Kiswahili - KCPE 2021 Prediction Set 4 (Questions and Answers)

Share via Whatsapp

Chagua jibu sahihi ujazie nafasi wazi 1-15.

Miaka mingi iliyopita, madola yanayostawi yamekuwa ___1___ wazalendo kutilia maanani mipango ya ___2___ uzazi na kupata wana wanaoweza__3__ barabara. Ni muhimu kwa vijana ___4___ vyema kabla ya kufunga ndoa hususan enzi kama hizi za janga ___5___ ukimwi. Zama za zama vijana ____6____ kuhusu maisha ya ndoa katika kila jamii. Vijana wa Mambosasa wanahitaji kuongozwa. Ni jambo la kushangaza na kusikitisha kuona kuwa ___7___ wavyele wamewatwika walimu jukumu ___8___ Badala ya wazazi kuwa ___9___ bora kwa watoto, wengine wao huwapotosha kwa vitendo vyao. Kila mtu ___10___ kufahamu kuwa vijana ndio tegemeo la taifa la baadaye.

kiswahili set 4 q1 10

___11___ Hadi maskanini pao kujipumzisha na kusubiri usiku ambao, kama usiku wa siku, ___12___ ulifika na kuleta huzuni na simanzi. Usiku huo ilifunika kote kwa weusi na kurudisha wasiwasi na hofu nyonyoni ___13___ Maria na Aisha. Hawakujua uhayawani upi ingewafika ___14___ mastakimu yao. Majambazi wabakaji walikuwa ____15____ siku atu mtawalia.

 kiswahili set 4 q11 15

Kutoka swali la 16 mpaka 30 jibu swali kulingana na maagizo.

  1. Darasa kwa wanafunzi ni kama ____ kwa walimu.
    A. pambajio
    B. majilisi
    C. ofisi                              
    D. maegesho
  2. Ugonjwa wa kutokwa na damu puani ni
    A. mjusi
    B. mjuzi
    C. kisunzi                          
    D. ria
  3. Chagua sentensi isiyo sahihi kisarufi:
    A. Darasani mlimofagiliwa ni safi.
    B. Uwanja kubwa kuna wachezaji wengi.
    C. Shambani palipolimwa panapendeza sana.
    D. Barabarani yote imejaa wasafiri.
  4. Chagua sentensi inayoonyesha wingi wa: "Jiko la kupikia limenunuliwa mjini."
    A. Majiko za kupikia zimenunuliwa mjini.
    B. Meko ya kupikia yamenunuliwa mijini.
    C. Majiko ya kupikia yamenunuliwa mijini.
    D. Meko za kupikia yamenunuliwa mjini.
  5. Ni sentensi ipi iliyoendelezwa vizuri?
    A. Linda alistakiwa kwa kuimba linda la Maria.
    B. Aisha alifaa nguo inayovaa akatunzwa
    C. Moshi alivuka majambazi waliowasha walipofuka barabara.
    D. Gharama ya maisha imepanda sana nazo bidhaa zimekuwa ghali.
  6. Sina mtu huyo endapo aliuawa na majambazi.
    A. yakini
    B. yamkini
    C. mujibu                          
    D. majibu
  7. Mfano wa kimilikishi katika sentensi: "Magazeti yetu mazuri ndiyo yaliyoteketea." Ni:
    A. yaliyoteketea
    B. ndiyo
    C. yetu                              
    D. mazuri
  8. Ni methali gani isiyo sawa na: 'Si vyote ving'aavyo ni dhahabu.
    A. Heri nusu shari kuliko shari kamili.
    B. Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti.
    C. Si vyote viowevu ni dhahabu.
    D. Uzuri wa kuyu ndani mabuu.
  9. Mtu akikuaga kwa kusema, 'Tuonane wiki ijayo! Utaamjibu
    A. aheri
    B. inshallah
    C. salmini                          
    D. binuru
  10. Chagua orodha ya maneno ambayo yote ni vielezi
    A. Asubuhi, pu, kijinga, maskanini
    B. Leo, kipofu, kimaskini, taratibu
    C. Dukani, mzuri, gundi, haraka
    D. Mara nyingi, kidogo, kula, au
  11. Mifano ya vivumishi vionyeshi hapa ni:
    A. Mimi, yeye, wao, nyingi
    B. hizo, change, lini, kumbe.
    C. humo, hivyo, hizi, lile
    D. zozote, nyingine, jingi, chenyewe.
  12. Nomino chuma inaorodheshwa katika ngeli ya:
    A. KI-VI
    B. LI-YA
    C. I-ZI                               
    D. I-I
  13. Ni neno gani lenye maana sawa na kumi?
    A. karne
    B. kikwi
    C. alfeni                            
    D. mwongo
  14. Ni neno gani inayoonyesha kauli ya kufanyiza? Simba
    A. anagopeka
    B. anaogofya
    C. anaogopewa                  
    D. anaogopea
  15. Taja orodha ya vivumishi tasa.
    A. Mgani, msafi, mkarimu, mnadhifu
    B. Mbona, gani, lini, nini.
    C. Ghali, safi, dhaifu, gani.
    D. Mrembo, mdogo, virefu, zuri.

Soma shairi hili kisha ujibu maswali 31 - 40

Nisemayo si dhihaka, tahadhari binadamu,
Mvuta bangi hakika, alozivuta wazimu,
Avuta akizunguka, huku zapanda stimu,
Bangi zinapomshika, huwapa mbuzi salamu.

Bangi zikikudhibiti, ulevi wake tumbaku,
Kofia hufanya koti, bata ukadhani kuku,
Kikaka cha kiberiti, ikafikiri sanduku,
Na usemapo husiti, wanena kama kasuku.

Waupoteza uhai, tahadhari makwambia,
Uivutapo hukai, ovyo wajibobokea,
Na chakula hakikai, ukilacho chapotea,
Wataka sima karai, au chapati tisia.

Kuna nayo tembo, ulevi ulo na zani,
Una udhia na mambo, na baa nyingi mwilini,
Tena huharibu umbo, na heshima kuwa duni,
Na mwendo huwa wa kombo, kwa pozi huwezekani

Tamati ni miujiza, uwapo u sakarani,
Akili hukugeuza, hujui wafanya nini,
Na ungi wa kuyajaza, masimbi mwako tumboni,
Na lugha Kiingereza, kama mtu wa Landani.

(Kutoka: Kusoma na kufahamu Mashairi. Na S. Karama na Kamal Khan. Uk wa 27)

  1. Shair hili lina vifungu vingapi?
    A. Vitano
    B. Vinane
    C. Kumi na sita                  
    D. Vinne
  2. Shairi hili ni la muundo gani?
    A. Tarbia.
    B. Takhmisa
    C. Utenzi                           
    D. Ngonjera
  3. Mshororo wa mwisho katika kila ubeti hauwezi kuitwa:
    A. Kituo
    B. Kiitikio
    C. Mkarara                        
    D. Lakabu
  4. Malenga anatuonya kuwa:
    A. Bangi humpa mtu siha njema.
    B. Bangi humfanya mtu kuwa razini.
    C. Bangi humfanya mvutaji punguani.
    D. Bangi humshangamsha mvutaji.
  5. Madhara ya bangi si pamoja na:
    A. Kuongea bila kikomo.
    B. Kula zaidi ya kiwango
    C. Kuwa na ndoto za mchana.
    D. Kupenda chapati na ugali.
  6. Mtumwa wa ugimbi kwa kawaida:
    A. Ana mwendo wa upogoupogo
    B. Hadhuriki kamwe.
    C. Hapati staha katika jamii.
    D. Hudhoofika na kuwa mgonjwa..
  7. Ubeti wa pili una mizani mingapi?
    A. Sitini na minne.
    B. Kumi na sita
    C. Minane.
    D. Minne
  8. Vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa mwisho ni:
    A. za-ka
    B. za-ni
    C. ni-za                             
    D. za-u
  9. Shairi hili lina mishororo mingapi?
    A. Sitini na minne
    B. Kumi na sita
    C. Mitano
    D. Ishirini
  10. Anwani mwafaka kwa shairi hili ni:
    A. Balaa ya ulevi
    B. pokea salamu mbuzi
    C. Mtu wa Landani
    D. Balaa ya Bangi

Soma habari hii kisha maswali 41-50

Mwalimu mkuu aliamuru kengele ya dharura igongwa. Kufumba na kufumbua wanafunzi wote wakajumuika kwenye uwanja wa gwaride. Walimu nao wakaandamana sanjari kama mchwa vichuguuni.

Wengine kutoka madarasani na wengine majilisini. Bila shaka walipiga foleni mbele ya wanafunzi jinsi ilivyokuwa ada na desturi. Uwanja ukafurika furifuri. Ungewaona ungedhania nyuki mzingani au nzi mzogani. Yakini mtu hakatai mwito aitwalo. Nayo mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo.

"Walimu na wanafunzi," alianza baada ya kukwangua mate kooni. Kuanzia saa tatu na dakika kumi na saba, nimepigaa marufuku matumizi ya Kiswahili hapa shuleni. Nyinyi walimu, nikimsikia mwalimu yeyote akiongea Kiswahili nitamkata mshahara. Shule ni yangu na kama hutaki kuwa hapa milango i wazi". Alifafanua kwa Kiingereza uchwarauchwara kilichochanganyikana na Kiswakinge na lughamama

"Wanafunzi wa shule hii sikilizeni, Kiswahili ni lugha ya Waarabu na wapumbavu. Haiwezi kukupelekea popote. Mtu yeyote akiongea lugha hii ni mshenzi. Hata wazazi wenu wangeulizwa wangesema wana wao wasifundishwe lugha hii," alifafanua kinaganaga.

"Mwalimu wa Kiswahili Bwana Mufti!" Alinigeukia, “Sitaki kusikia vipindi hivyo vya redio hapa vikisikilizwa na wanafunzi. Aidha nimekukataza kuzungumza na mwanafunzi yeyote nje ya darasa. Endapo utazungumza lazima utumie Kimombo, Pia sitaki kusikia wimbo wa taifa ukiimbwa kwa Kiswahili tena.

Muda si muda akawaita vikaragosi wake na kuwauliza wampe mjina ya wanafunzi waliozungumza Kiswahili asubuhi hiyo. Alipowapata wavulana watano, aliwaamuru wavue kaptura hadharani. Kisha aliwaadhibu kwa bakora ya ngozi ya kifaru.

Ama kwa hakika lugha ya Kiingereza ikikuwa imeshikilia mkia miaka mitatu mtawalia katika mtihani wa kitaifa. Jambo hili lilimkera Bwana Kiburi.

Je, ungalikuwa mwalimu Mufti na wanafunzi katika shule ya msingi ya Walakini ungalifanyaje? Ewe mwanafunzi hapo ulipo, utakapoadhibiwa usinyamaze. Ni haki yako kuongea Kiswahili mufti. Nenda kwenye kituo cha polisi uandikishe taarifa.

Wewe mhini hapo ulipo mtoto wako angekuwa mtangazaji kama Kaka Jos, Ken Walobora, Esther Githui na Jamila Muhammed, ungefanyaje? Na endapo angekuwa mtaalamu wa lugha kama Guru Ustadh Wallah, Dkt. K.W. Wamitila na Mathias Mumanyi? Dhuluma zii!

  1. Kengele iligongwa ili:
    A. Wanafunzi wajumuike kwenye paredi.
    B. Wanafunzi wafumukane kutoka gwarideni.
    C. Wanafunzi wahutubiwe na mwalimu Mkuu.
    D. Walimu na Wanafunzi wahutubiwe na Mwalimu Mkuu.
  2. "Walimu nao wakaandamana sanjari" maana ya kauli hii ni:
    A. enda sawasawa ubavu kwa ubavu
    B. kuandamana mmoja nyuma ya mwengine
    C. mkabala
    D. sambamba
  3. Bila shaka walipiga foleni mbele ya wanafunzi.' Ndiko kusema walimu:
    A. Walipanga mlolongo
    B. Walipiga magoti
    C. Waliketi mbele ya wanafunzi
    D. Waliwaadhibu waliopiga makelele
  4. Dharura hizi zote zilikuwa za:
    A. Kuimarisha Kiswahili
    B. Kuwaadhibu waliozungumza Kiswahili
    C. Kukataza ufundishaji wa Kiswahili
    D. Kukataza matumizi ya Kiswahili.
  5. Adhabu kwa walimu walioongea Kiswahili ingekuwa
    A. Kukatwa ujira
    B. Kuwafurusha kazini
    C. Kupiga deki sakafu
    D. Viboko na kukatwa mashahara
  6. Lugha za Mwalimu mkuu hazikuwa:
    A. Shaghalabaghala
    B. Uchwarauchwara
    C. Mufti na aula
    D. Ovyo ovyo
  7. Kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu lugha ya Kiswahili ni ya:
    A. Wataalam
    B. Zumbukuku na Waarabu
    C. Wasomi na waandishi
    D. Wakoloni
  8. Jambo lililomwudhi Mwalimu mkuu ni:
    A. Kiingereza kushika mkia shuleni
    B. Kiswahili kushikilia mkia katika taifa.
    C. Kiingereza kuwa nafasi ya mwisho kwenye mtihani wa kitaifa shuleni.
    D. Kiingereza kuwa cha mwisho shuleni na wilayani.
  9. Mwandishi anawashauri wanafunzi:
    A. Wakiadhibiwa waende kwenye kituo cha polisi.
    B. Kujua na kufahamu haki zao na kuzitetea.
    C. Kutoroka shuleni na kwenda kwenye kituo cha polisi.
    D. Kuwapiga wanaowaadhibu kwa kuongea Kiswahili.
  10. Kaka Jos, Ken Walobora, Dkt. Wamitila wote ni:
    A. Walimu wa Kiswahili
    B. Watangazaji
    C. Wataalam wa Kiswahili
    D. Walimu na watangazaji 

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa:

Andika insha . itakayomalizika kwa maneno haya:

.......Niliamini kuwa akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.

 



MAJIBU

kiswahili set 4 ms

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili - KCPE 2021 Prediction Set 4 (Questions and Answers).


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest