KISWAHILI PAPER 2 - KCSE 2019 MARANDA MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp
 1. UFAHAMU
  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
  HISTORIA YA KATIBA.. Katiba ni utaratibu wa sheria unaoweka mpango wa jamii kuendesha mambo. Ni muhimu kila raia ajue katiba ya nchi yake. . :: Katiba yaweza kuwa imeandikwa au haikuandikwa. Katika jamii za jadi, katiba ilihifadhiwa na kupokezwa kwa mdomo. Muindo wa kuandika katiba ulianza nchini Marekani mwaka 1787. - Ingawa katiba hii imefanyiwa mabadiliko hapa na palė, bado ni ileile. Kenya ilipowekwa chini ya himaya ya Uingereza. mwaka 1895, ilianza kutumia katiba ya Uingereza. Baada ya masetla wa kikoloni kujikita, Kenya kuwa koloni. Hii ililazimu pawe na katiba nyingine mwaka 1920. Waafrika waliupinga mfumo huu kwa sababu haukuwahusisha kikamilifu kwenye masuala ya uongozi. Utetezi wa wanasiasa uliilazimisha serikali ya Uingereza kuitisha makongamano mbalimbali kama vile lile la Devonshire na mengine ili kurekebisha katiba. Waafrika hawakuridhika.

  Wakaendelea kudai katiba mwafaka. Harakati hizi zilileta kuitishwa kwa kongamano la katiba la Lancaster. Lengo lilikuwa kuandika katiba itakayotumiwa nchini hadi leo. Kati ya wajumbe walioenda Uingereza kuandika katiba mwaka 1962 ni pamoja na Tom Mboya, Jean Marie Seroney, Julius Kiano, Jomo Kenyatta, Masinde Muliro, Oginga Odinga, Ronald Ngala, Daniel Arap Moi na James Gichuru. Wengine ni Martin Shikuku, Dennis Akumu, Taita Towett, Abdilahi Nassir, Jeremiah Nyaga na John Keen..Katiba ni kitovu cha taifa. Baina ya mambo inayotekeleza ni kuweka *: utaratibu na kanuni za utawala, kwa mfano, utawala wa kimikoa na serikali za wilaya. Pamoja na haya, katiba hufafanua vyombo vikuu vya serikali ,mamlaka yavyo na mipaka yavyo ya kutenda. Vyombo hivi ni bunge, mahakama, urais, jeshi n.k. Hali kadhalika, katiba hupambanua haki za raia.

  Hii hudumisha demokrasia na huwawezesha wananchi kupata uhuru na haki za kimsingi. Katiba hukinga haki za kila raia, hasa kutokana na udhalimu wa wengi au wenye uwezo mkubwa. Zaidi ya yote, katiba huimarisha asasi za umma ili kudumisha uwajibikaji. :: Katiba huhalalishwa na watawaliwa. Hii hutokea wanaposhirikishwa katika uandishi wake. Kuanzia miaka ya themanini, raia walianza kudai katiba igeuzwe. Mwamko wa kutaka mageuzi ulianza kwa harakati za kubadilisha mfumo wa kisiasa kutoka ule wa chama kimoja hadi ule wa demokrasia ya vyama vingi. Haja ya mfumo mpya wa kisiasa ulilenga kuwashirikisha wananchi katika utawala na kuondoa uimla.

  Harakati zilitia fora miaka ya tisini. Mambo yaliyochochea hali hii ni mengi. Kwanza, katiba iliyokuwa imeandikwa na watu wachache ilikuwa imefanyiwa marekebisho mengi. Marekebisho haya yalimpa rais mamlaka mengi juu ya serikali kuu ria vyombo tofauti vya serikali. Pili, viongozi na watu wenye uwezo na utajiri walipuuza katiba. Raia walihisi wanadhulumiwa. Walipinga hali ya wachache waliomzunguka rais kunufaika huku umma ukitengwa. Tatu, kutokana na uongozi uliokuweko wakati huo, wanawake, watoto na walemavu walidhulumiwa na kukosa uwakilishi ufaao.Hatimaye, pakawa na ongezeko la uharibifu wa mazingira, ufisadi na unyakuzi wa mali ya umma kama vile ardhi.

  Waliopigania katiba mpya walikuwa na haja ya katiba ambayo uandikaji wake ungewahusisha Wakenya wote. Mwanzoni, serikali ilipinga wito wa mabadiliko. Lakini mnamo mwaka 2001 iliunda Tume ya Marekebisho ya Katiba ili kutekeleza mahitaji ya wananchi. Tume hii iliwahamasisha na kuwashawishi raia kutoa maoni. Tume iliandaa vikao katika maeneo ya ubunge 210 ambapo wananchi walitoa mapendekezo kuhusu marekebisho ya katiba waliyotaka.

  Katika mapendekezo hayo raia walisisitiza mambo kadhaa. Jambo la kwanza ni utawala mwema na uwajibikaji wa viongozi na maafisa wa umma .Jambo lingine ni kulinda haki za binadamu zikiwemo za wanawake, watoto na .walemavu: Raia walidai kanuni za usawa na ulinganifu. Aidha walitilia mkazo mahitaji ya msingi kama chakula, afya nzuri, makao, elimu, usalama, uchumi, na kadhalika. Msingi wa mapendekezo hayo yote ni kuwepo na amani ya kitaifa, umoja na uadilifu ili kulinda maslahi ya wananchi wote na taifa.

  Maswali :
  1. Eleza kilichosababisha kongamano la katibala Lancaster. (3mks)
  2. Taja mambo matatu yaliyotiliwa mkazo na raia katika maoni yao kuhusu katiba. (alama 3)
  3. Eleza umuhimu wa katiba kwamujibu wa taarifa. (alama 3)
  4. Taja sababu zilizochangia ubadilishaji wa katiba. (alama 3)
  5. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika taarifa. (alama 3)
   1. Kitovu
   2. Harakati
   3. Hamasisha.
 2. UFUPISHO. (ALAMA 15)
  Soma kifungu kisha uyajibu maswali yanayofuata.

  Nidhamu ni kitu cha maana sana maishani mwa binadamu. Kila mwanafunzi anapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu sana.Akiwa na nidhamu hiyo, atakuwa mtu mwadilifu, anayeweza kustahiwa na kusadikika katika mambo, shughuli na hali tofauti 1. Kwanza, mtoto mwenye nidhamu huwa kama anga au nuru nyumbani mwao, shuleni na pia katika jamii.Watu wote wanampenda na kumheshimu. Wazee kwa vijulanga wote wanamtegemea kama msimamizi wa mambo nyeti ya maisha yao. Kwa hivyo, ni dhahiri shahiri kwamba mwadilifu hunufaika gana, kinyume ña mkaidi ambaye wahenga walimwambia kwamba atakosa kufaidi hadi siku ya Idi. * Pili, huwadia nyakati ambapo huwa kuna jambo la busara, mathalani jukumu ama dhima fulani ambayo huhitaji tu mwakilishi mmoja darasani, shuleni au katika jamii. Watu hapana shaka watamteua yule mwadilifu kuchukua nafasi kama hiyo. Ndio maana viranja wanaoteuliwa shuleni, huwa ni wanagenzi ambao tayari wamekwisha tiliwa katika mizani na kupigwa msaga madhubuti.

  Vile vile, mwadalifü daima atajiepusha na shutuma ha majanga yote yanayoweza kuchipuka. Kuna msemo maarufu, kwa busara yake iliyobusarisha mwadilifu kwamba "aliye kando haangukiwi na mti."Pia waliambiwa kwamba," pilipili usiyoila yakuwashiani?" Ni bayana kutokana na misemo hiyo miwili kwamba mwenye nidhamu hawezi kuhusishwa na majanga hatari yanayoweza kuwakumba watu.Walakini ni vyema kujiuliza, je, nidhamu huanzia wapi, na kwa nini kuna baadhi ya watoro ambao ni utovu wa nidhamu? Utovu wa nidhamu huanzia awali sana maishani mwa mja. Mtoto anapozaliwa, anategemea miongozo na mielekeo ya watu wazima ambao wako mazingirani mwake.Ndipo wakale wale waliokaramka walisema kwamba mtoto akibebwa, hutazama kisogo cha nina.

  Hivi ni kusema kwamba, nidhamu au utovu wa nidhamu huanzia nyumbani hadi shuleni, kisha hupanuka hadi kufikia kiwango ambapo mja anatangamana na watu wote katika maisha yake.Ikiwa sehemu moja ya ukuaji wa nidhamu maishani mwa mja itasambaratika, basi hawezi akawa mkamilifu kinidhamu maishani mwake.Kwa vile ni bayana kwamba mabaya yote ayatendayo duniani hulipwa na · Mola papa hapa duniani, watovu wa nidhamu wote huishia kuangamia, ama kujuta mpo kwa amali zao potovu. Ni kheri mja kujitahidi mwenyewe, kwani uhalifu haulipi chochote.

  Nini umahimu wa nidhamu? (maneno kati ya 50-55) (al. 1 ya mtiririko) :(alama 7.)
  Bila kubadilisha maana, fupisha aya nne za mwisho. (tumia maneno 55-60)(mtiririko alama 1) (alama 8)

 1. MATUMIZI YA LUGHA.
  1. Onyesha muundo wa silabi ya kwanza katika maneno yafuatayo. (alama 2)
   1. Chura
   2. Mbali
  2. Taja vigezo vya kuainisha irabu. (alama 2)
  3. Taja majukumu mawili ya viambishi awali katika kitenzi. (alama 2)
  4. Andika ukubwa wingi wa sentensi ifuatayo.
   Mbuzi yule ameumia mguu. (alama 2)
  5. Eleza ni kwa nini neno samehe ni la asili ya kigeni. (alama 1)
  6. Sahihisha sentensi ifuatayo. (alama 2)
   Mwanafunzi mwenye aliimba funguo yangu amepatikana.
  7. Eleza matumizi ya kiambishi ‘ku’ katika neno lifuatalo. (alama 1)
   hakukunyesha.
  8. Onyesha mzizi na viambishi katika neno lifuatalo. (alama 2)
   Wafao.
  9. Andika kwa usemi wa taarifa. (alama 2)
   “Fika mapema nikutume sokoni,” mama alimwambia mwanawe.
  10. Bainsisha virai katika sentensi ifuatayo .
   Anachukia kusoma riwaya yenye masuala ya kisiasa. (alama 3)
  11. Yakinisha katika nafsi ya tatu wingi. (alama 2)
   Sijasafiri kwenda marekani.
  12. Changanua sentensi ifuatayo kwa mchoro wa matawi.
   Mjomba anamkama ngombe wake. (alama 3)
  13. Tunga sentensi moja kudhihirisha matumizi ya shamirisho zifuatazo. (alama 3)
   1. Kutondo
   2. Kipozi
   3. ala
  14. Andika kinyume cha sentensi hii. (alama 2)
   Watoto wameombwa waanike nguo.
  15. Tumia kiambishi ‘ndi’ katika sentensi kama kishirikishi. (alama 1)
  16. Tofautisha sentensi zifuatazo kimaana. (alama 2)
   1. Tulipofika hotelini tulipewa soda na chupa.
   2. Tulipofika hotelini tulipewa soda kwa chupa.
  17. Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi ya alama zifuatazo. (alama 2)
   1. Kibainishi
   2.  Parandesi
  18. Bainisha ngeli za maneno yafuatayo. (alama 2)
   1. Uhondo
   2. Pua.
  19. Tumia neno hadi kama kihusishi cha (alama 2)
   1. Wakati
   2. Mahali.
  20. Andika sentesi ifuatayo upya kulingana na maagizo.(alama 2)
   Mkoba wa babu una viroboto (Anza kwa viroboto)
 1. ISIMU JAMII
  “ Beba! Beba-aa! Kila stage ni bao, kumi haitoshi hata adazi . Funga mshijpi karau mbele. …….
  1. Tambua sajili hii (alama 2)
  2. Eleza sifa nne zinazojitokeza katika dondoo hili (alama 4)
  3. Fafanua mambo manne yanayotatiza maendeleo ya Kiswahili shuleni. (alama 4)


MARKING SCHEME

 1. UFAHAMU
  1.  
   1. Waafrika hawakuwa wamehusishwa katika katiba ya mwaka wa 1920.
   2. Waafrika walitaka kuhusika katika masuala ya ukongozi.
   3. Utetezi wa wanasiasa ulilazimu serikali ya uingereza kuitisha kongamano. (3x1)
  2.  
   1. utawala mwema na uwajibikaji wa viongozi .
   2. Kulinda haki za binadamu zikiwemo za wanawake, watoto na walemavu.
   3. Kanuni za usawa na ulinganifu.
   4. Kutilia mkazo mahitaji ya kimsingi( 3x1)
  3.  
   1. Kuweka utaratibu na kanuni za utawala.
   2. Hufafanua vyombo vikuu vya serikali.
   3. Hupambanua haki za raia.
   4. Hukinga haki za raia
   5. Huimarisha asasi za umma.
  4.  
   1. Katiba ilikuwa imefanyiwa marekebisho mengi.
   2. Viongozi/Watu wenye uwezo walipuuza katiba.
   3. Uongozi uliokuweko uliwadhulumu wanawake, watoto na walemavu.
   4. Uharifu wa mazingira ,ufisadi na unyakuzi.
  5.  
   1. Kitovu –chenye umuhimu mkubwa.
   2. Harakati –Shughuli za kufanya jambo
   3. Hamasisha – Kufanya jambo lieleweke na kukubalika.
    Tanbihi
    Adhibu makosa ya kisarufi pindi yanapotokea. Usiadhibu zaidi ya nusu alama atakazozipata mtahiniwa katika swali husika.
    Adhibu hadi makosa sita ya hijai. (6x ½ ) =3
    Kosa lilelile lisiadhibiwe mara mbili.
 1. UFUPISHO
  1.  
   1. Mwenye nidhamu huwanuru/anga nyumbani, shuleni na katika jamii.
   2. Hupendelewanakuheshimiwa.
   3. Hutegemewa/kuwakiongozi
   4. Hunufaikasana
   5. Hupata fursa ya kuteuliwa katika dhima Fulani
   6. Hujiepushanashutumanamajanga. (6x1) (ut 1)
  2.  
   1. Hawezi kuhusishwa na majanga hatari.
   2. Utovu wa nidhamu huanzia mapema sana maishani mwa binadamu
   3. Mtoto hutegemea mwongozo wa mwelekezo wa watu wazima.
   4. Nidhamu /utovu wa nidhamu huanzia nyumbani hadi shuleni na kisha hupanuka.
   5. Sehemu moja ya nidhamu ya mja ikisambaratika hawezi kuwa mkamilifu.
   6. Watovu wa nidhamu huangamizwa na mola/hujutia.
   7. Mja ajitahidi mwenyewe
   8. Uhalifu haulipi chochote (7x1) + 1 (ut)
    a- 6
    b- 7
    ut-2
    Tanbihi
    Makosa 6 x ½ (Kisarufi)
    Makosa 6 x ½ (hijai)
    Ziada: Manenokumiyakwanza,toaalama 1
    Kilamanenomatanoyanayofuatatoanusualama.
 1. Maumizi ya lugha.
  1.  
   1. Chura
    ch –u
    k -  I                        
    (2x ½ ) = (alama 1)
   2. mba
    KKI       (alama 1)
  2.  
   1. Mkao wa ulimi chini
    kati
    juu                         (alama 2)
   2. Mahali Mbele
    kati
    nyuma
   3. Muundo wa midomo kuviringwa
    kutandazwa
    (vyovyoteviwili)
  3. Nafsi, ngeli, wakati, hali, kirejeshi, kitendwa, kitendewa , ukanusho, kujitendean.k (alama 2)
   (yoyotemawili)
  4. Mabuziyaleyameumiamaguu (alama 2)
   (kilaneno ½alama) (asipo pata neno la kwanza hakuna alama ya swali nzima)
  5. Kiishiosio ‘a’ (alama 1)
  6. Mwanfunzi aliyeiba ufunguo wangu amepatikana. (alama 2)
   (kila kitahiniwa ½alama )
  7. Ku ya kwanza – kukanusha wakati uliopita ya pili – Mahali
   (kikakitahiniwa ½ alama ) (alama 1)
   Wa   -     f   -   a   -   o
   nafsimzizikiishio ‘O’ rejeshi                         (alama 2)
   au
   wa     -   f   -   a - o
   kiambishiawali   mziziviambishitamati.                                     (alama 2)
   1. Mama alimwambiamwanaweafikemapemailiam (alama 2)
    (vitahiniwa ½ x4)
  8.  
   1. Anachukiakusoma – K .Kitenzi
   2. Riwaya yenye masuala ya kisasa K – nomino
   3. yenye masuala ya kisiasa K -Kivumishi (alama 3)
  9. Wamesafiri kwenda marekani. (alama 2) 
   KBBAFSGFWR         
  10. Mf. Mama alimpikia mgeni chai kwa sufuria
   kitondokipozi.       ala           (alama 3) (Kilakitahiniwanialama 1)
  11. Watoto wameamrishwa waanue (alama 2)
  12. Mf. Hiki ndicho changu (alama 1)
  13.  
   1. Walipewavituviwili
   2. Chupanikitumizi / ala (alama 2)
  14. Mf. Uhuru (raiswaKenya )amewauzang’ome wake.(alama 2)
   (kilaalamanimaki 1)
  15.  
   1. U-U
   2. I – Z (alama 2)
  16.  
   1. Mf.   i) Alilimahadijioni
   2. Alilimahadi pale.(alama 2)
  17. Viroboto vimo mkobani mwa babu. (alama 2)
 1. ISIMU JAMII
  1. Sajili ya sekta a matatu/utingo/uchukuzi wa abiria. (alama 2)
  2.  
   1. Mshangao/nidaa, mfano: Beba!
   2. Kuchanganya ndimi kwa mfano neno ‘stage’ badala ya kituo cha matatu/stesheni.
    -ulegevu wa sarufi kwa mfano, kumi haitoshi
    -Kauli fupifupi Beba!
    Matumizi ya msimu kwa mfano Karau mbele
    Lugha shairishi
    Msamiati teule: steji
  3.  
   • Matumizi ya kilugha cha sheng’
   • Athari za lugha ya kwanza (mama )
   • Kudumishwa kwa somo la Kiswahili na walimu wasioimudu.
   • kutengewa vipindi vichache vikilinganishwa na vya kiingereza.
   • Dhana potovu, kuwa Kiswahili ni lugha duni.
   • Wanafunzi kuwaiga wanasarakasi /wanasiasa wanaotumia lugha visivyo
   • Upungufu wa machapisho ya Kiswahili.
   • Upungufu wa walimu wa Kiswahili waliohitimu
    (zozote 4x1)

Download KISWAHILI PAPER 2 - KCSE 2019 MARANDA MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest