KCSE 2011 Kiswahili Paper 1 Questions with Marking Scheme

Share via Whatsapp
 1. Insha ya lazima.

  Wewe kama mwanafunzi umepata nafasi ya kumhoji Mkurugenzi wa habari nchini kuhusu umuhimu wa magazeti kwa wanafunzi wa shule za sekondari. Andika mahojiano hayo.

 2. “Magari ya matatu yameleta faida nyingi hapa nchini kuliko hasara.” Jadili.

 3. Pele hupewa msi kucha.

 4. Andika insha itakayomalizika kwa:
  “Nilipapia ile bilauri ya maji kwa pupa. Sikuwa na uhakika kuwa kiu yangu ingekatika.
  Nikapiga mafunda mawili, matatu. Baada ya ile bilauri yote, ndipo nilipotambua kuwa kweli maji ni uhai.”

MAAKIZO

 1. Hii ni insha ya mahojiano.
  • Mahojiano ni mojawapo ya tungo amilifu. Katika swali hili, mahojiano yanawashirikisha wahusika wawili. Mmoja, mwanafunzi (ambaye ndiye mwenye kuuliza maswali), na Mkurugenzi wa Habari ambaye ndiye anayejibu. Mhojiwa pia anaweza kuuliza maaswali ya kuchochea hoja/hisia za mhoji. Kwa mfano: Je, wewe kama kinara wa chama hiki, umechukua hatua zipi kuhakikisha kwamba wanafunzi wamenufaika kwa magazeti
  • Muundo
   • Ufungo uchukua mtindo wa tamthilia/mazungumzo. Majina ya wazungumzaji yaandikwe pembene, kisha yatengwe na mazungumzo halisi kwa kutumiua nukta pacha.
   • Sehemu tatu kuu zijitokeze
    1. Utangulizi
    2. Mwili
    3. Hitimisho
   • Katika utangulizi, mhoji na mhojiwa wasalimiane. Kisha mhoji ajitambulishe na kutambulisha mada wanayozingatia, amkaribishe mhojiwa na kumtaka kujitambulisha.
   • Katika sehemu ya mwili, mahojiano yasitawaliwe na mhusika mmoja sana. Mhoji aulize maswali ya kudadisidadisi. Mhojiwa pia anaweza kuuliza maswali ya kuchochea kuhusu mada. Tazama mfano:
    Mwanafunzi: Hujambo Bwana/Bibi.
    Mkurugenzi: Sijambo
    Mwanafunzi: Karibu katika mahojiano yetu ya leo ambapo tutaangazia umuhimu wa magazeti kwa wanafunzi wa shule za sekondari. Mimi ni Bi. Kipanga, mwenyekiti wa Chama cha Uhariri wa Magazeti hapa shuleni.
    Mkurugenzi: Nashukuru kukujua.
    Mwanafunzi: Hebu tuanze kwa wewe kujitambulisha na kueleza kuhusu kazi yako.
    Mkurugenzi:...............
  • MAUDHUI
   • Umuhimu ushirikishe: .
    • Magazeti ni nyenzo za kutolea mafunzo kwa wanafunzi. Kuna makala mengi ya kielimu yanayoweza kuwanufaisha wanafunzi.
    • Huweza kufahamisha kuhusu mambo na matukio hapa nchini na nje ya nchi.
    • Ni chombo cha kuburudisha na kuondoa uchovu wa kiakili. Makala ya michezo kama vile kujaza mraba, na soduku huweza kuburudisha.
    • Kwa mfano kupitia kwa tahariri na baarua kwa mhariri
    • Magazeti huwapa wanafunzi nafasi za kubadilishana mawazo, changamoto na tajriba zao, kwa mfano kupitia kwa tahariri na barua kwa mhariri.
    • Hushirikisha makala kuhusu utamaduni na hivyo kuwapa vijana njia ya kuwasilisha au kujifunza kuhusu utamaduni wao.
    • Matangazo ya kazi huwajuza watu kuhusu nafasi za kazi,
    • Hufunza maadili
    • Kukuza hamu ya kupenda kusoma
    • Baadhi huwa na maswali ya mitihani ambayo huwasaidia wanafunzi kudurusu.
    • Kukuza hamu ya kuwa waandishi
    • Kuna zawadi kwa wanaojibu maswali
  • Kukuza ubunifu makala kama vile tahariri huweza kuwaonyesha wanafunzi namna ya kutumia insha kwa upeo wa juu na kwa ukakamavu.
  • Katika hitimisho, mhoji amwuulize mhojiwa kutoa ushauri wake kwa wanafunzi wa shule za sekondari kuhusiana na umuhimu wa magazeti kwao.
  • Mahojiano yahitimishwe kwa mhoji kumshukuru mhojiwa na kuagana,
  • Vipengele vikuu ambavyo lazima vibainike
   • Kichwa
   • Utangulizi
   • Mwili
   • Muundo - Tamthillia/mtindo wa mazungumzo
   • Hitimisho
 2. Insha hii ni ya mjadala. Mtahiniwa aonyeshe boja za kuunga mkono na kupinga. Hoja ziweze kutetewa kwa ithibati. Kisha mtahiniwa ahitimishe kwa kuonyesha msimamo wake.
  • Muundo
   • Sehemu zifuatazo zijitokeze:
  • Utangulizi
   • Sehemu hii ionyeshe hoja za kijumla kuhusu magari ya matatu.
  • Mwili
   • Hoja zijadiliwe hapa. Tazama mifano.
  • Hoja za Kuunga mkono
   • Husaidia watu wengi ambao hawajamiliki aina yoyote ya vyombo vya usafiri kusafiri kwa wepesi.
   • Yameweza kutoa nafasi nyingi za kazi; kuanzia kwa wawekezaji, madereva, utingo, manamba, wauza vipuri vya magari na hata wanaoyatengeneza yakiharibika.
   • Huweza kujaa haraka yakilinganishwa na mabasi ambayo huchukua muda mrefu kujaa.
   • Huweza kupatikana kwa urahisi katika sehemu nyingi nchini iwe mijini au mashambani.
   • Wawekazaji wameweza kutajirika kutokana na uwekezaji wa biashara hii.
   • Ni biashara ambayo inaipa serikali kodi kubwa/mapato.
  • Hoja za kupinga
   • Matatu husababisha ajali nyingi zaidi humu kuliko magari mengine.
   • Ajali kutokana na matatu husababisha madhara mengi zaidi kama vile vifo vingi, majeruhi, kulemazwa kwa wingi, na hasara za kiuchumi.
   • Mashirika mengi ya bima hupata hasara kubwa kutokana na magari ya matatu na mengi hufilisika na kufunga biashara.
   • Biashara ya matatu huhimiza watu wengi kuwa wavivu, mathalani, mtu hawezi akatembea masafa mafupi hata kama aendako ni karibu kwa sababu magari ya matatu yako tele.
   • Biashara ya matatu imehusishwa na uzorotaji wa maadili ya kijamii. Wahudumu katika . sekta hii wamehusishwa na utumiaji na usafirishaji wa vileo kama afyuni, pombe haramu na kushiriki katika usherati.
   • Magari ya matatu husababisha msongamano barabarani hasa katika sehemu za mijini.
   • Magari ya matatu yamechangia katika uchafuzi wa mazingira kutokana na kelele za utingo, manamba na upigaji wa honi pamoja na moshi.
   • Biashara ya matatu imepotosha vijana wengi ambao wanavutiwa na kukimbilia biashara hii badala ya kuendelea na shuguli kama vile masomo yanayoweza kuwasaidia maishani pakubwa kuliko biashara hii.
  • Hitimisho:
   • Mtahiniwa aonyeshe msimamo wake kwa kueleza anaegemea katika kupinga au kuunga mkono.
 3. Hii ni insha ya methali. Methali hii ina maana kuwa upele hupewa mtu asiye na kucha kwa kuwa hana uwezo wa kujikuna. Maana ya ndani ya methali hii ni kwamba matatizo humkumba mtu ambaye hana ujuzi/uwezo /mbinu za kuyatatua.
  • Pele - Matatizo yanayomkumba mtu akakosa namna ya kuyatatua.
  • Kucha - uwezo /mbinu/njia za kutatua matatizo /ujuzi
  • Mtahiniwa aandike kisa kinachodhihirisha:
   • Mtu asiye na ujuzi wa jambo akiwa amepatikana na jambo hilo na hajui namna ya kulitatua.
    Au
   • Mtu mwenye kitu ambacho hakihitaji ilihali anayekihitaji hakipati.
    Au
   • Mtu ambaye ana uwezo na hali hapatwi na matatizo lakini yule asiye na uwezo anapatwa nayo.
 4. Hii ni insha ya mdokezo. Mtahiniwa aandike insha yenye kisa ambacho kinaonyesha akihangaika kwa kiu ya maji. Baada ya mahangaiko haya na kupata bilauri moja ya maji ndipo anapotambua umuhimu wa maji.
  • Yafuatayo yafuatwe katika kutuza swali hili.
   • Mtahiniwa aeleze hali ya kukosa maji.
   • Aeleze kilichotendeka kabla ya kupata maji.
   • Ajihusishe katika kisa.
   • Asiyejihusisha - amejitungia swali.
   • Ahusike katika hali ngumu ya kuhitaji maji.
   • Asiponukuu maneno aliyopewa, amejitungia swali,
   • Akinukuu sehemu ya maneno amejitungia swali.
   • Akiongeza sentensi moja, mbili au kifungu amejitungia swali.
   • Akiongezea maneno hadi matano aondolewe alama 2 baada ya kutuzwa.
Join our whatsapp group for latest updates

Download KCSE 2011 Kiswahili Paper 1 Questions with Marking Scheme.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest