Kiswahili Paper 2 Questions - Kapsabet Boys Post Mock 2023 Exams

Share via Whatsapp

MAAGIZO

 • .Karatasi hili lina maswali manne. (Ufahamu, ufupisho, lugha na Isimujamii)
 • Jibu maswali yote 


MASWALI

 

 1. FAHAMU: (ALAMA 15)
  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

  Tokea muundo mpya wa serikali ya ugatuzi uanze kutekelezwa miaka miwili iliyopita, kumeendelea kushuhudiwa matatizo mengi hali iliyopelekea kushuhudiwa kwa msururu wa migomo na maandamano ya raia.Fujo za karibuni kabisa ni zile zinazoshuhudiwa katika miji mikubwa za wachuuzi na wafanyibiashara wakipinga hatua za serikali za kaunti kuwatoza ushuru takribani kwa kila huduma na bidhaa ikiwemo wanyama,kuku na ndege.La kuhuzunisha zaidi katika baadhi ya majimbo imeripotiwa kuwa raia wamelazimishwa kulipa ushuru kwa kutaka tu kuona maiti za jamaa zao kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti!
  Wanasiasa wameonekana kuwa na wakati mgumu kutetea mfumo huu mpya wa ugatuzi huku baadhi wakisema kwamba matatizo yanayoshuhudiwa kwa sasa yametokana na ugeni wa mfumo huo.Wengine wameinyoshea kidole serikali ya kitaifa kwamba ndiyo inayosambaratisha muundo huu.Wengine wanahoji kuwa bado ni mapema na kwamba kunatajika muda mrefu ili kufaulu.
  Ni wazi kwamba kumekosekana nidhamu bora ya kusimamia maisha ya raia nchini Kenya.Matatizo yanayokumba raia kwa sasa ni dalili kuwa mfumo wa serikali ya ugatuzi umeongezea chumvi kwenye kidonda badala ya kutibu.Swali ni je,hadi lini nidhamu ya kusimamia raia itakuwa ni suala la majaribio na makosa?
  Hatua ya kuwarundikizia raia ushuru mkubwa ni kitendo cha unyonyaji na cha dhuluma kinachofaa kupingwa. La kufahamishwa hapa ni kwamba ushuru ndio njia kubwa ya kuzalisha mapato ya serikali zinazojifunga na mfumo wa kimagharibi wa kiuchumi wa kibepari ikiwemo Kenya.Asilimia 90 ya mapato ya serikali za kibepari huegemea ushuru. Kwa hivyo hatua ya serikali za kaunti katika kuwanyonya raia kwa kuwalipisha ushuru si ajabu bali ni thibitisho kuwa jamii ya Kenya inaongozwa na nidhamu ya kiuchumi ya ubepari mfumo wa unyonyaji na ukandamizaji.Ukweli unabakia kuwa ndani ya serikali za kibepari raia ndio hubebeshwa mzigo wa ushuru unaoishia matumboni mwa viongozi!
  Miito ya mabadiliko ya katika na ya miundo mipya ya kiutawala si lolote ila ni moja tu ya hatua za mfumo wa kibepari kujipa muda wa kuishi na kuziba aibu zake za kushindwa kusimimia maisha ya watu.Kufeli huku kwa mfumo huu kunashuhudiwa hadi kwenye nchi kubwa za kibepari kama Marekani na Uingereza hivyo nazo zimekumbwa tele na maandamano na fujo za raia wakilalamikia hali ngumu ya maisha.

  Maswali
  1. Yape makala haya anwani mwafaka. (alama 1)
  2. Eleza mtazamo wa wanasiasa kuhusu utepetevu wa mfumo huu. (alama 3)
  3. "Ugatuzi nchini Kenya ni mfumo wa kibepari" Thibitisha kauli hii kwa kurejelea makala (alama 3)
  4. Migomo ni zao la matatizo yaliyogatuliwa kutoka serikali kuu. Toa sababu nyingine zinazosababisha migomo katika serikali za ugatuzi (alama 4)
  5. Thibitisha jinsi mfumo wa ugatuzi umeongeza chumvi kwenye kidonda badala ya kutibu (alama2)
  6. Eleza maana ya maneno yafuatayo (alama 2)
   1. Ugatuzi ……………………………………………………………………………………….
   2. Kibepari…………………………………………………………………………………………
 2. MUHTASARI
  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali

  Katika siku za hvi karibuni ,kuwekuwa na malalamiko magazetini kuhusu tatizo la ajali za barabarani amabalo ni dhahiri kwa sasa limekuwa donda sugu.Janga hili kubwa si tiship tu kwa maisha na mali ya wakenya , bali pia kwa maendeleo ya uchumi wa taifa,hivyo linahitaji kutafutiwa ufumbuzi wa haraka .Ninaomba nitoe mapendekezo yangu kuhusu mikakati inayoweza kuchukulliwa ili kuepuka ama kukomesha matukio ya mara kwa mara ya ajali za barabarani.
  Ongezeko la matukio ya ajali za barabarani zinazosbabisha kukteketea kwa maisha ,kwanaza kabisa linatokana na uvunjaji wa sheria za usalama barabarni na ukosefu n auangalifu miongoni mwa baadhi ya madereva.Hata hivyo , abiria nao wanachangia kusababisha ajali hizo.Inasikitisha kuona kuwa baadhi ya abiria wanakubali kupakiwa kupita kiasi kwenye magari mithili ya mapakacha ya machungwa kama kwamaba wanalazimishwa kuyapanda kwa mtutu wa bunduki.Si ajabu vile vile kuona kuwa magari yanayopelekwa kwa mwendo wa kasi wa kupundukia, abiria wanakaa kimya kama kondoo wa kafara ama wanashangilia madereva hao.Ni ukweli usiopingika kuwa iwapo gari lililo katikati kasi kubwa litakumbwa na hitilafu ni vigumu kwa dereva kulimudu na kulidhibiti gari hilo.Litakuwa ni jambo la busara iwapo magari yote ya abiria yatafunguliwa vifaa vya kudhibiti kasi.Abiria na wananchi kwa jumla wana jukumu la kukemea na kuwakataza madereva wasiojali maisha ama kuwashtaki kwa vyombo vya dola.
  Aidha nipendekeza kuwa madereva wanaotiwa hatiani kwa makosa ya kuvunja sheria za usalama barabarani bila simile waadhibiwe vikali na ikabidi wapokonywe leseni zao.Licha ya hao ,inpasa halmasahauri inayohusika na utoajai wa leseni nchini,ihakikishe kuwa madereva wote wana lseseni halali kwa mujibu wa sheria , na kwamab siku zoe utaratibu wa kizitoa leseni unazingatiwa kwa dhati.Mathalani ,kabla ya kutolewa kwa leseni ihakikishwe kuwa kuna uthibitishso wa chuo cha dereva anapoomba leseni.Kwa utaratibu kama huu,hapana shaka kuwa vitendo vya kughushi leseni za bandia vitapungua na ajali zinazosababishishwa na madereva wasio na ujuzi hazitakuwepo kabisa.Mkakati mwingine ni kutoa mafunzo ya uhakika kwa madereva .Aidha vyuo hivyo vinavyotoa afunzo ya dereva viwe vinakaguliwa mara kwa mara na maofisa wa Baraza la Kitaifa la Usalama barabarani kwa lengo la kuhakisha kuwa mtaala rasmi wa mafunzo unatumiwa.
  Serikali, kwa upande wake, haina budi kutupia macho ukarabati wa barabara.Kwa hivi sasa,barabara ziko katikati hali ya kusikitisha.Ubovu wa barabara ,uadhaifu wa kingo za madaraja na ukosefu wa taa za kuongeza magarti kwenye makutano ya barabara, ni chanzo kinginecho cha ajali barabarani. Ni jukumu la Wizara ya Ujenzi kujenga utamaduni wa kukarabati miundo mbinu kwa kufanaya matengenezo ya mara kwa mara ya barabara. Chambillecho wahenga,usipoziba ufa utajenga ukuta.
  Hata ingawa hatua hizi ni njia madhubuti za kukabiliana na tattizzo la ajali za barabarani,itakuwa ndotyo kuzikomesha iwapo utekelezaji wa sheria za uslama barabarani utakuwa wa kutetereka .Sharti pawepo askari wa usalama barabarani ili kusaidia katika matumizi mazuri ya barabara,kuyakagua magari na leseni za usalama barabarani,
  Tatizo la ajali si jambo la kufumbia macho.Kinga ni bora kuliko tiba .Ninayo imani kuwa iwapo wananchi wataungana na serikali katika kuchukua hatua thabiti ili kupunguza ajali barabarani,maisha hayataendelea kuteketea ila yatokolewa.

  Maswali
  1. Ajali barabarani ni mwiba wa kujidunga.Thibitisha kwa kurejelea taarifa.
   (Maneno 40) (Alama 6)
   Jaribio (1 utiririko)
   Nakala safi
  2. Bainisha mambo muhimu yanayozungumziwa kwenye aya ya 3,4 na 5
   (maneno 80) (alama 7)
   Jaribio (1 utiririko)
   Nakala safi
 3. MATUMIZI YA LUGHA. (ALAMA 40)
  1. Taja sifa bainifu za sauti /e/ (alama 3)
  2. Eleza maumbo manne ya silabi na utoe mifano mwafaka (alama 2)
  3. Bainisha aina za nomino katika sentensi hii. (alama 3) Uhodari wa wanariadha wa Kenya unahitajika kote duniani.
  4. Tumia neno stahili katika sentensi kama (alama 2)
   1. Kitenzi kisaidizi
   2. Kitenzi kishirikishi
  5. Bainisha kishazi kitegemezi na huru katika sentensi hii. (alama 1)
   Wafanyikazi wane wataenda sokoni wakipewa ruhusa.
  6. Badilisha sentensi ifuatayo kuwa sentensi changamano. (alama 1)
   Alihudhuria sherehe hivyo ingawa hakualikwa.
  7. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi. (alama 4)
   Huyu kijana mkorofi atatusumbua tusipochukua tahadhari
  8. Andika sentensi hii katika usemi wa taarifa. (alama 2)
   “Tulienda kumtembelea mwalimu mkuu wetu juzi.” Mwanafunzi aliseme.
  9. Andika kwa ukubwa wingi. (alama 2)
   Paka huyu hatosheki kwa maziwa, amezoea panya.
  10. Taja na utoe mifano ya miundo mine katika ngeli ya U-ZI. (alama 2)
  11. Tunga sentensi yenye shamirisho kipozi, kitondo na shamirisho ala na kisha uzionyeshe aina hizo za shamirisho. (alama 3)
  12. Taja sifa mbili za kishazi kitegemezi. (alama 2)
  13. Tunga sentensi ukitumia vitenzi vifwatavyo katika kauli ya kufanyiza. (alama 2)
   1. La
   2. Fa
  14. Eleza dhana zifuatazo: (alama 3)
   1. Kizuiwa
   2. Mzizi
   3. Mofimu
  15. Fafanua majukumu mawili ya kiimbo. (alama 2)
  16. Eleza majukumu mawili ya parandesi. (alama 2)
  17. Tunga sentensi mbili tofauti kuonyesha matumizi ya kwa (alama 2)
  18. Taja vigezo viwili vya kuainisha viambishi. (alama 2)
 4. ISIMU JAMII (AL 10)
  1. Sajili ya wanahirimu ni gani? (alama 1)
  2. Taja na ueleze sifa nne mahsusi za lugha ya wanahirimu. (alama 4)
  3. Eleza mambo matano yanoyoathiri mtindo nafsi wa mtu katika matumizi ya lugha. (alama 5)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions - Kapsabet Boys Post Mock 2023 Exams.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?