Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - MECS Cluster Joint Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. Swali la lazima 
  Waziri wa elimu ameteua kamati ya kuchunguza sababu zinazopeleka shule mbalimbali kutomaliza silabasi kwa wakati ufaao na mapendekezo yake.Umeteuliwa kama katibu wa kamati hiyo .Andika ripoti kuhusu suala hilo
 2. Usafiri wa bodaboda umeleta madhara mengi katika jamii kuliko faida.Jadili
 3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo.
  Kikulacho ki nguoni mwako.
 4. Andika insha itakayomalizika kwa maneno:
  ……….Aha! kumbe mwungwana akivuliwa nguo huchutama.Sitaisahau siku hiyo kwani sijawahi kufedheheka maishani kama nilivyoaibika siku hiyo.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. Mtindo wa ripoti                      
  1. Kichwa cha ripoti 
  2. Utanguliza –jambo linalotafitiwa ,wadhamini /wafadhili,majukumu ya wanajopo/wanakamati,
   Muda wa uchunguzi,wanajopo wenyewe.
  3. Mbinu za ukusanyaji data.
  4. Matokeo ya uchunguzi –Vijimada vidogo vidogo kila kijimanda kishughulikiwe pekee na kwa ukamilifu.
  5. Hitimisho-Muhtasari wa yote yaliyopatikana kuwa yenye umuhimu
  6. Mapendekezo-Hatua za kuchukuliwa ili kudhibiti/kurekebisha hali Fulani.Huorodheshwa kwa nambari.    
  7. Sahihi –Sahihi ya anayeandika ,jina lake na wadhifa wake
   HOJA ;
   • Majanga ya kitaifa k.v. Ugonjwa wa korona
   • Migomo shuleni
    Ukosefu wa usalama
   • Matukio ya kitaifa k.v .Uchaguzi
   • Ukame
   • Tamaduni za baadhi ya jamii k.v.tohara  
   • Hali ya anga
   • Mtaala mrefu/silabasi ndefu
 2. Insha ya mjadala :
  Mtahiniwa anaweza
  kuunga mkono
  kupinga
  kushughulika pande zote mbili
  MADHARA
  • Ajali nyingi barabarani
  • Vifo kutokana na ajali
  • Ulemavu wa baadhi ya wahudumu na wasafiri
  • Kuzidisha gharama za huduma za hospitali
  • Vijana wengi wameacha shule
  • Kuenea kwa utovu wausalama
  • Kuvunjika kwa ndoa kwa kutowajibika kwa baadhi ya wahudumu
  • Zimesababisha msongamano barabarani
  • Kuharibu mazingira – kelele nyingi na moshi
  • Ongezeko la ufisadi – polisi wanaitisha hongo
  • Husababisha uzembe – watu hawatembei na mwishowe wanapatwa na magonjwa kama kisukari
   FAIDA
  • Uchumi wa nchi kuimarika/kuiuka
  • Zimeimarisha usafiri wa watu na mizigo
  • Zimebuni nafasi za kazi – wahudumu ,wauza vipuli,n’k.
  • Kupunguza uhalifu
  • Gharama ya utunzi na vipuli vyake si ghali
  • Huokoa wakati kutokana na kasi yake 
  • Kufikika kwa sehemu zisizofikika kwa magari
 3. Mtahiniwa abuni kisa/visa vitakavyodhihirisha ukweli wa methali hii.
  Kuwa mtu anayeweza kutudhuru ni yule anayetufahamu vizuri.Anaweza kuwa rafiki, mwanafunzi mwenzake, ndugu na jamaa,mwandani wa kisiasa/uongozi,wafanyakazi wenzako, n.k
 4. Mtahiniwa onyeshe uovu wa mtu anayethaminiwa/anayeaminika ni mwema anapofichuliwa yeye huaibika.

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - MECS Cluster Joint Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?