Ushairi Questions with Answers

Share via Whatsapp

USHAIRI 1

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

KAMA SODOMA!
Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Haihitaji makini, kwa mwenye macho mazima
Utaona walakini, mradi ukitizama
Wanazini hadharani, wana kwa watu wazima
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini.

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Wanazini hadharani, wana kwa watu wazima
Wanatafuna maini, vijana na kina mama
Hawana haya nyusoni, wameharamisha wema
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini.

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Hawana haya nyusoni, wameharamisha wema
Baba na binti ndani, wanacheza lelemama
Marijali wa mbioni, kujipagaza umama
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini.

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Marijali wa mbioni, kujipagaza umama
Wameikataa dini, toka tumboni mwa mama
Wadai Wataliani, watajirisha mapema
Yafanana na sodoma, mji yetu kwa yakini.

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Wadai ufirauni, watajirisha mapema
Hivyo mambo ya kigeni, yametunukiwa dhima
Uwaonapo fuoni, nusu uchi wa mnyama
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini.

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Uwaonapo fuoni, nusu uchi wa mnyama
Watu hawana imani, umezidi uhasama
Na viongozi wa dini, kuabudu darahima
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini.

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama sodoma!
Na viongozi wa dini, kuabudu darahima
Wamekeuka yamini, kati yao na Rahima
Wamemuasi Manani, na kusahau kiyama
Yafanana na sodoma, miji yetu kwa yakini.

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Wamemuasi manani, na kusahau kiyama
Ya Illahi tuauni, tuwe watu maamuma
Tukue katika dini, siku zetu za uzima
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini.

Maswali

  1. Bainisha bahari ya shairi hili ukijikita katika ruwaza zifuatazo (alama3)
    1. Mishororo
    2. Maneno
    3. Vina
  2. Eleza muundo wa shairi hili (alama4)
  3. Bainisha mbinu zifuatazo za kimtindo katika shairi hili (alama3)
    1. Tashbihi
    2. Taswira
    3. Tasfida
  4. Eleza toni ya shairi hili (alama1)
  5. Bainisha nafsi nenewa katika shairi hili (alama1)\
  6. Fafanua dhamira ya mtunzi wa shairi hili (alama2)
  7. Andika ubeti watatu kwa lugha tutumbi (alama4)
  8. Fafanua maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa na mshairi (alama2)
    1. Manani
    2. Marijali

MAJIBU

  1. Bainisha bahari ya shairi hili ukijikita katika ruwaza zifuatazo (alama3)
    1. Mishororo
      • Takhmisa –mishororo tano
    2. Maneno
      • Pindu-utao, mshororo wa mwisho wa ubeti unafanywa ukwapa wa mshororo wa kwanza ubeti unaofuata
      • Kikwamba – Neno/ukwapi wa mshororo wa kwanza kila ubeti ni lile/yale yale
    3. Vina – mtiririko 
      • Vina vyote, vya ndani vina urari (ni) aidha vina vya nche vina urari (ma)
  2. Eleza muundo wa shairi hili (alama4)
    • Beti nane
    • Mishororo 5 kila ubeti
    • Bipande viwili kila mshororo
    • Mizani kumi na sita kila mshororo
    • Vina vya ukwapi ni ‘ni’ na  vya utao ni ‘ma’
    • Lina kibwagizo
  3. Bainisha mbinu zifuatazo za kimtindo  katika shairi hili (alama3)
    1. Tashbihi – kidogo kama Sodom!
    2. Taswira-uwaonapo fuoni, nusu uchi wa mnyama
    3. Tasfida-wanatafuna maini (kushiriki ngano)
  4. Eleza toni ya shairi hili (alama1)
    • Kukashifu/kusuta/kushauri
  5. Bainisha nafsi nenewa katika shairi hili (alama1)
    • Wanajamii
  6. Fafanua dhamira ya mtunzi wa shairi hili (alama2)
    • Kukashifu utovu wa maadili katika jamii/mijini
    • Kuonyesha uozo uliopo mijini
  7. Andika ubeti watatu kwa lugha tutumbi (alama4)
    • Hakika, miji yetu imekuwa kama Sodoma.
    • Watu hawana haya kwani wametupilia mbali maadhili
    • Baba na binti zao hishiriki mapenzi wasichana wadog kuwa waja wazito. Miji yetu inafanana na Sodoma.
  8. Fafanua maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa na mshairi (alama2)
    1. Manani – Mola/Mungu
    2. Marijali - wasichana /mabinti

USHAIRI 2

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Maendeleo ya umma
Sio vitu maghalani
Kama tele vimesaki
Lakini havishikiki
Ama havikamatiki
Bei juu

Maendeleo ya umma
Sio vitu gulioni
Kuviona madukani
Kuvishika mikononi
Na huku wavitamani
Kama tama ya fisi
Kuvipata ng’o

Maendeleo ya umma
Sio vitu shubakani
Dhiki ni kwa mafakiri
Nafuu kwa mafakiri
Ni wao tu washitiri
Huo ni uistimari
Lo! Warudia

Maendeleo ya umma
Ni vitu kumilikiwa
Na wanyonge kupatiwa
Kwa bei kuzingatiwa
Bila ya kudhulumiwa
Na hata kuhadaiwa
Hiyo ni haki.

Maendeleo ya umma
Dola kudhibiti vitu
Vijapo nchini mwetu
Na kuwauzia watu
Toka nguo na sapatu
Pasibakishiwe na kitu
Huo usawa.

Maendeleo ya umma
Watu kuwa na kauli
Katika zao shughuli
Vikaoni kujadili
Na mwisho kuyakubali
Maamuzi halali
Udikteta la.

Maendeleo ya umma
Watu kuwa waungwana
Vijakazi na watwana
Nchini kuwa hakuna
Wote kuheshimiana
Wazee hata vijana.
Maswali

  1. Eleza dhamira ya shairi hili. (al.2)
  2. Baininsha tamathali mbili za usemi katika shairi hili. (al.2)
  3. Eleza umuhimu wa usambamba katika shairi hili. (al.2)
  4. Onyesha jinsi maendeleo ya umma yalivyo kinaya. (al.2)
  5. Eleza mambo ambayo mshairi anachukulia kuwa maendelo halisi ya umma. (al.4)
  6. Tambua matumizi ya mistari mishata kwa kutolea mifano. (al.2)
  7. Bainisha nafsi neni katika shairi hili. (al.1)
  8. Fafanua toni ya shairi hili. (al.1)
  9. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (al.4)

MAJIBU

  1. Eleza dhamira ya shairi hili.   (al.2)
    • Anadhamiria kuonyesha wanyonge wanastahili usawa na haki – na wanyonge kupatiwa kwa bei kuzingatiwa bila kudhulumiwa – ubeti wa 4
  2. Baininsha tamathali mbili za usemi katika shairi hili.              al.2)
    • Tashbihi – ni kama la moto, wavitamani kama tama ya fisi
    • Takriri – Maendeleo  ya umma
    • Nidaa – Lo!
  3. Eleza umuhimu tatu wa usambamba katika shairi hili. (al.2)
    • Maendeleo ya umma (urudiaji wa fungu) – kusisitiza ujumbe
    • Urudiaji wa silabi …..ni, ki – kuleta ridhimu
    • Urudiaji wa neno.
  4. Onyesha jinsi maendeleo ya umma ulivyo kinaya.  (al.2)
    • Ni kinaya kuwa tuna vitu tele lakini bei I juu
    • Ni kinaya kuviona  vitu madukani  lakini kuvipata ng’o
  5. Eleza mambo ambayo mshairi nachukulia kuwa maendelo halisi ya umma.  (al.4)
    • Vitu kumilikiwa  na wanyone kupiwa.
    • Bei kuzingatiwa bila kudhulumiwa
    • Dola kudhibiti vitu vijapo nchini mwetu.
    • Watu kuwa na kauli katika shughulika zao.
    • Watu kuwa waungwana.
  6. Tambua matumizi ya mstari mishata kwa kutolea mifano.  (al.2)
    • Mishororo ambayo si toshelezi katka shairi
    • Maendeleo ya umma
  7. Bainisha  nafsi neni katika shairi hili.    (al.1)
    • Ni mzalendo/mwananchi-nchini mwet ubeti 5
    • Mtetezi wa haki – ubeti 4
  8. Fafanua toni ya shairi hili.                                  (al.1)
    • Kuhamasisha
    • Kuzindua
  9. Andika ubeti wanne kwa lugha nathari.               (al.4)
    • Maendeleo ya umma ni kutafuta  vitu na kuwauzia wanyonge kwa bei nafuu pasi  na kunyanyasua wala kudanganywa na hivyo kulinda haki zao 

USHAIRI 3 
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
Aldli zangu
Zasimama ufuoni
Macho yake
Yakikagua bahari.
Papa, mkali kama mauti
Anahangaisha samaki
Kwa ndaro na maringo
Daima akijigamba
Kwamba baharini
Haupo uwezo unaomtisha
Wala tisho linalomweza.
Wakati anaendelea kutiririka
Huku miongoni mwa samaki
Wingu zito la huzuni
Likizidi usani.
Kama kwa sumaku
Samaki wanavutwa pamoja
Na nyuma ya ngao ya umoja
Wanaenda mwendo wa mbele
Waktimba nyimbo zenye cheche.
Kwa hasira zenye moto
Papa anaongeza ukali,
Bali umati wa samaki
Haulegei muumano
Wala mwendo wa mbele
Kupungua kasi.
Mashambulizi makali.
Bwaal Mashambulizi
Kutoka pande milioni
Dhidi ya papa muuaji.
Sasa baharini
Nyimbo za ufanisi
Zinapaa angani
Kama moshi wa ubani,
Na kubusu masikio
Kama muziki wa nyonga.

  1. Maudhui ya shairi hill yamegawanywa katika sehemu tatu. Zifafanue. (al. 3)
  2. Mbinu ya jazanda imetumika sana katika shairi hill. Thibitisha kwa kutoa mifano mitano. (al. 5)
  3. Onyesha mitindo mingine minne ambayo imejitokeza katika shairi hili. (al. 4)
  4. Tambua nafsi neni katika shairi hili. (al. 1)
  5. Jadili umuhimu wa aina mbili za urudiaji. (al. 2)
  6. Eleza umuhimu wa nidaa kama ambavyo imetumika katika shalri hili. (al. 2)
  7. Shairi hili linathibitisha toni kadhaa. Jadili ukweli huu kwa kutoa mifano mitatu. (al. 3)

Majibu

  1.    
    1. unyanyasaji wa raia/utawala mbaya.
    2. Juhudi za ukombozi/wananchi kudai uhuru
    3. Matunda/manufaa ya juhudi zao/malipo/utulivu na amani
  2.    
    1. Bahari- nchi
    2. mapapa- viongozi/wenye nguvu
    3. Samaki - raia/watu wa kawaida/wananchi
    4. Wingu nzito la huzuni - athari za uongozi mbaya
    5. Macho ya nafsini -  Ukaguzi wakel
    6. Samaki kuvutwa pamoja - ushinkiano wa wananchi 
    7. Ngao ya umoja - umoja wa wananchi
  3.  
    1. Tashbihi - Kama kwa samaki mkali
    2. Uhuishi - Akili kusimama
    3. chuku - tishio linalomweza
    4. Nidaa - Ewaa! Mashambulizi
    5. Taswira - mguso - Kubusu masikio
  4. Mzalendo/mwanaharakati/mwananchi wa taifa husika/ambaye amechora dhuluma za viongozi
  5. Umuhimu wa aina za unidiaji
    1. Takuiri ya maana - ndano, maringo kujigamba
      umuhimu - kusisitiza kuhusu maringo na kutojali kwa viongozi
    2. Neno - Samaki, papa
    3. Kiambishi/Sauti - wa - wanavutwa
      wanaenda
      umuhimu - kufanya shairi limbike/mahadhi/Ridhimu .
  6. Matumizi ya nidaa
    1. kusisitiza mashambulizil
    2. Kuonyesha mshangao - Ewaa!
  7. Hasira - kwa hasira zenye moto/nyimbo cheche
    1. Maringo.majigambo
    2. utulivu
    3. Huzuni - wingu nzito la huzuni.

USHAIRI 4
Soma shairi hili kisha ujibu maswali.

  1. Wenye vyao watubana, twaumia maskini,
    La kufanyiza hatuna, hali zetu taabani,
    Kwa sasa kilo ya dona, bei mia ishirini,
    Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

  2. Washindana matajiri, kwa bei siyo utani,
    Na pigo kwa mafakiri, tunao hali ya chini,
    Wazeni kutafakari, wanyonge tu madhilani,
    Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

  3. Limekuwa kubwa zogo, hakwendeki madukani,
    Fungu moja la muhogo, sasa shilingi miteni,
    Huo mkubwa mzigo, waelemea vichwani,
    Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

  4. Si hichi wala si kile, hakuna cha afueni,
    Bei imekuwa ndwele, wenye macho lioneni,
    Ukiutaka mchele, pesa jaza mfukoni,
    Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

  5. Waliko hao samaki, huko ndiko uchawini,
    Wachuuzi hawacheki, zimewatoka huzuni,
    Vibuwa havishikiki, kimoja kwa hamsini,
    Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

  6. Maisha yetu viumbe, yamekuwa hilakini,
    Wenye vyao kila pembe, wametukaa shingoni,
    Nyama ya mbuzi na ng’ombe, sasa hali maskini,
    Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

  7. Maji yamezidi unga, kwa lodi wa darajani,
    Kajitolea muhanga, kwa bei hawezekani,
    Mvao wake wa kanga, ni shilingi elifeni,
    Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

    Maswali
    1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 1)
    2. Jadili dhamira ya nafsi neni. (alama 2)
    3. Tambua toni ya shairi hili. (alama 1)
    4. Andika ubeti wa sita kwa lugha tutumbi. (alama 4)
    5. Onyesha vile kibali cha utunzi wa mshairi kilivyotumiwa kukidhi mahitaji ya kiarudhi. (alama 2)
    6. Taja na ueleze bahari mbili za ushairi ukizingatia. (alama 4)
      1. Ubeti
      2. Vina
    7. Tambua aina tatu za taswira ukirejelea shairi hili. (alama 3)
    8. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika kwenye shairi. (alama 3)
      1. Dona
      2. Zogo
      3. Waelemea

MAJIBU

  1. Wenye vyao wanatubana. al.1
  2. Dhamira ya nafsi neni nio kuangazia gharama ya juu ya maisha al.2
  3. malalamishi al.1
  4. Maisha ya viumbe yamefika mwisho na walionavyo wanaendelea kuwanyanyasa.Maskini hamudu bei ya nyama ya mbuzi wala ng’ombe.Wakubwa tuokoeni kwa dhiki tulizonazo.
  5.    
    1. Mazida – neno hilakini limetumika kuleta utoshelezi a mizani.
    2. Ukale ndwele limetumika kuleta urari wa vina al.2
  6.  
    1. Ubeti-mathnawi,lina vipande viwili katika kila ubeti.
    2. Ukara kwa sababu vina vya nje havibadiliki kutoka ubeti wa kwanza hai wa mwisho ilhali vile vya ndani vinabadilika.
  7.  
    1. Taswira oni-wenye macho lioneni
    2. Taswira mwendo-hakwendeki madukani
    3. Taswira hisi-zimewatoka huzuni
  8.  
    1. Dona-unga wa mahindi yasiyikobolewa
    2. zogo-hali ya kukosa utulivu
    3. Waelemea-uzito zaidi upand mmoja

USHAIRI 5

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

FUJO TUMBONI

Siku moja, miongoni mwa wengi
Virago vyetu migongoni
Tulianza safari
Kuhama janga la jangwa
Kutafuta bonde la rutuba
Na mvua nzitonzito
Kulima kwa nyoyo imara
Kuzima moto tumboni.

Miaka imepita
Na kupita
Bali, tuzo kutoka ardhi
Kwa wale ambao
Wamekauka kama kuni
Kutokana na nyimbo
Za kuishi ardhi
Ni moto tele tumboni

Lo! Maisha haya!
Ukweli mchungu!
Hii ng`ambo tunayolimia
Kwa kalamko zamisuli
Siyo tuliyoona
Kwa macho ya ndoto
Tulipoanza safari
Aka! Maisha haya!
Maisha yanadondoka njama!
Njama za malaika wa machozi
Za kuiba matunda ya udongo
Baada ya wakulima
Kugofuka kama mahame
Kutokana na makofi
Ya jua
Na mateke
Ya njaa.

MASWALI

  1. Eleza ujumbe wa shairi hili. (alama 4)
  2. Eleza maana ya kitamathali na kijuujuu ya mstari ‘Kuzima moto tumboni.’ (alama 2)
  3. Bainisha matumizi ya vipengele viuatavyo katika shairi.
    1. Mishororo mshata (alama 2)
    2. Usimulizi (alama 2)
  4. Thibitisha kuwa hili ni shairi huru. (alama 4)
  5. Eleza dhima ya aina mbili za urudiaji katika shairi hili. (alama 4)
  6. Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)

MAJIBU

  1. Eleza ujumbe wa shairi hili. (alama 4)
    1. Walianza safari ili kuhama janga la jangwa kutafuta bonde la rutuba.
    2. Walihama kutafuta mvua nzitonzito
    3. Walihama ili kupata pa kulima kwa nyoyo imara
    4. Walime ili pia kuzima moto tumboni
    5. Ardhi yenyewe imewageukia, inawadhuru.
    6. Ng’ambo wanayolima siyo waliyoazimia walipoanza safari.
    7. Malaika wa machozi (wenye uwezo mkubwa) wanafanya njama za kuiba matunda ya udongo.
    8. Wakulima wanakondeana kutokana na athari ya ukame.
      4x1=4
  2. Eleza maana ya kitamathali na kijuujuu ya mstari ‘Kuzima moto tumboni.’ (alama 2)
    1. Kumaliza njaa
  3. Bainisha matumizi ya vipengele viuatavyo katika shairi.
    • Mishororo mishata (alama 2)
      • Siku moja, miongoni mwa wengi
      • Virago vyetu migongoni
      • Bali, tuzo kutoka ardhi
      • Kwa wale ambao
      • Kutokana na nyimbo
      • Hii ng`ambo tunayolimia
      • Baada ya wakulima
        (Zozote 2x1=2)
    • Usimulizi (alama 2)
      • Nafsi neni anasimulia jinsi walivyopiga safari siku moja kutafuta maeneo yenye rotuba ili wayalime kwa ajili ya kujiondolea njaa.
      • Baadaye, kinyume kinatokea. Wenye uwezo wanawala jasho lao.
      • Wakulima kukondeana kutokana na athari za ukame na njaa.
        (Zozote 2x1=2)
  4. Thibitisha kuwa hili ni shairi huru. (alama 4)
    Halijafuata sheria/kanuni za utunzi wa mashairi ya kimapokeo. Kwa mfano:
    • Beti hazina idadi sare ya mishororo. Ubeti wa kwanza 8, wa mwisho 10
    • Mishororo haina idadi sawa ya vipande. Kwa mfano ubeti wa pili, mshororo wa tatu una vipande viwili vingine kimoja
    • Mishororo yake ina idadi tofauti ya mizani.
    • Beti zake hazina urari wa vina.
      (4x1=4)
  5. Eleza dhima ya aina mbili za urudiaji katika shairi hili. (alama 4)
    • urudiaji wa sauti – ‘i’ katika wengi, migongoni, safari
    • dhima: kujenga ridhimu/kulipa shairi mwonjo/kulipa shairi mdundo wa kimuziki
    • urudiaji wa silabi – imepita, kupita
    • dhima: kujenga ridhimu/kulipa shairi mwonjo/ mdundo wa kimuziki/ kuleta urari wa vina
    • urudiaji wa neno – nzitonzito, imepita, kupita
    • dhima:Kusisitiza wazo
  6. Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
    • Toni ya kukata tamaa – wakulima wametamauka kutokana na kutotimia kwa maazimio yao.
    • Huzuni – taswira ya wakulima walivyoteseka
    • Ya matumaini – walipoanza safari walitazamia kuzima njaa matumboni mwao.

USHAIRI 6

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Binadamu hatosheki, ni kiumbe chenye zani, kweli mja hapendeki
Kwa kweli haaminiki, hila ameficha ndani, la wazi ni unafiki
Ukweliwe haafiki, njama zake zi moyoni, usimwone ni rafiki,
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Wenginea watakuua, wakiona una pesa, hata zikiwa kidogo
Hizo kwao ni maua, hupupiwa zikatesa, wakizifuata nyago
Hadi kwenye wako au, pasipo hata kupesa, walakukupa kisogo
Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Pindi kinunua kitu, hafurahi shaitani, bali tajawa chukizo
Mtu kiwa mtukutu, tanuna mtimani, kwato ako tekelezo
Tamko lake 'subutu', kuondoa tumaini, na kukuliza wazo
Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Aliye na taraghani, taabu kuishi naye, kazi yake kujidai
Takusema faraghani, asosema kiwa naye, kupendeza maadui
Hana faida nyumbani, ni mtu akichimbaye, mradi usitumai
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Kwa hakika ni baka, kumkirimu mchawi, aliyejaa uchoyo
Bahati ina hadaa, kukupa alo sodawi, aibarili rowoyo
Mipangayo kwake jaa, na nia ya ustawi, huwiza kuvunja kaniyo
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Ninacho changu kilio, ninalia sanasana, kinyesi nimetupiwa
Ningetoa azinio, lakini uwezo sina, kwa mazito kuambiwa
Ama nitimue mbio, fuadini ninanena, akilini nazuiwa
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

  1. Jadili dhamira ya shairi hili.
  2. Eleza sababu za mtungaji kulalamika katika shairi hili.
  3. Eleza sifa za shairi hili.
  4. Andika ubeti wa tatu katika lugha tutumbi.
  5. Taja na utoe mifano ya mbinu za kimtindo zilizotumika katika shairi hili.
  6. Taja mbinu mbili alizotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi.
  7. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi. (Alama 2)
    1. zani
    2. faraghani

MAJIBU

  1. Jadili dhamira ya shairi hili.
    Kuonyesha vile tamaa ni hatari.
  2. Eleza sababu za mtungaji kulalamika katika shairi hili. (Alama 3)
    Mtu mwenye tamaa ni hatari kama nyoka
    Mwenye tamaa ana unafiki/masengenyo
    Mwenye tamaa anaweza kuua
    Mwenye tamaa ni mchoyo
  3. Eleza umbo la shairi hili. (Alama 4)
    Mishororo minne katika kila ubeti
    Migao/ vipande vitatu - ukwapi / utao / mwandamizi Nina vitatu
    Mizani 8, 8, 8.
    Lina Kibwagizo. Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
    Lina beti sita
    (hoja zozote 4x1=4)
  4. Andika ubeti wa tatu katika lugha nathari/ tutumbi. (Alama 4)
    Mwandishi anasema kuwa mwenye tamaa atakuwa na chuki iwapo utanunua kitu na anakuwa kam shetani kwani hafurahi. Mtu kama huyo atakasirika moyoni kwa kile ulichokifanya.
    Atakuonya ili akuvunje matumaini ya kutekeleza ulichona. Anamalizia kw akusema kuwa mtu mweny tamaa ni hatari kama nyoka.
  5. Taja na utoe mifano ya aina nne za tamathali za usemi zilizotumika katika shairi hili. (Alama 4)
    Takriri - kibwagizo Tashibihi - hatari kama nyoka Tashihisi - Bahati ina hadaa Nahau - Kinyesi kimetupiwa
  6. Toa mifano miwili tofauti ya uhuru wa kishairi katika shairi hili.
    (Alama 2) Inkisari - Ukweliwe, tajawa, asosema, alo, mpangoyo Mazida sheitani (Kurefusha she/ta/ni)
    Kufinyanga sarufi-Ninacho changu kilio badala ya ninacho kilio change nk 
  7. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi.
    (Alama 2)
    1. Zani = baa/ janga /balaa
    2. Faraghani - kwa siri

USHAIRI 7

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na
kotama Katika njia
iendayo Kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani; Nimuonapo huwa anatabasamu Kama mtu aliye
na hamu
Kushika mpini na kutokwa
jasholli kujikimu kupata
malisho.
Anapotembea anasikiliza
Videge vya anga
vinavyotumbuiza Utadhani
huwa vimemngojea Kwa
usiku kucha kuja kumwimbia
Pia pepo baridi kumpepea
Rihi ya maua zikimtetea Nao umande kumbusu
miguuni; Na miti yote
hujipinda migogo
Kumpapasa, kumtoa
matongo; Na yeye
kundelea kwa furaha
Kuliko yeyote ninayemjua
Akichekelea ha ha ha ha ha ha
.......Na mimi kubaki
kujiuliza
Kuna siri gani
inayomliwaza?
Au ni kujua au kutojua?
Furaha ya mtu ni furaha gani?
Katika dunia inayomhini? Ukali wa jua wamnyima zao Soko la dunia lamkaba
koo; Dini za kudhani zamsonga roho
Ayalimia matumbo ya
waroho. Kuna jambo gani linalomridhisha? Kama si kujua ni kutojua Lait angalijua, laity angalijua!

  1. Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili.
  2. Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili
  3. Fafanua aina tatu za taswira ukirejelea ubeti wa pili
  4. Maswali ya balagha katika shairi hili yanasisitiza maudhui yapi? (al.2)
  5. Kwa kutoa mifano, bainisha vipengele vitatu vya kimtindo katika shairi hili (alama3)
  6. Eleza toni ya shairi hili
  7. Bainisha nafsineni katika shairi hili
  8. Eleza sura ya shairi hili

MAJIBU

  1. Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili.
    • Mcheshi
    • Mwenye bidii
    • Maskini
      (alama 2)
  2. Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shoirihili (ala. 4)
    kababuze - babu zetu
    Khogaaf Aliye na kubwa hamu- Aliye na hamu kubwa
  3. Fafanua aina tatu za taswira ukirejelea ubeti wa pili (alama3)
    Taswira sikivu, anasikiliza videge vya anga vinavyotumbuiza Taswira mnuso; Rihi ya maua zikimletea
    Taswira mguso; umande kumbusu miguuni
  4. Maswali ya balagha katika shairi hill yanasisitiza maudhui yapi? (alama 2) Maswali ya balagha hukuza maudhui ya unyanyasaji
    Pia kunyimwa haki kwa binadamu maskini
  5. Kwa kutoa mifano, bainisha vipengele vitatu vya Kimtindo katika shairi hili (alama3)
    Tashihisi - umande kumbusu miguuni
    Kinaya-kuwa mrejelewa anafuraha ilhali anafanya kazi za sulubu (kulima) Tashibihi-Tabasamu kama mtu aliye na kubwa hamu
  6. Eleza toni ya shairi hili
    Huruma - mateso mrejelewa anayoyapitia
  7. Bainisha nafsineni katika shairi hili
    Mchunguzi/mpita njia wa karibu na mrejelewa
  8. Eleza muundo wa shairi hili
  9. Beti tatu
    Mistari mishata
    Mishororo haina mizani
    sawaHakuna urari wa vina

USHAIRI 8

SEHEMU A: USHAIRI.
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Haihitaji makini, kwa mwenye macho mazima
Utaona walakini, mradi ukitazama
Wanazini hadharani, wana kwa watu wazima
Yafanana na sodoma, miji yetu kwa yakini

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Wanazini hadharani, wana kwa watu wazima
Wanatafuna maini, vijana na kina mama,
Hawana haya nyusoni, wameharamisha wema,
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Hawana haya nyusoni, wameharamisha wema
Baba na binti ndani, wanacheza lelemama
Marijali wa mbioni, kujipagaza umama
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Marijali wa mbioni, kujipagaza umama
Wameikataa dini, toka tumboni mwa mama
Wadai Wataliani, watajirisha mapema
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Wadai Wataliani, watajirisha mapema
Hivyo mambo ya kigeni, yametunukiwa dhima
Uwaonapo fuoni, nusu uchi wa mnyama,
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Uwaonapo fuoni, nusu uchi wa mnyama
Watu hawana Imani, umezidi uhasama,
Na viongozi wa dini, kuabudu darahima
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Na viongozi wa dini, kuabudu darahima
Wamekeuka yamini, kati yao na Rahima
Wamemuasi Manani, na kusahau kiyama
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini
Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Wamemuasi manani, na kusahau kiyama,
Ya Illahi tuauni, tuwe watu maamuma
Tukue katika dini, siku zetu za uzima
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

Maswali

  1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 1)
  2. Bainisha bahari ya shairi hili ukijikita katika ruwaza zifuatazo. (alama 3)
    1. Idadi ya mishororo
    2. Mpangilio wa maneno
    3. Vina
  3. Ni ujumbe upi unaojitokeza katika shairi hili. (alama 5)
  4. Bainisha mbinu zifuatazo za kimtindo katika shairi hili. (alama 3)
    1. Tashbihi
    2. Taswira
    3. Tasfida
  5. Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
  6. Bainisha nafsinenewa katika shairi hili. (alama 2)
  7. Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)

MAJIBU

  1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka.    (alama 1)
    • Sodoma!
  2. Bainisha bahari ya shairi hili ukijikita katika ruwaza zifuatazo.    (alama 3)
    1. Idadi ya mishororo
      • Takhmisa/utano 
    2. Mpangilio wa maneno
      • Kikwamba – neon Miji wetu imetumika kuanza kila mshororo
      • Mkufu/upindu/unyoka/ukufu - neno miji yetu kwa yakini imetumika kutamatisha mshororo wa mwisho na kuanza mshororo wa kwanza kwenye kila ubeti.
    3. Vina
      • Mtiririko – vina vyake vya ukwapi na utao vinatiririka
  3. Ni ujumbe upi unaojitokeza katika shairi hili.  (alama 5)
    • Watu kuzini hadharani
    • Watu wameharamisha kutenda mema
    • Watu wamekataa dini
    • Kuna baadhi ya watu wanataka kujitajirisha mapema
    • Watu kuonea fahari vitu vya kigeni
    • Watu pia wmeasi mungu
    • Mshairi anahimiza watu wakue katika dini
  4. Bainisha mbinu zifuatazo za kimtindo katika shairi hili.    (alama 3)
    • Tashbihi mfano kidogo kama Sodoma
    • Taswira mfano uwaonapo fuoni,nusu uchi mnyama
    • Tasfida mfano wanatafuna maini
  5. Eleza toni ya shairi hili.    (alama 2)
    • Kukashifu/kusuta/kushauri.
  6. Bainisha nafsinenewa katika shairi hili.    (alama 2)
    • wanajamii
  7. Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari.      (alama 4)
    • Hakika miji yetu imekuwa sodoma,watu hawana haya kwani nwametupilia mbali maadili,baba na binti zao hushiriki mapenzi,wasichana wadogo kwa waja wazito.miji yetu inafanana na Sodoma       

USHAIRI 9

  1. Mbiu naipulizia, kwa wa hapa na wa ng’ambo,
    Kwani ngoja ‘mesikia, inaumiza matumbo,
    Kwa upole sitafyoa, hata kama kwa kimombo,
    Yafaa jihadharia, maisha yas,ende kambo;
  2. Maisha yas’ende kombo, kututoa yetu ari,
    Zingatia haya mambo, wetu walezi mukiri,
    Kuwa wana kwa viambo, huwa Baraka na kheri
    Watunzeni na maumbo, msijezusha hatari
  3. Msijezusha hatari, na nyingi hizi zahana,
    Wazazi haya si siri, mawi mnayoandama
    Twaeleza kwa uzuri, matendoyo yatuuma.
    Watoto tunayo mori, ni lini mtajakoma?
  4. Ni nani mtajakoma, na pombe ziso halali?
    Sio baba sio mama, mbona ny’hamtujali
    Mwafa ja nzi twasema, mwatuacha bila hali
    Hangaiko acha nyuma, kwani hamuoni hili?
  5. Kwani hamuoni hili, kila mwapigana
    Nyumbanizo hatulali, jehanamu tumeona
    Mwatusumbua akili, twaumia tena sana
    Achene na ukatili, kwani upendo hamna,
  6. Kwani upendo hamna, Kama mbwa mwatuchapa
    Mwatuchoma sisi wana, mioyetu yatupapa
    Pa kujificha hatuna, tumebaki tukitapa
    Maisha hamu hayana, timevunjwa na mifupa.
  7. Tumevunjwa na mifupa, hata leo uke wetu,
    Mwatubaka na kuapa, kutung’ata nyi’ majitu,
    Maisha hatujakopa, fahamu mkosa utu,
    Hayo makeke na pupa, mtakoma utukutu,
  8. Mtakoma utukutu, na kutumia mikiki,
    Na tabia zenye kutu, tumechoka nayo chuki,
    Hatutakubali katu, kutendewa yenya siki,
    Serikali fanya kitu, kwani nasi tuna haki.

Maswali

  1. Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili (alama 2)
  2. Fafanua tamathali nne za usemi zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 4)
  3. Taja nafsi neni katika shairi hili. (alama 1)
  4. Eleza bahari nne zinazowakilishwa katika shairi hili. (alama 4)
  5. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 4)
  6. Eleza maudhui matatu yanayojitokeza katika shairi hili. (alama 3)
  7. Huku ukitoa mfano taja uhuru mmoja wa mshairi ambao umetumiwa katika shairi hili. (alama 2)

MAJIBU

  1.                  
    1. Mwandishi anadhamiria kutuonyesha jinsi watoto wanadhulumiwa na
    2. kunyimwa haki na wazazi/watu waume
      zozote 2 x 1 = 2
  2. Tamathali nne za usemi
    1. Tashibihi – mwafa ja nzi, kama mbwa
    2. Methali – ngoja , mesikia, inaumiza matumbo
    3.  Msemo – kupuliza mbiu – kutangaza
    4. Jazanda – jehanamu tumeona
      Za kwanza 4 x 1 = 4
  3. Nafsineni ni mtoto 1 x 1 = 1
  4. Bahari
    1. Tarbia – mishoro 4 katika kila ubeti
    2. Pindu – utao wa mstari wa mwisho kuanza ubeti
    3. Ukaraguni - hakuna urariwa vina
    4. Manthawi – kila mshororo una vipandi viwili
    5. Sabilia – halina kibwagizo lina kimalizio
      Za kwanza 4 x 1 = 4
  5. Ubeti wa 4 kwa lugha nathari
    • Wanauliza ni lini wataacha kunywa pombe haramu
    • Wazazi wote baba na mama wanakunywa bila kuwajali
    • Wanakufa kama nzi nuia kuwaachia matatizo
    • Kwa nini hawaoni/hawatambui ukweli huu
      4 x 1 = 4
  6. Maudhui
    • Watoto ni Baraka katika jamii
    • Watoto wanaumia kwa matendo maovu
    • Madhara ya wazazi kunywa pombe
    • Watoto kupigwa vibaya na wazazi wao
    • Anakashifu ubakaji unaotekelezwa kwa watoto wa kike ya kwanza 3 x 1 = 3
  7. Uhuru wa kishairi
    • Inkisari – mesikia –nimesikia.
    • Kufinyanga sarufi – jehanamu tumeona- tumeona jehanamu
    • Ritifaa – nyi – nyinyi Za kwanza 1 x 2 = 2 Kutaja 1, Mfano 1

USHAIRI 10

Soma shairi hili kisha ujibu maswali.
Jicho, tavumiliaje, kwa hayo uyaonayo?
Kicho, utasubirije, maonevu yapitayo
Kwacho, lijalo na lije, nimechoka vumiliyo
Naandika!

Moyo, unao timbuko, maudhi tuyasikiayo
Nayo, visa na mauko, wanyonge wayakutayo
Kwayo, sina zuiliko, natoa niyahisiyo
Naandika!

Hawa, wanotulimiya, dhiki wavumiliayo
Hawa, mamiya mamiya, na mali wazalishayo
Hawa, ndo wanaoumiya, na maafa wakutayo
Naandika!

Hawa, sioni wengine, kwao liko angamiyo
Hawa, uwapa unene, watukufu wenye nayo
Hawa, bado ni wavune, kwa shida waikutayo
Naandika!

Bado, wawapo mabwana, wenye pupa na kamiyo
Bado, tafauti sana, kwa pato na mengineyo
Bado, tuling’owe shina, ulaji pia na choyo
Naandika!

Maswali

  1. Shairi hili laweza kuwekwa katika bahari zipi? Thibitisha kila jibu lako. (al 2)
  2. Eleza dhamira ya mshairi. (al 4)
  3. Onyesha mifano miwili ya uhuru wa kishairi jinsi ulivyotumika katika shairi. (al 2)
  4. Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (al 3)
  5. Tambulisha kwa mifano mbinu zozote mbili za sanaa katika shairi. (al 2)
  6. Fafanua sifa nne za kiarudhi zilizotumika katika ubeti wa tano. (al 4)
  7. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi. (al 3)
    1. Zuiliko
    2. Wavune
    3. Wenye pupa na Kamiyo.

MAJIBU

  1. Tarbia - Lina mishororo minne katika kila ubeti
    Msuko - Kibwagizo kimefupishwa.
    Ukara- Vina vya nje vinatiririka katika beti zote ilhali vya ndani havitiririki.
    Ukawafi- Una vipande vitatu (ukwapi, utao na mwandamizi) katika mishiroro ya kwanza mitatu ya kila ubeti isipokuwa kibwagizo
    Kikwamba – Katika beti za 3-5 neno moja ndilo linaanza kila mshororo.
    Sakarani – Kuna bahari kadhaa katika shairi.
    2x1=2
  2. Kuwahimiza watu (hasa wanyonge ✓) wainuke na kupinga ✓maovu na maonevu wanayofanyiwa na matajiri wenye uwezo.
    4x1=4
  3. Inkisari km vumiliyo – kuvumilia nanaandika.
    Mazida kurefusha k.m. angamiyo, vumiliyo n.k.
    Tabdila k.m mamiya badala ya mamia .
    2x1=2
  4. Hawa wanaotulimia wanavumilia✓ dhiki
    Wao ni wengi ✓ na ndio huzalisha mali.
    Wao ndio wanaoumia✓ na kupata mateso / taabu
    Wanayokumbana nayo.Ninaandika / ninasema
    3x1=3
  5. Takriri – hawa, bado, mamiya.
    Balagha – uyaonaje?
    Taharuki – Naandika!
    Inkisari – Hawa, ndo
    Kinaya – Watukufu wenye nayo
    2x1=2
  6. Kuna mishororo minne
    Kuna vipande vitatu katika mishororo ya kwanza mitatu na kimoja katika kibwagizo
    Vina vinatiririka / vinafanana
    Mizani haitoshani kutika mishororo yote mine.
    Lina beti tano.
    Lina kibwagizo.
    4x1=4
    1. Cha kunizuia / kizuizi / kizingiti / uoga / hofu/ pingamizi
    2. Wachovu /dhaifu /hafifu
    3. Walio na tamaa kubwa / walafi/ mabwanyenye
      3x1=2

USHAIRI 11
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
Kiapo kwao majaji, wanosimamia haki
Kwa sharia ni magwiji, wahalifu hawatoki,
Wengi wao ni walaji, kwa rushwa ni mashabiki,
Kwa rushwa mashabiki.
Kiapo kwa daktari, wagonjwa hawadhiliki,
Kazi zao ni dhariri, maradhi hayakwepeki,
Na wengine ni hatari, bila pesa hutibiki,
Bila pesa hutibiki.
Kiapo cha mawaziri, kwa mbwembwe na itifaki,
Na suti zao nzuri, shingo tai haitoki,
Na wengi wana dosari, ni kwa mikataba feki,
Ni kwa mikataba feki.
Kiapo cha magavana, mikoa kuimiliki,
Hujifanya ni mabwana, wala hawasogeleki,
Nayo nchi huitafuna, na kuwa haikaliki
Na kuwa haikaliki.
Kiapo cha maraisi, kwa mizinga na fataki
Na wageni mahususi, hualikwa kushiriki,
Ikulu wakijilisi, kwa wizi hawashikiki
Kwa wizi hawashikiki.
Viapo vya utiifu, kwa sasa havistahiki
Wanoapa ni wachafu, tena hawaaminiki,
Biblia misahafu, washikapo unafiki
Washikapo unafiki

  1. “Dhamira ya shairi hili ni kushtumu ukiukaji wa maadili ya kikazi.” Fafanua. (alama 3)
  2. Eleza namna vipengele vifuatavyo vya kimtindo vilivyotumika katika shairi hili.
    1. Usambamba (alama 2)
    2. Aina za taswira (alama 3)
  3. Bainisha toni katika shairi hili. (alama 2)
  4. Fafanua mbinu mbili alizotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili. (alama 4)
  5. Ainisha bahari kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo; (alama 3)
    1. Mpangilio wa vina
    2. Mizani
    3. Mpangilio wa maneno
  6. Fafanua muundo wa shairi hili. (alama 3)

MAJIBU

  1.    
    1. ukiukaji wa maadili ya kikazi
    2. majaji wanaostahili kutetea haki ni walaji rushwa
    3. madaktari hawawajibiki kwa matibabu na kuwa’ magonjwa hayatibiki
    4. madaktari wanakwerida kinyume na kiapo chao kwa kuweka pesa mbele.
    5. Licha ya mbwembwe nyingi za kiapo cha mawaziri, wana mikataba ghushi.
    6. Magavana wanatafuna nchi na kuwa haikaliki.
    7. Viongozi ni wanafiki hawaaminiki.
    8. Maraisi wanashabikia wizi.
    9. Waapaji ni wanafiki Zozote 3 x 1 =3
  2.           
    1.    
      • usambamba
      • Kila ubeti unaanza kwa neno kiapo
      • Sehemu ya utao ya mshororo wa tatu katika kila ubeti inarudiwa katika kimalizio
        alama 2 x 1 =2
    2.    
      • Taswira oni— kiapo cha mawaziri, shingo tai haitoki
      • Taswira sikivu- kwa mizinga na fataki
      • Taswira mwonjo- wengi wao ni walaji alama 3 x 1 = 3
  3. toni katika shairi
    1. Kulalamika- kuna ukosefu wa uwajibikaji kazini
    2. Kushtumu/ kusuta- majaji wanaostahili kutetea haki ni walajirushwa 1×2=2
  4. idhini/ uhuru wa mshairi
    1. Utohozi- feki
    2. Kuboronga sarufi- shingo tai haitoki
    3. Inkisari- wanosimama- wanaosimama alama 2x2=4
  5.      
    1. Mpangilio wa vina- ukara- vina vya nje vinatiririka ilhali vya ndani vinabadilika badilika
    2. Mizani- msuko- kimalizio kimefupishwa
    3. Mpangilio wa maneno- kikwamba- neno kiapo limetumika kuanzia mwanzo wa kila ubeti.
      Pindu- sehemu ya utao ya mshororo wa tatu katika kila ubeti inarudiwa katika kimalizio 3x1=3
  6.      
    1. shairi hili lina beti tano
    2. kila ubeti una mishororo minne
    3. lina pande mbili; ukwapi na utao
    4. kituo kimefupishwa
    5. vina vya nje vinatiririka ilhali vya ndani havitiririki
    6. mizani 16 kwa kila mshororo ila kwa kituo ni nane. Zozote 3x1=3

USHAIRI 12

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

Sahibu mwenda nyumbani, msalimu mke wangu
Mwambie ni kifungoni, huku kwa wazungu
Walonifunga katani, kutwaa uhuru wangu
Ila asihofu sana, nitarudi siku moja

Mwambie nawatamani, ninawahamu wanangu
Hata niwapo njozini, huwaona tu wanangu
Mavuno ya upeponi, ni sauti tu wanangu
Ila asihofu sana, nitarudi siku moja

Nina maradhi moyoni, niuhisio uchungu
Ni mateso mtimani, wala si vyao virungu
Nikiwaza kiamboni, huko makaoni kwangu
Ila asihofu sana, nitarudi siku moja

Mwambie anithamini, alitunze shamba langu
Lisitolewe rubuni, kwa yeyote mlimwengu
Kheri libaki porini, vimelea viwe chungu
Ila asihofu sana, nitarudi siku moja

Ukimuona hanani, hana chake wala changu
Sahibu mpe auni, kirudi takupa fungu
Wala usidai deni, kulitaka shamba langu
Ila asihofu sana, nitarudi siku moja

Sijui nikuamini, nikujuze siri yangu
Au nawe u mhuni, japo huna tena pingu
Nakwambia walakini, kam’manyishe mwenzangu
Ila asihofu sana, nitarudi siku moja

Kamwambe aole chini, chini ya ule mvungu
Kuna shimo kibulani, na ndani mna kijungu
Ya mumo humo mapeni, hiyo ndo akiba yangu
Ila asihofu sana, nitarudi siku moja

Asihofie katani, akumbuke yupo Mungu
Nitatoka gerezani, nipumue kula ndengu
Nitarudi na imani, japo yatande mawingu
Ila asihofu sana, nitarudi siku moja

Maswali

  1. “ila asihofu sana…”
    Fafanua kinyume kinachobainika katika dondoo hili kwa kumzingatia mtunzi wa shairi. (al. 6)
  2. Kwa kutoa mfano, eleza namna toni ya utunzi huu inakuza maudhui. (al. 2)
  3. Taja na ufafanue sifa zozote nne za mtunzi huyu. (al.4)
  4. Onyesha namna usambamba unajitokeza katika utunzi huu. (al. 2)
  5. Andika ubeti wa saba katika lugha nathari. (al. 2)
  6. Huku ukitoa mifano, eleza namna idhini ya kishairi ilivyotumika kukidhia mahitaji ya kiarudhi. (al. 2)
  7. Tambua nafsi neni na nafsi nenewa katika shairi. (al. 2) 

MAJIBU

  1. 'Kinyume katika dondoo : Ila asihofu sana: Sababu za kuhofu
    1. Amefungwa
    2. Anawakosa wanawe – anawaona njozini
    3. Ana maradhi
    4. Ana uchungu moyoni
    5. Huko gerezani anapigwa virungu
    6. Ana wasiwasi kuhusu shamba kutolewa rubuni
    7. Hamwamini anayetuma kwa mkewe
    8. Ana tumaini atarudi lakini hajui siku yenyewe
    9. Amenyimwa uhuru wake
      Zozote 6 x 1 =6
  2. Toni ya uchungu/huzuni/ - kunaonyesha hofu aliyonayo mtunzi kuonyesha wasiwasi wake.
    Kutaja toni x 1 kufafanua x 1 =2
  3. sifa za mtunzi
    1. Mwenye matumaini
    2. Ni mwajibikaji. Anajali familia/anajali hatima ya familia yake
    3. Mwenye mapenzi ya dhati – anaipenda familia yake
    4. Ana busara/hekima – ana akiba/ anatahadhari shamba lake lisije kupotea
    5. Ana mlahaka mzuri – ameunda urafiki na wenzake hadi anawatuma
    6. Ni mvumilivu – licha ya changamoto kifungoni hakati tama
    7. Mdadisi – anapekuapekua kama amwamini anayemtuma
    8. Mwenye kumbukizi – anakumbuka alikoficha pesa zake
    9. Ni mcha Mungu – anamshauri mkewe kuwa kuna Mungu
      4 x 1 =4
  4. Usambamba – urudiaji
    ubeti 2 ninawahamu wanangu
    huwaona tu wanangu
    ni sauti za wanangu x 2
  5. Mwambie mke wangu atazame mvunguni/ atapata shimo lililo na jumngu./ atapata ndani pesa ambazo nimehifadhi humo kama akiba/ asiwe na wasiwasi kwani ipo siku nirudi (1/2 x 4 = 2)
  6.                      
    1. Mkisari walonifunga – walionifunga – amefupisha ili apate wiano wa mizani
      - kam’manyishe – ukamumanyisha – kufupisha
      - ndo – ndiyo
    2. lahaja – aole – atazame – kupata uwiano wa mizani 2 x 1 =2
  7. Nafsi neni – mfungwa
    Nafsi nenewa – sahibu 2 x 1 =2

USHAIRI 13

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yaliyofuata.

Jambo lolote ni nia, kuweka yako azima,
Hasa ukikusudia, kulepuka la lawama,
Mola takusaidia, kila la ovu kuzama,
Ukiitaka salama, jua hasira hasara.

Hakika si masikhara, wa kale waliyosema,
Ni maneno ya busara, tena ni wasia mwema,
Kuwa hasira hasara, ghadhabu zisizokoma,
Ukiitaka salama, jua hasira hasara.

Mja katu haitaki, hasira kuziandama,
Punguza zako hamaki, moyo uwe na huruma,
Kwani zikizidi chuki, hapo huja uhasama,
Ukiitaka salama, jua hasira hasara.

Na uhasama ujapo, uadui kukwegema,
Hapo ndipo upatapo, kukufikia zahama,
Mwisho ndipo ujutapo, ikabaki kulalama,
Ukiitaka salama, jua hasira hasara.

La usawa sinyamai, kukweleza ni lazima
Chuki nyingi hazifai, hebu tuliza mtima,
Waweza tupa uhai, au nyingi darahima,
Ukiitaka salama, jua hasira hasara.

Upunguze wako mori, mwana na mtu mzima,
Upoze moyo wa hari, hasira zipate hama,
Subira huvuta heri, ikaleta na neema,
Ukiitaka salama, jua hasira hasara.

Kifaya nilipofika, hapa ndiyo kaditama,
Sahibu wasia shika, hasira si kitu chema,
Mtegemee Rabuka, atakulinda Karima,
Ukiitaka salama, jua hasira hasara.

MASWALI

  1. Toa anwani mwafaka kwa shairi hili. (Al. 1)
  2. Ainisha shairi hili kwa kuzingatia:- (Al. 4)
    1. Mishororo
    2. Vipande
  3. Fafanua umbo la shairi hili. (Al. 4)
  4. Dhihirisha matumizi ya idhini ya mshairi katika shairi hili. (Al. 3)
  5. Andika ubeti wa sita kwa lugha tutumbi. (Al. 3)
  6. Eleza toni ya shairi hili. (Al. 2)
  7. Ni nani nafsineni katika shairi hili? Eleza (Al. 1)
  8. Fafanua msamiati ufuatao kama ulivyotumika shairini. (Al. 2)
    1. Mtima
    2. Darahima

MAJIBU

  1.  
    • Kimuundo ni shairi. Unaweza pia kuchukuliwa kama utendi (shairi la ushujaa) kwa sababu unazungumzia sifa za shujaa na vita alivyopigana.
    • Kimaudhui ni sifo/wimbo wa sifa- unamsifu shujaa
  2.  
    1. Matukio ya ajabu kama vile.
      • Kusema na miungu alipozaliwa.
      • anayesema ana nguvu za kipekee japo ni kilema.
      • Anayesema kazaliwa akishika mkuki
    2. Matumizi ya chuku kama vile:
      • maadui elfu kufa anaposhika silaha.
      • Kufagia vijiji vinane kwa pigo moja la kiganja chake.
    3. Utungo unahusu shujaa wa vita- amegpigana vita vingi visivyohesabika
    4. Anayesemwa amezungukwa na migogoro – mahasidi waliochukua mashamba na wasaliti.
    5. Utungo umechanganya historia na mambo ya kidini – anazungumza na miungu anapozaliwa – haya ni mambo ya kiimani.
  3.  
    1. kejeli/stihizai – anaitwa jana la ajabu.
    2. chuku:
      • Kijiji kizima kuja kuona mtoto
      • Maadui elfu kufa kwa anayesemwa kushika silaha
      • Mwili kuwa na nguvu za majagina mia moja
    3. ritifaa – anazungumza na mahasidi ambao hawapo kana kwamba wapo.
    4. tashbihi:
      • Maadui wamwonapo hutetemeka kama jani
      • Kuwayeyusha kama barafu
    5. sitiari:
      • umekuwa nahodha
      • Akili yako sumaku
    6. usambamba:
      • Likalovya change kidari
      • Likanavya chako kipaji
    7.  taswira:
      • Mama alivyolia na kujilovya machozi na kumlovya mwanawe
      • Alivyopigana na utawala wake au jamii yake. Kijiji kizima kinavyomiminika kwake nyumbani.
  4.        
    1. Waume huoa wake wengi – Anasema, Uke wenza ukamhimiza kuchukua buruji kueneza habari.
    2. vilema walitupwa kichakani – Ilosema kwa moja kauli utokomezwe chakani utupwe.
    3.  Ni wafugaji – Kutupoka mifugo.
  5. Anayeimba ni mama. Anasema nilipokuopoa.
  6. tofauti kati ya mighani na visasili;
    • Mighani husimulia kuhusu mashujaa, ilhali visasili husimulia asili ya vitu.
    • Mighani husimulia historia ya jamii, ilhli visasili husimulia mianzo ya vitu au mambo ulimwenguni.
    • Katika mighani, wahusika ni mijagina, ilhali katika visasili wahusika ni vitu tofauti kama vile miungu, wanyama na binadamu.
    • Mighani hueleza sifa za majagina , ilhali visasili hueleza mianzo ya desturi.

USHAIRI 14

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Ngakua na mto, ya kuonea
Ngalisana kito, cha kuchezea
Kilicho kizito, cha kuelea
Kikamuenea, akivae.
Makusudi yangu, Ngaliandaa
Ngafinyanga chungu, cha mduwaa
Ngatia vitangu, vinavyong’aa
Ili ziwe taa, kwa apikae.
Mkungu wa tano, wa mduwara
Ulo bora mno, kisha imara
Ulo na maono, kuwa ni dira
Kwenye barabara, itindiae
Ngaomba baraka, kwake Rabana
Punje za nafaka, kila aina
Chunguni kuweka, kwa kulingana
Hajaangu suna, yule alae.
Ngalifanya bidii, kwenda mwituni
Sio kutalii, kukata kuni
Ya miti mitii, huko jikoni
Isio na kani, ni iwakae.
Kwa yangu mabega, nikathubutu
Ngabeba mafiga, yalo matatu
Bila hata woga, kwenye misitu
Simba tembo chatu, sinitishie.
Miti yenye pindi, na jema umbo
Ngajenga ulindi, mwema wimbombo
Fundi aso fundi, penye kiwambo
Moyo wenye tambo, apekechae.
Singaajiri, ngachimba mimi
Kisima kizuri, cha chemichemi
Maji ya fahari, ya uzizimi
Jua la ukami, siyaishae
Tamati nafunga, kwa kuishia
Mato ndo malenga, kanikimbia
Nahofu kutunga, mabeti mia
Asije chukia, ayasomae.

  1. Fafanua ujumbe wa shairi hili. (alama 2)
  2. Kwa kurejelea ubeti wa pili, eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi alioutumia mshairi. (alama 4)
  3. Andika ubeti wa saba kwa lugha nathari. (alama 2)
  4. Fafanua muundo wa ubeti wa nane (alama 2)
  5. Bainisha mbinu mbili za kimtindo katika shairi hili. (alama 2)
  6. Eleza aina tatu za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 3)
  7. Fafanua aina mbili za taswira zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 2)
  8. Eleza toni ya shairi hili. (alama 1)
  9. Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2)

MAJIBU

  1.      
    1. Shairi linazungumzia tatizo la upofu. mf. ngakuwa na mato.
    2. Kwamba mtu aliyepatwa na tatizo la upofu huwa hawezi kufanya mambo ambayo zamani aliyamudu bila tatizo.
      AU.
      Nafsineni inasikitikia hali ya kutomudu kujifanyia mambo kwa sababu ya upofu. 1x2= kutaja 1, kueleza 1
  2. Inkisari – imetumika ili kudumisha ulinganifu wa mizani, mfano: Ngaliandaa- ningaliandaa
    Ngafinyanga – ningalifinyanga
    Ngatia – ningetia
    Tabdila – imetumiwa ili kuleta urari na vina
    Mfano: Mduwaa – mduara
    apikae – apikaye
    vinavyong’aa – vinavyong’aa. 2x2=4 kutaja- 1, sababu 1
  3. Ningetumia miti iliyopinda na yenye umbo zuri kutengenezea kijiti. Ningekipekechea kijiti hiki kwenye tundu la wibombo mwema/mzuri kupekechea moto kwa ufundi mkuu kiwamboni. Ningekua bingwa ningekuwa na moyo shupavu na kupekecha moto/ningekuwa fundi stadi katika upekechaji wa moto. (2x1=1)
  4. Vipande viwili kila mshororo
    1. Mishororo minne
    2. Mshororo wa kwanza una mizani kumi, ilhali wa pili hadi wa nne una mizani kumi na moja. 2x1=2
  5.      
    1. Uradidi – ulo – ubeti 3
      mato – ubeti 1, 9
    2. Tashhisi – mato ndo malenga kanikimbia. 2x1=2
  6.    
    1. Urudiaji wa sauti – ubeti wa 1, a, a,
    2. Urudiaji wa silabi – ubeti wa 1 to, to, to
    3. Urudiaji wa maneno – ulo –ubeti wa 3
    4. urudiaji wa miundo sawa ya mistari
      ngalisana kito, cha kuchezea
      ngalifinyanga chungu cha mduwaa 3x1=3
  7. Taswira mguso – ngafinyanga chungu cha mduwa
    Taswira mwendo – ngafanya bidii, kwenda mwituni
    Taswira hisi – Nahofu kutunza, mahali mia, asije chukia ayasomae. 2x1=2
  8. Toni ya kuhuzunisha/masikito/kuhurumia/majuto
    Nafsineni inakosa/shindwa kufanya mambo mengi
    Maishani kwa sababu ya kukosa macho. 1x1=1
  9. Kipofu/mnyonge – asiye na uwezo wa kumudu/ kujifanyia mambo yake kwa sababu ya upafu. 1x2=2

USHAIRI 15

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Hizi bombo mwaanika, wa ndizini nashtuka,
Peupe mwazianika, kwenye jua kukauka,
Zingine zimeraruka, aibu zinatufika,
Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha.

Nako kule kwenye bafu, mwaziweka hizo chafu,
Hilo nalo nakashifu, mkitoa nitasifu,
Kuziweka maji chafu, hilo ndilo ninahofu,
Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha.

Kwenye meza wazileta, wana wenu wakipata,
Wageni wakijateta, aibu haitatupata?
Muondoeni utata, hizo zenu twazipata,
Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha.

Kwa heshima tudumuni, tufaapo za mwilini,
Tamaduni jifunzeni, msiige uzunguni,
Za bafuni zi jikoni, zi watoto makononi,
Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha.

Wino wangu kibindoni, nitatua tamatini,
Za ndani ziwe za ndani,msonyeshe hadharani,
Za bafuni si jikono, msiweke kabatini,
Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha.
MASWALI

  1. Pendekeza kichwa mwafaka katika shairi hili.    (alama 1)
  2. Eleza toni ya shairi hili.   (alama 1)
  3. Tambua nafsineni katika shairi. (alama 1)
  4. Jadili matumizi ya mitindo ifuatayo ya lugha katika shairi hili.
    1. Kinaya     (alama 2)
    2. Usambamba   (alama 2)
    3. Balagha          (alama 1)
  5. Onyesha kuwepo kwa uhuru ufuatao katika shairi.     (alama 3)
    1. Tabdila
    2. Kubananga sarufi
    3. Inkisari
  6. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha mjazo.  (alama 4)
  7. Eleza muundo wa shairi hili.  (alama 5)

MAJIBU

  1. Pendekeza kichwa mwafaka.
    • Aibu, Aibu kwetu
  2. Eleza toni ya shairi hili
    • Toni ya kukasifu/kushtumu/kukejeli mienendo ya kutojali.
    • Toni ya kughadhabika Kwa kutojali.
    • Toni ya kushauri kuhusu heshima na usiri.
  3. Tambua nafsineni wa shairi
    • Mhusika ambaye amepata aibu kutokana na mienendo ya watu kuanika mavazi ovyo ambayo anahisi ni vibaya.
  4. Jadili matumizi ya mitindo ifuatayo
    1. Kinaya
      • Ni kinaya kuwa angependa mavazi fulani yafichwe ilhali yamefichwa bafuni.
      • Ni kinaya kuwa anataka zikauke bila kuanika /ilhali zimefichwa.
      • Ni kinaya kuwa wageni wanaibika ilhali wenyewe huzitumia na huanika kwao
    2. Usambamba
      • Miundo sawa  ya mistari/mishororo-anikeni kwa kuficha,z ndani mkisafisha.
      • Urudiaji wa maneno –anika,kuficha.
      • Urudiaji wa silabi-ka(ubeti wa kwanza) fu(ubeti wa pil) ta (ubeti wa tatu)
    3. Balagha
      • Ubeti wa mwisho mshororo wa pili-aibu haitatupata?
  5. Onyesha kuwepo kwa uhuru ufuatao katika shairi
    1. Tabdila – muondoeni badala ya mwondoeni.
    2. Kubananga sarufi - anikeni kwa kuficha,za ndani mkisafisha. Badala ya mkisafisha za ndani mzianike kwa kuficha.
    3. Inkisari - tufaapo badala ya tunapofaa.
  6. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya mjazo/Nathari.
    • Mshairi anasema kuwa nguo za ndani zinazoanikwa ovyo/popote,watoto/wana huzipata na kutembea nazo hata mezani kwa wageni.Hili huleta aibu kubwa na hivyo hushauri watu waanike kwa tahadhari.
  7. Eleza muundo wa shairi hili
    • Shairi hili lina beti tano.
    • Kila ubeti una mishororo minne.
    • Shairi hili lina kibwagizo ambacho ni :anikeni kwa kuficha , za ndani mkisafisha.
    • Idadi ya mishororo inatoshana kaika kila mshororo;kumi na sita.
    • Kila mshororo una vipande viwili, ukwapi na utao.
    • Vina vyake vinatofautiana  kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.

USHAIRI 16

YALIMWAGIKA

Lilianza kama wazo, nikawaza,
     Niwe na watoto,
Si vikwazo, ghafla mama yao akapatikana,
    Kwa rutuba yake,
       Akavimba
      Kumbe ni mapacha,
          furaha!

     Majina walishapewa,
Imani kudumu, watazaliwa,
       Tungo wakatungiwa,
         Amani na Imani,
    Baba yao ni malenga
        Anatayeita maneno.
         Maneno yanaitika.
               Nikasubiri.
Wazazi walitamani kupakata,
              Amani na Imani
Iwe yao burudani, siyo kama zamani
           Wachezee zuliani.
         Baba niwaweke kifuani
 Na migongoni bila susu, kwa mama yao
   Si mtoto hutizama kisogo cha ninake?
             Tukangoja!
Furaha kote nyumbani iliwatanda,
   Kuyaona makinda yao, kwa kitanda,
   Wadondokwe udende, wawapende!
Mama anyonyeshe, kiwatazama machoni,
   Kuwagusa mashavuni, waliapo.
Watulie Amani na Imani.

  Ukutani ni kiwimbo, baba alishawatungia,
Kushotoni ni wa kike, kuumeni kijanadume
             Watulie, Baba yao aliwazia
               Wazo likaanza kupokwa.
                   Hospitali wakiwasili.

Wiki zikajenga miezi
  Tamati ikajongea
Kawanunulia mavazi
     Walifaa kuvaa
       Hawakuvaa!
Vijulanga miezi saba, pukachaka!
   Kifo ni mwewe, kikaninyakulia.
          Amani na Imani.
                  Tunalia!
           Pema peponi wanetu!
MASWALI

  1. Eleza jinsi usimulizi ulivyotumika kwenye shairi.   (alama 1)
  2. Eleza sifa tatu zinazoafiki shairi hili kuwa huru.      (alama 3)
  3. Shairi hili ni la tanzia. Thibitisha.                             (alama 1)
  4. Tambua mandhari ta tanzia.       (alama 1)
  5. Tambua nafsineni kwenye ubeti wa kwanza.     (alama 1)
  6. Eleza toni ya shairi.     (alama 2)
  7. Onyesha mifano miwili ya matumizi ya sadfa katika shairi.   (alama 3)
  8. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha tutumbi.     (alama 4)
  9. Eleza maana ya msamiati huu kulingana na shairi.   (alama 4)
    1. Vijulanga
    2. Susu
    3. Akavimba
    4. Kiwimbo

MAJIBU

  1. Eleza jinsi usimulizi ulivyotumika kwenye  shairi.
    • Ushairi umesimulia safari kabla ya ndoa na katika ndoa.
  2. Eleza sifa tatu  zinazoafiki shairi hili kuwa shairi huru.
    • Idadi ya mishororo katika kila ubeti si sawa.
    • Idadi ya vipande katika kila mshororo si sawa.
    • Idadi ya mizani katika kila mshororo  inatofautiana.
    • Limechukua miundo mbali mbali lilivyoandikwa.
    • Shairi hili halina kibwagizo.
    • Vina vyake vinachanganywa/halina mtiririko wa vina.
    • Shairi hili lina alama nyingi za uakifishaji.
  3. Shairi hili ni tanzia
    • Kuna kifo cha mapacha waliotarajiwa kuzaliwa na walisuburiwa sana na wazazi zao.
  4. Tambua mandhari ya tanzia
    • Hospitalini ndiko walikofia mapacha.
  5. Tambua nafsineni kwenye ubeti wa kwanza
    • Baba / bwana mtarajiwa/mwanamume.
  6. Eleza toni ya  shairi.
    • Toni ya huzuni /majonzi kutokana na kifo cha mapacha Amani na Imani
  7. Onyesha mifano miwili ya matumizi ya sadfa  katika shairi.
    • Baba anawaza kuhusu watoto na kumpata mke papo hapo wa kuoa.
    • Msemaji anasema  akataka’ watoto’ na ghafla  ujauzito unakuwa wa mapacha.
    • Watoto wanapewa majina Imani na Amani na baadaye mimba kugundulika ni ya mapacha  kiume na kike.
  8. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha tutumbi.
    • Muda uliendelea kusonga wakisubiri watoto wao kuzaliwa.
    • Wakanunuliwa mavazi mbalimbali wakitarajiwa kuwapokea japo halikutimia.watoto wakafa  mimba ikiwa ya miezi saba  na kuombolezwa.
  9. Eleza maana ya misamiati ifuatayo.
    1. Vijulanga -Vitoto
    2. Susu-kitambaa cha kuzuia haja za mtoto.
    3. Akavimba-akawa mjamzito
    4. Kiwimbo.- wimbo mfupi

USHAIRI 17

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Weusi likosa nini?

  1. Sie watu weusi, lipataje weusi?
  2. Kila kitu kibaya, hupewa sifa mbyaya.
  3. Sifa hii ‘eusi’, yaleta wasiwasi.
  4. Rangi hii hakika, ni wapi ilitoka?
  5. Ibada za Weusi, harusi kuzitusi.
  6. Kama mtu mweusi, Lusifa ni mweusi
  7. Ibada ya Weupe, hupokewa peupe
  8. Adamu naye Hawa, weupe walipewa
  9. Yesu Mwana wa Mungu, alikuwa Mzungu
  10. Malaika wa Mungu daima ni Wazungu
  11. Mweusi ti hatendi, silaumiwe pindi
  12. Mweusi duniani, likosa kitu gani?
  13.  Mweusi jilaumu, measi yako damu.
  14. Mweusi umeiga, hata ya kutoiga
  15. Asojali mkuu, atavunjika guu
  16. Baa mejikatia, nani takulilia?

MASWALI:

  1. Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu yako. (alama 2)
  2. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
  3. Toa mifano miwili ya matumizi ya mbinu ya inkisari katika shairi hili na uyaandike katika
  4. Eleza maudhui ya shairi hili. (alama 2)
  5.  Ni nini dhamira ya mtungaji wa shairi hili? (alama 2)
  6. Kwa kutoa mifano matatu, eleza matumizi ya lugha mkato. (alama 6)

MAJIBU

  1. Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu yako. (alama 2)
    • Shairi hili ni la tathmina kwa kuwa beti zake ni za mstari mmoja mmoja ambao una maana kamili. Ni la bahari ya manthawi kwa sababu mistari yenyewe imagawanywa katika vipande viwiliviwili.
  2. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
    • Shairi hili lina beti kumi na sita za mshroro mmoja mmoja. Kila mshororo una ukwapi na utao, yaani, vipande viwiliviwili.
    • Mishororo ni ya urefu wa mizani saba bsaba , jumla, kumi na nne. Beti za shairi hizi zina vina viwili kila mmoja, yaani, cha ukwapi na cha utao, ambavyo vinafanana lakini vinabadilika kutoka ubeti hadi mwingine. Kwa mfano, vina vya ubeti wa kwanza ni ‘si’ bali vya ubeti wa pili ni ‘ya’
    • Umbo kwa jumla ni:
      -7si, -7si. Ubeti wa kwnza
      -7ya, -7ya. Ubeti wa pili
  3. Toa mifano miwili ya matumizi ya mbinu ya inkisari katika shairi hili na uyaandike katika lugha ya kawaida. (alama 4)
    • Mifano ya matumizi ya inkisari katika shairi ni:
      Neno badala ya
      Lipataje tulipataje; tuliupataje
      Naye na yeye
      Silaumiewe asilaumiwe
      Likosa alikosa
      Jilaumu ujilaumu
      Measi umeasi
      Asojali asiyejali
      Mejitakia umejitakia
      Takulilia atakayekulilia
  4. Eleza maudhui ya shairi hili. (alama 2)
    • Maudhui ya shairi hili ni malalamiko. Mweusi analalamika juu ya rangi nyeusi aliyopewa na hasa jinsi inavyohusishwa na jambo lolote baya kiasi cha rangi nyeusi kuleta wasiwasi.
    • Analalamika kuwa ibada za watu weusi hutukanwa kwa raha huku za weupe (wazungu) zikikubaliwa hadharani.
    • Manung’uniko yanasema Mweusi (Mwafrika) amefananishwa na Lusifa (Shetani) huku Adamau na Hawa, malaika wa Mungu na Yesu Mwana wa Mungu wamelinganishwa na Weupe.
    • Kuna sikitiko ya kuwa Mwafrika atendapo jambo hulaumiwa wakati huo.
    • Hatimaye ni shutuma dhidi ya Mwafrika huyo huyo ya kuwa ajilaumu yeye mwenyewe kwa kuiasi damu yake (asili yake); kuiga ovyo na kutojali ya mkuu.
  5. Ni nini dhamira ya mtungaji wa shairi hili? (alama 2)
    • Dhamira ya mtungaji wa shairi hili ni kuuupinga ubaguzi dhidi ya Wafrika kwa kuwapndelea
    • Wazungu. Tena ni kuwashauri watu weusi (Wafrika) wasiikane asili yao na mambo yao kwa kuiga yale ya watu weupe (Wazungu) kwani wanajiletea balaa wao wenyewe.
  6. Kwa kutoa mifano matatu, eleza matumizi ya lugha mkato. (alama 6)
    • Mifano ya matumizi ya lugha ya mkato ni: Ubeti wan ne, ‘Rangi hii hakika ni wapi ilitoka’ badala ya ‘Kwa hakika, rangi hii ilitoka wapi?’
    • Ubeti wa kumi na moja, utao, ‘silaumiwe pindi’ badala ya ‘pindi asilaumiiwe’. Ubeti wa kumi na tatu, utao, ‘measi yako damu’ badala ya ‘umeaiasi damu yako’ Ubeti wa kumi na sita, utao nani takulilia? Badala ya ‘ni nani atakayekulilia?’

USHAIRI 18
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yafuatayo. 

Nikumbuke mwanangu, 
Kila asubuhi unapoamka 
Kwenda kazini, 
Unapochukua sabuni ya kunukia, 
Na dodoki jororo. 

Na kopo la koligeti,
Kwenda kukoga hamumuni,
Penye maji ya bomba, 
Yaliyochujwa na kutakaswa, 
Mororo… 

Kumbuka nyakati zile, 
Za staftahi ya sima na mtama, 
Ndizi na nagwa, 
Kwa mchicha na kisamvu, 
Na ulipokwenda choo,
Ulilia kwa uchungu 

Nikumbuke,
Unapotoka nyumbani asubuhi maridadi, 
Katika suti ya moto,
Miwani ya pembe, 
Viatu vya Parisi, 
Saa ya dhahabu, 
Unapong’oka kwenda kazini, 
Katika Volvo, 
Katika njia iliyosakafiwa 

Kumbuka, 
Nyakati zile,
Mimi na mamako, 
Tulinyojidamka, 
Mara tu kwale wa kwanza,
Alipoanza kukoroma, 
Jogoo wa kwanza hajawika, 
Mimi nikachukua mundu na panga, 
Mamako jembe na shoka,
Tukaelekea porini, 
Kufyeka na kuchimbua 

Nahubaki wajiandaa kwenda shule… 
Nikumbuke, 
Saa za jioni, 
Unapovalia kitanashati. 

  1. Thibitisha kuwa utungo huu ni shairi (alama 2) 
  2. Fafanua toni ya utungo huu. (alama 1) 
  3. Huku ukitoa mifano,linganua kati ya mistari toshelezi na mistari mishata. (alama 4) 
  4. Eleza maudhui yoyote matatu yanayojitokeza kwenye shairi. (alama 3)
  5. Kwa kutoa mifano tambua aina nne za taswira. (alama 4)
  6. Eleza mbinu za kimtindo zilizotumika katika shairi hili kando na taswira. (alama 4) 
  7. Tambua nafsi neni katika shairi hili na udhibitishe. (alama 2)

MAJIBU

  1. Umegawika katika beti 
    Kila ubeti una mishororo ingawa idadi inatofautiana katika kila ubeti (2 x 1= 2) 
  2.      
    1. Toni ya kusihi-nikumbuke mwanangu 
    2. Kushauri /wasia/nasaha-nikumbuke (1 x 1 =1) 
  3. Mistari toshelezi ni mistari iliyokamilika kimaana ilhali mistari mishata ni mistari mishata  isiyokamilika kimaana. 
    Mifano;mstari toshelezi-Nikumbuke mwanangu  mstari mshata-staftahi ya saa nane alasiri 
    (kulinganua, alama 2, mifano 2 x 2=4) 
  4. Umaskini-Wazazi wa mnenewa walikuwa wakiishi maisha ya uchochole huku wakifanya  kazi ya ukulima. 
    Mapenzi ya wazazi kwa watoto-wazazi wanawajibika kwa kuhakikisha kwamba wanalisha na kusomesha watoto wao. 
    Kazi/ajira-baba anamwambia mwanaye kwamba amkumbuke anapoenda kazini. 
    Elimu-nahubaki wakijiandaa kwenda shule (zozote 3 x 1 = 3) 
  5.        
    • Taswira mnuso mf. Sabuni ya kunukia
    • Taswira hisi mf ulilikia kwa uchungu
    • Taswira sikivu mf. Jogoo wa kwanza hajawika
    • Tawsira mwendo mf. Tukaelekea porini n.k
      (4x 1 = 4) 
  6. mbinu rejeshi/kisengere nyuma Kumbuka nyakati zile
    • utohozi Parisi  koligeti-
    • Mdokezo mf. Mororo... 
    • Chuku mf maji yaliyochujwa na kutakaswa
    • Takriri mf. Nikumbuke 
    • Usambamba mf. Unapotoka, unapochukua, unapong’oka ( 1x4 =4)
  7. nafsi neni – mzazi wa kiume – (mimi na mamako)
    (kutaja 1 ithibati 1)

USHAIRI 19

UMOJA WA MENDE 
Wadogo tena wadudu, ila wajua kuvuna, wasikokupanda,
Wakija utawabudu, kwa sura tunafanana, wanavyojipenda,
Nyoyo zidunde dududu! Watabaki kujibana, waje kukuponda,
          Mende wanao umoja, waonapo pana lishe.

Huja usiku usiku, waja wanapojilaza, wasionekane,
Huwacha yao shauku, ila wanapeleleza, wasijulikane,
Wametafuna mabuku, akili wamezijaza, nd’o tusiwaone,
           Mende wanao umoja, waonapo pana lishe.

Wao ni kama mapanya, huuma kipulizia, kukutulizisha,
Wanapenda kudanganya, huku mejinyamazia, kukupofuzisha,
Usiwaone waminya, kwa kutukandamizia, kwani wanachosha,
             Mende wanao umoja, waonapo pana lishe.

Wao huja taratibu, kwa vipindi vya misimu, vijulikanavyo,
Hurudi bila aibu, vitano vikishatimu, tuwapendezavyo,
Wakatutia ububu, kutulisha na vya sumu, watuongozavyo,
             Mende wanao umoja, waonapo pana lishe.

Tumbo lake la kiriba, tayari limeshashiba, linamusokota,
Lataka tena kushiba, wenye nyumba tuna tiba, tutamuokota,
Wakishatupa kibaba, kina mama kwa wababa, si tunajitata,
               Mende wanao umoja, waonapo pana lishe.

Mwishowe tunafungua, apite akaingie, ndani kabatini,
Humo mlimo murua, twataka atuchungie, vyetu vya thamani,
Mwishowe anararua, ndani amejifungie, wamtakiani?
                Mende wanao umoja, waonapo pana lishe.

Hubeba na familia, wana na bibi za kwake, wale kwa pamoja,
Nasi tukivumilia, kufikike kule kwake? Ng’o! sekunde moja,
Hadi ije kufikia, kuosha kabati lake, hapa tu pamoja,
                Mende wanao umoja, waonapo pana lishe.

Kachukuwe yake dawa, mende tukawakatae, tukawafukuze,
Tuseme tunazo mbawa, nd’o mende tuwakomee, siye tujikuze,
Tuwang’atue machawa, tuseme tuondokee, tukawachukize,
                 Mende na wao umoja, tuje wapa redikadi.
(Kutoka: Meja S. Bukachi – Diwani ya Kupe)

MASWALI

  1. Tambua mende wanaorejelwa na mshairi. (Alama 1)
  2. Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili. (Alama 1)
  3. Nani nafsi nenewa katika shairi hili? (Alama 1)
  4. Taja tamathali za lugha zilizotumika katika shairi hili. (Alama 2)
  5. Fafanua uhuru wa ushairi alioutumia malenga. (Alama 2) 
  6. Weka shairi hili katika bahari mbalimbali. (Alama 3)
  7. Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (Alama 4)
  8. Tambua mambo manne anayolalamika nafsi neni kuhusu mende. (alama 4)
  9. Vifungu vifuatavyo vina maana gani katika shairi? (alama 2) 
    1. vitano vikishatimu
    2. Tuwang’atue machawa

MAJIBU

  1. Tambua mende wanaorejelwa na mshairi. (Alama 1)
    • Wanasiasa/ viongozi wa kisiasa
  2. Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili. (Alama 1)
    • Kuonesha jinsi wanasiasa wanavyowalaghai wananchi kabla ya kuanza kuwanyonya. 
  3. Nani nafsi nenewa katika shairi hili? (Alama 1)
    • Wananchi/ raia
  4. Taja tamathali za lugha zilizotumika katika shairi hili. (Alama 2)
    • Jazanda- mende- wanasiasa.
    • Kinaya- mende huja kwa upole ila ni hatari.
    • Taswira- huja usiku usiku.
    • Tashbihi- wao ni kama mapanya.
    • Balagha- kufika kule kwake?                 (Zozote 2×1= 2)
      Mtahiniwa lazima atoe mfano katika shairi ndipo atuzwe alama kamili.
  5. Fafanua uhuru wa ushairi alioutumia malenga. (Alama 2)
    • Kufinyanga sarufi/ msimbo- yao shauku- shauku yao.
    • Inkisari- mejinyamazia- wamejinyamazia
    • Tabdila- kachukuwe- kachukue    (Zozote 2×1= 2)
      Mtahiniwa lazima atoe mfano katika shairi ndipo atuzwe alama kamili.
  6. Weka shairi hili katika bahari mbalimbali. (Alama 3)
    • Ukawafi- mishororo yake imegawika katika vipande vitatu isipokuwa mshororo wa nne. 
    • Ukaraguni- vina vyako vyote vinabadilikabadilika kutoka ubeti hadi mwingine.
    • Msuko- mshororo wa mwisho umefupishwa.     (Zozote 2×1= 2)
      (kutaja ½ kueleza ½ )
  7. Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (Alama 4)
    Wao ni kama mapanya ambao huuma na kupuliza ili kukutuliza. Wanapenda kudanganya huku wamejinyamazia ili kukupofusha.
    Usiwaone wanaminya kwa kutukandamiza kwani wanachosha. Mende wana umoja waonapo pana lishe.

    (matahini ahakiki kazi ya mtahiniwa)
  8. Tambua mambo manne anayolalamika nafsi neni kuhusu mende. (alama 4)
    • Wanavuna wasikopanda.
    • Wanaponda watu.
    • Hawataki hila zao zionekane.
    • Huuma wakipulizia.
    • Wanapenda kudanganya.
    • Wanatukandamiza na kutuchosha.
    • Huwaonga wananchi.
    • Hujificha wapatapo kura.
    • Hurarua kila kitu bila kujali wananchi.    (Zozote 4×1= 4)
  9. Vifungu vifuatavyo vina maana gani katika shairi? (alama 2) 
    1. vitano vikishatimu- baada ya miaka mitano
    2. Tuwang’atue machawa - tuwaondoe uongzini

USHAIRI 20

WASIA

Huno wakati mufti, vijana nawausia
Msije juta laiti, mkamba sikuwambia
Si hayati si mamati, vijana hino dunia
Uonapo vyang`aria, tahadhari vitakula

Japo aula kushufu, na machoni vyavutia
Dunia watu dhaifu, yaugua nasikia
Vijana nawasarifu, falau mkisikia
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

Jepusheni na zinaa, mlale penye sheria
Msije andama baa, makaa kujipalia
Jepusheni na zinaa, madhara kukadiria
Uonapo yyang’aria, tahadhari vitakula.

Ngawa waone wazuri, nadhifu kukuvalia
Wajimwaie uturi, na mapoda kumichia
Si mlango nyumba nzuri, ngia ndani shuhudia
Uonapo vyang’aria , tahadhari vitakula.

Wawapi leo madume, anasa walopapia?
Wamepita ja umeme, leo yao sitoria
Shime enyi wana shime, bora kumcha Jalia
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula

Nambie faida gani, nambie ipi fidia
Upatayo hatimani, waja wakikufukua
Ila kufa kama nyani, kasoro yako mkia
Uonapo vyang`aria, tahadhari vitakula.

Vyatiririka tariri, vina vyanikubalia
Alo bora mshairi, pa tamu humalizia
Nahitimisha shairi, dua ninawapigia
Uonapo vyang’aria , tahadhari vitakula.

Ewe Mola mtukuka, si shaka wanisikia
Wakingie wanarika, na anasa za dunia
Amina wangu Rabuka, dua yangu naishia
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

MASWALI:

  1. Ni ujumbe gani wanaopewa vijana kupitia shairi?. (alama 4)
  2. Bainisha tamathali mbili za usemi katika shairi hili. (alama 2)
  3. Eleza bahari ya shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo. (alama 2)
    1. idadi ya vipande katika mshororo
    2. mpangilio wa vina katika beti.
  4. Eleza mbinu zozote mbili za kishairi zilizotumika katika shairi hili. (alama 2)
  5. Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari (alama 4)
  6. Eleza toni ya shairi hili. (alama 1)
  7. Tambua: (alama 2)
    1. Nafsi neni
    2. Nafsi nenewa
  8. Eleza umuhimu wa mbinu ya kimtindo iliyotumika katika ubeti wa tano. (alama 2)
  9. Eleza maana ya msamiati: ‘aula’ (alama 1)

MAJIBU

  1. Ni ujumbe gani wanaopewa vijana kupitia shairi?. (alama 4)
    • Kujitahadharisha na vyote vinavyong’aa sababu vinadhuru.
    • Kujiepusha na zinaa.
    • Wasifikirie wanaovalia kinadhifu na kujipodoa ndio wazuri na kuwaandama.
    • Wasiandame / Kupapia anasa.
    • Kumcha Jalia.
    • Kuvumilia na kujikaza. (zozote 4 x1 = 4)
  2. Bainisha tamathali mbili za usemi katika shairi hili. (alama 2)
    • Tabaini – si hayati , si mamati.
    • Msemo – Makaa kujipalia
    • Kaza kamba.
    • Mdokezo wa methali – si mlango nyumba nzuri (zozote 2x1 = 2)
  3. Eleza bahari ya shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo. (alama 2)
    1. idadi ya vipande katika mshororo
      Mathinawi - migao miwili katika kila mshororo. (alama 1)
    2. mpangilio wa vina katika beti.
      Ukara – vina vya ndani vinatofautiana lakini vya nje vinafanana. (alama 1)
  4. Eleza mbinu zozote mbili za kishairi zilizotumika katika shairi hili. (alama 2)
    • Tabdilia – huno – huo.
    • Inkisani – Mkemba – mkaamba
    • Alo – aliye
    • Ngia – ingia ndani
    • -Utohozi – sitoria
    • Lahaja – hino
    • Kuboronga sarufi – makaa kujipalie. (alama 2x1)
  5. Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari (alama 4)
    • Ingawa vitu vitaonekana na kuvutia machoni, dunia ina udhaifu na maovu mengi. Vijana
    • nawasihi iwapo mtanisikia , tahadhari
    • na vyote vinavyong’ara kweli
    • vinawezeza kukudhuru.
  6. Eleza toni ya shairi hili. (alama 1)
    • Kushauri – mashauri anawashauri vijana kujihadhari na dawa za kuleya
  7. Tambua: (alama 2)
    • Nafsi neni – mshauri /mzazi /mhenga.
    • Nafsi nenewa – Vijana.
  8. Eleza umuhimu wa mbinu ya kimtindo iliyotumika katika ubeti wa tano. (alama 2)
    • Balagha – wawapi leo madume, anasa walopapia?
    • Umuhimu – kuibua hisia za nafsi nenewa kuhusu kupapia anasa na raha.
  9. Eleza maana ya msamiati: ‘aula’ (alama 1)
    Aula – bora nzuri.

USHAIRI 21

Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuatia.

Tusitake kusimama, bila kwanza kutambaa
Au dede kuwa hima , kabula hatujakaa
Tutakapo kuchutama, kuinama inafaa
Tujihimu kujinyima, makubwa kutoyavaa

Tusitake kuenenda , guu lisipokomaa
Tujizonge na mikanda, inapochangiza njaa
Na mazuri tukipenda , ni lazima kuyandaa
Tujiase kujipinda , kujiepusha na balaa.

Tusitake uvulana , au sifa kuzagaa
Tukishikiye nyonga sana, tunuiyapo kupaa
Kama uwezo hapana , tutolee dagaa
Tujiase hicho kina, maji yanapojaa

Tusitake vya wenzetu ,walochuma kwa hadaa
Wanaofyatua vitu, na kisha vikasambaa
Uwezo hatuna katu, umaskini fazaa
Tujihimu kula vyetu, siendekeza tamaa.

Mtaka kuiga watu , hufata kubwa rubaa
Vyao vijalie kwetu , vifaa vingi vifaa
Tunamezwa na machatu, tusibakishwe dhiraa
Tujihimu kilo chetu, hata kama twapagaa.

Maswali;

  1. Tambua mkondo wa shairi hili.(alama 2)
  2. Tambua bahari ya shairi kwa kuzingatia ;
    1. vina
    2. mishororo
    3. Vipande kaitika kila mshororo.( alama 6)
  3. Ni nini dhamira ya shairi hili.(alama 2)
  4. Thibitisha shairi hili ni la kiarudhi. (alama 4)
  5. Kwa kutolea ithibati ni ni uhuru gani wa ushairi uliotumika katika shairi hili.(alama 4)
  6. Eleza dhima urudiaji katika shairi hili.(alama 2)

MAJIBU

  1. Tambua mkondo wa shairi hili.(alama 2)
    • Hili ni shairi la arudhi-la kimapokeo. - alama 2
  2. Tambua bahari ya shairi kwa kuzingatia;
    1. Vina
      • Ni shairi la ukara kwani  vina vya kati vinabadilika badilika na vya mwisho havibadiliki.-(alama 2)
    2. mishororo
      • Ni shairi la tarbia-lina mishororo minne katika kila ubeti (alama 2
    3. Vipande kaitika kila mshororo
      • Hili ni shairi la mathinawi-kila mshororo una vipande viwili (alama 2)
  3. Ni nini dhamira ya shairi hili.(alama 2)
    • Dhamira ya shairi hili ni tahadhari dhidi ya tama ya kuiga watu wengine kabla ya kupata vitu tunavyovitaka. (alama 2)
  4. Thibitisha shairi hili ni la kiarudhi. (alama 4)
    • Lina mishororo minne katika kila ubeti
    • Lina vipande viwili katika kila mshororo
    • Lina vina 
    • Limegawika katika beti     alama 4
  5. Kwa kutolea ithibati ni  ni uhuru  gani  wa ushairi uliotumika katika  shairi hili.(alama 4)
    • tabdila-kabula-kabla, tushikiye-tushikie, tunuiyapo-tunuiapo
    • inkisari-walochuma-waliochuma, siendekeze-tusiendekeze, kujepusha-kujiepusha
    • mazda-kuenda-kwenda
    • kikale-vijaile-vimejaa
    • kuboronga sarufi-au dede kuwa hima-au kuwa hima wakati tungali dede, kuinama inafaa-inafaa kuinama
      zozote 4*1=4
  6. Eleza dhima urudiaji  katika shairi hili.(alama 2)
    • urudiaji wa sauti-/a/ kuleta rithimu ya shairi na urari wa vina
    • urudiaji wa neno –tusitake –kusisitiza ujumbe
    • urudiaji wa silabi-tu-rithimu  katika shairi
      zozote 2*1=2

USHAIRI 22

  1. Sidhani ni kichekesho, kesho kuwepo sidhani
    Vilivyoko ni vitisho, viwewe na visirani
    Mimi kupe kwenye josho, la sumu iso imani
    Kesho yangu imeshaliwa.
  2. Kesho yangu imeshaliwa, isibaki hata kitwa
    Kwamba hai nitakuwa, kesho na kesho kutwa
    Hilo haliwezi kuwa, na wakati limepitwa
    Na i wapi kesho yangu?
  3. Sikwambii mtondoo, au ni mtondogoo
    Ajapowika jogoo, kesho sipo ng'oo
    Hata simu za "haloo", hazinipati "haloo"
    Nitaituhumu kesho.
  4. Kesho nitaituhumu, kwa sababu ya hasama 
    Hasama ya mahasimu, waliolishana njama
    Kutaka kunihujumu, wanizulie nakama 
    Itokapi yangu kesho?
  5. Wa kwanza huyu Ukimwi, daima aniotea
    Kwa dawa huyu hazimwi, haachi kuturingia
    Amekuwa kama zimwi, mtu lisilomjua 
    Ati nipangie kesho?!
  6. Nipange yangu matanga, au kujenga nyumba?
    Nipange kung'oa nanga, au shairi kuimba?
    Nipangeni cha kupanga, biashara za mtumba?
    Kesho si ukoo wangu.
  7. Ukimwi nduguze wako, Ebola na Malaria
    Kichomi na sekeneko, mno wajifaragua 
    Maadamu wangaliko, vipi kesho kuwazia?
    Kesho si ndu yangu mwandani.
  8. Mimi napangia leo, maana kesho sijui
    Usafiri nifanyao, kwenye vyombo anuwai
    Una mikasa kibao, majanga ya kila nui
    Salama yangu i wapi?
  9. I wapi salama yangu, huku wapo wa kijicho
    Ngaa nipatapo changu, waingiwa mpekecho
    Kunipikia majungu, nikikosa changu hicho
    Waso nitakia kesho!
  10. Kesho wasonitakia, watele kama siafu
    Majambazi nasinzia, tapeli na wazinifu
    Roho yangu wapania, kunipeleka kwa ufu
    Nipewe jina "Hayati"
    1. Ujumbe wa shairi hili unakatisha tamaa. Thibitisha. (4)
    2. Hili ni shairi la aina gani? (1)
    3. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari.  (4).
    4. Eleza mbinu nne za lugha zilizotumiwa. (4)
    5. Andika bahari kwa kuzingatia vigezo; (2).
      Mizani
      Vina
    6. Onyesho jinsi mshairi alivyotumia idhini yake ya kishairi. (2).
    7. Taja;  (3)
      Toni 
      Nafsi - neni
      Nafsi- nenewa. 

MAJIBU

  1. Ujumbe wa shairi hili unakatisha tamaa. Thibitisha. (alama 4)
    Kuna vitisho, viwewe na visirani.
    Kesho yangu imeshaliwa na hakuna uhakika wa kuifikia.
    Hapigiwi simu na marafiki
    Anahujumiwa na watu bila sababu.
    Kuna magonjwa mbalimbali kama vile Ukimwi na ebola na hayana tiba. 
    Kuna majambazi na matapeli waliojaa kila mahali. Zozote nne
  2. Shiari hili ni la Tarbia kwa sababu lina mishororo minne katika kila ubeti.
  3. Mwandishi anaanza kwa kusema kuwa  anaituhumu kesho yake kwa sababu ya uhasama. Anasema uhasama huu unatokana na mahasimu wanaopanga njama ya kumhujumu. Wanataka tu kumsababishia nakama. Mwandishi anamalizia kwa kuuliza kesho yake itatoka wapi na haya mambo yote yanayomzunguka yanaitishia hiyo kesho.
  4. Isitiari- mimi kupe
    Kinaya- kesho yangu imeliwa
    Tanakali ya sauti-  sipo ng'oo
    Utohozi- haloo
    Tashihisi- huyu Ukimwi
    Swali la balagha- Salama yangu i wapi?
    Tashibihi- kama siafu
    Nahau-kung'oa nanga
  5. Mizani- msuko kwa sababu mizani ya kibwagizo ni michache/ kibwagizo ni kifupi
    Vina- ukaraguni- kila kipande kinajitegemea kivina
  6. Kufinyanga sarufi- kesho kuwepo sidhani badala ya sidhani kuwepo kesho
    Inkisari- iso badala ya isiyo/ Waso badala ya wasio
    Tabdila- kitwa badala ya kichwa zozote mbili
  7. Toni – ya kukata tamaa/ kuudhika/ kukosa matumaini/ kuonya
    Nafsi – neni- mtu asiye na uhakika na kesho yake/ aliyekata tamaa
    Nafsi- nenewa.- watu kwa jumla/ mahasimu/ wale wanaodhulumu/ wote wanaohujumu

USHAIRI 23

SIONDOKI

  1. Eti
    Niondoke!
    Nimesaki; licha ya risasi
    Vitisho na mauaji, siondoki.

  2. Mimi
    Siondoki
    Niondoke hapa kwangu!
    Kwa mateke hata na mikuki
    Marungu na bunduki, siondoki.

  3. Hapa
    Siondoki
    Mimi nipahame!
    Niondoke hapa kwangu!
    Fujo na ghasia zikizuka
    Na kani ya waporaji, siondoki.
  4. Haki
    Siondoki
    Kwangu siondoki
    Niondoke hapa kwangu!
    Nawaje; waje wanaokuja
    Mabepari wadhalimu, siondoki.

  5. Kamwe
    Siondoki
    Mimi niondoke hapa
    Niondoke hapa kwangu!
    Ng’oo hapa kwangu!
    Katizame chini mti ule!
    Walizikwa babu zangu, siondoki.

  6. Sendi
    Nende wapi?
    Si’hapa kitovu changu!
    Niondoke hapa kwangu
    Wangawa na vijikaratasi
    Si kwamba hapa si kwangu, siondoki.

  7. Katu
    Siondoki
    Sihitaji karatasi
    Niondoke hapa kwangu
    Yangu mimi ni ardhi hii
    Wala si makaratasi, siondoki.

    MASWALI
    1. Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili. (alama 2)
    2. Fafanua sifa mbili za nafsineni (alama 2)
    3. Eleza muundo wa shairi hili (alama 4)
    4. Eleza umuhimu wa kihisishi katika shairi (alama 2)
    5. Onyesha jinsi mwandishi alivyotumia usambamba katika shairi (alama 2)
    6. Ukirejelea shairi, eleza namna mtunzi alivyotumia idhini zifuatazo (alama 3)
      1. Inkisari
      2. Kufinyanga lugha
      3. Udondoshaji wa neno
    7. Taja mbinu tatu za lugha katika shairi (alama 3)
    8. Toa mfano mmoja mmoja wa mishororo ifuatayo (alama 2)
      1. mshororo mshata
      2. mshororo kifu

MAJIBU

  1. Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili. (alama 2)
    1. Kuangazia/ kuonyesha nia ya mabepari/ Viongozi dhalimu kuwahamisha watu katika ardhi
      • Kuwahimiza watu/ wanyonge kupigania haki/ardhi yao
  2. Fafanua sifa mbili za nafsineni (alama 2)
    • Mwenye msimamo dhabiti- siondoki kamwe
    • Mtamaduni- anakataa kuhama kwenye ardhi kwa kuwa babu zake walizikwa hapo
    • Mkakamavu/ jasiri- haogopi lolote, …na waje wanaokuja mabepari wadhalimu siondoki
  3. Eleza muundo wa shairi hili (alama 4)
    • Lina beti saba
    • Mishororo sita katika kila ubeti
    • Idadi ya mizani inabadilika katika kila mshororo
    • Vina vinabadilika
    • Mishororo haijagawika katika vipande isipokuwa mshororo wa mwisho katika kila ubeti.
  4. Eleza umuhimu wa kihisishi katika shairi (alama 2)
    • kuchimuza/ kusisitiza ujumbe kwamba nafsineni haondoki
    • kubainisha hisia za nafsineni
  5. Onyesha jinsi mwandishi alivyotumia usambamba katika shairi (alama 2)
    • Urudiaji wa vishazi -Niondoke hapa kwangu
    • Urudiaji wa neno- siondoki
  6. Ukirejelea shairi, eleza namna mtunzi alivyotumia idhini zifuatazo (alama 3)
    1.  Inkisari
      • Sendi- siendi,
      • nende- niende
    2. Udondoshaji wa neno
      • si’hapa- si ni hapa
      • katiza chini mti ule- katizame chini ya mti ule
    3. Kufinyanga lugha
      • yangu mimi ni ardhi hii- ardhi hii ni yangu mimi
      • kwangu siondoki- siondoki kwangu
  7.  Taja mbinu tatu za lugha katika shairi (alama 3)
    1.  NIdaa- niondoke!
    2. Balagha-nende wapi?
    3. Takriri- Siondoki siondoki siondoki
  8. Toa mfano mmoja mmoja wa mishororo ifuatayo (alama 2)
    1. Mishororo kifu
      • Siondoki
      • Kwangu siondoki
      • sihitaji karatasi
    2. Mishororo mishata
      • Ng’oo hapa kwangu
      • Fujo na ghasia zikizuka
      • Kwa mateke hata na mikuki

USHAIRI 24

SHAIRI LA  A

Falaula ngalijua, singalikuwa kijana,
Kwa sababu sikujua, kajipata mvulala,
Mengi mambo nikajua, nikashinda wasichana,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.

Mwili wangu kabadilli, toto hadi utu uzima,
Sauti yangu kabadili, nikajiola mzima,
Kakiuka maadili, dunia nikaizima,
Kweli ujana moshi, ukienda haurudi.

Masikiongu katonga, herini nikavalia,
Nywele yangu nikasonga, na mikufu kuvalia,
Video pia runinga, tazama bila tulia,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.

Malaika kapata, moyo wangu kapambika,
Jina lake kaloreta, mie wangu malaika,
Penzi langu kalipata,mambo mengi katendeka,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.
Moyongu kausumbua, nilipomtia mboni,
Penzi lanisumbua, aingiapo moyoni,
Sautiye kazindua, yatoa nyoka pangoni,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.

Penzi lake kalionja, kwangu likawa asali,
Nikawa kionjaonja, kuliwasha kawa kali,
Vitabungu nikakunja, navyo kavitupa mbali,
Kweli ujana ni moshi , ukienda haurudi.

Mzigo kabebesha, ukamwachisha skuli,
Mashakani kaniingisha, nikawa sasa silali,
Kulisaka suluhisho, likawa sasa ghali,
Kweli ujana ni moshi, ukienda haurudi.

SHAIRI LA B

Mhariri nipe fursa, nifichue jambo hili,
Nipige wengi msasa, nakusihi tafadhali,
Ukweli wajue sasa, wamakinike ki hali,
Samaki pale barini,kweli huwa si mmoja.

Nawajuza mahawara, pale walipo hakika,
Si ya neni kihasira, ukweli nautamka,
Wayaepuke madhara, wazidi kumakinika
Samaki pale barini, kweli huwa si mmoja.

Dunia imegeuka, waja leo wana shani,
Wazidi kuhangaika, watatizika moyoni,
Utesi umeshazuka, mashambani na mijini,
Samaki pale barini, kweli huwa si mmoja.

Mahaba yakigeuka, hakika huwa ni dhiki,
Ugomvi uje kuzuka, uharibu urafiki,
Wakosane washirika, wapigane kila mwezi,
Samaki pale barini, kweli si mmoja.

Lakini sasa tengeni, vigogo niwasaili,
Iwapo ni hayawani,mpungufu kiakili,
Unisamehe sabini, kwa kosa moja kwa kweli,
Samaki pale barini kweli huwa si mmoja.

Hakika huwa si vyema, kibaya kukimiliki,
Mchongaji nayasema, natangaza uhakika,
Mtu mate huyatema, iwapo hayamezeki,
Samaki pale barini, huwa si mmoja.

Nafumbua fumbo wazi, mnielewe vizuri,
Nafasili ya mapenzi, yalokumbwa nazo zari,
Yalofitinika wazi, hapo ndipo nashauri,
Samaki pale barini, huwa si mmoja.

Maswali

  1. Jadili maudhui katika shairi A na shairi B (Alama 6)
  2. Eleza muundo wa shairi la A (Alama 4)
  3. Toa mifano ya uhuru wa utunzi uliotumiwa katika shairi la B. (Alama 2)
  4. Andika ubeti wa nne wa shairi la A katika lugha nathari. (Alama 4)
  5. Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika mashairi haya. (Alama 4)
    1. Nikajiola
    2. Mzigo kambebesha
    3. Shani
    4. Zari

MAJIBU

  1. linganisha kimaudhui
     Maudhui A  Maudhui B
     Kijana alijiingiza kwenye anasa
    Akapuuza masomo
    Akampachika msichana mimba akaacha shule.
    Kijana sasa anajuta kwa vitendo vyake.
     Marafiki waliobadilika na kuwa masahidi.
    Amekatisha urafiki.
    Walio katika ndoa ambao uhusiano wao umeharibika na kutengana
  2.    
    • Tarbia – Lina mishororo minne katika kila ubeti.
    • Mathnawi – Limegawika katika vipande viwili.
    • Ukaraguni- vina vya kati na vya nje vinabadilikabadilika katika kila ubeti.
    • Kibwagizo – kweli ujana ni moshi, ukienda hauridi.
    • Mizani 16- kwa kila mshororo (Zozote 4x1 = 4)
  3. Uhuru wa utunzi
    1. Shairi A
      • Inksari – ngalijua, sautiye.
      • Kutotaja dhamiri – Kajipata badala nikajipata au kumpa
      • Lahaja – nikajiola – nikajiona.
      • Kubironga sarufi – malaika kumpata – kumpata malaika.
    2. Shairi B
      • Inkisari – nayasema.
      • Kuboronga sarufi – ukweli wajue sasa – wajue ukweli sasa.
        (Tuza zozote 2x1 = 2)
  4. Lugha nathari (Alama 4)
    • Nikampata malaika na akaupamba moyo wangu. Malaika wangu anaitwa karoleta. Alilipata penzi langu na mambo mengi yakatendeka . Ni kweli ujana ni moshi ukienda haurudi.
  5.  
    1. Nikajiola – nikajiona
    2. Mzigo kambebesha – Nikamdunga mimba.
    3. Shani – vituko
    4. Zari – shida , mahangaiko.

USHAIRI 25

MKWARUZANO WA NDIMI

Huyo! Mshike huyo!
Hakuna bunduki wala kifani
Bomu na risasi hata hawazijui
Lakini mno wanashambuliana
Kwa ndimi zilizonolewa kwa makali
Vipande vya matusi silaha zao.

Yu imara mmoja wao
Akirusha kombora la neno zito!
Limtingishe adui wake
Na kumgusa hisia kwa pigo kuu
Pigo linalochoma moyoni kama kichomi
Kuchipuza joto la hasira na kisasi
Katika mapigano yaso na kikomo

Filimbi ya suluhu inapulizwa kuwaamua!
Nani anayekubali suluhu?
Roho zinakataa katakata
Huku ukaidi ukinyemelea na kutawala kote
Mapandikizi ya watu yakipigana
Vita shadidi visivyo ukomo
Vita vya ndimi!

Magharibi sasa
Jua linapungia mkono machweo
Nalo giza likinyemelea kwa kiburi na kasi
Sisikii tena sauti za misonyo
Mate ya watesi yamekauka
Makanwa yao yamelemewa na uchovu
Sasa wameshikana mikono
Ishara ya suluhu.

Maswali

  1. Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu. (alama 2)
  2. Eleza dhamira ya mshairi. (alama 2)
  3. Eleza kanuni za utunzi alizotumia mshairi. (alama 4)
  4. Fafanua mbinu zozote mbili za lugha katika ubeti wa mwisho wa shairi. (alama 2)
  5. Jadili toni ya mshairi katika beti tatu za awali. (alama 2)
  6. Tambua matumizi ya mistari mishata na utoe mifano miwili. (alama 2)
  7. Andika mishororo ya kwanza mitatu katika ubeti wa 4 kwa lugha ya nathari. (alama 3)
  8. Eleza athari tatu za vita vya ndimi (alama 3)

MAJIBU

  1. Shairi huru kwa sababu halina urari wa vina wala mizani. (alama 2)
  2. Kuonyesha jinsi kugombana ni kubaya na wagombanao huchoka na wakapatana
  3.                          
    1. Matumizi ya mshororo toshelezi na mshata
    2. Matumizi ya beti
    3. Matumizi ya mishororo
    4. Matumizi ya lugha ya mkato
    5. Matumizi ya mbinu za kishairi-yaso (inkisari) zozote 4 (alama 4)
  4. Tashihisi
    • Jua linapungia mkono machweo
    • Nalo giza likinyemelea kwa kiburina
      Takriri - sasa
      (alama 2)
  5. Toni ya kukerwa anaonyesha kuchukizwa na tabia ya kugombana kwa matusi (alama 2)
  6. Mapandikizi ya watu yakipigana
    Yu imara mmoja wao
    Lakini mno wanashambuliana
    Nalo giza likinyemelea kwa kiburi na (alama 2)
  7. Wakati wa jioni umefika. Jua linazama kwani ni wakati wa machweo. Giza linaingia kwa kishindo kikubwa. (3x1) (alama 3)
  8.                        
    1. Vinamtingiza adui (alama 3)
    2. Vinagusa hisia
    3. Vinachipuza joto la hasira na kisasi za kwaza 31=3
    4. Vinachochea mapigano yasiyo na kikomo

USHAIRI 26

  1.  Sidhani ni kichekesho, kesho kuwepo sidhani
    Vilivyoko ni vitisho, viwewe na visirani
    Mimi kupe kwenye josho, la sumu iso imani
    Kesho yangu imeshaliwa.

  2. Kesho yangu imeshaliwa, isibaki hata kitwa
    Kwamba hai nitakuwa, kesho na kesho kutwa
    Hilo haliwezi kuwa, na wakati limepitwa
    Na i wapi kesho yangu?

  3. Sikwambii mtondoo, au ni mtondogoo
    Ajapowika jogoo, kesho sipo ng'oo
    Hata simu za "haloo", hazinipati "haloo"
    Nitaituhumu kesho.

  4. Kesho nitaituhumu, kwa sababu ya hasama
    Hasama ya mahasimu, waliolishana njama
    Kutaka kunihujumu, wanizulie nakama
    Itokapi yangu kesho?

  5. Wa kwanza huyu Ukimwi, daima aniotea
    Kwa dawa huyu hazimwi, haachi kuturingia
    Amekuwa kama zimwi, mtu lisilomjua
    Ati nipangie kesho?!

  6. Nipange yangu matanga, au kujenga nyumba?
    Nipange kung'oa nanga, au shairi kuimba?
    Nipangeni cha kupanga, biashara za mtumba?
    Kesho si ukoo wangu.

  7. Ukimwi nduguze wako, Ebola na Malaria
    Kichomi na sekeneko, mno wajifaragua
    Maadamu wangaliko, vipi kesho kuwazia
    Kesho si ndu yangu mwandani.

  8. Mimi napangia leo, maana kesho sijui
    Usafiri nifanyao, kwenye vyombo anuwai
    Una mikasa kibao, majanga ya kila nui
    Salama yangu i wapi?

  9. I wapi salama yangu, huku wapo wa kijicho
    Ngaa nipatapo changu, waingiwa mpekecho
    Kunipikia majungu, nikikosa changu hicho
    Waso nitakia kesho!

  10. Kesho wasonitakia, watele kama siafu
    Majambazi nasinzia, tapeli na wazinifu
    Roho yangu wapania, kunipeleka kwa ufu
    Nipewe jina "Hayati"

MASWALI

  1. Ujumbe wa shairi hili unakatisha tamaa. Thibitisha. (4)
  2. Hili ni shairi la aina gani? (1)
  3. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (4).
  4. Eleza mbinu nne za lugha zilizotumiwa. (4)
  5. Andika bahari kwa kuzingatia vigezo; (2).
    Mizani
    Vina
  6. Onyesho jinsi mshairi alivyotumia idhini yake ya kishairi. (2).
  7. Taja; (3)
    Toni
    Nafsi - neni
    Nafsi- nenewa.

USHAIRI 27
Milingoti
Wanakwenda... wanakwenda..."
Wanapiga hatua labda!
Labda... labda... labda!
Mwendo wa dhana yao!
Wanakwenda kumbe wamesita.
Safari ya kuwepo na kutokuwepo!
Hatua zao kubwa: chapchap...
Miondoko sawa na jongoo
Wanakwenda pasi na kwenda
Safari ya dhana... pekee
Hatua zao kubwa na nia pia
Nia zin'otoka ndani kuishia ndani
Maishilio ni nafsi zao
Wanapiga hatua kubwa
ela wametwama!
Kisha: kwa magondi husimama
pasi na nguvu huja kuima
kutaka kugusa mbingu.
Mara mojamoja hutazama chini,
kuchungua mbilikimo
na kuhakikisha,
jinsi walivyoziteka akili zao
kuzichezea, kuzisuguasugua
mchezo wenye manufaa kwao
Mara nyingine hutazama chini
kutemea mate mbilikimo
"Rasharasha ya marashi!"
Utawasikia wakisema;
Na
ajabu mbilikimo hufarijika!
Hivyo daima huendelea kwenda
Huku wamesimama milingoti
Kwa nadra hutokezea kusikia
Mmoja ameshateguka
na kupoteza uzani
kwa ule unene wao
Na kisha hulalama na kulani
eti wameangushwa na mbilikimo!

  1. "Dhamira ya nafsneni ni kukashifu tabia za nafsinenwa," Thibitisha.
  2. Changanua mtindo katika shairi hili.
  3. Chambua muundo wa shairi hili.
  4. Fafanua toni inayodhihirika katika shairi hili.
  5. Bainisha nafsineni katika shairi hili.
  6. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha nathari.

MAJIBU

  1. "Dhamira ya nafsneni ni kukashifu tabia za nafsinenwa," Thibitisha. (alama 5)
    • Nafsinenwa hawajielewi - Wanakwenda kumbe wamesita. 
    • Nafsinenwa ni mabinafsi - Nia zin'otoka ndani kuishia ndani, Maishilio ni nafsi zao
    • Nafsinenwa wana pupa na kukosa utaratibu na mpangilio - Wanapiga hatua kubwa, ela wametwama!
    • Nafsinenwa ni wenye tamma - pasi na nguvu huja kuima, kutaka kugusa mbingu
    • Nafsinenwa ni walaghai na wenye mbinu hasi za kujitakia makuu - na kuhakikisha, jinsi walivyoziteka akili zao, kuzichezea, kuzisuguasugua, mchezo wenye manufaa kwao
    • Nafsinenwa ni wenye dharau - Mara nyingine hutazama chini, kutemea mate mbilikimo
    • Nafsinenwa ni wenye kulaumu na kulaani wengine wanpokumbwa na shida - Na kisha hulalama na kulani , eti wameangushwa na mbilikimo!
      Zozote 5x1 = 5
  2. Changanua mtindo katika shairi hili. (alama 5)
    • Nidaa - Wanapiga hatua labda! Labda... labda... labda! Mwendo wa dhana yao!
    • Mdokezo - Wanakwenda... wanakwenda... Safari ya dhana... pekee
    • Takriri - Labda... labda... labda! 
    • Tanakuzi - Wanakwenda kumbe wamesita, Safari ya kuwepo na kutokuwepo! 
    • Tanakali za sauti - Hatua zao kubwa: chapchap... 
    • Tashbihi - Miondoko sawa na jongoo
    • Jazanda-Nia zin'otoka ndani kuishia ndani, kutaka kugusa mbingu, kutemea mate mbilikimo 
    • Taswira - Wanakwenda... wanakwenda... kutaka kugusa mbingu. kutemea mate mbilikimo 
    • Litifati - "Rasharasha ya marashi!" 
    • Ukwelikinzani - Wanakwenda kumbe wamesita. Wanakwenda pasi na kwenda
      Zozote 5x1 = 5
  3. Chambua muundo wa shairi hili. (alama 3)
    • Shairi lina beti saba 
    • Idadi ya mizani ya kila mshororo inabadilika badilika 
    • Idadi ya mishororo katika kila ubeti inabadilika badilika 
    • Beti za zna kipande kimoja 
    • Vina vya nje vinatofautiana kutoka ubeti hadi ubeti
      zozote 3x1 = 3
  4. Fafanua toni inayodhihirika katika shairi hili. (alama 2)
    Toni ya kukashifu / kukejeli / kudhihaki - Wanakwenda kumbe wamesita. Wanakwenda pasi na kwenda
    Yoyote 1x2 (kutambua moja na kutoa ithibati moja)
  5. Bainisha nafsinenwa katika shairi hili.
    (alama 2) Wakubwa katika jamii – Mara mojamoja hutazama chini,
    1x2=2
  6. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha nathari. (alama 3)
    Ni nadra wakubwa kupata shida ila hilo inanetoken who halalamika na kulonni kuwa shida hiyo imesababishwa na wanyonge.

USHAIRI 28

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Binadamu hatosheki, ni kiumbe chenye zani, kweli mja hapendeki
Kwa kweli haaminiki, hila ameficha ndani, la wazi ni unafiki
Ukweliwe haafiki, njama zake zi moyoni, usimwone ni rafiki,
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Wenginea watakuua, wakiona una pesa, hata zikiwa kidogo
Hizo kwao ni maua, hupupiwa zikatesa, wakizifuata nyago
Hadi kwenye wako au, pasipo hata kupesa, walakukupa kisogo
Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Pindi kinunua kitu, hafurahi shaitani, bali tajawa chukizo
Mtu kiwa mtukutu, tanuna mtimani, kwato ako tekelezo
Tamko lake ‘subutu’, kuondoa tumaini, na kukuliza wazo
Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Aliye na taraghani, taabu kuishi naye, kazi yake kujidai
Takusema faraghani, asosema kiwa naye, kupendeza maadui
Hana faida nyumbani, ni mtu akichimbaye, mradi usitumai
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Kwa hakika ni baka, kumkirimu mchawi, aliyejaa uchoyo
Bahati ina hadaa, kukupa alo sodawi, aibarili rowoyo
Mipangayo kwake jaa, na nia ya ustawi, huwiza kuvunja kaniyo
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Ninacho changu kilio, ninalia sanasana, kinyesi nimetupiwa
Ningetoa azinio, lakini uwezo sina, kwa mazito kuambiwa
Ama nitimue mbio, fuadinininanena, akilini nazuiwa
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

  1. Jadili dhamira ya shairi hili. (Alama 1)
  2. Eleza sababu za mtungaji kulalamika katika shairi hili. (Alama 3)
  3. Eleza umbo la shairi hili. (Alama 4)
  4. Andika ubeti wa tatu katika lugha nathari/ tutumbi. (Alama 4)
  5. Taja na utoe mifano ya aina nne za tamathali za usemi zilizotumika katika shairi hili (Alama 4)
  6. Toa mifano miwili tofauti ya uhuru wa kishairi katika shairi hili . (Alamfa 2)
  7. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi. (Alama 2)
    1. Zani
    2. Faraghani 

MAJIBU

  1. Kuonyesha vile tamaa ni hatari.
  2. Mtu mwenye tamaa ni hatari kama nyoka
    Mwenye tamaa ana unafiki / masengenyo
    Mwenye tamaa anaweza kuua
    Mwenye tamaa ni mchoyo
  3. Mishororo minne katika kila ubeti
    Migao/ vipande vitatu – ukwapi / utao / mwandamizi /Vina vitatu
    Mizani 8, 8, 8.
    Lina Kibwagizo- Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
    Lina beti sita (hoja zozote 4x1=4)
  4. Mwandishi anasema kuwa mwenye tamaa atakuwa na chuki iwapo utanunua kitu na anakuwa kama shetani kwani hafurahi. Mtu kama huyo atakasirika moyoni kwa kile ulichokifanya.
    Atakuonya ili akuvunje matumaini ya kutekeleza ulichonua. Anamalizia kw akusema kuwa mtu mwenye tamaa ni hatari kama nyoka.
  5. Takriri – kibwagizo
    Tashibihi – hatari kama nyoka
    Tashihisi – Bahati ina hadaa
    Nahau – Kinyesi kimetupiwa
  6. Inkisari – Ukweliwe, tajawa, asosema, alo, mpangoyo
    Mazida sheitani (Kurefusha she/ta/ni)
    Kufinyanga sarufi- Ninacho changu kilio badala ya ninacho kilio change nk
  7.        
    1. Zani = baa/ janga /balaa
    2. Faraghani – kwa siri

USHAIRI 29
Monyara
Nakumbuka kwa dhiki Mto Monyara
Tuliochelea kukaribia kingo zake
Tukatulia kwanza; ukakamavu kujihamia
Kwa kunyenyekea wingi wa yake maji
Yaliyojiendea utadhani yamesimama.

Ni katika mto huu
Ambapo samaki wakubwa tulivua
Maguo kuyatakasa japo kwa kunyemelea
Na walevi stadi wakachelea kuuvuka
Ulipofura na kupita kwa kiburi
Kwa kushiba maji yake
Yaliyofanya mawimbi madogo.

Ni hapa ambapo marehemu nyanya
Mkono alinishika na njia kuniongoza
Juu ya ulalalo wa miti
Vikapu vyetu hewani vikielea;
Mimi nikishika changu kwa mkono mmoja
Naye akikiachilia chake kujishikisha kichwani
Masafa baina yetu na mtambo
Uliokwenda kwa maji
Tuliyapunguza kwa kila hatua tulopiga.

Ni katika mto huu ambapo
Samaki tuliowavua tuliwapasua na kuwasafisha
Na hivyo kuuficha umaskini wetu
Ulotuzuia kununua mnofu wa bucha
Ni hapa ambapo wanawake walifika
Mawe ya kusagia kupata
Ni katika mto huu ambapo
Waumini walifika kutakaswa kwa ubatizo
Baada ya ulevi, uzinzi na kufuru nyinginezo.

Ni hapa ambapo ilisimuliwa kuwa
Hata wachawi walifika kufanya vitimbi vyao
Baada ya utawala wa jua kumezwa na nguvu za giza
Sasa Monyara nilioijua haipo tena
Zimebaki kingo zilizokaukiana
Kama uso wa mrembo aliyekosa mafuta
Siku ayami.

Mto huu ambapo pembeni mwake
Watoto walipashwa tohara
Maji yake yakishangilia, umekonda
Na mbavu zake nje kutoa
Na sasa vitoto vikembe vinazikanyaga
Vikijiendea zao kusaga mahindi
Juu mlimani
Katika mtambo wa Kizungu
Usioisha kulalamika
Nao wanawake hawaji tena
Kutafuta mawe ya kusagia wimbi
Imebaki njia ya walevi warejeao nyumbani
Nayo miti iliyosimama wima ukingoni
Iliisha kuanguka kwa kuleweshwa na pumzi za walevi
Wasioisha kupita hapa

  1. Onyesha umuhimu wa Mto Monyara kwa wanakijiji. (alama 4)
  2. Toa mifano ya mishata inavyojitokeza shairini. (alama 2)
  3. Eleza aina tatu za taswira zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 3)
  4. Fafanua mtindo katika shairi hili. (alama 3)
  5. Tambua nafsi neni ya shairi hili. (alama 1)
  6. Jadili idhini ya kishairi katika shairi. (alama 3)
  7. Andika ubeti wa pili katika lugha nathari (alama 2)
  8. Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)

MAJIBU

  1. Onyesha umuhimu wa Mto Monyara kwa wanakijiji. (alama 4)
    1. Kuvua samaki ambao watatumiwa kama kitoweo;
    2. Nguo zilioshewa humo;
    3. Maji yake yaliendesha mtambo, kinu cha kusagia unga;
    4. Mawe ya wanawake ya kusagia waliyapata humo;
    5. Waumini walibatizwa/walitakaswa katika maji ya mto huo baada ya dhambi za ulevi na uzinzi;
    6. Wachawi waliutumia kufanya vitimbi vyao;
    7. Watoto walipashwa tohara kando yake, maji yalishangilia waliopashwa tohara
      (Hoja zozote 4x1= alama 4)
  2. Toa mifano ya mishata inavyojitokeza shairini. (alama 2)
    Mshororo usiokamilika, unakamilikia katika ule unaofuata.
    Ni katika mto huu ambapo
    Ni hapa ambapo ilisimuliwa kuwa
    (zozozte 2x1=alama2)
    Tathmini jibu la mwanafunzi
  3. Eleza aina tatu za taswira zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 3)
    1. Taswira mwendo: kuenda ka maji, kuuvuka mto, vitoto kuenda kusaga mahindi;
    2. Taswaira mguso: Mikono ya nyanya na msimulizi kushikana.
    3. Taswira mwono: maji kusimama, vikabu kichwani na mkononi.
      (za kwanza 3x1=3)
  4. Fafanua mtindo katika shairi hili. (alama 3)
    1. Mbinu rejeshi: kumbukumbu za hali ya awali yam to Monyara;
    2. Tashihisi: mto ulipita kwa kiburi na ulishida maji yake; mto umekonda na kutoa mbavu zake nje;
    3. Taswira: msimulizi na nyanya tunawaona wakishikana mikono wakivuka mto kwa kupita juu ya ulalo wa miti;
    4. Tashibihi: maji yalijiendea utadhani yamesimama,
    5. Utohozi: bucha;
  5. Tambua nafsi neni ya shairi hili. (alama 1)
    1. Mjukuu;
    2. Msimulizi
      (Hoja1x1=1)
  6. Jadili idhini ya kishairi katika shairi. (alama 3)
    1. Inkisari: tulopiga- tuliyopiga Ulotuzuia-uliotuzuia;
    2. Kuboronga msamiati: Miundo mibaya ya sentensi, mfano, ukakamavu kujihamia- kujihami na ukakamavu, Mawe ya kusagia kupata – Kupata mawe ya kusagia
    3. Mazda: kujihamia- kujihami
    4. Utohozi: Bucha
      (zozote 3x1=alama3)
  7. Andika ubeti wa pili katika lugha nathari (alama 2)
    1. Msimulizi anaeleza kuwa walivua samaki wakubwa katika Mto Monyara kabla haujakauka. Kwa kuwa maji ya mtohuo yalikuwa mengi kutokana na kufurika, waliogopa kuoshea nguo ndani yake na hivyo wakazioshea kando. Walevi waliokunywa pombe ng’ambo ya pili waliporejea makwao, waliogopa kuuvuka kutokana na wingi wa maji yake. Mto ulipofurika ulifanya mawimbi kidogo kuonyesha maji yalikuwa ya kina kirefu.
      (Zozote 4x12)
  8. Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
    1. Toni ya kutamauka/kukata tamaa- Mto Monyara uliowapa wenyeji matumaini ya maisha mema sasa hauko, umekauka

USHAIRI 30

USHAIRI
Wafungwa wa kila mahali
Niarifu zenu idhilali
Maombolezo na machofu mlokabili

Wavuvi wa kila bahari
Leteni nyavu zilokumba hatari
Na nguvu za mawimbi mlohimili

Mafalahi wa kila jimbo duniani
Nileteeni yenu matambara leteni
Leteni hiyo mikono majuruhi
Na yalonyauka matiti
Na kucha zenu maiti
Nyote leteni kwangu
Leteni haraka leteni

Naunda mikitaba yakini
Ya dhiki za maskini
Kumpelekea Manani
Ishapotiwa saini
na midomo ya wala njaa
lakini, enyi mafukara wa dunia
Hofu yangu kubwa namwambia
Mungu huenda ikatukia
Hajui kusoma ... hili nachelea

Maswali

  1. Ainisha shairi hili. Toa sababu ya jibu lako. (alama 2)
  2. Tetea kwa kutoa hoja nne kauli kuwa utungo huu ni ushairi. (alama 4)
  3. Idhini ya mshairi inajitokeza vipi? (alama 3)
  4. Eleza ujumbe uliofumbatwa katika utungo huu. (alama 3)
  5. Ukitolea mifano, onyesha mbinu inayotawala katika shairi hili. (alama 2)
  6. Ubeti wa mwisho unakatisha tamaa. Thibitisha. (alama 3)
  7. Eleza muundo wa ubeti wa kwanza na wa pili. (alama 3)

MAJIBU

  1. Shairi huru (kimapinduzi). Halizingatii arudhi za utunzi.
  2.                      
    1. kuwepo kwa mishororo
    2. kuwepo kwa beti
    3. matumizi ya lugha ya mkato
    4. vina vinajitokeza kwa kiwango fulani
  3.                      
    1.  inkisari (kufupisha kwa maneno) km. Mlokabili badala ya mliokabili, zilokumba badala ya zilizokumba, mlohimili badala ya mliohimili
    2. kuboronga sarufi/kufinyanga sarufi – niarifu zenu idhilali badala ya niarifu idhilali zenu,, nileteeni yenu matambara – nilteeni matambara yenu
    3. tabdila – mikitaba – mikataba, majutuhi - majeruhi
  4. Mateso na dhiki zinazowakumba maskini –ya dhiki ya maskini kumpelekea Manani
    Hali duni ya maisha licha ya kujibidiisha kazini – matambara
    Hatari katika kufanya kazi – nyavu zilizokumba hatari, na nguvu za mawimbi mlohimili
  5. Takriri- leteni nyavu ..., nileteni yenu matambara leteni
  6. Msimulizi anasema anaunda mikataba ya dhiki za maskini ili amplekee Mungu, lakini hofu yake kubwa ni kuwa huenda ikatukia kuwa Mungu hajui kusema – anachelea hilo
  7. Mizani
    Ubeti wa kwanza            ubeti wa pili
    9                                          9
    10                                       12
    14                                       12
    Mishororo mitatu katika kila ubeti
    Vina
    Vina vya mwisho
    Ubeti wa 1
    -li
    - li
    - li
    Ubeti wa 2
    -ri
    - ri
    - li

 

USHAIRI 31
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo.
Msambe naja kuteta, nina wema wa kalima,
Moto wanikatakata, maini yangu yachoma,
Ili nipate takata, ukweli wote ‘tasema,
Anayekataa pema, pabaya panamuita.

Bahati ni kama nyota, humemeta na
Kuzima, Sikimbilie
mafuta, ukatae Kula
sima, Anayekataa pema,
pabaya Panamuita.

Haraka zina matata, angaza mbele na
Nyuma, Tenda mambo kwa kusita,
Usije ukalalama, Keti
pako ukipata, Kwa muradi
wa uzima, Anayekataa
Pema, pabaya panamuita.

Pema si penye mafuta, au pa wali
Na nyama, Pema watu hutafuta,
Utulivu na hekima, Si hoja penye
Ukata, pa watu hali ya nyuma,
Anayekataa pema, pabaya
Panamuita

Mahali pema ambata, kwa vitendo na huduma,
Sikae penye matata, palipojaa hasma,
Lau kama pamemeta, hapafai kwa daima,
Anayekataa pema, pabaya panamuita
Maswali

  1. Lipe anwani mwafaka shairi hili. (alama 1)
  2. Bainisha bahari mbili za shairi hili. (alama 2)
  3. Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4)
  4. Fafanua dhamira ya mshairi. (alama 1)
  5.  Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4)
  6. Onyesha jinsi mshairi alivyotumia uhuru wake. (alama 3)
  7. Kwa kutoa mifano, bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili. (alama 2)
  8. Eleza maana ya msamiati ufuatao. (alama 3)
    1. Kalima
    2. Mafuta
    3. Ukata

MAJIBU

  1. Lipe anwani mwafaka shairi hili (al 1)
    Anayekataa pema, pabaya pamuita
  2. Bahari mbili za shairi hili (al 2)
    1. sakarani
    2. Masivina – halina urari wowote wa vina
  3. Muundo wa shairi hili (al 4)
    1. Beti nne
    2. Lina kibwagizo ‘Anayekataa pema, pabaya pamuita’.
    3. Halijazingatia mtoshelezo wa mishororo ktk kila ubeti
    4. Halina urari wa vina
  4. Dhamira ya shairi ni kuhimiza kuhusu umuhimu wa uadilifu na mienendo inayofaa. (al 1) hakiki
  5. Mahali pema si pale ambapo pana vizuri bali palipo na utulivu na hekima. Hata kama pana umaskini, mtu anapokataa mahali pema huitwa na pabaya. (al 4)
  6.                      
    1. Inkisan - Tasema
      - sikimbilie
    2. Msamiati wa kale- mato badala ya macho
    3. Kuboronga sarufi – keti pako ukipata
    4. Tabdila – muradi (zozote 3)
  7. Tamathali mbili za usemi (al 2)
    Tashbihi – Bahati ni kama nyota.
    Jazanda - mafuta, wali na nyama zimetumika kijazanda (zozote 2)
  8. Maana ya
    1. Kalima – usemi
    2. Mafuta – mng’aro
    3. Ukata - umaskini

USHAIRI 32

  1. Mbiu naipuliza, kwawa hapana ng’ambo,
    Kwa aningoja ‘mesikia, inaumiza matumbo,
    Kwa upole sitafyoa, hata kamna kwa
    kimombo, Yafaa jihadharia, maisha ya s’ende kombo.
  2. Maisha ya s’ende kombo, kututoa yetu ari,
    Zingatia haya mambo, wetu wale
    zimukiri, Kuwa wana kwa viambo,
    huwa Baraka na kheri watunzeni
    na maumbo, msie zusha hatari.
  3. Msije zusha hatari, na nyingi hizi zahama,
    Wazazi haya si siri, mawi mnayoandama
    Twaelezea kwa uzuri, matendoyo
    yatuuma Watoto tunayo mori, ni lini
    mtaja koma?
  4. Ni lini mtaja koma, na pombe siso halali?
    Sio baba sio mama, mbona ny’
    hamtajali? Mwafa ja nzi twasema,
    mwatua chabi la hali Hangaiko acha nyuma,
    kwani hamuoni hili?
  5. Kwani hamuoni hili, kila saa mwapigana Nyumbanizo hatulali, jehanamu tumeona
    Mwatusumbua akili, twaumia ten asana Achene na ukatili, kwani upendo hamna.
  6. Kwani upendo hamna, kamam mbwa mwatuchapa
    Mwatuchoma sisi wana, mio yetu yatupapa
    Pa kujificha hatuna, tumebaki tukitapa
  7. Tumevujwa na mifupa, hata leo uke wetu,
    Mwatubaka na kuapa, kutung’ata nyi’ majitu,
    Hayo makeke na pupa, mtakoma utukufu
  8. Mtakoma utukufu, nakutumia miki
    Na tabia zenye kutu, tumechoka nayo chuki
    Hatutakubali katu, kutendewa yenye siki Serikali fanya kitu,
    kwani nasi tuna haki

Maswali

  1. Fafanua tamathali nne za usemi zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 2)
  2. Taja nafsi nne katika shairi hili. (alama 1)
  3. Eleza bahari mbili zinaowakilishwa katika shairi hili. (alama 4)
  4. Andika ubeti wa nne kwa lugha ya nathari. (alama 4)
  5. Eleza maudhui matatu yanayojitokeza katika shairi hili. (alama 3)
  6. Eleza umuhimu wa mbinu mbili amabazo mshairi ammetumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi. (alama 4)

MAJIBU

  1. Maswali balagha- na pombe siso halali?
    Mbona ny’ hamtajali.
    Isitiari- kutang’ata nyi majitu
    Tashbihi- kama mbwa mwatuchapa
    Mwafa ja nzi. (zozote 1x4)
  2. Mtoto (mwana)
  3. Lina mishororo mine hiyo ni Tarbia.
    Kina cha kubwagiza kimechukuliwa ili kuwa mwanzo wa ubeti unaofuata hivyo huitwa pindu au mkuju/nyoka.(zozote 1x2)
  4. Nilini wazazi wataacha kutumia pombe haramu na kuwajali watoto wao kwani wanakunywa na kuwaachia mateso na mahangaiko mengi bila kujali. (alama 4)
  5. Ukatili, malezi, ulevi. Mwanafunzi aeleze ipasavyo. (alama 3)
  6. Mazida –mshairi amerufusha baadhi ya … ili kuafikia urari wa k.m. nyumbanizo, matendoyo
    Liksani- mshairi amefupisha baadhi ya maneno pia kuafiki urari wa viua- mio, ny’
    Kuburanga sarufi- kwani upendo kamua badala ya kwani hamna upendo-ili kuleta urari wa viua katika mishororo. (mwanafunzi ataje mbili na kueleza.( zozote alama 2x2

USHAIRI 33
Soma shairi lifuatalo kasha ujibu masuali

  1. Mkata ni mkatika, harithi hatorithiwa
    Sina ninalolishika, wala ninalochukuwa
    Mlimwengu kanipoka, hata tone la muruwa!
    Mrithi nini wanangu?
  2. Sina ngo’ombe sina mbuzi,sina kondesi na buwa
    Sina hata makaazi, mupasayo kuyajuwa
    Sinamazurimakuzi, jinsi nilivyoachiwa
    Mrithi nini wanangu?
  3. Sina kazi sina bazi, ila wingi wa shakawa
    Sina chembe ya majazi, mno ni kukamuliwa
    Nakwa’cheni upagazi, mgumu kwenu ku’tuwa
    Mrithi nini wanangu?
  4. Sina sikuacha jina, mkatahatasifiwa
    Hata nifanye la mana, mno ni kulaumiwa
    Poleni wanangu sana, sina kwenu cha kutowa
    Mrithi nini wanangu?
  5. Sina leo sina jana, sina kesho kutwa liwa
    Sina zizi sina shina, wala tawi kuchipuwa
    Sina wanangu mi sana, la kwacha nakuraduwa
    Mrithi nini wanangu?
  6. Sina utu sina haki, mila yangu meuliwa
    Nyuma yangu ilidhiki, na mbele imekaliwa
    N’na wana na mikiki, hadi n’tapofukiwa
    Mrithi nini wanangu?
  7. Sinai la kesho kwenu,wenyewe kuiongowa
    Muwane kwanyingi,mbinu Mwende pasi kupuwa
    Leo siyo, keshoyenu,kama mutaji kamuwa
    Mrithi nini wanangu?
    (Kina cha maisha A.S.Mohammed)
    MASWALI
    1. Eleza hali ya mzungumzaji katika shairi hili ( alama 4)
    2. Eleza dhamira kuu ya mshairi kulitunga shairi hili (alama 2)
    3. Ni nani anayezungumziwa na nafsi neni katika shairi hili? (alama 2)
    4. Eleza toni ya shairi hili (alama 2)
    5. Fafanua mbinu tatu za lugha zilizo tumiwa katika shairi hili (alama 3)
    6. Tambua bahari ya shairi hili ukizingatia. (alama 4)
    7. Mizani
    8. Vina
    9. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya tutumbi (alama 3)

MAJIBU

  1. Hali yamzungumzaji. (al 4)
    • maisha yenye umaskini mkubwa.
    • maisha yasiyo kuwa na matumaini.
    • maisha yaliyo kosa thamani.
    • maisha yenye kusikitisha. (4x 1 = 4)
  2. Dhamira kuu ya mshairi (al 2)
    kuwahimiza wanawe maishani ili kuhakikisha maisha mema ya baadaye kwa vile hali ya sasa ni ya kimaskini. (2 x 1 = 2)
  3. mzungumziwa – watoto (al 1)
    nafsi neni – mzazi (2 x 1 = 2) (al 1)
  4. toni ya shairi (al 2)
    • masikitiko
    • kutamauka/kukosa matumaini
    • ya kuhuzunisha..Mwanafunzi athibitishe (1x 2= 2)
  5. mbinu tatu za lugha zilizotumika. (al 3)
    • sitiari – mkata ni mkatika
    • Balagha – mrithi nini wanangu?
    • takriri – sina (3 x 1 = 3)
  6. Bahari ya shairi ukizingatia. (al 4)
    mizani – msuko
    vina - ukara Mwanafunzi athibitishe(2 x 2 =4 )
  7. Ubeti wa mwisho – lugha ya nathari. (al 3)
    mshairi ana matumaini kwamba wanawe wataimarisha maisha yao ya baadaye .Anawashauri wafanye bidii, wakabiliane na matatizo bila hofu. (3 x 1 = 3)Tathmini mishororo

USHAIRI 34

Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali
Jama, Jama, Jamani
Mbona twabebeshwa mateso hivi
Mizigo mikubwa ya dhiki kama
Kwamba hatuna haki ya kusema
Kukataa ndoa za lazima
Kukataa kuozwa wazee
Kukataa kukatishwa masomo
Kukataa tohara ya lazima
Jama, Jama Jamani
Iweje tuteswe mateso haya
Na watu wasio kuwa hata na haya kama
Kwamba hatuna haki ya kulalamika
Kulalamikia kutumikishwa kama mayaya
Kulalamikia kudhalilishwa kiunyama
Kulalamikia kutolindwa na sheria
Jama, Jama, Jamani
Sasa hii ni awamu nyingine
Na macho tumeyafungua kabisa
Tumekataa kudhalilishwa kabisa
Tumekataa kuteswa kama watumwa
Tumekataa tohara ya lazima
Tumekataa kuozwa....... Tumekataa! Tumekataa
Hii awamu ya ’Haki ya mtoto wa kike’
Maswali

  1. Hili ni shairi la aina gani? (alama 1)
  2. Taja na ueleze mambo matatu muhimu yaliyozungumzwa na mshairi (Alama 3)
  3. Eleza muundo wa shairi hili (Alama 4)
  4. Taja mbinu mbili za lugha alizotumia mshairi kufanikisha shairi lake (Alama 4)
  5. Kwa nini mshairi huyu anasema hii ni ’awamu’ nyingine? (Alama 3)
  6. Eleza matumizi ya mishata katika shairi hili (alama 2)
  7. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa na mshairi (alama 3)
    1. awamu
    2. kudhalilishwa
    3. Dhiki

MAJIBU

  1. Hili ni Shairi Huru
    Mambo matatu muhimu yaliyozungumziwa na mshairi na maelezo ya kila moja.
    Kutaja alama 1/2
    Kueleza alama 1/2
    Jumla 1)
  2.    
    1. Mateso
      • Mizigo mikubwa ya dhiki
      • Hakuna haki ya kunena
    2. Ndoa ya lazima
      • Kuozwa kwa wazee
      • Kukatishiwa masomo
    3. Tohara
      • Tohara ya lazima
      • Hawaruhusiwi kusema chochote
    4. Sheria
      • Haiwalindi
      • Kudhalilishwa kinyama
    5. Awamu tofauti
      • Wamekataa kudharauliwa
      • Wamekataa kuteswa
      • Wamekataa tohara za lazima.
  3. Muundo wa shairi
    1. Ni wimbo ambao haufuati muundo wowote wa ushairi
    2. Ni shairi huru
    3. Halina mpangilio wowote wa kiarudhi
    4. Halina mgao wa mishororo
    5. Halina vina wala mizani
    6. Halina kibwagizo
    7. Lina beti 3
    8. Mishororo inatofautiana katika kila ubeti
  4. Mbinu mbili za lugha alizotumia mshairi. Maelezo ya kila moja
    1. Nyimbo-Amezitumia Kwa njia mwafaka ili anase hisia za wasomaji.
    2. Takriri-Amejaribu pia kusisitiza ili kuwekea uzito yale anayozungumzia.
      Anataka msomaji apate mvuto mzuri kwa lile analolizungumzia. Mfano tumekataa kudhalilishwa, tumekataa kuteswa, tumekataa tohara.
    3. Mdokezo. Mfano Tumekataa kuozwa ...
    4. Tashbihi . mfano ubeti wa pili- Kutumikishwa kama ya
  5. Sababu za mshairi kusema; ‘hii ni awamu nyingine’
    1. Ulikuwa ukurasa mpya wa maisha.
    2. Kuna mabadiliko ya kuondoa ukandamizaji.
    3. Wanawake wamekataa kuozwa kwa lazima.
    4. Wamekataa kudhalilishwa kabisa
  6. Mishata ni mishororo ambayo hupatikana katika shairi huru ambayo maana yake haikamiliki katika mshororo huo bali hukamilika katika mshororo unaofuata
    Imetumiwa kukamilishia ujumbe ili ueleweke na kuwasilisha ujumbe vilivyo
  7. Maana ya maneno
    1. awamu-Kipindi
    2. kudhalilishwa-kukandamizwa/ kudunishwa / kufedheheshwa
    3. dhiki-shida

USHAIRI 35

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo

  1. Mkata ni mkatika, harithi hatoridhiwa
    Sina ninalolishika, wala ninalochukuwa
    Mlimwengu kanipoka, hata tone la muruwa!
    Mrithi nini wanangu?
  2. Sina ngo’mbe sina mbuzi, sina konde sina buwa
    Sina hata makaazi, mupasayo kuyajuwa
    Sina mazuri makuzi, jinsi nilivyoachwa
    Mrithi nini wanangu?
  3. Sina kazi sina bazi, ila wingi wa shakawa
    Sina chembe ya majazi, mno nikukamuliwa
    Nakwa’cheni upagazi, ngumu kwenu ku’tuwa
    Mrithi nini wanangu?
  4. Sina sikuachi jina, mkata hatasifiwa
    Hata nifanye la mana, mno mi kulaumiwa
    Poleni wangu sana, sana kwenu cha kutowa
    Mrithi nini wanangu?
  5. Sina leo sina jana, sina kesho kutwaliwa
    Sina zizi sina shina, wala tawi kuchipuwa
    Sina wanangu mi sina , sana la kuacha kuraduwa
    Mrithi nini wanangu?
  6. Sina utu sina haki, mila yangu meuliwa
    Nyuma yangu ili dhiki, na mbele imekaliwa
    N’nawana na miliki, hadi nitakapofukiwa
    Mrithi nini wanangu?
  7. Sina ila kesho kwenu, wenyewe kuiongowa
    Muwane kwa nyinyi mbinu, mwende pasi kupumuwa
    Leo siyo kesho yenu, kama mutajikamuwa
    Mrithi nini wanangu?
  1.    
    1. Taja mambo yoyote mawili ambayo mtunzi angewarithisha wanawe. (alama 2)
    2. Eleza sababu ya mtunzi kutoweza kuwarithisha wanawe. (alama 3)
    3. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 4)
    4. Dondoa mifano miwili miwili ya : (alama 2)
      1. Inkisari
      2. Tabdila
    5. Chambua shairi hili kwa upande wa :
      1. Dhamira (alama 2)
      2. Muundo (alama 4)
    6. Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kama vilivyotumiwa katika shairi. (alama 3)
      1. Mlimwengu kanipoka
      2. Sina konde sina buwa.
      3. Wingi wa shakawa.

MASWALI

  1.      
    • makazi mabovu
    • upagazi
    • kutothaminiwa
    • dhiki
    • kufanya kesho ya wengine nzuri
  2.      
    • ni maskini hohehahe / hana kitu
    • aliporwa kila kitu.
    • hana mifugo.
    • hana kazi yoyote.
    • hana sifa / umaarufu.
    • ana makazi mabovu.
  3.      
    • sina jina nitakawacha kwani maskini hasifiwi
    • hata nikifanya jambo la maana ninalaumiwa tu.
    • poleni sana wanangu kwa kuwa sina la kuwatolea.
    • mtarithi nini wanangu?
  4.        
    1. inkisari
      • Mana – maana
      • Meuliwa – imeuliwa
      • Nitapofukiwa – nitakapofukiwa.
    2. tabdila
      muruwa - murua
      kutowa -kutoa
      kuchipuwa -kuchipua
      kuiongowa - kuiongoa
      kupumuwa - kupumua
  5.    
    1. dhamira
      • Kuwahimiza watu kufanya bidii wakiwa vijana.
      • Kulalamika kwamba maskini hana haki / huonewa / hapewi nafasi.
    2. muundo
      • Shairi ni aina ya tarbia / unne.lina mishororo minne katika kila ubeti.
      • Mishororo ya kwanza mitatu imegawika katika sehemu mbili (ukwapi na utao).
      • Kila kipande kina mizani nane na kila mshororo una mizani kumi na sita.
      • Vina vya kati vinatofautiana kutoka ubeti mmoja hadi mwingine, lakini vina vya mwisho ni sawa katika shairi zima katika mishororo ya kwanza mitatu.
      • Shairi hili lina kibwagizo ambacho kimefupishwa.
        Mrithi nini wanangu?
      • shairi hili lina beti saba.
  6.    
    1. mlimwengu kunipoka - mlimwengu kanipokonya.
    2. sina konde sina buwa - sina shamba sina chochote.
    3. wingi wa shakawa – mashaka mengi.

USHAIRI 36

Mungu naomba subira, subira nayo imani
Imani iliyo bora, bora hapa duniani
Duniani mwa kombora, kombora nayo hiani
Hiani pamwe ukora wenye kuhini.

Kuhini kwenye kiburi, kiburi na ufidhulu
Ufidhuli wa kudhuri, kudhuri wangu muwili
Muwili hata kiclari, kidari kuwa thakili
Thakili kisinawiri, kisinawiri misuli.

Misuli kuwa hafith, hafifu kama muwele
Muwele wa hitilafu, hitilafi ya nduwele
Nduwele kutakilifu, kutakilifu milele
Milele kutoniafu, kutoniafu na vishale.

Vishale vinitomele, vitomele vikwato
Vikwato pia maole, maole kufanya mito
Mito ya matozi tele, tele mithili kitoto
Kitoto kilo vipele, vipele vyenye fiakuto.

Fukuto lanipa neno, neno hili kutamka
Kutamka wazi vino, vino subira kutaka
Kutaka imani mno, mno n’sipate wahaka
Wahaka wa matukano, matukano na mashaka.

Mashaka haya ya leo, leo yawe yamepita
Yaniepita na vilio, vilia vipishe nyota
Nyota njema ing’arao, ing’arao kunikita
Kunikita salamani, salamani nikadata.

 

  1. Kwa nini nafsi neni anaomba subira na amani. (al.2)
  2. Shairi hili ni la Bahari gani kwa kuzingatia;
    1. Mpangilio wa maneno. (Al. 4)
    2. Mpangilio wa vina.
  3. Kwa kutolea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi. (al.4)
  4. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (al.4)
  5. Kwa kutolea mifano, elezea jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi. (Al.6)

MAJIBU

  1. Kwa nini nafsi neni inaomba subira na amani. (al.2)
    • Ili asiwe na wasiwasi wa kutukanwa na kuhiniwa
    • Ili aepuke kufanyiawa mabaya (2 x2 =4)
  2. Shairi hili ni la Bahari gani kwa kuzingatia;
    1. Mpangilio wa maneno. (Al. 4)
      • Pindu/mkufu/nyoka
    2. Mpangilio wa vina.
      • Ukaraguni
  3. Kwa kutolea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi. (al.4)
    • Tashbihi – hafif kama muwele/ tele mithili kitoto
    • Takriri / uradidi – subira- subura, kiburi – kiburi, neno – neno (2 x2 =4)
  4. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (al.4)
    • Misulu kuwa dhaifu sana kama ya mgonjwa, hasa mgonjwa mwenye tatozo la uwele ambalo unasumbua daima na usiosikia dawa/ unaofisha/ usio na tiba
  5. Kwa kutolea mifano, elezea jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi. (Al.6)
    • Lahaja/ lugha kale – pamwe – pamoja na, matozi – machozi
    • Mazda – muwili – mwili
    • Inkisari – kitoto kilo vipele – kitoto kilicho na vipele n’sipate – nisipate
      (3 x 2 = 6)

USHAIRI 37

Niokoa muokozi, uniondolee mashaka
Kuyatukua siwezi, mjayo nimedhikika
Nimekitiri simanzi,ni katika kuudhika
Mja wako nasumbuka,nipate niyatakayo

Mja wako nasumbuka,nataka kwao afua
Nirehemu kwa haraka,nami nipate pumua
Naomba hisikitika,na mikono hiinua
Mtenda ndiwe moliwa,nipate niyatakayo

Mtenda ndiwe moliwa,we ndiwe Mola wa anga
Mazito kuyaondoa,pamoja na kuyatenga
Ukauepusha ukiwa,ya pingu zilonifunya
Nikundulia muwanga,nipate niyatakayo

Nikundulia muwanga,nipate toka kizani
Na huzuni n’ondolea,itoke kwangu moyoni
Mambo mema niegheshea,maovu nisitamani
Nitendea wa manani,nipate niyatakayo

Igeuze yangu nia,dhaifu unipe mema
Nili katika dunia,kwa afia na uzima
Moliwa nitimizia,yatimize yawe mema
Nifurahike mtima,nipate niyatakayo.

Maswali

  1. Eleza bahari zozote mbili za shairi hili (alama 4)
  2. Eleza muundo wa shairi hili (Alama 4)
  3. Mshairi ametumia uhuru wake wa utunzi. Eleza mifano minne huku ukitoa mifano (alama 4)
  4. Andika ubeti wa pili katika lugha nathari (alama 4)
  5. Fafanua dhamira ya mtunzi wa shairi hili (alama.2)
  6. Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumika katika shairi (alama 2)
    1. Nimedhihika
    2. Nifurahike mtima

MAJIBU

  1.                           
    • Mathnawi - pande mbili
    • Ukaraguni - vina hubadilika badilika
    • Pindu - sehemu ya mshororo wa mwisho unaanza mshororo unaofuatia
  2.          
    • beti tano
    • Mishororo mine kila ubeti
    • Kila mshororo pande mbili
    • Kila upande mizani mine
    • Hamna kibwagizo
  3.         
    • Inkisari-nondolea-niondolee
    • Zilonifunga-zilizonifunga
    • Mazida-muokozi-mwokozi
    • Kuboronga sarufi-iseuze yangu nia
    • Tabdila-afia-afya
  4.          
    • Kiumbe wako nimeteseka mno
    • Naoma unip afueni na unipe afueni na unirehemu
    • Niwaomba nikikusulia wewe diwe
    • Unayeweza kunipa ninayohitaji
  5.         
    • Kuonyesha njia hana nguvu
    • Mungu ampe maisha mema
    • Anataka Mungu anitoe gizani
    • Amekumbwa na majaribu
  6.         
    1. Nimeteseka
    2. Nichangamke/nistarehe

USHAIRI 38
Jogoo anapowika, ana jambo atangaza
Atangaza kuamka, limeshatanduka giza,
Giza limeshaondoka, uache kujidumaza,
Mwanamke amka!

Jogoo anapowika, mwanamke amjuza
Amjuza kuamka, amulikwe na mwangaza,
Mwangaza umeshafika, aache kujilegeza,
Mwanamke amka!

Jogoo anapowika, mwanamke ahimiza,
Ahimiza kutimka, mbio ili kujikuza,
Kujikuza si dhihaka, elimu kuitukuza,
Mwanamke amka!

Jogoo anapowika, mwanamke amkuza,
Amkuza kuzizika, tamaduni za kuviza,
Kuziviza kwa haraka, mila zinazopumbaza,
Mwanamke amka!

Jogoo anapowika, mwanamke atukuza,,
Atukuza amefika, kupokea yake tuza,
Tuza ya kurevuka, muamko kutangaza,
Mwanamke amka!

Jogoo anapowika, mwanamke akataza,
Akataza kutotaka, minyanyaso ya kuliza,
Kuliza na kuudhika, hakiye kugandamiza,
Mwanamke amka!

Jogoo anapowika, mwanamke amwongoza,
Amwongoza umefika, muda wa kuongoza,
Kuongoza kwa hakika, umma pasi kujitweza,
Mwanamke amka!

Jogoo anapowika, mwanamke azoweza,
Azoweza kurauka, kwa bidii kujikaza,
Kujikaza na kutoka, jikoni kulomviza,
Mwanamke amka!

  1. “Mtunzi wa shairi hili ananuia kumzindua nafsinenewa.” Jadili. (alama 7)
  2.  Ainisha bahari sita za shairi hili. (alama 6)
  3. Onyesha mbinu tatu alizozitumia mshairi kukidhi mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili. (alama 3)
  4. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha tutumbi. (alama 4)

MAJIBU

 

USHAIRI 39

Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata
Kiza nene kimetanda
Ukungu na umande
Zinashindana
Umweso unamulika
Radi nayo inapiga
Kimya!

Bundi na milio yao
Ama kweli, kimila si mazuri mambo.
Mebainika usiku, usiku mkuu, wa kiza nene.
Kiza! Kiza! Kiza!
Balaa! Balaa! Balaa!
Beluwa! Beluwa! Beluwa!
Sinyaa! Sinyaa! Sinyaa!

Kabla,
Inajipenyeza kwa umbali
Kwa umbali hakika
Inuka! Zungumza! Wamefika!
Hakika, sina cha kuwaeleza!
Hakika, zaidi ya kuwakemea, kuwakemea, kuwakaripia, kuwafokea,
Hakika, hakuna kutia, hakuna kutoa
Hakika, Hisabati kueleweka hakupo.
Haki, ukiukaji, melandana kama ulimi na mate!

Dovu hili dovu kubwa!
Lima hili, pandikizi
Uzito wa nanga, kukwepa hakukwepeki.
Wanasema faraghani, kwa mihemko!
“Watatu maghulamu,
Zao la ushuhuba, kando na mkataba.”
Ingawa, kwangu mimi, maana yaniambaa.

Kabla,
Najua fika kuwa,
Tumbo ndilo kisukumo, chanzo hasa.
Uki ulioacha, ndicho chanzo cha migogoro.
Migogoro isiyo ukomo
Kutokomea tokotoko.
Kwangu mezaa madhara.

Lakini.

Kabla ya Kabla,
Hafifu maninga yanatazama
Mwanga ukinyemelea,
Ishara kuwa,
“Yamekwisha!”
Tetesi zimekuwa feki! Kwa vile,
Nijuavyo,
Hata wawili wetu mabanati,
Hakika,
Ni zao la takrima ya akraba yako mnuna.
Hakika,
Ulikuwa ardhi tambarare.

  1. Kwa kutolea mifano, fafanua masuala makuu sita anayoyazungumzia mshairi. (alama 6)
  2. Onyesha vipengele vifuatavyo vilivyotumika katika shairi. (alama 6)
    1. Aina za taswira
    2. Taashira
    3. Aina za usambamba
  3. Huku ukitolea mifano, bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2)
  4. Fafanua toni inayojitokeza katika ubeti wa mwisho. (alama 2)
  5. Pambanua muundo wa shairi hili. (alama 4)

MAJIBU

 

USHAIRI 40

Jibu swali la 4 au la 5

  1. Soma shairi hili kisha ujibu maswali:

    Wanaume ni Wanyama

    Nakumbuka vyema sana, sisahau siku ile
    Nilipoitwa na nina, akanipa ya kivyele
    Mwanangu u msichana, nakuasa usikile
    Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.

    Kuwa umevunja ungo, ni hali ya maumbile
    Bora uwapo na bongo, anasa uzikimbile,
    Ukijitia maringo, utatungwa mimba mbele
    Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.

    Ngawa waje na manoti, “Nakupenda” wakwambile
    Wakuvalie makoti, usiwaachie mbele
    Hata wapige magoti, wambile mna kelele
    Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.

    Ngono ni tendo la suna, Amina sikimbile
    Wala miguu halina, kwamba lingekukimbile
    Muhimu kwako Amina, kwanza uthamini shule
    Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.

    Kuzurura mitaani, si tabia njema ile
    Unapotoka nyumbani, fululiza hadi shule
    Si kwenda vichochoroni, kuwaona kina wale
    Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.

    Uwe mwana msikizi, yano uyazingatile
    Mengine kuhusu penzi, mwanangu taonywa shule
    Kama mameyo mzazi, nimekuonya kimbile
    Si watu waone vile, wanaume ni wanyama

    Wakaja kina Hamadi, mwana wa Mzee Sule
    Kwangu wakapiga hodi, hata mkuu wa shule
    Ila nikajitahidi, kukwepa mitego ile
    Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.

    Na kuna Karisa, mwanafunzi kule shule
    Akawa hunipapasa, name pia vilevile
    Mwishowe itakupasa, tugawe tunda tulile
    Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.

    Nani akachovya uto, wa asali tamu vile
    Na kisha aape kuto, kula asali milele
    Kuwa mjamzito, wamenifukuza shule
    Si waone vile, wanaume ni wanyama.
    Karisa yu vilevile, angali ywaenda shule
    Na mie kitumbo mbele, ninajikuna upele
    Yameshatumia yale, niloonywa siku ile
    Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.

    Maswali:
    1. Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu. (alama 2)
    2. Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2)
    3. Bainsha mambo manne ambayo nafsineni anatoa kama ushauri kwa nafsinenewa. (alama 4)
    4. Huku ukitoa mifano, bainisha vipengele vitatu vya kimtindo ambapo mshairi ametumia kufanikisha uwasilishaji wa utungo huu. (alama 3)
    5. Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu. (alama 3)
    6. Andika ubeti wa sita kwa lugha nathari. (alama 4)
    7. Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2)

MAJIBU

  1. Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu. (alama 2)
    1. Ni tarbia (alama 1)
    2. Lina mishororo minne katika kila ubeti (alama 1)

  2. Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2)
    1. Kuwafunua macho vijana hasa wasichana kuhusu hatari zilizopo katika ujana
    2. Linalenga kuwatahadharisha wasichana dhidi ya hadaa kutoka kwa wanaume.(1x1=02)

  3. Bainsha mambo manne ambayo nafsineni anatoa kama ushauri kwa nafsinenewa.(alama 4)
    1. Akimbie anasa
    2. Asijitie maringo
    3. Asitungwe mimba
    4. Wanaume wakimwambia wanampenda awakimbie
    5. Asishiriki ngono
    6. Asizurure mtaani
    7. Akitoka nyumbani afululize
    8. Asitembee vichochoroni
    9. Ajiepushe na wanaume, ni mnyama (Za kwanza 4 x 1 = 4)

  4. Huku ukitoa mifano, bainisha vipengele vitatu vya kimtindo ambapo mshairi ametumia kufanikisha uwasilishaji wa utungo huu. (alama 3)
    1. Jazanda/istiari – wanaume ni wanyama (afafanue)
    2. Balagha – nani akachovya uto, wa asali tamu vile
    3. Takriri - si watu waona vile, wanaume ni wanyama
    4. Nahau –umevunja ungo – umekomaa (Za kwanza 3 x 1 = 3)

  5. Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu. (alama 3)
    1. Inkisari
      1. ngawa – ingawa
      2. Taonywa – utaonywa
      3. Mameyo – mama yako

    2. Tabdila –
      1. ukimbile – ukimbie
      2. Usikile – usikie
      3. Uzingatile – uzingatie

    3. Kubananga sarufi /kufinyanga sarufi/ miundo ngeu ya kisintaksia
      1. Ngoma ni tendo la suna, Amina sikimbilie – Amina sikimbilie ngono ni tendo la suna
      2. Kuzurura mitaani, si tabia njema ile – ile tabia ya kuzurura mitaani si njema
        (Za kwanza 3 x 1 = 3)

  6. Andika ubeti wa sita kwa lugha nathari. (alama 4)
    1. Uwe mwana anayesikia/ msikivu wa kuzingatia
    2. Mambo kuhusu mapenzi utaonywa shuleni
    3. Kama mama yako mzazi ninakuonya kimbele
    4. Ajihadhari na wanaume kwa sababu ni wanyama (Zozote 4 x 1 = 4)

  7. Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2)
    1. Mama yake mshauriwa kwa mfano, mamayo mzazi, nakuonya ukimbile

USHAIRI 41

Soma shairi hili kisha ujibu maswali:

Nikiwa na njaa na matambara mwilini
Nimehudumika kama hayawani
Kupigwa na kutukanwa
Kimya kama kupita kwa shetani
Nafasi ya kupumzika hakuna
Ya kulala hakuna
Ya kuwaza hakuna
Basi kwani hili kufanyika
Ni kosa gani lilotendeka
Liloniletea adhabu hii isomalizika?

Ewe mwewe urukaye juu angani
Wajua lililomo mwangu moyoni
Niambie pale mipunga inapopepea
Ikatema miale ya jua
Mamangu bado angali amesimama akinisubiri?
Je, nadhari hujitokeza usoni
Ikielekea huku kizuizini?

Mpenzi mama, nitarudi nyumbani
Nitarudi hata kama ni kifoni
Hata kama maiti yangu imekatikakatika
Vipande elfu, elfu kumi
Nitarudi nyumbani
Nikipenya kwenye ukuta huu
Nikipitia mwingine kama shetani
Nitarudi mpenzi mama...
Hata kama kifoni.

Maswali

  1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka (alama 1)
  2. Tambua nafsineni katika shairi hili (alama 1)
  3. Eleza toni katika shairi hili (alama 1)
  4. Taja mambo manne ambayo mshairi analalamikia (alama 4)
  5. Fafanua dhamira katika shairi hili (alama 2)
  6. Thibitisha kuwa hili ni shairi huru (alama 4)
  7. Taja na ufafanue sifa mbili za mshairi (alama 2)
  8. Fafanua mbinu tatu za kimtindo zilizotumika katika ubeti wa tatu. (alama 3)
  9. Eleza maana ya maneno yafuatoyo kama yalivyotumiwa katika shiari hili (alama 2)
    1. Hayawani
    2. Nadhari

MAJIBU

  1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka (alama 1)
    1. Mama nitarudi
    2. Nitarudi
    3. Kizuizini alama 1 (asizidishe maneno sita)

  2. Tambua nafsineni katika shairi hili (alama 1)
    1. Nafsineni ni aliye kizuizini. Anauliza iwapo mamake angali anasimama na kusubiri akitazama kule kizuizini aliko nafsineni (atambue na athibitishe alama 1/0)

  3. Eleza toni katika shairi hili (alama 1)
    1. Toni ya masikitiko / uchungu wa moyoni/huzuni kwa mfano, anasikitikia hali yake ya kuvaa matambara, njaa, kufanyiswha kazi tele
    2. Toni ya matumaini kwa mfano, mshairi ana matumaini kwamba siku moja atatoka kizuizini (atambue na athibitishe alama 1/0)

  4. Taja mambo manne ambayo mshairi analalamikia (alama 4)
    1. Kuachwa njaa
    2. Kufungwa
    3. Kufukuzwa
    4. Kutopewa nafasi ya kupumzika, kulala na kuwaza
    5. Kuvaa matambara
    6. Kufanyizwa kazi kama mnyama (Zozote 4 x 1 = 4)

  5. Fafanua dhamira katika shairi hili (alama 2)
    1. Mshairi anadhamiria kulalamikia/kukashifu namna anatumiwa vibaya kizuizini
    2. Mshairi anakashifu madhila na mateso ambayo wafungwa hutendewa
    3. Kumpa mamake matumaini kwamba atatoka kizuizini siku moja (Zozote 2 x 1 = 2)

  6. Thibitisha kuwa hili ni shairi huru (alama 4)
    1. Kuna matumizi ya mistari mishata
    2. Idadi ya mishororo inabadilikabadilika kutoka ubeti mmoja hadi nyingine
    3. Silabi za mwisho katika kila mshororo zinatofautiana
    4. Idadi ya mizani katika kila mshororo inatofautiana (Zozote 4 x 1 = 4)

  7. Taja na ufafanue sifa mbili za mshairi (alama 2)
    1. Ni mwenye kulalamika kwa mfano, analalamikia hali yake ya kuwa na njaa, kupigwa
    2. Mwenye matumaini kwa mfano, anatumai kuwa siku moja atatoka kizuizini
    3. Mwenye mapenzi kwa mfano, anampenda mamake na kumwita mama mpenzi
      (Zozote 2 x 2 = 4) kila sifa itolewe mfano - atuzwe 2/0

  8. Fafanua mbinu tatu za kimtindo zilizotumika katika ubeti wa tatu. (alama 3)
    1. Takriri kwa mfano, neno nitarudi limerudiwarudiwa
    2. Mdokezo kwa mfano, nitarudi mama mpenzi
    3. Tashibihi kwa mfano, kupitia mwingine kama shetani
    4. Balagha kwa mfano, Ni kosa gani lilotendeka - Liloniletea adhabu hii isomalizika? (Za kwanza 3 x 1 = 3)

  9. Eleza maana ya maneno yafuatoyo kama yalivyotumiwa katika shiari hili (alama 2)
    1. Hayawani - mnyama
    2. Nadhari - fikira
      (Za kwanza 2 x 1 = 1)

USHAIRI 42
Kila mdharau chake
Kuzimu wenda kuona, kila mdarau chake,
Cha kwake akakikana, kutumai cha mwenzake,
Fahamu anayo lana, mpiga chake mateke,
            Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona.

Siringe na kujivuna, chako ukakipa teke,
Unajivuna, chako ukakipa teke,
Unavunja lako jina, ili watu wakucheke,
Ana lana kwa Rabana, kila mdharau chake,
              Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona

Chako japo si cha mana, kibaya mtu ni chake,
Unavunja lako jina, ili watu wakucheke,
Ana lana kwa Rabana, kila mdharau chake,
               Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona

Awe Fatu na Amina, Asha ndung yake,
Katu hawatafanana, kila mtu hadhi yake,
Kila mjuzi wa mama, huwa hadharau chake
                  Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona

Tama naomba amina , kilicho chetu tushike,
Kidumu na kulingana, na tukipe hadhi yake,
Ana lana kwa Rabana, kila mdharau chake,
                    Kila mdharau chake, kuzimu enda kuona

Maswali:

  1.  
    1. Eleza ujumbe unaosisitizwa katika shairi hili (alama2)
    2. Mshairi anatoa ushauri gani katika utungo huu? (alama 2)
  2. Neno lana limefupishwa:
    1. Kwa nini limefupishwa (alalma2)
    2. Kutokana na shairi hili toa neno jingine lililofupishwa, kisha uliandike ukamilifu wake. (alama2)
  3. Eleza maana ya;
    1. chako ukakipa teke. (alama2)
    2. unavunja lako jina (alama 2)
  4.  
    1. Mstari wa mwisho wa kila ubeti wa shairi hili huitwaje (alama 1)
    2. Andika methali yenye maana karibu sawa na mstari wa mwisho wa kila ubeti wa shairi hili   (alama2)
  5. katika ubeti wa 4 kwa nini mshairi akasema (alama 2)
    Awe Fatu na Amina, au Asha ndungu yake, katu hawatafanana?
  6. Eleza maana ya:
    1. Kuzimu
    2. Kutumai
    3. Hadhi

MAJIBU

  1.  
    1. Yule anayedharau kitu chake na kukiona kuwa hakina thamana aatakuja kujuta.
    2. Mtu kama huyo pia atapata laana kutoka kwa mola. Chako hata kama hakina thamani ukipende na kukipalilia, usitamani cha mwingine. Kila mtu ana bahati yake alioumbiwa na Mungu.
      Penda chako na kukipalilia usitamani cha mwenzako.
  2.  
    1. Kutosheleza mizani/kupata idadai kamili ya mizani
    2. Wenda-unaenda/enda-anaenda/japo—ijapo/mana-maana/tama-tamati/kutumai-kutumaini.
  3.  
    1. Kuachana nacho/ kukidharau chako/kukiona chako duni/kikiona hakifai.
    2. Unaharibu sifa zako/unaharibu hadhi yako/unalizika jina lako/ unajipaka tope
  4.  
    1. Kibwagizo/kipokeo/mkarara/kiitikio.
    2. Kitu cha mwenzio usikilalie mlango wazi.
  5. Kila mtu ana bahati yake na uwezo wake. Hakuna watu wawili duniani walio na bahati/uwezo sawa,haa kama ni nduguyo.
  6.  
    1. Jehenamu/kuona mabaya/mabaya kukufukia/kujutia.
    2. Kutamani/kutegemea.
    3. Bahati/ kipawa/ uwezo.

USHAIRI 43
Sikate tama
Umeanguka, inuka, simama kama mnazi
Umechunika,inuka, tia dawa kwa ujuzi
Sasa inuka,inuka, kijana ianze kazi
Sikate tama

Usife tama, nyanyuka, ni muweza wa kutenda
Kuna hadaa ,nyanyuka,anza tena kujipinda
Dunia baa, nyanyuka,anza tena kujiunda
Sikate tamaa

Sivunjwe moyo, dunia hivyo itakunyanyasa
Futa kiliyo, dunia hiyo idhibiti sasa
Ipe kamiyo, dunia kamwe, siache kufusa
Sikate tama.

Una nguvuu, simama, wewe upambano nao
Una werevu, simama, uzepuke njama zao
Usiche kovu, simama, ujifunze vumilio
Sikate tamaa
(S.A Mohamed)

Maswali:

  1. Eleza lengo la shairi hili (alama2)
  2. Mshairi anatumia mtindo gani ili kusisitiza ujumbe wake? Toa mfano moja. (alama 3)
  3. Kulingana na mshairi tungewezaje kuepuka njama unazofanyiwa? (alama 1)
  4. Mshairi anamaanisha nini kwa kusema usicho kovu? (alama2)
  5. Kwa nini mshairi akasema: sikate tama badala ya usikate tama? (alama2)
  6. Kuvujwa moyo kunaleta matokeo gani? (alama 1)
  7. Eleza muundo wa ubeti wa kwanza wa shairi hili (alama 4)
  8. Taja sifa mbili zozote zinazoewa msomaji (alama2)
  9. Mshairi anasema: “ umeanguka, umechunika,futa kiliyo.” Mambo haya matatu yanachangiza vipi katika kuendeleza lengo la mshairi. (alama 3)

MAJIBU

  1. Mshairi ana himiza aliyepata shida asife moyo bal ajitokokote na aanze tena
  2. Takriri-kurudia kibwagizo-sikate tama.kikwamba-kuruda kwa neno/maneno umeanguka,umechunika inuka.
  3. Kusimama imara,kutumia akili ulizonazo.
  4. Usifikirie yaliyopita(shida) lakini utie bidii na kuangalia na kutenda ya sasa.
  5. Kufupisha ili kutosheleza mizani
  6. Kuangamia.
  7. Mishororo mine(tarbia).Migao 3 kwa mishororo 10 kwa ubeti –ka-ka-zi isipokuwa kibwagizo
    Mizani 5-3-8=16
  8.  
    • Ana uwezo wa kutenda
    • Ana werevu wa kutenda
    • Ana nguvu za kutenda
  9. Yanamhimiza aliyepata shida afute kilio(ajitahidi kuweza kutatua shida aliyopata).

USHAIRI 44
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Maendeleo ya umma
Sio vitu maghalani
Kama tele vimesaki
Lakini havishikiki
Ama havikamatiki
Bei juu

Maendeleo ya umma
Sio vitu gulioni
Kuviona madukani
Kuvishika mikononi
Na huku wavitamani
Kama tama ya fisi
Kuvipata ng’o

Maendeleo ya umma
Sio vitu shubakani
Dhiki ni kwa mafakiri
Nafuu kwa mafakiri
Ni wao tu washitiri
Huo ni uistimari
Lo! Warudia

Maendeleo ya umma
Ni vitu kumilikiwa
Na wanyonge kupatiwa
Kwa bei kuzingatiwa
Bila ya kudhulumiwa
Na hata kuhadaiwa
Hiyo ni haki.

Maendeleo ya umma
Dola kudhibiti vitu
Vijapo nchini mwetu
Na kuwauzia watu
Toka nguo na sapatu
Pasibakishiwe na kitu
Huo usawa.

Maendeleo ya umma
Watu kuwa na kauli
Katika zao shughuli
Vikaoni kujadili
Na mwisho kuyakubali
Maamuzi halali
Udikteta la.

Maendeleo ya umma
Watu kuwa waungwana
Vijakazi na watwana
Nchini kuwa hakuna
Wote kuheshimiana
Wazee hata vijana.

Maswali

  1. Eleza dhamira ya shairi hili. (al.2)
  2. Baininsha tamathali mbili za usemi katika shairi hili. (al.2)
  3. Eleza umuhimu tatu wa usambamba katika shairi hili. (al.2)
  4. Onyesha jinsi maendeleo ya umma ulivyo kinaya. (al.2)
  5. Eleza mambo ambayo mshairi nachukulia kuwa maendelo halisi ya umma. (al.4)
  6. Tambua matumizi ya mstari mishata kwa kutolea mifano. (al.2)
  7. Bainisha nafsi neni katika shairi hili. (al.1)
  8. Fafanua toni ya shairi hili. (al.1)
  9. Andika ubeti wanne kwa lugha nathari. (al.4)

MAJIBU

  1. Eleza dhamira ya shairi hili. (al.2)
    • Anadhamiria kuonyesha wanyonge wanastahili usawa na haki – na wanyonge kupatiwa kwa bei kuzingatiwa bila kudhulumiwa – ubeti wa 4
  2. Baininsha tamathali mbili za usemi katika shairi hili. (al.2)
    • Tashbihi – ni kama la moto, wavitamani kama tama ya fisi
    • Takriri – Maendeleo ya umma
    • Nidaa – Lo!
  3. Eleza umuhimu tatu wa usambamba katika shairi hili. (al.2)
    • Maendeleo ya umma (urudiaji wa fungu) – kusisitiza ujumbe
    • Urudiaji wa silabi …..ni, ki – kuleta ridhimu
    • Urudiaji wa neno.
  4. Onyesha jinsi maendeleo ya umma ulivyo kinaya. (al.2)
    • Ni kinaya kuwa tuna vitu tele lakini bei I juu
    • Ni kinaya kuviona vitu madukani lakini kuvipata ng’o
  5. Eleza mambo ambayo mshairi nachukulia kuwa maendelo halisi ya umma. (al.4)
    • Vitu kumilikiwa na wanyone kupiwa.
    • Bei kuzingatiwa bila kudhulumiwa
    • Dola kudhibiti vitu vijapo nchini mwetu.
    • Watu kuwa na kauli katika shughulika zao.
    • Watu kuwa waungwana.
  6. Tambua matumizi ya mstari mishata kwa kutolea mifano. (al.2)
    • Mishororo ambayo si toshelezi katka shairi
    • Maendeleo ya umma
  7. Bainisha nafsi neni katika shairi hili. (al.1)
    • Ni mzalendo/mwananchi-nchini mwet ubeti 5
    • Mtetezi wa haki – ubeti 4
  8. Fafanua toni ya shairi hili. (al.1)
    • Kuhamasisha
    • Kuzindua
  9. Andika ubeti wanne kwa lugha nathari. (al.4)
    • Maendeleo ya umma ni kutafuta vitu na kuwauzia wanyonge kwa bei nafuu pasi na kunyanyasua wala kudanganywa na hivyo kulinda haki zao 

USHAIRI 45
Joseph Kiponda : Taifa ni Ushuru

Lau kama ingakuwa, madhali tuna uhuru
Watu kodi kutotowa, na kuifanya kufuru
Vije nchi ingakuwa, taifa bila ndururu
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru

Hivi taifa kumea, nakuendelea mbele
Kwamba lajitegemea, haliwategei wale
Yataka kujitolea, ushuru bila kelele
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru

Wafanyikazi wa umma, mfano mwema walimu
Wauguzi mahashuma, daktari wahadimu
Bila hizi darahima, vipi wangalihudumu?
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru

Si vyema kuombaomba, kwa wageni kila mara
Huwa twajifunga kamba, na kujitia izara
Adha zinapotukumba, kujitegemea bora
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru.

Miradi ya maendeleo, yahitaji darahima
Ndo tufikie upeo, ulio dunia nzima
Wadogo na wenye vyeo, bila kodi tutakwama
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru

Ushuru si kwa wanyonge, wasokuwa na uwezo
Watozwe hata wabunge, na wengine wenye nazo
Yeyote asijitenge, kodi akalipa bezo
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru

Kwetu kutoa ushuru, ndiko kujitegemea
Pasiwepo na udhuru, sio wa kuelea
Huwa ni kama kiguru, asenao kutembea
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru.

Maswali

  1. Ujumbe unaowasilishwa katika shairi hili, una hadhira legwa. Zitaje. (al.3)
  2. Kwa kutolea mifano, eleza aina tatu za idhini ya kishairi alizozitumia mshairi. (al.3)
  3. Huku ukitoa mifano, taja aina tatu za takriri zinazojitokeza katika utungo huu. (al.3)
  4. Fafanua bahari zinazojitokeza katika shairi hili. ( al.4)
  5. Andika ubeti wa nne katika lugha nathari. (al.4)
  6. Taja mbinu tatu za kifani zilizotumika katika shairi hili. (al.3)

MAJIBU

  1.  
    • Wafanyikazi wa umma
    • Maskini na tajiri
    • Wadogo na wenye vyeo.
  2.  
    • Inkisari –maendeleo , ndo/ndio
    • Tabdila – Kutotowa /kutotoa
    • Kuboronga sarufi-Kujitegemea bora/bora kujitegemea.
  3.  
    • Takriri neno-shuru ubet 2
    • takriri sialbi – vina katikati kila ubeti
  4.  
    • Mathnawi- vipande 2 kila mshororo
    • Ukaraguni – vina vinabadilika ubeti hadi mwingine
    • Kibwagizo- mshororo wa mwisho umerudiwa kila ubeti .
    • Tarbia – mishororo 4 kila ubeti.
  5.  
    • Si vizuri kuomba misaada ya kigeni kila wakati.
    • Hivyo ni sawa na kuwa mateka
    • Ni vyema kujitegemea kwa shida zetu
    • Taifa haliwezi kuimarika bila ushuru

  6.  
    • Maswali balagha – vipi wangalihudumu
    • Jazanda /sitiari- twajifunga kamba/ kiguru
    • Tashbihi – ni kama kiguru

USHAIRI 46
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

Kiapo kwao majaji, wanosimamia haki
Kwa sharia ni magwiji, wahalifu hawatoki,
Wengi wao ni walaji, kwa rushwa ni mashabiki,
Kwa rushwa mashabiki.

Kiapo kwa daktari, wagonjwa hawadhiliki,
Kazi zao ni dhariri, maradhi hayakwepeki,
Na wengine ni hatari, bila pesa hutibiki,
Bila pesa hutibiki.

Kiapo cha mawaziri, kwa mbwembwe na itifaki,
Na suti zao nzuri, shingo tai haitoki,
Na wengi wana dosari, ni kwa mikataba feki,
Ni kwa mikataba feki.

Kiapo cha magavana, mikoa kuimiliki,
Hujifanya ni mabwana, wala hawasogeleki,
Nayo nchi huitafuna, na kuwa haikaliki
Na kuwa haikaliki

Kiapo cha maraisi, kwa mizinga na fataki,
Na wageni mahususi, hualikwa kushiriki,
Ikulu wakijilisi, kwa wizi hawashikiki
Kwa wizi hawashikiki. 

Viapo vya utiifu, kwa sasa havistahiki
Wanoapa ni wachafu, tena hawaaminiki,
Biblia misahafu, washikapo unafiki
Washikapo unafiki

Maswali

  1. ‘’Dhamira ya shairi hili ni kushtumu ukiukaji wa maadili ya kikazi.’’ Jadili. (alama 3)
  2. Eleza namna vipengele vifuatavyo vya kimtindo vilivyotumika katika shairi hili.
    1. Usambamba ( alama 2)
    2. Aina za taswira ( alama 3)
  3. Bainisha toni katika shairi hili. (alama 2)
  4. Fafanua mbinu mbili alizotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili. (alama 4)
  5. Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo; ( alama 3)
    1. Mpangilio wa vina
    2. Mizani
    3. Mpangilio wa maneno
  6. Fafanua muundo wa shairi hili. (alama 3)

MAJIBU

  1. ukiukaji wa maadili ya kikazi
    • majaji wanaostahili kutetea haki ni walaji rushwa
    • madaktari hawawajibiki kwa matibabu na kuwa magonjwa hayatibiki
    • madaktari wanakwenda kinyume na kiapo chao kwa kuweka pesa mbele.
    •  Licha ya mbwembwe nyingi za kiapo cha mawaziri, wana mikataba ghushi.
    • Magavana wanatafuna nchi na kuwa haikaliki.
    • Viongozi ni wanafiki hawaaminiki.
    • Maraisi wanashabikia wizi.
    • Waapaji ni wanafiki
      Zozote 3
  2. mbinu za kimtindo
    1. usambamba
      • Kila ubeti unaanza kwa neno kiapo
      • Sehemu ya utao ya mshororo wa tatu katika kila ubeti inarudiwa katika kimalizio
        Alama 2
    2. aina za Taswira
      • Taswira oni- kiapo cha mawaziri, shingo tai haitoki
      • Taswira sikivu- kwa mizinga na fataki
      • Taswira mwonjo- wengi wao ni walaji
        Alama 3
  3. toni katika shairi
    • Kulalamika- kuna ukosefu wa uwajibikaji kazini
    • Kushtumu/ kusuta- majaji wanaostahili kutetea haki ni walaji rushwa
      1*2= 2
  4. idhini/ uhuru wa mshairi
    • Utohozi- feki
    • Tabdila- dakitari
    • Kuboronga sarufi- shingo tai haitoki
    • Inkisari- wanosimama- wanaosimama
      Alama 4
  5. Aina ya shairi
    1. Mpangilio wa vina- ukara- vina vya nje vinatiririka ilhali vya ndani vinabadilika badilika
    2. Mizani- msuko- kimalizio kimefupishwa
    3. Mpangilio wa maneno- kikwamba- neno kiapo limetumika kuanzia mwanzo wa kila ubeti.
      Pindu- sehemu ya utao ya mshororo wa tatu katika kila ubeti inarudiwa katika kimalizio
      Alama 3
  6.                
    1. shairi hili lina beti tano
    2. kila ubeti una mishororo mine
    3. lina pande mbili; ukwapi na utao
    4. kituo kimefupishwa
    5. vina vya nje vinatiririka ilhali vya ndani havitiririki
    6. mizani 8, 8 kwa kila mshororo ila kwa kituo n inane.
      Zozote 3
      Tamthilia kigogo

USHAIRI 47
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Maendeleo ya umma
Sio vitu maghalani
Kama tele vimesaki
Lakini havishikiki
Ama havikamatiki
Bei juu
Maendeleo ya umma
Sio vitu gulioni
Kuviona madukani
Kuvishika mikononi
Na huku wavitamani
Kama tama ya fisi
Kuvipata ng’o
Maendeleo ya umma
Sio vitu shubakani
Dhiki ni kwa mafakiri
Nafuu kwa mafakiri
Ni wao tu washitiri
Huo ni uistimari
Lo! Warudia
Maendeleo ya umma
Ni vitu kumilikiwa
Na wanyonge kupatiwa
Kwa bei kuzingatiwa
Bila ya kudhulumiwa
Na hata kuhadaiwa
Hiyo ni haki.
Maendeleo ya umma
Dola kudhibiti vitu
Vijapo nchini mwetu
Na kuwauzia watu
Toka nguo na sapatu
Pasibakishiwe na kitu
Huo usawa.
Maendeleo ya umma
Watu kuwa na kauli
Katika zao shughuli
Vikaoni kujadili
Na mwisho kuyakubali
Maamuzi halali
Udikteta la.
Maendeleo ya umma
Watu kuwa waungwana
Vijakazi na watwana
Nchini kuwa hakuna
Wote kuheshimiana
Wazee hata vijana.
Maswali

  1. Eleza dhamira ya shairi hili. (al.2)
  2. Baininsha tamathali mbili za usemi katika shairi hili. (al.2)
  3. Eleza umuhimu tatu wa usambamba katika shairi hili. (al.2)
  4. Onyesha jinsi maendeleo ya umma ulivyo kinaya. (al.2)
  5. Eleza mambo ambayo mshairi nachukulia kuwa maendelo halisi ya umma. (al.4)
  6. Tambua matumizi ya mstari mishata kwa kutolea mifano. (al.2)
  7. Bainisha nafsi neni katika shairi hili. (al.1)
  8. Fafanua toni ya shairi hili. (al.1)
  9. Andika ubeti wanne kwa lugha nathari. (al.4)

MAJIBU

  1. Eleza dhamira ya shairi hili. (al.2)
    Anadhamiria kuonyesha wanyonge wanastahili usawa na haki – na wanyonge kupatiwa kwa bei kuzingatiwa bila kudhulumiwa – ubeti wa 4
  2. Baininsha tamathali mbili za usemi katika shairi hili. (al.2)
    Tashbihi – ni kama la moto, wavitamani kama tama ya fisi
    Takriri – Maendeleo ya umma
    Nidaa – Lo!
  3. Eleza umuhimu tatu wa usambamba katika shairi hili. (al.2)
    Maendeleo ya umma (urudiaji wa fungu) – kusisitiza ujumbe
    Urudiaji wa silabi …..ni, ki – kuleta ridhimu
    Urudiaji wa neno.
  4. Onyesha jinsi maendeleo ya umma ulivyo kinaya. (al.2)
    Ni kinaya kuwa tuna vitu tele lakini bei I juu
    Ni kinaya kuviona vitu madukani lakini kuvipata ng’o
  5. Eleza mambo ambayo mshairi nachukulia kuwa maendelo halisi ya umma. (al.4)
    Vitu kumilikiwa na wanyone kupiwa.
    Bei kuzingatiwa bila kudhulumiwa
    Dola kudhibiti vitu vijapo nchini mwetu.
    Watu kuwa na kauli katika shughulika zao.
    Watu kuwa waungwana.
  6. Tambua matumizi ya mstari mishata kwa kutolea mifano. (al.2)
    Mishororo ambayo si toshelezi katka shairi
    Maendeleo ya umma
  7. Bainisha nafsi neni katika shairi hili. (al.1)
    Ni mzalendo/mwananchi-nchini mwet ubeti 5
    Mtetezi wa haki – ubeti 4
  8. Fafanua toni ya shairi hili. (al.1)
    Kuhamasisha
    Kuzindua
  9. Andika ubeti wanne kwa lugha nathari. (al.4)
    Maendeleo ya umma ni kutafuta vitu na kuwauzia wanyonge kwa bei nafuu pasi na kunyanyasua wala kudanganywa na hivyo kulinda haki zao

USHAIRI 48
Joseph Kiponda : Taifa ni Ushuru

Lau kama ingakuwa, madhali tuna uhuru
Watu kodi kutotowa, na kuifanya kufuru
Vije nchi ingakuwa, taifa bila ndururu
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Hivi taifa kumea, nakuendelea mbele
Kwamba lajitegemea, haliwategei wale
Yataka kujitolea, ushuru bila kelele
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Wafanyikazi wa umma, mfano mwema walimu
Wauguzi mahashuma, daktari wahadimu
Bila hizi darahima, vipi wangalihudumu?
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Si vyema kuombaomba, kwa wageni kila mara
Huwa twajifunga kamba, na kujitia izara
Adha zinapotukumba, kujitegemea bora
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru.
Miradi ya maendeleo, yahitaji darahima
Ndo tufikie upeo, ulio dunia nzima
Wadogo na wenye vyeo, bila kodi tutakwama
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Ushuru si kwa wanyonge, wasokuwa na uwezo
Watozwe hata wabunge, na wengine wenye nazo
Yeyote asijitenge, kodi akalipa bezo
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Kwetu kutoa ushuru, ndiko kujitegemea
Pasiwepo na udhuru, sio wa kuelea
Huwa ni kama kiguru, asenao kutembea
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru.
Maswali

  1. Ujumbe unaowasilishwa katika shairi hili, una hadhira legwa. Zitaje. (al.3)
  2. Kwa kutolea mifano, eleza aina tatu za idhini ya kishairi alizozitumia mshairi. (al.3)
  3. Huku ukitoa mifano, taja aina tatu za takriri zinazojitokeza katika utungo huu. (al.3)
  4. Fafanua bahari zinazojitokeza katika shairi hili. ( al.4)
  5. Andika ubeti wa nne katika lugha nathari. (al.4)
  6. Taja mbinu tatu za kifani zilizotumika katika shairi hili. (al.3)

MAJIBU

  1. Wafanyikazi wa umma
    • Maskini na tajiri
    • Wadogo na wenye vyeo.
  2. Inkisari –maendeleo , ndo/ndio
    Tabdila – Kutotowa /kutotoa
    Kuboronga sarufi-Kujitegemea bora/bora kujitegemea.
  3. Takriri neno-shuru ubet 2
    takriri sialbi – vina katikati kila ubeti
  4. Mathnawi- vipande 2 kila mshororo
    Ukaraguni – vina vinabadilika ubeti hadi mwingine
    Kibwagizo- mshororo wa mwisho umerudiwa kila ubeti .
    Tarbia – mishororo 4 kila ubeti.
  5. Si vizuri kuomba misaada ya kigeni kila wakati.
    Hivyo ni sawa na kuwa mateka
    Ni vyema kujitegemea kwa shida zetu
    Taifa haliwezi kuimarika bila ushuru
  6. Maswali balagha – vipi wangalihudumu
    Jazanda /sitiari- twajifunga kamba/ kiguru
    Tashbihi – ni kama kiguru

USHAIRI 49
Daima alfajiri na mapema

Hunipitia na jembe na kotama

Katika njia iendayo kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani;
Nimuonapo huwa anatabasamu
Kama mtu aliye na kubwa hamu

Kushika mpini na kutokwa jasho
Ili kujikimu kupata malisho.
Anapotembea anasikiliza
Videge vya anga vinavyotumbuiza

Utadhani huwa vimemngojea
Kwa usiku kucha kuja kumwimbia;
Pia pepo baridi kumpepea

Rihi ya maua zikimletea
Nao umande kumbusu miguu;
Ni miti yote hujipinda migongo

Kumpapasa, kumtoa matongo;
Na yeye kuendelea kwa furaha

Kuliko yeyote ninayemjua

Akichekelea ha hahahahahaha ...
Na mimi kubaki kujiuliza
Kuna siri gani inayomliwaza?
Au ni kujua au kutojua?
Furaha ya mtu ni furaha gani

Katika dunia inayomhini?
Ukali wa jua wamnyima zao

Soko la dunia lamkaba koo;
Dini za kudhani za msonga roho

Ayalimia matumbo ya waroho;
Kuna jambo gani linamridhisha?
Kama sikujua ni kutokujua

Laiti angalijua, laiti angalijua!

  1. Eleza matatizo manne yanayompata mzungumziwa. (Alama 4)
  2. Eleza mtindo wa lugha uliotumiwa na mshairi na utoe mifano. (Alama 8)
  3. Taja nafsineni katika shairi hili. (Alama 1)
  4. Eleza toni ya shairi hili. (Alama1 )
  5. Taja mbinu mbili za uhuru wa kishairi uliotumika na utoe mifano. ( Alama 2)
  6. Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya nathari. (Alama 4)

MAJIBU

  1.           
    • Ukali wa jua unaharibu zao.
    • Soko la dunia ni mbaya.
    • Dini za kudhani zamsonga roho.
    • Analimia waroho au wenye pupa. (4x1)

  2.      
    • Tashbihi
      • Katika njia iendayo kondeni
      • Kama walivyofanya babuze zamani.
    • Balagha
      • Kuna jambo gani linamridhisha
      • Kuna siri inayomliwaza.
    • Tanakali za sauti – Alichekelea ha ha ha ha ...
    • Taswira - videge vya anga vinavyotumbuiza
    • Tashihisi – Nao umande kumbusu miguu.
    • Msemo - kumkaba koo – kuumiza.
    • Takriri - Laiti angalijua, laity angalijua. (4x2)
  3. Mkulima (1x1)
  4. Malalamishi/huruma (1x1)
  5. Kuboronga sarufi
    • Kama mtu aliye na hamu kubwa.
    • Lahaja - kotama. (2x1)
  6. Kila asubuhi anapita akiwa na jembe akielekea shambani. Kama walivyofanya babu zake.Ninapomuona huwa ana furaha kama mtu aliye na tamaa kubwa ya kulima na kutokwa na jasho ili apate kujilisha. (4x1)

USHAIRI 50

Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili
Kwa kazi nihusike, samahani, unahili kimwili
Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili

Vitisho pamwe kelele, ninavicha, kwa nafsi na mwili
Ila ugonjwa utimile, umechacha, na kuudhili mwili
Msikose simile, magalacha, si gurudumu mwili.

Vingekuwepo viraka, kuutia, ngeushuruti mwili
Kifundi kivipachika, kuingia, hata kuridhi mwili
Upya ukaungilika, kuvutia, roho na wake mwili.

Lakini kamwe haiwi, kuvipata, vipande vyake mwili
Si hofu kupata mawi, sitajua, kupigania mwili
Hata kufutwa sikawi, nitakita, kidete nao mwili.

Kazi ninaithamini, ni hakika, akilini na mwili
Ila kamwe siamini, kusagika, damu, jasho na mwili
Uwele hususani, kioneka, nguvu hitishi mwili.

  1. Liweke shairi hili katika bahari tatu. (Alama 3)
  2. Eleza dhamira ya mshairi. (Alama 2)
  3. Elezamuundowashairihili. (Alama 4)
  4. Toa mifano ya uhuru wa kishairi uliotumika. ( Alama 4)
  5. Eleza kwa kifupi maudhui matatu yanayojitokeza katika shairi hili. (Alama 3)
  6. Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya nathari. (Alama 4)

MAJIBU

  1.      
    • Ukawafi
    • Tathlitha
    • Ukara (3x1)
  2. Anaonyesha vile mfanyakazi mwenye bidii ambaye anaugua na kushindwa kufanya kazi. (1x2)
  3.          
    • Lina mishororo mitatu kila ubeti
    • Lina beti tano
    • Kila mshororo umegawa vipande vitatu
    • Vina vya kati havifanani lakini vya mwisho vinafanana.Lina silabi hizi 8,4,7 (4x1)
  4.         
    • Inkisari – ngeushuruti
    • Tabdila - Utimile
    • Kufinyanga lugha - lakini kamwe haiwi. Zozote (2x2)
  5.     
    • Magonjwa
    • Kazi
    • Bidii
    • Dhuluma kutoka kwa waajiri. (3x1)
  6.       
    • Ningetaka kufika leo lakini mwili una maumivu.
    • Niweze kufanya kazi lakini mwili unakataa.
    • Ningependa kuwa mmoja wanaohusika lakini mwili umeshindwa. ( 4x1)

Ushairi 51

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Ewe hisia!
Umeniamshia ndoto niloisahau zamani
    nyimbo ya kale
    na mdundo usonivutia
    ila hayawani na mwangu rohoni.

Tulia sasa tulia
Hebu tulia ewe hisia ulo mtimani
Nataka katu kusisimka
         kwa sauti yako laini
Kwani njia zetu ni
         daima hazioani

Umesubutu vipi kuniita
      kutoka mwako ngomeni
     ulimosahauliwa tangu zamani
Basi yawache maombolezi yako yaso maoni,
     yawateke hao mashujaa wa kale
     wafu walo kaburini.

Hebu tulia, usiniingilie
         Usinihangaishe!
Kukuandama katu haimkini
Kwani hata sasa…kwa kukuwaza tu dakika hini
         naona majuto ya mbali moyoni
         kama kwamba nimegawa wangu wakati
         na wazimu, majinuni.
Basi nenda zako hisia…shuu…hebu tokomea.

Maswali

  1. Huu ni utungo wa aina gani?           (alama 2)
  2. Huku ukitoa mifano, fafanua sifa zinazoufanya utungo huu kuwa shairi      (alama 5)
  3. Mistari mishata ni nini? Toa mifano kwenye shairi hili.         (alama 4)
  4. Fafanua tamathali za kifasihi katika shairi hili.         (alama 3)
  5. Eleza mbinu tatu alizotumia mtunzi kutosheleza kaida za kishairi.         (alama 6)

Majibu

  1. Ushairi huru/ shairi la kimapinduzi – kwa sababu utungo huu hauzingatii urari wa vina, urari wa mizani n.k.
    Kutaja  - alama 1
    Sababu – alama 1
  2.  
    • Kuwepo kwa mishororo
    • Umegawika katika beti
    • Baadhi ya mishororo inaelekea kuwa na vina
    • Matumizi ya takriri
    • Matumizi ya lugha ya mkato   (5 x 1 = 5 )
  3. Ni mistari isiyokamilika kimaana na huhitaji msomaji kuusoma mstari unaofuata ili kupata maana. Kwa mfano:
    • nyimbo ya kale – ubeti 1
    • na muundo unaovutia – ubeti 1
    • kwa sauti yako laini – ubeti 2
    • daima hazioni – ubeti 2
    • Kutoa maelezo ya mshata – alama 2
      Mifano yoyote miwili – alama 2
  4.  
    • Tashihisi – hisia kupewa uhai
    • Sitiari – ndoto, hisia
    • Tashbihi – majuto ya mbali moyoni kama kwamba …  (zozote 3 x1 = 3)
  5.  
    • Inkisari: niloisahau badala ya niliyoisahau
    • Tabdila: umesubutu badala ya umethubutu
    • Kikale: mtimani badala ya moyoni   (3 x 2 = 6

Ushairi 52

Soma shairi lifwatalo kisha uyajibu maswali yanayoliandama:
Naandika yangu haya, kwa uwezo wa Wadudi,
Kanipa njema afiya, kumsifu sina budi,
Nifundishie insiya, hino methali ya jadi,
Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo

Ago mchama huuya, mbele mambo yakizidi,
Hurudi pakawa kaya, kupapenda hana budi,
Kwingi angawayawaya, ago shuruti arudi,
Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo.

Kule kwetu Mwarakaya, kijiji chetu cha jadi,
Yalidhihirika haya, bwana mmmoja mkaidi,
Aloalikwa ulaya, kadhani ‘mepata sudi,
Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo,

Alidhani hatauya, ‘endapo nchi baidi,
Na kusema bila haya, kwa inda na ukaidi,
Kwamba akenda ulaya, harudi kwenya samadi,
Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo.

Aliranda akitaya, kwa mbwembwe na zake tadi,
Nguo moto kazitiya, nyumbaye akainadi,
Kasema vyote ‘ishiya; kurudi sina ahadi
Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo.

Matusi aliyamwaya, mengi yasiyo idadi,
Mkewe kamwita yaya, na kudharau abidi,
Kanena ‘mekata waya’, ng’ambo nenda kufaidi,
Mchama ago hayeli, huenda akauya papo,

Ng’ambo alielekeya, kwa vishindo kama radi,
Kumbe aliyemwendeya, kabambwa kwa ufisadi,
Vya watu amebugiya, rushwa na kuhepa kodi,
Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo.

Kombo yakamwendeya, mambo mno yakazidi,
Akabakia kuliya, nyumbani ataka rudi,
Nyumba ipi ‘taingiya’, hana tena tabaradi,
Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo

Maswali

  1. Kwa kutolea ushahidi ufaao shairini, jadili kifupi maswala matatu makuu ambayo mtunzi ameyashughulikia.       (alama 6)
  2. “Mtunzi huyu ni bingwa wa kutumia lugha kupitisha ujumbe.” Tetea.        (alama 4)
  3. Fasiri ujumbe wa mtunzi katika ubeti wa sita.                                                    (alama 4)
  4. Nafsi nenewa katika shairi hili ni nani? Thibitisha.                                            (alama 2)
  5. Zaidi ya tarbia, ungelipangaje tena shairi hili?                                                    (alama 2)
  6. Fafanua msamiati ufwatao kama ulivyotumika shairini:                                   (alama 2)
    1. Baidi
    2. ‘mekata waya’

Majibu

  1. Kwa kutolea ushahidi ufaao shairini, jadili kifupi maswala matatu makuu ambayo mtunzi ameyashughulikia.           (alama 6)
    • Mabadiliko- Bwana aliyealikwa ng’ambo anafikiri maisha yake yameongoka lakini afikapo huko mambo yanamwendea kombo. Inamlazimu kurudi nyumbani alikotoka kwa kiburi akisema kuwa asingerejea.
    • Majuto- Bwana aliyehamia ng’ambo kwa kiburi kikuu anaishia kunyenyekea mambo yanapomharibikia kule.
    • Ufisadi- Mwenyeji wa Bwana anayealikwa ng’ambo anashikwa kwa kushiriki ufisadi.
    • Tamaa na ubinafsi- Bwana anayetoa ualishi wa mwenzake kumzuru ng’ambo anashitakiwa kwa ufisadi na kukwepa kodi hali zinazodhihirisha tamaa.
      Hoja 3 za mwanzo X 2= alama 6
      Tanbihi: Swali hili linatahini maudhui; tathmini majibu mengine ya mtahiniwa
  2. “Mtunzi huyu ni bingwa wa kutumia lugha kupitisha ujumbe.” Tetea.                      (alama4)
    Tanbihi: Swali linatathmini mtindo/mbinu za lugha.
    • Methali- Mchama ago hanyeli, huenda akauya hapo.
    • Takriri- Kibwagizo “mchama ago hanyeli, huenda akauya papo” ni mfano wa uradidi.
    • Kinaya- Bwana anayeenda ng’ambo kwa kiburi analaimika kunyenyekea afikapo huko na kumpata mfadhili wake ameshikwa kwa ufisadi/ alitarajia maisha mema huko na kuishi huko milele lakini hali zinamharibikia.
    • Istiari/jazanda- Samadi katika ubeti wa nne ni kiashiria cha umaskini/kutoendelea.
    • Tashbihi- Ng’ambo alielekeya, kwa vishindo kama radi.
    • Taswira-Tashbiha katika (v) hapo juu inajenga picha ya jinsi Bwana huyu anaondoka kwao kwa vurugu. Pia jazanda ya samadi inatujengea taswira ya umaskini.
    • Nahau- Kombo yakamwendeya.
    • Balagha-nyumba ipi taingiya…
    • Msemo- mekata waya-amekata uhusiano
      Hoja zozote 4X1= alama 4
  3. Fasiri ujumbe wa mtunzi katika ubeti wa sita.                                                         (alama 4)
    • Alitumia lugha chafu sana
    • Akamdunisha mkewe pamoja na wengine wengi.
    • Akasema kuwa amekata uhusiano na kuwa angeenda kufanikiwa kule ng’ambo.
    • Ahamaye hachafui atokapo kwa kuwa huenda akarudi hapo.
      Hoja 4X1= alama 4
  4. Nafsi nenewa katika shairi hili ni nani? Thibitisha.                                              (alama 2)
    • Yeyote anayefanikiwa kuhama alipopazoea.
    • Mtunzi anatahadharisha dhidi ya kutoka alipokuwa akiishi mja kwa dharau/kiburi kwa vile kuna uwezekano wake kurudi hapo.
      Hoja 4X1= alama 4
  5. Zaidi ya tarbia, ungelipangaje tena shairi hili?                                                     (alama 2)
    • Mathnawi-lina vipande viwili katika kila mshororo.
    • Mtiririko-vina vyote vya ndani vinafanana tangu mwanzo hadi mwishi; vya nje vilevile.   Hoja 2X1= alama 2
  6. Fafanua msamiati ufwatao kama ulivyotumika shairini:                                    (alama 2)
    1. Baidi -tofauti
    2. ‘mekata waya’- amekatiza uhusiano

Ushairi 53

MBELE YA SAFARI

  1. Ilipoanza safari , ilianza kwa dhiki
    Tulishikana kwa ari, kwenda safari ya haki
    Tukawa ni majabari, nyoyo zisitaharuki
    Tukajizatiti
  2. Njaa ikawa dhabiti ,na kiu kutamalaki
    Nasi tulitia dhati tusijali kuhiliki
    Ingawa mbele mauti ,dhila na mingi mikiki
    Tukajizatiti
  3. Huu mwisho wa safari, tukaambiwa ni haki
    Shangwe kwetu na fahari,utumwa hatuutaki
    Kuwa mbele ya safari , juhudi iliyobaki
    Tukajizatiti
  4. Ile ilikuwa ndoto , mwisho wake mafataki
    Nguvu zimechomwa moto,sahala ‘mekuwa dhiki
    Wagombanio kipato,utashi haukatiki
    Nakutabakari
  5. Msafara ukasita , kwenye mlima wa haki
    Kijasho kinatuita , mlima haupandiki
    Basi sote ‘kijipeta, kukikwea kima hiki
    Twataka hazina
  6. Tukiwa migongo wazi ,tukainama kwa shaki
    Tukawa’chia ukwezi , kialeni wadiriki
    Wakapanda bila kazi ,Kuteremsha miliki
    Wakaitapia
  7. Wakafikia makazi,ya pumbao na ashiki
    Huko wakajibirizi, kwenye raha lakilaki
    Wakaisahau ngazi, ya umma ulomiliki
    Mbele ya safari
  8. Na hazina yetu sote, kuishusha hawataki
    Wamo wanatema , kwa umati halaiki
    Imezima nia yote ,kiza hakitakasiki
    Mbele ya safari
    1. Eleza safari inayolejelewa katika shairi hili. (al 2)
    2. Onyesha kinaya cha safari inayozungumziwa. (al 6)
    3. Taja na ueleze bahari mbili za shairi ukizingatia : (al 4)
      1. Mizani ;
      2. Vina
    4. Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari. (al 4)
    5. Eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi zilizotumiwa katika ubeti wa sita. (al 4)
    6. Eleza umbo/ muundo wa shairi hili. (ala 2)

Majibu

  1.  
    • Kupigania uhuru /haki /kujiendeleza kiuchumi
    • Washiriki /walisimama /walitaka milki pamoja.    (2 x1)
  2. Kinaya
    • Viongozi kujinufaisha -raia maskini.
    • Viongozi kudharau raia -kuwatemea mate.
    • Raia kupigania uhuru -kutofaidika
    • Kutoafikia maazimio -milki ya haki
    • Walianza safari pamoja -mwishowe wanabaguliwa.   (4 x 1=4)
  3.  
    1. Mizani -msuko -mshororo wa mwisho wa kila ubeti umefupishwa.
    2. Vina-ukara -vina vya kati vinabadilika vya tamati vinatirirka. (2x2=4)
      (Kutaja 1 na kueleza 1)
  4. Mshairi analalamika kuwa viongozi walipofikia hali nzuri ya Maisha tamaa ilizidi huku wakiwa na starehe za kila aina huku akiwasahau waliowapa nafasi za uongozi ili kufikia hali yao ya sasa. (4x1=4)
  5.  
    • Inkisari-Tukawa’chia -Tukawachia-kutosheleza mizani.
    • Kuboronga sarufi -kialeni wadiriki -wadiriki kialeni -urari wa vina.
    • Tabdila -shaki-shaka-urari wa vina
    • Lahaja /kikale -kialeni-kialeni-upekee wa msamiati /mapigo ya kimziki.    (za kwanza 2x2)
  6.  
    • Lina beti nane.
    • Mishororo minne kwa kila ubeti.
    • Mshororo wa mwisho umefupishwa katika kila ubeti.
    • Msishororo wa kwanza hadi wa tatu katika kila ubeti vina vipande viwili.
    • Kila mshororo una mizani kumi na sita na wa mwisho una mizani sita katika kila ubeti .
    • Vina vya ndani havifanani ilihali vile vya nje vinafanana.( 4 x ½ = 2)

Ushairi 54

Shimo: Ali Salim Zakwany

  1. Mwambieni kibushuti, asiruke shimo lile
    Kimo chake kama goti, kwenda ng'ambu sifikile
    Mtu haoli bahati, akasahau umbile
    Kila muwania mbele, na nyuma 'sisahawile
  2. Afanyayo ni hatari, sijitie mpulele
    Mambo yote ajasiri, shari asithibutile
    Mjalia watu kheri, shairi ni yake vivile
    Kila muwania mbele, na nyuma 'sisahawile
  3. Asambe ndiyo busara, kutenda kitendo kile
    Itamuwia hasara, na madhara kama yale
    Mola mwingi wa subira, ajapo chomwa vidole
    Kila muwania mbele, na nyuma 'sisahawile
  4. Licha na yeye nyadungo, chuya katika mchele
    Hata warefu ja pondo, hawatusi shimo lile
    Walojaribu kitendo, shimoni watumbukile
    Kila muwania mbele, na nyuma sisahawile
  5. Nimefika kituoni, nasema mumuwasile
    Mfua maji ngamani, ili kwamba sizamile
    Chombo huungia mwambani, na nahodha ni yuyule
    Kila muwania mbele, na nyuma 'sisahawile

Maswali

  1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 1)
  2. Fafanua toni ya shairi hili. (alama 4)
  3. Taja na utoe mifano ya tamathali za usemi mbili zinazopatikana katika shairi. (alama 4)
  4. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
  5. Kwa kutoa mifano minne, eleza aina moja ya idhini ya kishairi iliyotumika zaidi katika shairi. (alama 3)
  6. Andika ubeti wa tano kwa lugha ya nathari. (alama 4) 

Majibu

  1.                      
    1. Nyuma sisahau vile.
    2. Muwanie mbele.
    3. Jiepusheni na balaa (alama 1)
  2. Toni ya
    1. Masikitiko - msimulizi anasikitika na tabia za mtu Pulani.
    2. Tahadhari - Mjalia watu kheri, shari ni yake pia
    3. Dharau - Licha ya yeye nyadundo. Cheya katika mchele. Hata...
    4. Ombi - nasema mumuwasile. (alama 4)
  3.            
    • Jazanda:
      1. Chombo huingia mwambani na nahodha ni yuyule
      2. Mfua maji ngamani
    • Tashbihi:
      1. kimo chake kama goti
      2. warefu ja pondo
      3. madhara kama yale (kutaja 1, mfano 1, 2x 2 = 4)
  4. Ni shairi la beti 5.
    • Kila ubeti una mishororo 4
    • Kila mshororo una vipande viwili, ulewapi na utao.
    • Vina vya ndani vimebadilika ila vya nje vimefanana
    • Shairi lina mkarara/kibwagizo. (zozote 4 x 1 = 4)
  5. mazida
    • sisahawile badala ya sisahau
    • asithubutile badala ya asithubutu
    • sifikilie - sifike
    • yuyule – yuyu (kutaja 1, mifano 4 x ½ = 2, jumla 3)
  6. Nimefika mwisho nasema mmpe wasia. Anayetoa maji chomboni akiwa katikati ya chombo hicho ni kwa sababu asizame. Na ikumbukwe kwamba huenda mrama na akawa nahodha wa kila siku. Kila anayewania yaliyoko mbele asisahau aliyowacha nyuma.
    (alama 4)

Ushairi 55

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo;

Sinisumbue akili, nakusihie mwandani,
Afiya yangu ni dhalili, muno nataka amani,
Nawe umenikabili, nenende sipitalini,
Sisi tokea azali, twenda zetu mizimuni,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani!

Mababu hawakujali, wajihisipo tabani,
Tuna dawa za asili, hupati sipitalini,
Kwa nguvu ya kirijali, mkuyati uamini,
Kaafuri pia kali, na dawa ya ndwele fulani,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani!

Mtu akiwa halali, tumbo lina walakini,
Dawa yake ni shubili, au zogo huauni,
Zabadi pia zahali, kwa maradhi yako ndani,
Au kwenda wasahili, wenyewe walo pangani,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani!

Mtu kwenda sipitali, ni kutojuwa yakini,
Daktari kuona mwili, tanena kansa tumboni,
Visu vitiwe makali, tayari kwa pirisheni,
Ukatwe kama figili, tumbo nyangwe na maini,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani!

Japo maradhi dhalili, kuteguliwa tegoni,
Yakifika sipitali, huwa hayana Kifani,
Waambiwa damu kalili, ndugu msaidieni,
Watu wakitamali, kumbe ndio buriani,
Nifuateni sipitali, na dawa ziko nyumbani!

Mizimu yakupa kweli, wakueleze undani,
Maradhiyo ni ajali, yataka vitu dhamani,
Ulete kuku wawili, wa manjano wa kijani,
Matunda pia asali, vitu vya chanoni,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani!

Maswali

  1. Lipe shairi hili anwani mwafaka. (alama 2)
  2. Liweke shairi hili katika bahari mbili. (alama 2)
  3. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 4)
  4. Kwa nini mshairi anakataa kwenda hospitali? (alama 2)
  5. Ni nani nafsi neni katika shairi hili? (alama 1)
  6. Tambua toni ya shairi hili. (alama 1)
  7. Eleza muundo wa ubeti wa pili. (alama 4)
  8. Eleza jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumika katika shairi hili. (alama 2)
  9. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi. (alama 2)
    1. Pangani
    2. Nenende

Majibu

  1. Lipe shairi hili anwani mwafaka.
    • Sipitali sendi, Nifwateni sipitali, Dawa ziko nyumbani . 1x2=2
  2. Liweke shairi hili katika bahari mbili.
    • Mtiririko – vina vya ukwapi na utao vinafanania.
    • Mathaawi – shairi lina vipande viwili. 1x2=2
  3. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari.
    • Mtu akienda hospitali ni kutojua vizuri. Kuwa daktari akiona mwili, atasema ni sratani ya tumbo. Atatia visu makali kujitayarisha kufanya upasuaji/paresheni, atakukata vyungo vya ndani. Kwa nini kwenda nyumbani na dawa ziko nyumbani. 4x1=4
  4. Kwa nini mshairi anakataa kwenda hospitali?
    • Tangu zamani wao huenda mizimuni.
    • Dawa za kiasili zipo.
    • Hapendi upasuaji.
    • Anafuata kielelezo cha mababu zetu. Zozote 3x1=3
  5. Ni nani nafsi neni katika shairi hili?
    • Mgonjwa/anayeugua 1x1=1
  6. Tambua toni ya shairi hili.
    • Huzuni/masikitiko/malalamiko 1x1=1
  7. Eleza muundo wa ubeti wa pili.
    • Mishororo minne.
    • Vipande viwili kila mshororo.
    • Mizani 16 kila mshororo.
    • Vina vya ndani ni –li na vya nje ni –ni. 4x1=4
  8. Eleza jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumika katika shairi hili.
  9. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi. (alama 2)
    1. Pangani – palipona mizimu/mizimuni.
    2. Nenende – niende.

Ushairi 56

Soma shairi hili kisha ujibu maswali.
Mwanadamu mambo yake, kueleweka muhali
Ubavuni umuweke, umtowe kule mbali
Maskanini afike, umtindie fahali
Utamu anufaike, sima, bada au wali
Hatimaye ateuke, kwa viliwa vya samli
Mwanadamu simuamini, afadhali nyama lumbwi.

Mwanadamu umjenge, awe mwenye kutajika
Mambo yake uyapange, ukawa wahangaika
Uwashe wake muwenge, uhakikishe wawaka
Nao mkono umuunge, vyake viwe vyaungika
Dhorubani umkinge, asipate kudhurika
Mara atakusahau, wema wako kafukia.

Mwanadamu mpe cheo, kuwa akutumikie
Amani yako umpeo, fanaka uirajue
Kwake iwe kimbilio, wamini akukwamue
Mwisho takuwa kilio, shika sikio ujue
Ndio wake mwelekeo, yuauma avuvie
Mwanadamu mgeuze, pande zote umtizame.

Mwanadamu mfadhili, kwa kila lililo jema
Pasiwe hata dalili, ya kwake kukosa wema
Viteko siwe akali, kumbizo zikaterema
Binadamu takudhili, dhili zako kuzitema
Licha ya zote jamili, mwanadmu si muema
Mwanadamu ni mtu, lakini nusu mnyama

  1. Onyesha kinaya cha mwanadamu anayezungumziwa. (alama 4)
  2. Fafanua toni ya shairi hili. (alama 2)
  3. Taja na ueleze bahari nne za shairi hili. (alama 4) 
  4. Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2)
  5. Onyesha mbinu nne alizotumia malenga ili kutosheleza mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili. (alama 4)
  6. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha nathari. (alama 4)

Majibu

  1. Onyesha kinaya cha mwanadamu anayezungumziwa. (alama 4)
    • Mwanadamu analinganishwa na lumbwi kumaanisha kuwa anaweza kukugeuka baada ya kumsaidia.
    • Binadamu baada ya kuyapanga mambo yake umjenge hadi awe wa kutajika anakuja kukusahau na kufukia wema wako.
    • Mwanadamu hata ukampigania hadi akapata cheo kwa nia kuwa akusidie baadaye anakuja kukusababishia kilio.
    • Binadamu anakuja kusema dhili zako hata baada ya kumfadhili kwa kila jambo jema hadi akajaa vicheko.
  2. Fafanua toni ya shairi hili. (alama 2)
    • Toni ya huzuni - Mwisho takuwa kilio, shika sikio ujue.
    • Toni ya majuto – Mwanadamu simuamini, afadhali nyama lumbwi
    • Toni ya kukashifu - Mwanadamu ni mtu, lakini nusu mnyama
      (1 x 2= 2, kujata =1, maelezo/mfano = 1)
  3. Taja na ueleze bahari nne za shairi hili. (alama 4) 
    • Tasdisa/usita – kila ubeti una mishororo sita.
    • Kikwamba – neno mwanadamu lirudirudiwa mwanazoni mwa kila ubeti
    • Mathnawi – vipande viwili kila mshororo
    • Ukaraguni – vina vinabadilikabadilika.
    • Sabilia – shairi lina kiishio.
  4. Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2) 
    • Mshauri nasaha / kiathirika cha usaliti au kigeugeu – anashauri kuhusu tabia za binadamu. (1 x 2= 2) d
  5. Onyesha mbinu nne alizotumia malenga ili kutosheleza mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili. (alama 4)
    • Inkisari - takuwa – utakuwa.
      Dhima - kupata urari wa mizani
    • Kuboronga sarufi
      • Mambo yake uyapange – uyapange mambo yake
      • Uwashe wake muwenge – uwashe mwenge wake
      • Nao mkono umuunge – nao umuunge mkono
      • wema wako kafukia – kafukia wema wako
      • Ndio wake mwelekeo – ndio mwelekeo wake
      • pande zote umtizame – umtizame pande zote.
        Dhima - kupata urari wa vina.
    • Tabdila - umtowe - umtoe
      • umtizame – umtazame.
        Dhima - kuleta mahadhi katika shairi / lugha ya kishairi.
    • Mazida
      • umuweke – umweke.
      • Muwenge – mwenge
      • Muema - mwema
        Dhima - kupata urari wa mizani
    • Lahaja
      • umtindie – umchinjie
      • viteko – vicheko.
        Dhima – kuleta upekee wa lugha ya kishairi.
    • Vikale
      • maskanini . makazi
      • akali – kidogo.
        Dhima – kuleta upekee wa lugha ya kishairi. 

        Kutaja na mfano- ½, dhima -½ (za kwanza 4 x 1 = al 4)
  6. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha nathari. (alama 5)
    Mshairi anasema kuwa binadamu licha ya fadhili zote unazoweza kumpa hadi akawa anafurikwa na furaha bado atakusaliti na kusema mabaya kukuhusu. Anamlinganisha binadamu na mnyama.

Ushairi 57

UTU NI NINI?
Utu na ubinadamu, ni kama yai na kuku
Utu ni ile nidhamu, mola aliyokhuluku,
Ubinadamu ni damu, ya utu wa kila siku,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake.

Ye yote mwanaadamu, ana asili ya utu,
Ya’ni kwenye yake damu, hakikosi hiki kitu,
Utu sifa maalumu, ya mtu kuitwa mtu,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake

Utu ni kiumbe hai, tunacho chaonekana
Utu kamwe haudai, tabia ya kujivuna,
Utu ni ule uhai, ushikao uungwana,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake

Utu huweza pimika, kwa hisia ya akili,
Huweza kuhifadhika, kulingana na fadhili,
Utu huweza pendeka, palipo na maadili
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake

Utu unayo aibu, na tabia ya muhali,
Utu huenda na jibu, la Imani na ukweli,
Utu huiona tabu, tabia ya ujahili,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake 

Filosofia ya utu, inapinga ubinafsi,
Utu hautaki kitu, cha upeke wa nafsi,
Utu hauna kiatu, cheupe au cheusi,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake.

Utu wa kweli kwa mja, ni wenzake kuwajali,
Utu huiona haja, ya kujua watu hali,
Utu ni kuwa pamoja, kwenye shida mbalimbali,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake.

Utu ni ubinaadamu, udugu na wenzi wako,
Utu wote waheshimu, kwa nidhamu na kicheko,
Utu ona mwanadamu, sijitenge peke yako,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake

Ingawaje tu dhaifu, katika ubinafsi,
Utu kweli nausifu, ubinadamu halisi,
Utu ni sifa tukufu, iletayo kila nemsi,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake

  1. Tambua aina ya shairi hii kwa kutolea ithibati. (alama 2)
  2. Taja sifa tano za mtu mwenye utu kulingana na shairi. ( alama 5)
  3. Tambua mbinu mbili za kimtindo zilizotumiwa na mshairi. (alama 2)
  4. Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo. (alama 3)
    1. vipande
    2. vina
    3. mpangilio wa maneno
  5. Tambua nafsineni katika shairi. (alama 1)
  6. Tambua mbinu tatu alizotumia mshairi ili kukidhi mahitaji ya kiarudhi. (alama 3)
  7. Andika ubeti wa saba kwa lugha nathari. (alama 4)

Majibu

  1. Tambua aina ya shairi hii kwa kutolea idhibati. (alama 2)
    Tarbia – mishororo minne katika kila ubeti
    Kutaja -1
    Kueleza-1
  2. Kwa hoja nne fafanua ujumbe wa mshairi. Taja sifa tano za mtu mwenye utu kulingana na shairi.(alama 5)
    • Mtu mwenye nidhamu
    • Mtu mwenye utu hana tabia ya kujivuna
    • Mtu mwenye utu husema ukweli.
    • Mtu mwenye utu hana ubinafsi
    • Mtu mwenye utu huwajulia wengine hali.
    • Mtu mwenye hushirikiana na wengine.
    • Mtu mwenye utu huwaheshimu wenzake.
    • Mtu mwenye utu huwajali wenzake
    • Mtu mwenye utu hupendeka
    • Mtu mwenye utu ni muungwana. (za kwanza 5x1 = 5)
  3. Tambua mbinu mbili za kimtindo zilizotumiwa na mshairi. (alama 2)
    • Tashbihi – ni kama yai na kuku
    • Takriri/urudiaji – mtu kuitwa mtu.
    • Uhuishi/tashihisi – utu kamwe haudai, utu huiona tabu.
    • Utohozi – filosofia – philosophy
      (za kwanza 2 x 1 = 2)
  4. Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo. (alama 3)
    • Vipande – mathinawi – migao miwili
    • Vina –ukaraguni – vina vinabadilika katika kila ubeti.
    • Mpangilio wa maneno – kikwamba – neno utu kuanzia katia baadhi mishororo (3x1=3)( akitaja bahari tu atuzwe)
  5. Tambua nafsi neni katika shairi. (alama 1)
    Mshauri – anashauri watu kuwa na utu.
    • Tambua mbinu tatu alizotumia mshairi ili kukidhi mahitaji ya kishairi.(alama 3)
  6. Tambua mbinu tatu alizotumia mshairi ili kukidhi mahitaji ya kiarudhi.
    • Inkisari – yani – yaani, tabu - taabu
    • Kuboronga sarufi – kwenye yake damu – kwenye damu yake, hiki kitu – kitu hiki
    • Msamiati wa kale – mja - mtu
    • Mazda – ubinaadamu – ubinadamu
    • utohozi – filosofia (zozote 3 x1 = 3)
  7. Andika ubeti wa saba kwa lugha nathari. (alama 4)
    • Utu wa kweli wa mtu ni kuwajali wenzake /na kuona haja ya kuwajulia watu hali/. Utu ni kushirikiana na wengine kwenye shida mbalimbali/. Utu wowote wa mtu ni kuwajali wenzake.
      ( asitumie koma, na aondoe uhuru wa mshauri wote, asitumie muundo wa beti) ( 4x 1) 

Ushairi 58

Soma shairi lifuatalo kwa makini, halafu ujibu maswali yanayofuatia

Hakika yamekithiri, ni asoyajua?
Wazazi wayahubiri, na hivyo kutubagua
Hayana kamwe fahari, ila kweli yatua.
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Mwanamke siyo huyo? Baba mtu anasema
Mwanamke kwani huyo? Anateta naye mama,
Sababu waitoayo, haina nguvu wima,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Kabila letu ni hili, sharuti uoe huko,
Unazomewa ukali, kuoa nje ni mwiko.
Hivyo twafanywa dhalili, viumbe tuso mashiko
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Wanachunguza tabaka, ndipo wazushe wahaka
Wauliza kwa haraka, wajue lake tabaka,
Wasioridhika wafika, arudi alikotoka,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Waichuja yake dini, ndo ndoa ibarikiwe
Lazima yake imani, iwe sawa na yakuwe
Huu kweli ni uhuru, wataka uondolewe,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Japo mwanipa elimu, uhuru ninautaka,
Na mie muniheshimu, nipate nilomtaka
Kuoa kitu adhimu, so mchezo kwa hakika
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Nawashauri wazazi, twahitaji kupumua,
Wawili ndo waamuzi, haa Mungu anajua,
Wasifu pasi ajizi, kwa yao njema hatua,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Ndoa akivunjikana, wawili wajisakeni
Isije kusemekana, wazazi ndio kiini,
Ndiposa hata Rabana, situtie lawamani,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Aliye na masikio, mesikia kwa makini,
Tusitamani kilio, mtihani tulo vitani,
Wakioa sema ndio, Mola asikulaani
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Maswali

  1. Lipe shairi hili anwani mwafaka. (al.1)
  2. Shairi hili laweza kuwekwa katika bahari mbili. Zitaje huku ukitoa mifano. (al.2)
  3. Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili. (al.2)
  4. Eleza ujumbe unaojitokeza katika shairi hili. (al.4)
  5. Jadili muundo wa shairi hili. (al.4)
  6. Taja aina mbili za urudiaji katika shairi. (al.2)
  7. Ukizingatia shairi ulilopewa, eleza jinsi mshairi alivyotumia uhuru wake. (al.2)
  8. Taja toni ya shairi hili. (al.1)
  9. Eleza maaana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika kwa shairi.
    1. Wahaka
    2. Yamekithiri (al.2)

Majibu 

start pre-m 2023

last - 4494

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Ushairi Questions with Answers.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Read 12997 times Last modified on Tuesday, 05 September 2023 11:52
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest