Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Kapsabet Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO KWA WATAHINIWA

 1. Andika jina lako, shule na nambari yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 2. Andika tarehe ya mtihani na utie sahihi yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 3. Jibu maswali yote.
 4. Andika majibu yako katika nafasi ulizoachiwa baada ya kila swali katika kijitabu hiki cha maswali.
 5. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

 1. SEHEMU YA A: UFAHAMU (alama 15)
  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali
  “Swala la idadi kubwa ya watoto wadogo wanaoendelea kumiminika mijini na kuonekana wakiranaranda mijini ovyo,halijapewa umuhimu wowote wa haja na serikali za nchi nyingi,licha ya mijadala katika warsha anuwai,zilizofanyika kujadili swala hili nyeti.
  Kwa kutokuwa na sheria ama sera iliyo wazi kuhusu haki na usalama wa watoto,sarikali zetu hazina budi kukubali kubeba uzito wote wa lawama. Hii ni kwa sababu, serikali zetu zimelipuuza na kuvalia miwani swala hili kwa kuchukulia kuwa litapotea lenyewe katika hewa yabisi. Yafaa ifahamike kuwa usalama wetu katika siku zijazo utategemea jinsi tutakavyolikabili ana kwa ana tatizo hili wakati huu. Wakati wa kutenda ni sasa. Aidha, watoto hawa wanaokulia mitaani bila malezi,maelekezo wala mwongozo mwafaka wa kimaisha, wanakua bila mapenzi hivyo hawajui maana ya kupenda. Wanachokijua ni chuki na haja ya kulipiza kisasi didhi ya jamii iliyowachonga jinsi walivyo. Hawajali lolote hata kifo. Wako tayari kujikabidhi kwa haini yeyote mwenye nia mbaya,bila kujali matokeo, muradi tu, wapate riziki.
  Tunapendekeza kwa serikali, washika dau kama vile mashirika ya kujitolea, viongozi wa dini, shule, vyuo na wananchi kwa jumla wachange bia katika kutafuta mikakati ya kulitatua tatizo hili kabla halijageuka kuwa janga la kijamii ambalo tutashindwa kulimudu. Mpango wa vijana hawa kujiunga na huduma ya taifa ni jambo linalofaa kutiliwa maanani.
  Tunapendekeza makao Zaidi ya watoto wanaozurura mijini yajengwe ambapo watapata mafunzo ya kiufundi yatakayowawezesha kujitegemea maishani. Badala ya kulitegea mgongo swala hili, serikali zinawajibika kuwasajili hawa watoto ili waweze kuunganishwa na familia na koo zao. Utafiti uliofanywa na wataalamu wa Elimu jamii umebainisha kuwa ni asilimia kumi tu ya watoto hawa wa mitaani wasiokuwa na mahali wawezapo kupaita nyumbani. Asilimia tisini iliyobaki, angalau wana mahali wanapoweza kupaita nyumbani ilhali wanaendelea kuwa mitaani. Wazazi tumesahau wajibu wetu. Wengi wetu tumelikimbia jukumu la ulezi tulilopewa na muumba. Hawa waliojipaka masizi mwilin mzima, wanaozurura ovyo mitaani, si matokeo ya maumbile;hawakuja duniani kwa sadfa, hawakuulizwa wala kushauriwa. Makosa ni yetu wazazi. Tuliwaleta hapa duniani, kisha tukawakimbia.Hatutasamehewa duniani na akhera.
  Mwenye njaa hana miiko. Ili kijiruzuku, hawa watoto daima wanachumia jaani.Kwa kudura ya jalia, huenda siku moja watalia kivulini. Asiyekuwa na wake ana mungu.Aghalabu, watoto wanaozurura mitaani hupewa pesa na wafadhili. Wakati mwingine wanaiba. Maisha haya ya kuomba au kuiba wanaona yanaridhisha Zaidi kuliko kumenyeka na kazi ya kibarua kutwa kucha. Kwa bahati mbaya, watoto hawa wamatumia pesa wanazopata kutoka kwa wafadhili kujichimbia kaburi. Aidha pesa wanazopatiwa watoto hawa wanazitumia kununulia gundi badala ya chakula.
  Wafadhili wanashauriwa wawape chakula hawa watoto badala ya pesa taslimu. Kusema kweli, unapompa mtoto wa mitaani pesa,utakuwa unainua biashara ya mwenye kiwanda cha gundi,jambo ambalo litakuwa sawa na kuweka sahihi mkataba wa kifo cha mtoto mwenyewe.
  Wataalamu wa afya wanaonya kuwa gundi ikivutwa kwa muda mrefu inaweza kusababisha upofu au kifo.Wataalamu hawa wanazidi kutuarifu kuwa matumizi ya muda mrefu ya gundi huathiri ubongo,figo na maini. Mtumiaji pia anaweza kupoteza uwezo wa kutembea na hata kupooza kabisa.
  Sababu wanazotoa hawa watoto ni kwamba, uvutaji gundi,huwaondolea njaa,baridi ya usiku na kuwatuliza mawazo. Ni jambo la kusikitisha kwamba tunaendelea kushuhudia bila kujali hawa watoto ambao ni kiungo cha jamii yetu,wakijiangamiza. Wananchi kwa ujumla hawaha budi kuhamasishwa dhidhi ya athari ya matumizi ya gundi.Wafanya biashara wanaowauzia watoto hawa gundi yafaa wakome,la sivyo wachukuliwe hatua.Kutolitatua tatizo hili la watoto wa mitaani hivi sasa,kutapeleka kuwako kwa kizazi cha mitaani ambacho kitazaliwa mitaani,kulelewa mitaani,kuoa mitaani na kufia mitaani.Kadiri mataifa yanavyoendelea kujitia hamnazo kuhusiana na swala hili,ndivyo tunavyokubalia jinai itawale,sasa na wakati ujao.
  Hawa watoto watakapokua,watageuka kuwa wapigaji watu kabari,majambazi,wezi wa kutumia nguvu ama watatumiwa na mahaini kutimiza uhaini wao.Hawa watoto wenye njaa,watalazimika hatimaye,kuwatoa wenywe shibe tonge mdomoni.Matokeo ya hali hii ni kwamba katika siku zijazo,hawa ndio watu watakaotunyima starehe ya kulala unono.Watatuchafya mitaani,majumbani,vijijini na kutuvizia mabarabarani.Tuna sababu nzuri ya kutiwa hofu na tatizo hili,kwani jinsi kizazi kinavyozidi kupanuka,inaonekana tumelitega bomu ambalo litakuja kutulipukia usoni mwetu.”

  Maswali
  1. Taja jambo moja linalochangia kuweko kwa watoto wanaorandaranda mitaani. (alama 1)
  2. Maisha ya mitaani huathirije watoto? ( alama 3)
  3. Tatizo la watoto wanaorandaranda mitaani laweza kutatuliwaje? (alama 3)
  4. Eleza maana ya: (alama 2)
   1. Hawa watoto wanachumia jaani
   2. Jinsi kizazi cha mitaani kinavyozidi kupanuka,inaonekana tumelitega bomu ambalo litakuja kutulipukia usoni mwetu. (alama 2)
   3. Mwenye njaa hana miiko. (alama 2)
  5. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika kwenye taaria: (alama 2)
   1. Aidha:
   2. Gundi:
 2. UFUPISHO:(ALAMA 15)
  Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yafuatayo
  Lugha ndio msingi wa maandishi yote. Bila lugha hakuna maandishi. Kila jambo tufanyalo kuhusiana na lugha husitawisha ufahamu wetu wa mambo tusomayo. Mazoezi katika kuandika husitawisha ufahamu katika kusoma kwa sababu katika kuandika ni lazima kuyatumia maneno vizuri na kufahamu ugumu wa usemi. Twajifunza matumizi ya lugha katika kuzungumza na kuwasikiliza wengine wakizungumza. Lugha tusomayo ni anina ya lugha ya masungumzo.
  Kuna ujuzi mwingi katika kuzungumza kama vila michezo ya kuigiza, hotuba, majadiliano na mazungumzo katika darasa. Haya yote husaidia katika uhodari wa matumizi ya lugha. Ujuzi wa kila siku utasaidia katika maendeleo ya kusoma na usitawi wa msamiati. Ikiwa mwanafunzi amemwona ndovu hasa, atakuwa amejua maana ya neno ndovu vizuri zaidi kuliko mwanafunzi ambaye hajawahi kumwona ndovu bali ameelezwa tu vile ilivyo. Vilevile ujuzi wa kujionea sinema au michoro husaidia sana katika yaliyoandikwa. Ikiwa mwanafunzi ana huzuni au ana furaha, akiwa mgonjwa au amechoka au amefiwa, haya yote ni ujuzi. Wakati juao mwanafunzi asomapo juu ya mtu ambae amepatikana na mambo kama huyo hana budi kufahamu zaidi.
  Karibu elimu yote ulimwenguni huwa imeandikwa vitabuni. Hata hivyo, lugha zote hazina usitawi sawa kuhusu fasihi. Kwa bahati mbaya lugha nyingine hazijastawi sana na hazina vitabu vingi. Fauka ya hayo , karibu mambo yote yanayohusiana na elimu huweza kupatikana katika vitabu kwenye lugha nyingine.
  Inambidi mwanafunzi asome vitabu au majarida juu ya sayansi au siasa au historia, lakini haimbidi kusoma tu juu ya taaluma fulani anayojifunza . Inafaa asome juu ya michezo, mambo ya mashairi na juu ya mahali mbalimbali ili kupata ujuzi wa mambo mengi.
  1. Fupisha aya za kwanza mbili kwa kutumia maneno 65 (alama 10, 1 ya utiririko)
   Matayarisho
   ……………………………………………………………………………………………………
   Jibu
   …………………………………………………………………………………………………
  2. Kwa kuzingatia habari zote muhimu na bila kupoteza maana asilia, fupisha aya ya mwisho
   (Maneno 30) (alama 5 utiririko)
   Matayarisho
   ……..
   Jibu
   ……………
 3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
  1. Toa mifano miwili miwili ya (al.2)
   1. Sauti ghuna ambazo ni vipasuo ………………………………………….…………..
   2. Sauti sighuna ambazo ni vikwamizo ………………………………….………………
  2. Onyehsa mofimu katika neno Aliyemcha (al.2)
  3. Andika sentensi yenye muundo ufuatao (al.2)
   KN(W+V) + KT (t +RH)
  4. Tumia neno shirika kama nomino na kama kielezi katika kutunga sentensi moja (al.2)
  5. Kwa kutunga sentensi vumisha nomino nguruwe kuwa kivumishi cha idadi bainifu. (al.1)
  6. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya kutendewa (al.1)
   Mtoto wa waziri amekufa
  7. Yakinisha sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu wingi (al.2)
   Msomi hakutuzwa siku hiyo
  8. Tunga sentensi moja inayobainisha maana mbili tofauti za neno chuma (al.2)
  9. Tambua kiima na aina za yambwa katika sentensi ifuatayo. (al.4)
   Mwalimu mkuu hupigiwa nguo pasi na Maria
  10. Kwa kutumia mifano mwafaka fafanua miundo yoyote miwili ya kirai nomino (al.2)
  11. Andika sentensi ifuatayo kwa wingi (al.2)
   Mgeni huyo na mwingine walikula wali kwa uma
  12. Andika neno lenye silabi funge yenye muundo wa konsonanti moja (al.1)
  13. Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika udogo wingi (al.2)
   Ng’ombe wangu ana ndama mdogo
  14. Tunga sentensi zenye mipangilio ifuatayo; (al.4)
   1. Kishazi tegemezi na kishazi huru
   2. Kishazi tegemezi na kishazi tegemezi
  15. Eleza matumizi ya ‘ki’ katika sentensi ifuatayo: (al.3)
   Nyamunga na kitoto wamekuwa wakila, wakiimba kikasuku
  16. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mchoro wa matawi. (al.4)
   Mtoto wa mjomba alikuja kwetu nyumbani jana
  17. Andika kwa msemo wa taarifa. (al.2)
   ‘Yafaa tumwendee mama mkubwa ili atushauri juu ya jambo hili,’ Amina alipendekeza.
  18. Andika kinyume cha: (al.1)
   Chakula hiki kitamu nitakimeza
  19. Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo. (al.2)
   1. Kiwakilishi nafsi huru
   2. Kiwakilishi nafsi kiambata
 4. ISIMUJAMII (alama10)
  1. Tofautisha kati ya kuhamisha msimbo na kuchanganya msimbo. (alama 2)
  2. Taja mambo mawili yanayochangia katika uhamishaji msimbo. (alama 2)
  3. Taja kaida mbili zinazotawala maamkizi katika jamii huku ukitoa mifano mwafaka. (alama2)
  4. Fananisha sifa zozote nne za sajili ya maabadini na mahakamani. (alama 4)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. UFAHAMU: ALAMA 15
  1.    
   1. Wazazi kukwepa jukumu la ulezi.
   2. Kutokuwa na sheria/sera iliyo wazi kuhusu usalama wa watoto
    Hoja yoyote 1x1=1
  2.    
   1. Hukosa mapenzi.
   2. Hukosa malezi,maelekezo na mwongozo mwafaka maishani
   3. Huiga tabia bofu K.M kuvuta gundi na kuiba.
   4. Njaa
    Zozote 3x1=3
  3.    
   1. Kutiliwa maanani kwa mpango wa vijana wa kujiunga na huduma ya taifa
   2. Kuongeza makao ya watoto na kuwapa mafunzo ya kiufundi
   3. kuwasajili watoto ili waweze kuunganishwa na familia zao
   4. Wafadhili wawape chakula badala ya pesa taslimu
   5. Wanaowauzia gundi wahamasishwe dhidi ya matumizi yake
    Zozote 3x1=3
  4.    
   1. Tegemeo lao ni makombo na takataka iliyo mapipani (alama 2)
   2. Kutolitatua tatizo la watoto wanaorandaranda mitaani kutatuletea matatizo
   3. Mhitaji hachagui chochote (alama 2)
  5.       
   1. Aidha-pia
   2. Gundi- Kitu kiolevu na kinachonata kunachonuswa na watoto kama kileo 1x2=2
 2. UFUPISHO: (ALAMA 15)
  Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali yafuatayo
  Lugha ndio msingi wa maandishi yote. Bila lugha hakuna maandishi. Kila jambo tufanyalo kuhusiana na lugha husitawisha ufahamu wetu wa mambo tusomayo. Mazoezi katika kuandika husitawisha ufahamu katika kusoma kwa sababu katika kuandika ni lazima kuyatumia maneno vizuri na kufahamu ugumu wa usemi. Twajifunza matumizi ya lugha katika kuzungumza na kuwasikiliza wengine wakizungumza. Lugha tusomayo ni anina ya lugha ya masungumzo.
  Kuna ujuzi mwingi katika kuzungumza kama vila michezo ya kuigiza, hotuba, majadiliano na mazungumzo katika darasa. Haya yote husaidia katika uhodari wa matumizi ya lugha. Ujuzi wa kila siku utasaidia katika maendeleo ya kusoma na usitawi wa msamiati. Ikiwa mwanafunzi amemwona ndovu hasa, atakuwa amejua maana ya neno ndovu vizuri zaidi kuliko mwanafunzi ambaye hajawahi kumwona ndovu bali ameelezwa tu vile ilivyo. Vilevile ujuzi wa kujionea sinema au michoro husaidia sana katika yaliyoandikwa. Ikiwa mwanafunzi ana huzuni au ana furaha, akiwa mgonjwa au amechoka au amefiwa, haya yote ni ujuzi. Wakati juao mwanafunzi asomapo juu ya mtu ambae amepatikana na mambo kama huyo hana budi kufahamu zaidi.
  Karibu elimu yote ulimwenguni huwa imeandikwa vitabuni. Hata hivyo, lugha zote hazina usitawi sawa kuhusu fasihi. Kwa bahati mbaya lugha nyingine hazijastawi sana na hazina vitabu vingi. Fauka ya hayo , karibu mambo yote yanayohusiana na elimu huweza kupatikana katika vitabu kwenye lugha nyingine.
  Inambidi mwanafunzi asome vitabu au majarida juu ya sayansi au siasa au historia, lakini haimbidi kusoma tu juu ya taaluma fulani anayojifunza . Inafaa asome juu ya michezo, mambo ya mashairi na juu ya mahali mbalimbali ili kupata ujuzi wa mambo mengi.
  1. Fupisha aya za kwanza mbili kwa kutumia maneno 65 (alama 10, 1 ya utiririko)
   Matayarisho
   • Kila jambo tufanyalo katika lugha hustawisha ufahamu wake.
   • Mazoezi ya kuandika hustawisha ufahamu wa kusoma.
   • Twajifunza matumizi ya lugha katika kuzungumza na kuwasikiliza wengine.
   • Lugha iliyoandikwa ni ya aina ya mazungumzo.
   • Ujuzi mwingi katika kuzungumza hupatikana shuleni.
   • Ujuzi wa kila siku husaidia katika maendeleo ya kusoma na msamiati.
   • Husaidia kufahamu yaliyoandikwa.
   • Hali ya mwanafunzi kujionea sinema ni ujuzi.
   • Matatizo na shida ambazo wanafunzi hupitia pia ni ujuzi.
  2. Kwa kuzingatia habari zote muhimu na bila kupoteza maana asilia, fupisha aya ya mwisho
   (Maneno 30) (alama 5 utiririko)
   Matayarisho
   • Karibu elimu yote imeandikwa vitabuni.
   • Lugha zote hazina ustawi mwingi.
   • Nyingine hazina vitabu ama zina vitabu vingi.
   • Mwanafunzi anayesoma anafaa kusoma mengi kando na taaluma anayoisoma.
 3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
  1. Toa mifano miwili miwili ya (al.2)
   1. Sauti ghuna ambazo ni vipasuo /b/ /d/ /g/
   2. Sauti sighuna ambazo ni vikwamizo /f/ /th/ /sh/ /h/
  2. Onyesha mofimu katika neno Aliyemcha
   a-nafsi/ngeli li-wakati ye-kirejeshi m-yambwa mtendewa ch-mzizi a-kiishio
  3. Andika sentensi yenye muundo ufuatao (al.2)
   KN(W+V) + KT (t +RH)
   Yule mtukutu alikuwa chini ya mti
  4. Tumia neno shirika kama nomino na kama kielezi katika kutunga sentensi moja (al.2)
   Wafanyakazi wa shirika lile walifanya kazi kwa ushirikiano/kishirika
  5. Kwa kutunga sentensi vumisha nomino ng’ombe kwa kivumishi cha idadi bainifu. (al.1)
   Ng’ombe sita wamepelekwa malishoni
  6. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya kutendewa (al.1)
   Mtoto wa waziri amekufa
   Waziri amefiwa na mtoto wake
  7. Yakinisha sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu wingi (al.2)
   Msomi hakutukuzwa siku hiyo
   Wasomi watakuwa wametuzwa siku hiyo
  8. Tunga sentensi moja inayobainisha maana mbili tofauti za neno chuma (al.2)
   Kifaa cha madini
   Tafuta pesa
   Toa matunda mtini
   Bakari alichuma matunda ya parachichi kwa kutumia kifaa kilichotengenezwa kwa chuma
  9. Tambua kiima na aina za yambwa katika sentensi ifuatayo. (al.4)
   Mwalimu mkuu hupigiwa nguo pasi na Maria
   Mwalimu mkuu – yambwa tendewa/kitondo
   nguo –yambwa tendwa/kipozi
   pasi – yambwa ala/ kitumizi
   Maria - kiima
  10. Kwa kutumia mifano mwafaka fafanua miundo yoyote miwili ya kirai nomino (al.2)
   Nomino pekee (N)
   Kiwakilishi (W)
   N+U+N – Nomino +Kiunganishi +Nomino
   N+V – Nomino + Kivumishi
   N+V+V – Nomino + Kivumishi + Kivumishi
   N+V+E – Nomino + Kivumishi + Kielezi
   N+S – Nomino + Kishazi
  11. Andika sentensi ifuatayo kwa wingi (al.2)
   Mgeni huyo na mwingine walikula wali kwa uma
   Wageni hao na wengine walikula wali kwa nyuma
  12. Andika neno lenye silabi funge yenye muundo wa konsonanti moja (al.1)
   m-toto
   m-tu
  13. Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika udogo wingi (al.2)
   Ng’ombe wangu ana ndama mdogo
   Vigombe vyangu vina vidama vidogo
  14. Tunga sentensi zenye mipangilio ifuatayo; (al.4)
   1. Kishazi tegemezi na kishazi huru
    Mtoto aliyewasili leo amerudi kwao
    K.T K.H
   2. Kishazi tegemezi na kishazi tegemezi
    Angalilima kwa bidii angalivuna mavuno tele
    K.T K.T
  15. Eleza matumizi ya ‘ki’ katika sentensi ifuatayo: (al.3)
   Nyamunga na kitoto wamekuwa wakila, wakiimba kikasuku
   kitoto – udogo
   wakila , wakiimba – vitendo viwili kufanyika kwa wakati mmoja
   kikasuku – ki ya kielezi
  16. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mchoro wa matawi. (al.4)
   Mtoto wa mjomba alikuja kwetu nyumbani jana
       S
   KN KT
      N     V       N         T           V         E           E
   Mtoto wa mjomba alikuja kwetu nyumbani jana
  17. Andika kwa msemo wa taarifa. (al.2)
   ‘Yafaa tumwendee mama mkubwa ili atushauri juu ya jambo hili,’ Amina alipendekeza.
   Amina alipendekeza kuwa ilifaa wamwendee mama mkubwa ili awashauri juu ya jambo hilo
  18. Andika kinyume cha: (al.1)
   Chakula hiki kitamu nitakimeza
   Chakula hiki kichungu nitakitema
  19. Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo.
   1. Kiwakilishi nafsi huru
    Mimi hupika vizuri/sisi/wewe/nyinyi/yeye/wao
   2. Kiwakilishi nafsi kiambata
    Aliondoka jana/wa/ni/tu/u/m
 4. ISIMUJAMII
  1.    
   • kuhamisha msimbo ni kutumia lugha fulani katika mazungumzo kisha ukaanza kutumia lugha nyingine tofauti na ile ya kwanza.
   • Kuchanganya ndimi ni matumizi ya maneno au msamiati wa lugha zaidi ya moja katika mazungumzo. 
  2.    
   1. Ukosefu wa msamiati unaofaa katika lugha hiyo.
   2. Wazungumzaji kutojua lugha husika vizuri.
  3.    
   1. Wakati – kwa mfano kuna maamkizi ya asubuhi kama vile “subalkheri”, na ya jioni kama vile “masalkheri”.
   2. Umri – kwa mfano mtu wa umri mdogo humwamkua mkubwa wake “shikamoo” naye hujibu, “ marahaba”.
    (2 x 1 =2)
  4.      
   1. Mtu mmoja hutawala mazugumzo kama vile hakimu, wakili, kasisi, shehe n.k.
   2. Mazungumzo hurejelea kanuni zilizoandikwa kama vile sheria za nchi, Korani, Biblia n.k.
   3. Lugha ya heshima hutumika kama vile mheshimiwa, dada, ndugu n.k.
   4. Mazungumzo hutolewa mahali maalum kama vile mahakamani, msikitini, kanisani au hekaluni.
   5. Lugha sanifu hutumika ili ieleweke vizuri.
   6. Mazungumzo huweza kueleweka tu na wahusika wenyewe.
    (zozote 4 x 1= 4)
    • Ondoa nusu alama kwa kila kosa tofauti la hijai hadi makosa 4, yaani alama 2
    • Ondoa nusu alama kwa kila kosa tofauti la sarufi hadi makosa 4, yaani alama 2.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Kapsabet Mock Exams 2021/2022.

Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students

Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest