KCSE 2016 Kiswahili Paper 3 Questions with Marking Scheme

Share via Whatsapp

SEHEMU A: HADITHI FUPI

K. Walibora na S. A. Mohamed: Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine

 1. Lazima
  Jadili maudhui ya elimu kwa mujibu wa “Kanda la Usufi”, “Shaka ya Mambo” na “Tazama na Mauti”. (Alama 20)

SEHEMU B: RIWAYA

K. Walibora: Kidagaa Kimemwozea

Jibu swali la 2 aula 3

 1. Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya: Kidagaa Kimemwozea. (Alama 20)

 2. “Wasemao husema, atafutaye hachoki.”
  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
  2. Kauli hii ina maana gani kwa mujibu wa muktadha huu. (Alama 2)
  3. Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (Alama 14)

SEHEMU C: TAMTHILIA

T. Arege: Mstahiki Meya

Jibu swali la 4 au la 5

 1. “Anwani Mstahiki Meya ni kinaya.” Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia. (Alama 20)
 2. “.. .dawa ya adui ni kummegea unachokula.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
  2. Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa Cheneo. (Alama 16)

SEHEMU D: USHAIRI

Jibu swali la 6 aula 7

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

  Kilio cha Lugha

  Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze
  Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
  Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
  Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia,

  Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanvasa
  Hamna nami imani, wala kupanga siasa.
  Mwasema sayansini. siku ningalitosa.
  Mwanambia nikotosa. kuiva sijafika.

  Ela muelewe sana. Maamuma na Imamu.
  Mulipokuwa vijana. kwenu nilikmva timamu.
  Sasa mumesoma sana. mwaniona ni haramu.
  Mujue kuwa dawamu. utumwa mwauridhia.

  Mzaliwapo mwalia, ‘maa', maneno ya kwanza.
  Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza.
  Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza,
  Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.

  Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza,
  Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza,
  Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza,
  Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?

  Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao,
  Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
  Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
  Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.

  Enyi viongozi wetu ipangeni nadharia,
  Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
  Lugha hata ‘mbusha watu, tuche kuriaria,
  Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia.

  Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote,
  Msamiati huwa, ni wa Afrika yote,
  Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote,
  Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.

  Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi,
  Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi,
  Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
  Kwao ‘meomba kiasi, ili kujizidisha.

  Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya,
  Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya,
  Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya,
  Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia.

  Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana,
  Kukua imeridhia, msamiati kufana,
  Wengine wataijulia, kwa rnarefu na mapana,
  Lugha yenu ya maana, mwaipuuza yalia.
  1. Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu. (Alama 2)
  2. Kwa kutoa hoja nne, eleza kwa nini shairi hili likaitwa kilio cha lugha. (Alama 4)
  3. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (Alama 4)
  4. Eleza toni ya shairi hili. (Alama 2)
  5. Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu. (Alama 3)
  6. Bainisha nafsineni katika shairi. (Alama 2)
  7. Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi. (Alama 3)
   1. nasongwa
   2. kuriaria
   3. adinasi

 2. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

  T. Arege: Barabara

  Barabara bado ni ndefu
  Nami tayari nimechoka tiki
  Natamani kuketi
  Ninyooshe misuli
  Nituliza akili.

  Lakini

  Azma yanisukuma
  Mbele ikinihimiza kuendelea
  Baada ya miinuko na kuruba
  Sasa naona unyoofu wake
  Unyoofu ambao unatisha zaidi.

  Punde natumbukia katika shimo
  Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
  Ghafla nakumbuka ilivyosema
  Ile sauti zamani kidogo
  "Kuwa tayari kupanda na kushuka.”

  Ingawa nimechoka
  Jambo moja li dhahiri
  Lazima nifuate barabara
  Ingawa machweo yaingia
  Nizame na kuibuka Nipande na kushuka.

  Jambo moja nakukumbukia: Mungu
  Je. nimwombe tena? Hadi lini?
  Labda amechoshwa na ombaomba zangu
  Nashangaa tena!

  Kitu kimoja nakiamini
  Lazima niendelee kijitahidi kwa kila hatua mpya
  Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
  Nikinaswa na kujinasua
  Yumkini nitafika mwisho wake
  Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.
  1. Eleza toni ya shairi hili. (Alama 2)
  2. Tambua nafsineni katika shairi hili. (Alama 2)
  3. Mshairi ana maana gani anaposema “Kuwa tayari kupanda na kushuka” wa tatu? katika ubeti (Alama 2)
  4. Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili ukizitolea mifano mwafaka. (Alama 10)
  5. Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili. (Alama 2)
  6. Eleza maana ya: (Alama 2)
   1. kuruba
   2. barabara yenye ukungu

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

 1.  
  1.  Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii. (Alama 10)
  2. Ili kuweza kufanikisha uwasilishaji wa utanzu wa nyimbo kwa hadhira eleza mambo anayohitaji mwimbaji. (Alama 10)

MAAKIZO

SEHEMU B: RIWAYA

K. Walibora: Kidagaa Kimemwozea

Jibu swali la 2 au la 3

 1. Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya: Kidagaa Kimemwozea. (Alama 20)
  • Elimu inasaidia kuelezea hisia za mtu kupitia maandishi. Mfano - Amani ameandika mswada kuonyesha msimamo wake katika masuala tofautiElimu iliyosisitizwa ni elimu ya kujielewa. Elimu ya kujua mtu atoka wapi na anaelekea wapi kwa mujibu wa Amani. Elimu imesawiriwa kuwa muhimu licha ya utajiri na kutosheka maishani. Baada ya muda mrefu, Amani anarudi chuoni na kupata shahada ya kwanza katika Fasihi na Falsafa. Elimu ni njia ya kujipatia heshima na umaarufu. Nasaba Bora alimheshimu ndugu yake kwa uwezo wake katika lugha. Hakupenda wakati ambapo inamlazimu kusoma hotuba kwa kiingereza asichokielewa
  • Wasio na elimu wanabaki kutaabika. Mfano Chwechwe Makweche baada ya kuacha masomo katika darasa la saba na kuwa mchezaji shupavu, analemewa na maisha baada ya kuvunjika pfupaja la mguu.
  • Elimu imetumiwa kama chombo cha kuwakweza baadhi ya raia katika madaraka - kama Majisifu anapata kazi kutokana na elimu yake.
  • Elimu pia imetumiwa kama chombo cha mapinduzi kwa kutetea haki za wanyonge. Mfano - Madhubuti anapomaliza masomo yake Urusi anaungana na Amani kuleta mabadiliko Sokomoko.
  • Imani katika dini inajitokeza ambapo kila linapojitokeza jambo mbaya watu hukimbilia dini.
  • Kwa upande mwingine dini imebainishwa kama chombo cha kuadilisha.
   Mfano: babake Nasaba Bora na Majisifu aliwalea kwa mwongozo wa bibilia huku akiwasihi waishi kwa umoja na upendo.
  • Dini pia huweza kutumiwa kama hifadhi ya maovu. Kwa mujibu wa
   Majisifu maovu mengi kama vile mauaji hufanywa katika jina la Mungu kutokana na unafiki. Dini ina jukumu la kuwapoza wanaomboleza. - Dini imetekeleza jukumu la kuunganisha familia pamoja mfano: Babake Nasaba Bora alihakikisha familia yake imeunganishwa na dini.
 2. “Wasemao husema, atafutaye hachoki.”
  Haya ni maneno ya msimulizi yanamhusu
  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
   • Majuhuni aliyejitahidi kumfurahisha mpenziwe Mitchelle aliyekuwa amekataa kuolewa naye mpaka ajenge jumba la kifahari. Licha ya jitihada zake Majununi, Mitchelle alikataa kuolewa na Majununi na baadaye Maajununi akaamua kutooa kamwe
  2. Kauli hii ina maana gani kwa mujibu wa muktadha huu. (Alama 2)
   • Majununi hakufa moyo katika harakati za kutaka kumwoa Mitchelle. Alijitahidi kutimiza matakwa ya mpeni wake kwa kujenga nyumba nyingine.
  3. Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (Alama 14)
   • Imani anatafuta haki ya kunyimwa malezi ya wazazi wake waliouliwa kinyama. Imani anatafuta haki ya familia yake iliyonyanganywa shamba lao.
   • Amani anatafuta haki ya Ami yake Yusufu.
   • DJ anatafuta haki baada ya kushambuliwa na jibwa lake Nasaba Bora.
   • Amani anatafuta haki ya mswada uiiokataliwa na wachapishaji na baadaye kuchapishwa kwa jina la mtu mwingine.
   • Chwechwe Makweche anatafuta haki ya kuumia michezoni bila kufidiwa.
   • Watoto wa Majisifu wanalilia haki ya kuishi kama binadamu wengine licha ya ulemavu wao. Amani anatafuta haki ya kudhulumiwa na mtemi Nasaba Bora kwa kizingizio kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mkewe Bi Zuhura. Amani atafuta haki ya kujua waliokuwa wazazi wa kitoto Uhuru baada ya yeye kulazimishwa kukilea licha ya kuwa hakuwa babake. Amani na Imani wanatafuta haki ya kufungwa kwa kizingizio kuwa walimwuua mtoto Uhuru. Wanafunzi wa mwalimu Majisifu wanatafuta haki ya kufunzwa vyema baada ya Mwalimu wao kutohudhuria shule kwa muda mrefu. Yusufu anatafuta haki baada ya kusingiziwa kumwuua Chichiri Hamadi.
   • Raia wa Sokomoko wanatafuta haki dhidi ya Nasaba Bora anayewapokonya ardhi, mali, mabiruti na wake wao.
   • Wafungwa wanatafuta haki kwa kukosa kufikishwa mahakamani.
   • Waandishi wengi chipukizi kama Amani wanatafuta haki ya kazi zao baada ya kuibiwa miswada yao na akina Majisifu.

SEHEMU C: TAMTHILIA

T. Arege: Mstahiki Meya

Jibu swali la 4 au la 5

 1. “Anwani Mstahiki Meya ni kinaya.” Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia. (Alama 20)
  Anwani Mstahiki Meya ni kinaya kwa vile anayeitwa Mstahiki anatakiwa kuwa mtu wa kuheshimiwa. Kama kiongozi heshima hutokana na uongozi bora unaowafanya raia kuonea fahari uongozi wa kiongizi wao. Hata hivyo, Mstahiki Meya hakustahiki kuitwa kiongozi kwa sababu zifuatazo:
  • Wafanyakazi wa mji wanaendelea kufanya kazi kwa muda mrefu bila mshahara.Hospitali hazina dawa na wagonjwa wanakufa kutokana namagonjwa yanayoweza kutibiwa kwa urahisi,
  • Kuna njaa kiasi kwamba wafanya kazi wake wanakula mabaki ya chakula kutoka nyumbani mwake na kuugua.
  • Anapanga na Bili jinsi wataipunja baraza kupitia kesi ya mwenye kandarasi anayedai haki yake.
  • Anadanganya kuwa ameagiza dawa kutoka ng'ambo huku akijua fika kuwa hajaagiza.
  • Anawatenga wanaodhamiria kumsaidia kuongoza vizuri kama vile Siki na Diwani III.
  • Anaharibu aasasi za serikali kama vile hospitali huku mkewe akienda ng'ambo kujifungua.
  • Anawaita viongozi wa wafanya kazi ofisini mwake akijua kuwa hakuwa na mpango wa kushughulikia malalamiko yao.
  • Badala ya kusuluhisha matatizo yanayokumba mji wa Cheneo kwa majadiliano, anaamua kutumia vyombo vya utawala kunyamazisha upinzani.
  • Ananyakua ardhi ya umma na kujigawia pamoja na marafiki zake hasa Bili.
  • Anaidhinisha kutotozwa kodi kwa madiwani huku wafanya kazi wa kawaida wakilazimishwa kufanya kazi kwa miezi mingi bila mshahara kutokana na nakisi ya kifedha.
  • Anashiriki katika wizi wa fimbo ya Meya ishara ya mamlaka ya cheo chake.
  • Anaingilia mambo yasiyo na maana yoyote kama vile ukubwa wa mayai aliyopikiwa badala ya kushughulikia matatizo katika Cheneo kwa busara ifaayo.
  • Anakiri kudanganywa na Bili na kuwategemea madiwani ambao hawakuwa na ujuzi wa kutosha.
  • Anawahonga madiwani ili wamuunge mkono badala ya kuwatambua kama wawakilishi wa wananchi watakaompa ukweli wa mambo ili kuongoza anavyostahili.
  • Anamhonga mhubiri ili aendelee kumwombea yeye badala ya kubadili uongozi wake unaoendelea kuzorotesha hali mjini Cheneo.
  • Anaendelea kumlipa Bili kwa huduma isiyo na manufaa yoyote. Bili alijua kuwa alikuwa akimdanganya Meya na mambo yanapoharibika anatoroka pasipo kwaheri.
  • Anapogundua alidanganywa mambo yalikuwa yameharibika kiasi cha kutobadilika.
  • Anahakikisha kuwa masiahi ya kiafya ya wenye mamlaka yameshughulikiwa huku raia wake wakugua na kufa kwa ukosefu wa huduma hospitalini.
  • Anautambua urafiki wa kusifiwa zaidi ya utaaiamu. Diwani III na Siki hawakutambuliwa kwa vile katika kumwmbia Meya ukweli walionekanan kama maadui wake,
  • Anakosa kufikiria na kufanya maamuzi huru na kutokana na haya anadanganywa na waliojali masilahi yao kama Bili na Diwani ! na Diwani II.
 2. “.. .dawa ya adui ni kummegea unachokula.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4) 
   • Anayesema maneno haya ni Bili akimwambia Mstahiki Meya. Wamo ofisini mwake Mstahki Meya. Walikuwa wakizugumza kuhusu mwanakandarasi aliyekuwa ameshtaki Baraza akidai pesa zake.
  2. Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa Cheneo. (Alama 16) 
   • Dawa inayorejelewa ni ufisadi. Ufisadi umezorotesha hali katika Cheneo kwa njia mbalimbali kama:
   • Meya anaidhinisha kuongezewa mishahara kwa madiwani ili wamuunge mkono. Hazina ya baraza inamomonyoka zaidi. Madiwani hawampi ushauri wa kweli na uongozi unaanguka.
   • Meya anamgawia Bili viwanja vinne. Bili anaishia kumpa ushauri wa kuporosha. Meya anaifisidi hazina ya baraza kwa kumpeleka Bili na familia yake kwa burudani.
   • Meya anaunda kamati nyingi ili kuwahonga madiwani wanaomuunga mkono. Anaishia kushauriwa kufanya maamuzi yasiyo ya busara, anakataa kuwasikiliza wafanya kazi, mji umejaa urundo, wageni wanakosa kufika na uongozi wa Meya unaanguka.
   • Meya anamlipa Bili kwa huduma ambayo kwa ukweli hajatoa. Huu unakuwa mzigo kwa hazina ya baraza.
   • Meya anaidhinisha Diwani I na Diwani II kulipwa 'overtime' na hali hawajafanya lolote. Anaishia kumpa Bili upenyu wa kushauri wauze fimbo ya Meya.
   • Meya anaidhinisha kutotozwa kodi kwa madiwani kwa kutaka wamuunge mkono. Hili linalinyima baraza pato na kuzidisha nakisi ya fedha.
   • Meya anamhonga mhubiri kwa sadaka ili aendelee kumwombea. Mhubiri anashindwa kumkosoa Meya, uongozi unaanguka.
   • Bili anamshauri Meya amwambie mwanakandarasi alishtaki baraza ili apewe fidia kwa kukatizwa kwa kandarasi. Meya anapata fungu lake pia.
   • Raia wanachukua hongo kutoka kwa viongozi. Wanawachagua na kuendeleza uongozi mbaya. Meya anamwambia Siki kuwa hata akitaka uongozi mara nne, tano na sita atapewa kwani ana akili na uwezo wa ushawishi.
   • Ufisadi unamfanya Meya kumshirikisha Bili katika maamuzi muhimu ya Baraza, na hali Bili si mfanya kazi wa Baraza. Bili anaishia kumporosha Meya.
   • Ufisadi unamfanya Diwani I (Bwana Usalama) kufanikisha wizi wa fimbo ya Meya. Anatoka nayo kasha anatangaza kwamba kulitokea rabsha ikaibwa.
   • Ufisadi unamfanya Meya, Diwani 1, Diwani II na Bili kutotoa siri kuhusu nyama ya kuiba fimbo ya Meya linapata hasara.

SEHEMU D: USHAIRI

Jibu swali la 6 au la 7

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

  Kilio cha Lugha

  Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze
  Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
  Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
  Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia,

  Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanvasa
  Hamna nami imani, wala kupanga siasa.
  Mwasema sayansini. siku ningalitosa.
  Mwanambia nikotosa. kuiva sijafika.

  Ela muelewe sana. Maamuma na Imamu.
  Mulipokuwa vijana. kwenu nilikmva timamu.
  Sasa mumesoma sana. mwaniona ni haramu.
  Mujue kuwa dawamu. utumwa mwauridhia.

  Mzaliwapo mwalia, ‘maa', maneno ya kwanza.
  Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza.
  Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza,
  Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.

  Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza,
  Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza,
  Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza,
  Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?

  Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao,
  Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
  Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
  Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.

  Enyi viongozi wetu ipangeni nadharia,
  Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
  Lugha hata ‘mbusha watu, tuche kuriaria,
  Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia.

  Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote,
  Msamiati huwa, ni wa Afrika yote,
  Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote,
  Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.

  Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi,
  Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi,
  Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
  Kwao ‘meomba kiasi, ili kujizidisha.

  Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya,
  Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya,
  Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya,
  Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia.

  Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana,
  Kukua imeridhia, msamiati kufana,
  Wengine wataijulia, kwa rnarefu na mapana,
  Lugha yenu ya maana, mwaipuuza yalia.

  1. Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu. (Alama 2)
   • Tarbia - mishororo mine katika kila ubeti.
  2. Kwa kutoa hoja nne, eleza kwa nini shairi hili likaitwa kilio cha lugha. (Alama 4)
   • Kiswahili chapuuzwa kuwa hakijakomma
   • Waliosoma hawakienzi Kiswahili wakifikiria hawana haja na lugha hii.
   • Viongozi hawakienzi Kiswahili katika kujenga siasa.
   • Kiswahili hakipewi nafasi.
   • Waafrika hawaoni utajiri wa Kiswahili kuwa na msamiati kutoka Afrika nzima.
  3. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (Alama 4)
   • Kila mmoja aelewe
   • Mlipokuwa vijana mlikitumia Kiswahili.
   • Baada ya kusoma mmeanza kukidharau
   • Kwa kufanya hivi mjue mwafurahia utumwa.
  4. Eleza toni ya shairi hili. (Alama 2)
   • Toni ya huzuni - lugha ya mtu mweusi chalia.
  5. Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu. (Alama 3)
   • Inkisari - kiwa - nikiwa
   • Mazida - muelewe - mwelewe
   • Tabdila - mulithamini - mlithamini.
   • Kuboronga lugha - hamna name imani - hamna imani name.
   • Utuhozi - risaruni.
  6. Bainisha nafsineni katika shairi. (Alama 2)
   Hafsheni
   • Mtetezi wa lugha ya Kiswahili anayelalamikia kupuuzwa kwa Kiswahili.
   • Aliyezinduka na kutambua umuhimu wa Kiswahili barni Afrika.
  7. Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi. (Alama 3)
   1. nasongwa 
    • Nasagwa – naumia
   2. kuriaria 
    • kuzurura, kurandaranda
   3. adinasi
    • binadamu
 2. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

  T. Arege: Barabara

  Barabara bado ni ndefu
  Nami tayari nimechoka tiki
  Natamani kuketi
  Ninyooshe misuli
  Nituliza akili.

  Lakini

  Azma yanisukuma
  Mbele ikinihimiza kuendelea
  Baada ya miinuko na kuruba
  Sasa naona unyoofu wake
  Unyoofu ambao unatisha zaidi.

  Punde natumbukia katika shimo
  Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
  Ghafla nakumbuka ilivyosema
  Ile sauti zamani kidogo
  "Kuwa tayari kupanda na kushuka.”

  Ingawa nimechoka
  Jambo moja li dhahiri
  Lazima nifuate barabara
  Ingawa machweo yaingia
  Nizame na kuibuka Nipande na kushuka.

  Jambo moja nakukumbukia: Mungu
  Je. nimwombe tena? Hadi lini?
  Labda amechoshwa na ombaomba zangu
  Nashangaa tena!

  Kitu kimoja nakiamini
  Lazima niendelee kijitahidi kwa kila hatua mpya
  Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
  Nikinaswa na kujinasua
  Yumkini nitafika mwisho wake
  Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.

  1. Eleza toni ya shairi hili. (Alama 2) 
   • Toni ya mahimaini - lazima niendelee kujitahidi kwa kila hatua.
   • Toni ya uchovu - Nami tayari nimechoka tiki.
  2. Tambua nafsineni katika shairi hili. (Alama 2)
  3. Mshairi ana maana gani anaposema “Kuwa tayari kupanda na kushuka” wa tatu? katika ubeti (Alama 2)
   • Kuwa tayari kukabiliana na uzuru na ugumu wa maisha
  4. Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili ukizitolea mifano mwafaka. (Alama 10) 
   • Taswira - picha inayojitokeza unaposoma kazi ya fasihi n.k. wa miinuko na kuruba.
   • Taswira kinzani - Nizame na kuibuika
   • Nipande na kushuka.
   • Taashira - Barabara kuimarisha maisha.
   • Mswali balagha - hadi lini?
   • Uzungumzi nafsi - mizame na kuibuka, -Nipanda na kushuka.
  5. Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili. (Alama 2)
   • Msemaji ameshangaa kuwa amekuwa akiomba kwa muda na anatilia shaka iwapo Mungu amechoshwa na maombi yake.
  6. Eleza maana ya: (Alama 2)
   1. kuruba
    • Hali ya kuwa na vikwazo na magumu ya maisha.
   2. barabara yenye ukungu
    • Mkondo wa maisha ambapo anayokubaliana nayo mja si wazi. Kila hisia huibua mambo mapya.

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

 1.  
  1.  Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii. (Alama 10)
   • Nyimbo huhifadhi historia ya jamii. Mfano nyimbo za siasa, nyimbo za sifa, nyimbo za vita.
   • Huhifadhi na kupitisha utamaduni k.v mbolezi hubeba utamaduni wa jamii kuhusu kifo.
   • Huliwaza kv. Mboiozi Kuonyesha ustadi/ubora wa jamii.
   • Huhamasisha
   • Hudimisha
   • Kukuza utangamano
   • Ni njia ya kutakwa hisia
   • Huadilisha.
   • Kukashifu tabia hasi
   • Kusifu tabia chanya
   • Hukuza uzalendo kuimarisha ubunifu.
  2. Ili kuweza kufanikisha uwasilishaji wa utanzu wa nyimbo kwa hadhira eleza mambo anayohitaji mwimbaji. (Alama 10)
   • Kuwa na sauti ya kurutia
   • Kuihusisha hadhira
   • Kuieiewa hadhira
   • Kuelewa utamaduni wa hadhira
   • Kutumia viziada lugha
   • Kuwa mkakamavu
   • Aelewe lugha ya hadhira
   • Awe mbunifu
   • Ahusishe masuala ibuka yanayoathiri jamii ili kupitisha maadili yafaayo.
   • Awe na kumbukumbu nzuri.
   • Avae maleba
   • Abadilishetoni kulingana na ujumbe
   • Kutumia ala kwa njia mwafaka ili kukuza mvuto wa utungo wake.

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download KCSE 2016 Kiswahili Paper 3 Questions with Marking Scheme.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest