Maswali na Majibu ya Insha katika Tamthilia ya Kigogo

Share via Whatsapp

Kigogo Insha Questions and Answers

Maswali ya Insha

Haya ni maswali ambayo hutoa kauli inayohitaji kujibiwa kwa kirefu na kwa kina. Swali linaweza kuwa la jumla yaani linalohusu Tamthilia nzima. Pia, swali laweza kulenga sehemu ya kazi husika katika nyanja na maudhui, wahusika na hulka zao, mafunzo na fani. Maswali haya huhitaji zaidi uwezo wa kukumbuka wa mtu, kupanga hoja na kuelezea msimamo au maoni yake kuhusiana nayo. Mtahiniwa anahitajika kutoa hoja na kuziteteta kwa mifano dhabiti. Mtahiniwa asitumie vistari vistari, afafanue hoja kikamilifu akiandamisha mifano mingi kutoka kwa Tamthilia.

Swali la Insha 1

Jadili mbinu wanazotumia wanasagamoyo kujikomboa kutoka utawala dhalimu wa Majoka (Alama 20)

  • Migomo-walimu na wauguzi wanapana mgomo kulalamikia mshahara duni
  • Maandamano-wafanyikazi wa Majoka and Majoka company wanaandamana kulalamikia bei ya chakula kupandishwa katika vioski
  • Wanaharakati-Tunu na sudi kuwashawishi wanasagamoyo kuutambua na kuupinga uovu unaoendelezwa na Majoka. Wanaenda mangweni kuwazindua wanasagamoyo
  • Makabiliano ya ana kwa ana-Tunu na sudi wanaenda Ofisi ya Majoka na kumkosao dhidhi ya kufunga soko la chapakazi
  • sheria-Tunu anatumia uanasheria aliousomea kule ngambo kuwatetea wanasagamoyo…anaendeleza uchunguzi dhidhi ya mauaji ya jabali
  • Mikutano-Tunu na Sudi wanapanga mkutano mkubwa katika Lango kuu la sokoni kumshinikiza Majoka kulifungu soko
  • Kususia mikutano ya Majoka-wanasagamoyo wanadinda kuhudhuria mkutano wa sikukuu ya uhuru na badala yake kwenda Mkutano wa Tunu na Sudi lagoni mwa Soko la Chapakazi
  • Kukataa vishawishi-Sudi anakataa vishawishi ya Majoka ya kupewa Likizo ughaibuni na malipo kambambe iwapo angekubali kuchonga kinyago cha Nao bi Marara/sudi kukataa kijikekei cha uhuru
  • Upinzani/kujitosa katika siasa-Jabali anaanzisha chama cha Mwenge ili kukabili majoka kisiasa. (Hoja Zozote 10 X 2)

Swali la Insha 2

  1.  
    1. Fafanua mbinu kumi anazotumia Majoka katika kuuendeleza uongozi wake(alama 10)
    2. Eleza namna mbinu ya ishara ilivyotumiwa katika tamthilia ya Kigogo (alama 10)

Fafanua mbinu kumi anazotumia Majoka katika kuuendeleza uongozi wake(alama 10)

  • Uvumi kwa mfano – Sudi na Ashua wanaiwinda roho ya Tunu
  • Ahadi za uwongo – kutoa chakula kwa wasiojiweza
  • Zawadi - keki za uhuru
  • Vitisho - Akiwa chopi watamwaga unga
  • Mapendeleo - Tunu na Ashua walipewa kazi wakakataa. Ashua angekuwa mwalimu mkuu katika shule mojawapo za Majoka kama angekubali.
  • Sela   - Wanaompinga wanafungwa jela k.v. Sudi anasema amefungwa mara nyingi katika jela alikofungwa Ashua.
  • polisi - polisi wanatawanya waandamanaji
  • Mabavu   - Madai ya kuwafukuza wafadhili wa wapinzani ili wavunje kambi zao Sagamoyo, Nguvu zaidi kutawanya waandamanji
  • Kudhibiti vyombo vya dola - Majoka kutaka kufunga vituo vyote kibaki Sauti ya Mashujaa
  • Ulaghai   - mf. Kuongeza mishahara ya walimu na wauguzi kisha kupandisha kodi.
  • mavamizi - mf. Tunu kuvamiwa na kuvunjwa muundi
  • Ulinzi - Majoka ana walinzi wengi.    (10 x 1 = 10)

Eleza namna mbinu ya ishara ilivyotumiwa katika tamthilia ya Kigogo (alama 10)

  • Kinyago cha kike kinachochongwa na Sudi na kukiita shujaa halisi wa Sagamoyo kinaashiria shujaa wa kike atakayelikomboa Jimbo la Sagamoyo dhidi ya uongozi dhalimu
  • Fimbo ya Kenga yenye kichwa cha Nyoka ni ishara ya jinsi alivyokuwa katili kwa raia. Kwa mfano, anamuua Jabali
  • Uchafu wa soko ya chapakazi ambao unamsababisha hata Mzee Kenga kuziba pua yake anapoenda huko ni ishara ya maovu yaliyokithiri jimboni Sagamoyo.
  • Kitendo cha Majoka kuzungumza na babu yake anapozirai ni ishara kuwa wafu walikuwa wakimwita madhali naye aliokuwa amewaua
  • Majoka kuvaa mkufu shingoni wenye kidani cha umbo la swila ni ishara ya namna Majoka alivyokuwa hatari kwa maisha ya raia wa jimbo la Sagamoyo.
  • Kujaa kwa maziara jimboni Sagamoyo hadi hakuna nafasi ya kuwazika wafu wengine ni ishara ya mauaji yaliyokuwa yametekelezwa na Majoka.
  • Kilio na machozi mengi ndani ya ziwa lililofunika damu ni ishara ya raia waliouliwa na Majoka wanalilia haki yao.
  • Kutojaa kwa raia jinsi ilivyo kawaida katika mkutano wa kuadhinisha sherehe za uhuru pamoja na siku ya kuzaliwa kwa Majoka ni ishara ya raia kuasi Majoka kutokana na uongozi wake dhalimu.
  • Hali ya Majoka kujiona ndani ya ziwa lililofurika damu ni ishara ya mauaji mengi ya raia aliyokuwa akitekeleza katika uongozi wake.
  • Damu ya Jabali anayoiona Majoka ikitiririka mikononi mwake akiwa amezirai ni ishara kuwa yeye ndiye aliyemuua Jabali

Swali la Insha 3

Kwa kurejelea tamthlia ya 'Kigogo ya Pauline Kea, onyesha jinsi ambavyo viongozi wengi katika nchi za kiafrika wamejawa na tamaa.  (alama 20)

  • Tamaa ya kupata sanamu/ Majoka anataka Sudi amtengenezee sanA
  • Tamaa ya kupata kodi. Majoka anawatoza kodi wafanyibiashara wa soko la Chapakazi kwa manufaa yao.
  • Tamaa ya shule zao kufunzwa na walimu waliofuzu vyuoni. Majoka anamrai Ashua afunze katika shule zake.
  • Tamaa ya kuungwa. Majoka anapata uungwaji mkono kupitia watu kama Ngurumo, Asiya na Boza -
  • Anawapa hongo ili wamuunge mkono.
  • Tamaa ya kupewa sifa lufufu. Kwa mfano Majoka lazima atangazwe katika vyombo vya habari.
  • Tamaa ya kutafutia wanao wachumba. Majoka anamtaka Tunu aolewe na mwanawe Ngao Jur.
  • Tamaa ya mapenzi - Majoka ana tamaa ya kupendwa na Ashua.
  • Tamaa ya kujenga nyumba za kifahari. Majoka anatamani kujenga hoteli ya kifahari katika soko la Chapakazi.
  • Tamaa ya usalama - Majoka ana walinzi wengi.
  • Starehe na anasa. Majoka ana tamaa ya burudani. Anaenda kuogelea katika hoteli ya‘ Majoka and Majoka resort’
  • Tamaa ya viongozi kurithisha jamaa zao uongozi.

Swali la Insha 4

Tamthilia ya kigogo inazungumza kuhusu hali halisi katika mataifa mengi ya kiafrika. Jadili. 20

  • Uongozi mbaya unaoendelezwa na majoka
  • Unyakuzi wa ardhi majoka kipande cha ardhi palipokuwa soko la chapa kazi na kujenga hoteli ya kifahari majoka and majoka Resort.
  • Mauaji – vijana waoandama wanauawa. Mpinzani k.m Jabali
  • Vitisho wanasagamoyo wanaishi kwa hofu. Tunu kuvunjwa mguu.
  • Matumizi ya vyombo vya dola. Askari wanatawanya waandamanaji pasi kupata haki zao.
  • Maandamano na migomo wafanyikazi wanagoma kutetea haki zao. Walimu na wauguzi.
  • Uongozi wa kinasaba/ukoo familia ya Ngao inatawala Ngao bin Marara, Majoka bin marara aliyekusudia kumrithisha mwanawe Ngao Junior.
  • Ufisadi wanasagamoyo wanatozwa kodi ya juu
  • Ubadhirifu wa mali ya umma. Pesa za mkopo zinatumika kufadhili mradi wa uchongaji vinyago.
  • Umaskini Ashua anaenda kuomba msaada kwa majoka
  • Ukoloni mamboloea
  • Juhudi za mapinduzi
  • Ubaguzi wa wa kinjisia hasa kwa wanawake – Tunu alikejeliwa kuwa angereuliwa kama kiongozi wa sagamoyo.
  • Matumizi mabaya ya vyombo vya habari. 10x2 = 20

Swali la Insha 5

“Wananchi katika mataifa ya Afrika wanakumbwa na tatizo la uongozi mbaya.” Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa mujibu wa Tamthilia. (alama 20)

  • Unyakuzi wa mali ya umma – Majoka anaamua kulifunga Soko la Chapakazi ili kujenga hoteli ya kifahari.
  • Ubinafsi – Majoka anavibomoa vibanda vya Wanasagamoyo na kupanga kujenga hoteli yake ya kifahari.
  • Utepetevu/ukosefu wa uwajibikaji – wananchi wanalipa kodi lakini wanakosa huduma kusafishiwa soko na huduma za maji taka.
  • Vitisho – Majoka anatisha kumfuta Kingi kazi
  • Viongozi wamekosa maadili ya kikazi – Majoka anamrai Ashua mkewe Sudi ili aendeleze ufuska naye.
  • Kuwatesa wapinzani – Tunu na Sudi wanateswa lakini wanaendelea kupigania mageuzi
  • Kuvunja sheria – Majoka anampa Mamapima kibali cha kuuza pombe haramu ambayo ni kinyume na katiba
  • Wizi wa kura –Majoka anasema kuwa hata wasipompa kura atashinda
  • Ubaguzi katika utoaji wa kandarasi  - kandarasi ya kuoka keki inatolewa kwa Asiya ambaye ni mke wa Boza
  • Matumizi mabaya ya pesa za umma – pesa zinatumiwa katika shughuli za kuchonga vinyago
  • Utawala wa kiimla na wa kutojali – Wanasagamoyo hawana usemi wowote; Majoka anasema kuwa atajenga hoteli watu wapende wasipende
  • Mauaji ya kikatili – watu wasio na hatia wanauawa; Jabali
  • Kuzwazulia watu wasio na hatia  - Ashua anazuiliwa na Majoka bila kosa lolote
  • Wanasagamoyo wanakabiliwa na unyonyaji – bei ya chakula kwenye kioski cha kampuni imepanda maradufu tangu soko lilipofungwa
  • Kuwanyima wanasagamoyo haki ya kaundamana – wanaharamisha maandamano
  • Unasaba – Majoka anamwajiri Kenga ambaye ni binamuye kama mshauri wake mkuu
  • Viongozi wanatumia nafasi zao kuwaangamiza vijana  - matumizi ya dawa za kulevya – wanfunzi katika shule ya Majoka Academy wadungana sumu ya nyoka
  • Utapeli  - Kuwaongezea  walimu mshahara na wauguzi na kuongeza kodi
  • Kurithisha uongozi – Majoka anapanga kutambulisha Ngao Junior kuwa kiongozi mpya mpya badala ya Wanasagamoyo kumchagua kiongozi wao
  • Kuruhusu biashara ya ukataji wa miti - Matumizi mabaya ya vyombo vya dola – polisi wanatumiwa kuwatawanya waandamanaji.

Swali la Insha 6

Vijana katika tamthilia ya kigogo wamesawiriwa kwa jicho hasi. Fafanua. alama 20

Ni walevi. Vijana ndio wanashiriki katika ulevi mwingi. Ngurumo na vijana wenzake hushinda kwa mamapima kunywa pombe haramu yenye madhara mengi mwilini. Wanafurahia kufungwa kwa soko maana wanakunywa pombe mchana wote. Hawana mahali pa kwenda ila mangweni wanafurahia pombe wanayonunuliwa na watu wa kigogo.

Ni wajinga. Ngurumo anafikiri kusherehekea uhuru lazima mtu anywe pombe na ndipo haamini kuwa siti aliwacha pombe. Ujinga wa ngurumo unadhihirika pia kwa kufikiria mashujaa wa uhuru ni wale tu walishikwa na kufungiwa korokoroni.

Vijana ni wapenda anasa. Vijana wanaendelea kunywa pombe licha ya athari zake. Baadhi ya vijana walikuwa wamefika na wengine kupofuka lakini wengine waliendelea kunywa tu ngurumo akiwa na wanafunzi wenzake wanaenda mongweni kwa mamapima kujiburudisha kwa pombe haramu. Boza alikwenda pata fufunu kuwa mkewe hakuwa mwaminifu. Hakutenda lolote hadi alipoambiwa wazazi akataka kumpiga nguruma.

Ni wahalifu. Mtu 1 and mtu II wanatumia dawa za kulevya. Wanajidunga sindano. Ngurumo na kundi lake la vijana walimshambulia tunu kwa kusudi la kumuua. Alinusurika lakini akavunjwa miguu.

Wanatumiwa vibaya Kisiasa. Vijana hutumiwa kuonyesha umaanifu wa mwanasiasa. Wanahongwa kuhudhuria mkutano. Kenga anapoona watu wamekataa kuhudhuria mkutano wa majoka anajuta kuwa wangejua wangekodisha mabasi yanalete vijana na kina mama wajaze uwanja.

Vijana ni wazinzi. Ngurumo anatumia ukereketwa wake kama mfuasi wa majoka kumtafutia kandarasi hii kumshawishi asiye kushiriki uroda naye. Hii ni licha ya kwamba aisye ni mkewe boza.

Vijana ni vikaragosi. Ngurumo na vijana wenzake ni wazalendo bubu. Wanamfuata na kumuunga mkono licha ya dhuluma zake kwa umma wa sogamoyo. Ngurumo anadai kura yake atampa majoka au sivyo ampe paka wake.

Fisadi. Wanakubali kuhongwa kwa pombe haramu na wafuasi wa majoka

Wenye taasubi. Ngurumo anadai hawezi kupigia mwanamke kura.

Vijana ni wasaliti. Ngurumo anasaliti juhudi za vijana wenzake kwa kukubali kutumiwa kuwahangaisha na hata kuwapiga. M.f yeye ni miongoni mwa waliompiga na kumvunja tunu mguu.

Vijana wanadhulumiwa. vijana watano katika kiwanda cha majoka wanauawa kwa kushiriki maandamano ya kupinga kupandishwa kwa bei ya vyakula.

Vijana wanapuuzwa. Japo wamesona wengi hawana ajira majoka na kinga wanadharau shahada ya uzamifu aliyonayo Tunu.

Vijana wanafanywa makabila. Wanafunzi katika shule ya majoka academy wanajidunga sumu ya nyoka ( dawa za kulevya) hivyo kuwa makabeji ambapo hawana matumaini maishani.

Kutaja     = 1,  Kweleza = 1   (hoja 1 x 2= 20)

Swali la Insha 7

Kenga alichangia pakubwa msiba wa Wanasagamoyo. Thibitisha kwa hoja zozote kumi. (Alama 20).

Kutoa ushauri mbaya kwa Majoka km kufunga soko na watu wengi walilitegemea.

Kuzorotesha usalama- alihutubia wahuni pale chini ya mbuyu na aliwatumia kuvuruga usalama. Alikuwa akipanga njama fulani.

Kupiganisha raia/ kufunga raia bure. Anamwambia Majoka aite Husda ofisini ili pakitokea vurugu kati ya Husda na Ashua, asingizie Ashua na kumtia ndani.

Kupendekeza wanaharakati wadhulumiwe- wanaharakati wawekewe vidhibiti mwendo na basi Majoka akawafukuza wafadhili na hivyo kulemaza upiganiaji haki.

Kupendekeza polisi watumie nguvu dhidi ya waandamanaji. Majoka basi akaamuru polisi watumie nguvu zaidi na kukatokea vifo.

Kupendekeza mauaji – ya wapinzani kama vile Jabali. Ya wanaharakati Tunu na Sudi kwa kupinga uongozi mbaya wa Majoka./ ya Chopi kwa sababu Majoka alisema Chopi anajua mengi kuliko inavyostahili.

Anaunga mkono udikteta- Majoka anapotaka kumrithisha Ngao Junior uongozi, Kenga anasema jambo hilo linafaa nah ii inanyima raia nafasi ya kuchaguana.

Kupendekeza runinga ifungwe na iadhibiwe kwa kupeperusha maandamano ya raia jambo amabalo lingeharibia sifa uongozi wa Majoka. Anasema Runinga ya Mzalendo ichukuliwe hatua lakini kituo cha Sauti ya Mashujaa kibakie.

Kutopinga miradi isiyo na faida na hata kuisimamia. Anafanikisha mradi wa kuchonga ambao unafilisi nchi na raia watalazimika kulipa deni kwa miaka mingi.

Kukubali kugawiwa ardhi ya umma. Majoka anamgawia kipande cha ardhi cha soko la Chapakazi alichonyakua.

Kufanikisha ubomoaji wa vibanda sokoni Chapakazi. Alisimamia ubomoaji bila kujali raia waliotegemea soko kwa mapato yao.

Kukubali ajira kwa njia ya mapendeleo- alikuwa binamuye Majoka na basi kuendeleza unasaba badala ya kupatia mtu ambaye angetoa ushauri mwafaka wa kuleta maendeleo.

Kuharamisha maandamano na basi kunyima raia haki ya kupigania haki yao ya kufunguliwa soko. Anamshauri Majoka kuyaharamisha.

10x1 (kadiria hoja yoyote nyingine ambayo ni sahihi)

Swali la Insha 8

Eleza nafasi ya mwanamke katika jamii ya Kigogo. (al.20)

  • Wanawake wamechorwa kama wasomi.mf Tunu, Ashua
  • Watetezi wa haki.m.f Tunu
  • Wenye msimamo dhabiti.m.f Tunu
  • Walezi wema .M.f Bi. Hashima
  • Wenye bidii. M.f Ashua
  • Wafanya biashara haramu.M.f Asiya
  • Ni washerati. M.f Asiya
  • Ni washauri wema .M.f Tunu
  • Ni wapenda anasa.M.f Husda
  • Ni fisadi. m.f Asiya
  • Ni adui wa mwanamke mwenzake.M.f Husda kwa Ashua
  • Wamesawiriwa kama jasiri .m.f TTunu Na Ashua
  • Ni wazindushii.M.f Tunu anawazidua wanasagamoyo.
  • Wamesawiriwa kama wenye tamaa ya mali k.m Ashua Anadai kuchoka kupendwa kimaskini na Husda aliolewa na majoka kwa sababu ya tamaa ya mali.
  • Wanawake wanadhalilishwa, majoka anawadunisha Tunu na Ashua.
  • Wameschorwa kama pambo la kumfurahisha mwanamume.km Husda
  • Wenye matumaini. Tunu
  • Wamesawiriwa kama watu walio na ushirikiano Bi. Hashima, kuwalea watoto wa Ashua.
  • Wamesawiriwa kama wenye utu.m.f Bi. Hashima (zozote 20)

Swali la Insha 9

Kuyaopoa mataifa machanga kutoka kwa kinamasi cha madhulumu kuna gharama yake. Ukirejelea tamthilia ya Kigogo, ipatie nguvu kauli hii. (al. 20)

Kuuawa - Wapinzani wa uongozi Sagamoyo wanauawa katika jitihada za kuisaidia Sagamoyo. Jabali aliuawa kwa kuwa mpizani wa majoka.

Kushambuliwa na vijana. Vijana walitumwa kumvamia Tunu, nia ikiwa kumuua. Aliishia kuumizwa vibaya kiasi cha kufanya atumie kiti cha magurudumu.

Kudhihakiwa. Tunu anadhihakiwa na waliouunga mkono uongozi wa Majoka. Alipokwenda Mangweni, anadhihakiwa kwa kuambiwa kwanza aolewe.

Vifungo. Ashua anafungwa kwa kukataa matakwa ya majoka. Kufungwa kwake kulikuwa na nia ya kumshinikiza Sudi amchonge Majoka kinyago.

Kugotanishwa. Tunu na Sudi wanachochewa kukosana ili waachane na harakati za ukombozi. Tunu anachochewa dhidi ya Sudi kwa kuambiwa kuwa yeye na Ashua ndio walikuwa wakiwinda roho yake.

Kukatiziwa vyanzo vya riziki. Sudi na Ashua wanaachwa bila namna ya kupata riziki baada ya soko la chapakazi kufungwa na majoka.

Vitisho. Sudi anatishwa na Kenga kuwa ulimi wake ungemtoma kwenye bahari mchafukoge.

Umaskini. Ashua anavaliwa na uhitiaji kiwango cha kumwendea Majoka kutafuta usaidizi. Watoto wao na Sudi (Pili na Pendo) wanalala njaa.

Watu kufurushwa makwao. Jamii ya kina Siti inaandikiwa vibarua vya kusema wahame Sagamoyo. Hii inatokana na wao kutouunga mkono uongozi wa Majoka.

Matusi. Sudi anarejelewa na Majoka kama Zebe. Majoka ananuia kumdunisha machoni pa mkewe Ashua.

Ndoa zao kuingiliwa. Majoka anapania kuisambaratisha ndoa ya Sudi na Ashua. Anamshawishi Ashua aachane na Sudi na akubali kuolewa naye.

Vyombo vya habari kufungwa. Baadhi ya vyombo vya habari kama vile runinga ya Mzalendo inafungwa kwa kupeperusha habari kuhusu watetezi wa haki.

Kupigwa marufuku kwa maandamano. Kenga anamshauri Majoka kutangaza kuwa maandamano yote ni haramu.

Kukabiliwa kwa nguvu wanapoandamana. Polisi wanatumia nguvu kupita kiasi kuwakabili waandamanaji. Matumizi haya ya nguvu yalipelekea kuumizwa kwa watu na kuuawa kwa vijana kiwandani.

Usaliti kutoka kwa wenzao. Juhudi za kuleta ukombozi zinapingwa na baadhi ya Wanasagamoyo kama vile Ngurumo, Asiye na Boza.

Kutimuliwa kwa wafadhili wa watetezi wa haki. Majoka anatoa pendekezo la wafadhili wa harakati za ukombozi kuvunja kambi.

Kukabiliwa na taasubi ya kiume. Tunu anapuuzwa na baadhi ya watu kwa kuwa ni mwanamke. Ngurumo anasema, "Heri nimpe paka (kura)...lakini si mwanamke."

Kupumbazwa kwa baadhi ya wananchi. Baadhi ya wananchi wanapinga harakati ya ukombozi kwa kuwa walipumbazwa na Majoka na watu wake kwa kuachiwa kitu pale mangweni. Kutenganishwa wakati mikutano muhimu Wakati Tunu na Sudi wanaenda kwa Majoka kusema naye, majoka anawatenga ili aweze kukabiliana na kila mmoja.

Kuishi kwa hofu na wasiwasi. Bi. Hashima anaeleza jinsi ambavyo wanaishi kwa wasiwasi kutokana na dhiki wanazokutishwa na uonghozi wa Majoka.

Kukosa muda wa kuwa na familia. Sudi alikuwa na shughuli nyingi za kiukombozi, zilizomfanya kukosa muda wa kuwa familia yake.

Swali la Insha 10

Fafanua mbinu zifuatazo kwa kutolea mifano mwafaka

  1. Kweli kinzani (alama 10)
  2. Taashira (alama 10)

Kweli Kinzani

Habari zinazotolewa na mjumbe katika rununu ni za kinaya, kuwa Wanasagamoyo wasirudishe maendeleo nyuma bali wafurahie ufanisi ambao umepatikana katika kipindi cha miaka tisini baada ya uhuru.

Ujumbe huu ni kinaya kwa vile Sagamoyo hakuna maendeleo wala ufanisi. Watu wana njaa na wanakosa mambo ya kimsingi kama vile maji, elimu na matakwa mengine mengi.

Boza anadai kuwa kulipa kodi ni kujenga nchi na kujitegemea. Kauli hii ni kinaya kwa vile kodi wanayolipa wanasagamoyo haitumiki kujenga nchi kwa vyovyote vile.

Sudi anasema kuwa katika kipindi cha mwezi mzima wa uhuru wale mali walizochuna kwa miaka sitini. Ni kinaya kwa kuwa hakuna walichovuna, viongozi hujilimbikizia mali.

Boza anamwambia Sudi kuwa wanatia doa kwa kila jambo nzuri.Ni kinaya kwa vile hakuna mambo mazuri ambayo Majoka amefanya Sagamoyo.

Wanasagamoyo kusheherekea miaka sitini ya uhuru ni kinaya kwani hakuna cha muhimu kusheherekewa, hakuna maendeleo Sagamoyo.

Boza anadai kuwa kinyago chake chapendeza na kufanana na shujaa Marara Bin Ngao, ni kinaya kwani kinyago hicho hakifanani na shujaa huyo.

Mzee Majoka kudai kuwa anamheshimu sudi ni kinaya. Majoka hana heshima kwa raia wake, nia yake ni kutaka Sudi amchongee kinyago -Kenga kumwambia Sudi kuwa ipo siku atamtafuta mzee Majoka ni kinaya kwani Sudi hana haja naye.

Majoka kudai kuwa takataka za soko zitaaribu sifa nzuri za jimbo la Sagamoyo ni kinaya kwa vile hakuna sifa nzuri Sagamoyo. Viongozi wanaendeleza maovu na hata kupanga mauaji.

Kauli ya Husda kuwa Ashua ni kimada wa Majoka ni kinaya kwa vile Ashua hana nia yoyote na Majoka. Amefika kwake kuomba msaada.

Ni kinaya kwa polisi Sagamoyo kutawanya waandamanaji.Polisi wanapaswa kulinda na kutetea haki za wananchi.

Majoka kusema kuwa Sagamoyo wanajiweza ni kinaya.Watu wana matakwa mengi ni maskini, wana njaa na hata kupata ufadhili kitoka nje kwa miradi isiyo muhimu. zozote 10x1=10

Taashira

Kinyago cha shujaa anachochonga Sudi kwamba shujaa huyo ni mkubwa kuliko jina lake na urembo wa shujaa huyo ni bora zaidi. Shujaa anayerejelewa hapa ni Tunu yale ambayo anatendea Sagamoyo ni makuu kuliko jina lake, kutetea haki za wanyonge.

Husda anamwambia Ashua kuwa hawezi kumtoa tonge kinywani hivi hivi.tonge ni Majoka bwanake Husda kuwa Ashua hawezi kumnyanganya bwana.

Husda kumwita Majoka pwagu, pwagu ni mwizi na Majoka amewaibia wanasagamoyo,ananyakua ardhi, anaiba kodi na kuwalaghai wanasagamoyo.

Husda anamwambia Ashua kuwa ameshindwa kufuga kuku na kanga hatamweza. Kuku ni mumewe Sudi, na Kenga ni Majoka, kwamba Ashua ameshindwa kumtunza Sudi na Majoka hampati

Tunu kuwekewa vidhibitimwendo ni kukomeshwa au kuwekewa vikwazo ili afe moyo kutetea haki za wanasagamoyo.

Majoka anasema kuwa hatatumia bomu kuulia mbu. Anamrejelea Tunu kuwa mbu kunaanisha hatatumia nguvu nyingi kumwangamiza.

Majoka anasema ili kuongoza Sagamoyo ni lazima uwe na ngozi ngumu, kumaanisha ni lazima uwe mkali na mwenye nguvu.

Jukwaa kupakwa rangi kwa ajili ya sherehe ya uhuru ni kufunika uozo ulio Sagamoyo.

Majoka anaposema salamu zinamgoja Sudi kwake, salamu ni Ashua mkewe aliye ndani ya jela.

Majoka anamshauri Sudi anawe mikono iwapo anataka kula na watu wazima. Kunawa mikono ni kukubali kuchonga kinyago ndiposa Ashua mkewe aachiliwe.

Chopi anamwambia Sudi iwapo shamba limemshinda kulima aseme.Shamba anarejelea Ashua kuwa iwapo Ashua amemshinda kutunza, aseme atunziwena Majoka.

Siafu huwa wengi na si rahisi kuwamaliza. Siafu ni wanasagamoyo ambao ni wengi kuliko Majoka na si rahisi kuwashnda.Hatimaye raia wanamshinda Majoka. (uk52) zozote 10x1=10

Swali la Insha 11

Tamthilia ya Kigogo ni ya kisasa . Thibitisha ukweli wa kauli hii. (al 20)

  1. Kuwepo kwa migomo katika tamthilia. Nchi nyingi duniani zinakumbwa na migomo ya wafanyakazi.
    Hii ni kama ilivyo katika Kigogo ambapo walimu na madaktari wanagoma kwa kuwa wanalipwan mishahara duni.
  2. Kuwepo kwa urithishaji wa uongozi. Viongozi wengi duniani hurithisha wanao au watu wa koo zao uongozini. Majoka anamwambia Kenga kuwa alikuwa na azma ya kumtangaza Ngao Junior kama mrithi wake wa kisiasa katika sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwake.
  3. Kuwepo kwa maandamano ya wanaharakati. Utawala wa kiimla utokeapo katika nchi mbalimbali duniani, hutokea wanamapinduzi ambao huwa na lengo la kuzikomboa nchi zao kutokana na tawala hizo. Tunu, Sudi na wafuasi wao wanashirikiana kumwondoa Majoka mamlakani.
  4. Utegemezi wa mikopo na misaada kutokana ughaibuni. Sagamoyo, kama nchi nyingine zinazoendelea duniani, inategemea mikopo na misaada kutoka nchi za ughaibuni. Mikopo yenyewe italipwa kwa kipindi cha miaka mia moja.
  5. Baadhi ya washauri wa viongozi wengi duniani huwapotosha. Kenga anmpotosha Majoka kwa ushauri mbaya kisha mwishowe anamsaliti.
  6. Wananchi kulipa kodi bila kupata huduma wanazostahili. Baadhi ya serikali katika nchi mbalimbali hukusanya kodi na kukosa kuwapa wananchi huduma muhimu. Serikali ya Majoka inakusanya kodi yay a juu lakini haidumishi usafi wa mazingira. Soko la chapakazi lina uvundo na maji-taka. Hii ni licha ya wanasagamoyo kulipa kodi ambayo ingesaidia katika uzoaji wa taka hizi. Tunu analalamikia kutokuwepo kwa huduma za matibabu, usafiri, maji safi, nguvu za umeme, elimu na kadhalika.
  7. Sera mbaya za uongozi zinazosababisha umaskini. Nchi nyingi duniani zimekumbwa na umaskini kutokana na ser mbovu za uongozi. Majoka na vikaragosi wake wanafunga soko la chapakazi linilotegemewa na watu wengi. Hali hii inasababisha umaskini. Wahusika kama vile Ashua wanashindwa kukidhi mahitaji ya familia zao.
  8. Utabaka. Utabaka huwepo katika nchi nyingi duniani. Huwa pana mpaka mkubwa baina ya matajiri na maskini. Hii ni kama ilivyo katika Sagamoyo.
  9. Viongozi mashuhuri kuidhinisha biashara haramu. Katika baadhi ya nchi duniani, viongozi mashuhuri ndio wanaoidhinisha biashara haramu. Mamapima anamweleza Tunu kuwa alikuwa na kibali cha uuzaji wa pombe haramu kutoka kwa Majoka.
  10. Viongozi wengi katika baadhi ya nchi duniani husahau wanachi waliowachagua. Viongozi kama hawa huendelea kujilimbikizia mali. Majoka anaendelea kujinufaisha kwa mali ya uuma akiwa na vikaragosa wake huku wananchi wakihangaika.
  11. Viongozi katili kuwaangamiza wapinzani wao. Katika nchi zinazoongozwa na viongozi wa kiimla, wapinzani huuawa huku wengine wakijeruhiwa vibaya. Jabali anauawa kwa amri ya Majoka huku Tunu akijeruhiwa vibaya.

Swali la Insha 12

  1. Jadili dhamira ya mwandishi wa Tamthilia ya Kigogo. (alama 10)
  2. Fafanua jinsi Ujenzi wa jamii mpya umeshughulikiwa na mwandishi. (alama 10)
  1.  
    • Kuonyesha umuhimu wa kupinga uongozi mbaya- kuboresha maisha- wananchi wana haki ya kuongozwa vizuri.
    • Kukashifu utepetevu wa viongozi – kutoletea nchi maendeleo yaliyotarajiwa- soko chafu na ukosefu wa kazi.
    • Kuhimiza ushirikiano katika kuondoa uongozi mbaya. Lazima raia waukabili na kuuondoa uongozi wa aina hii.
    • Kufichua uovu wa viongozi- ufisadi, usherati, dhulma, kujilimbikizia mali, ubinafsi, ubadhirifu nk.
    • Kuonyesha madhara  ya ulevi- vifo, upofu, utepetevu nk.
    • Umuhimu wa elimu-kuleta ukombozi- vijana wana mchango mkubwa sana. Km Tunu
    • Kuonyesha athari za umaskini- ukosefu wa kazi na mahitaji ya kimsingi.
    • Kukashifu washauri wabaya wa viongozi – huleta uongozi mbaya.
    • Kuonyesha changamoto za wanaopigania haki- kuumizwa, kuuawa, kutishwa nk.
    • Mwandishi anadhamiria kuonyesha uongozi mbaya na athari zake hasa katika mataifa yanayoendea.Viongozi hutumia mbinu mbalimbali kuongoza zinazowanyanyasa wananchi huku wakijinufaisha wenyewe bila kujali.
    • Kuonyesha kuwa ili kujenga jamii mpya, mapinduzi ni muhimu na ni sharti wananchi wajitolee kwa uzalendo ili kupigania haki zao na usawa na kupinga viongozi wasiofaa.
    • Mwandishi anaonyesha kuwa licha ya changamoto zinazomkumba mwanamke katika jamii, mwanamke ana nafasi muhimu katika uongozi na kuleta maendeleo katika jamii.    zozote 10
  2.      
    • Usafishaji nafsi- Majoka kuwa tayari kubadilika. Viongozi uacha mabaya na kutenda mema. Uk 84/85
    • Usalama kuimarika. Bwana Kingi kukubali kulinda usalama badala ya kutawanya waandamanaji. Uk89. Uk 90 Kingi kukataa kupiga risasi waliotaka Tunu achaguliwe.
    • Kuchagua viongozi waadilifu- uk 89- Wanasagamoyo kusema hawatakubali kuchagua viongozi wanaowaita wajinga.
    • Kufuata katiba- uk 90 Kingi kusema watu wana mamlaka makubwa kuliko amri za Majoka. Kingi anasema hana ruhusa ya kuvamia watu ambao hawajavunja sharia baada ya Majoka kutaka wapigwe risasi .
    • Kufuata sharia- Majoka anaposema amefuta kazi Kingi kwa kutofuata amri yake ya kupiga waandamanaji risasi, Kingi anamwambia lazima afuate utaratibu  wa kufuta mtu kazi. Uk91
    • Kukubali ukweli- Kingi anakubali uongozi dhalimu umefika mwisho na kuomba msamaha huku akijiunga na umati ilhali Majoka alikataa na kumwiita kunguru. uk 91
    • Kuomba msamaha- Mamapima anaomba msamaha kwa kuuza pomba haramu huku akijua kuwa aliwaponza, aliwapunja, aliwadhuru na alikuwa na tamaa.  uk 92
    • Kuchagua viongozi wanaofaa- kupatia Tunu uongozi hata kama ni mwanamke mradi yuko tayari kuongoza kwa haki.
    • kushirikiana bila kujali maneno ya watu- Tunu na sudiwalishirikiana kupigania haki bila kujali vile watu walisema ulikuwauhusianao wa kimapenzi.
    • kuacha maovu – Mamapima kuapa kuwa hatauza pombe haramu tena inayoua na kupofusha.

Swali la Insha 13

  1. Kufungwa kwa soko la Chapakazi kunawaathiri Wanasagamoyo vibaya. Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano kumi. (al. 10)
  2. Badala ya viongozi wa Sagamoyo kuwasaidia wananchi kupiga hatua kimaendeleo wanazibomoa juhudi zao. Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano kumi. (al. 10)
    1. Ulevi unaongezeka-Ngurumo anasema Kuwa mauzo ya pombe yalikuwa yameongezeka.
    2. Raia wanakataa kuhudhuria sherehe za majoka
    3. Uchumi wa jimbo unapungua wachuuzi hawalipi ushuru tena
    4. Majoka anaondolewa mamlakani-soko ni miongoni mwa Sababu
    5. Tunu anavamiwa na kupigwa kwa sababu anatetea kafunguliwa kwa soko
    6. Sudi Kombe na Bora wanahamisha Karakana yao na kuipeleka nyumbani. kwa sudi
    7. Vibanda vilivyokuwa karibu na soko vinabomolewa ili Majoka apate nafasi ya kujenga hoteli
    8. Njaa - Pili na Pendo wanalala njaa kwa sababu Sudi hana namna
    9. Kutishiwa kufungwa kwa Runinga ya mzalondo - Hii ni kwa sababu runinga. hii inapeperusha maandamano,
    10. Majoka anasema kuwa wafadhili wa Tunu wakunje jamri
    11. Maandamano - Raia wanaandamana ili kumhimiza majoka afungue soko
    12. Mauaji - vijana 5 wanaangamia warati wa maandamano haya
    13. Kisasi - majoka ana kisasi dhidi ya Tunu Kwa sababu ya kuongoza maandamano dhidi ya kunywa kwa soko na Majoka.
    14. Utegemezi - Ashua anaenda kwa Majoka, kuomba msaada wa chakula
    15. Kunyatuliwa mamlakani - sababu moja wapo inayowafanya raia kumchagua kwa sababu ya kufunga soko
    16. Kupanda kwa bei ya chakula
    17. Wafadhili wa Tunu wanafunishwa na Majoka
  1. Athari za kufungwa kwa soko
    1. Kukosa mahali pa kuuzia bidhaa - Sudi Bora na Kombe, wanakosa mahali pa kuuzia bidhaa zao.
    2. Njaa- watoto wake Sudi wanakosa chakula.
    3. Kuna mgogoro unaozuka kati ya Ashua na Sudi
    4. Migomo inaongezeka mfano mgomo Kwenye Kiwanda cha Majoka and Majoka.
    5. Umaarufu wa Tunu unazidi 60%
    6. Wachuuzi wengine wanakimbilia ulevini
    7. Bei ya chakula inapandishwa mara dufu
    8. Majoka anapata nafasi ya kulipiza kisasi
    9. Ardhi ya Soko inanyakuliwa na Majoka ili ajenge hoteli ya kibinafsi
    10. Majoka anawapa marafika zake ardhi
    11. Vijana watano wanauwawa kwenye maandamano
    12. Tunu anavamiwa na kujeruhiwa ili aache kuongoza maandamano
    13. Ashua anaenda kukopa kutoka kwa Majoka ambaye anachukua fursa hiyo na kulipiza kisasi
    14. Majoka anatishia kuwafunza wafadhili wa Tunu na kufunga kituo cha Runinga cha Mzalendo.
    15. Wananchi wanasusia sherehe za Uhuru ambazo zimeandaliwa na Majoka na Kuhudhuria mkutano wa Tunu kwenye Lango kuu.
    16. Kodi ya wachuuzi inakosa.

 Swali la Insha 14

Fafanua jinsi mwandishi alivyofaulu kutumia mbinu zifuatazo katika kuijenga tamthilia ya Kigogo.

  1. Kinaya (alama 8)
  2. Jazanda (alama 12)
  1. KINAYA 
    1. Habari zinazotolewa na mjumbe katika rununu ni za kinaya kuwa wanasagamoyo wasirudishe maendeleo nyuma bali wafurahie. ufanisi. Ukweli ni kuwa hakuna maendeleo
    2. Boza anadai kuwa kulipa kodi ni kujenga nchi na kujitegemea. Ni kinaya kwa vile kodi wanayolipa haitumiki kujenga nchi.
    3. Boza anamwambia Sudi kuwa wanatia doa kwa kila jambo nzuri. Ni kinaya kwa vile hakuna mambo mazuri ambayo majoka ameyafanya. (uk.5)
    4. Wanasagamoyo kusherehekea miaka sitini ya uhuru ni kinaya kwani hakuna cha muhimu kusherehekea.
    5. Majoka kudai kuwa takataka za soko zitaaribu sifa nzuri za jimbo la sagamoyo ni kinaya kwa vile hakuna sifa nzuri Sagamoyo.
    6. Kauli ya Husda kuwa Ashua ni kimada wa Majoka ni kinaya kwa vile Ashua hana nia yoyote na Majoka.
    7. Ni kinaya kwa polisi Sagamoyo kuwatawanya waandamaji. Polisi wanapaswa kulinda na kutetea haki za wananchi.
    8. Majoka kusema kuwa Sagamoyo wanajiweza ni Kinaya. Watu wana njaa. Sagamoyo yenye inapata ufadhili kutoka nje kwa miradi isiyo muhimu.
    9. Ni kinaya Kenga anapomwambia Majoka aache moyo wa huruma, Majoka hana huruma, anapanga mauaji.
    10. Ashua anasema kuwa katika jela kuna amani na amechoshwa na Sudi. Ni kinaya kwani Ashua anapata maumivu akiwa jelani.
    11. Madai ya Ngurumo nikinaya kuwa tangu soko kufungwa Sagamoyo ni pazuri mno. Watu hawana mahali pa kuuzia bidhaa.
    12. Ngurumo kusema kuwa pombe ni starehe ni kinaya kwani watu wanaangamia kutokana na pombe. 6x2=12
  2. JAZANDA.
    1. Husda anamwambia Ashua kuwa hawezi kumtoa bonge kinywani hivhivi. Bonge ni Majoka bwanake Husda kuwa Ashua hawezi kumnyang’anya bwana.
    2. Husda kumwita Majoka, pwagu, pwagu ni mwizi na Majoka amewaibia wanasagamoyo; ananyakua ardhi, anaiba kodi. (uk 27)
    3. Husda anamwambia Ashua kuwa ameshinda kufuga kuku na kanga hatamweza. Kuku ni mumewe sudi, na kanga ni Majoka. (uk.28)
    4. Majoka anasema kuwa hatatumia bomu kuulia mbu. Anamrejelea Tunu kuwa mbu. (uk.35) maanisha kuwa hatatumia nguvu nyingi kumwangamiza.
    5. Siafu huwa wengi na si rahisi kuwamaliza. Siafu ni wanasagamoyo ambao ni wengi kuliko majoka na si rahisi kuwashinda. (uk.52)
    6. Tunu anasema kuwa moto umewaka na utateketea wasipouzima. Mto ni harakati za mapinduzi sagamoyo.
    7. Hashima anamwonya Tunu asijipeleke kwenye pango la joka. Pango la joka anarejelea majoka na watu wake ambao ni katili na wauwaji
    8. Kinyago cha mke mrembo shujaa anachochonga sudi kinaashiria Tunu ambaye ni shujaa wa kweli
    9. Jazanda ya marubani ambao hawaendeshi vyombo vyao vizuri ni viongozi ambao hawaongozi kwa haki.
    10. Chombo anachopanda Majoka kinaenda kinyume badala ya kwenda mbele, majoka hajafanya maendeleo sagamoyo kwa sababu ya ufisadi na tamaa.

Swali la Insha 15

Mwandishi wa tamhtilia ya Kigogo amefanikisha katika kutumia ishara ili kufanikisha maudhui.(alama 20)

  • Fimbo ya Kenga yenye kichwa cha nyoka ni ishara ya jinsi alivyokuwa katili kwa raia.
  • Kitendo cha Majoka cha kuzungumza na babu yake anapozirai ni ishara kuwa wafu walikuwa wakimwita madhali ndiye aliyekuwa amewaua.
  • Majoka kuvaa mkufu  wa  shingoni wenye kidani cha umbo la swila ni ishara namna Majoka alivyokuwa hatari kwa maisha ya raia wa Sagamoyo.
  • Kilio na machozi mengi ndani ya ziwa lililofunika  damu ni ishara ya raia waliouliwa na Majoka wanalilia hali yao.
  • Kutojaa kwa raia ilivyo kawaida katika mkutano wa kudumisha sherehe za Uhuru pamoja na siku ya kuzaliwa kwa Majoka kutokana na uongozi wake dhalimu.
  • Hali ya Majoka kujiona ndani ya ziwa lililofurika damu ni ishara ya mauaji mengi ya raia aliyokuwa  akitekeleza katika uongozi wake.
  • Damu ya Jabali anayoiona Majoka ikitiririka  mikononi mwake akiwa amezirai ni ishara kuwa ndiye aliyemuua Jabali.
  • Bastola ya Majoka n silaha au chombo cha kuwatishia watawaliwa na watetezi wa  dhidi ya maovu ya kiongozi.
  • Chai ya mkandaa-kinywaji cha watu maskini.
  • Nyoka –kuashiria ushirikina na ukatili wa Majoka.
  • Chai ya maziwa –kinywaji cha  watu tajiri.
  • Chombo cha safari ya angani huashiria uongozi au madaraka.Majoka ni mojawapo wa marubani  yaani yeye ndiye kiongozi ambaye huwalaghai anawaongoza.
  • Embe lililoiva kupita kiasi ni ishara ya kuzorota kwa uchumi wa Sagamoyo.
  • Gari la kifahari la Kenga-hali ya utajiri wa kupindukia na ubepari.
  • Hoteli za kifahari-huashiria sherehe ya tabaka la juu.
  • Kinyago –kuashiria hali ya viongozi kupenda uluwa. Kupenda makuu kwa kutaka majina ya watu wa mbari zao na zaidi kusifiwa milele kwani walipigania uhuru.
  • Kiti cha kifahari cha Majoka –kuashiria tabaka la juu kiuchumi, tabaka lenye starehe kutokana na utajiri wake.
  • Mbuyu ni makao ya shetani –kuashiria dhuluma za kiongozi –Kenga anawahutubia wananchi chini ya mti wa mbuyu.
  • Ndoto ya Tunu-ufunuo wa madhila ya wapiginiaji /wanajamii wakati a uongozi  uliopita  wa babake Majoka , Marar bin Ngao.
  • Pombe ni ishara ya utovu wa maadili katika jamii.
  • Redio-kuashiria maendeleo ya kiteknolojia yanayotumiwa na viongozi kujikuza wenyewe.
  • Televisheni-ishara ya maendeleo katika uwanja wa mawasiliano.Ni kinaya kwa sababu hatuoni maendeleo haya ya kimawasiliano yakichangia kuboresha hali za maisha ya  mwananchi  wa kawaida.
  • Soko chafu-ni ishara ya uozo wa kimaadili wa kisiasa.
  • Sumu ya nyoka –ishara ya dawa ya kulevya na masaibu yanayotokana na kunyanyaswa kwa wafanyikazi wa tabaka la chini na viongozi.
  • Kinyago cha mwanamke- kuonyesha kuwa mwanamke pia ana uwezo wa kuwa kiongozi.
  • Keki- ni ishara ya rasilimali za nchi- ambapo wananchi wanapata makobo tu huku mgao mkubwa ukiwaendea viongozi
  • Maziara kujaa-kuashiria kuuawa kwa watu wengi  chini ya uongozi wa Mjoka.
  • Uvundo sokoni-kuashiria kutowajibika kwa viongozi katika kusafisha soko hata baada ya kuchukua kodi-

Swali la Insha 16

Mandhari ya soko la chapa kazi yamezua maudhui na sifa kadhaa za wahusika. Jadili’ (alama 20)

  • Maudhui
    1. Ukosefu wa kazi – Sudi amesomea uanasheria lakini anachonga vinyango sokoni.
    2. Ufisadi – Ashua anasema wanalipa kodi lakini serikali ya Majoka anawaitisha kwa kutaka kitu zaidi.
    3. Uchafuzi wa mazigiria – wakati maji yanayopita mitaroni ni chafu na yananuka vibaya kutokana na kemikali inayotoka kwa kampuni ya Majoka and Majoka Company.
    4. Matumizi ya teknolojia – kusikizwa kwa habari kutoka kwa redio.Biashara – Ashuua anachuuza maembe , Boza ,Sudi naKkombe wanachonga vinyago.
    5. Ubadhirifu wa mali ya umma – Kenga anamshauri Sudi kuchonga kinyago na kumwahidi kumtunza kutokana na fedha ya ufadhili.
    6. Uongozi mbaya – kusherehekea uhuru kwa mwezi moja.
    7. Utu – Ashua kuwaletea Sudi , Boza na Kombe – chai ya mkandaa kwa maandazi.
  • Wahusika
    SUDI
    1. Mwepesi wa kukasirika. 
    2. Ana kipawa cha uchongaji
    3. Mzinduzi wa mambo – anapowaambia wenzake athari za kusherehekea uhuru kwa mwezi mmoja.
    4. Mwepesi wa hasira – Boza anapomkasirisha anataka kumpiga.
  • ASHUA .
    1. Mkarimu.
    2. Mtambuzi wa mambo – alitambua kuwa uongozi wa serikali kuitisha kitu zaidi ni kuwadhulumu wafanyabiashara.
    3. Ni mtani – anawaita Kombe shemeji
    4. wahusika wengine ni Boza na Kenga
      (mwanafunzi azingatie wahusika wawili kisha awatolee sifa tano tano kila mmoja. )

Swali la Insha 17

Mgala muue na haki umpe. Thibitisha ukweli wa methali hii ukimrejelea mhusika Husda. (alama 20)

  • Maana ya methali hii ni kuwa mgala anapaswa kulaumiwa inapobidi lakini apewe sifa anapostahiki. Hutumiwa kutukumbusho kuwa inafaa kuwwalaumu watu kutokana na udhaifu wao lakini tuwasifu wanapostahili. Husda ni wa kulaumiwa kwa sababu zifuatazo.
  • Husda ni mdaku. Ashua anamwita mdaku na msambazaji wa kanda za umbeya kwenye vikao vya masengenyo.
  • Mwenye wivu anamwonea wivu Ashua kwa kupendora na majoka. Anahiari kupigana na Ashua ili amlinde mumewe asinyakuliwe. Pia anamwonea wivu Ashua kwa kuwa amesoma hadi chuo kikuu.
  • Msherati anamtazama chopi lwa macho ya uchu na kumtamani namna chopi alivyovaa na kutembea. Anafanya haya yote nyuma ya miwani mweusi.
  • Mwenye matusi anamwita Ashua hawara kwa kumdhania ni mpenzi wa Majoka wa pembe za chaki.
  • Mpenda makuu aliolewa na Majoka kwa sababu ya mali za Majoka ila hakumpenda majoka akizipenda mali zake.
  • Fisadi anahakikisha Asiya mkoi wake amepata kandarasi ya kuoka keki ya uhuru
  • Mvumilivu alivumilia kuishi katika ndoa yenye dhuluma Majoka alizoea kumpiga Husda. Anatisha kumchafua Husda pale ofisini aatajileta fujo
  • Mwenye utu andhihirisho utu kwa jinsi anavyomshuglukikia mumewe akipozirai. Anamwambia chopi ampigie daktari wa Majoka simu. Pia anaandamana na mumewe hadi hospitalini na namwachi peke yake.
  • Mwajibikaji anawajibika kumtunza mumewe akiwa hospitalini.

Swali la Insha 18

  1. Jadili athari za tabia zifuatazo kwa wananchi wa Sagamoyo.
    1. Ulevi. (al 3)
    2. Maandamano. (al 3)
    3. Usherati. (al 3)
    4. Kutegemea mikopo. (al 3)
    5. Tamaa. (al 3)
  2. Fafanua mbinu tano alizozitumia Majoka kufanikisha uongozi wake. (al 5
  1. Jadili athari za tabia zifuatazo kwa wananchi wa sagamoyo.
    1. Ulevi. (alama 3)
      • Vifo vya watu.
      • Watu wamepofuka.
      • Biashara haramu kuhalalishwa.
        3×1= al 3
    2. Maandamano ( alama 3)
      • Vifo- vijana watano.
      • Wafanyakazi kuongezwa mshara mdogo- wauguzi na walimu.
      • Yalileta mabadiliko ya uongozi baadaye..watu walimkataa majoka.
      • Yalizindua watu kuhusu haki zao.
        3×1= al 3
    3. Usherati.(alama 3)
      • Uliharibu ndoa- asiya ngurumo,boza.. Ndoa ya husda na majoka.
      • Ulimpa asiya kandarasi ya kuoka keki ya uhuru.
      • Ulimpa asiya kibali cha kuendeleza biashara yake ya kuuza pombe haramu. 3×1= al 3
    4. Kutegemea mikopo (alama 3).
      • Uliwekea wanasagamoyo madeni mengi.
      • Ulipandisha gharama ya Maisha juu, ili kujaribu kulipia madeni hayo.
      • Yalifanya wanasagamoyo kupinga uongozi wa majoka. 3×1= al 3
    5. Tamaa (alama 3)
      • Ilifanya majoka kujaribu kukatalia uongozini.
      • Ilimfanya majoka kunyakua arddhi za umma kwa manufaa yake..mfano ardhi ya soko la chapa kazi.
      • Tamaa ya ilimfanya husda kuoleka kwa majoka. 3×1= al 3
  2. Fafanua mbinu TANO alizotumia majoka kufanikisha uongozi wake. (alama 5)
    • Vitisho.
    • Mauaji.
    • Matumizi ya vyombo vya dola.polisi,bunduki,vitoza machozi

Swali la Insha 19

  1. Juhudi za kujikomboa za jamii kutokana na matatizo yanayowakumba zinatingwa na changamoto si haba. Fafanua ukiegemea tamthilia ya Kigogo. (al 10)
  2. Kutokomaa na kutoadilika kwa viongozi ni kizingiti kikubwa cha maendeleo katika jamii ya Wanasagamoyo. Eleza kwa kutumia hoja kumi. (10)
  1. juhudi za kujikomboa za Wanasagamoyo zinatingwa na changamoto nyingi.
    • Kuuliwa kwa viongozi wao-jabali aliuliwa kupitia ajali ya barabarani.
    • Kuvamiwa na kuumizwa kwa viongozi wapinzani-tunu anachapwa na kuumizwa mfupa wa muundi.
    • Vijana kuuliwa wakiandamana kutokana na bei za juu za chakula.
    • Kingi anafutwa kazi anapopinga amri ya kuwapiga watu risasi.
    • Ashua anatiwa ndani Sudi anapokataa kumchongea kinyago majoka na kuupinga uongozi wake.
    • Vijana wanawasaliti wenzao wanaopigania haki za jamii. Ngurumo anapinga mpango wa kuwaunganisha wanasagamoyo kupigania haki zao.
    • Vijana wanaopinga uongozi dhalimu wa majoka wanatupiwa vijikaratasi wahame Sagamoyo hata kama ndiko nyumbani kwao.
    • Kina Boza na Kombe wanaongwa na vijikeki ili waendelee kuwa vikaragosi wa uongozi wa Majoka.
    • Juhudi za kujikomboa na uongozi mmbaya wa majoka zinatingwa na mpango wa Majoka na watu wake wa kuwanunulia pombe ili wasione haja ya kufunguliwa kwa soko.
    • Wanasagamoyo wanalemazwa kwa kufungiwa soko ili waendelee kumwabudu Majoka na uongozi wake.
    • Kituo cha runinga ya mzalendo kinafungwa kwa kuwazindua wananchi kuhusu haki zao.
    • Majoka ametawala Nyanja zote za kiuchumi za jimbo na kuwalemaza wananchi kiuchumi ili wakose uwezo wa kumpinga. Ana kampuni, shule na mahoteli ilhali wananchi wengi ni maskini.
    • Majoka anatumia polisi vibaya. Maandamano yote yazimwa kwa vitoza machozi na risasi.
    • Majoka anaeneza propaganda za kuwapiganisha wanaharakati. Wavamizi wa Tunu waliotumwa na Majoka wanamwambia kuwa roho yake inawindwa na Sudi na Ashua kutokana na uhusiano wake na Sudi.
      10x1=10
  2. kutokomaa kwa viongozi na kutoadilika ni kizingiti cha maendeleo ya jamii.
    • Ufisadi wa Majoka unafanya vijana wengi kupoteza maisha kutokana na unywaji wa pombe haramu aliyoihararisha.
    • Ulafi wa majoka unamsukuma kunyakua kiwanja cha soko la Chapakazi lililokuwa tegemeo la kiuchumi la wengi.
    • Kutokamaa kwa Majoka kunamfanya aamrishe kupigwa risasi kwa wananchi waliokuwa wakiandamana kutokana na kufungwa kwa soko.
    • Kutokomaa kwa Majoka kidemokrasia kunamfanya umwangamize mpinzani wake Jabali ili asipingwa na yeyote.
    • Ulafi wa majoka unafanya awauzie vijana dawa za kulevya shuleni hivyo kuwafanya kuwa mazuzu na makabeji.
    • Kutokana na kutokomaa kwa Majoka, anakosa kujua umuhimu wa miti kwa mazingira hivyo anafungulia biashara ya ukataji wa miti kiholela inayoathiri mazingira na ukulima kwa jumla..
    • Kutokomaa kwake pia kunamfanya akope mikopo kutoka nchi za nje ili kufadhili miradi isiyomuhimu. Wananchi watalipa madeni haya kwa miaka mia moja.
    • Kutoadilika kwa Majoka kunamfanya ampe Asiya kibali cha kuuza pombe hivyo kuwasukumiza vijana wengi katika ulevi na matumizi ya dawa za kulevya badala ya kujenga nchi.
    • Kandarasi sagamoyo zinapeanwa kwa mapendeleo kwa marafiki wa karibu wa uongozi wa Majoka. Asiya ndiye muokaji wa keki za uhuru jambo ambalo ni hatari kwa uchumi kwani ni ufisadi.
    • Elimu sagamoyo pamoja na mambo mengine kama umeme, maji safi na huduma za afya ni ndoto kwa Wanasagamoyo wengi. Hii ni kutokana na uongozi mbaya wa Majoka.
    • Uongozi katika serikali ya Majoka ni wa kinasaba. Mshauri wake mkuu ni binamu yake na ana mpango wa kumrithisha Ngao Junior uongozi wa jimbo.
    • Ukware na kutoadilika kwa Majoka kunaathiri ndoa yake na kumkosanisha na wananchi wengine kama Ashua anayetaka ampende kwa nguvu.
    • Wananchi Sagamoyo hawana haki ya kujitetea. Wanaondamana wakabiliwa vikali na polisi huku walimu na wauguzi wakiongezewa mishahara huku kodi ikizidishwa maradufu.
      10x1=10

Swali la Insha 20

Utawala mbaya ni tatizo sugu linalozikumba nchi nyingi za kiafrika. Jadili, kwa kurejelea matukio ishirini katika tamthilia ya Kigogo. (alama 20)

  1. Uongozi umesalia katika familia moja ya kina Majoka tangu uhuru ulipopatikana.
  2. Badala ya kupiga vita pombe haramu, serikali inatoa kibali cha kuuza pombe hiyo kinyume na sheria.
  3. Badala ya kulinda usalama, polisi wanatumiwa kuwatawanya na kuwapiga watu wanaoandamana kwa amani.
  4. Viongozi wa upinzani ambao wanapinga utawala wa kiimla wa Majoka wanauawa k.v Jabali.
  5. Majoka ana unafiki kwani anasema wasiruhusu watu wachache waliojazwa kasumba za kikoloni kuwarejesha katika utumwa. Yeye anatenda mambo yayo hayo anayoyakashifu.
  6. Watawaliwa wanapumbazwa kwa nyimbo na matangazo kwenye vyombo vya habari. Wimbo wa kizalendo unatumiwa kumsifu Ngao, kiongozi wa Sagamoyo.
  7. Viongozi k.v Majoka wanapanga kuongeza misharara ya walimu na wanguzi kisha wapandishe kodi.
  8. Viongozi kutumia propaganda. Wanatumia vyombo vya Dola k.v tevevisheni na askari kama njia ya kuoneza propaganda zao.
  9. Utawala unajaribu kutumia hila kuwatenganisha Tunu na Sudi ili kudhoofisha upinzani. Majoka anapendekeza Tunu aolewe na Ngao Junior.
  10. Mojaka anapanga njama ya kumuua Ngurumo kisha anapendekeza chatu mmoja atolewe kafara ili watu wasitilie maanani kifo chake.
  11. Serikali inakopa pesa nyingi kugharamia miradi duni ya kuchonga vinyago.
  12. Ardhi ya sokoni inagawiwa washiriki wa karibu wa Majoka k.v Kenga.
  13. Serikali inashiriki katika biashara ya kukata na kuuza miti badala ya kutunza mazingira.
  14. Badala ya kuchimba mabwawa ya maji itakayowanufaisha wananchi wote, viongozi wanajichimbia visima katika maboma yao.
  15. Viongozi wanatumia vyeo vyao kuwashinikiza watu kutekeleza matakwa yao. Majoka anapanga njama ya kumtia Ashua mbaroni ili amshinikize Sudi kumchongea kinyago.
  16. Majoka anaagiza watu kusherehekea uhuru wa jimbo lao kwa mwezi mmoja.
  17. Soko la Chapakazi linanuka uvundo wa maji chafu kwenye mitaro licha ya wananchi kulipa kodi.
  18. Kandarasi zinapoanwa kwa njia ya ufisadi.
    Ngurumo mshiriki wa karibu wa Majoka anakula uroda na Asiya na kumpendekeza apewe kandarasi ya kuoka keki.
  19. Majoka and Majoka Company inatengeneza dawa za kulevya na kuharibu vijana akiwemo Ngao Junior.
  20. Majoka and Majoka Academy inawaharibu wanafunzi na kuishia kuwa makabeji kwa kutumia dawa za kulevya.
  21. Majoka anakopa pesa kutoka mataifa ya magharibi kufadhili miradi duni ya kuchonga vinyago.
  22. Mama pima anapika pombe haramu kwa kibali cha Majoka ilhali ni kinyume na katiba.
  23. Majoka anaagiza televisheni ya wazalendo ifungwe ibaki tu yake ya sauti ya mashujaa.
  24. Majoka anatumia ushirikina katika uongozi wake. Nembo ya chama chake ni swira / nyoka.

Swali la Insha 21

  1. Kwa kutolea hoja kumi, onyesha matumizi ya kinaya ili kufanikisha maudhui mbalimbali katika tamthilia ya Kigogo. (al 10)
  2. Jumuiya ya Sagamoyo inakumbwa na udhalimu chungu nzima. Thibitisha kwa hoja kumi. (al 10)
  1. Kwa kutolea hoja kumi, onyesha matumizi ya kinaya ili kufanikisha maudhui mbalimbali katika tamthilia ya Kigogo. (al 10)
    • Habari zinazotolewa na mjumbe katika rununu ni za kinaya, kuwa wanasagamoyo wasirudishe maendeleo nyuma bali wafurahie ufanisi ambao umepatikana katika kipindi cha miaka sitini baada ya uhuru.- uongozi mbaya
    • Ujumbe huu ni kinaya kwa vile Sagamoyo hakuna maendeleo wala ufanisi. Watu wana njaa na wanakosa mambo ya kimsingi kama vile maji, elimu na matakwa mengine mengi -umaskini
    • Boza anadai kuwa kulipa kodi ni kujenga nchi na kujitegemea. Kauli hii ni kinaya kwa vile kodi wanayolipa wanasagamoyo haitumiki kujenga nchi kwa vyovyote vile. ubadhirifu
    • Sudi anasema kuwa katika kipindi cha mwezi mzima wa uhuru wale mali walizochuna kwa miaka sitini. Ni kinaya kwa kuwa hakuna walichovuna, viongozi hujilimbikizia mali. Ubadhirifu/ umaskini
    • Boza anamwambia Sudi kuwa wanatia doa kwa kila jambo nzuri. Ni kinaya kwa vile hakuna mambo mazuri ambayo Majoka amefanya Sagamoyo. (uk5) mapuuza
    • Wanasagamoyo kusherehekea miaka sitini ya uhuru ni kinaya kwani hakuna cha muhimu kusheherekewa, hakuna maendeleo Sagamoyo. Uongozi mbaya
    • Boza anadai kuwa kinyago chake chapendeza na kufanana na shujaa Marara Bin Ngao, ni kinaya kwani kinyago hicho hakifanani na shujaa huyo. ubinafsi
      Mzee Majoka kudai kuwa anamheshimu sudi ni kinaya. Majoka hana heshima kwa raia wake, nia yake ni kutaka Sudi amchongee kinyago. (uk13) ubinafsi
    • Kenga kumwambia Sudi kuwa ipo siku atamtafuta mzee Majoka ni kinaya kwani Sudi hana haja naye. ulaghai
    • Majoka kudai kuwa takataka za soko zitaharibu sifa nzuri za jimbo la Sagamoyo ni kinaya kwa vile hakuna sifa nzuri Sagamoyo. Viongozi wanaendeleza maovu na hata kupanga mauaji. 25unyakuzi wa ardhi
    • Ni kinaya kwa polisi Sagamoyo kutawanya waandamanaji. Polisi wanapaswa kulinda na kutetea haki za wananchi. udhalimu
    • Majoka kusema kuwa Sagamoyo wanajiweza ni kinaya. Watu wana matakwa mengi, ni maskini, wana njaa na hata kupata ufadhili kutoka nje kwa miradi isiyo muhimu.mapuuza
    • Ni kinaya Kenga anapomwambia Majoka aache moyo wa huruma, kwa sababu Majoka hana hata chembe cha huruma. Anapanga mauaji na kunyanyasa raia. 34 ukatili
    • Majoka anaposema kuwa juhudi za Tunu kuandaa migomo hazitamfikisha mahali ni kinaya kwa vile Tunu wanafanikiwa katika maandamano yao na hata kuungwa mkono na wengi. Utetezi wa baki
    • Ni kinaya kwa Ashua kumwambia Sudi kuwa ni kosa lake kutiwa ndani. Kosa ni la Majoka na njama yake ya kutaka kuchongewa kinyago. uchochezi
    • Ashua anasema kuwa katika jela kuna amani na amechoshwa na Sudi. Ni kinaya kwani Ashua anapata maumivu akiwa jelani. Mabadiliko/ukatili
    • Uvumi unaoenea kuwa Sudi na Ashua ndio wanaowinda roho ya Tunu ni kinaya kwani wote hawa ni wanamapinduzi wanaopigania haki Sagamoyo. Ulaghai/ propaganda
    • Madai ya Ngurumo ni kinaya kuwa tangu soko kufungwa Sagamoyo ni pazuri mnc. Eti mauzo ni maradufu ilihali watu hawana mahali pa kuuzia bidhaa zao, kifungwa kwa soko kunawaangaisha raia hata zaidi.60 mapuuza
    • Ngurumo kusema kuwa pombe ni starehe ni kinaya kwani watu wanaangamia kutokana na pombe, wengine kuwa vipofu.mapuuza
    • Watu wengi wanatarajiwa kufika katika uwanja wa ikulu ya Majoka kusherehekea uhuru siku ya sherehe lakini ni kinaya kwa kuwa ni watu kumi tu ambao wanafika. Mabadiliko/mapuuza
    • Mamapima kusema pombe inaondoa karaha ilhali inasababisha karaha kwa kuua, kupofusha, uzembe, kufuja familia. Tamaa ubinafsi/mapuuza
    • Raia kuimba nyimbo za kusifu Ngao badala ya kumkashifu kwa udhalimu wake. mapuuza
    • Mzee Majoka kudai kuwa anamheshimu sudi ni kinaya. Majoka hana heshima kwa raia wake, nia yake ni kutaka Sudi amchongee kinyago. (uk13) unafiki
      Mifano mingine yoyote mwafaka ya kinaya na maudhui
  2. Jumuiya ya Sagamoyo inakumbwa na udhalimu chungu nzima. Thibitisha kwa hoja kumi. (al 10)
    Dhuluma
    1. Kumwaga kemikali sokoni - serikali ya Majoka inamwaga taka za kemikali sokoni zinazowasababishia ndwele zisizo majina.
    2. Matumizi ya vitisho
      Bi. Hashima anasema kuwa serikali ya Majoka imewajaza hofu. Wanaishi kwa woga.
    3. Kubebeshwa mzigo wa madeni.
      Serikali ya Majoka inakopa pesa nyingi wanazotumia vibaya huku wananchi
      wakilazimika kulipa.
    4. Kufunga soko la chapa kazi.
      Majoka anafunga soko la chapa kazi bila kuwazia maslahi ya wanasagamoyo
      wanaolitegemea kwa riziki.
    5. Kuongeza Kodi. Baada ya kuwaongeza walimu na wauguzi mishahara, majoka anapandisha Kodi na hivyo kuwahini.
    6. Kutokuwa na bima ya matibabu.
      Babake Tunu anapofia kazini Majoka aliwanyima fidia kwa madai kuwa hakuwa na bima ya afya.
    7. Kupandisha bei ya bidhaa.
      Wafanyakazi kiwandani wamegoma kudai haki baada ya bei ya bidhaa kuongezwa huku soko likiwa limefungwa.
    8. Kufunga vyombo vya habari na kuwanyima wanasagamoyo haki ya kupata taarifa.
    9. Kukusanya kodi pasi na kusafisha soko.
      Wanasagamoyo wanaofanyia kazi katika soko la chapa kazi wanatozwa kodi ilihali haitumiki kulisafisha soko.
    10. Kufungwa jela bila hatia km Ashua
      Hakiki majibu mengine sahihi

Swali la Insha 22

“Jamii imemkandamiza mwanamke.“ Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea Tamthilia ya Kigogo.

  1. Kudharauliwa - Majoka anasema wanawake ni wanawake tu.
  2. Kutumiwa kama chombo cha mapenzi - Majoka anataka kuishiriki mapenzi na Ashua kama kigezo cha kumpa msaada.
  3. Kupigwa - Tunu anapigwa na kuvunjwa mguu na Chopi,Ngurumo na vijana wengine.
  4. Kutusiwa - Majoka anasema « sina time ya wanawake »
  5. Kufungwa bila hatia - Majoka anamfunga Ashua kwa madai ya kuzua vurugu katika ofisi ya serikali.Ilikuwa ni njia ya kulipiza kisasi kwa Sudi na kumnasa Ashua.
  6. Kunyimwa kura - Tunu anapoenda mangweni kujaribu kuwakomboa walevi wamuimbia nyimbo za kumkejeli. Ngurumu anadai kuwa hawezi kumpa mwanamke kura.
  7. Kutopewa nafasi ya uongozi katika jamii - Kenga anamwuliza Sudi iwapo Sagamayo ishawahi kuwa na Shujaa wa kike.
  8. Kupangiwa njama ya kuuwawa - Kenga na Majoka wanapanga njama ya kumwangamiza Tunu.Wanawatuma vijana,akiwepo Chopi kumwangamiza lakini wanamvunja mguu.
  9. Kuishi kwa hofu - Hashima anasema kuwa yeye na Tunu wake wanaishi kwa hofu,kila waamkapo wanapiga alhamdulillahi.
  10. Kusalitiwa katika ndoa - Majoka anasema kuwa hampendi Husda bali alimwoa ili kutimiza wajibu wake kama kiongozi.Majoka anampenda Ashua.

Swali la Insha 23

Eleza jinsi maudhui yafuatayo yanavyojitokeza katika Tamthilia ya Kigogo

  1. Utabaka (alama 5)
  2. Usaliti (alama 5)
  3. Umaskini ( alama 5)
  4. Dhuluma ( alama 5)
  1. Utabaka
    • Majoka na Kenga ni wa tabaka la juu ilhali wafanyakazi wa sokoni ni wa tabaka la chini
    • Majoka anamiliki mali nyingi huko sagamoyo, kwa mfano- Majoka and Majoka Academy, Majoka and Majoka modern Resort
    • Matajiri kama majoka wanapata huduma bora za kiafya , anaye hata daktari wake huku huduma za afya Sagamoyo zikidorora
    • Tabaka la juu lina fedha za kuendeleza miradi yao kwa haraka kama vile ujenzi wa hoteli ya kifahari ilhali ni vigumu kwa maskini kupata lishe au kumudu bei ya vyakula
    • Tabaka la juu linatumia tabaka la chini kutimiza malengo yake. Vijana wahuni kwa mfano wanalipwa na wanasiasa ili wamuumize Tunu
    • Tabaka la chini halina vitu vya kimsingi kama mavazi kwa mfano Ashua ilhali Husda ana mavazi mazuri ya kisasa. Sudi ni maskini kiasi kwamba anashindwa kumpa mkewe pesa za matumizi.
      Zozote 5
      Kadiria majibu ya mwanafunzi
  2. Usaliti
    • Majoka anawasaliti wafanyabiashara kwa kuwafungia soko la chapakazi
    • Majoka anawasaliti wafanyakazi kwa kupandisha kodi licha ya hali ngumu ya maisha
    • Majoka anamsaliti Ashua kwa kumpangia njama ya kumkutanisha na mkewe Husda na kufungwa korokoroni
    • Majoka aliwasaliti wanahabari kwa kupanga kuwafungia vituo vya habari kwa kupeperusha habari za maandamano
    • Boza aliwasaliti wafanyakazi wenzakekwa kumuunga mkono Majoka licha ya kuwa aliwafungia soko walikofanyia biashara
    • Boza anawasaliti wenzake kwa kukosa kuwapasha habari kuhusiana na mradi wa kuchonga kinyagoKenga alimsaliti Majoka kwa kuungana na wananchi mambo yanapomharibikia Majoka
    • Uongozi wa Sagamoyo unawasaliti wananchi kwa kuwatupia vijikaratasi wahame Sagamoyo si kwao
    • Serikali ya Majoka inawasaliti walimu na madaktari kwa kuwaongezea mshahara na kisha kupandisha kodi
    • Asiya aliwasaliti wananchi kwa kuwauzia pombe haramu iliyodhuru afya yao na hata kupelekea maafa
  3. Umaskini
    • Wachongaji vinyago walitoka tabaka la chini. Wanakunywa chai ya mkandaa
    • Watoto wa Sudi wanalala njaa. Hii inamlazimu Ashua kwenda kuomba msaada kwa Majoka
    • Mamapima anauza pombe haramu kama njia ya kujipatia riziki
    • Mzee Majoka ana mpango wa kutoa chakula kwa wale wasiojiweza. Hii ni ithibati tosha kuna umaskini katika jimbo la Sagamoyo
    • Soko la Chapakazi linapofungwa wafanyakazi wanahangaika. Soko hili ni la walalahoi ambao walitarajia kuchuma riziki ya kila siku kutoka soko hili.
  4. Dhuluma
    • Majoka napanga njama na Kenga na kumfungia Ashua kwa kisingizio kuwa alizua rabsha ofisini mwake
    • Korokoroni Ashua alipigwa na kujeruhiwa
    • Tunu alivamiwa na wahuni na kuvunjwa muundi wa mguu
    • Majoka na Kenga walipanga njama ambapo jabali aliaga dunia katika ajali ya barabarani.
    • Watu wanaoandamana wanapigwa na polisi na wengine kuuawa.
    • Serikali ya Majoka inafunga soko la Chapakazi ambalo lilikuwa tegemeo la kila siku
    • Hashima anatujulisha kuwa kumekuwa na umwagikaji mwingi wa damu pale Sagamoyo kiasi cha damu kuitia ardhi najisi.

Swali la Insha 24

Eleza athari zozote kumi za tamaa na ubinafsi kwa kurejelea tamthilia ya kigogo. (Alama 20)

  • Umaskini – Hii inatokana na kunyakuliwa kwa ardhi ya soko la Chapakazi
  • Ari ya mapinduzi – Tamaa na ubinafsi wa watawala vinakarifisha wazalendo kama Tunu na Sudi na wanaanzisha harakati za kuung’oa mamlakani uongozi wa Majoka.
  • Uchafuzi wa mazingira – Tamaa ya wanaviwanda inawasukuma kutupa kemikali na taka kwenye mitaro ya maji.
  • Utabaka – kuna matajiri Sagamoyo kama Majoka kutokana na tamaa ya kuwa na mali nyingi. Kuna maskini kwa mfano walevi.
  • Matumizi mabaya ya vyombo vya dola- kutokana na tamaa ya kutaka kusalia mamlakani Majoka anatumia vyombo vya dola kama polisi na jela kutekeleza unyama.
  • Vyombo vya habari
  • Ukame – ukataji miti ovyo umesababisha maziwa na mito kukauka. Biashara hii imekubaliwa na Majoka.
  • Kuathirika kisaikolojia – Tamaa na Ubinafsi wa Majoka unamfanya kutekeleza ukatili ambao unaifanya nafsi yake kumuhukumu.
  • Unyanyasaji – Tamaa ya viongozi inawafanya wadai kodi kubwa ambayo haitumiwi kuimarisha soko la chapakazi.
  • Tamaa ya kukopa kopa fedha katika mataifa ya nje kunaachia wanajamii mzigo wa kulipa madeni hayo kwa muda mrefu.
  • Tamaa na ubinafsi wa wafuasi wa Majoka kama vile Boza na Ngurumo vinawafanya kufumbia macho uozo wa kigogo Majoka.
  • Vifo
  • Njaa
  • Utengano katika jamii

Swali la Insha 25

Kwa kurejelea tamthilia nzima ,jadili jinsi mwandishi alivyotumia jazanda (alama 20)

Jazanda ni mlinganisho wa vitu viwili moja kwa moja bila kutumia viunganishi

  • Sumu ya nyoka – kurejelea dawa za kulevya au pombe hatari na haramu
  • Maji machafu na harufu mbali sokoni – maovu ya kiutawa uliotokana na utovu wa maadili wa viongozi
  • Keki ya taifa – raslimali za nchi ambazo zinawanufaisha viongozi tu na jamaa zao huku wananchi wa kawaida wakipata mapato duni
  • Wanafunzi kuwa makabeji – Wanafunzi kuathirika akili kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya
  • Kuku na kipanga – kuku ni wanajamii kipanga ni viongozi haki haupatikani kwa urahisi
  • Wingu la kupita na la kutanda – maandamano yanayoendelea
  • Kukata mti kufurusha ndege – ilikuwazuia watu kuandamana, viongozi waangamizwe.
  • Chombo cha usafiri na rubani – uongozi na kiongozi (Uongozi mbaya wa Majoka)
  • Chombo cha babu kutikisa chombo cha Majoka – tofauti zao za kiaadili. Majoka hayuko tayari kubadilika
  • Kisima kilichiingiwa paka na maji yasiyonyweka – uharibifu na maangamizi – kuporomoka kwa uongozi wa Majoka.
  • Mshumaa uwakao – kiongozi anayefaa kuwaletea wengine matumaini na kuwaendeleza
  • Ulaji wa asali ya nyuki- msaada au maafikio ya mtu.Ashua amemkumbuka msaada alioupata awali na kurejea kwa majoka kupata usaidizi Zaidi.
  • Ziwa la damu itiririkayo mikononi damu Majoka aliyomwaga kutokana na mauaji ya kiutawala
  • Ngawa na minyororo iliyomfunga Majoka utabiri wa kuporomoka kwa utawala wake na labda kutiwa gerezani
  • Udongo na mfinyanzi – udongo ni watu dhaifu wa chini . mfinyanzi ni viongozi – wanyonge hawana uwezo wa kupinga viongozi
  • Udhibiti mwendo – njia za kuzuia wanaharakati kama /tunu
  • Kucheza na Simba anayenyonyesha – kufanya kitendo cha hatari
  • Chatu – kikosi cha kutekeleza maovu na mateso
  • Msumari kusema ukweli
  • Kuwaka moto – mambo kuwa mabaya
  • Shamba limekushinda kulima – Sudi – kushindwa kumdhibiti mkewe
  • Panya amejileta mwenyewe kwa paka
    Ashua amejileta ofisini mwa Majoka ambaye amekuwa akimtamani
    Kutia vyanda kwenye mdomo wa Simba kufanya kitendo hatari
  • Jukwaa la mbao na magunia – kuonyesha uduni na umaskini wa watu wa tabaka la chini
  • Pango la joka – eneo hatari – Tunu anatahadharishwa kwenda mkutanoni
  • Kubeba maisha kwa mbeleko – usiyachukulie mambo kwa uzito sana
  • Kujipaka matope – kuharibu sifa – Majoka anahofia kuharibiwa sifa wakati wa maandamano.

Swali la Insha 26

Kwa kurejelea Tamthilia ya Kigogo eleza jinsi mwandishi alivyotumia mbinu ya Majazi (al 20)

Majazi
Ni mbinu ya kuwapa wahusika (pamoja na kitu ama mahali) majina kulingana na tabia na sifa zao.

  • Majoka. Nyoka mkubwa ni joka. Wingi wake ni majoka. Nyoka ni mnyama atambaaye mwenye sumu kali aitumiayo kuwaangamiza wadudu na wanyama wengine ili awale. Majoka ana mbinu nyingi kama matumizi ya polisi (sumu yake) anaowatumia ili kuwapinga na kuwaangamiza wapinzani wa sera zake.
  • Tunu ni kitu ambacho ni adimu kupatikana na chenye kutumika kwa nadra. Mhusika Tunu anajitokeza kama mwanamke wa pekee anayezawadiwa kwa Wanasagamoyo ili kuwakomboa kutoka kwa uongozi mbaya wa Majoka.
  • Sudi ni bahati njema. Sagamoyo ina bahati kumpata Sudi anayeandamana na Tunu ili kupambana na jamii iliyojaa taasubi na ukandamizaji.
  • Kenga. Kumkenga mtu ni kumfanya kuamini jambo lisilo la kweli. Kenga anatumiwa na Majoka ili kuwalaghai watu na kuwafanya kukubaliana na sera duni za Majoka ili ajidumishe uongozini.
  • Husda. Kuhusudu ni kuwa na jicho la matamanio fulani. Husda anamhusudu Ashua kwa kisomo chake. Aidha anahusudu mali ya Majoka na kuolewa naye. Husda alimwangalia Chopi kwa macho yenye uchu.
  • Boza ni mtu mpumbavu. Mhusika Boza anaushabikia uongozi mbaya wa Majoka na amejawa na ubinafsi.
  • Siti ni jina la heshima kwa mwanamke. Siti anawasaidia Tunu na Sudi katika kuendeleza harakati za ukombozi.
  • Ngurumo ni sauti kubwa ya mvumo. Sauti hii huisha baadaye. Ngurumo anawatisha Tunu na Sudi huku akimshabikia Majoka. Baadaye anauawa na chatu wa Majoka.
  • Chopi ni kutembea kwa kuchechemea.Mhusika Chopi anatumwa ovyo na Majoka na kulemazwa na shughuli.
  • Pendo ni kuthamini kitu. Pendo anapendwa na kuthaminiwa na babake.
  • Kingi ni mfalme katika mchezo wa drafti (staranji). Kingi anakuwa mfalme katika ukombozi wa Sagamoyo kwa kukataa kuwaamrisha polisi kuwavamia wananchi.
  • Chapakazi. Kuchapa kazi ni kuifanya kwa bidii. Wanasagamoyo wanalipigania soko lao la Chapakazi wanakofanyia shughuli zao ili kupata mkate wao wa siku.
  • Sagamoyo. Kusaga ni kuvunjavunja. Kusaga moyo ni kuondoa matumaini na kuangamiza kabisa. Wanasagamoyo wanatamaushwa na uongozi mbaya wa Majoka anayewanyanyasa na kunyakua mali yao.
  • Majoka – Nyoka mkubwa mwenye sumu.
    Majoka ni mkali na anatekeleza maovu mengi dhidi ya Wanasagamoyo mfano mauaji.
  • Tunu- Zawadi
    Anawafaa Wanasagamoyo kwa kupigania haki zao k.v kufunguliwa kwa sokola Chapakazi. 
  • Husda- Mtu mwenye chuki/ Mtu mwenye kijicho.
    Husda anamwonea Ashua kijicho kwa kuwa amesoma hadi chuo kikuu.
  • Mamapima- Anapima pombe na kuwauzia walevi Mangweni
  • Sudi- Bahati njema
    – Anabahatika kumwoa Ashua mwanamke mwenye bidii na msomi.
    Pia amebahatika kuwa na kipawa cha uchongangi vinyago.
  • Sagamoyo- Kuponda moyo.
    Wanasaga wanapitia mateso na maumivu makali ya moyo
  • Chapakazi- Mahali pa kufanyia kazi kwa bidii.
    Wanasagamoyo wanatia bidii ili kuweza kujikimu.
  • Boza- Mtu mjinga/ mpumbavu.
    Boza anaiunga mkono serikali kipofu.
    Mke wake anazini na Ngurumo lakini yey hajui.
  • Kenga- Kulaghai/ kuhadaa
    -Kufanya mtu aamini jambo lisilokuwa la kweli
    -Ushauri potovu wa Kenga unachangia kuporomosha utawala wa majoka
    -Pia alimdanganya majoka kuwa mabo yako shwari na mwishowe anamgeuka na kujiunga na Tunu.
    Kombe- Aina ya mmea unaotambaa wenye sumu kali
    -Kombe alikuwa sumu kwa akina Sudi kwa kuwa alikuwa akihusiana na m rengo wa Majoka na hakutaka kuonyesha msimamo wake wazi.
  • Ngurumo- Ni sauti kubwa k.v ya Simba au inayosikika angani wakati wa mvua.
    Ngurumo alikuwa na hulka kama za ngurumo za radi. Anatumiwa kuuana na kuwapiga wapinzani wa Majoka.
  • Chopi- Kitendo cha kukosa kuwa imara
    -Chopi ana tabia za mtu aliyelewa na hakuzingatia maagizo anayopewa na Majoka.
  • Siti- Jina la heshima kwa mwanamke ambalo hutanguliziwa kabla ya jiana lake.
    -Siti alikuwa mfanyikazi wa Majoka na Majoka academy na inasemekana wafanyikazi wa hapo waliheshimiwa.

Swali la Insha 27

“Hatuwezi kukubali kutawaliwa kidhalimu tena!”

  1. Huku ukitoa mifano kumi, jadili namna wanasagamoyo walilemaza juhudi zao za kujikomboa. (al. 10 )
  2. Fafanua jinsi udhalimu unavyoendelezwa sagamoyo. (al. 10)
  1.                        
    • Askari kuwapiga waandamanaji / Ashua jelani.
    • Vijana/ wahini kutumiwa katika mauaji
    • Kuwachagua viongozi waba ya
    • Wengine ka Kengak kutoa ushauri mbaya ili wafaidike
    • Kuuza pombe haramu inayodhuru – mama pima
    • M,ajoka kufunga soko
    • Vyombo vya habari kueneza propaganda
    • Viongozi kueneza ukabila/ vijikaratasi
    • Majoka/ viongozi kufuja pesa za umma
    • Kubomoa vibanda vya wafanya ,biashara
    • Majoka kutoa kibali cha ukataji miti
    • Kutosafisha soko ilhali kodi inalipwa
    • Vijana kujituma katika ulevi/dawa za kulevya
  2.                          
    • Kufungwa kwa soko la sagamoyo ni dhuluma kwa wafanya biashara.
    • mauji ya Jabali na waandamanaji
    • Ashua kuzuiliwa bila sababu.
    • Ashua kufanyiwa uhuni na majoka.
    • Ashua kupigwa kwenye seli
    • Mazingira machafu na wanasagamoyo walipa kodi
    • Kuvamiwa na kupigwa kwa Tunu
    • Majoka kukataa kutoa msaada wa chakula kwa wahitaji
    • Kutoa kodi ya juu
    • Kufunga vyombo vya habari mf. Runinga ya mzalendo.
    • Kutumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanji
    • kukosa haki mahakamani.
    • Kuruhusu pombe haramu
    • Kuvivig’oa vibande vya wanasagamoyo
    • kujenga kiwanda cha sumu ua kuwa watu

Swali la Insha 28

Tathmini maudhui ya ndoa kwa mujibu wa tamthilia ya kigogo. (Al 20)

  1. Wanandoa wanasaidiana katika kuzikimu familia zao kwa kufanya kazi wote – kwa mfano, sudi na mkewe Ashua wafanya biashara katika soko la Chapakazi ili kujikimu kimaisha.
  2. Baadhi ya wanandoa wanapendana – Kwa mfano, Ashua anapompelekea mumewe sudi chai na mahamri sokoni, Sudi anasimama na kumkumbatia. Aidha sudi anamwita mkewe Ashua honey na sweetie, akiwa kwenye chumba cha wafungwa.
  3. Baadhi ya wanandoa si waaminifu – Kwa mfano, Asiya/mamapima anazini na Ngurumo ilhali ana mumewe, Boza. Isitoshe, hata Ngurumo ana mkewe. Hata Majoka anamwendea kinyume mkewe Husda kwa kutaka kuzini na Ashua.
  4. Baadhi ya ndoa hazina mapenzi ya kweli – kwa mfano, majoka anapozirai anazungumza na mkewe Husda na kumwambia kuwa hampendi kamwe na kumwambia kwamba ampendaye ni Ashua; mkewe sudi. Aidha Majoka anadai kwamba hata mkewe Husda hampendi/anachopenda ni mali zake.
  5. Ndoa inakabiliwa na tatizo la unafiki – Majoka anabainisha kwa husda anajifanya kuwa anampenda (Majoka) bali anachokipenda ni mali zake.
  6. Ndoa imekumbwa na tatizo la ujane – Bi. Hashima anabaki mjane baada ya kufiwa mumewe.
  7. Baadhi ya wanandoa wana tamaa ya mapenzi nje ya ndoa – Majoka anatamani Ashua, mkewe sudi, ilhali ana mkewe. Isitoshe, naye Husda anatamani Chopi kwa kumtazama kwa macho ya uchu ilhali ana mumewe, Majoka.
  8. Uchochezi ni chanzo ya kuvunjika kwa ndoa -. Ashua anamwomba mumewe, sudi talaka baada ya Majoka kumchochea dhidi yake, hali inayotishia kuvunjika kwa ndoa yao.
  9. Baadhi ya wanamume wanawadhulumu wake wao – kwa mfano, Husda anapozua rabsha ofisini baada ya kumkuta majoka na Ashua, Majoka anamwambia kuwa angeleta fujo angemchafua.
  10. Mwanaume ambaye ameoa na anatembea na mwanamke ambaye hajaolewa ni tishio la kuvunjika kwa ndoa, kwa mfano, Ashua anamtaka mumewe sudi kumpa talaka kwa sababu ya kutembea na Tunu mara kwa mara ilhali Tunu hajaolewa; hivyo kumshuku kuwa mpenziwe.
  11. Baadhi ya wanawake wanawataabisha wanaume kwa kutoridhika na wanachopewa na wanaume wao. Kwa mfano, Sudi anampa mkewe Ashua kila anachokiambua lakini Ashua haridhiki. Anataka Zaidi ya uwezo wa sudi hali ambayo imeleta mgogoro baina yao.
  12. Wanawake ni wasaliti katika ndoa – Ashua anamsaliti mumewe sudi kwa kumwambia kwamba amechoka kupendwa kimaskini ilhali anajua kwamba kipato cha sudi si kikubwa kwa sababu anafanya kazi duni ya kuchonga vinyago sokoni Chapakazi.
  13. Wanaume wanatoa ahadi za uwongo kwa wanawake wakati wa kuchumbiana – Kwa mfano, Sudi alimuahidi Ashua mengi kabla ya kumwoa lakini hakuyatimiza hali inayomchochea Ashua kutaka kuivunja ndoa yake.
  14. Baadhi ya wanandoa ni waaminifu – Kwa mfano, Ashua anakataa kufanya mapenzi na Majoka kwa kumwambia kuwa yeye ni mke wa mtu (sudi)
  15. Jukumu la mwanamke limedhiririka katika ndoa – kupika – Majoka amantaka mkewe Husda ampikie chapatti kwa kuku. Aidha, Ashua ampikia sudi chai na mahamri na kumpelekea kwenye karakana anakochongea vinyago.
  16. Wazazi wawatafutia wanao wa kiume mke wa kuoa – Kwa mfano, Majoka anamrai Tunu kukubali kuozwa kwa Ngao Junior, mwanawe Majoka lakini Tunu anakataa.
  17. Wanawake wanaochelewa kuolewa wanakejeliwa na wanajamii wenzao – Kwa mfano, walevi kule Mangweni wanamwimbia Tunu wimbo wa kumkejeli kwa kuchelewa kuolewa ilhali ana elimu ya kutosha.
  18. Jukumu la mwanamume katika ndoa ni kuikimu familia – Boza anamsuta Sudi kuwa jukumu la mwanamume si kukimbizana na waandamanaji bila kuikimu familia.
  19. Kuna ndoa za Lazima – Majoka akiwa amezirai anatetea jinsi alivyolazimishwa kumwoa Husda hali iliyomsababishia kulia usiku nzima. (UK. 75)
  20. Umaskini ni chanzo cha kuvunjika kwa ndoa. Kwa mfano , Ashua anamwitisha mumewe sudi talaka akidai kwamba amechokwa kupendwa kimaskini.
  21. Mapenzi ni wenzo muhimu katika kumchagua mwenzi wa ndoa. Kwa, mfano Majoka anapotaka Tunu aolewe na mwanawe Ngao Junior, Tunu anamwuliza iwapo anaona kuwa hawezi kusubiri akaolewa na mwanamume ampendaye.
  22. Ndoa imesawiriwa kama jambo, la Lazima kwa yeyote anayetaka kuwa kiongozi. Tunaambiwa kwamba Majoka alilazimishwa kumwoa Husda ili kutimiza wajibu wake katika jamii kama kiongozi

Swali la Insha 29

  1. Jadili mchango wa wasomi katika hali ya maisha ya Wanasagamoyo (alama 10)
  2. Fafanua umuhimu wa mazungumzo kati ya Majoka na Daktari katika kujenga tamthilia ya Kigogo.  (alama 10)
  1. Wasomi 
    1. Wanachangia kuendeleza uchumi✓. Hata wanapokosa ajira, wajiajiri. Sudi anachonga vinyago; Ashua anauza mandazi.
    2. Wanapigania haki za wanyonge. Tunu na Sudi wakiwa chuoni walikuwa viongozi wa harakati✓ za kupigania haki.
    3. Wanawazindua Wanasagamoyo kuhusu haja ya kuwa na uongozi unaozingatia misingi ya kidemokrasia. Tunu na Sudi wanawahamasisha Wanasagamoyo kuhusu haki zao.
    4. Wanaukosoa uongozi. Tunu anamkabili Majoka na kumwambia kwamba Wanasagamoyo wana haki ya kuishi.(uk. 45).
    5. Wanahimiza haja ya kuzingatia maadili ya kijamii. Ashua anaheshimu asasi ya ndoa. Anakataa ushawishi wa Majoka.
    6. Wanachangia kuboresha hali ya utendakazi katika taaluma zao. Walimu wagoma ili kupata mazingira mazuri ya kufanyia kazi.
    7. Wanatoa kielelezo cha uongozi ufaao. Tunu anasema kwamba wanahitaji viongozi wanaofahamu matatizo yao.
    8. Wanafunza kuhusu umuhimu wa familia na malezi. Sudi anamwambia Ashua awafikirie watoto wao. (uk. 48)
    9. Wanaunda na kuimarisha itikadi za kijinsia zinazowawezesha kuleta mabadiliko katika jamii. Licha ya Sudi na Tunu kushukiwa kuwa wapenzi, hawalegezi juhudi zao za kuuhamasisha umma. Sudi anachonga kinyago cha mwanamke.
    10. Kuwakosoa wanyonge ambao wanatumiwa kama vibaraka. Tunu anamuuliza Ngurumo kipi muhimu; dhifa au kufunguliwa kwa soko. Sudi anawatanabahisha kina Boza kuhusu swala la majitaka.
    11. Baadhi yao wanaendeleza ubaguzi wa kijinsia. Ngurumo anasema hawezi kumpa mwanamke kura.
    12. Wanasisitiza umuhimu wa elimu na ustaarabu. Ashua anasema kutoelimika kuna tatizo (uk. 28), naye Husda anasema elimu bila ustaarabu haifai.
    13. Baadhi wanakwamiza juhudi za kupigania haki. Ngurumo anatumiwa na Majoka kumpiga na kumnyamazisha Tunu.
    14. Daktari anatoa huduma za matibabu kuboresha afya za Wanasagamoyo.
      5 × 2
  2.  Majoka na Daktari
    1. Kuendeleza mgogoro wa kinafsia✓. Majoka anasema kuna kilio kikubwa ndani kwa ndani. (uk. 73)
    2. Kuchimuza✓ matukio ya awali; kwa mfano kuuawa kwa Jabali (uk. 73)
    3. Kudokeza hatari✓ iliyomngojea Majoka - mikono yangu imefungwa kwa minyororo (uk. 73)
      Majoka kusema yuko katika safari ya jongomeo
    4. Kuonyesha udhaifu✓ wa uongozi wa Sagamoyo.Majoka anamuuliza Daktari/ Babu kama ndiye rubani wa ombwe hilo. ( uk. 74)
    5. Kujenga sifa✓ za mhusika. Tunasawiriwa tamaa ya Husda inayomfanya kusaha kwenye ndoa ya mateso/ uchungu na furaha/ Majoka ni mwenye taasubi/anaishi na mke huyo
    6. Yaangazia usaliti✓ katika ndoa. Majoka anakiri kuwa anampenda Ashua; hampendi mkewe Husda.
    7. Kuonyesha nafasi ya mwanamke✓ katika jamii; Wanasawiriwa kama wasioweza kutegemewa. Majoka anasema hawashikiki.
    8. Kuonyesha ukosefu wa uwajibikaji wa uongozi✓. Majoka anasema hajashika usukani (uk. 80)
    9. Kuonyesha kuwa Wanasagamoyo wamezinduka. Majoka anasema wanaililia✓ damu yake ( uk.79)
    10. Kuonyesha kwamba Sagamoyo haipigi hatua kimaendeleo✓. ( uk. 81) Chombo kinakwenda kinyume.
    11. Kuonyesha swala la mgongano✓ kati ya utawala wa Babu na ule wa Majoka. Majoka anasema kwamba athari ya chombo cha Babu/kinatikisa chake ( cha Majoka) na kukifanya kutaka kuubadilisha mkondo.
    12. Kumtanabahisa/kumsuta✓ Majoka kuhusu uongozi wake, na kumwonyesha haja ya kubadilika. Babu anasema: Huoni kisima kimeingiwa paka na maji hayanyweki tena?

Swali la Insha 30

Tamthilia ya “Kigogo” ni kioo cha uhalisia wa maisha ya jamii nyingi za Kiafrika. Thibitisha.

  1. Uongozi mbaya- Majoka hajali haki za raia, wala kujali uhuru wa vyombo vya dola haheshimu katiba.
  2. Mauaji ya watu – watu wasio na hatia katika Sagamoyo wanuawa kwa mfano mpinzani wake Jabali, waandamanaji.
  3. Usaliti – Sagamoyo imesalitiwa na viongozi.Majoka anasaliti wananchi kwa kushughulikia mambo yake binafsi. Asiya anamsaliti mumewe ndoani kwa kushiriki uroda ili apate mradi wa kuoka keki.
  4. Ulipaji wa kisasi – Majoka anamtia nguvuni Ashua ili alipe kisasi kwa Sudi kwa kuwa alimuoa hurulaini ambaye Majoka alimpenda.
  5. Suala la migogoro – kundi la akina Tunu linazozana na watawala kwa kudai haki za Wanasagamoyo ziheshimiwe.
  6. Ubinafsi –utawala wa Majoka ni wa kibinafsi.wanafunga soko la Chapakazi kwa manufaa yao wenyewe.
  7. Ukoloni mamboleo – kuna kutegemea misaada kutoka nch za kigeni. Majoka anapokea mkopo kutoka mataifa ya nje ambao unatakiwa kulpwa kwa muda wa miaka mia moja.
  8. Athari za ulevi na mihadarati – sagamoyo imejaa vijana waraibu wa unywaji pombe haramu. Ngurumo na waraibu wenzake wanaonekana mangweni kwa mama pima. Wanafunzi wa Majoka Academy wanatumia dawa za kulevya ambazo huwageuza makabeji.
  9. Ufisadi – Ngurumo anadai kuwa watu kigogo wanapitia pale wakipewa vijisenti. Kenga anatoa ushauri mbaya kwa Majoka ili ajinufaishe.
  10. Matumizi mabaya ya viombo vya dola – Chopi na askarijela ni wakatili na wapyaro.
  11. Unyakuzi wa ardhi – Majoka ananyakua uwanja wa Chapakazi ili ajenge hoteli ya kifahari.
  12. Kuangamiza wapinzani – Jabali aliuawa na utawala wa Majoka .
  13. Tenga tawala – Majoka anagawanya wanasagamoyo ili awatawale kwa urahisi.
  14. Elimu duni – wanafunzi wanatumia dawa za kulevya na kuwa makabeji.
  15. Utawala wa kiimla – Majoka anatawala kwa kutumia mabavu.
  16. Ulevi – pale mangweni Ngurumo wanaathirika kwa ulevi.
  17. Matabaka- kuna vigogo wenye mali huku wale wengi wakiwa walalahoi wasio na kipato.
  18. Ukosefu wa uwajibikaji – njaa inatokana na kufungwa kwa soko la Chaakazi
  19. Ufujaji wa mali ya umma – Kenga anamrubuni Sudi kwa fedha nyingi.
  20. Uchafu - mandhari ya soko ni machafu na Sudi anasema kuwa wanasumbuliwa na aina nyingi ndwele .
  21. Uharibifu wa mazingira.
  22. Migomo na maandamano.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Maswali na Majibu ya Insha katika Tamthilia ya Kigogo.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest