Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Asumbi Girls Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

SEHEMU A : FASIHI SIMULIZI

 1. LAZIMA (ALAMA 20)
  1. Jadili sifa zozote nne za mtambaji bora. (alama 4)
  2. Fafanua hasara zozote nne za miviga. (alama 4)
  3. Jadili hatua tano zinazofuatwa wakati wa utafiti. (alama 5)
  4. Tofautisha istilahi zifuatazo za Fasihi Simulizi. (alama 3)
   1. Matambiko
   2. pembezi
   3. Misimu 
  5. Eleza sifa nne za maapizo. (alama 4)

SEHEMU B: RIWAYA
ASSUMPTA MATEI: CHOZI LA HERI   
Jibu swali la 2 au la 3

 1. Mwandishi amejadili kwa kina maudhui ya mapuuza. Thibitisha . (alama 20)
  Au
 2. Maisha yangu yalijaa shubiri tangu utotoni. 
  1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
  2. Fafanua mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili. (alama 4)
  3. Jadili jinsi mwandishi amesawiri suala la ukatili. (alama 12)

SEHEMU C: HADITHI FUPI
Chokocho na Kayanda(Wah)Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
Jibu swali la 4 au la 5

 1. Jadili maudhui yaliyoonyeshwa kwenye mabano kutoka hadithi zifuatazo.(alama 20)
  1. Tumbo Lisiloshiba (utabaka)
  2. Masharti ya Kisasa (Unyumba)
  3. Mkubwa (Ufisadi )
  4. Mwalimu Mstaafu (Elimu)
   au
 2. Tulipokutana Tena
  1. Jadili istilahi za lugha zinazojitokeza katika kifungu hiki. (alama 4)
   ‘Bogoa gani huyo?’ Kazu alibadilisha toni ya sauti na mng’aro wa sura yake. Alikuwa tayari kajaa huzuni ingawa hadithi yenyewe alikuwa haifahamu vizuri. Usoni pake ulisimama unyeti na juu ya ngozi ya uso wake huruma zilijitokeza. Ndivyo alivyo Kazu kila siku. Anaweza kubadilika mara moja kama uso wa mtoto mchanga.
  2. Jadili umuhimu wa Bi Sinai katika hadithi hii. (alama 8)
  3. ‘Jijini ni kuzuri. Kuna majumba makubwa, utapanda magari mazuri mazuri ya marafiki zetu, utakula vyakula vitamu na kupewa nguo za fahari. Utapelekwa shule kusoma na kuandika.‘ Kwa Bogoa , maneno haya ya babake  ni kinaya.  Thibitisha kwa hoja nane.  (alama 8)

SEHEMU D: TAMTHILIA 
KIGOGO  PAULINE KEA
Jibu swali la 6 au la 7

 1.      
  1. Jadili dhamira ya mwandishi wa Tamthilia ya Kigogo. (alama 10)
  2. Fafanua jinsi Ujenzi wa jamii mpya umeshughulikiwa na mwandishi. (alama 10)
   au
 2. Kutia kwa kulia na kutoa kwa kushoto.
  1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
  2. Fafanua mbinu ya lugha iliyotumika. (alama 2)
  3. Fafanua sifa nne za msemaji wa maneno haya. (alama 4)
  4. Jadili mbinu hasi za uongozi katika Tamthilia. (alama 10)

SEHEMU E: USHAIRI  (Alama 20)

 1. SOMA SHAIRI  KISHA UJIBU MASWALI.
  1. Sidhani ni kichekesho, kesho kuwepo sidhani
   Vilivyoko ni vitisho, viwewe na visirani
   Mimi kupe kwenye josho, la sumu iso imani
   Kesho yangu imeshaliwa.
  2. Kesho yangu imeshaliwa, isibaki hata kitwa
   Kwamba hai nitakuwa, kesho na kesho kutwa
   Hilo haliwezi kuwa, na wakati limepitwa
   Na i wapi kesho yangu?
  3. Sikwambii mtondoo, au ni mtondogoo
   Ajapowika jogoo, kesho sipo ng'oo
   Hata simu za "haloo", hazinipati "haloo"
   Nitaituhumu kesho.
  4. Kesho nitaituhumu, kwa sababu ya hasama 
   Hasama ya mahasimu, waliolishana njama
   Kutaka kunihujumu, wanizulie nakama 
   Itokapi yangu kesho?
  5. Wa kwanza huyu Ukimwi, daima aniotea
   Kwa dawa huyu hazimwi, haachi kuturingia
   Amekuwa kama zimwi, mtu lisilomjua 
   Ati nipangie kesho?!
  6. Nipange yangu matanga, au kujenga nyumba?
   Nipange kung'oa nanga, au shairi kuimba?
   Nipangeni cha kupanga, biashara za mtumba?
   Kesho si ukoo wangu.
  7. Ukimwi nduguze wako, Ebola na Malaria
   Kichomi na sekeneko, mno wajifaragua 
   Maadamu wangaliko, vipi kesho kuwazia?
   Kesho si ndu yangu mwandani.
  8. Mimi napangia leo, maana kesho sijui
   Usafiri nifanyao, kwenye vyombo anuwai
   Una mikasa kibao, majanga ya kila nui
   Salama yangu i wapi?
  9. I wapi salama yangu, huku wapo wa kijicho
   Ngaa nipatapo changu, waingiwa mpekecho
   Kunipikia majungu, nikikosa changu hicho
   Waso nitakia kesho!
  10. Kesho wasonitakia, watele kama siafu
   Majambazi nasinzia, tapeli na wazinifu
   Roho yangu wapania, kunipeleka kwa ufu
   Nipewe jina "Hayati"
   1. Ujumbe wa shairi hili unakatisha tamaa. Thibitisha. (4)
   2. Hili ni shairi la aina gani? (1)
   3. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari.  (4).
   4. Eleza mbinu nne za lugha zilizotumiwa. (4)
   5. Andika bahari kwa kuzingatia vigezo; (2).
    Mizani
    Vina
   6. Onyesho jinsi mshairi alivyotumia idhini yake ya kishairi. (2).
   7. Taja;  (3)
    Toni 
    Nafsi - neni
    Nafsi- nenewa.  


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1.      
  1.      
   • mbunifu – awe na uwezo wa kuwasilisha hadithi kwa namna ya kuwachangamsha. Abuni hadithi upya mara tu anapoitamba.
   • Afahamu lugha- Awe na ufahamu mpana wa lugha husika na utamaduni unaohusika ili awasilishe vyema ngano yake.
   • Afahamu hadhira yake na mahitaji yao- wake , waume, watoto, vijana, nk . apatane vyema na mazingira yake ya kisimulizi.
   • Mcheshi- ili kuinasa makini ya hadhira yake.
   • uwezo wa ufaraguzi na afahamu mbinu zifaazo za sanaa na maonyesho – uwezo wa kuunda, kugeuza na kuwasilisha kazi ya fasihi simulizi papo hapo.
   • Afahamu tabia za binadamu- mambo yanayofurahisha, kuudhi, kuchangamsha, kuvutia au kumpendeza. Pia wafahamu mikondo mbalimbali ya jamii.
   • Sauti yake isikike na ibadilike ipasavyo.
   • Ashirikishe hadhira yake-  anaweza kuwauliza maswali,  waimbe nyimbo nk
   • Jasiri – aweze kuzungumza hadharani bila haya hasa masuala ya aibu.
   • Afahamu utamaduni wa hadhira yake ili atoe ujumbe kwa njia inayokubalika na hadhira na asije akatumia ishara au maneno yasiyokubalika pale.
  2.      
   • Zingine hazina faida yoyote
   • Zingine zaweza kusifu tamaduni zinazodhalilisha watu fulani
   • Zaweza kuleta utengano kati ya majirani hasa zile zinahifadhi siri
   • Zaweza kuleta matabaka
   • Zingine huenda kinyume na mabadiliko ya wakati. Baadhi ya matendo wakati wa matanga na unyago yamepitwa na wakati.
   • Huweza kusababisha tofauti ya kijinsia kv jando na ndoa kwani humdhalilisha mwanamke na kumtukuza zaidi mwanamume.
   • Ina gharama – mavazi, chakula, zawadi,nk
   • Baadhi hujaza hofu.
  3.      
   1. Maandalizi_ mada ya utafiti, mawanda ya utafiti, walengwa, kipindi cha utafiti, kibali, mbinu za kukusanya na kuhifadhi na gharama ya utafiti.
   2. Utafiti na ukusanyaji wa data yenyewe. Kuhusisha mbinu mbalimbali kama vile kuhoji, hojaji, kushuhudia au kujaza fomu.
   3. Kurekodi data kwa kuandika- kunasa habari ama kupiga picha za kawaida ama video au zote tatu.
   4. Kuchunguza data – ili kutafsiri na kuandika upya neno kwa neno bila kupotosha maana halisi ya lugha asili.
   5. Kuchambua/ kuchanganua na kufasiri data ili kupata matokeo kamili ya utafiti na mapendekezo. 
  4.    
   1. Sadaka au ada inayotolewa kwa Mungu, mizimu, pepo au miungu ili wasaidie binadamu kutatua mambo magumu, kuomba radhi au kutoa shukrani. Matatizo ni kama vile ukame, magonjwa, kukosa watoto, mafuriko au janga lolote lililomshinda binadamu nguvu na uwezo.
   2. Tungo za sifa za watu wa aina fulani wanaosifika kwa matendo yao au nafasi walizo nazo katika jamii kv matendo ya kishujaa au kujitolea kwao. Km viongozi, walezi wazuri, waganga, nk
   3. Semi zinazozuka na kutumiwa na kundi fulani la wanajamii kama misemo ya mawasiliano baina ya wanakikundi hicho./    Ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka tu kutegemea mazingira maalum./    Ni semi ndogo ndogo za kupita. Huzuka katika mazingira fulani  na hufa baada ya kutokuwepo kwa mazingira yale.
  5.    
   • Hutolewa kwa watu waliotenda kinyume na matarajio ya jamii zao.
   • Baadhi yalitolewa kabla ya ulaji wa viapo.
   • Yanaweza kutolewa moja kwa moja na aliyeathirika.
   • Huaminiwa yanaleta maangamizi kwa jamii, hivyo wanajamii hushauriwa kuyaepuka kwa kutenda mema.
   • Hutumia lugha fasaha na mtoaji kwa kawaida huwa mlumbi.
   • Hutumia lugha kali ya kuonya  na kujaza woga ili watu waache maovu.
 2.      
  • Viongozi kuharibu misitu. Msitu wa Mamba. Kukata miti ya makaa na mbao.
  • Mwalimu kupachika mwanafunzi mimba. Fumba kwa Rehema 
  • Kutupa mtoto kwenye taka. Aliyeokotwa na Neema.
  • Kuacha familia. Annete. Naomi. Subira
  • Kutorudi nchini. Wanawe Kiriri wanakatalia ughaibuni badala ya kurudi kumsaidia biashara na kujenga nchi 
  • Kutogharamia malezi. Fumba kuachia Chandachema nyanyake.
  • Kumwaga taka. Mtaa wa Sombera
  • Wanasiasa kupuuza vijana baada ya kuwafanyia kampeni.
  • Kutahiri wasichana. Tuama. Wasichana wanakufa
  • Kupuuza umuhimu wa masomo. Zohali kufanya mapenzi akiwa shuleni na kupachikwa mimba.
  • Mamake Umu kukataa kusaidia ombaomba
  • Kuuzia raia mahindi yaliyoharibika.
  • Raia kupokea hongo. Wanapuuza jukumu lao la kuboresha uongozi. Papa anatoa hongo na basi kuendeleza uongozi mbaya.
  • Tindi kupuuza ushauri wa mama kutorudi nyumbani baada ya saa kumi na moja magharibi na anarudi siku inayofuata. Kifo cha Lemi. 
  • Terry kupuuza Ridhaa kuhusu milio ya bundi kuwa mbiu ya mgambo na kuishia kuchomwa na Kedi.
  • Kupuuza kuelekeza mtoto. Wazazi wa Zohali waliodhalilisha badala ya kumwelekeza alipopata mimba na akatoroka nyumbani.
  • Polisi kurusu magari makuukuu barabarani kwani yanamilikiwa na miamba isiyogusika
  • Viongozi kutoimarisha viwango vya
  • Sauna/ Umu. Kutenganisha na nduguze.
  • Fumba/ Rehema. Mimba na kumkatiza masomo
  • Fumba/ Chandachema. Kutokea
  • Satua/ Chandachema. Kuteta vitu vidogo kuisha na alijua hana walezi.
  • Tenge/Kimai. Kuwa na uhusiano nje ya ndoa
  • Maya/ Sauna. Kumbaka
  • Kimbaumbau/ Naomi. Kumtaka mapenzi kumsingizia, kumtusi na kumfuta kazi.
  • Wazazi wa Zohali/ Zohali
  • mlevi/ Pete. Kumbaka
  • Pete/ kitoto chake cha pili
  • Mama Pete/Pete. Kumwachia nyanya ulezi bila kutuma mahitaji
  • Mama na wajomba wa Pete/ Pete. Kumkatizia masomo ili wamwoze kwa Fungo aliye na wake watatu tayari.
   zozote 20
 3.      
  1.      
   • Maneno ya Chandachema
   • Kwa Zohali, Umu, Kairu na  Mwanaheri
   • Bwenini shuleni Tangamano
   • Walikuwa wakihadithia maisha yao ili kumliwaza Umu asione kuwa ni yeye tu amepitia magumu.
  2.    
   • chuku- maisha kujaa shubiri tangu utotoni
   • jazanda- shubiri-mahangaiko/ shida/tabu/ matatizo
  3.    
   • Kuchoma. Kedi kuchoma familia ya Ridhaa./ Raia kuchoma Lemi. 
   • Kunyakua wa ardhi ya wengine.
   • Wakoloni kuchukua ile ardhi ya Waafrika iliyokuwa na rutuba.
   • Kulazimishwa kazi. Wakoloni kutumia vijana.
   • Kulawitiwa. Vijana walilalitiwa na hakuna aliyewatetea.
   • Vitisho. Mwekevu kutukanwa na kutishwa na wanaume anapowania uongozi.
   • Mauaji. Polisi kuua wakimbizi/
   • Kukatwa. Subira
   • Kubakwa. Lime na Mwanaheri. / Maya kubaka Sauna.
   • Kutishia afya. Viongozi kumwaga taka mtaa wa Sombera.
   • Kuuzia raia mahindi yaliyoharibika.
   • Kuteka nyara. Sauna
   • Kudhalilisha watoto. Wazazi wa Zohali.
   • Kupachika mwanafunzi mimba. Fumba kwa Rehema.
   • Tohara kwa wasichana. Tuama kuunga mkono.
   • Kuozwa mapema. Pete kuozwa na mamake na wajomba kwa Fungo.
   • Kuavyawa. Pete/ Sauna waliavya mimba na kunyimana nafasi ya kuishi.  
    Zozote 12
 4.      
  1.    
   • Matajiri hawajali maskini
   • Wananyakua ardhi ya maskni ili kusuluhisho matatizo yao
   • Matajiri wanaishi jijini kwenye hali nzuri na Wananchi wanaishi kwenye hali duni.
   • Makao tofauti. Jijini kuna majumba ya kifahari yaliyosimama kwa majivuno matupu ilhali Madongoporomoka watu wanaishi vibandani
   • Matajiri wananyanganya wa tabaka la chini uraia.
   • Viongozi kuwekea vikwazo vya sheria ili wasitetee mali zao wanazowapoka.
   • Wanasheria wanadhulumu wanyonge kwa kukosa uaminifu ndio maana Mago anasema watafute wanasheria waaminifu.
   • Viongozi wanawatenga wanyonge katika maamuzi ya maendeleo ya nchi. 3
   • Wanyonge wanafanya biashara duni km Mago  huku matajiri wakimiliki maduka ya biashara kubwakubwa jijini.
   • Polisi kutumiwa na tabaka la juu kufurusha wanyonge huku wanyonge wakikosa mtetezi.
   • La juu linamiliki magari na la chini 
  2.      
   1. Ndoa huhitaji uvumilivu. Dadi anavumilia miaka tisa ya ndoa kwa Kidawa licha ya kuwa alikerwa na masharti ya kisasa aliyolazimishwa na Kidawa.
   2. Katika ndoa ni muhimu kuwa wanandoa wawe na usawa wa mawazo na mtazamo. Dadi na Kidawa wanatofautiana kimtazamo kwani Dadi ni mtamaduni ilhali Kidawa ni mwanamke wa kisasa na basi hali hii inaleta migogoro kati yao.
   3. Maelewano ni muhimu katika kudumisha ndoa yoyote ile. Dadi anakosa kuelewa hasa masharti ya Kidawa lakini bado anatia saini kuyafuata. Mwishoni anaishia kuwa na majonzi katika ndoa.
   4. Katika ndoa ili mwanaume aonekane kuwa tosha lazima amdhibiti mke wake. Dadi anakerwa kuwa anaonekana mtaani kuwa yeye si mwanamume tosha kwa kuwa ametiwa maganjani na kudhibitiwa na mkewe.
   5. Katika ndoa ni muhimu  kuwa sawa kielimu kwani tofauti ya kielimu  inaibua kutoelewana katika ndoa.
   6. Uaminifu ni muhimu. Dadi aliukosa na akaishia kujiumiza.
   7. Wanasaidiana kazi za nyumbani ingawa Dadi anahisi zinafaa kuwa za mwanamke.
   8. Kupanga uzazi. Walipata mtoto mmoja kwa mujibu wa masharti ya kisasa.
   9. Ndoa inathaminiwa. Kidawa anaacha kazi ili ndoa yake idumu.
  3.      
   • Mkubwa (Ufisadi )
   • Kuhonga wapiga kura. Mkubwa alihonga raia kwa vitenge, kanga, mchele, na sukari ili wamchague.
   • Kuhonga ili kuteuliwa na chama. 
   • Kuhonga wenye msiba ili wamchague 
   • Kuhonga wanandoa kwa sufuria na magunia ya vyakula ili wamchague Mkubwa.
   • Mkubwa kuhonga Ng'weng'we ili amfungulie Mkumbukwa kabla ya kujibu mashtaka ya kupatikana na mihadarati.
   • Mkubwa kuhonga Ng'weng'we ili amrudishie mihadarati iliyokuwa imenaswa na askari ili biashara iendelee
   • Mkubwa kuhonga ili kesi ya dawa ifutiliwe.
  4.    
   1. Ni chanzo cha mtu kupata ajira. Mwalimu Mosi amesoma na anaweza kufanya kazi ya ualimu.
   2. Elimu humpa mtu busara. Mwalimu Mosi anaweza kuwapa nasaha wanafunzi wake.
   3. Wasiowajibikia elimu yao huishia maskini kama Jairo aliyepuuza masomo.
   4. Elimu haifai kuwa chanzo cha utabaka. Mwalimu Mosi anamruhusu Jairo kuhutubu japo hajasoma.
   5. Elimu huepusha maovu katika jamii. Kwa mfano, mauaji, ukwepuzi anaozungumzia Jairo.
   6. Elimu huhitaji mtu awe na matumaini. Mwalimu Mosi aliwapa matumaini ya kufuzu wanafunzi.
   7. Huwapa waja matumaini ya maisha bora usoni. Watu walisoma wakiwa na matumaini ya kujiendeleza maishani baadaye.
   8. Walimu huchangia pakubwa ufanisi wa wanafunzi.
   9. Hujenga uhusiano mwema baina wanajamii.
   10. Hukuza vipaji vya wanafunzi. Walioimba na kucheza ala za muziki.
   11. Ni chombo cha kupinga ubaguzi. 
   12. Ni chombo cha kuheshimisha. Mosi anasifiwa na wanafunzi kwa kuwaelekeza na kuwafunza.
   13. Ni ghali. Sabina kufukuzwa shuleni ili akanunue vitabu.
   14. Ina wajibu wa kuandaa nustakabali wa wanafunzi na kuwafanya watu bora  baadaye.
 5.      
  1. ‘Bogoa gani huyo?’ Kazu alibadilisha toni ya sauti na mng’aro wa sura yake. Alikuwa tayari kajaa huzuni ingawa hadithi yenyewe alikuwa haifahamu vizuri. Usoni pake ulisimama unyeti na juu ya ngozi ya uso wake huruma zilijitokeza. Ndivyo alivyo Kazu kila siku. Anaweza kubadilika mara moja kama uso wa mtoto mchanga.
   • Utohozi- toni
   • Kinaya- kujawa na huzuni bila kujua hadithi
   • Taswira- huwakosesha watoto raha. Bogoa anatamani kuishi na Sebu ili kuepuka mateso ya Bi  Sinai
   • Tashibihi- kama uso wa mtoto mchanga.
  2.      
   • Anakuza maudhui ya kufanyisha watoto kazi za nyumbani badala ya kuenda shule.
   • Anakuza sifa ya Bogoa kuwa mvumilivu.
   • Anakuza sifa ya Bogoa kuwa msiri.
   • Anakuza sifa ya Bogoa mwenye bidii. Alikuwa akiamka alfajiri kupika mandazi
   • Anakuza maudhui ya ukatili na  udhalimu.
   • Anaendeleza maudhui ya ubaguzi.
   • Anakuza maudhui usaliti, 
   • Anakuza maudhui  malezi
   • Anakuza sifa ya wazazi wa Bogoa kuwa hawajawajibika kwa kumwachia ulezi wa mtoto wao na hata walipomtembelea hawakuuliza bogoa hali ya maisha..
   • Kielelezo cha matajiri wanaonyanyasa wanyonge.
   • Kielelezo cha marafiki wabaya. Alikuwa ameahidi wazazi wa Bogoa kuwa angemlea Bogoa vizuri na hata kumpeleka shule lakini hakufanya hivyo.
    Zozote 8
  3.      
   • Bogoa alikatazwa kucheza na watoto wa Bi Sinai.
   • Kunyimwa haki ya kujieleza. Wazazi wake hawaruhusiwi kuzungumza na mwana wao.
   • Kunyimwa haki ya kupata elimu. Bi Sinai anamfanyisha Bogoa kazi basi ananyimwa fursa ya kwenda shule.
   • Kunyimwa haki ya usingizi. Bogoa alilazimika kuamka alfajiri ili kuchoma maandazi ya kuuza shuleni. Siku moja usingizi unamchukua na maandazi yanaungua.
   • Kunyimwa haki ya mlo mzuri. Bogoa anaruhusiwa kula makoko na makombo waliyoacha watu baada ya kushiba.
   • Kupigwa. Bogoa alipochelewa kutoka mchezoni alikuwa akipigwa vibaya.
   • Kutusiwa. Bi Sinai alikuwa akimtusi na kumsimbulia.
   • Bogoa kulia kwenye sufuria na wengine sahanini. Alikula wa mwisho.
   • Kutishwa. Sinai kutisha Bogoa kuwa angemkata ulimi akiambia mtu kuhusu maisha ya pale.
   • Kuchomwa viganja na Sinai kwa kuunguza maandazi.
   • Kukoseshwa watoto raha. Bogoa anatamani kuishi na Sebu ili kuepuka mateso ya Bi  Sinai
 6.      
  1.      
   • Kuonyesha umuhimu wa kupinga uongozi mbaya- kuboresha maisha- wananchi wana haki ya kuongozwa vizuri.
   • Kukashifu utepetevu wa viongozi – kutoletea nchi maendeleo yaliyotarajiwa- soko chafu na ukosefu wa kazi.
   • Kuhimiza ushirikiano katika kuondoa uongozi mbaya. Lazima raia waukabili na kuuondoa uongozi wa aina hii.
   • Kufichua uovu wa viongozi- ufisadi, usherati, dhulma, kujilimbikizia mali, ubinafsi, ubadhirifu nk.
   • Kuonyesha madhara  ya ulevi- vifo, upofu, utepetevu nk.
   • Umuhimu wa elimu-kuleta ukombozi- vijana wana mchango mkubwa sana. Km Tunu
   • Kuonyesha athari za umaskini- ukosefu wa kazi na mahitaji ya kimsingi.
   • Kukashifu washauri wabaya wa viongozi – huleta uongozi mbaya.
   • Kuonyesha changamoto za wanaopigania haki- kuumizwa, kuuawa, kutishwa nk.
   • Mwandishi anadhamiria kuonyesha uongozi mbaya na athari zake hasa katika mataifa yanayoendea.Viongozi hutumia mbinu mbalimbali kuongoza zinazowanyanyasa wananchi huku wakijinufaisha wenyewe bila kujali.
   • Kuonyesha kuwa ili kujenga jamii mpya, mapinduzi ni muhimu na ni sharti wananchi wajitolee kwa uzalendo ili kupigania haki zao na usawa na kupinga viongozi wasiofaa.
   • Mwandishi anaonyesha kuwa licha ya changamoto zinazomkumba mwanamke katika jamii, mwanamke ana nafasi muhimu katika uongozi na kuleta maendeleo katika jamii.
    zozote 10
  2.      
   • Usafishaji nafsi- Majoka kuwa tayari kubadilika. Viongozi uacha mabaya na kutenda mema. Uk 84/85
   • Usalama kuimarika. Bwana Kingi kukubali kulinda usalama badala ya kutawanya waandamanaji. Uk89. Uk 90 Kingi kukataa kupiga risasi waliotaka Tunu achaguliwe.
   • Kuchagua viongozi waadilifu- uk 89- Wanasagamoyo kusema hawatakubali kuchagua viongozi wanaowaita wajinga.
   • Kufuata katiba- uk 90 Kingi kusema watu wana mamlaka makubwa kuliko amri za Majoka. Kingi anasema hana ruhusa ya kuvamia watu ambao hawajavunja sharia baada ya Majoka kutaka wapigwe risasi .
   • Kufuata sharia- Majoka anaposema amefuta kazi Kingi kwa kutofuata amri yake ya kupiga waandamanaji risasi, Kingi anamwambia lazima afuate utaratibu  wa kufuta mtu kazi. Uk91
   • Kukubali ukweli- Kingi anakubali uongozi dhalimu umefika mwisho na kuomba msamaha huku akijiunga na umati ilhali Majoka alikataa na kumwiita kunguru. uk 91
   • Kuomba msamaha- Mamapima anaomba msamaha kwa kuuza pomba haramu huku akijua kuwa aliwaponza, aliwapunja, aliwadhuru na alikuwa na tamaa.  uk 92
   • Kuchagua viongozi wanaofaa- kupatia Tunu uongozi hata kama ni mwanamke mradi yuko tayari kuongoza kwa haki.
   • kushirikiana bila kujali maneno ya watu- Tunu na sudiwalishirikiana kupigania haki bila kujali vile watu walisema ulikuwauhusianao wa kimapenzi.
   • kuacha maovu – Mamapima kuapa kuwa hatauza pombe haramu tena inayoua na kupofusha.
    zozote 10
 7.    
  1.      
   • Maneno ya Kenga
   • Anamwambia Majoka
   • Ofisini mwa Majoka
   • Wanaongea kuhusu mshahara wa walimu na wauguzi kuongezwa na Majoka anasema wataiongeza kisha waongeze kodi ili wafanye hesabu ya kutia na kutoandio Kenga akamwambia maneno haya.
  2.      
   • kinaya- Kutia kwa kulia na kutoa kwa kushoto
   • tanakuzi- kutia na kutoa
  3. Kenga
   • Mshawishi
   • Mpyaro
   • Mwenye vitisho
   • Mwenye hasira
   • Dhalimu
   • Mwoga
   • Fisadi
   • msaliti
   • karagosi
   • nafiki
   • mwoga
   • katili
   • mshauri mbaya
  4.    
   • Kuua wapinzani. Jabali
   • Kuwapa likizo ndefu. Anataka kuwafurahisha kwani wafanyakazi hawataenda kazini.
   • Kuharamisha maandamano. Ili raia waache kupinga kufungwa kwa soko. 
   • Kufurusha wafadhili wa wapiganiaji haki. Wafadhili wa akina Tunu na Sudi wanatakikana wavunje kambi ili kudhoofisha kifedha.
   • Unafiki/hila/udanganyifu. Kuongeza walimu na wauguzi mshahara lakini anapandisha kodi hivyo hawajafaidika.
   • Kuvunja sheria. Kufuta Kenga kazi kinyume cha katiba kwa kukataa kufyatua risasi kwa raia ambao hawajafanya makosa.
   • Kufukarisha raia. Ili wamtegemee km kufunga soko ambalo ni tegemeo la raia. Ashua anakosa chakula na watoto wakala njaa na akamwendea Majoka msaada. 
   • Kutumia wahuni. Majoka kutumia wahuni kupambana na wapinzani wake km Tunu kuvamiwa na kuvunjwa mguu kwa kupinga soko kufungwa. 
   • Kujaza hofu. Bi Hashima waishi kwa hofu.
   • Kutumia jela. Kufunga Ashua ili mumewe Sudi achongee Majoka kinyago alichokuwa amekataa hapo mbeleni.
   • Kutumia askari. Polisi wanatumia vitoa machozi na risasi ili wasiendelee kupiga soko kufungwa.
   • Kutumia vishawishi na hongo. Tunu na Sudi wanapatiwa kazi katika kiwanda cha Majoka ili wamuunge mkono kisiasa lakini wanakataa. 
   • Kufunga vyombo vya habari. Runinga ya Mzalendo. Kwa kukashifu vitendo vya Majoka kwa kupeperusha maandamano moja kwa moja kupinga kufungwa kwa soko.
   • Tenga tawala. Majoka kutaka kuongea na Tunu na Sudi kando kando, mhuni mmoja kumwambia Tunu kuwa Sudi na Ashua ndio wanawinda  roho yake. 
   • Unasaba. Kuteua binamuye Kenga kuwa mshauri wake mkuu ili iwe rahisi kutekeleza maovu km kuua Jabali.
 8.      
  1. Ujumbe wa shairi hili unakatisha tamaa. Thibitisha. (alama 4)
   Kuna vitisho, viwewe na visirani.
   Kesho yangu imeshaliwa na hakuna uhakika wa kuifikia.
   Hapigiwi simu na marafiki
   Anahujumiwa na watu bila sababu.
   Kuna magonjwa mbalimbali kama vile Ukimwi na ebola na hayana tiba. 
   Kuna majambazi na matapeli waliojaa kila mahali. Zozote nne
  2. Shiari hili ni la Tarbia kwa sababu lina mishororo minne katika kila ubeti.
  3. Mwandishi anaanza kwa kusema kuwa  anaituhumu kesho yake kwa sababu ya uhasama. Anasema uhasama huu unatokana na mahasimu wanaopanga njama ya kumhujumu. Wanataka tu kumsababishia nakama. Mwandishi anamalizia kwa kuuliza kesho yake itatoka wapi na haya mambo yote yanayomzunguka yanaitishia hiyo kesho.
  4. Isitiari- mimi kupe
   Kinaya- kesho yangu imeliwa
   Tanakali ya sauti-  sipo ng'oo
   Utohozi- haloo
   Tashihisi- huyu Ukimwi
   Swali la balagha- Salama yangu i wapi?
   Tashibihi- kama siafu
   Nahau-kung'oa nanga
  5. Mizani- msuko kwa sababu mizani ya kibwagizo ni michache/ kibwagizo ni kifupi
   Vina- ukaraguni- kila kipande kinajitegemea kivina
  6. Kufinyanga sarufi- kesho kuwepo sidhani badala ya sidhani kuwepo kesho
   Inkisari- iso badala ya isiyo/ Waso badala ya wasio
   Tabdila- kitwa badala ya kichwa zozote mbili
  7. Toni – ya kukata tamaa/ kuudhika/ kukosa matumaini/ kuonya
   Nafsi – neni- mtu asiye na uhakika na kesho yake/ aliyekata tamaa
   Nafsi- nenewa.- watu kwa jumla/ mahasimu/ wale wanaodhulumu/ wote wanaohujumu

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Asumbi Girls Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?