Kenya Certificate Of Secondary Education (KCSE 2009) Kiswahili Karatasi ya Tatu

Share via Whatsapp
  1. RIWAYA
    UTENGANO: S.A Mohamed

    Swali la lazima

    "Katu asingajitia kibuibui na kutanga na njia. Lo, kuchoshwa na shimiri za baruti anazoshindiliwa moyoni mwake."
    1. Eleza  muktadha wa dondoo hili (alama 4)
    2. Taja na ufafanue tamathali ya usemi iliyotumika katika dondo hili. (alama 4)
    3. Eleza umuhimu wa kisa kinachorejelewa na dondoo. (alama 4)
    4. Kwa kurejelea matukio mengine katika riwaya ya Utengano, Fafanua maudhui mawili yanayoashiriwa na dondoo hili. (alama 8)

  2. USHAIRI
    Jibu swali la 2 au la 3
    Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata:

    KIBARUWA; Abdilatif Abdalla

    Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa!
    Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo kunweshezewa
    Kwenye shamba hilo kubwa sasa imeshaiva kahawa
    Na bunize ni matone ya damu yangu niliyotowa
    Ndipo mte ukatipuza!

    Buni hiyo itakaangwa buni hiyo itapondwapondwa
    Buni hiyo itasagwa na buni hiyo itafyondwafyondwa
    Bali itabaki nyeusi kama ngozi yangu Kibaruwa

    Waulize ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
    Iulize na mtio kwa furaha maji itiririkao
    Uulize na upepo mkali kwa ghadhabu uvumao

    Viulize: Ni nani araukaye na mapema kuzitema mbuga na kuzilaza?
    Viulize: Ni nani akweaye minazi tangu kuchapo hadi lingiapo giza?
    Viulize: ni nani abebeshwaye mizigo hadi maungo yakageuka shaza?
    Halafuye hana faida moja apatayo wala malipo yanayotosheleza-
    Isipokuwa kusundugwa na kutupiwa matambara na vyakula viliyooza?
    Viulize: Ni nani huyo ni nani!

    Viulize: Ni nani ayalimaye mashamba na kuyapaliliya?
    Na mimea kochokocho ikajaa kwa uzito ikajinamiya?
    Hatimaye nani atajirikaye mali yakammiminikiya
    Akaota na kitambi kama mja mzito wa miezi tisiya
    Na akaongeza magari na wanawake kutoka na kuingiya?
    Viulize: Ni nani huyo ni nani!

    Na hao ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
    Nayo hiyo mito kwa furaha maji itiririkao
    na huo upeo mkali wenye ghadhabu uvumao
    Vyote hivyo vitatu vitakujibu kwa umoja wao:
    "Ni kibaruwa Manamba ndiye mtendaji hayo!"

    1. Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2)
    2. Kwa kutoa mifano, eleza aina mbili za idhini ya kishairi alizotumia mshairi. (alama 4)
    3. Kwa kurejelea ubeti wa tatu taja na ueleze tamadhali ya usemi na mbinu ya kimuundo iliyotumika. (alama 4)
    4. Huku ukitoa mifano, eleza kwa kifupi mwelekeo wa mshairi kuhusu vibarua. (alama 4)
    5. Andika ubeti wa tano katika lugha ya nathari (alama 4)
    6. Onyesha utata wa maana katika matumizi ya Kibaruwa Manamba. (alama 2)

  3. Soma shairi hili kisha ujubu maswali yanayofuata;

    Kila Mchimba Kisima
    Musa Mzenga
    1. Tenda utendapo tendo, tenda tendo kwa hekima,
      Lindamane mwenendo, sawa na yako kalima,
      Kalima yenye upendo, kufurahisha mtima,
            Kila mchimba kisima,budi huingia mwenyewe.

    2. Utendapo la faraja, tendo ni yako salama,
      Ya kukupa kila tija , na ushindi wa daima,
      Upate njema daraja, duniani na kiyama,
             Kila mchimba kisima, budi huingia mwenyewe.

    3. Utendapo la miuja, tendo ni yako nakama
      Ya kukutia harija, hasara kukuandama,
      Usione afuwaja, mwanzo na yako hatima,
            Kila mchimba kisima, budi huingia mwenyewe.

    4. Nakwambia uelewe, pulika ninayosema,
      Si ari ya mwenginewe, kumnyoa kwa lazima,
      Mtu hufunza mwanawe, kwanza ajue heshima,
            Kila mchimba kisima, budi huingia mwenyewe.

    5. Nisipokwambia wewe, kukufunza kila jema,
      Kusudi nikuongowe, uepukwe na tuhuma,
      Matusi ndimi nipawe, ila na kila lawama,
             Kila mchimba kisima, budi huingia mwenyewe.

    6. Hii ni heri ujuwe, matusi kunigandama,
      Hadhi usiniuzuwe,hamithilishwa na nyama,
      Fikiri moyo utuwe, nikupapo taaluma
            Kila mchimba kisima, budi huingia mwenyewe.

    7. Shika tena utambuwe, wasia huu ni mwema,
      Matendo usipunguwe, mazuri kutenda hima,
      Yatende ubarikiwe, upawe na taadhima,
            Kila mchimba kisima, budi huingia mwenyewe.

    8. Yakupasa uchunguwe, Kila jambo kulipima,
      Upime ufafanuwe, mambo yote kwa alama,
      La kuwaka ulijuwe, Pia lipi la kuzima,
            Kila mchimba kisima, budi huingia mwenyewe.


    1. Eleza maudhui ya shairi hili. (alama 4)
    2. Ujumbe unaowasilishwa katika shairi hili una hadhira lengwa tatu. Zitaje na utoe mifano. (alama 2)
    3. Eleza umuhimu wa kipokeo kinachotumiwa katika shairi hili. (alama 4)
    4. Andika ubeti wa tano kwa lugha ya nathari. (alama 4)
    5. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi.
      1. afuwaja
      2. taaluma (alama 2)

        TAMTHILIA
        KITHAKA WA MBERIA: Kifo Kisimani

        Jibu swali la 4 au la 5


  4. Huku ukitoa mifano mwafaka, fafanua mbinu zozote kumi zinazotumiwa na utawala wa Bokono kuendeleza udhalimu katika nchi ya Butangi. (alama 20)

  5. Eleza huku ukitumia mifano mwafaka mbinu za kimtindo zifuatazo zinavyotumiwa katika tamthilia ya Kifo kisimani.
    1. Kinaya
    2. Ucheshi (alama 20)

      HADITHI FUPI
      K.W WAMITILA: Mayai Waziri wa Maradhi

      Jibu swali la 6 au la 7

  6. "Mwanamke katika Mayai Waziri wa Maradhi amefungwa katika ngome ya kijamii." Jadili. (alama 20)

    FASIHI SIMULIZI

    1. Ni nini maana ya mawaidha katika Fasihi Simulizi? (alama 2)
    2. Huku ukitoa mifano mwafaka fafanua muundo wa mawaidha katika Fasihi Simulizi. (alama 4)
    3. Eleza sifa saba za mawaidha katika Fasihi Simulizi. (alama 14)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kenya Certificate Of Secondary Education (KCSE 2009) Kiswahili Karatasi ya Tatu.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest