nyote, akikosa mwakosa nyote kisha mnapeana moyo wa matumanini.

Utendakazi katika jamii huwa rahisi panapokuwa na amani. Kwanza mtu huweza kuzitimiza shughuli zake za kulisukuma gurudumu la maisha bila kuhofia jicho la jirani. Ni rahisi pia kuwa na msaragambo hasa katika kazi za kuifaa jamii pasi kujali kabila wala koo. Kazi kama kukarabati kisima kijijini au kurekebisha barabara iharibikapo huifaa jamii nzima. Umoja na hisia ya udugu ndicho kigezo kikuu cha kuiendeleza jamii kwa jumla.

Amani huwezesha kuwa na utulivu kazini. Mathalani shughuli za zaraa huendelea bila kuchachawizwa ambapo upandaji na uvunaji hutendeka katika majira yafaayo. Jamii iliyo na amani hupata chakula cha leo na akiba ya kesho. Kazi za ujira pia hufanyika vyema kwani waajiriwa huenda kazini bila wahaka na kuzifanya gange zao bila mpapatiko nyoyoni. Wafanyabiashara halikadhalika huendesha shughuli zao bila wasiwasi wa kuharibiwa walivyowekeza. Kunawini kwa biashara ni ishara ya kunawiri kwa jamii na dola kwa jamii.

Uthabiti wa taifa huletwa na amani. Mataifa mengine hushirikiana na nchi yoyote ile iliyo na amani kuimarisha maisha ya wananchi. Nchi isiyo na amani hunyimwa usaidizi na misaada. Ni bayana kuwa amani huchangia pakubwa katika ustawi wa mtu binafsi, jamii, nchi na ulimwengu kwa jumla. Ni jukumu letu sote kuhakikisha kuwa tunadumisha amani na nafsi zetu na wenzetu na tuelewe kuwa ukosefu wa amani ni chembe cha maangamizi na mvuruga amani ni hasidi mkubwa wa maendeleo.

  1. Kulingana na aya ya kwanza
    A. Adamu na Hawa hawakuwa na jukumu la kukaa na amani na viumbe wengine.
    B. kuwa na usalama, utulivu wa mtu binafsi na kutozozana na wengine ndiyo amani.
    C.dhambi ya mwanadamu sio chanzo cha mafarakano baina ya watu na wanyama.
    D. halikuwa kusudi la muumba kumuumba binadamu mwenye wivu.
  2. Chagua jibu lisilo sahihi kulingana na kifungu
    A. Amani ikiwepo binadamu huishi kwa utangamano.
    B. haifai kumwonea mtu wivu anapokushinda kwa hili au lile.
    C. utulivu katika jamii huwa kikwazo kikubwa katika utendakazi.
    D. nchi isiyotetereshwa huwa madhubuti kisiasa na watu wake huwa makini kuimarisha.
  3. Aya ya tatu imebainisha kwamba
    A. mtu aliyejitosheleza katika maisha haishi na watu wengine katika jamii.
    B. si vyema kuvunja kinu na mchi ulioomba.
    C. watu wanastahili kufaana kunaponyesha tu.
    D. hakuna mwanadamu hamhitaji mwanadamu mwingine katika maisha ya kawaida.
  4. Mtu anayetangamana na wenzake
    A. hujifunza mbinu za kumsaidia afanikiwe ili awe bora maishani.
    B. huwa na inda wenzake wanapostawi zaidi kumshinda.
    C. hushindwa kupiga hatua kwa sababu ya ushindani mkubwa.
    D. huzua rabsha na kueneza uvumi kuhusu mbinu za wenzake za kufanikiwa
  5. Ni methali gani inafaa zaidi maelezo ya aya ya mme?
    A. Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
    B. Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
    C. Mbwa hafi maji akiona ufuko.
    D. Hamadi kibindoni silaha iliyo mkononi.
  6. kwamba
    A. kuwepo kwa amani katika jamii huwezesha kila mtu kujiendeleza binafsi.
    B. ukabila ni kigezo kikuu cha kuleta maendeleo katika jamii.
    C. ni vyema kumwogopa jirani kwani hujui analofikiria kukuhusu moyoni mwake.
    D. kila mwanajamii abebe mzigo wa kusukuma gurudumu la maisha yake.
  7. Kwa mujibu wa aya ya tano: Amani
    A. huchochea uzembe wa watu na kuzifanya kazi zao kusimama.
    B. huwezesha kila mja kutia bidii katika kazi na kuzalisha matunda mema.
    C. huleta wasiwasi katika nyoyo za wanadamu.
    D. huchangia ukosefu wa hela na chakula nchini.
  8. Kwa mujibu wa aya ya mwisho nchi isiyo na amani
    A. hupewa msaada wa kujikomboa kutoka ghasia
    B. hunufaika kutokana na uthabiti wa mataifa mengine yaliyoimarika.
    C. hutengwa na nchi nyingine na hata kunyimwa usaidizi wa aina yoyote ile.
    D. huimarisha maisha ya nchi na wananchi wake.
  9. Maana ya msaragambo kulingana na kifungu
    A. kuzua vita baina ya watu wanaofanya kazi.
    B. kung'ang'ania raslimali zilizoko katika jamii.
    C. kuvurugana na watu wengine wa jamii yako.
    D. kushirikiana na wengine katika kazi bila kulipwa.
  10. Kichwa kinachofaa zaidi taarifa hii ni
    A. Amani Nchini Mwetu.
    B. Amani Haiji ila kwa Ncha ya Upanga.
    C. Umuhimu wa Amani.
    D. Jinsi ya Kuimarisha Amani.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.

Tuliingia garini na dereva wa kike, kwa jina Rasha, akaliwasha moto na kuliondosha kwa njia ya kipekee. Alishika usukani kwa mkono wa yamini huku ule mwingine ukikamata kigoe cha kubadilisha gia. Mara tu tulifika kwenye mzunguko wa barabara na gari letu likageuka na kushika barabara kuu ya kuelekea jijini Giza.

Japo tulisukwasukwa garini kama maziwa ndani ya kibuyu kutokana na hali ya barabara, mwendo wetu ulikuwa wastani na tulipishana na magari kadhaa njiani. Niliona matrela yanayokokota mabehewa ya kila aina. Mabasi ya rangi zote yalitupita huku yakipiga honi zao kuzindua madereva wenye magari madogo. Baada ya muda mfupi tulifika kwenye mlima maarufu uitwao sweta. Moele yetu kulikuwa na lori kubwa lenye shehena. Rasna alilazimika kukanyaga breki ghafla na kupunguza kasi. Hatukuweza kupita kwa sababu kulikuwa na upete manjano katikati ya barabara. Tulipomaliza upinde, mstari manjano ulianza kukatikakatika Barabara ilikuwa laini na dereva akachapuza gari.

Muda huo wote nilikuwa makini nikisoma ishara za barabarani. Baada ya kufika Nyakoe niliona ishara ya mpindo. Mbele kidogo barabara ilianza kupindapinda. Ilimlazimu dereva kukanyaga breki mara kwa mara. Nilipomwuliza chanzo cha harufu ya mpira kuchomeka, alinijibu, "Ni msuguano wa padi za gari."

Masafa machache mbele hali ya barabara ilianza kuharibika, lami ilikuwa imechubuka na kuacha mabonde. Tulipunguza mwendo huku tukijaribu kurunda kulia na kushoto kwa lengo la kuhepa mashimo. Magari mawili yalikuwa yamegongana kando ya barabara huku trafiki wakipima kwa utepe na kudadisi na kuandika. "Ajali hii lazima imesababishwa na mpando huo," nilijiwazia.

Baada ya Mosocho, barabara ilikuwa shwari isipokuwa matuta ya kupunguza mwendo. Hakukuwa na ishara yoyote na gari letu lilidunda karibu livunje springi. Karibu na Matieko, niliona kipande cha chuma cha pembctatu kimeandika, "kizuizi cha polisi". Tulisimama na baada ya ukaguzi, walitutakia safari njema. Niliona mabango ya kuonya madereva juu ya wanyama, mengine makubwa yalionya kuhusu kutangaza bidhaa mbalimbali. Nilivutiwa zaidi na kima waliosimama juu ya mti aina ya mparachichi.

Ghafla nya ilianza kunyesha kidindia. Dereva aliwasha waipa japo tuliona kwa shida. Barabara ikawa telezi na magari yakawasha taa na kuenda polepole. Ukungu ulishamiri. Tayari gari moja lilikuwa limelala chali. Nadhani dereva alipuuza ishara za barabarani.

Mbele kidogo ishara ya njiapanda ilijitokeza nasi tulifuata ya kushoto. Hapa barabara ilikuwa kavu na laini. Nilishangazwa na jinsi magari yalivyobugunya masafa, yote yakielekea upande mmoja. Kufumba ya kufumbua tuliingia jijini Giza. Kulikuwa na mlolongo wa magari yaliyofuatana unyounyo mwendo wa kinyor ya. Lakini ‘matatu' ziliyapita magari mengine upesi na kuomba kupishwa kwa ishara ya mkono. Yalipuuza tumizi ya taa za barabarani.

Muda si muda, nilihisi gari letu likiyumbayumba kumbe ilikuwa ni pancha. Lakini tulipata mahali pa kuegesha karibu na mpitomilia. Baada ya kulibadilisha gurudumu tuliendelea na safari yetu salama salimini.

  1. Chagua jawabu lisilo sahihi kulingana na aya ya kwanza
    A. gari liliondoshwa stani kwa mtindo wa aina yake.
    B. dereva alishika usukani kwa mkono wa kulia.
    C. mkono wa kushoto wa dereva ulishika kigoe cha kubadilisha gia.
    D. gari lilipopita mzunguko, dereva aliongeza kasi yake.
  2. Kurushwarushwa garini kulitokana na nini?
    A. Barabara iliyokuwa mbovu.
    B. Gari lililokuwa katara.
    C. Mwendo wa wastani wa dereva.
    D. Magari mengi yaliyokuwa barabarani.
  3. Maana ya 'akachapuza gari'ni
    A. akapunguza kasi.
    B. akaongeza kasi.
    C. akaliondoa gari barabarani.
    D. akalisimamisha gari.
  4. Kulingana na aya ya tatu, chagua alama ya barabara iliyokuwa Nyakoe.
    kiswa set q44
  5. Ni ajali ngapi zilizotajwa katika kifungu?
    A. Moja.
    B. Tatu.
    C. Mbili.                            
    D. Nne.
  6. Kulingana na kifungu, dereva alilazimika kutoka upande wa kulia hadi ule wa kushoto kwa kuwa
    A. alitaka kukwepa mashimo.
    B. alitaka wafike haraka.
    C. alitaka kuhepa asigonge magari mengine.
    D. magari yalikuwa yamegongana.
  7. "Ghafla mvua ilianza kunyesha kidindia’' maana ya kifungu hiki ni
    A. mvua ilinyesha kwa wingi.
    B. mvua iliacha kunyesha.
    C. mvua ilinyesha bila kikomo.
    D. mvua ilinyesha ndogondogo.
  8. Kulingana na aya ya sita ajali husababishwa na
    A. mvua inayosababisha barabara kuwa telezi,
    B. madereva kutofuata sheria za barabarani.
    C. kuendesha magari kwa kasi.
    D. ukungu mwingi barabarani.
  9. Wasafiri walipokaribia jijini Giza
    A. magari yaliendeshwa polepole.
    B. magari yalipishana kwa kasi.
    C. gari lao lilipata ajali.
    D. magari yalielekea pande tofauti tofauti
  10. Maana ya methali, 'mwenye nguvu mpishe imejitokeza katika kifungu hiki inadhihirishwa na
    A. magari kuendeshwa mwendo wa kinyonga kwenye msongamano.
    B. magari yote yalisimama kukaguliwa na polisi kabla ya kuendelea na safari.
    C. matatu ziliyapita magari mengine bila kujali sheria za barabarani.
    D. ajali nyingi zilitokea barabarani.

INSHA

Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu kuhusu

UMUHIMU WA KILIMO

_______________________________________________________________________

 



MAJIBU

kiswahili set 2 ms

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili - KCPE 2021 Prediction Set 2 (Questions and Answers).


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest