Maswali na Majibu ya Insha katika Tumbo Lisiloshiba

Share via Whatsapp

Tumbo Lisiloshiba Insha Questions and Answers

Maswali ya Insha

Haya ni maswali ambayo hutoa kauli inayohitaji kujibiwa kwa kirefu na kwa kina. Swali linaweza kuwa la jumla yaani linalohusu Hadithi nzima. Pia, swali laweza kulenga sehemu ya kazi husika katika nyanja na maudhui, wahusika na hulka zao, mafunzo na fani. Maswali haya huhitaji zaidi uwezo wa kukumbuka wa mtu, kupanga hoja na kuelezea msimamo au maoni yake kuhusiana nayo. Mtahiniwa anahitajika kutoa hoja na kuziteteta kwa mifano dhabiti. Mtahiniwa asitumie vistari vistari, afafanue hoja kikamilifu akiandamisha mifano mingi kutoka kwa Hadithi.

Swali la Insha 1

  1. Eleza namna maudhui ya ndoa yalivyosawiriwa katika hadithi ya Masharti ya Kisasa (alama 13)
  2. Kwa kurejelea hadithi ya Shibe inatumaliza,eleza namna maudhui ya ufisadi yanavyojitokeza (alama 7)

Eleza namna maudhui ya ndoa yalivyosawiriwa katika hadithi ya Masharti ya Kisasa (alama 13)

  • Mwanaume humposa wanamke. Dadi alienda nyumbani kwa Kidawa kumposa
  • Mwanamke ndiye huamua wakati wa kuolewa na nani wa kumwoa. Kidawa alimchagua Dadi baada ya muda refu
  • Ndoa huandamana na masharti. Dadi alipewa masharti na Kidawa ili akubali kuolewa naye.
  • Wanandoa hufanya kazi pamoja ili kukithi mahitaji ya nyumbani. Dadi anachunza samaki na kidawa ni metroni
  • Wanaume hawafurahi wake wao wanapotangamana na wanaume wengine. Kidawa anaposimama kuongea na wanaume,Dadi anadhika sana.
  • Wanandoa husaidia kazi za nyumbani, Dadi anasaidia kidawa kazi za nyumbani kama vile kuosha vyombo na kufagia.
  • Wanandoa wanapanga uzazi,Dadi na Kidawa wanapanga kuwa na mtoto mmoja pekee
  • Mwanamke anaajiriwa. Kidawa aliajiriwa shuleni kama metroni.
  • Mwanamke anajinunulia nguo na fashoni nyingine. Kidawa ananunua viatu na kanzu anayaovalia kwenda kazini.
  • Ndoa imekosa uaminifu. Dadi anashuku kuwa Kidawa ana mapenzi na mwalimu mkuu.
  • Kiwango cha elimu si kikwazo katika ndoa. Kidawa anaolewa na Dadi licha ya kuwa ana kisomo cha juu kuliko Dadi.
  • Mwanamke amekengeuka. Kidawa anapenda fashoni
  • Wote wawili. Mwanamke na mwanaume wanachangizana nyumbani
  • Kuna makubaliano ya kufanya mambo kwa pamoja (13x1=13)

Kwa kurejelea hadithi ya Shibe inatumaliza,eleza namna maudhui ya ufisadi yanavyojitokeza (alama 7)

  • Mzee Mambo hafanyi kazi wizarani ilhali analipwa mshahara mkubwa kuliko Sasa na Mbura wanaofanya kazi wizarani
  • Mambo anatumia runinga ya taifa inayofaa kuufahamisha umma masuala yataifa lao kwa maslahi yake. Anaitumia kupeperusha sherehe inauofahamika nyumbani kwao.
  • Mambo anaifilisi serikali kwa kutumia pesa za serikali kugharamia sherehe zake binafsi. DJ na wenzake wanalipwa mabilioni ya pesa za serikali kwa kusimamia sherehe hii.
  • DJ anaipunja serikali kwa kutumia mtaji wa bohari kuu ya dawa za serikali kufungua duka lake la dawa.
  • Dj anaifilisi serikali kwa kupokea huduma za maji,umeme na matibabu bure ilhali wananchi maskini wanazilipia.
  • Wafanyakazi wa umma wanaibia serikali saa za kazi. Sasa na Mbura wanahudhuria shere zilizofanyika kwa Mambo siku nzima ilhali walipaswa kuwa kazini.
  • Mzee Mambo anatumia magari ya serikali kwa maslahi yake binafsi. Kwa mfano, anayatumia kusomba maji, chakula, kuwaleta jamaa wa Mambo shereheni na mapambo. (7x1=7)

Swali la Insha 2

Ukirejelea hadithi zifuatazo, eleza jinsi maudhui ya mapenzi na asasi ya ndoa yanavyojitokeza.   (alama 20)

  1. Mapenzi ya kifaurongo
  2. Masharti ya kisasa
  3. Ndoto ya Mashaka
  4. Mtihani wa maisha

Mapenzi ya kifaurongo

  • Ndoa iliyotarajiwa ya Dennis na Penina ilitawaliwa na unafiki. Penina anamjia Dennis na wazo la kuwa wapenzi bila kuzingatia hali duni ya familia yake. Dennis anapokosa ajira anamfukuza
  • Inatawaliwa na kuhimiliana
  • Imetawaliwa na kukata tamaa - Penina anakata tamaa baada ya Dennis kukosa kazi
  • Imezingirwa na utabaka wa kiasili
  • Mapenzi hukua, huugua na hufa 5 x 1 = 5

Masharti ya kisasa

  • Ndoa ya Dadi na Kidawa
  • Ndoa inayodhibitiwa na masharti
  • Ndoa ya kugawana majukumu
  • Ndoa ya kupanga uzazi
  • Ndoa inayoruhusu mwanamke kufanya kazi. Kidawa anafanya kazi ya umetroni usiku na kuuza bidhaa mtaani
  • Baadhi ya watu huingilia ndoa za wenzao kama njia ya kuona mapenzi yamevunjika baina ya wanandoa husika 5 x 1 = 5

Mtihani wa maisha

  • wazazi wa Samueli ni wenye mapenzi wanaonyesha mapenzi kwa mtoto huyu wao kwa kumpeleka shuleni akajipatie elimu
  • Samuel anaonyesha mapenzi kwa Nina. Kwa muda amekuwa mpenziwe
  • Nina anaamini kuwa mwanaume huyu ni bingwa kutokana na kudanganywa alikodanganywa na mwanaume huyu
  • mamake Samueli ana mapenzi ya dhati kwake, baada ya Samuel kujaribu kujitoa uhai mamake anamsihi waende nyumbani “Twende zetu nyumbani mwanangu.”  zozote 4 x 1 = 4

Ndoto ya Mashaka

  • Kuna ndoa ya Mashaka na Waridi
  • Kuna ndoa ya mtumwa na mumewe mzee Rubeya
  • Tatizo la kwanza ni ndoa ya kulazimishwa. Mashaka na Waridi walitoka kwenye matabaka mawili tofauti
  • Waridi - tabaka la kitajiri
  • Mashaka - tabaka la maskini
  • Kuna kutohusisha wanawake katika ndoa. Mamake Waridi hakuhusishwa katika harusi
  • Ndoa inakumbwa na tatizo la malazi bora - upendo, kujikubali, ukosefu wa taasubi ya kiume
  • Kuna changamoto zinazojitokeza baada ya kifo cha mmoja. Mashaka anawachwa yatima
  • Kuna utengano katika ndoa. Waridi anatengana na mumewe kutokana na hali ngumu ya kiuchumi

Swali la Insha 3

  1. Eleza ufaafu wa anwani mapenzi ya kifuaurongo kwa kurejelea mhusika Penina. Al.10
  2. Eleza nafasi ya elimu katika maisha ya wanajamii ukirejelea hadithi: Mtihani wa maisha.

Eleza ufaafu wa anwani mapenzi ya kifuaurongo kwa kurejelea mhusika Penina. Al.10

Kifaurongo ni mmea wenye sifa ya kujifisha mara unapoguswa. Mwandishi akejeli mahusiano yaliyojengwa katika msingi wa unafiki.

  • Penina anajifanya kumjali Dennis katika hali yake ya kunywa uji na kuonyesha huzuni. Anamtia Dennis mshawasha wa mapenzi ila si mapenzi kamili.
  • Msimulizi anadai wavulana wengi wameangamia katika utandabui wa mapenzi baada ya kufanyiwa makuruhu na wasichana wenye tabia ya kifaurongo.
  • Penina anadai atakuwa na Dennis kwa mazuri na mabaya lakini alimwacha alipokosa ajira.
  • Penina asema kuwa hafanyi mzaha na kuwa hawezi kumchagua mpenzi kwa msingi wowote kama si mapenzi. Mwishowe alivunja ndoa yake kwa sababu Dennis alikuwa fukara. Hii ni tabia ya kifaurongo.
  • Penina hataki kuitwa mpenzi wa Dennis na amtaka atafute msichana wa kufu yake akidai mgomba changaraweni haupandwi ukamea.
  • Penina amfukuza Dennis nyumbani alipokosa kazi ilhali alikuwa ameapa hangemsaliti kwa vyovyote vile. Hoja 5 x 2 = 10

Eleza nafasi ya elimu katika maisha ya wanajamii ukirejelea hadithi: Mtihani wa maisha.

  • Wanafunzi wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne ili kubaini hatima yao. Samueli awaza kuwa matokeao ya mthihani yangekuwa daraja ya ufanisi.
  • Elimu ina daraja/viwango – Samueli anatarajia kuingia chuo kikuu anapokamilisha kidato cha nne.
  • Katika masomo kuna kufeli.
  • Wanafunzi wanahofia matokeo ya mtihani wa kidato cha nne k.m Samueli.
  • Wanafunzi wanaojiamini kupindukia huathiriwa kisaikolojia wanapofeli.
  • Wanakunzi lazima watimize matakwa Fulani kabla ya kupatiwa matokeo yao.
  • Wanafunzi wengine wanaonea aibu matokeo yao.
  • Jinsia ya kike inapiku jinsia ya kiume masomoni k.m Dada zake Samueli.
  • Jinsia ya kike inabaguliwa masomoni. Babake Samueli ameweka matumaini yake kwa Samueli.
  • Watoto wanatarajiwa kupita mtihani wanusuru familia zao.
  • Wanafunzi wanaichukulia elimul na masomo kwa mzaha na kejeli.
  • Samueli aliona shule kama jela. 10 x 1 = 10

Swali la Insha 4

Safari ya elimu ni kama ua la waridi ambalo licha ya upendezaji wake, huzingirwa na miiba. Jadili adha za safari hii kwa hoja tano tano kutoka kwa kila mojawapo wa hadithi fupi zifuatazo: Mapenzi ya Kifaurongo, Mame Bakari, Mwalimu Mstaafu na Mtihani wa Maisha.

Tanbihi: swali hili linamhitaji mtahiniwa kuonyesha changamoto zinazoikumba elimu.

Mapenzi ya Kifaurongo

  • Ugumu wa kuelewa mambo shuleni – Dennis Machora na wenzake wanapata kugumiwa na mambo wanayofunzwa katika mhadahara chuoni. Kauli za Daktari Mabonga hazieleweki upesi.
  • Utabaka shuleni – Dennis mwenye jadi ya kimaskini anatatizwa na maisha chuoni anakojipata akitagusana na wenzake kutoka familia za kitajiri.
  • Kejeli za walimu – Daktari Mabonga anawajekeli wanafunzi wake kwenye mhadhara kila wanapomwuliza maswali.
  • Kuchekwa na wanafunzi wengine – Wanafunzi wanamcheka sana Dennis anapomwomba Daktari Mabonga kutumia lugha nyepesi katika mhadhara.
  • Kutamauka shuleni – Dennis anakatizwa tamaa na masomo anapoyaona kama madubwana ambayo hakujua yalitoka wapi.
  • Utashi /Umaskini huwakumba baadhi ya wanafunzi – Dennis anajipata na uhitaji wa vitu muhimu vikiwemo malazi bora, chakula n.k. Analazimika kulalia shuka zilizozeeka na kuchanikachanika na pia kunywa uji anapokosa chakula.
  • Upweke/Ubaguzi shuleni – Wanafunzi wa familia za kitajiri huona haya hujinasibisha na wenzao wasio na chochote. Dennis anajipata katika upweke kutokana na hili.
  • Anasa/ Mapenzi shuleni – Wanafunzi katika Chuo cha Kivukoni wanatumbukia kwenye anasa na masuala ya mapenzi , Dennis anawaona wenzake wakitembea huku wameshikana wawili wawili.
  • Kukosa kazi baada ya kusoma – Dennis anatafuta kazi bila ya mafanikio licha ya kuhitimu na shahada ya uanahabari kutoka kutoka chuoni.

Mame Bakari

  • Mimba za mapema kwa wasichana – Sara anajipata na ujauzito unaomtatiza kimawazo akiwa mwanafunzi.
  • Kubakwa kwa wanafunzi wa kike – Sara anabakwa na janadume asilolijua majira ya saa tatu unusu akitoka ‘twisheni’.
  • Kutengwa kwa wanafunzi wajawazito – Sara anawazia kutengwa na watu wote wa kando na wa karibu.
  • Wanafunzi kukosa wa kuwasikiliza wanapopatwa na balaaa mishani - Sara anawaza jinsi ambavyo hakuna mtu ambaye angemwelewa baada ya kubakwa.
  • Kufukuzwa shuleni kwa wasichana wajawazito/ kukatiziwa masomo – Sara anawazia jinsi ambavyo mwalimu mkuu angemfukuza kwa kusema shule ni ya wanafunzi sio wamama.
  • Msongo wa mawazo/ Shinikizo za akilini – Sara anajiwa na wazo la kujitoa uhai, hata hivyo nalikomesha wazo hilo.
  • Uavyaji mimba – Wanafunzi wa kike huweza kulazimika kuavya mimba ili wafiche hali zao. Wazo hili liliwahi kumjia Sara na akalitupilia mbali.
  • Kuaibishwa – Sara anawazia ambavyo mwalimu mkuu angemwita mama hadharani.

Mwalimu Mstaafu

  • Ubaguanaji kwa misingi wa wepesi wa kupata mambo darasani – Jairo alibaguliwa katika sherehe ya kustaafau kwa mwalimu Mosi kwa kuwa hakuwa hodari masomoni hivyo hakutajirika baada ya shule.
  • Dhana potovu ya baadhi ya wanafunzi – Jairo alikuwa na dhana ya kwamba mwalimu Mosi kwa kuendelea kumpa matumaini shuleni alikuwa anamharibia wakati.
  • Mtazamo hasi dhidi ya masomo – Jairo hakupenda masomo. Kwake waliosoma na kufanikiwa ni wakora.
  • Baadhi ya wanafunzi huwa na uwezo wa chini wa kuelewa mambo darasani – Jairo alipata sufuri ambazo mwalimu Mosi alimpa matumaini kwamba zingepisha mia mia.
  • Walimu kupata lawama kutokana na upungufu wa wanafunzi – Jairo anamlaumu Mwalimu Mosi kwa mapungufu yake shuleni.
  • Baadhi ya wanafunzi huzipuuza nasaha za walimu – Jairo alipuuza kabisa ushauri alioupata kutoka kwa Mwalimu Mosi kuhusu kuepuka ufuska, ulevi n.k.

Mtihani wa Maisha

  • Wasi wasi utokanao na matokeo ya mtihani – Samueli anajipata moyo ukimtuta anapokwenda kuyapokea matokeo ya mtihani wake wa kidato cha nne.
  • Walimu kuwadunisha wanafunzi – Samueli anasema vile ambavyo Mwalimu mkuu hakuwahi kumwamini.
  • Dharau kutoka kwa walimu – Mwalimu mkuu anamwonyesha dharau Samueli anapoingia ofisini kuyapokea matokeo yake. Anamtupia matokeo yake badala ya kumpa kwa njia nzuri.
  • Wanafunzi kupumbazwa na sifa wanazopaliwa na wenzao – Samueli alipokuwa akisoma, alipumbazika na umaarufu kutoka kwa wanafunzi wengine akasahau kutia bidi. Wenzake walimtambua kama ‘rasta’ shuleni.
  • Kuvunjwa moyo na matokeo duni ya mtihani – Samueli anavunjika moyo anapopata matokeo duni ya mtihani.
  • Mapenzi ya mapema – Samueli anaingilia uhusiano wa kimapenzi na msichana kwa jina Nina.
  • Udanganyifu wa wanafunzi kwa wazazi wao – Samueli anamdanganya babake kuwa hakupata matokeo ya mtihani kwa kuwa hakukamilisha kulipa karo.
  • Baadhi ya wanafunzi huwakosea heshima walimu- Samueli anamrejelea mwalimu mkuu kama ‘hambe’.
  • Wanafunzi kwenda mbali kupata elimu – Samueli alilazimika kusomea shule iliyokuwa mbali na nyumbani.
  • Kusalitika kwa wazazi – Wazazi wa Samueli wanahisi kusalitika baada ya mtoto wao mvulana, waliyemtegemea sana kufeli mtihani wa kidato cha nne.
  • Elimu ya msichana kutodhaminiwa sana – Babake Samueli aliona fahari kumwona mtoto wa kiume akifanikiwa, licha ya kuwa binti zake wawili Bilha na Mwajuma walifaulu katika mtihani ya sekondari na walikuwa vyuoni.

Tanbihi: Mwanafunzi anaweza kupendekeza hoja nje ya zilizotolewa kwenye mwongozo huu. Hivyo, mtahini atathmini hoja za mwanafunzi.

Hoja tano kutoka kwa kila hadithi ( 5 × 4 = 20)

Swali la Insha 5

``Wahusika katika hadithi shibe inatumaliza wanatumia uhuru wao vibaya.’’ Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano.  alama 20

  • Mzee mambo anatumia uhuru wa cheo chake serikalini vibaya kwa kupokea misharaha kutoka wizara mbalimbali ilhali hafanyi kazi yoyote.
  • Sasa na mbura wanatumia uhuru wao vibaya kwa kupanga na kupangilia wapi kwa kudoea badala ya kushiriki katika shughuli ya ujenzi wa jamii.
  • Wananchi wa taifa la Mzee Mambo wanatumia uhuru wao vibaya kwa kuzingatia kirenda kazini bila kujali kama wanfanya kazi yoyote. Muhimu si kwenda/ kazini ila kufanya kazi.
  • Mzee mambo anatumia uhuru wake vibaya kwa kutumia mali na wakati wa taifa kuandaa sehere zisizo na msingi wowote. Anaandaa sherehe kubwa kwa madai ya kusheherekea kuingizwa kwa mtoto wake ``nasari’’.
  • Mambo anatumia magari ya serikali kuhudumu katika sherehe yake.
  • Walaji katika sherehe ya kuingizwa kwa mtoto wa kwanza wa Mzee mambo nasari wanatumia uhuru wao wa kula vibaya kwa vile hawachunguzi kile wanachokula
  • Vyombo vya habari vinatumia uhuru wao vibaya kwa kupeperusha sherehe ya kibinafsi moja kwa moja badala ya kumulika mambo yanayoathiri taifa.
  • Dj na wengine wenye nafasi katika taifa wanatumia uhuru kupokea mabilioni ya pesa za serikali kutumbuiza katika sherehe za mtu binafsi.
  • DJ na wenzake wanatumia uhuru wao kupata huduma za maji, umame, matibabu miongoni mwa huduma nyingine bila malipo huku wananchi wakalazimika kulipia huduma hizi kwa dhiki na ufukara.
  • Sasa na mbura wanatumia uhuru wao wa kula kila kitu kibaya na kizuri, wanachokijua na wasichokijua,vyao na vya wenzao hata vya kuokotwa. Hili linawaweka katika hatari ya kupatwa na maradhi kama kisukari na saratani.    Hoja ( 1x 2 = 2)    ( 10 x 2= 20)

Swali la Insha 6

Kwa kurejelea hadithi ya Mapenzi ya Kifaurongo, Mame Bakari, Nizikeni Papa Hapa , Mtihani wa Maisha na Mkubwa, eleza changamoto zinazowakumba vijana. (al.20)

Mapenzi ya Kifaurongo.

  • Ukosefu wa karo -wazazi wa Dennis kufanya kazi kwa majirani kudunduiza karo yake.
  • Ukosefu wa hela za matunzo – Dennis hana cha kupika ila uji mweupe bila sukari.
  • Mapenzi shuleni – wanafunzi wa Chuo kikuu cha Kivukoni wanahusiana kimapenzi.
  • Masomo magumu – wanafunzi hawaelewi anayofunza Dkt. Mabonga.

Mame Bakari

  • Ubakaji – Sara anabakwa na jana dume.
  • Kuavya mimba – Sara anatupilia mbali wazo la kuavya.
  • Kujitia kitanzi – Sara alilikataza wazo la hili likome hata kumpitikia.
  • Kutengwa –Alijiona akitengwa na jamii kwa jumla.

Nizikeni Papa Hapa

  • Mapenzi ya kiholela - Otii kuhusiana na Rehema bila kujali ushauri wa mwendani wake.
  • Ukimwi – Otii anaugua gonjwa lenye dalili zote za UKIMWI.
  • Kuumia kazini – Otii anaumia mguu akiichezea timu yake ya Bandari.
  • Kutelekezwa na waajiri wao – anapoumia timu yake haikumjali wala kumfidia.

Mtihani wa Maisha

  • Kutembea kwenda shule – Samueli anatembea kilomita sita kila siku kwenda shuleni.
  • Ukosefu wa karo – babake Samueli analazimika kuuza ng`ombe ili kulipa karo.
  • Mapenzi shuleni – Samueli anahusiana na Nina.
  • Kufeli mtihani wa kitaifa – Samueli anafeli mtihani wake.

Mkubwa

  • Umaskini- Mwavuli wa Mubwa umetoka mistari mitatu.
  • Matumizi ya dawa za kulevya – vijana wengi vichochoroni anakopitia Mkubwa wanatumia dawa hizi.
  • Ufisadi – wanafunzi wa profesa wanahongwa kumpigia Mkubwa kura.
  • Kufungwa – vijana wanaotumiwa kulangua dawa na wanaozitumia wanapokamatwa hutiwa kizuizini.

Swali la Insha 7

  1. “Mame Bakari”
    Kwa mujibu wa hadithi hii, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka. (alama 10)
  2. “Masharti ya Kisasa”
    “…mapenzi ni mateso, ni utumwa, ni ukandamizaji, ni ushabiki usio na maana.”
    Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi. (alama 10)

“Mame Bakari”
Kwa mujibu wa hadithi hii, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka. (alama 10)

  • Tukio la kubakwa linampotesea fahamu na anaaibika sana anapozinduka na
    kujipata akiwa uchi uk 47
  • Mwanamke kujeruhiwa - Baada ya Sara kubakwa na janadume lile,
    anaharibiwa na kuvuja damu.
  • Mwanamke kuvunjiwa ujanajike na utu wake.
  • Maisha ya mwanamke kuingiliwa na kuharibiwa.
  • Masomo yake yanakatizwa - mwalimu mkuu alimkabidhii Sara barua ya
    kumfukuza shuleni (uk 49)
  • Mwalimu mkuu hamsikilizi wala kumhurumia - badala yake aliongoza
    kumkejeli na kumweleza ile haikuwa shuke ya wazazi bali wa wasichana.
    Anasema hawafundishi wanawake hapo.
  • Mwanamke anateseka kiakili - Sara anaingiwa na mawazo mengi jinsi
    atakvyoukabili ule ujauzito. Anafikiria hata kuitoa ile mimba, kuhama kwao na hata kujiua.
  • Mwanamke katika umri mdogo anabebeshwa mimba jinsi Sara alivyofanysihwa. Mzigo huo ungekuwa na changamoto nyingi kutokana na umri wake mdogo.
  • Kuishi adhabu ya wazazi - Sara anahofia babake angemchinja kwa ujauzito
    wake.
  • Kuogopa kutoa taarifa ya kubakwa kwa wazazi kwa sababu wazazi hawangemwamini.
  • Kuishi maisha ya kimaskini - msimulizi anaeleza kuwa Sara angekunjiwakunjiwa matambatra yake na kurushiwa nje. Kila mara mwanamke anapobakwa, anayelaumiwa ni mwanamke na hata huonwa kama shetani. Uk 48 (hoja 10 x 1 = 10)

“Masharti ya Kisasa”
“…mapenzi ni mateso, ni utumwa, ni ukandamizaji, ni ushabiki usio na maana.”
Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi. (alama 10)

  • Mtahiniwa azingatie masharti ambayo mwanamume anafaa ayazingatie pamoja na athari zake katika maisha y andoa.)
  • Dadi ndiye mchuma riziki-yeye ni muuza samaki na apatacho kinatumiwa kuilisha jamaa yake. Pesa za mkewe ni za kununua mavazi ya fasheni mpya mpya na mapambo.
  • Dadi anasaidia kazi za nyumbani lakini mkewe Kidawa hatosheki na hayo. Kidawa hakubali kuwa mwanamume kazi ni za nje si za ndani na kuwa Dadi kufanya kazi za ndani ni hisani tu. Uk 60.
  • Dadi analazimika kushika shughuli za upishi kama vile kukuna nazi na kutia mboga tui.
  • Dadi anaosha nyumba, kufagia, kufua na hata kupiga nguo pasi. Wanandoa kujiwekea masharti ya uzazi. Wanahiari kumzaa mtoto mmoja tu kutokana na athari za usasa.
  • Dadi hataki mkewe atembeze bidhaa za kuwauzia wateja. Kila mara mkewe anapofanya hivyo, anaumia sana. Anaiona hiyo kama fursa ya mkewe kuhusiana na wanaume wengine. Uk 61.
  • Dadi anaona ugumu wa masharti ya mkewe katika maisha ya ndoa lakini anashinda kumweleza. Licha ya kuwa Dadi aliona ugumu wa kuzingatia masharti aliyowekewa na mkewe, hangeyavunja. Angefanya hivyo  ndoa yao ingevunjika na huko kungekuwa ni kumvunja yeye pia.
  • Dadi kushuku mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na mwalimu mkuu. Hali hiyo inampa wasiwasi sana hata anashindwa kula.
  • Kila mara Dadi alitarajiwa kuwa baada ya kula angeviondoa vyombo mezani na hata kuvisafisha.
  • Dadi anapoamua kuzua mpango wa kupeleleza uhusiano wa mkewe na mwalimu mkuu, anafumaniwa na watu akiwa amepanda paipu na anaaguka na kuumia vibaya sana jambo linalomshutua sana mkewe pamoja na mwalimu mkuu anayelazimika kumwitia ambulensi impeleka hospitalini

Swali la Insha 8

  1. Tulipokutana Tena – Alfa Chokocho
    Jadili jinsi maudhui ya umaskini yalivyoshughulikiwa katika hadithi ya ‘Tulipokutana Tena’. (al.10)
  2. Mame Bakari
    Kina dada wanaobakwa wanakabiliwa na changamoto nyingi. Tetea. (al. 10)

Tulipokutana Tena – Alfa Chokocho
Jadili jinsi maudhui ya umaskini yalivyoshughulikiwa katika hadithi ya ‘Tulipokutana Tena’. (al.10)

  • Watoto kukosa elimu
  • wazazi wa Bogoa walishindwa kuelimisha
  • Wazazi kushindwa kuwalea watoto wao
  • Kudharauliwa kwa watoto maskini
  • Watoto wa maskini kufanyishwa kazi za sulubu
  • Maskini kukosa mavazi
  • Kukosa nauli
  • Watoto wa maskini kudhulumiwa
  • Maskini kubaguliwa (Pogogo ni ya watu wa chini)
  • Watoto kuwalaumu wazazi wao - Bogoa hapendi wazazi
  • Maskini wanalaumiwa bila hatia - waliokosa kuenda shule walidhaniwa watoto -
  • Ukosefu wa upangaji uzazi unazidisha umaskini.

Mame Bakari
Kina dada wanaobakwa wanakabiliwa na changamoto nyingi. Tetea. (al. 10)

  • Tukio la kubakwa linampotozea fahamu na anaaibika anapozinduka na kujipata
    akiwa uchi
  • Mwananmke kujeruhiwa - Sara anavuja damu nyingi
  • Mwananmke kuvunjiwa ujanajike na utu wake
  • Maisha ya mwanamke kuingiliwa na kuharibiwa
  • Kukatizwa masomo
  • Kukejeliwa - mwalimu mkuu
  • Mwanamke anateseka kiakili
  • Sara ana mawazo mengi
  • Mwanamke kubebeshwa mimba katika umri mdogo
  • Kuishi adhabu ya wazazi
  • Sara anahofia babake
  • Kuogopa kutoa habari ya kubakwa kwa wazazi kwa sababu hawangemwamini
  • kuishi maisha ya kimaskini
  • Kulaumiwa hata kama ni yeye aliyebakwa 

Swali la Insha 9

Onyesha jinsi wahusika wafuatao wanavyochangia katika kufanikisha maudhui kwenye hadithi Masharti ya kisasa:

  1. Kidawa
  2. Dadi

Kidawa

  • Ndoa;anakubali kuolewa na Dida hata baada ya kutoa masharti ya kisasi ambayo anatarajia kuwa Dida angezingatia.
  • Mapenzi,anampenda Dida kwa hivyo anakubali kuacha kazi yake shuleni ili mapenzi yao yasimbaratike kutokana na wivu wa Dida.
  • Bidii,anafanya kazi mbalimbali kwa wakati moja ili aweze kuyakidhi mahitaji ya familia yake licha ya kuwa Dadi hapendezwi na hali hii
  • Nafasi ya mwanamke,ameonyesha mwanamke kama mwenye mapenzi kwa mumewe na pia mwenye bidii. Anaonyesha bidii kwa kufanya kazi kadhaa na kukubali kuacha kazi hizo ili kulinda ndoa yake.
  • Usasa anaamini kuwa katika ndoa za kisasi mwanamke na mwanaume wana nafasi na majukumu sawa kwenye familia zao.
  • Elimu; amesoma madarasa kumi na mawili;pia pia anafanya kazi ya umetroni shuleni.
  • Ajira; kidawa anafanya kazi ya umetroni shuleni ambapo anawalinda wanafunzi wa kike bwenini, pia anauza nguo na viatu.
  • Uaminifu,yeye ni mwaminifu katika ndoa yake licha ya kuwamumewe anashuku kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwalimu mkuu.
  • Mabadiliko;annamini katika mtindo tofauti wa maisha kati ya mke na mume tofauti na ilivyokuwa kitambo,mwanamke na mwanaume wanafaa kushirikiana katika ndoa.
  • Utamaduni,anamwarifu Dadi kuwa aende ampose kwao ili amwoe ,haya ni kuwa mujibu wa utamaduni.

Dadi

  • Wivu;kutokana na hisia za wivu,Dadi anafikiria kuwa mkewe kidawa ana mahusiano ya mapenzi na mwalimu mkuu,anafanya uchunguzi kuhusu jambo hili.
  • Taasabi ya kiume ;Dadi anaamini kuwa nyumbani kuna kazi za mwanaume na zile za wanawake,mwanaume hafai kufanya kazi za jikoni.
  • Mapenzi;Dadi alimtafuta kidawa kuwa mkewe wa ndoa ingawa kidawa alikuwa amewakataa wanaume wengine kadhaa.
  • Ndoa;anafaulu kumshawishi kidawa kuwa mkewe wa ndoa ingawa kidawa alikuwa amewakataa wanaume wengine kadhaa.
  • Elimu;Dadi anaamini kuwa ingawa hakusoma sana shuleni yeye si mjinga hivyo ana uwezo wa kutambua mambo mbalimbali.
  • Ajira;Dadi anafanya kazi ya uchuuzi wa samaki kwa vile hakusoma sana.
  • Ujanja,anapoelekea shuleni,anafanya ujanja wa kupitia kwa mwalimu mkuu
    abainishe iwapo yupo nyumbani au la.
  • Utamaduni,anaamini kuwa kuna kazi za wanawake na wanume nyumbani kwa mujibu wa utamaduni wa kiafrika.
  • Uasherati anashuku kuwa kidawa ana mahusiano ya kimapenzi na mwalimu mkuu hili ni tendo la kiusherati.
  • Nafasi ya mwanamke;Dadi anaamini kuwa majukumu ya mwanamke ni kutekeleza kazi ya jikoni.

Swali la Insha 10

  1. Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki. (alama 10)
  2. Shibe inatumaliza; Salma Omar
    Jazanda ni mbinu mojawapo ya mbinu za lugha zilizo tumiwa kwa ukamilifu. Ukirejelea hadithi shibe inatumaliza fafanua mifano kumi. (alama 10)

Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki. (alama 10)

  • Viongozi kuweka vitego na vikwazo vya sheria ili watu wadogo wasiweze kutetea mali zao.
  • Kutowahusisha maskini katika maamuzi muhimu yanayoathiri maisha yao.
  • Kunyakua ardhi ya madongoporomoka ambapo watu maskini waliishi.
  • Kupanga njama za kuwapatia wanyonge visenti vichache ili waondoke madongoporomoka.
  • Jitu la miraba mine kula chakula chote bila kubakishia wateja.
  • Wanamadongoporomoka kubomolewa vibanda vyao na mabuldoza.
  • Askari wa baraza kutimua watu waliokuwa wanabomolewa.
  • Jeshi la polisi kulinda askari wa baraza wakibomoa vibanda vya wanamadongoporomoka.
  • Askari kuwapiga virungu watu.
  • Kueneza zisizo za ukweli
  • Mawakili kuwalaghai watu wanaodai haki

Mifano kumi ya Jazanda katika 'shibe inatumaliza'

  • 'sasa' na 'mbura' - kusasambura (kumaliza kila kitu kuto kila kitu, kupora mali yote.
  • sherehe - mipango isiyo na maana ya kufilisi mali ya umma
  • mchele wa mbeya - Bidhaa za kigeni na zenye manufaa makubwa
  • mchele wa mbeya - Bidhaa za humu nchini na zenye manufaa makubwa
  • Njaa uroho/uchi wa kupora mali ya umma serikalini
  • Kupakua vyakula - kupora mali ya umma
  • Shibe - unyakuzi wa mali kwa wingi zaidi
  • Kivuli (Mzee mambo) - mtu asiye na maana kama kivuli chake
  • Vyetu vyao - mali ya umma mali ya wananchi
  • Kioo cha taifa wasapu fesibuku, kalamu na karatasi = Hadharani (uporaji wa mali ya umma unafanywa kila mtu akijua lakini hakuna hatua inachukuliwa)
  • ( wimbo wa sijali lawama = Hii ni tabia yatakriban viongozi watu. Tabia ya kutojali wanayofanya au lawama kutoka kwa wananchi.
  • Ni kana kwamba wao wanaoimba wimbo moja.
  • Mtahini ahakik majibi yoyote (10 x 1=10)

Swali la Insha 11

Jadili maudhui yaliyoonyeshwa kwenye mabano kutoka hadithi zifuatazo.(alama 20)

  1. Tumbo Lisiloshiba (utabaka)
  2. Masharti ya Kisasa (Unyumba)
  3. Mkubwa (Ufisadi )
  4. Mwalimu Mstaafu (Elimu)
    1. Matajiri hawajali maskini
      • Wananyakua ardhi ya maskni ili kusuluhisho matatizo yao
      • Matajiri wanaishi jijini kwenye hali nzuri na Wananchi wanaishi kwenye hali duni.
      • Makao tofauti. Jijini kuna majumba ya kifahari yaliyosimama kwa majivuno matupu ilhali Madongoporomoka watu wanaishi vibandani
      • Matajiri wananyanganya wa tabaka la chini uraia.
      • Viongozi kuwekea vikwazo vya sheria ili wasitetee mali zao wanazowapoka.
      • Wanasheria wanadhulumu wanyonge kwa kukosa uaminifu ndio maana Mago anasema watafute wanasheria waaminifu.
      • Viongozi wanawatenga wanyonge katika maamuzi ya maendeleo ya nchi. 3
      • Wanyonge wanafanya biashara duni km Mago  huku matajiri wakimiliki maduka ya biashara kubwakubwa jijini.
      • Polisi kutumiwa na tabaka la juu kufurusha wanyonge huku wanyonge wakikosa mtetezi.
      • La juu linamiliki magari na la chini 
    2.      
      1. Ndoa huhitaji uvumilivu. Dadi anavumilia miaka tisa ya ndoa kwa Kidawa licha ya kuwa alikerwa na masharti ya kisasa aliyolazimishwa na Kidawa.
      2. Katika ndoa ni muhimu kuwa wanandoa wawe na usawa wa mawazo na mtazamo. Dadi na Kidawa wanatofautiana kimtazamo kwani Dadi ni mtamaduni ilhali Kidawa ni mwanamke wa kisasa na basi hali hii inaleta migogoro kati yao.
      3. Maelewano ni muhimu katika kudumisha ndoa yoyote ile. Dadi anakosa kuelewa hasa masharti ya Kidawa lakini bado anatia saini kuyafuata. Mwishoni anaishia kuwa na majonzi katika ndoa.
      4. Katika ndoa ili mwanaume aonekane kuwa tosha lazima amdhibiti mke wake. Dadi anakerwa kuwa anaonekana mtaani kuwa yeye si mwanamume tosha kwa kuwa ametiwa maganjani na kudhibitiwa na mkewe.
      5. Katika ndoa ni muhimu  kuwa sawa kielimu kwani tofauti ya kielimu  inaibua kutoelewana katika ndoa.
      6. Uaminifu ni muhimu. Dadi aliukosa na akaishia kujiumiza.
      7. Wanasaidiana kazi za nyumbani ingawa Dadi anahisi zinafaa kuwa za mwanamke.
      8. Kupanga uzazi. Walipata mtoto mmoja kwa mujibu wa masharti ya kisasa.
      9. Ndoa inathaminiwa. Kidawa anaacha kazi ili ndoa yake idumu.
    3.      
      • Mkubwa (Ufisadi )
      • Kuhonga wapiga kura. Mkubwa alihonga raia kwa vitenge, kanga, mchele, na sukari ili wamchague.
      • Kuhonga ili kuteuliwa na chama. 
      • Kuhonga wenye msiba ili wamchague 
      • Kuhonga wanandoa kwa sufuria na magunia ya vyakula ili wamchague Mkubwa.
      • Mkubwa kuhonga Ng'weng'we ili amfungulie Mkumbukwa kabla ya kujibu mashtaka ya kupatikana na mihadarati.
      • Mkubwa kuhonga Ng'weng'we ili amrudishie mihadarati iliyokuwa imenaswa na askari ili biashara iendelee
      • Mkubwa kuhonga ili kesi ya dawa ifutiliwe.
    4.    
      1. Ni chanzo cha mtu kupata ajira. Mwalimu Mosi amesoma na anaweza kufanya kazi ya ualimu.
      2. Elimu humpa mtu busara. Mwalimu Mosi anaweza kuwapa nasaha wanafunzi wake.
      3. Wasiowajibikia elimu yao huishia maskini kama Jairo aliyepuuza masomo.
      4. Elimu haifai kuwa chanzo cha utabaka. Mwalimu Mosi anamruhusu Jairo kuhutubu japo hajasoma.
      5. Elimu huepusha maovu katika jamii. Kwa mfano, mauaji, ukwepuzi anaozungumzia Jairo.
      6. Elimu huhitaji mtu awe na matumaini. Mwalimu Mosi aliwapa matumaini ya kufuzu wanafunzi.
      7. Huwapa waja matumaini ya maisha bora usoni. Watu walisoma wakiwa na matumaini ya kujiendeleza maishani baadaye.
      8. Walimu huchangia pakubwa ufanisi wa wanafunzi.
      9. Hujenga uhusiano mwema baina wanajamii.
      10. Hukuza vipaji vya wanafunzi. Walioimba na kucheza ala za muziki.
      11. Ni chombo cha kupinga ubaguzi. 
      12. Ni chombo cha kuheshimisha. Mosi anasifiwa na wanafunzi kwa kuwaelekeza na kuwafunza.
      13. Ni ghali. Sabina kufukuzwa shuleni ili akanunue vitabu.
      14. Ina wajibu wa kuandaa nustakabali wa wanafunzi na kuwafanya watu bora  baadaye.

Swali la Insha 12

Tulipokutana Tena

  1. Jadili istilahi za lugha zinazojitokeza katika kifungu hiki. (alama 4)
    ‘Bogoa gani huyo?’ Kazu alibadilisha toni ya sauti na mng’aro wa sura yake. Alikuwa tayari kajaa huzuni ingawa hadithi yenyewe alikuwa haifahamu vizuri. Usoni pake ulisimama unyeti na juu ya ngozi ya uso wake huruma zilijitokeza. Ndivyo alivyo Kazu kila siku. Anaweza kubadilika mara moja kama uso wa mtoto mchanga.
  2. Jadili umuhimu wa Bi Sinai katika hadithi hii. (alama 8)
  3. ‘Jijini ni kuzuri. Kuna majumba makubwa, utapanda magari mazuri mazuri ya marafiki zetu, utakula vyakula vitamu na kupewa nguo za fahari. Utapelekwa shule kusoma na kuandika.‘ Kwa Bogoa , maneno haya ya babake  ni kinaya.  Thibitisha kwa hoja nane.  (alama 8)
  1.    
    • Anakuza maudhui ya kufanyisha watoto kazi za nyumbani badala ya kuenda shule.
    • Anakuza sifa ya Bogoa kuwa mvumilivu.
    • Anakuza sifa ya Bogoa kuwa msiri.
    • Anakuza sifa ya Bogoa mwenye bidii. Alikuwa akiamka alfajiri kupika mandazi
    • Anakuza maudhui ya ukatili na  udhalimu.
    • Anaendeleza maudhui ya ubaguzi.
    • Anakuza maudhui usaliti,
    • Anakuza maudhui  malezi
    • Anakuza sifa ya wazazi wa Bogoa kuwa hawajawajibika kwa kumwachia ulezi wa mtoto wao na hata walipomtembelea hawakuuliza bogoa hali ya maisha..
    • Kielelezo cha matajiri wanaonyanyasa wanyonge.
    • Kielelezo cha marafiki wabaya. Alikuwa ameahidi wazazi wa Bogoa kuwa angemlea Bogoa vizuri na hata kumpeleka shule lakini hakufanya hivyo.    Zozote 8
  2. ‘Bogoa gani huyo?’ Kazu alibadilisha toni ya sauti na mng’aro wa sura yake. Alikuwa tayari kajaa huzuni ingawa hadithi yenyewe alikuwa haifahamu vizuri. Usoni pake ulisimama unyeti na juu ya ngozi ya uso wake huruma zilijitokeza. Ndivyo alivyo Kazu kila siku. Anaweza kubadilika mara moja kama uso wa mtoto mchanga.
    • Utohozi- toni
    • Kinaya- kujawa na huzuni bila kujua hadithi
    • Taswira- huwakosesha watoto raha. Bogoa anatamani kuishi na Sebu ili kuepuka mateso ya Bi  Sinai
    • Tashibihi- kama uso wa mtoto mchanga.
  3.      
    • Bogoa alikatazwa kucheza na watoto wa Bi Sinai.
    • Kunyimwa haki ya kujieleza. Wazazi wake hawaruhusiwi kuzungumza na mwana wao.
    • Kunyimwa haki ya kupata elimu. Bi Sinai anamfanyisha Bogoa kazi basi ananyimwa fursa ya kwenda shule.
    • Kunyimwa haki ya usingizi. Bogoa alilazimika kuamka alfajiri ili kuchoma maandazi ya kuuza shuleni. Siku moja usingizi unamchukua na maandazi yanaungua.
    • Kunyimwa haki ya mlo mzuri. Bogoa anaruhusiwa kula makoko na makombo waliyoacha watu baada ya kushiba.
    • Kupigwa. Bogoa alipochelewa kutoka mchezoni alikuwa akipigwa vibaya.
    • Kutusiwa. Bi Sinai alikuwa akimtusi na kumsimbulia.
    • Bogoa kulia kwenye sufuria na wengine sahanini. Alikula wa mwisho.
    • Kutishwa. Sinai kutisha Bogoa kuwa angemkata ulimi akiambia mtu kuhusu maisha ya pale.
    • Kuchomwa viganja na Sinai kwa kuunguza maandazi.
    • Kukoseshwa watoto raha. Bogoa anatamani kuishi na Sebu ili kuepuka mateso ya Bi  Sinai

Swali la Insha 13

Jadili maudhui ya uwajibikaji kama ambavyo yamejitokeza katika hadithi ya Mwalimu Mstaafu. (al. 20)

  1. Uwajibikaji
    1. Wazazi na wanafunzi wanafika shuleni kumzawidi mwalimu Mosi kwa sababu ya kazi nzuri
    2. Mwalimu Mosi anawasuta wanafunzi wake kwa kuendeleza ubaguzi
    3. Mwalimu mosi anawaomba watu kumpigia Jairo makofi
    4. Mwanafunzi mmoja wa zamani anajitolea kumpelekea a Mwalimu Mosi vitu kwa gari lake
    5. Sera anamsihi mwalimu Mosi aikubalie fimilia ya Jairo ikae pale kwake
    6. Mwailmu Mstaafu Mosi anaipa famila ya Jairo nyumba
    7. Mkewe Mosi anamwambia mwalimu mstaafu amchuke kama mkewe lakini mwalimu mstaafu anakataa
    8. Mkewe Jairo na mkewe Mosi wanafanya kazi kwa ushirika
    9. Mosi anampeleka bintiye Jairo mjini akanunue vitabu vya hesabu.
    10. Mosi na mkewe wanampeleka bintye Jairo kwa shule ya bweni
    11. Jairo anapotaka Kujitasha majini, kijiji kizima kinamzuia asifanye hivyo
    12. Mosi alipokuwa mwalimu aliwashauri wanafunzi wake dhidi ya ulevi
  2. Kutowajibika
    1. Jairo hakuzingatia masomo alipokuwa shuleni hata baada ya kushauriwa na kuhimizwa na Mwalimu Mosi 
    2. Anumtishia maisha mwalimu Mosi eti kwa kukioa Kitoto chake.
    3. Pia anaitoa familia yake kama zawadi
    4. Anaitelekeza familia yake kwa mwalimu mstaafu - hakufika huko kwa siku ayami
    5. Bi Sera anampendekeza mumewe amchukue mkewe Jiaro kama mkewe
    6. Watu wanamjaza Jairo maneno ya uongo na kumafanya ashikwe na hasira
    7. Jairo anataka kumuua mwalimu Mosi eti kwa kukica kitoto chake anenda kwake na panga kukitenganisha kichwa chake na kiwiliwili chake
    8. Pia anapopata kuwa ule ulikuwa uvumi tu anataka kujitosa majini afe
    9. Mwalimu Mstaafu Mosi hakumwambia

Swali la Insha 14

Onyesha namna mwandishi alivyoshughulikia maudhui yaliyo kwenye mabano katika hadithi zifuatazo.

  1. Tulipokutana tena. (ukiukaji wa haki za watoto) (alama 14)
  2. Mtihani wa maisha (Elimu). (alama 6)
  1. Tulipokutana Tena.
    1. Bi. Sinai kumnyima Bogoa uhuru wa kucheza na wenzake ila kwa kutoroka.
    2. Bi. Sinai Kumlazimisha Bogoa kwenda kuuza mandazi shuleni badala ya kusoma.
    3. Bogoa kupigwa na Bi Sinai alipopatikana akicheza na watoto wa majirani.
    4. Bi. Sinai kumchoma Bogoa viganja vyake kwa kutumia kijinga cha moto kwa kuyaacha maadazi yaungue.
    5. Bi. Sinai kumpa Bogoa makoko na makombo ya chakula, kulia vyunguni na sufuriani wengine wakila sahanini.
    6. Bi. Sinai kutompa Bogoa hata sekunde moja kuwa na wazazi wake.
    7. Bi. Sinai kumlazimisha Bogoa kufanya kila kitu alichoamrishwa kufanya. Kumenya vitunguu, maji, kuparia samaki, kuchanja kuni.
    8. Babake Bogoa kumtishia kuwa angempiga iwapo angekataa kwenda mjini.
    9. Wazazi wa Bogoa kumtoa nyumbani kwao na kumtelekeza kwa rafiki yao ambaye ni Bi. Sinai.
    10. Wazazi wa Bogoa kumdanganya kuwa akienda mjini anapelekwa shuleni, mavazi mazuri mwishowe hali haiwi hivyo. 7x2=14
  2. MTIHANI WA MAISHA.
    1. Wanafunzi wanaofeli katika mtihani hukata tamaa maishani na hata kutaka kujitoa uhai. Samueli anataka kuchupia bwawani kuepuka fedheha.
    2. Elimu ina gharama. babake Samueli anuza ng’ombe wote kumsomesha mwanawe.
    3. Wanafunzi kufedheheka wanapofeli mtihani wao. Samueli anatamani kuzibadilisha gredi zake duni.
    4. Wanafunzi wa shule za kutwa hulazimika kutembea masafa marefu kwenda shuleni. Samueli anatembea kilomita sita kila asubuhi kwenda shuleni.
    5. Wazazi hukasirika watoto wao wanapokosa kufaulu katika mtihani. Babake Samueli anakasirishwa na matokea duni ya mwanawe hata anampa kamba ya kujinyonga.
    6. Elimu pia huathiri uhusiano baina ya wanafunzi. Samueli anashuku uhusiano wake na mpenzi wake iwapo utaendelea kwa sababu yake kuwa na matokeo duni katika mtihani.
    7. Walimu wanakosa kuamini uwezo wa wanafunzi wao. Samueli anajua kuwa mwalimu mkuu hakuamini uwezo wake masomoni. (6x1=6)

Swali la Insha 15

MAPENZI KIFAURONGO: Kenna Wasike
“Hadi sasa mimi ni kama rubani aliyeharibikiwa na ndege angani.”
Onyesha ukweli wa dondoo hili.
(alama 20)

  • Dennis alitokea katika familia ya kimaskini hangemudu mavazi mazuri kama ya wenzake chuoni au vifaa meme vya kisasa kama vile ipad, tarakilishi n.k.
  • Dennis hakusomea shule za kifahari kama wenzake chuoni.
  • Somo la Dakatari Mabonga linamvunja moyo Dennis na anahisi hapo hapamweki kwa vila namna anavyoendesha somo hilo anawaitia fadhaa. (uk 14)
  • Dennis anapomwomba mhadhiri atumie lugha nyepesi, darasa nzima linamcheka huku mwalimu akimkejeli kuwa ipapo alinuia kuwachekesha hajui kuchekesha.
  • Dennis kinyume na wenzake hana pa kukimbilia mambo yanapoharibika chuoni – wengine wataajiriwa na jamaa zao huku wengine wakiwa na wachumba wanaofanya kazi za kifahari serikalini na watawafadhili na kuwaondoshea kero la elimu ya juu.
  • Chuoni Dennis anaishi maisha duni. Malazi yake yamechanikachanika. Hana chakula na analazimika kupika uji mweupe na kuunywa kama chamcha.
  • Dennis anatafuta kazi sana baada ya kufuzu kama mtangazaji wa redio-kazi kwake inakuwa ni kuitafuta kazi yenyewe.
  • Dennis anakosa nafasi ya ajira kwenye shirika la kuchapisha magazeti. Kazi hiyo anapewa Shakila kwa sababu mamake ni mkurugenzi wa kamppuni hiyo – hapa anafanyiwa ubaguzi moja kwa moja.
  • Baada ya Penina kutambua Dennis hakufanikiwa kupata kazi, hataki hata amwite mpenzi. Hampikii kwa sababu alipotoka asubuhi hakuchangia chochote.
  • Penina anamfukuza Dennis pale kwao nyumbani na anamweleza asija akamwambia mtu kuwa waliwahi kuwa wapenzi.

Swali la Insha 16

Ndoto ya Mshaka: Ali Abdulla Ali
Mwandishi wa hadithi hii anatupa taswira ya jamii iliyozongwa na masaibu yanayotamausha. Tetea ukweli wa kauli hii. (alama 20)

  • Mashaka hakupata malezi mema – alikosa lishe bora. Chakula kilikuwa ni tikitimaji na matango.
  • Mashaka katika umri mdogo aliwapoteza wazazi na kulelewa na Bi. Kidege.
  • Mamake mlezi (bI. Kidege) anakabiliwa na maradhi ya miguu hivyo anashindwa kuzumbua riziki yao.
  • Mashaka anashiriki katika ajira katika umri mdogo ili wapate rizsiki yeye na mamake mlezi (uk 72)
  • Punde Mashaka anapokamilisha masomo ya chumba cha nane, mamake mlezi anaaga dunia na kumwacha katika ukiwa.
  • Ndoa ya Mashaka haikuwa ndoa ya kutajika – ilikuwa ni ndoa ya kulazimishiwa licha ya umaskini wake.
  • Mashaka anabaguliwa na Mzee Lubeya na mkewe ambao ni wakwe zake kwa umaskini wake. Wanalazimika kuhamia Yemeni kukimbia aibu.
  • Mashaka na mkewe Waridi kuishi kimaskini katika chumba kibovu. Anaeleza kuwa shida ziliwatamiria kila upande. (uk 74)
  • Mashaka na Waridi Kuwazaa watoto wengi ambao wanashindwa kuwapa malezi mema. Watoto wa kike kulala chini kwenye chumba kimoja na mamao ilhali wale wa kiume waliombewa jikoni kwa Chakupewa walikolala kama nyau. (uk 75)
  • Mazingira ya pale kwa kina Mashaka ni mabovu. Harufu ya choo kinachokumbatia chumba chao kuhamia chumbani mwao. Kuna mfereji wa maji chafu unaotema maji yake kwenye Mto Msimbazi (uk 74)
  • Mashaka na familia yake hawana choo – wanakwenda haja zote kwenye karatasi za plastiki na kuzitupa ovyo.
  • Viongozi kusaliti raia wanyonge – waakati wa mafuriko huwatangazia wahame mabondeni lakini hawawapi makao bora. (uk 75) – hawasemi waende wapi.
  • Mashahara wa mkia wa mbuzi aliopewa Mashaka kazini haungemruhusu kununua vifaa vya nyumbani. Aidha nafasi ya chumba chao haingetosha.
  • Waridi na watoto wanamtoroka Mashaka bila kuaga. Aliwahi kudokeza kuhusu kutoroka kwake katika wimbo ambao Mashaka hakuuelewa wakati huo (uk 77)

Swali la Insha 17

  1. Salma Omar Hamad- SHIBE INATUMALIZA
    “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza.”
    Onyesha jinsi kula kuliwamaliza wazungumzaji na wahusika wengine katika hadithi hii (Alama 10)
  2. Kenna Wasike- MAPENZI YA KIFAURONGO
    Jadili Suala la umaskini na athari zake kama ilivyo katika hadithi ya Mapenzi ya Kifaurongo (Alama 10)
  1. Salma Omar Hamad- SHIBE INATUMALIZA
    “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza.”
    Onesha jinsi kula kuliwamaliza wazungumzaji na wahusika wengine katika hadithi hii (Alama 10)
    • Mzee Mambo ni waziri kivuli wa wizara zote, hafanyi kazi maalumu kiasi kwamba haoni umuhimu wake. Hata hivyo, yeye hupakua mshahara (uk 37).
    • Viongozi wanatumia mali ya umma kufanikisha maslahi yao. Mzee Mambo anatumia magari ya serikali kubebea maji na kuwapeleka watoto kwenda kuogeshwa (uk 39).
    • Viongozi wanatumia pesa za umma kuandaa sherehe zisizo na maana. Mzee Mambo anasherehekea mwanawe kujiunga na chekechea na yule mdogo kumea vijino viwili (uk 38).
    • Viongozi wanakula bila kufanya kazi. Mzee Mambo anakiri kuwa kinachoangaliwa zaidi ni kwenda kazini bali si kufanya kazi (uk 37), aidha, katika sherehe hakupikwi, kunaliwa tu (uk 39).
    • Huku Sasa na Mbura wakijinufaisha, wanyonge wanahangaika kwa kukosa chakula. Kidogo walicho nacho kinachukuliwa na viongozi wanaokula wanyonge wakiteseka. Wamepuuzwa wanyonge. Viongozi wanakula tu. Wanadai kuwa wanakula vyao vya wenzao (uk 44). 
    • Viongozi kama Sasa na Mbura wanajinyakulia mali nyingi. Hawachukuliwi hatua yoyote bali wanaachwa kuendeleza uovu wao. Mbura anasisitiziwa kuwa aendelee kuwasasambura wananchi.
    • Uongozi wa kina Mambo haujali maumivu ya wananchi. Wanatumia falsafa potovu ya ‘kutojali lawama’ za wanyonge. Muziki anaousikiza Mzee Mambo unadhihirisha kuwa viongozi hawajali sheria.
    • Dj analipwa pesa nyingi kwa kuwatumbuiza watu.           (zozote 5×2)
  2. Kenna Wasike- MAPENZI YA KIFAURONGO
    Jadili Suala la umaskini na athari zake kama ilivyo katika hadithi ya Mapenzi ya Kifaurongo (Alam 10)
    • Chuoni, Dennis anakumbwa na tatizo kubwa la utabaka. Wanafunzi kutoka familia zenye nafasi walikuwa na simu za thamani, wengine walibeba vipakatalishi na iPad zao mikononi (uk 13) huku naye asiweze kupata hata chochote. Umaskini huu ulileta mpaka kati ya wanafunzi maskini na tajiri wasiweze kukaribiana.
    • Siku moja Dennis akiwa chumbani mwake baada ya kupika uji wa mahindi bila sukari kutokana na umaskini wake, Penina, binti yake Bw. Kitime, Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Afya (uk 19) anabisha mlangoni pake.
    • Penina anamweleza kuwa lengo la kuja kwake ni kumtaka wawe wapenzi. Anamweleza hadharani kuwa kando na mapenzi ya wazazi, kuna mapenzi mengine anayoyakosa na anayataka kutoka kwake Dennis. Dennis anasita kujihusisha kwa mapenzi na msichana huyu wa kitajiri kwa kuhofu kutemwa tena; mapenzi ya kifaurongo.
    • Wanakuwa kwenye mapenzi. Mapenzi yao yanadumu kwa muda wa miaka miwili. Wanapomaliza chuo, wanahamia kwenye mtaa wa watu wa pato la wastani, Newzealand, licha ya kuwa hawajapata kazi. Wazazi wake Penina wanawalipia kodi.
    • Dennis anatafuta kazi kwa kila njia bila mafanikio. Anakosa kazi katika shirika la uchapishaji magazeti kwa kushindwa kujibu swali moja la kwanza.
    • Kukosa kazi kunamfanya Penina kumwamrisha asanye kila kilicho chake na aondoke. Akamfukuza na kumtaka aione nyumba yake paa. Haya yote yanatokana na hali mbaya ya umaskini wa Dennis.
      (zozote 5×2- Mtahini atathmini majibu ya watahiniwa)

Swali la Insha 18

  1. Jadili matumizi ya kinaya  katika hadithi ya “ Shibe inatumaliza’’ (alama 10)
  2. “Tunakula tu. Vyetu na vya wenzetu… Na watakozaliwa miaka hamsini ijayo.”
    Thibitisha ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari kwa kutoa hoja kumi. (alama 10)
  1. Ni saa sita kamili na jua limewaka ila  sasa Mbura wamejikunyata
    • Mzee mambo ana vyeo anavyopata mishahara kupitia kuavyo ila hajui maana yavyo umuhimu wavyo wala majukumu yavyo.
    • Katika taifa la Mzee Mambo kinachoangaliwa Zaidi ni kwenda kazini wala si kufanya kazi.
    • Mzee Mambo hafanyi kazi ilhali ndiye anayepokea mshahara mkubwa kuliko wale wanaofanya kazi kama Sasa na Mbura.
    • Ni kinaya serikali kufuja mali ya umma. Kugharamia sherehe za mtu binafsi(Mzee Mambo)ambaye anaifisidi serikali iyo hiyo kwa kulipwa mshahara bila kufanya kazi.
    • Sasa na Mbura walikuwa wamepakua chakula mara mbili na kukila lakini wanapopakuwa mara ya tatu mwandishi anasema kuwa huo ndio wakati walipoanza kula.
    • Sasa na Mbura wanafanya kazi kwa kujituma na kujitutumua ila kazi yenyewe ni ya ukwe isiyo na malipo.
    • Mwandishi anasema kuwa Sasa na Mbura hawana wasichofanya lakini hawana wafanyacho.
    • Ni kinaya kwa mzee Mambo kufisidi serikali na kujiliwaza kwa neno lake Mola kuwa Mungu humpa amtakaye bila ya kiwango maalum ilhali ameliibia taifa lake.
    • DJ anamfanyia kazi mzee mambo lakini analipwa mshahara na serikali badala ya kulipwa na mzee Mambo.
    • DJ mwenye pesa halipi huduma za maji, umeme na matibabu ilhali raia maskini wanalipia huduma hizo. (zozte 10x1=10)
  2.      
    • Mzee Mambo kupakua mshahara licha ya kuwa waziri kivuli.
    • Kuandaliwa kwa sherehe isiyo na umuhimu wowote – kwa sababu mmoja ameota jino na mwingine anajiunga na nasri skuli
    • Magari ya serikali kutumiwa katika sherehe ya kibinafsi
    • Waliohudhuria sherehe kula vyakula vingi bila kujali lawama
    • Unyakuzi wa dawa za umma – DJ anamiliki duka ambalo mtaji wake ni bohari kuu ya dawa za serikali
    • DJ na wenzake kuchota mabilioni ya pesa kwa sherehe
    • Mawaziri wawili kufanya kazi katika wizara moja – Sasa na Mbura
    • DJ kupata huduma za umeme bila malipo licha ya kuwa na pesa.
    • Sasa na Mbura kuibia serikali muda wa kufanya kazi kwa kwenda kuhudhuria sherehe nyumbani mwa Mambo.
    • Mzee Mambo anatumia mabilioni ya serikali kugharamia sherehe nyumbani kwake.
    • Mzee Mambo anatumia magari ya serikali kusomba maji, kubeba jamaa zake kuelekea kwenye sherehe nyumbani kwake.
    • Mzee Mambo anatumia runinga ya taifa kupeperusha sherehe  ya kibinafsi ilhali anastahili kupeperusha maswala ya kitaifa.

Swali la Insha 19

  1. EUNICE K. Mtihani wa Maisha
    Jadili changamoto zinazokumba sekta ya elimu ukirejelea hadithi ya mtihani wa maisha. (al. 8)
  2. S. O. Hamad: Shibe Inatumaliza
    “Shangwe. Hoihoi. Nderemo. Vifijo ndio mchezo wao wakishapakua. Muziki laini wa taarabu unatumbuiza na ndani yake mna vijembe.”
    Kwa kurejelea hadithi hii, jadili ukweli wa maneno yaliyopigiwa mstari. (al. 12)
  1.                              
    1. matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yamesawiriwa kama daraja la kuwavusha wanafunzi hadi ufanisi na uluwa – Samueli alitegemea matokeo ya kidato cha nne kuwa daraja kati yake na ufanisi na uluwa.
    2. wanafunzi wanaiona shule kama jela. Baada ya kupokezwa matokeo ya mtihani, Samueli anafurahi na kumshukuru Mungu kuwa sasa hayupo kwenye jela iitwayo shule.
    3. matokeo ya kidato cha nne yanawasababishia wanafunzi woga. Wanafunzi waliokuwa wameenda kupokea matokeo yao ya kidato cha nne katika shule ya upili ya Busukalala walikuwa na hofu na misheshe nafsini mwao kwa kutofahamu iwapo walikuwa wamefaulu au wamefeli.
    4. elimu ina gharama – Baba Samueli anawauza ng’ombe ili kupata karo ya kumlipia Samueli.
    5. baadhi ya wanafunzi wamepujuka kimaadili – mfano, Samueli anamwita mwalimu wake mkuu hambe. Aidha anawaita wanafunzi wenzzake mahame, wadaku, wambea na chakubimbi
    6. baadhi ya wanafunzi hawang’amui wanayofundishwa. Kwa mfano, Samueli anasema kuwa mto Limpopo upo Misri na mto Zambezi upo Tanzania ilhali sivyo ilivyo
    7. wanafunzi wanaenda shuleni kwa miguu kila siku. Samueli alitembea kila siku kilomita sita kuelekea shuleni Busukalala.
    8. Kuanguka mttihani kunawatia wanafunzi wasiwasi. Baada ya kung’amua kwamba amefeli, Samueli anashindwa cha kuenda kuwaambia wazazi wake hasa babake.
    9. wazazi wanthamini elimu ya mtoto wa kiume kuliko ya mtoto wa kike – licha ya Bilha na Mwajuma kufaulu, baba yao aliwaona kuwa wanawake tu – fahari yake ya dhati ilikuwa katika kumwona mwanawe wa kiume Samueli – akifua dafu.
    10. wanafunzi wanakiuka mipaka ya uhusiano wao kwa kuanza kuhusiana kimapenzi kwa mfano, badala ya kuhusiana kimasomo, Nina na Samueli wanahusiana kimapenzi
    11. Wanafunzi wavulana wanatumia uongo ili kuwavutia wenzao wa kike. Kwa mfano, Samueli anamhadaa Nina kuwa yeye ni bingwa masomoni ili akubali kuwa mpenziwe.
    12. Kuanguka mtihani ni chanzo cha mwanafunzi kuwa mwongo- baada ya kufeli mtihani, Samueli anamhadaa babake kuwa mwalimu mkuu hakumpa matokeo ya mtihani
    13. Kufeli mtihani ni chanzo cha baadhi ya wanafunzi kujiua. Baada ya kufeli mtihani, Samueli anapanga kujiua. Anajitosa kwenye bwawa la maji ila anaokolewa na mpita njia.
      Zozote 8 x 1=8
  2. Shibe Inatumaliza
    1. sasa na mbura hawafanyi chochote cha kuwafaa maishani ila kusubiri kupewa.
    2. Mzee mambo ni waziri kivuli – hana wizara kamili lakini anapokea mshahara.
    3. viongozi/mawaziri hujiamulia kima cha mshahara wanachopokea.
    4. mzee mambo anapewa wadhifa ili kuongeza walaji
    5. Dini inatumiwa kuhalalisha haramu “Hadhaa min fadhil rabbi!”
    6. Viongozi wanabadiri fedha za umma – wanatumia kwa anasa- kusheherekea kuota kwa mtoto/mtoto kuingia shule ya chekechea.
    7. wanapofanya jambo linaloonekana la kifadhila wanajidai kwa mitandao/vyombo vya habari ili wajulikane kwa ufadhili wao.
    8. wanatumia magari ya umma /serikali kwa shughuli za kibinafsi.
    9. wanaandaa vyakula vya kila aina ilhali kama sasa na Mura huwa wenye njaa.
    10. shughuli kubwa katika sherehe ni kula bila kutoa mchango wa aina yoyote
    11. wanakula hawajali asili ya vyakula hivi
    12. walaji ni walafi, hula kupita kiasi
    13. Wakisha kula kazi yao huwa kulala – si kufanya kazi
    14. walaji hawavipendi vyakula vyao vya asili, wanashabikia mchele wa plastiki
    15. viongozi wanaibia umma la lawama haziwashtui kamwe
    16. dawa huibwa kutoka kwa mabohari ya serikali na kuuzwa katika maduka ya binafsi
    17. iongozi wanapata huduma za umeme, tiba bila kulipia ilhali maskini wanahangaika
    18. wanajiangamiza kwa kujiletea maradhi kama presha, bolisukari, saratani, vidondo vya tumbo, obesity.
    19. waliacha kufikiria kwa vile wanapata kila wanachokihitaji.
    20. watu wasio na elimu ndio viongozi
    21. mtu mmoja ana vyeo zaidi ilhali wengine hawana kazi zozote.

Swali la Insha 20

Huku ukirejelea diwani ya Tumbo lisiloshiba fafanua matatizo yanayokumba vijana katika jamii (alama 20)

 Umaskini. Hadithi ya ‘Mapenzi ya kifaurongo’ Dennis Machora anakunywa uji bila sukari

  • Hana pesa/maskini
  • Ni zikeni papa hapa Otii anaishi kwenye kibanda kilichotalizwa kwa udongo na kuezekwa kwa makuti
  • Dawa za kulevya. Hadithi ‘Mkubwa’ vijana wanakufa kwa sababu ya kutumia dawa za kulevya.
  • Kubakwa ‘mame Bakali’ Sara anabakwa akitoka kuhudhuria masomo ya ziada usiku.
  • Kuavya mimba ‘Shogake dada ana ndevu’ SAfia anaavya mimba, inayosababisha kifo chake.
  • Kuvunjika kwa Uchumba ‘Mapenzi ya kifaurongo Peninah anavunja uchumba wake na Dennis Machora kwa sababu ya Dennis kuwa maskini.
  • Ukosefu wa ajira ‘Mapenzi ya Kifaurongo’ Dennis amekamilisha masom ya chuo kikuu lakini ametafuta ajira kwa miaka mitatu bila mafanikio.
  • Magonjwa – Nizikeni papa hapa’ Otii anaambukizwa virusi vya ukimwi Rehema Wanjiru
  • Tamaa ya Mapenzi “Nizikeni papa hapa” Otii ana tamaa ya mapenzi.
  • Mimba za mapema ‘hadithi ya Mame Bakari’
  • Mhusika Sarah
  • ‘Shogake dada ana ndevu’ Safia.
  • Malezi duni- Mashaka alikosa mapenzi ya wazazi wake
    Elimu duni- Mashaka hakupata masomo ya kiwango cha kumpa kazi.

Swali la Insha 21

Mtoto wa kiume amesawiriwa kupitia changamoto si haba katika jamii ya sasa.Tetea kauli hii
ukirejelea hadithi ya Ndoto ya Mashaka , Mapenzi kifaurongo na Masharti ya kisasa. (alama 20)

  1. NDOTO YA MASHAKA
    Kutojichagulia mke -Mtoto wa kiume hana hiari ya kujichagulia mchumba ,Mashaka analazimishiwa Waridi kama mke wake akiwa hana chochote. Waliowavamia chumbani mwake ni MzeeRubeya baba yake Waridi,Sheikh Mwinyimvua,kaka yake Waridi Mansuri na Rafiki ya keIdi.
    Mstahimilivu -Mtoto wa kiume anastahili kustahimili madhila na hana pa kutorokea kukiwa na shida .Waridi anapokabiliwa na shida katika ndoa hujitorokea na kumwacha mume wake Mashaka akiwa pweke
    Upweke – Mtoto wa kiume kushindwa kustahimili anapokumbana na upweke .Babake Mashaka upweke ulimshinda akafariki na wakazikwa Pamoja na mke wake.
    Majukumu – Mtoto wa kiume anaachiwa majukumu ya ulezi Biti Kidebe alikuwa haishi kulala mikia miguu yake iliyomuuma.Hivyo,licha ya yeye kumlea Mashaka, naye Mashaka akamlea huyu bibi.Alitafuta kila aina ya vijikazi alivyoviweza tangu akiwa mtoto.Alipomaliza shule tu Biti Kidebe akafariki na kumwa mpweke.
    Kubaguliwa kwa Mtoto wa kiume-Aibu ni madhila mengine yanayomkumba Mtoto wa kiume . Ndoa ya Mashaka na waridi ilimtia Rubeya aibu kwa kuwa binti yake ameolewa na fukara.Mzee Rubeya na familia yake wakaamua kurudi kwaoYemeni.
    Kuachwa kwa sababu ya umaskini-Mashaka alikuwa na kazi duni yenye mshahara wa mkia wa mbuzi–alikuwa mlinzi wa usiku
    Katika kampuni za Zuia Wizi Security(ZWS).Watoto wake wavulana walilala jikoni kwa jirani Chakupewa.Nafasi ilikuwa duni kabisa.Ilibidi mkewe apikie nje ya chumba chao isipokuwa,nyakati za mvua ambapo jiko huwekwa juu ya kinu kuzuia maji yanayotiririka.Siku moja Mashaka aliporudi kutoka kazini alikuta Waridi ametoroka na Watoto wote.Toka wakati huo hakuwaona tena.Akabaki mnyonge na mpweke zaidi.Utengano huo ulimfanya ajutie ufukara wake na kuuona kuwa ni udhia mkubwa maishani.
    Msongo wa mawazo wanapopatwa na madhila – Mtoto wa kiume anapatwa na fikra nyingi za kujilaumu kutokana na shida nyingi zinazomuandama,Mashaka alikuwa na mawazo mazito na maswali yasiyo na majibu–kwa nini ‘Jumuiya za kimatiafa zinafumbia macho suala la ufukara?
    Ni ufukara uliomtenganisha yeye na Waridi,yeye na Watoto wake na kumwacha katika lindi la maumivu. Mashaka alijipa moyo kuwa Subira huenda ikamletea heri.Hata hivyo,aliendelea kusubiri
    Akitarajia kuwa mambo yatabadilika.Lakini mambo hayakubadilika.
  2. MAPENZI KIFAURONGO
    Ukosefu wa ajira baada ya kuhitimu chuo kikuu -Mtoto wa kiume anakosa kazi hata baada ya kuhitimu masomoni kwa sababu ya ufisadi katika jamii.Dennis anakosa kazi katika shirika la magazeti kwa kukosa kumjua mtu ilhali Shakil ananatafutiwa kazi na mamake kwa sababu anacheo kikubwa kazini mwake.Ni mkurugenzi mkuu.Dennis anaposaka kazi kwingi na anakosa .Miaka mitatu baada ya kufuzu chuoni na bado alikuwa akifanya‘tarmacking’ yaani kutafuta kazi.
    Migogoro ya mapenzi –Mtoto wa kiume hana hiari kuachwa katika mahusiano ya kimapenzi. Rafiki wa kiume wa kwanza wa Penina anaachwa na Penina kusingiziwa kutokuwa mwaminifu na vilevile Dennis anaaachwa na Penina kwa misingi ya kuwa maskini
    Kutamauka kwa masomo- Masomo chuoni kwa Mtoto wa kiume yanakuwa una ugumu kiasi kwamba wanafunzi wanahiari kufanya kazi ya matatu na kukusanya kodi za nyumba zinazomoilikiwa na wazazi wao.Dennis na wanafunzi wengine wanakaliwa na ugumu wamasomo katika chou kikuu.
    Msongo wa mawazo kwa sababu ya umaskini, -Jambo hili linamtatiza Mtoto wa kiume ,Dennis anasumbuka kiakili kwa sababu ya hali na asili yake ya umaskini,anabaki mara nyingi kutamani kumezea mate magari makubwa yanayoendeshwa na wenye pesa Dennis anakiri kuwa “kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani’..
    Utabaka katika jamii unaadhiri Mtoto wa kiume kwani anakosa kupendwa kwa sababu hana mali.Hali hii inaanzia chuoni baina ya wanafunzi .Umaskini unaleta matatizo kati ya masomo na mapenzi ya DennisMachora na Penina , Dennis anafinyika kimawazo kuhusu ikiwa kijana maskini anaweza kupendwa na msichana wa tabaka la juu,mwenye nacho anapita juu na mwenzake mchochole anapita chini
    Kukejeliwa kwa kutoelewa – Mtoto wa kiume anastahali kuwa mtambuzi/mjuzi na kuwa na ufahamu wa mambo ,Dennis anachekwa na wanafunzi wenzake hasa msichana mmoja anayecheka hadi kuanguka kwa sababu ya Dennis kutaka ufafanuzi wa mafumbo ya Daktari Mabonga .Vile vile anaposhindwa kujibu maswali wakati wa mahojiano–anaaibika
    Kujitegemea na kukimu familia – Dennis hapewi pesa za masurufu na wazazi wake anafaa kujimudu kupata chakula,hata ingawa wazazi wake ni maskini ,Penina anashangaa jinsi anavyokunywa uji,vilevile wanapomaliza chuo Penina anakaa tu nyumbani akimtegemea Dennis kwa kila kit una anapouliza kupewa anamwambia hajachangia chochote .
  3. MASHARTI YA KISASA
    Kutunza familia - Mtoto wa kiume ndiye anayetarajiwa kuikimu familia yake hata kama ana kazi duni na mshahara mdogo Dadi ndiye mchuma riziki yeye ni muuza samaki na apatacho kinatumiwa kuilisha jamaa yake.pesa za mkewe ni za kununua fasheni mpya mpya na mapambo.
    Kusaidia katika kazi za nyumba bila hiari -Madhila mengine yanayomkunba Mtoto wa kiume ni kulazimishwa kusaidis kazi nyumbani bila hiari yake .Dadi anasaidia kazi za nyumbani lakini mkewe Kidawa hatosheki na hayo.Kidawa hakubali kuwa mwanamume kazi ni za nje si za ndani na kuwa Dadi kufanya kazi za ndani ni hisani tu.
    Kutomwamini mke katika ndoa -Mtoto wa kiume anakumbana na madhila ya kutomwamini mke katika ndoa tunapoona Dadi hataki mkewe atembeze bidhaa za kuwauzia wateja.Kila mara mkewe anapofanya hivyo,anaumia asana.Anaiona hiyo kama fursa ya mkewe kuhusiana na wanaume wengine. Dadi anapoamua kuzua nmpango wa kupeleleza uhusiano wa mkewe na mwalimu mkuu
    Kudhibitiwa na mke katika ndoa - Dadi anaona ugumu wa masharti ya mkewe katika Maisha ya ndoa lakini anashinda kumweleza.Licha ya kuwa Dadi aliona ugumu wakuzingatia masharti aliyowekewa na mkewe,hangeyavunja.Angefanya hivyo ndoa yao ingevunjika na huko kungekuwa ni kumvunja yeye pia. Dadi aliogopa kuambiwa kuwa yeye si mwanaume tosha
    Kufuata amri za mke na anapokiuka na hata kumpeleleza kupata lawama kutoka kwa jamii - Kila mara Dadi alitarajiwa kuwa baada ya kula angeviondoa vyombo mezani na hata kuvisafisha. Dadi analazimika kushika shughuli za upishi kama vile kukuna nazi na kutia mboga tui. Dadi anaosha nyumba, kufagia, kufua na hatakupiga nguo pasi .Anafumaniwa na watu akiwa amepanda paipu na anaanguka na kuumia vibaya sana jambo linalomshutua sana mkewe Pamoja na mwalimumkuu
    Anayelazimika kumwitia ambulensi impeleke hospitalini.
    Kufuata masharti anayowekewa na mke bila kukaidi -Mtoto wa kiume analazimishwa kufuata masharti asiyoyapenda kwa sababu ya kumpenda mke -Kwa kuwa Dadi alimpenda kidawa alikubali masharti ya kisasa bila kuyaelewa kama vile kukosa uamuzi juu ya idadi ya Watoto atakayetaka Anapangiwa masharti ya uzazi.Hana hiari ila kukubali kuwa na mtoto mmoja tu
    Msongo wa fikra -Madhila ya msongo wa mawazo yanampata Mtoto wa kiume hasa anapowazia uaminifu wa ndoa yao.Dadi kushuku mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na mwalimu mkuu.Hali hiyo inampa wasiwasi sana hata anashindwa kula. Kidawa kufanya kazi za umetroni kunafanya asimwamini
    Dhihaka kutoka jamii – Mtoto wa kiume anakejeliwa na kuonekana kama asiyekuwa mume wakutosha mkewe kidawa akionekana anasimama na kunena na wanaume wengine .Mtoto wa kiume kufanya kazi za kike kwa sababu hana kipato kikubwa ikilinganishwa na mwanamke. Ncha nyingi za Maisha zinamfanya Kidawa atembeze bidhaa za uarabuni mitaani Jambo lililozidisha shauku ya Dadi kwa kidawa. Bi Zuhura alimkejeli Dadi kwa kumtaka amparalie samaki .Maneno ya watu yalimfanya Dadi aache kusaidia kazi za nyumbani
    Kuteuliwa kwa mapenzi na mke bila hiari -Mtoto wa kiume anasuhubiwa na hata kuchaguliwa na mwanamke .Mwanamke ana uhuru wakijiteulia mume ,Kidawa alijiteulia Dadi
    Hashirikishwi katika maamuzi muhimu-Mtoto wa kiume hashirikishwi katika maamuzi muhimu ya ndoa,anampa Dadi masharti ya kumsaidia,anamwaaamulia idadi ya watoto watakaopata ,masharti atakayofuata katika ile ndoa
    Heshima - Mtoto wa kiume haheshimiwi kwa kuwa na kiwango cha chini cha elimu na kazi duni anazozifanya. Dadi anaamini kuwa ingawa hakusoma sana shuleni yeye si mjinga hivyo ana uwezo wakutambua mambo mbalimbali ila Kidawa ana kisomocha juu. Dadi anafanya kazi ya uchuuzi wa samaki kwavile hakusoma sana

Swali la Insha 22

  1. Eleza umuhimu wa mazungumzo kati ya Sasa na Mbura katika kujenga hadithi ya Shibe inatumaliza. Alama 10
  2. Fafanua jinsi suala la malezi lilivyoshughulikiwa katika hadithi ya Tulipokutana Tena na Mtihani wa Maisha. Alama 10
  1. Umuhimu wa Mazungumzo kati ya Sasa na Mbura katika Kujenga Hadithi ya Shibe Inatumaliza
    1. Yanaibua suala la ubadhirifu wa mali ya umma-jungu linateremshwa kwa gari la ikulu uk.39
    2. Ubinafsi na ulafi unajitokeza-wana vyao kisha pia ni wenye vyetu uk. 40
    3. Yanaonyesha namna viongozi wanavyoshiriki katika ubadhirifu wa mali ya umma. Sasa anamwambia mbura wawahi chakula/walijaza vyakula kwenye sahani zao.
    4. Yanaidhihirisha ufaafu wa anwani-Wanakula lakini hawashibi. Uk. 41
    5. Yanachimuza madhara ya kula sana-sukari, presha, saratani na kadhalika.
    6. Yanaonyesha umuhimu wa vyombo vya habari katika kukomesha hali ubadhirifu wa mali ya umma.-sasa alishtuka
    7. Yanaendeleza ploti ya hadithi-yanaibua masuala yanayoshughulikiwa katika hadithi. Swala la shibe kwa jumla.
      Zozote 5x2=10
  2. Namna Suala la Malezi Lilivyoshughulikiwa katika hadithi ya Tulipokutana Tena na Mtihani wa Maisha.
    Tulipokutana Tena
    1. Wazazi wa Bogoa wanayakwepa majukumu ya ulezi na kumpokeza Bogoa Bi. Sinai.
    2. Wazazi wa Bogoa wanashindwa kumudu mahitaji ya kumsingi kutokana na umaskini wao kv sabuni.
    3. Walezi wa watoto wanawadhulumu. Bi. Sinai anamtumikisha Bogoa; anamchoma.
    4. Walezi wanawabagua watoto; watoto wengine wanasoma ilhali Bogoa hapelekwi shuleni. Anachoma mandazi.
    5. Walezi wanawatisha watoto. Bi. Sinai anamwonya Bogoa dhidi ya kusema madhila aliyopitia mikononi mwake.
    6. Wazazi wanawadanganya watoto-Babake Bogoa anamdanganya kuwa angempeleka kwa marafiki zake ambao ni watu wazuri. Kumbe ni katili.-Bi. Sinai.
    7. Watoto wanatengwa na familia zao bila hiari yao-Bogoa analia san asana wanapotaka kumpeleka kwa marafiki zao lakini hasikizwi na wazazi. Uk. 114
    8. Baadhi ya wazazi wanawasomesha wanao. Kuna wanafunzi katika shule ambamo Bogoa aliuza mandazi.

Swali la Insha 23

Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki. (al.20)

TUMBO LISILOSHIBA.

  1. Viongozi kuweka vitego na vikwazo vya sheria ili watuwadogo wasiweze kutetea mali zao.
  2. Kutowahusisha maskini katika maamuzi muhimu yanayoathiri maisha yao.
  3. Kunyakua ardhi ya madongoporomoka ambapo watumaskini waliishi.
  4. Kupanga njama za kuwapatia wanyonge visenti vichache iliwaondoke madongoporomoka.
  5. Jitu la miraba mine kula chakula chote bila kubakishiawateja.
  6. Wanamadongoporomoka kubomolewa vibanda vyao namabuldoza.
  7. Askari wa baraza kutimua watu waliokuwawanabomolewa .
  8. Jeshi la polisi kulinda askari wa baraza wakibomoavibanda vya wanamadongoporomoka.ix
  9. Askari kuwapiga virungu watu.

SHIBE INATUMALIZA.

  1. Mzee mambo kulipwa kwa vyeo viwili alivyovifanyia kazi.
  2. Waajiriwa kwenda kazini na kukosa kufanya kazi.
  3. Viongozi kuibia wananchi kwa kujipakulia mshahara
  4. Waajiriwa wawili kufanya kazi moja – Sasa na Mbura nimawaziri wa wizara moja.
  5. Mzee mambo kuandaa sherehe ya kuingiza watoto nasarikwa kutumia pesa za umma.
  6. Mzee mambo kuandaa sherehe kwa kutumia rasimali zanchi- magari, vyakula.
  7. Sasa na mbura kula vyakula vyao na vya wenzao.

Swali la Insha 24

Kwa kurejelea hadithi ya mapenzi ya kifaurongo na shogake dada ana ndevu fafanua changamoto zinazowakumba vijana. (al.20)

  1. MAPENZI YA KIFAURONGO.
    • Dennis na wanafunzi wengine wanakaliwa na ugumu wa masomo katika chuo kikuu.
    • Umaskini matatiza masomo na mapenzi ya dennis machora.
    • Utabaka baina ya wanafunzi chuoni.
    • Ukosefu wa ajira baada ya kuhitimu chuo kikuu kwa Dennis na penina.
    • Mapuuza ya wahadhiri k.m Dkt. Mabonga.
    • Migogoro ya mapenzi rafiki wa kwanza wa penina wanatengana na pia tunamwona penina wakitengana na Dennis.
    • Kutamauka masomo chuoni yanakuwa unagumu kiasi kwamba wanafunzi wanaiali kufanya matatu na kukusanya kodi.
    • Njaa- Dennis alikuwa na unga wa kutengeneza uji kikombe kimoja bila sukari.Kuna mapenzi ya kiholela miongoni mwa wanafunzi wa chuo kikuu, walitembea wakishikana mabega.
    • Shirikizo la rika – dennis alitamani kuvaa kama wenzake na vile vile kuwa na vifaa vya kieletroniki kama vya wenzake. ( zozote 10x1)

  2. SHOGAKE DADA ANA NDEVU.
    1. Mapenzi miongoni mwa wanafunzi yanaathiri masomo yao.
    2. Mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi k.m safia.
    3. Kuna uavyaji wa mimba. K.m safia .
    4. Mauti kifo cha safia.
    5. Unafiki wa kidini k.m safia na kimwana.
    6. Mapuuza ya wazazi yanapelekea watoto wao kupotoka kimaadili.
    7. Kuna undanganyifu wa vijana kwa wazazi wao k.m safia kumdanganya mamake.
    8. Kuna utovu wa maadili miongoni mwa vijana k.m mkadi alikuwa na vitendo viovu kushinda shetani.
    9. Vijana wanapata changamoto katika maandalizi ya mtihani wa mwisho ndipo safia wanaungana kudurusu pamoja na kimwana.
    10. Kutokuwepo kwa mawasiliano baina ya wazazi na watoto wao unawakosesha maelekezi mema.

Swali la Insha 25

Kwa kurejelea hadithi zifuatazo,jadili changamoto wanazopitia Watoto; (alama 20)

  1. Tulipokutana Tena
  2. Mame Bakari
  3. Ndoto ya Mashaka
  1. Tulipokutana Tena
    • Bogoa ananyimwa haki ya kulelewa na wazazi wake na kupelekwa kwa Bi Sinai
    • watoto kukosa mapenzi ya walezi wao. Bogoa anasema kwa Bi Sinai kulikuwa Jehanamu, alitukanwa
    • watoto kunyimwa haki ya elimu. Bogoa hakupata nafasi ya kusoma; anafurahi anapofundishwa Abjadi na Sebu
    • watoto kunyimwa haki ya kucheza Bogoa alikatazwa kucheza na watoto wengine na Bi Sinai
    • watoto kutumikishwa; Bogoa anatumiwa na Bi Sinai kupika maandazi kisha kuyauza shuleni
    • watoto kudanganywa ; Bogoa alidanganywa na babake akikubali kwenda kuishi kwa rafiki yake angekula vizuri avae vizuri na kupelekwa shule. Huu ulikuwa uongo .
    • watoto kutopewa nafasi ya kujieleza. Babake Bogoa anakosa kumsikiliza alipokuwa akijieleza kuwa hakutaka kwenda mjini – Babake anatisha kumchapa
    • watoto kutenganishwa na ndugu zao
    • watoto kutopewa lishe bora; Bogoa alipewa makombo baada ya kila mtu kula; alikula kwenye sufuria wengine wakila sahanini
    • Bogoa anatenganishwa na ndugu zake anapopelekwa kwa Bi Sinai
    • Watoto kukosa mahitaji ya msingi, Bogoa kukosa hata sabuni, mavazi na viatu
      (anatembea miguu safari ndefu bila viatu)
    • kudhulumiwa – kuchomwa

  2. Mamake Bakari
    • Watoto kudhulumiwa kimapenzi Sara anabakwa na janadume anapotoka kudurusu twisheni
    • Watoto kutoaminiwa, Sara anasema kuwa hata angemwambia babake kwamba amebakwa hangemwamini
    • Watoto kufukuzwa shuleni; Sara anasema kwamba angakabidhiwa barua ya kufukuzwa shuleni “Hatufundishi wanawake hapa tunafundisha wasichana”
    • Watoto kutengwa na wenzao, Sara anasema kuwa wanafunzi wengi wangemtenga kama mgonjwa wa ukoma wangebaini kuwa ni mjamzito

  3. Ndoto Ya Mashaka
    • Watoto kuwa mayatima, Mashaka anaachawa na wazazi wake wanapofariki
    • Ajira ya watoto – Mashaka anajihusisha na kazi ya vibarua ili kusaidiana na Biti Kidebe
    • Watoto kulelewa katika mazingira duni – mazingira ni machafu na hapakaliki
    • Wakati wa mvua – watoto wa Mashaka na Waridi wanateseka
    • Watoto kukumbwa na umaskini – watoto wa Mashaka na Waridi wanaishi maisha ya kimaskini, hawana malazi, wanalala katika chumba cha Jirani yao (Chakupewa)
    • Watoto kutenganishwa na wazazi wao waridi anawatenganisha watoto na baba yao wanapoenda Yemeni

Swali la Insha 26

  1. Eleza umuhimu wa mazungumzo kati ya Sasa na Mbura katika kujenga hadithi ya Shibe inatumaliza. Alama 10
  2. Fafanua jinsi suala la malezi lilivyoshughulikiwa katika hadithi ya Tulipokutana Tena na Mtihani wa Maisha. Alama 10
  1. Umuhimu wa Mazungumzo kati ya Sasa na Mbura katika Kujenga Hadithi ya Shibe Inatumaliza
    1. Yanaibua suala la ubadhirifu wa mali ya umma-jungu linateremshwa kwa gari la ikulu uk.39
    2. Ubinafsi na ulafi unajitokeza-wana vyao kisha pia ni wenye vyetu uk. 40
    3. Yanaonyesha namna viongozi wanavyoshiriki katika ubadhirifu wa mali ya umma. Sasa anamwambia mbura wawahi chakula/walijaza vyakula kwenye sahani zao.
    4. Yanaidhihirisha ufaafu wa anwani-Wanakula lakini hawashibi. Uk. 41
    5. Yanachimuza madhara ya kula sana-sukari, presha, saratani na kadhalika.
    6. Yanaonyesha umuhimu wa vyombo vya habari katika kukomesha hali ubadhirifu wa mali ya umma.-sasa alishtuka
    7. Yanaendeleza ploti ya hadithi-yanaibua masuala yanayoshughulikiwa katika hadithi. Swala la shibe kwa jumla.
      Zozote 5x2=10
  2. Namna Suala la Malezi Lilivyoshughulikiwa katika hadithi ya Tulipokutana Tena na Mtihani wa Maisha.
    Tulipokutana Tena
    1. Wazazi wa Bogoa wanayakwepa majukumu ya ulezi na kumpokeza Bogoa Bi. Sinai.
    2. Wazazi wa Bogoa wanashindwa kumudu mahitaji ya kumsingi kutokana na umaskini wao kv sabuni.
    3. Walezi wa watoto wanawadhulumu. Bi. Sinai anamtumikisha Bogoa; anamchoma.
    4. Walezi wanawabagua watoto; watoto wengine wanasoma ilhali Bogoa hapelekwi shuleni. Anachoma mandazi.
    5. Walezi wanawatisha watoto. Bi. Sinai anamwonya Bogoa dhidi ya kusema madhila aliyopitia mikononi mwake.
    6. Wazazi wanawadanganya watoto-Babake Bogoa anamdanganya kuwa angempeleka kwa marafiki zake ambao ni watu wazuri. Kumbe ni katili.-Bi. Sinai.
    7. Watoto wanatengwa na familia zao bila hiari yao-Bogoa analia san asana wanapotaka kumpeleka kwa marafiki zao lakini hasikizwi na wazazi. Uk. 114
    8. Baadhi ya wazazi wanawasomesha wanao. Kuna wanafunzi katika shule ambamo Bogoa aliuza mandazi.
      5x1=5

Mtihani wa Maisha

  1. Watoto wanapelekwa shuleni bila kubaguliwa. Babake Samueli anawasomesha ndugu zake wa kike. Pia Samweli anasomeshwa.
  2. Wazazi kuamini kuwa kufeli katika mtihani wa shuleni ni kufeli katika mtihani wa maisha. Kwa mfano babake Samueli anaamini alifeli mtihani. Anafaa kufa.
  3. Wazazi kuamini kuwa kusomesha mtoto wa kiume ndiko kunakoweza kuwakwamua kutoka katika lindi la umaskini. Babake Samueli anaamini kuwa kumsomesha Samweli kungemwopoa kutoka katik umaskini.
  4. Watoto kuwadanganya wazazi. Baba Samwuli haamini.
  5. Mama Samueli anamwonyesha mwanawe upendo. Hataki ajiue.
  6. Watoto wanafahamu hulka za wazazi wao. Samueli anajua mama angemwelewa ilhali baba angempiga kinyama kwa kufeli mtihani.
  7. Watoto wanashiriki katika mahusiano ya kiholela wakiwa shuleni. Samueli na Nina.
  8. Wazazi wanajaribu kila juhudi kuwasomesha watoto wao hata katika hali ya umaskini. Baba Samueli anauza takribani kila kitu kuwasomesha.

Swali la Insha 27

Shogake dada ana ndevu Alifa Chokocho
Jadili sifa kumi za Safia (al. 20)

  • Huyu ni binti wa Bw. Masudi na Bi. Hamida.
  • Anasifika mno kwa tabia yake nzuri isiyokuwa na doa lolote.
  • Katika masomo yake alikuwa anaiongoza darasa
  • Ana kipawa cha uzingativu wa kiwango cha juu.
  • Ni msaidizi wa mama yake Bi. Hamida
  • Anamudu kazi zote za nyumbani
  • Anazifanya bila manung'uniko yoyote 
  • Ni mwenye tamaa: anatamani kufanya mapenzi na akatumia hila kutimiza lengo lake .
  • Alikuwa amejivika ngazi ya kondoo nje, ndani mbwa mwitu
  • Ni mjanja: anatumia maarifa na hila za kila namna ili kupata fursa ya kufanya mapenzi
  • Ni mwenye hasira: Bi Hamida anapomdadisi kuhusu hali yake ya kutapika, anapandisha hasira na kukimbia chumbani mwake.
  • Ni mwongo anadanganya kuwa ana malaria sugu
  • Anadanganya kuwa Kimwana anakuja ili wajadiliane kumbe anayekuja ni mvulana mwenye ndevu ndevu na wanafanya mapenzi
  • Ni muuaji anatoa mimba na kukidhulumu kiume kisicho na hatia. Mambo hayakwenda sawa na yeye akafariki
  • Ana ubinafsi: anafikiria yeye tu bila kujua madera ya kiumbe kilichomo ndani tumboni mwake
  • Ni mchangamfu: 'eye ana tabia ya uchangamfu ndiyo sababu mama aliyabaini mabadiliko haraka

Swali la Insha 28

Jadili suala la uozo wa maadili katika jamii huku ukirejelea hadithi zozote nne katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (alama 20)

Mapenzi ya Kifaurongo

  • Maadili ya walimu na wakufunzi yameanza kurora. Dkt. Mabonga ndiye mhadhiri. Dkt. Mabonga anawakata wanafunzi tamaa ya kukisoma Kiswahili. Hayajibu maswali wanayomuuliza kwa kuyaona kuwa maswali ya wanafunzi wa kidato cha kwanza. Aidha, anawataka wautumie msamiati wake ambao wanafunzi wengi wanauona kuwa usiku wa giza.
  • Chuoni, Dennis anakumbwa na tatizo kubwa la utabaka. Wanafunzi kutoka familia zenye nafasi walikuwa na simu za thamani, wengine walibeba vipakatalishi na iPad zao mikononi (uk 13) huku naye asiweze kupata hata chochote. Umaskini huu ulileta mpaka kati ya wanafunzi maskini na tajiri wasiweze kukaribiana.
  • Kuna mapenzi ya kiholela baina ya wanafunzi. Siku moja Dennis akiwa chumbani mwake baada ya kupika uji wa mahindi bila sukari kutokana na umaskini wake, Penina, binti yake Bw. Kitime, Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Afya (uk 19) anabisha mlangoni pake.
  • Penina anamweleza kuwa lengo la kuja kwake ni kumtaka wawe wapenzi. Anamweleza hadharani kuwa kando na mapenzi ya wazazi, kuna mapenzi mengine anayoyakosa na anayataka kutoka kwake Dennis. Dennis anasita kujihusisha kwa mapenzi na msichana huyu wa kitajiri kwa kuhofu kutemwa tena; mapenzi ya kifaurongo.
  • Wanakuwa kwenye mapenzi. Mapenzi yao yanadumu kwa muda wa miaka miwili. Wanapomaliza chuo, wanahamia kwenye mtaa wa watu wa pato la wastani, Newzealand, licha ya kuwa hawajapata kazi. Wazazi wake Penina wanawalipia kodi.
  • Dennis anatafuta kazi kwa kila njia bila mafanikio. Anakosa kazi katika shirika la uchapishaji magazeti kwa kushindwa kujibu swali moja la kwanza.
  • Kukosa kazi kunamfanya Penina kumwamrisha asanye kila kilicho chake na aondoke. Akamfukuza na kumtaka aione nyumba yake paa. Mapenzi ya kifaurongo yakatimia mwisho wake

    Shogake Dada Ana Ndevu
  • Safia ni mwanawe Bw. Masudi na Bi Hamida. Yupo shule ya msingi akisubiri kufanya mtihani wa kujiunga na shule ya upili. Ni msichana hodari sana masomoni; kila mtihani akishika nambari ya kwanza.
  • Wazazi wake Safia, hasa Bi Hamida anamwonea mwanawe fahari na kujawa na kiburi kinachomfanya kuwasimanga wasichana wa wazazi wengine walioshindwa kujitunza kama Safia wake, aliyejitandaza ushungi na kujifunika hata awapo nyumbani. Bi Hamida anamhurumia Mkadi, mtoto wa Habiba Chechei (uk 29), tabia zake ni za dosari.
  • Safia anawaomba wazazi wake ruhusa wamkubalie amlete shogake; Kimwana, nyumbani kwao ili wadurusu naye   masomo. Wazazi wake wanamkubalia ombi lake.
  • Kimwana akawa yuaja amejitandaza kila mahali kama ilivyo desturi yao. Wazazi wake Safia wakawashauri wawe     wakijifungia ndani wanapodurusu ili wasisumbuliwe na watoto.
  • Siku zilipopita, Safia akaanza kubadilika na kutapika. Wazazi wake wakamshuku lakini wakaamua kuwa si vyema   kumwazia mtoto wao vibaya.
  • Kitendawili kiliteguliwa na Lulua – kidugu chake Safia. Kitoto hiki kilimweleza mamake kuwa siku moja Subira         alipokuja kucheza nao mchezo wa kujificha, alienda chumbani kwa dadake kujificha. Alimpata Safia amelala kitandani na shogake Kimwana; naye kimwana alikuwa na ndevu.
  • Simu ya mkononi ya Bwana Masudi ilipoita na kuipokea, anapata habari kuwa Safia kafariki katika kliniki alikoenda kuavya mimba.

    Mame Bakari
  • Hadithi hii inamhusu Sara. Anakumbuka kisa kilichomtokea zamani na kumwacha kwenye huzuni na uchungu. Alitamani jambo hili lisingekuwa la kweli.
  • Analikumbuka janadume lililomvizia siku moja akitoka darasa la ziada (twisheni), likamwangusha na kumbaka kisha likamwacha amezirai. Anapoamka ndipo anapogundua kuwa amebakwa.
  • Tokeo la kisa hiki ni kwamba Sara alipata ujauzito. Aliogopa kumwambia baba yake kwa kuhofia kukaripiwa na hata kufukuzwa nyumbani. Aliogopa kutengwa na kusemwa na jamii.
  • Aliwaza jinsi mwalimu mkuu angemfukuza shule. Aliwaza jinsi dunia ilivyobadilika na kumkandamiza mwanamke hata awe ndiye mdhulumiwa. Jamii inamkweza mwanamume licha ya ukatili wake.
  • Baada ya tafakuri, Sara anaamua kumdokezea rafiki yake, Sarina, kuhusu matatizo yake. Wanakubaliana kuyaweka siri hadi Sara atakapojifungua. Sarina anamhudumia Sara kwa moyo na ari wakisubiri siku iwadie ajifungue.
  • Siku moja Sara na Sarina walimhadithia Beluwa (dadake Sarina – daktari) kuhusu kisa cha Sara. Beluwa akaahidi kuwa akimhudumia Sara mara kwa mara. Aliahidi kuliweka jambo hili siri.
  • Siku moja Beluwa alimtaka Sara kufika hospitalini kwake kwa matibabu zaidi. Sara na Sarina waliandamana hadi       hospitalini ambako walimkuta babake Sara na mamake wakimsubiri.
  • Sara alipigwa na bumbuazi asijue la kufanya. Aligutuka hajielewi. Aliporudiwa na fahamu, babake anamnyamazisha na kumweleza kuwa kosa si lake. Anamtaka Sara ajifungue mtoto wa kike awe ‘Mame Bakari’, mkewe wa utani. Malipo yote ya kuutunza ujauzito wa Sara yaligharamiwa na babake hadi akajifungua.
  • Mtoto alipozaliwa kuliandaliwa sherehe. Watu wengi wakawa wanasherehekea mafanikio ya Sara. Mara kelele zikaanikiza kutoka nje. Sara alipotoka, alikuta ni lile janadume lililombaka limekabiliwa na umati. Anachukua tofali     kulimaliza lakini analihurumia. Ghafla, umati unalivamia na kuliangamiza.Nizikeni Papa Hapa
  • Suala la mapenzi ya kiholela miongoni mwa vijana limechacha. Otii amepelekwa hospitalini madaktari wakashindwa kumponya na kuamuru arudishwe nyumbani. Amekonda sana.
  • Wanachama wa Chama cha Watu wa Nyumbani wanakusanyika na kuanza kujadiliana jinsi ya kuchangisha pesa za kununua jeneza, mavazi ya kumvisha maiti pamoja na pesa za kukodisha magari ya kumchukua maiti hadi kwao Sidindi, karibu na Kisumu ilhali Otii angali hai. Otii anawaeleza kuwa anataka akifa azikwe palepale Kisumu Ndogo. Mwenyekiti wa Chama cha Watu wa Nyumbani anampuuza.
  • Pale kitandani Otii anaukumbuka wakati wake akiichezea Bandari FC. Alikuwa mchezaji hodari na tegemeo. Watangazaji wote wa kandanda walimwangazia. Aidha, aliichezea timu ya taifa, Harambee Stars.
  • Alicheza kwa kujituma hadi mambo yalipoharibika alipovunjika mguu kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza – Tanzania wakati wa mechi ya nusu fainali kuwania kombe la klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati. Alikuwa karibu kuwafunga wapinzani wake Yanga alipovunjwa mguu.
  • Baada ya kupona, Otii akaamua kuasi soka na kuanza kazi ya mshahara duni katika Halmashauri ya Bandari kutokana na kutelekezwa na serikali na Bandari FC.
  • Siku moja akiwa kwenye klabu, anadondokewa na Rehema Wanjiru na mwishowe wanakuwa wapenzi. Rafikiye Otii anamwonya dhidi ya wasichana warembo wa Mombasa. Otii anajilinganisha na nzi afiaye kidondani na kukiri kuwa hamwachi Rehema. Wanashiriki ngono isiyo na kinga.
  • Muda mrefu unapita bila Otii kuonana na Rehema wake. Baadaye anaelezwa kuwa Rehema alirudi kwao Meru; bila hata kumuaga. Aidha, anapata habari kuwa Rehema ni mgonjwa na muda mfupi baadaye anapata khabari za kifo cha Rehema.
  • Otii naye anaanza kuona dalili za ugonjwa wake. Hana udole. Anaendesha, vipele mwilini, kukohoa kusikokoma. Otii aliugua kwa miaka minne. Kabla ya kifo chake, alitoa kauli moja tu “Nizikeni papa hapa.”
  • Wanachama wa Chama cha Watu wa Nyumbani waliutia mwili wa Otii kwenye jeneza la kifahari na magari yakaanza safari ya kuupeleka mwili nyumbani kwao Sidindi. Gari linapofika Mtito Andei, kunatokea ajali mbaya inayosababisha kifo cha watu arubaini baada ya magari sita kusagikasagika. Mwenyekiti wa Chama cha Watu wa Nyumbani anaponea   bila jeraha lolote. Anajuta mbona hakuusikia wito wa Otii aliyesisitiza.

Swali la Insha 29

Fafanua jinsi suala la elimu limeshughulikiwa katika Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine kwa kurejelea hadidhi zifuatazo:

  1. Mapenzi ya Kifaurongo                                                                             (alama 5)
  2. Shogake Dada ana Ndevu                                                                               (alama 5)
  3. Mtihani wa Maisha                                                                                         (alama 5)
  4. Mwalimu Mstaafu                                                                                           (alama 5)
  1. Mapenzi ya kifaurongo
    • Dennis anasema kuwa wazazi wake wamejitaabisha ili apate elimu
    • Dkt. Mabonga yumo ukumbini anasomesha somo la Fasihi
    • Dennis anasema kuwa wengi wa wanafunzi wenzake walisomea katika shule za mkoa na kitaifa
    • Mwanzoni mwa hadithi, wanafunzi wamo darasani wakifunzwa somo la Fasihi
    • Msimuli anaeleza kuwa kuna watu waliosoma sana kama Dkt. Mabonga
    • Elimu inatarajiwa kuwa nyenzo ya kuboresha maisha.Denis anatarajia kuwa akifuzu masomoni, Somo la Kiswahili litamfaa hasa kuwa mwandishi mtajika wa kazi ya fasihi
    • Dennis anapoenda kutafuta ajira anakutana na Shakila, msichana waliyekuwa wakisoma pamoja katika Chuo Kikuu cha Kivukoni
    • Katika jamii husika, elimu inatarajiwa kumwezesha mtu kupata ajira-Dennis anaenda kutafuta ajira akiwa na vyeti vyake vya elimu
  2. Shogake Dada ana Ndevu
    • Safia ni mwanafunzi anayetarajiwa kufanya mtihani ya kuingia kidato cha kwanza
    • Safia huibuka wa kwanza kabisa darasani- tunaelezwa kuwa ni hodari masomoni
    • Safia anawaomba wazazi wake ruhusa ya kumleta Kimwana nyumbani ili wadurusu pamoja
    • Wazazi wa Safia wanamshauri kuwa wawe wakifunga mlango kwa ndani wanapodurusu na Kimwana ili wasisumbuliwe na dadake mdogo
    • Kuna elimu ya dini-Bwana Masudi anasema kuwa Safia anatawaliwa na zile staha za kumwogopa Mungu kwa mujibu wa sheria, kanuni na amri zote alizoamrisha Mungu kupitia dini yao
  3. Mtihani wa Maisha
    • Samueli yuko kwenye foleni ya kuyaona matokeo yake ya mtihani wa kidato cha nne
    • Dada zake Samueli walipasi mitihani yao ya kidato cha nne kwenye Shule ya Upili ya Busukalala
    • Dadake Samueli, Bilha,ni mwanafunzi wa katika Chuo Kkuu cha Kenyatta naye Mwajuma ni mwanafunzi katika Chuo cha Ualimu cha Eregi
    • Elimu inatarajiwa kuwa nguzo ya kujikwamua kutoka kwa umaskini kwani mamake Smueli ana matumaini kuwa Samueli akifaulu masomoni basi hali yao ya maisha itakuwa bora
    • Samueli anapochukua matokeo yake wanafunzi ambao ndio mwanzo wamemaliza kipindi cha mwisho wanamzunguka wakitaka kujua alichopata
    • Kutofuzu katika elimu kunakatisha tamaa kwani babake Samueli anamhimiza ajitie kitanzi kwa sababu ameanguka mitihani
  4. Mwalimu Mstaafu
    • Mwalimu Mosi ni mwalimu mstaafu aliyewafunza wanafunzi wengi walioshia kufaulu maishani
    • Elimu ni mhimili mkuu katikakuboresha maisha kwani kuna wengi walioelimishwa na Mwalimu Mosi na sasa wana vyeo mbalimbali
    • Wanafunzi wa Mwalimu Mosi hawamsahau kwa nasaha, hekima na ustaarabu wake
    • Mwalimu Mosi hutaka kuandika tawasifu yake kuhusu maisha yake alivyosoma hadi chuo cha ualimu na kufundisha kwa zaidi ya miaka thelathini

Swali la Insha 30

Ukirejelea hadithi zifuatazo kwenye Diwani, eleza jinsi maudhui ya umaskini yanavyojitokeza. (al.20)

  1. Tumbo Lisiloshiba.
  2. Mapenzi ya kifaurongo.
  3. Ndoto ya mashaka.
  4. Mtihani wa maisha.
  1. Ukirejelea hadithi zifuatazo kwenye Diwani, eleza jinsi maudhui ya umaskini yanavyojitokeza. (al.20)
    • Wenyeji wa madongoporomoka waliishi kwa vibanda.
    • Walikosihi watu wepesi wasio na mashiko.
    • Watu wadogo (maskini) wanawekewa mitego na vikwazo vya sheria ili mali yao inyakuliwe.
    • Maskini wanafinywa kama takataka na matajiri, jambo linalowakasirisha- mzee mego
    • Ardhi ya maskini (wasiokuwa na nguvu ) lazima inayakuliwe.
    • Eneo la madongoporomoka (wanakoishi) Lina vibanda vinavyozungukwa na uozo na bubujiko la maji machafu.
    • Mzee mego na wenzake wanakumyua chai kwenye mkahawa mshenzi (hali duni)
      Hawakuhusishwa /kushauriwa katika ujenzi wa taifa.
  2. Mapenzi ya kifaurongo.
    • Dennis anaweza kuhuzu asili yake ya kimaskini.
    • Wazazi wa Dennis huamka asubuhikutafuta vibarua vya kuwalimia matajiri mashamba.
    • Dennis anasema kuwa wazazi wake hawana mahitaji.
    • Shuka zilizotandikwa kitandan imwa Denis zimezeeka na kuchanikachanika.
    • Dennis anatafunwa na njaa – mchele umekwisha, anapika uji
  3. Ndoto ya mashaka
    • Mashaka anafanya kazi za vibaraua almuradi wajikimu na mamake (biti Kidebe)
    • Walipewa vishamba vya kulima ili wapate chakula.
    • Mashaka na waridi wanapoona hawakuwa na chochote (siku hiyo hatuna hili na lile).
    • Waliishi kwa chumba kimoja kwa muda mrefu tangu waowane.
    • Chumba cha kupangwa (watu tisa)
    • Mabinti walibanana kwenye kitanda kidogo na wavulana walioweza kwa jirani.
    • Walikaa karibu na choo ambacho hufurika mvua inaponyesha.
    • Mashaka anakula kiporo wakati wa chamcha
  4. Mtihani wa maisha
    • Samueli anatembea kilomita sita kwenda shule kutwa.
    • Samueli anatazamia kukwamua familia yake kwenye umaskini.
    • Baba Samueli anauza ng’ombe kumsomesha Samueli.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Maswali na Majibu ya Insha katika Tumbo Lisiloshiba.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest