KCSE 2018 Kiswahili Paper 2 with Marking Scheme

Share via Whatsapp

QUESTIONS

  1. UFAHAMU (Alama 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

    Mabibi na mabwana, ndugu wapenzi, alianza Bi. Mkesha, "huu ni mwaka wa tano tangu tufanye uchaguzi mkuu uliowapa vigoda wenzetu hawa. Katika kipindi hiki kumetokea mengi ya kujipigia kidari, pametokea pia mengi, mengi mabaya ya kuitia jamii ya Tungama izara Tumejipa mkono wa tahania kwa uteuzi wetu mzuri. Vilevile tumeiisuta kwa uteuzi usio wa kuridhisha

    Ndugu wapenzi, sina haja ya kuwakumbusha yote ambayo tumepitia; mmeyashuhudia yote. Ila ninayotaka kusema ni kwamba malengo yetu ya kuwateua viongozi yamesalitiwa. Ndugu zangu, itakumbukwa kwamba watangulizi wetu walianza safari ya kurejesha utu wa Mwafrika wakiwa na nia thabiti ya kuwabwaga maadui watatu wa maendeleo. Je, mnawajua maadui hao? Ni ujinga, magonjwa na umaskini. Waanzilishi wa taifa hili, pamoja na viongozi waliowafuata walipigania huduma za bure za afya, na elimu ya bure na ya lazima kwa wote. Vijana wetu walijitoma ugani kuzamia lulu ya elimu; wakavidhihaki vitabu hadi kufikia kilelecha cha elimu. La kusikitisha ni kwamba elimu hii imekuwa laana kwao. Mnajua kisa na maana ya hali hii? Natija iliyotarajwa haikupatikana. Na haya si mageni kwetu. Mnajua wapo vijana humu vijijini ambao wamepiga lami kwa miaka na mikaka bila kuambulia kazi za hadhi ambazo waliahidiwa huko vyuoni. Hatimaye hawa hawa wenye shahada mbili, na wengine hata tatu, ndio wanaokuwa matarishi wa wale ambao walichechemea masomoni. Vijana wengine, kwa kukosa hata huo utarishi, wameamua kuanzisha biashara rejareja ili kujikimu; wamekosa la mama, wanaamwa la mbwa. Sina haja ya kuwafafanulia kiini cha hali hii ya kutamausha.

    Ni dhahiri kwamba uthabiti wa taifa lolote lile hutegemea uthabiti wa uongozi, na uaminifu wa raia wake katika kuuwajibisha huo uongozi. Hata hivyo, inasikitisha kwamba wengi wetu tumejipoka uwezo wa kuuwajibisha uongozi kwa kuwa mawindo rahisi ya uzungukaji mbuyu. Huu ndio uwele ambao umeufisidi utu wetu na kutusahaulisha thamani za kitaifa. Hebu niambie ewe mama mwenzangu, kuna faida gani kuuza kura yako kwa kibaba cha unga na noti ya shilingi mia moja, ati kwa kuwa unaambiwa, 'Ukinichagua nitahakikisha kwamba ile Affirmative Action imezingatiwa? Ipo haja gani kuchomwa na jua ukiwafuata hawa hawa viongozi, ukiwaimbia nyimbo za kuwatia raia kichaa cha shangwe ili kuwapembeja wawapigie kura? Je, faida kwako imekuwa gani? Hujangojea kwa kipindi chote hiki kusakafiwa kwa hiyo barabara uliyoahidiwa siku ulipouza kura yako? Na ile ahadi ya 'mwenzetu' ya kuwaajiri vijana wetu kwenye Jeshi la Wanamaii imetimia2 Hatujashuhudia watu wa akraba moja wakisombwa kutoka humu kijijini kwenda kuchukua nyadhifa katika mashirika ya umma?"

    Kweli waso haya wana mji wao, Bi. Mkesha amejikosha kweliweli." Bi. Kuli alimwambia mwenzake Bi Kengemeka kisha akaendelea." Anatuambia yepi mageni ambavo masikio haya yangu yaliyokula chumvi ya miongo sita ushei ya miaka hayajasikia?

    "Anasema tumpe nafasi ajitome kwenye uwanja wa majogoo," akajibu Bi. Kengemeka, "atakuwaje tofauti na hao wanaume? Hata hao wanawake tumewahi kuwapa nafasi, wakatutenda zaidi ya wanaume. Usinikumbushe kura yangu niliyoipoteza kwa kumkweza Bi. Shali kwenye usukani. Siwezi kusahau namna ile ahadi ya maji ya mabomba na kuchimbwa kwa visima ilivyoishia kwenye kauli yake tu."

    Tumetendwa sote mwenzangu," alisema Bi. Kuli, inasikitisha kwamba dau la masomo ve wanangu limeenda mrama huku nikikimlilia huyo huyo Bi. Shali. Kila mara tunasikia kainitia vyombo vya habari kwamba serikali imeanzisha Hazina ya Eneobunge kuyafadhili masomo ya watoto kutoka familia maskini. Lengo kuu, nasikia, ni kuhakikisha kwamba asilimia kubwa ya watoto haipati fursa ya kujiunga na shule tu, bali pia inakamilisha masomo 'Hata hivyo, huu ni mwaka wa tatu tangu wanangu watatu waache masomo kutokana na ukosefu wa karo. Na usidhani ni karo ya shule ya kitaifa la hasha! Ni karo ya shule za kuwa ambapo niliwapeleka baada ya huyu huyu Bi Shali kunitilia huku akinitolea huko kuhusiana na ufadhili wa masomo."

    "Usinikumbushe yaliyomtika mwanangu Neema," alisema Bi. Kengemeka huku akitwaa ukingo wa kanga yake kujipangusa machozi "Mwana huyu alikaa nyumbani kwa muhula nzima," akaendelea Bi. Kengemeka," dhiki ya kuwaona wenzake wakienda shuleni huku yeye anabaki nyumbani ikamfanya kuwa windo rahisi la mmoja wa hao wabunge akaambulis ambao hakuulalia wala kuuamkia. Mwenyewe mbunge ameshika hamsini zake kana kwamba hakufanya lolote. Mwanangu Jabali naye amehiari kuwa kibarua katika shamba la mbunge wa sasa. Mwenyewe anasema anataka kudunduiza pesa ili arudi shuleni kukamilisha mwaka wake wa mwisho. Na usidhani ni hao wangu tu waliofikwa na ya kuwalika. Tumewaona wana wa wenzetu tuliopiga foleni pamoja kuwateua hao hao wabunge, wakitumiwa kama masoko ya dawa za kulevya. Wengine wamegeuzwa walanguzi wa dawa bizi." Bi. Kengemeka alikamilisha uzungumzi wake na kushusha pumzi kana kwamba ameutua mzigo mzito.

    Hata hotuba ya Bi. Mkesha ilipofikia ukingoni, Bi. Kuli alimwambia mwenzake, "Ninavyoona ni kwamba wanasiasa wote wamcfinyangwa kutoka aina sawa ya udongo. Ikitokea kwamba tutampa huyu Bi. Mkesha kura, tumpe kwa kulazimika kikatiba kupiga kura, tusiwe na matarajio makuu. Inasikitisha kwamba vijana wetu waadilifu hawataki kujitia najisi kwa kuingilia siasa. Yule kijana wetu Angaza angekubali rai ya wazee kujitoma ulingoni tungemuunga mkono.
    1. "Malengo yetu ya kuwateua viongozi yamesalitiwa." Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hoja sita kutoka kwenye taarifa.(alama 6)
    2. Eleza mchango wa wanyonge katika hali ya uongozi nchini Tungama (alama 3)
    3. Bainisha mbinu nne ambazo Bi. Mkesha anatumia kuishawishi hadhira yake. (alama 4)
    4.                      
      1. Andika kisawe cha, 'kuwapembeja' kwa mujibu wa taarifa(alama 1)
      2. Andika maana ya, 'amejikosha' kulingana na taarifa.(alama 1)
  2. UFUPISHO (Alama 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

    Tangu jadi, jamii za Kiafrika zilikuwa na majukumu bayana ya kijinsia. Kila jamii ilipania kuyarithisha majukumu haya kwa vijana wa vizazi tofautitofauti. Katika jamii nyingi. vikao maalumu viliandaliwa ili kuwaelekeza vijana kuhusu namna ya kukabiliana na majukumu Vao ya kijamii. Nyakati nyingine mafunzo haya yalitolewa katika vipindi vya burudani kama vile utambaji wa ngano. Kadhalika, maarifa mengi kuhusu namna ya kukabaliana na majukumu moto za jinsia mahususi yalitolewa kupitia sherehe maalumu za kitamaduni almaarufu miviga. Mifano ya sherehe hizi ni kama vile upashaji tohara, arusi, na hata matanga

    Jamii za zamani, kama zilivyo za kisasa, zilikuwa na matarajio mahususi kwa watu wa i zote Mathalani, katika jamii nyingine za Kiafrika, mwanamume ndive alivetaraiiwa kuikimu Bile vake katika kipindi cha Usasi na kuhemera kwa mfano, mwanamume ndiye aliyekuwa na jukumu la kwenda kichakani kuwinda. Hali kadhalika, mwanamume ndiye aliyetarajiwa kufanya kazi zilizohitaji nguvu kama vile kufyeka misitu kwa ajili ya kutengeneza mashamba. kuchimba migodi, kuchonga mawe, kufua vyombo vya dhahabu na fedha, kuchonga vinyago. na kazi nyingine zilizohitaji nguvu. Mke naye alitengewa jukumu la ulezi, si wa watoto wake tu, bali pia wa mume wake, na hata jamii pana. Ilikuwa jukumu la mwanamke kubaki nyumbani kumpikia mumewe na watoto, kufua nguo na kunadhifisha mazingira. Wakati mwingine waume wao walipojitoma msituni kupigania uhuru, wanawake ndio waliowapikia chakula na kutafuta mbinu za kuwafikishia huko huko msituni.

    Watoto wa kike walifunzwa kuzilinda jamii zao, si kwa mali tu, bali pia kwa hali Walifunzwa kwamba furaha na afya ya familia zao, kimwili, kihisia na kisaikolojia ilimtegemea mama. Ndiye aliyehakikisha kwamba familia yake imepata lishe bora, ndiye aliyekuwa mwalimu wa kwanza wa watoto wake; akawafunza namna ya kujithamini na kuwathamini wenzao akawafunza pia namna ya kutatua migogoro yao kwa njia ifaayo. Kwa upande mwingine, watoto wa kiume walifunzwa umuhimu wa kuwa watu wa kutegemewa na jamaa zao, pamoja na kubuni mikakati ya kuzihakikishia familia zao usalama

    Jamii ya kisasa inazidi kukua na kutwaa uchangamano, nayo mitazamo ya binadamu kuhusu masuala na hali mbalimbali inaendelea kubadilika. Siku hizi kwa mfano, si ibra kupata kwamba majukumu ambayo awali yalikuwa yametengewa jinsia mahususi sasa yametwaliwa na jinsia zote. Imedhihirika kwamba kupanda kwa gharama ya maisha kumezua haja ya waume kwa wake kushirikiana bega kwa bega kuchumia vyungu vya familia zao. Asilimia ya wanawake ambao wanafanya kazi za ajira katika mashirika ya umma na ya kibinafsi imepanda. Kadhalika, kinyume na zamani, idadi kubwa ya wanawake imesoma. Hakika wapo wanawake wengi ambao wameibuka kuwa magwiji katika taaluma kama vile uhandisi, udaktari na usoroveya ambazo awali zilikuwa milki ya wanaume pekee. Ulingo wa siasa nao umetwaa sura mpya. Idadi ya wabunge wanawake inaendelea kupanda kila kuchapo. Wapo pia wanawake ambao wamejiunga na vikosi vya kulinda usalama; jambo ambalo halikuwa la kawaida katika jamii nyingi hapo awali. Wanaume nao wametwaa kazi ambazo awali zilitengewa wanawake pekee. Katika baadhi ya jamii za Kiafrika, mwanamume ambaye alipatikana jikoni alichukuliwa kuwa anaufedhehesha ukoo. Siku hizi si ajabu kuwapata akina baba wengine wakiziandalia familia zao vyakula. Vilevile idadi ya wanaume wanaosomea kazi ya uuguzi inazidi kuongezeka. Pia wapo wanaume ambao wanafanya kazi ya ususi na kuwarembesha wanawake. Hali hii ya mwingiliano wa majukumu haisaidii tu kukabiliana na changamoto ya tofauti za kijinsia, bali pia hupalilia mshikamano wa kijamii. Watu wanapobadilishana zamu katika kutekeleza majukumu ya kijamii huthaminiana. Hujiona kama wanaotegemeana kwa hali zote, na kwa njia hii utangamano hujengeka zaidi Kadhalika, kubadilishana majukumu ni njia bora ya kufidia udhaifu wa wenzetu.

    Ni dhahiri kwamba kumekuwa na mwingiliano mkubwa wa kimajukumu, hali ambayo imeziwezesha jamii nyingi kufikia ufanisi mkubwa. Hata hivyo, imebainika kwamba hali hii inaelekea kumomonyoa faida ambazo jamii nyingi zimepata kwa wanaume na wanawake kushirikiana kutekeleza majukumu anuwai. Mathalani, wazazi wengi siku hizi wamo mbioni kutafuta elimu, ama kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kikazi, au kwa kukamia malipo zaidi. Kuna baadhi ya wazazi ambao hujisajili kwa kazi mbalimbali, si kwa sababu wanahitaji maarifa fulani, bali kwa sababu wanataka kuwapiku wenzao katika ndoa. Matokeo ni kwamba mume na mke wanajipoka muda wa kukaa pamoja na kufahamiana, pengo la kimahusiano nalo linajengeka, hali ambayo imesababisha kusambaratika kwa baadhi ya ndoa. Hali kadhalika imebainika kwamba. kwa sababu ya mume na mke kuwa mbioni kujiendeleza kitaaluma na kielimu, malezi ya watoto yameanza kutetereka. Jukumu la kuwalea watoto na vijana limetelekezewa vijakazi, vitwana na hata vibonzo!

    Ibainike kwamba kila jambo sharti liwekewe mipaka. Yapo majukumu ambayo sharti yatekelezwe na jinsia maalum, yumkini kwa sababu za kimaumbile. Yapo majukumu kama vile malezi ya watoto ambayo sharti yachangiwe na kila jinsia.
    1. Fupisha ujumbe wa aya tatu za kwanza kwa maneno
      Matayarisho
      .........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
      Nakala Safi  .........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
    2. Eleza masuala ambayo mwandishi anaibua katika aya nne za mwisho. (maneno 90)
      (alama 8, 1 ya mtiririko)
      Matayarisho
      .........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
      Nakala Safi  .........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
  3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
    1. Andika sauti zenye sifa zifuatazo: (alama 2)
      1. kipasuo ghuna cha midomoni
      2. irabu ya kati, chini
      3. kikwamizo sighuna cha kaakaa gumu
      4. nazali ya ufizi
    2. Bainisha silabi zilizowekewa shadda katika maneno yafuatayo:(alama 1)
      1. miambakofi
      2. yatazoleka
    3. Andika neno lenye muundo ufuatao:(alama 2)
      1. kiambishi ngeli, wakati uliopita, mzizi, kauli tendwa, kauli tenda (kiishio)
      2. kiambishi cha wingi, mzizi
    4. Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maagizo.(alama 4)
      1. Uaminifu wa mtu humfanya aheshimiwe.
        (Badilisha nomino iliyopigiwa mstari kuwa kivumishi.)
      2. Shama.Tegea na Koru ndio walioibuka washindi.
        (Tumia kiwakilishi nafsi badala ya maneno yaliyopigiwa mstari.)
      3. Mchuuzi alinunua mboga zilizofungwa pamoja.
        (Tumia nomino ya jamii badala ya maneno yaliyopigiwa mstari.)
      4. Seluwa ni mtiifu. Maria ni mtiifu pia.
        (Unganisha kuwa sentensi moja yenye kihusishi cha kulinganisha.)
    5. Nomino zifuatazo zimo katika ngeli gani?(alama 1)
      1. ugwe 
      2. limau
    6. Unganisha sentensi zifuatazo kuunda sentensi ya masharti. Moto ulidhibitiwa. Kulikuwa na vifaa vya kutosha.(alama 2)
    7. Andika sentensi ifuatayo katika wingi.(alama 1)
      Nahodha alilikwepa jabali hilo, chombo kikafika ufuoni salama.
    8. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao: (alama 2)
      nomino, kishazi kitegemezi, kitenzi, nomino, kivumishi, kielezi
    9. Andika sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali ya mazoea.(alama 1)
      Barabara nyingi zimesakafiwa.
    10. Unganisha sentensi zifuatazo kwa kuanza kwa neno: Wanafunzi(alama 2)
      Wageni wamefika. Wanafunzi wamefurahi.
    11. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa.
      Nguo ambazo zinauzwa kwenye duka hilo zinavutia. (alama 1)
    12. Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maagizo (alama 4)
      1. Muutu aliwalea watoto wa Maki.
        (Anza kwa: Watoto wa Maki.)
      2. Maji yalijaa. Maji yalimwagika.
        (Unganisha kuunda sentensi changamano.)
    13. Tumia kielezi cha kiasi badala ya kile kilichopigiwa mstari.
      Sewe alituelezea jambo hilo kinaganaga(alama 1)
    14. Ainisha xirai katika sentensi ifuatayo.(alama 2)
      Viongozi wengi walikuwa waadilifu mno kabla ya Uchaguzi Mkuu.
    15. Changanua sentensi zifuatazo kwa kielelezo cha mstari.
      1. Hili lake lilikuwa limeiva lakini hatukujua.(alama 2)
      2. Mkufu wa Umu unapendeza mno.(alama 1)
    16. Andika maana mbili zinazojitokeza katika sentensi
      Medi anasema atawarithisha nyumba yake.(alama 2)
    17. Akifisha sentensi ifuatayo.
      jihadhari akasema kulei uamuzi wako unaweza kukuathiri vibaya.(alama 2)
    18. Kanusha sentensi ifuatayo.
      Mkulima anahitaji magunia haya.(alama 1)
    19.                        
      1. Karimu ni kwa choyo.......................... ni kwa kukashifu na .......................... ni kwa tele.(alama 2)
      2. Maarufu ni kwa mashuhuri, ukoo ni kwa ....................ilhali faida ni kwa......................( alama 2)
    20. Tunga sentensi moja kubainisha maana mbili za neno: kata.(alama 2)
  4. ISIMUJAMII (Alama 10)
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Ndugu wapenzi, waumini wenzangu, mbazi hii haionyeshi huruma ya Mwenyezi Mungu kwetu wakosefu tu, bali pia inatufunza umuhimu wa unyenyekevu na msamaha.
    1. Bainisha sifa tatu za sajili ya kidini zinazojitokeza katika makala haya (alama 3)
    2. Fafanua vipengele vingine saba vya kimtindo ambavyo mhubiri huyu angetumia kufanikisha mazungumzo yake.(alama 7)

MARKING SCHEME

  1.                        
    1.                      
      1. Vijana kusoma na kutopata kazi.
      2. Waliosoma kupewa kazi za hadhi ya chini huku wasiosoma wakiwa wakubwa
      3. Raia kuteua viongozi wasiofaa kwa sababu ya ufisadi.
      4. Raia kutopata huduma walizoahidiwa, kama vile maji ya mabomba.
      5. Watoto wa maskini kutopata elimu licha ya kuwepo kwa hazina ya eneo bunge.
      6. Nyadhifa za juu kutwaliwa na watu wa nasaba moja/ukabila/unasaba.
      7. Viongozi kuwatumia vijana kulangua dawa.
      8. Viongozi kuwatunga mimba watoto.
      9. Ajira ya watoto.
      10. Hazina ya eneo bunge kutowafaidi watoto wanaohitaji zaidi msaada.
        6x1= 6
    2.                        
      1. Kupoteza nafasi ya kuuwajibisha uongozi kwa kupokea hongo/kuuza kura.
      2. Kuwaimbia viongozi nyimbo ili kuwapembeja raia wawapigie kura.
      3. Kuamini kwamba wanasiasa wote ni sawa, kukata tamaa ya kuchagua kiongozi mwadilifu.
      4. Baadhi ya wale waadilifu kutojiunga na siasa - kwa mfano, Angaza.
        3x1=3
    3.                          
      1. Kujinasibisha na wasikilizaji wake - ndugu wapenzi, mama mwenzangu.
      2. Maswali ya balagha ili kuwachochea/ kuwavutia kwake. Je, mnajua...
      3. Kuwasawiri wasikilizaji kama wanaofaa-haya si mageni/anayasawiri mambo kama ya kawaida ili yeye na hadhira yake wayafasiri kwa namna sawa.
      4. Kuwaonyesha wasikilizaji wake kuwa ni mwenye mamlaka ya kuleta uthabiti katika uongozi.
      5. Anajitenga na wanasiasa wengine na (kwa) kudokeza udhaifu wao..... hawa hawa viongozi ... ahadi ya 'mwenzetu'...
        4x1 = 4
    4.                  
      1. Kuwapembeja - kuwarai, kuwalaghai.
        1x1 = 1
      2. Amejikosha-amejitoa lawamani.
        1x1=1
  2.                          
    1.                        
      1. Majukumu ya kijinsia yalikuwa bayana.
      2. Majukumu yalirithishwa kwa vizazi.
      3. Vijana walifunzwa kukabiliana na majukumu.
      4. Jamii kuwa na matarajio kuhusu jinsia.
      5. Mwanaume kutarajiwa kukimu familia.
      6. Mama kuwa na jukumu la malezi.
      7. Watoto wa kike kutarajiwa kuzilinda familia.
      8. Mama kuwa mwalimu.
      9. Watoto wa kiume kufunzwa kuwa wa kutegemewa.
        6x1=6
        1 ya mtiririko
    2.                          
      1. Watoto wa kike walifunzwa kuzilinda jamii zao.
      2. Mama ndiye aliyekuwa mwalimu wa kwanza wa watoto wake.
      3. Watoto wa kiume walifunzwa umuhimu wa kuwa watu wa kutegemewa.
      4. Uchangamano wa jamii umesababisha kubadilika kwa mitazamo.
      5. Majukumu yameingiliana. Kwa mfano, wake wanafanya mambo ambayo awali hayakufanywa na jinsia hiyo. 
      6. Idadi ya wanawake wanaofanya kazi ya ajira imeongezeka. 
      7. Wanawake kusomea taaluma na nyanja zilizotengewa wanaume awali.
      8. Wanaume kufanya kazi zilizotengewa wanawake. 
      9. Hali ya mwingiliano wa kimajukumu hupalilia mshikamano na kukabiliana na tofauti za kijinsia.
      10. Hufidia udhaifu wa wenzao.
      11. Mwingiliano wa majukumu unaweza kuathiri vibaya faida iliyotarajiwa, kama vile kutelekezea malezi kwa vijakazi. 
      12. Baadhi hujisajili kwa kazi ili kushindana na wenzao. 
      13. Hali hii huzua utengano na kusambaratika kwa ndoa.
      14. Kila jambo sharti liwe na mipaka kuna majukumu yanayostahili kutengewa tu jinsia maalum na mengine jinsia zote/mipaka hii idumishwe.
        7x1=7
        1 ya mtiririko
  3.                    
    1.                                      
      1. /b/, /m/
      2. /a/
      3. /sh/
      4. /n/
    2.                      
      1. Miambakofi
      2. Yatazoleka
    3.                    
      1. ki - li - nunu - liw-a
        wa-li-tembe-lew-a
        zi-li-jeng-ew-a
        Alama 1/0
      2. Mi-kate  - {mi} wingi
                        {kate} mzizi
      3. Vi-ti - {vi} wingi
                 {ti} mzizi
      4. Ny-ufa - {ny} wingi
                     {ufa} mzizi
        Alama 1/0
    4.                                      
      1. Mtu mwaminifu huheshimiwa.
        Alama-1/0
      2. Wao ndio walioibuka washindi.
        Alama-1/0
      3. Mchuuzi alinunua kicha cha mboga.
        Alama 1/0
      4. Seluwa ni mtiifu kama Maria/ Seluwa ni mtiifu kuliko Maria.
        Alama 1/0
    5.                  
      1. Ugwe - U - ZI.
        Alama 1/2
      2. Limau - LI-YA
        Alama 1/2
    6.                  
      1. Vifaa vya kutosha visingalikuwapo moto usingalidhibitiwa.
      2. Kama vifaa vya kutosha visingekuwepo moto usingedhibitiwa.
      3. Kama pasingekuwa na vifaa vya kutosha moto haingedhibitiwa.
      4. Vifaa vya kutosha visingekuwepo moto usingedhibitiwa.
        1x 2 = 2
    7. Manahodha waliyakwepa majabali hayo vyombo vikafika fuoni salama.
      Alama 1/0
    8. Kwa mfano: Wanafunzi   waliotia bidii masomoni     walipata    alama    nzuri          mno.
                             ↓                           ↓                           ↓             ↓          ↓               ↓
                      Nomino           kishazi kitegemezi         kitenzi     Nomino   kivumishi     kielezi
      Alama 2/0
    9. Barabara nyingi zitakuwa zikisakafiwa.
      au
      Barabara nyingi zitakuwa zinasakafiwa.
      Alama 1/0
    10. Wanafunzi wamefurahia kufika kwa wageni.
      Au
      Wanafunzi wamefurahi wageni walipofika
      Au
      Wanafunzi wamefurahi baada ya wageni kufika.
      Alama 2/0 
    11. Maguo ambayo yanauzwa kwenye majiduka hayo yanavutia.
      Alama 1/0
    12.                    
      1. Watoto wa Maki walilelewa na Muutu.
        Alama 2/0
      2. Maji yalipojaa yalimwagika.
        Au
        Maji yalijaa yakamwagika.
        Au
        Maji yaliyojaa yalimwagika.
        Au
        Baada ya maji kujaa yalimwagika.
        Alama 2/0
    13. Sewe alituelezea jambo hilo tena.
      Au
      Sewe alituelezea jambo hilo mara mbili/mara kwa mara.
      Alama 1/0
    14. viongozi wengi --kirai nomino
      walikuwa waadilifu mno - Kirai tenzi
      waadilifu mno -kirai vumishi
      kabla ya uchaguzi mkuu -kirai husishi
      uchaguzi mkuu - kirai nomino.
      4x1/2 = 2
    15.                                            
      1. KN (W+V) +KT (Ts + T) +U+KN (Ø) + KT (T)
        Alama 2/0
      2. KN(N+KH)KT(T+E) Au KN(N+W+N) +KT( T+E)
        Alama 1/0
    16.                    
      1. Nyumba ni ya Medi.
      2. Nyumba ni ya mtu mwingine.
      3. Medi ndiye atairithisha nyumba.
      4. Mtu mwingine ndiye atairithisha nyumba.
      5. Nyinyi (nafsi ya pili) ndio mtakaorithishwa.
      6. Wao (nafsi ya tatu) ndio watakaorithishwa.
        2x1=2
    17.  "Jihadhari" akasema Kulei, "uamuzi wako unaweza kukuathiri vibaya."
      4x1/2=2
    18. Mkulima hahitaji magunia haya.
      Alama 1/0
    19.                  
      1. kusifu - kukashifu
        kupongeza - kukashifu
        chache/haba/kidogo-tele
        2x1 = 2
      2. Nasaba/akraba/mlango/ -ukoo
        Natija/tija - faida
        2x1 = 2
    20. Maana zifuatazo zijitokeze:
      1. Kugawanya/kutenganisha, pengine kwa kisu. 
      2. Ondoa sehemu ya kitu, kwa mfano, kukata ujira/kupunguza kitu. 
      3. Chombo cha kuchotea maji mtunguni. 
      4. Eneo la ardhi/sehemu inayoongozwa na kiongozi fulani k.v. Lokesheni.
      5. Kitambaa au majani yaliyoviringwa kwa ajili ya kuwekwa kichwani kubebea mzigo.
        2x1=2
  4.                        
    1.                            
      1. Kuibua utangamano kwa kuwarejelea waumini kama ndugu', 'wenzangu'.
      2. Kutaja jina la mwenyezi Mungu./msamiati wa kidini.
      3. Kumsawiri binadamu kama anayehitaji huruma ya Mungu ni mwenye dhambi anayetegemea huruma.
      4. Kurejelea vifungu/mifano kutoka msahafu.
        3 x1=3
    2.                          
      1. Atumie lugha inayoeleweka na hadhira.
      2. Avute makini ya hadhira kwa kuwashirikisha, kwa mfano kupitia maswali ya balagha, kuwarejesha kwenye msahafu.
      3. Kutasifidi lugha pale inapohitaji.
      4. Lugha isiyowatia waumini unyanyapaa kwa mfano, aepuke kutumia kauli kama vile, "ukimwi unawapata wenye dhambi... utakuua". Huenda kuna walioathiriwa moja kwa moja na ugonjwa wenyewe.
      5. Kuzingatia fomyula na mtindo maalum/uliokubalika wa kuendeshea ibada ili wasikanganyike.
      6. Kurudia baadhi ya kauli ili kuwaaminisha waumini/kuwafanya waelewe.
      7. Kuchanganya msimbo ili kurahisisha uelewa.
      8. Kutumia miondoko na ishara ambazo zinakubalika na jamii-lugha husika.
      9. Pale anapohitajika/inapobidi atumie toni kali ya kuonya.
      10. Atumie lugha inayotia tumaini na matarajio miongoni mwa waumini kuwa hali zao hata zingawa ngumi, zinaweza kutengenea.
      11. Atumie mbinu za kushawishi/lugha ya kushawishi ili kuwavutia waumini na kuwadumisha kwenye dhehebu lake.
      12. Lugha ya kuelekeza kushauri.
        Kwa mfano: "Kesheni mkiomba"
        "Kaeni tayari kwani hamjui siku atakaporudi”.
        7x1=7
        Tanbihi: Mifano itolewe ili atuzwe alama (I) kamili.
Join our whatsapp group for latest updates

Download KCSE 2018 Kiswahili Paper 2 with Marking Scheme.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest