Muhtasari wa Kigogo - Tamthilia ya Kigogo

Share via Whatsapp


Onyesho la Kwanza

Tendo la kwanza.

Ni katika karakana ya soko la Chapakazi,Sudi, Boza na Kombe wanafanya kazi ya uchongaji.Sudi amefungulia radio huku wakiendelea na kazi yao.Ashua anawaletea chai ya mkandaa na mahamri na kuondoka.

Habari inatolewa kwa wananchi wa Sagamoyo kuwa wana kipindi cha mwezi mzima kusheherekea uhuru wao, wawaku buke majagina wao waliopigania uhuru na kuwanasua kutoka utumwani, wimbo wa kizalendo unachezwa mara kwa mara.

Sudi anatofautiana na mpango wa kusheherekea uhuru kwa mwezi mzima; kwake majagina wanaosheherekewa hawakufanya lolote katika historia ya Sagamoyo.
Kuna uchafuzi wa mazingira, viongozi hawajawajibika kusafisha soko wanadai kodi na kitu juu pia vitisho kwa wanasagamoyo.

Wazo kuu.

Kuna wale ambao wanaunga viongozi mkono kwa sababu wanafumbwa kwa mambo yasiyo ya kimsingi.Aidha kuna wale ambao wamezinduka na kuhisi kuwa viongozi hawajawajibika. Sudi haoni umuhimu wa sherehe za uhuru kupewa maandalizi ya kifahali na kipindi cha mwezi mzima.

Tendo la pili.

Katika karakana sokoni,Kenga anawatembelea Sudi, Boza na Kombe.Ametumwa na Majoka kuchukua vinyago vya mashujaa.Ni msimu wa mashujaa Sagamoyo, Sudi anachonga kinyago cha shujaa wa kike ambaye kwake ni kiongozi halisi wa Sagamoyo.Shujaa huyo hakufanya lolote, bali analifanyak sasa katika jimbo la Sagamoyo.

Miradhi ya kuchonga vinyago inafadhiliwa kutoka nje na wananchi wanatakiwa kulipa baada ya mwaka mmoja.

Sudi anashawishiwa kuchonga kinyago cha Ngao ili maisha yake yabadilike na jina lake kushamiri; aidha apewe likizo ya mwezi mmoja ughaibuni.Sudi anakataa kuchonga kinyago, Kenga anawapa keki lakini Sudi hali kwa kuwa ni makombo.Kombe anazinduka kutokana na kauli hii, anamuunga mkono Sudi.Kenga anaondoka kisha Tunu anawasili huku akihema na kusema kuwa mzee Kenga anapanga njama ya kuhutubia wahuni.Wote wanaondoka.

Wazo kuu.

Maskini wanatumikizwa, wanadhalalishwa, kuletewa makombo na kukumbukwa katika kipindi fulani tu ili kufaidi viongozi wao.
Miradi isiyo muhimu inafadhiliwa na wananchi kupakia na jukumu la kulipa ufadhili huo kupitia kodi.Viongozi hushawishi wanyonge ili kuwatumikia.

Tendo la tatu

Ni katika nyumba ya Sudi barazani baada ya soko kufungwa.Tunu na Sudi wanafika kiwandani anapofanya kazi Siti, wafanyakazi wanagoma na vijana watano kuuliwa na wafanyakazi kuumia.

Kiini cha maandamano ni bei ya chakula Kupandishwa soko linapofungwa.
Sudi na Tunu wamejitolea kutetea haki na uhuru wa wanasagamoyo hata kama ni kwa pumzi zao za mwisho baada ya kufaulu.

Wazo kuu.

Kuna maandamano na migomo,walimu na wauguzi wanagoma.Migomo hiyo inatokana na kutowajibika kwa viongozi ambao wana nia ya kujifaidi.



Onyesho la pili

Tendo la kwanza.

Ni ofisini mwa Mzee Majoka, anaongea kwa simu Chopi anapoingia.Ashua anafika kumwona Majoka,anataka kumkumbatia lakini Ashua anakataa.Majoka anakasirika Ashua anapomwita mzee na kufurahi anapomwita Ngao, jina lake la ujana.

Ashua amefika kuomba msaada lakini Majoka anamtaka kimapenzi.Anajaribu kumbusu lakini Ashua anakwepa.Majoka anamshawishi, anajisifu na kujilinganisha na Lyonga wa uswahilini na Samsoni Myaudi.

Majoka anasema kuwa soko limefungwa kwa sababu ya uchafu, anatenga eneo hilo ili kujenga hoteli ya kifahari.Wanasagamoyo wanalitegemea soko hilo kula, kuvaa na kuendesha maisha yao.

Ashua anakataa kazi ya ualimu anayopewa Majoka and Mahoka academy, angekuwa mwalimu mkuu katika shule mojawapo ya kifahari.

Wazo kuu.

Viongozi hunyanyasa wachochole ili kujifaidi, Majoka anafunga soko na kunyakua eneo hilo kujijengea hoteli ya kifahari.Anataka kutumia mali na mamlaka yake kumteka Ashua kimapenzi.

Tendo la pili.

Husda anamkabili Ashua kwa hasira, anamtusi kuwa kidudumtu, shetani wa udaku na mwenye kuwinda wanaume wa watu.Wanaangushana na Ashua kuzabwa makofi.
Sauti ya kenga inamjia Majoka akilini kuwa soko lifungwe ili kulipiza kisasi kwa Sudi na Ashua, kisha Ashua aitwe ofisini na Husda wakabiliane.
Mwango na Chopi wanawachukua Ashua na Husda ndani, agizo linatolewa Husda atolewe ndani baada ya nusu saa.

Wazo kuu.

Wanyonge hutafutwa kwa lolote lile na kunyanyaswa.Viongozi hutumia mamlaka yao hata kupanga njama kuwateka wanyonge,Ashua kutiwa ndani ni njama iliyopangwa.



Onyesho la tatu

Tendo la kwanza.

Ni ofisini mwa mzee Majoka, wana mazungumzo ya faragha na mshauri wake Kenga.

Njama yao ya kumtia Ashua ndani inatimia kisha wanamtarajia Sudi, achonge kinyago cha shujaa ndiposa Ashua aachiliwe.

Kenga anamwonyesha Majoka picha za waandamanaji gazetini.Kuna habari kuwa Tunu aliongoza maandamano kisha kuwahutubia wanahabari kuwa:

  • pesa za kusafisha soko zimefujwa,
  • soko lilifungwa badala ya kusafishwa,
  • haki za wauzaji zimekiukwa,
  • hawatalegeza msimamo wao hadi soko lifunguliwe.

Majoka anapanga kumwadhibu Tunu.

Maoni ya wengi gazetini ni kuwa,Tunu apigigwe kura za kuongoza Sagamoyo.Kenga anamshauri Majoka kutangaza kuwa maandamano hayo ni haramu kisha Polisi watumie nguvu, Majoka anapinga wazo hilo kwa kuwa;

maandamano yatatia doa sherehe za uhuru,
Tunu atazidi kupata umaarufu.

Tunu ana mpango wa kuleta wachunguzi kutoka nje kuangalia ajali ya Jabali.Majoka anasema wazuie uchunguzi huo naye Kenga anakiri kuwa itawagharimu kwa kuwa watatumia mbinu tofauti.

Majoka anaamua kuwashughulikia Tunu na Sudi.
Kuhusu mishahara ya wauguzi na waalimu, wanaafikiana waongezwe kwa asilimia kodogo kisha kodi ipandishwe.

Wazo kuu.

Viongozi wanatumia mbinu tofauti kutawala;

• kupanga njama,
• kuadhibu waandamanaji,
• kutojali maslahi ya wanyonge.

Hata hivyo, wananchi wamezinduka na nia yao ni kubadili uongozi usiofaa.

Tendo la pili.

Majoka akiendelea kusoma gazeti,Kenga anarejea kwa vishindo kuwa kuna habari zinazoenea katika mitandao ya kijamii na kupeperushwa katika runinga ya mzalendo.
Kenga anashauri kuwa, runinga ya mzalendo ichukuliwe hatua, maandamano yanaonekana kuharibu sherehe za uhuru.Majoka anamlaumu Chopi kwa polisi kutowatawanya waandamanaji.

Tunu na Sudi wanafika, wanaagizwa kuingia na Majoka anatoa bastola, na kuwaambia Kenga wamzuie na askari.

Wazo kuu.

Habari za maandamano zinazidi kuenea na Majoka ana wasiwasi kutimuliwa mamlakani kwa kuwa Tunu anazidi kupata imaarufu.
Viongozi hutumia vyombo vya dora visivyo, Majoka anapanga vituo vya habari vifungwe na kibakie kituo kimoja tu Sagamoyo.

Tendo la tatu.

Ni ofisini mwa mzee Majoka,Tunu na Sudi wanaingia.Majoka anataka kusema na kila mmoja lakini wanakataa kwa kuwa na nia moja.
Sudi anaarifiwa kuwa Ashua mkewe yuko ndani kwa kuleta fujo katika ofisi ya kiserikali.

Majoma anamshawishi Tunu kuwa amampangia jambo la kifahari, kumwoza Ngao Junior atakaporejea kutoka ng`ambo.

Tunu hakubaliani ma kauli hii, anamkabili Majoka na kumwambia ukweli kuwa wao ni wahuni na wauaji.Tunu anatishiwa kutiwa ndani.Tunu anafichua ukweli, Majoka walipie kila tone la damu waliyomwaga Sagamoyo

Majoka anagharamia masomo ya Tunu hadi ng`ambo; ni haki yake kuwa babake alifia Majoka company

Wazo kuu.

Viongozi hushawishi wapinzani kwa ahadi ili wawaunge mkono, hata hivyo wanamapinduzi wanashikilia msimamo wao.

Tendo la nne.

Ni katika chumba cha wafungwa.Sudi amefika kumwona Ashua ambaye anadai kuwa ni kosa lake Sudi kutiwa ndani.Ashua anaomba talaka.

Ashua hataki tena mapenzi ya kimaskini, amechoka na kuchukua mkondo tofauti.Kwake anahisi kuna kitu baina ya Tunu na Sudi.

Wazo kuu.

Asasi ya ndoa inaonekana kuwa na changamoto.Kuna kutoaminiana katika ndoa,Ashua anashuku uhusiano baina ya Tunu na Sudi.



Onyesho la nne.

Tendo la kwanza.

Ni nyumbani kwa kina Tunu, Bi.Hashima anapepeta mchele huku akiimba.Siti anafika na habari kuwa wahame Sagamoyo sio kwao.

Hali Sagamoyo inaonekana kubadilika ardhi inateketea na mito na maziwa yanakauka. Kigogo amefungulia biashara ya ukataji miti.

Tunu anafika akihema baada ya kuota kuwa Mzee Marara anamfukuza akitaka mkufu wake wa dhahabu.

Tunu amaumizwa mfupa wa muundi,uvumi unaenea kuwa Sudi na Ashua ndio wanawinda roho ya Tunu.

Tunu anataka kukutana na Majoka na watu wake.Hashima anaona hatari Tunu akienda kukutana nao.

Wazo kuu.

Hali Sagamoyo inazidi kubadilika, kiangazi kimesababishwa na kigogo kufungulia ukataji miti, viongozi hawajali maslahi ya wananchi.
Viongozi hueneza uvumi ili kutawanya wananchi, hata hivyo; vijana wamejitolea kujenga jamii mpya licha ya vikwazo vinavyowakumba.

Tendo la pili.

Tunu na Sudi wanafika Mangweni ambapo shughuli za ulevi zimeshika kani, wanaletewa kileo lakini wanakataa.

Ngurumo anaonekana kusheherekea uhuru, kwa mujibu wa Sudi,mashujaa Sagamoyo ni waliouliwa msituni wakipigana, waliohangaisha wakoloni na kuwatimua.

Tunu amefika Mangweni kuwaalika katika mkutano mkubwa utakaofanyika katika soko la Chapakazi siku ya maadhimisho ya uhuru.

Kulingana na Ngurumo, mkutano huo si muhimu, cha muhimu kwake ni kuendelea kulewa kwa mamapima

Mtu mmoja anagaragara kwa sababu yu hoi, wengine walizikwa kwa sababu ya pombe na wengine kuwa vipofu.

Mtu huyo anamshawishi Tunu asipoteze bahati yake ya kuolewa na Ngao Junior.

Wazo kuu.

Watu wanapumbazwa hasa walevi kwa pombe na kuendelea kutetea viongozi wasiofaa.
Tunu na Sudi wamejitolea kutetea wanyonge Sagamoyo, wameandaa mkutano kuzindua umma.



Onyesho la tano.

Tendo la kwanza.

Ni katika hoteli ya Majoka and Majoka modern resort, Husda anafika kutoka kuogelea.Kenga naye anafika na habari kuwa mipango haikwenda walivyopanga,Tunu hakuvunjwa mguu.Chopi anapangiwa kwenda safari kwa kutotekeleza njama hiyo.

Sokoni, taka zote zimeondolewa, vibanda vimeng`olewa, vifaa vya ujenzi vimewasili kutoka bandarini na kuna ulinzi mkali.

Chopi anafika na habari mbaya kuwa Ngurumo amenyongwa na chatu akitoka Mangweni.Majoka anaagiza Ngurumo azikwe kabla ya jua kutua.

Ushauri wa Majoka ni kuwa chatu mmoja atolewe kafara, na baada ya watu kuandanana waachwe katika hali ya taharuki.

Chopi tena anarejea na habari kuwa Ngao Junior kapatikana katika uwanja wa ndege akiwa na sumu ya nyoka, Majoka anazirai.

Wazo kuu.

Viongozi hupanga njama za kuwaangamiza wapinzani wao.

Viongozi wanaishi maisha ya kifahari huku maskini wakihangaika.

Viongozi hawajali hata vifo vya wananchi vikitokea.

Tendo la pili.

Ni ndani ya ambulensi, Majoka hataki kufungua macho kuliona ziwa la damu.Majoka anasema yuaelekea jongomeo, kuwa amefungwa minyororo.Anataka safari isitishwe kwa kuwa haina stara.

Majoka anamfananisha Husda kama mke anayeishi ndani ya ngozi ya kondoo (kuwa Husda ni mnafiki). Husda anapenda mali ya Majoka na alilazimishwa kumwoa lakini moyo wake unampenda Ashua.

Daktari anamjuza Husda kuhusu kifo cha Ngao Junior,anazirai.

Wazo kuu.

Asasi ya ndoa imesawiriwa kuwa na changamoto; Husda hakumpenda Majoka ila aliolewa naye kwa sababu ya pesa.

Ili kuokoa asasi ya ndoa, wanaume wanapaswa kujidadisi, wawe na heshima na waseme na wake zao.Wake nao wajirudi ili ndoa zidumu.



Onyesho la sita.

Tendo la kwanza.

Ni katika chumba cha wagonjwa, hali ya Majoka inaonekana kurejea.Anahukumiwa kuwa msaliti kwa wanasagamoyo na mashtaka mengine mengi.

Mayowe yanasikika na Majoka anadai kuwa hivyo ni vilio, wanalilia damu yake kisha Majoka anazungumza na babu ndotoni.

Majoka anawachukia marubani kwa kuwa waongo ilihali yeye pia ni rubani(kiongozi), hang`amui mambo kwa vile hajapambua ngozi yame ya zamani.Safari haijaanza au pengine chombo kinaenda kinyume badala ya mbele.

Safari ya babu na Majoka inatofautiana, Majoka anashauriwa asalimu amri, achague sauti ya moyo na babu yake.

Babu anamshauri Majoka afungue masikio, macho na moyo wake kwa kuwa maisha yana ncha mbili.

Kulingana na babu, kuna misimu ya fanaka na ya kiangazi, kadhia na kuishi kwa kutojali ni muhali. Mkwea ngazi huteremka hivyo mtu achague kutenda mema, kwa maana wema hauozi. Mtu akiishi kwa wema, atajiandikia tarijama njema huku ahera.

Wazo kuu.

Maovu yana mwisho na kila aliye juu hatakaa juu milele.Wema ni muhimu katika maisha ya binadamu.



Onyesho la saba.

Tendo la kwanza.

Ni katima uwanja wa ikulu ya Majoka palipoandaliwa sherehe.Ni saa nne na watu kumi tu ndio wamefika, wengine wako sokoni.

Sauti inasikika kwa mbali watu wakimsifu Tunu.Majoka anaelekea ilipo sauti, Kenga na umati wanawafuata.

Wazo kuu.

Wananchi wana nguvu zaidi kuliko viongozi .Wananchi wana mchango mkubwa kujikomboa kutokana na shida wanazozipitia zinazoletwa na uongozi mbaya.
Ili kujenga jamii mpya, wanachi hawana budi kuzinduka na kuleta mapinduzi.

Tendo la pili.

Ni katika lango la soko la Chapakazi, Majoka anawahutubia watu na kuwaita wajinga.Kenga anamnyanganya kinazasauti.
Tunu anabebwa juu juu na watu, anawahutubia huku wakimpigia makofi.

Amejitolea kutetea haki za wanasagamoyo ili;

  • wapate maana halisi ya uhuru,
  • watendewe haki,
  • soko lifunguliwe na kujengwa upya,
  • huduma muhimu ziletwe karibu kama vile; hospitali, barabara, maji, vyoo, nguvu za umeme, elimu, ajira kwa vijana na kadhalika.

Tunu anahimiza wanasagamoyo wachague viongozi wanaolinda haki za wanyonge na kuwajibika.

Majoka kwa hasira anaamuru watu wapigwe risasi, Kingi anapokataa kwa kuwa ni kinyume cha katiba kufyatua risasi anafutwa. Kenga anasalimu amri, anajiunga na umati.
Kingi na Kenga wanajiunga na umati, wanashangiliwa, walinzi nao wanajiuzuru.

Majoka kwa hasira anadai kuwa hata asipopigigwa hata kura moja atashinda.
Tunu anasindikizwa jukwaani, mamapima anafika kuomba msamaha.Anajuta sana kwa kuwalaghai walevi na kukiri kuwa aliwapunja kwa kuongozwa na tamaa ya pesa, sasa wamemgeuka.

Sudi anafika na kinyago, anasema kuhusu maana ya uhuru: shujaa ni mmoja tu Sagamoyo, ambaye ni Tunu.

Wazo kuu.

Kila kilicho na mwanzo kina mwisho, uongozi wa Majoka unafikia nwisho.Juhudi za wanamapinduzi zimezaa matunda.Maana ya uhuru sasa imepatikana na wananchi wanatarajia mengi mema.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Muhtasari wa Kigogo - Tamthilia ya Kigogo.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest