Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - KCSE 2020 Past Papers

Share via Whatsapp

 

Maagizo

 • Andika insha mbili. lnsha ya kwanza ni ya lazima.
 • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
 • Kila insha isipungue maneno 400.
 • Kila insha ina alama 20.
 • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
 1. Lazima
  Wewe ni katibu wa jopokazi ambalo limeteuliwa kuchunguza sababu za wanafunzi wa shule za upili kupuuza masomo ya kiufundi. Andika ripoti ya uchunguzi huo huku ukitoa mapendekezo.
 2. Maktaba ya shule yenu haina magazeti. Andika makala kuonyesha umuhimu wa maktaba hiyo kuwa na magazeti.
 3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo:
  Mpanda ovyo hula ovyo.
 4. Tunga kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo:
  Msongamano wa wanunuzi, wapitanjia na wasukuma mkokoteni katikati mwa wachuuzi wa kila aina ulinitanabahisha kuwa nimefika mji wa Tafaruku.


Mwongozo wa Kusahihishia

 1. Hii ni ripoti.
  Yafuatayo yazingatiwe:
  1. Muundo
   Sura ya ripoti idhihirike.
   1. Kichwa – kionyeshe kiini cha uchunguzi.
   2. Utangulizi
    • Mtahiniwa ataje jopokazi: wanachama walioteuliwa, aliyeteua jopokazi
    • Hadidu za rejea (Masharti na mipaka ya utekelezaji wa kazi
     iliyopangiwa jopokazi.)
    • Sampuli lengwa - habari zilikokusanywa.
    • Njia za ukusanyaji – hojaji, mahojiano, majadiliano kwenye vikundi.
   3. Mwili – hoja zijadiliwe humu; vichwa vidogo vitumiwe.
    1. sababu/mapuuza/matokeo
    2. Mapendekezo
    3. Hitimisho 
    4. sahihi, jina, tarehe (kimalizio)
  2. Maudhui
   Baadhi ya hoja ni:
   1. Msisitizo mkubwa kwenye masomo ya kiakademia.
   2. Kutokuwa na vielelezo tosha vya watu waliofanikiwa kwa kufuatia masomo ya aina hii.
   3. Masomo haya kutohimizwa katika shule nyingi kwa sababu ya ukosefu wa vifaa.
   4. Ukosefu wa walimu waliohitimu katika taaluma hizi.
   5. Shinikizo kutoka kwa wazazi - wanafunzi wajishughulishe na masomo
    mengine.
   6. Mtazamo hasi kuwa baadhi ya masomo kama vile ufundi wa mabomba ni duni.
   7. Hapajawa na mfumo bayana unaoonyesha hatua ambazo mwanafunzi/mwanagenzi atapitia hadi pengine Chuo Kikuu.
   8. Mafunzo mengine ya kiufundi ni ghali.
   9. Vyuo vichache vya kiufundi katika sehemu za mashambani.
   10. Vyuo vingine vya kiufundi vimegeuzwa kuwa vyuo vikuu, hivyo wanafunzi kutoona umuhimu wa vyuo vya kiufundi.
   11. Baadhi huenda wasimudu masomo ya kisayansi, hivyo kukata tamaa.
   12. Masomo haya yanahitaji mtaji ndipo anayesomea apate ajira.
   13. Mtazamo potovu kuwa masomo haya ni ya mapato ya chini.
   14. Walimu kuwavunja wanafunzi moyo.
   15. Masomo haya hayana mvuto kwa wanafunzi.
   16. Masomo haya huwafunga wanafunzi kuhusika wenyewe.
   17. Mtazamo hasi wa kijinsia, utamaduni,itikadi n.k.
    N/B Hoja zingine ziko wazi.
              Apewe mkwaju wa hoja.
    Mtahiniwa atoe angaa pendekezo moja.Akitoa mawili au zaidi, ni bora zaidi.Asiye na pendekezo atakuwa amepungukiwa kimaudhui hivyo asipite kiwango cha C (alama 10).
    1. Mtaala usisitize masomo ya kiufundi kuanzia ngazi za chini.
    2. Vyuo vya Ualimu vihușishe ufundishaji wa masomo ya kiufundi.
    3. Serikali iongeze ufadhili kwa masomo ya kiufundi.
    4. Kuwe na mfumo bayana unaoonyesha taaluma ambayo mwanafunzi atasomea akifuatia masomo ya kiufundi.
     Kipengele kimoja kisimkwaze mwanafunzi akakosa 45
     N/B -Akiandika ripoti ya kawaida atakuwa amepotoka kimtindo, hivyo akadiriwe vilivyo,
 2. Makala yaonyeshe umuhimu wa magazeti.
  Sura ya Makala idhihirike.
  Baadhi ya hoja ni:
  1. Kujuza kuhusu yanayojiri nchini/ulimwenguni.
  2. Kupalilia usomaji wa mapana.
  3. Hukuza ubunifu - mwanafunzi atajifunza mitindo mbalimbali ya uandishi.
  4. Kufunzia/kujifunzia sajili za magazeti.
  5. Baadhi huwa na safu ya kufunzia vipengele vya lugha.
  6. Hukuza stadi za kuhariri.
  7. Hupalilia uwazaji wa kina, kwa mfano kupitia kujaza mraba.
  8. Kupalilia mazoea ya kusoma.
  9. Kufanikisha somo la maktaba.
  10. Kupalilia mbinu za kitafiti/mazoea ya kudadisi.
  11. Kuburudisha
  12. Kuimarisha masomo kupitia kwa maswali na majibu
   *Aadhibiwe 45 iwapo atakosa sura ya insha.
   *Atakayepinga pekee amepotoka kimaudhui.
   *Atakayepinga na kuonyesha umuhimu, apate mkwaju kwa umuhimu -atakuwa amepungukiwa kimtindo
 3. Hii ni insha ya Methali.
  Kisa kidhihirishe maana ifuatayo:
  Mtu asipotia bidii katika jambo matokeo yake huwa hafifu...
  AU
  Kiasi cha kufanikiwa katika jambo hutegemea matayarisho/mikakati ambayo inawekwa.
  Baadhi ya hali ambazo zinaweza kujitokeza ni:
  1. Mwanafunzi kutojitayarisha ipasavyo kwa ajili ya mtihani na hatimaye kupata alama
   zisizoridhisha.
  2. Wakulima wakose kujiandaa ipasavyo, mwishowe wapate mavuno haba 
  3. Shirika likose kuweka mikakati ifaayo kuimarisha pato lake; lisipate faida, mwishowe
   lifilisike.
  4. Mlezi kutowaelekeza watoto ipasavyo, watoto kuinukia kuwa wasiotegemewa.
  5. Mwajiri kutojaribu kuimarisha uhusiano wake na waajiriwa wake, migogoro izidi, uzalishaji mali uathirike vibaya
   Tanbihi
   1. Vipengele vitatu vya kimuundo vijitokeze; Utangulizi, mwili, hitimisho.
   2. Kichwa cha makala kidhihirike.
   3. Sharti insha idhihirishe juhudi hafifu/mikakati hafifu/ukosefu wa kujiandaa na baadaye hali/matokeo yasiyoridhisha
   4. Atakayejihusisha au akahusisha mtu mwingine atakuwa amejibu swali
   5. Ashughulikie pande zote mbili za methali. Atakayeshughulikia upande mmoja asipite alama 10 (c+)
 4. Hii ni insha ya kibunilizi.
  Mtahiniwa atunge kisa ambacho kinaoana na mwanzo huu.
  Usimulizi unaweza kubainisha hali zifuatazo:
  1. Msimulizi asimulie yaliyotokea baada ya kuwasili, labda hata anaibiwa.
  2. Msimulizi aonyeshe alikoenda baada ya kuwasili, labda anapokelewa na mwenyeji wake; kisha asimulie maisha yake huko kwa mwenyeji wake.
  3. Anaweza kuwa anapitia hapa tu; pengine anatoka garini kupumzika kabla ya
   kuendelea na safari yake. Baadaye anaendeleza usimulizi wake hadi panapoishia
   safari.
  4. Msimulizi anaweza kuanza kwa kauli hizi, kisha akaturudisha nyuma kusimulia kisa
   ambacho kinamleta hapa. (mbinu rejeshi) 
  5. Anaweza pia kusimulia maisha ya watu wa mji huu.
  6. Akikosa kunakili dondoo, lakini amelenga kisa aadhibiwe kimtindo.
  7. Akiandika kisa ndotoni, atakuwa amejibu swali, bora ioane na mahitaji ya swali.
  8. Si lazima ataje mji wa Tafaruku.
  9. Kisa kiwe na kichwa.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - KCSE 2020 Past Papers.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest